Habari Motomoto

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

UNC RADIO.

KURUNZI YA UNC.
LABAN MRIMA KATANA.

TOLEO LA HABARI .

UTANGULIZI.

Asaalam aleikum hujambo popote ulipo natumai umzima na buheri wa afya kabisa, Zimetimia saa saba
adhuhuri saa za Afrika mashariki, karibu tena kwenye Makala yetu ya Kurunzi ya UNC siku ya kumi na
sita, mwezi ukiwa ni wa tano mwaka elfu mbili ishirini na tatu, jina langu ni Laban Mrima, makinika nami
sasa hadi tamati.

 Mahakama kuu mjini Mombasa imeagiza polisi kukoma kuingilia shughuli za kidini katika kanisa
la mhubiri Ezekiel Odero lilipo maeneo ya Mavueni, kaunti ya Kilifi.
 Uamuzi huu unajiri baada ya mhubiri huyo kutafuta ulinzi kwenye kanisa hilo, akidai ya kwamba
amekua akisumbuliwa kiholela na vyombo vya dola.
 Haya yanajiri huku akaunti kumi na tano za benki zinazomilikiwa na mhubiri Ezekiel Odero,
zikisalia kifungoni hata baada ya mhubiri huyo kupelekea ombi la kufunguliwa kwa akaunti hizo
hapo jana.
 Vilevile pia, mahakama hio ikiongozwa na jaji mkuu Olga Osewe, ilihalalisha ombi la kufungwa
kwa kituo cha televisheni kinachohusishwa na shughuli za mhubiri huyo hadi pale maelekezo
kamili kutoka kwa idara ya mawasiliano nchini itatathmini kibali cha kituo hicho.
 Kesi hii imeratibiwa kusikilizwa tena mnamo tarehe ishirini na tisa mwezi huu huku mhubiri
Odero na timu yake ya kisheria wakitarajiwa kuwasilisha hoja zao na ushahidi wa kutosha ili
kutetea msimamo wao mahakamani.

 Na katika kaunti ya Bomet ni kwamba polisi sita wamefikishwa hospitalini baada ya kujeruhiwa
na kundi la vijana, wanaokhisiwa kufikia idadi ya mia mbili, waliopatikana wakivuna majani chai
bila ya idhini kwenye shamba la majani chai linalomilikwa na kampuni ya Finlays.
 Tukio hili linajiri likifuatwa na lingine lililomuacha polisi mwengine na majeraha mabaya ya
kichwa baada ya kuvamiwa na panga kwenye kivangaito chenye matukio sawa na hayo ya jana
mwezi uliopita.
 Tukisalia kwenye habari hiyo ni kwamba mtu mmoja ameweza kusombwa na maji kwenye mto
itare katika eneo bunge la Konoin kaunti hiyo ya Bomet, alipokua katika harakati za kuwakwepa
polisi hao.
 Mshukiwa mwengine kwenye zogo hilo mwenye umri wa miaka kumi na sita anaendelea
kuuguza majeraha ya risasi ambayo ilifyatuliwa kimakosa kweye makabiliano hayo.
 Vile vile pia gari la polisi liliweza kuteketezwa na vijana hao waliokuwa na ghadhabu kubwa kwa
ukosefu wa kazi nchini.

 Kwengineko ni kwamba Rais William Samoei ameipiga kalamu bodi nzima inayohusika na
shughuli za afya kwa umma almaarufu KEMSA ikiongozwa na mheshimiwa Josphine Mburu na
mwenzake Terry Ramadhani, kwenye zogo la ufujaji wa pesa takribani bilioni nne, zilizoratibiwa
kwenye tenda ya usambazaji wa vyandarua vya kujikinga na mbu nchini.
 Haya yanajiri baada bodi hio kuanikwa hadharani na wanahabari wa kampuni ya Nation
kutokana na kile kilichoonekana kama ufisadi wa hali ya juu, na unyanyasaji wa huduma za
wananchi wa kawaida nchini.
 Vyandarua hivyo vilitarajiwa kuwasaidia wananchi wa tabaka la nchini kwenye sekta ya afya
haswa kujikinga na magonjwa ya malaria yanasababishwa na mbu.

 Tukiangaangaa hadi kaunti ya Kericho ni kwamba wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya


Litein, wagomea shule mnamo siku ya ijumapili baada ya ratiba ya burudani kubadilishwa
shuleni humo.
 Wanafunzi hao wanaokhisiwa kufikia idadi ya elfu moja na mia tisa, waliweza kuonyesha
ghadhabu na hasira zao kwa kuvunja vioo vya madarasa na mabweni huku wakiharibu mitandao
ya utambulisho shuleni humo.
 Hali hiyo hiyo pia imeweza kushuhudiwa katika kaunti ya Bomet baada ya wanafunzi wa shule
ya upili ya wavulana ya Kipsuter kugoma baada ya mwalimu wao mkuu kupewa uhamisho.
 Duru zakuaminika zinaarifu ya kuwa wanafunzi hao waliandamana kwa amani, mnamo siku ya
ijumatatu asubuhi hadi kwenye ofisi za kinara wa elimu wa kaunti hiyo, ila hakuna hasara
yoyote au madhara yoyote yaliyofanywa na vijana hao.

 Katika habari zengine za kuleta mpwito wa furaha ni kuhusiana na chuo chetu chenye matawi ya
juu hapa nchini na duniani, chuo kikuu cha Nairobi.
 Hii nii baada ya chuo hiki kusalia kuwa chuo cha pekee hapa nchini kuorodheshwa kwenye vyuo
elfu mbili bora duniani, kwenye orodha hio iliofanywa na chama kikuu cha kuorodhesha vyuo
duniani almaarufu Centre for World University Rankings(CWUR).
 Chuo kikuu cha Nairobi kimejizolea alama sitini na nane nukta mbili kati ya mia moja na kushika
nafasi ya elfu moja , mia nne ishirini tano, nafasi ishirini na tano nyuma kulingana na orodha
iliofanywa miaka mitatau hapo nyumani na idara hiyo.
 Ikumbukwe kwamba chuo hicho kimetanguliwa na vyuo vingine viwili vya Afrika mashariki
ambavyo ni chuo kikuu cha Addis ababa cha Ethiopia na kile cha Makerere nchini Uganda
ambavyo vimeshika nafasi ya mia nane sitini na mbili na mia tisa hamsini mtawalia kwenye
orodha hio.
 Haya yanajiri wakati chuo kikuu cha Nairobi kikichakarika na kukabiliana na ongezeko la deni
chuoni humo huku ikirekodi idadi ya chini ya wanafunzi walioweza kujiunga na chuo hicho
mwaka huu.
KIMATAIFA.

 Kwenye rubaa za kimataifa ni kwamba Rais wa Urusi Vladmir Putin, ametoa kauli ya kwamba
mustakabali wa nchi yake ipo mikononi mwa wanajeshi waliovitani dhidi ya taifa jirani la
Ukraine.
 Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa maadhimisho ya siku ya ushindi huko
jijini Moscow , Putin alikiri ya kuwa kesho ya taifa hilo, ipo mikononi mwa wanajeshi
wanaoipigania nchi hio kwenye vita vya kibiashara kati yao na Ukraine, vilivyoanzishwa rasmi na
Rais huyo mapema mwaka jana.
 Kwenye hafla hio ambayo gwaride la kijeshi la taifa hilo lilikuwa likiadhimisha siku ya ushindi wa
kihistoria kwenye nchi hiyo, ambapo muungano wa Soviet ulishinda vita dhidi ya Ujerumani.
 Haya yanajiri huku Putin akituma waraka wa kuthibitisha uvamizi wake dhidi ya Ukraine, huku
akilaumu nchi za magharibi zenye uwezo mkubwa kiutawala duniani kwa kuchochea vita hivyo.

MICHEZO.

 Michezoni ni kwamba timu ya Manchester United inayonolewa na mdachi Erik Ten Haag,
inatembelea kamba kwenye safari ya kufuzu kombe la mabingwa barani Ulaya msimu ujao
baada ya vigogo wa Anfield, naizungumzia Liverpool kuinyuka timu ya Leicester City magoli
matatu kwa nunge na kusonga karibu na timu za Mnachester united na Newcastlle united
zinazoshikilia nafasi ya nne na tatu mtawalia.
 Liverpool ikiwa imebakisha mechi mbili kwenye ratiba yake ya msimu huu, inashikilia nafasi ya
tano ikiwa na pointi sitini na tano, alama moja nyuma ya Manchster United na Newcastle united
ila ikumbukwe timu hizi mbili zimebakisha mechi tatu kuhitimisha msimu mzima.Kazi kwao
United na Liverpool, nyasi ziumie, kipute kinoge.

 Na tukiingia pale darajani Stamford bridge, ni kwamba aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa timu
za Tottenham na PSG Mauriccio Pochetino, amekubali kutwaa mikoba ya kocha Graham Potter
aliyepigwa kalamu kwenye kambi ya Chelsea.
 Pochetino ataanza kandarasi yake msimu ujao huku akiwa na kibarua kigumu kuirudisha timu
hiyo, katika ubora wake kwani kwa hivi sasa inashikilia nafasi ya kumi na moja kwenye ligi hiyo,
ikiwa ni wazi kwamba hawatweza kushiriki kwenye mitanange yoyote ile ya bara Ulaya msimu
ujao.

Hapo ndipo nahitimisha Kurunzi ya saa saba,shukrani za dhati kwa msikilizaji wangu kwa kuwa nami
hapa UNC Radio, jina langu ni nLaban Mrima.

You might also like