Professional Documents
Culture Documents
Katiba Ya Kikundi
Katiba Ya Kikundi
1.0 UTANGULIZI
1
Kikundi cha Upendo Group kilianzishwa tarehe 10/7/2021 kikundi kilianza na wanachama apatao
kumi na nane (18). Kikundi makao yake makuu ni Machimbo.
Hadi Dec 2022 kikundi kina wanachama hai wanaoelewa malengo ya kikundi wapatao kumi tano (15)
wakipatikana machimbo Dar salaam.
2
4.0 MUONGOZO WA KATIBA KATIKA MAMBO YATAKAYOKUWA
YANASAIDIWA NA KIKUNDI
Katiba hii ya kikundi cha upendo group inatoa muongozo kwenye mambo yatakayokuwa yanasaidiwa
na kikundi kiujumla ifuatavyo;-
4.1 KUFIWA.
Katiba inaelekeza kuwa kikundi cha upendo group kitasaidia au kutoa msaada iwapo msiba utakuwa
ni wa;-
I. Mwanachama Mwenyewe
II. Baba Mzazi au Mlezi
III. Mama Mzazi au Mlezi
IV. Mtoto
V. Mama Mkwe au Mlezi
VI. Baba Mkwe au Mlezi
VII. Mume
VIII. Ndugu wakaribu ambae unaishi nae kama mwanao na ambae hana wazazi.
3
4.1.3 Kila mwanachama itatazimika kujumuika kwa kumpa pole mwanachama aliyefiwa, na kama
msiba ni wa kusafirisha (mkoani) basi itasubiriwa arudi na wanachama wote kwa pamoja wataenda
nyumbani kwa mfiwa kumpa pole.
4.2 UGONJWA
Kwa mujibu wa katiba watu watakaopaswa kusaidiwa na kikundi wakati wa ugonjwa ni hawa
wafuatao;-
a) Mwanachama mwenyewe
b) Mume
c) Mtoto
4.2.0 UTARATIBU WA KUSAIDIA WAKATI WA UGONJWA KWA MUJIBU WA KATIBA
a) Ili kikundi kiweze kutoa msaada wa ugonjwa kwa mwanachama anayeuguza au kuuguliwa ni
lazima mgonjwa awe amelazwa kwa muda wa siku tatu (3) na wanakikundi wawe na Taarifa
kupitia kwa kamati ya kuona kytembelea wagonjwa.
b) Baada ya kujiridhisha na hatua ya awali (1) kikundi kitatoa fedha kiasi cha shilingi 70000 na
atakabidhiwa muuguzi
c) Na baada ya fedha hiyo kutoka kwenye mfuko wa chama na kukabidhiwa kwa muuguzi kila
mwanachama itampasakuchangia kiasi cha taslimu cha shilingi Elfu tano (5000) ili kujazia mfuko
wa kikundi kwa kile kilichopungua.
4.3 UZAZI
4.3.0 UTARATIBU WA KUSAIDIA MWANACHAMA ALIYE KWENYE UZAZI
a) Ikiwa mwanachama amejifungua basi kila mwanachama atachanga kiasi cha shilingi Elfu 5000 na
kukabidhiwa mwanachama aliyejifungua.
b) Wanakikundi kwa pamoja watamtembelea mwanachama aliyejifungua.
4.4 HARUSI
4.4.0 UTARATIBU WA KUSAIDIA MWANACHAMA MWENYE HARUSI
a) Ikiwa mwanachama ana harusi basi atagawa kadi kwa wanakikundi ili waweze kuchangia.
b) Kwa mujibu wa katiba hii, mwanachama mwenye harusi ni lazima atoe Taarifa kwenye kikundi
miezi mitatu kabla iwapo harusi hiyo ni ya kikristo na iwapo harusi hiyo ni ya kiislamu basi atatoa
Taarifa kwa kikundi mwezi mmoja kabla.
c) Iwapo mwanachama atakuwa na sherehe ya mtoto wa kumzaa atachangiwa kiasi cha eifu ishirini
na tano kwa kila mwanachama.
d) Kampani ni elfu tano kwa mtu unaeishi naye.
4
b) Iwapo ikitokea mtu anataka kujiunga na kikundi cha upendo group itamlazimu kulipa kiasi cha
shilingi ………………………………………………………… ili awe mwanachama.
c) Kwa mwanachama mpya ataanza kupata msaada wa kikundi baada ya kumaliza miezi mitatu (3)
tangu kujiunga kwake.
d) Kwa kila mwanachama mpya itamlazimu kulipa shilingi Elfu mbili(2000) kwa ajili ya kupata
katiba ya kikundi
e) Kwa mujibu wa katiba, idadi ya wanachama wa kikundi cha upendo group kuzidi ishirini na moja
(21)
f) Wanachama kwa kikundi cha upendo group watakuwa wanakutana kwenye kikao cha pamoja
walau mara moja (1) kwa mwezi.
g) Kwa mujibu wa katiba maudhurio ya kikao cha kikundi hayana udhuru. Iwapo mwanachama
hataudhuria kikao kwa sababu moja au nyingine hata kama ni msiba atapaswa kulipa faini ya kiasi
cha shilingi Elfu mbili (2000).
h) Iwapo kuna mwanachama hajaelewa sehemu au kifungu chochote cha katiba anaweza kuomba
ufafanuzi au maelezo kwa katiba.