Bomowa Bomowa

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 9

KANISA LA MTAKATIFU STEFANO GACHIE

LAWALETEA

BOMOWA - BOMOWA
MTAYARISHI MKUU:

MTAYARISHI:

MTUNZI: Joanne Shiveka

MWELEKEZI: Marotso Mukwambo

INKISIRI

Je, ni haki vyombo vya serikali kuvamia biashara (duka la kuuza maabadi)
iliyoanzishwa na vijana wenye bidii maishani kwa lengo la kufanya ubomozi ili
kujenga kiwanda cha samaki? Je, vilio vya vijana wanyonge vitapata kusikika?

WAHUSIKA

WATEJA - WAUMINI
1.

2.

3.

4.

5.

VIJANA - WACHAPAKAZI

1.

2.

3.

4.

5.

SERIKALI - TINDIKALI

1.

2.

3.

4.

5.

BOMOWA BOMOWA

VIJANA

Jamaniye duka letu, takatifu limenoga


Vitabu ni vya kikwetu, vya kusali takatifu

Rozari nazo wakwetu, meremeta utukufu

Wateja ni wa kikwetu, wa Imani takatifu

WAUMINI

Sisi nasi ni wateja, tena ni waumini

Sanamu rozari kuja, kununuwa kwa imani

Vijana wetu wa tija, mejikaza kisabuni

VIJANA

Karibieni wateja, hata twauza ubani

SERIKALI

Duka hili lifungeni,tumetumwa kubomowa

Na wateja ondokeni, ama tutawabomowa

Kiwanda kitajengwani, cha samaki wakuamwa

Virago vikusanyeni, wakati wa kubomowa

WAUMINI

Hatutawatazama tu, kiwanyayasa vijana

Uko wapi wenu utu, mulopewa na Rabana?

VIJANA

Tupeni siku tatu tu, Tutabanduka vijana

WAUMINI
Hakuna cha masiku tu, musibanduke vijana

SERIKALI

Semi zenu sitisheni, tumekuja kubomowa

VIJANA

Semi zetu sikizeni, masikini mwabomowa

WANAHARAKATI

Semi zao sikizeni, duka kwao ni mauwa

SERIKALI

Dereva wapuuzeni, tingatinga kubomowa

VIJANA

Tunao ndugu wachanga, tunawalipia karo

Chakula chao wachanga, ni sisi twakichakuro

Ukilitia mchanga, watawafukuza karo

Tunahofia majanga, yatafichuwa danguro

SERIKALI

Si notisi tuliwapa, kuifunga biashara?

VIJANA

Si leseni mulitupa, kufunguwa biashara?

Ushuru pia twawapa, ona mwaleta madhara

WAUMINI
Wapeni lizowalipa, ndo wafunge biashara

VIJANA

Sisi ni mavijana tu, ni kundi la mayatima

Wazazi lifariki tu, magonjwa liwaandama

Kachanga pesa zetu tu, duka hili kusimama

Bidhaa zake Mungu tu, kibomoa tutakwama

SERIKALI

Sizitaje shida zenu, hata mimi ni yatima

Nendeni kajenge kwenu, ardhi hii mutahama

Twafwata sheria zenu, kiwanda kitasimama

Kusanya sanamu zenu, tingatinga yajitoma

WAUMINI

Walichukuwa mikopo, kuanzisha biashara

VIJANA

Karotasi ni mukopo, ndo maisha iwe bora

Lakini sasa mikopo, imegeuka madhara

WAUMINI

Watalipaje mikopo, kibomoa biashara?


SERIKALI

Kiwanda tutakijenga, cha samaki bila shaka

WAUMINI

Kiwanda hamutajenga, tutavuruga mashaka

VIJANA

Tumechoshwa zenu chenga, haki zetu mezishika

SERIKALI

Mukizidi kutupinga, kwenye koo tawashika

WAUMINI

Ona misalaba nani,mwataka kuipakata

Rozarizo ukutani, munataka kuvinata

Mishumaa nazo nani, hamna huruma hata?

Hata ubani jamani, mwapania kata kata?

SERIKALI

Sijibize weye mbuzi, kama ndege kuniasi


Wafanana na viazi, na kamasi la wasasi

WAUMINI

Situite sisi mbuzi, tawakuna bila wasi

Siisi ni sisimizi,tutawafika kwa kasi

(Tingatinga)

WAUMINI

Vizuizi tuundeni , wabomowe sisi kwanza

Na picha mitandaoni, kurasa zile za kwanza

VIJANA

Tuzikeni muchangani, tingatinga kutufyonza

Mikopo tulipewani, kuna haja kutuponza?

VIJANA/WAUMINI

Wabomoaji mezidi, Limuru mulibomowa

Mushadha nayo kazidi, Gasharage kubomoa

Ruaka nayo munazidi,Gashiye munabomowa

Mara hii mukizidi, tabidi kuwabomoa

(Haki yetu)

WAUMINI

Baba tizama kondoo, tizama wabomowaji

Mejitia ujogoo, ibilisi mupa taji

SERIKALI

Nyiye kwetu fondogoo, akili zenu za maji


Ni ujinga wa ukoo, mwateseka vichwa maji

(Haki Yetu)

SERIKALI

Halo halo bwana mkubwa, kuna shida lokesheni

Wameungana pakubwa, tetesi mitandaoni

VIJANA

Twawaeleza wakubwa, fidiya watulipeni

SERIKALI

Tutafanyani mkubwa, kwenye twita mefikani

VIJANA

Hatutaki tiagasi , tunataka mabomu

SERIAKLI

Hawataki tiagasi, wanataka mabomu

VIJANA.

Tumezoea magesi, kutachafuka humu

SERIKALI

Wanazidisha tetesi, fesibuku instagramu

WAUMINI

Tizameni kalivari, zioneni pembe tatu

Misalaba misumari, kuna Mungu wa Utatu

Mishumaa yenye ari, imewaka mara tatu

Mwanga wake wenye shari, waangaza mara tatu


KANJO

Haya basi tulieni, suluhisho tunawapa

Ardhi tumeipateni, wiki kesho tutawapa

Fidia tawalipeni, mikopo pia twawapa

Ya dijitali leseni, kesho kutwa tutawapa

(Kushangilia)

WOTE

Sisi sote meshikana, (ona) duka letu litang'ara (kweli)

waumini kufaana (sana), tumezika masihara (chwara)

Jukumu letu vijana, (Kenya) jikaza simba marara (raaa)

Tazidi uza vijana (sote), oneni wanavyong'ara

BOMOWA BOMOWA ZIMEKWI-SHA!

You might also like