Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 137

Condensed Great Controversy in Swahili

VITA KUU
Baina ya Kristo na Shetani
Ellen G. White

VALIYOMO
Sura Ukurasa
Dibaji 7
1. Uasi Mkuu 9
2. Siri ya Kuasi 16
3. Watengenezaji wa Kanisa la Zamani 29
4. Jinsi Luther Alivyoleta Matengenezo Makubwa 53
5. Maendeleo ya Matengenezo ya Dini 42
6. Kushindsva Kuendelea 50
7. Ujumbe wa Malaika wa Kwanza 53
8. Ujumbe wa Malaika wa Pili 63
9. Kilio cha Usiku wa Manane 69
10. Patakatifu 76
11. Ujumbe wa Malaika wa Tatu 81
12. Jukwaa Lililo Imara 88
13. Madanganyifu ya Shetani 92
14. Imani Iuu va Kuone-ca na Mizimu 98
15. Sauti Kuu 106
16. Mwisho wa Rehema 109
17. Wakati wa Taabu ya Yakobo 114
18. Kuokolewa kwa Watakatifu 117
19. Ujira wa Watakatifu 121
20. Miaka Elfu 123
21. Ufufuo wa Pili 126
22. Kumtawaza Kristo 129
23. Sauti ya Pili 136
24. Ulimwengu Mpya 140

Ujumbe wa Mwandishi kwa Wasomaji wa Kitabu Hiki


KWA njia ya mwangaza wa Roho Mtakatifu, mambo ya shindano baina ya wema na
uovu, ambalo limeendelea tangu zamani, yamefunuliwa kwa mwandishi wa kitabu hiki. Mara
kwa mara niliruhusiwa kuona yaliyofanywa nyakati nyingine maalum katika shindano kuu baina
ya Kristo, aliye Mkuu wa Uzima, na Sababu ya wokovu wetu, na Shetani aliye mkuu wa uovu, na
sababu ya dhambi, mwasi wa kwanza wa amri takatifu za Mungu. Uadui wa Shetani juu ya Kristo
umeonyeshwa juu ya wafuasi wake. Chuki ile aliyokuwa nayo juu ya sheria ya Mungu, shauri lue
fake la udanganyifu, ambalo kwalo hufanya uongo kuonekana kana kwamba ni kweli, tena kwalo
wanadamu huongozwa wakakisujudia kiumbe badala ya Muumba: mambo haya yameonekana
tangu awali. Jitihada ya Shetani katika kueleza vibaya tabia za Mungu, na katika kuongoza
wanadamu wamdhanie Mungu kwa namna isiyo ya haki, hata wamwogope n kumehukia badala
ya kumpenda; jinsi ambavyo amejaribu kubatili amri ya Mungu, na lcuongoza wanadamu ili
wafikiri kwamba wamekuwa huru, tena ya kama haiwalazimu kufuata matakwa ya sheria yake;
jinsi ambavyo anawadhulumu wale wanaothubutu kuyapinga madanganyifu yake, haya ndiyo
mashauxi ambayo ameyafuata katika vizazi vyote... .
Katika vita kuu ya mwisho, Shetani atafanya namna ile ile, atakuwa n nia ile ile, tena
atakuwa n kusudi sawa na file alilokuwa nlo tangu zamani zote za kale. Mambo yaliyofanywa
zamani yatafanywa tena, isipokuwa mashindano yajayo yatakuwa niakali mno jinsi isivyokuwa
duniani tangu awali. Madanganyifu va Shetani yatakuwa werevu zaidi, mashambulio yake
yatakuwa magumu zaidi, kama yamkini, atawapoteza hata wateule wa Mungu. (Soma Marko
13:22, na Mathayo 24:24). . . .
Kusudi la kitabu hiki siyc kuonyesha mambo mapya hasa juu ya siku za kale, ila kueleza
mambo ya hakika yanayohusika na mambo yajayo. Walakini, yakitazamiwa na kufikiriwa jinrsi
yalivyo sehemu ya shindano baina ya nguvu za nuru na za giza, mambo haya ya zamani huone-
kana kuwa na maana mpya; kwa ajili yake nuru inaangaza siku zijazo, ikimulika njia yao ambao,
kama watengezaji wa zamani wa dini, wataitwa, hata kwa kujihatarisha maisha, wawe mashahidi
kwa ajili ya "Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu." Ufunuo 1:1.
Makusudi ya kitabu hiki ndiyo kufunua mambo ya shindano kuu baina ya kweli na
uongo; kudhihirisha hila za Shetani, tena namna anavyoweza kushindwa; kueleza habari za uovu
jinsi ulivyo, kuonyesha chanzo cha dhambi na jinsi itakavyomalizwa, na kueleza mambo haya
kwa namna ya kufaa kwa kudhihirisha haki na wema wa Mungu katika yote awatendeavyo
wanadamu; na kuonyesha sheria yake jinsi ilivyo takatifu na isivyobadilika; haya ndiyo makusudi
ya kitabu hiki. Tena ombi la mwandishi ndilo hili: ili, kwa mvuto wa maneno yake, watu wapate -
kuokolewa katika nguvu za giza, wapate kustahilishwa "kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu
katika nuru," kwa sifa yake aliyetupenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yetu. (Kol. 1:12; Gal. 2:20.)
Ellen G. White

You might also like