Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

Utangulizi

Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au
mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Kol 1:16 SUV

Hapo Mwanzo Mungu aliumba vitu vyote ikiwa ni pamjo nasisi alituumba na kutupatia
majukumu kila mmoja atakayofanya hapa duniani tunaposoma Mwanzo

''Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale
samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.''
Mwa 1:26 SUV

''BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na
kuitunza.''
Mwa 2:15 SUV

NJOZI NA UTUME
Mungu alituumba kwa kwa aijili ya mambo 2 makubwa hapa duniani
1. Kutawala
2. Kazi na Matunzo

Baada ya dhambi majukumu yaliongezeka na baadhi ya maagizo ya awali kuhafifishwa


''nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake;
huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.''
Mwa 3:15 SUV

Mungu hakutuacha vivyo hivyo alitupatia tumaini la wokovu wetu na jukumu letu kubwa
hapa duniani ili tuweze kukombolewa na hatima tuondokane katika pambano kuu hili
ambalo uwanja wake wa vita umekuwa hapa duniani

Shetani amekuwa adui mkubwa wa mwanadamu akimdanganya na kumshawishi


kutenda uovu ili asipate kukombolewa ingawa Mungu alituhakikishia ukombozi kupitia 
Yesu Kristo Mwanawe na kwa kuhakikisha agano lake hilo alilowaambia adam na hawa
edeni lilitimia pindi Kristo alipo sulubiwa msalabani na uovu wote wa shetani kuthibitika
na Kristo kuinuliwa juuu
''Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.''
Kol 2:10 SUV

Kristo aliye na mamlaka yote  na enzi  ametukamilisha sisi ili tuweze kutenda kusudi letu
maishani mwetu katika maisha haya na ya baadae baada ya dhambi kutoweka ''Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Alikuwako
ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu
haukumtambua.''
Yn 1:3, 10 SUV
Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na
mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya
sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana,
Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni
hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa
Mungu.
Gal 4:4-7 SUV

Njozi yangu ya utume katika fungu la Kol 1:16 ni kufanyika Mwana wa Mungu na
kumiminiwa Roho mtakatifu na kisha kutenda yote yaliyo mapenzi ya Mungu

''Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na
ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini
twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama
alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo
mtakatifu.''
1 Yoh 3:1-3 SUV

''Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana;
enendeni kama watoto wa nuru,''
Efe 5:8 SUV
Bwana ametuagiza  tuenende kuhubiri injili ''Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote
kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;''
Mt 28:19 SUV
Kuhubiri injili kupitia mitandao ya kijamiii kwa vifaa vya kieletronics na pia kuhubiri kwa
njia ya matendo yangu yanayomuinua Kristo na Kumtukuza yeye na mahali pa kazi
popote pale Mungu na Aniongoze

"Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu
mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako. Maadamu
mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu,
akaenda zake, .................."
Yn 12:35-36 SUV

You might also like