UNABII WA MIAKA 2300 - ShareHope Ministries

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

ShareHope Ministries

Receive It! Experience It! Share it!!!

OCT
4
2015

UNABII WA MIAKA 2300

(https://sharehopeministries.files.wordpress.com/2015/01/526113_165760220227768_96151278_n.jpg)
Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: Unabii wa Miaka 2300


(https://sharehopeministries.files.wordpress.com/2015/10/unabii-wa-miaka-2300-ev-peter-i-jefter.docx)

Daniel 8:13, 14…. 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza
huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo
ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za
jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2)
ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme
Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa
katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli
Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia
akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka
upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji
pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa
ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-
kanyaga

Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu
nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe
ndogo, iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia
katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye
uso mkali, afahamuye mafumbo………atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa
falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na
pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.

Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi
lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea
sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi
likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo
ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu
mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari
sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha
patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo
patakatifu patakapotakaswa.

Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo
inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu
(2300).

Nini tafsiri yake miaka hii 2300??

Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300
lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.

Katika kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.

1. nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo
1:5………… ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa
na siku kamili 2300
2. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6………siku arobaini, siku moja kwa
mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300..
Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.
3. Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine
kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.

Mwanzo wa miaka hii ni upi?

Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa
majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu………,25 Basi ujue na
kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu…..
kutakuwa na majuma saba………….

Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70×7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa
juu ya taifa la Israeli.

Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo
mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa
amri wote wenye kutunza hazina…..hata kiasi cha cha talanta mia za fedha …. kila neon
litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa
mbinguni…….. Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya
Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)….katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490
tunasalia na miaka 1810.

490+1810=2300.na
Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu
ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na
huishia mwaka 1844 B.K.

Bwana atubariki tukutane sehemu ya pili kujifunza matukio makubwa yaliyotabiriwa na kutokea katika
kipindi hiki cha miaka 2300.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

By ShareHope Ministries
• Posted in Bible Studies

Blog at WordPress.com.

You might also like