Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

Solly & Flory Corporation

E-mail: www.sollydaddy92@gmail.com
www.frolidahilali5@gmail.com
Contact: +255 (0)769 567 263 / +255 (0)753 907 403
Solly & Flory Corporation
ATAPE - KIHONDA NET EVENT-Morogoro
Nyayo Za Matumaini
IBADA SIKU YA SABATO LEO Tarehe 20 Mei, 2023

UJUMBE LANGONI
By Pastor Paul Semba
Fungu kuu: Luka 16:27-31
“27Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28kwa
kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa
pa mateso. 29Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30
Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu,
watatubu. 31Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa
hata mtu akifufuka katika wafu”

~ LUTU _ Mwanzo 12,13

“Iko hatari kwa mkristo kuweka makao ya kudumu katika mijengo ya


kidunia”

MUNGU anatutaka tuweke mawazo yetu mbinguni.

Lutu alivutiwa na mji wa Sodoma kutokana na uchumi/fahari ya mji ule, wala


hakuangalia tabia ya watu wa mji ule.

Sodoma ulikuwa mji wa uovu (Ulijaa uovu)

Ezekiel 16:49

“49Tazama, uovu wa umbu lako, Sodoma, ulikuwa huu; kiburi, na kushiba


chakula, na kufanikiwa, hayo yalikuwa ndani yake na binti zake; tena hakuutia
nguvu mkono wa maskini na mhitaji”
Dhambi kuu tatu (3) za mji wa Sodoma

 Kiburi
 Kushiba chakula
 Mafanikio

2 Petro 2:6-7

“6tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akaipindua na kuifanya majivu,


akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;
7
akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa
ufisadi wa hao wahalifu”

Yuda 1:6, 7 – Sodoma walibadili mambo ya Asili.

“Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao
yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya
siku ile kuu. 7Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando,
waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili
yasoyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Sodoma na Gomora
Mwanzo 19:1- Mkewe Lutu pamoja na Lutu waliwakarimu wale wageni
(Malaika)

“Basi wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa
mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama
kifudifudi.

Mara zote Lutu alikuwa akilalamika na kuzuia uovu uliokuwa ukiendelea katika
mji ule.
Mungu alishuka katika mji wa Sodoma ili aone kama iko njia ya kuwaokoa watu
wake.

Mwanzo 19:15

“15Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae


mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu”

Lakini Lutu alikawia kawia / alionyesha kusitasita hakuw ana utayari wa


kuondoka.

Mwanzo 19:17

“17.....Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po
pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea”. Huu ulikuwa ujumbe wa Yesu, LAKINI
MKEWE LUTU ALIGEUKA

Kugeuka – Ilimaanisha MUNGU ni muongo.

NI SAA YA KUJIPONYA NAFSI YAKO, USITAZAME MTU


YEYOTE

Kauli za Yesu

 Jiponye nafsi yako


 Usikawie
 Usigeuke nyuma

Lutu alitoka nje ya Sodoma si kwa sababu ya miguu yake wala juhudi zake
bali ni kwa sababu ya maombi ya Ibrahimu.
“Kuna nguvu katika maombi, tunapofanya maombi yetu binafsi tususahau
kuwaombea ndugu zetu, jamaa zetu, rafiki zetu bila kuwasahau wazazi wetu”

BWANA AWABARIKI SANA

Prepared by Mr Solly and Ms Flory

©2023

You might also like