Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 13

_Tunaanza somo letu kwa Kisa Cha tukio ambalo lilipangwa makusudi wakati Kristo akiwepo duniani,

Biblia inasema;*_👇🏽👇🏽

_*Luka 8 43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili,
[aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,*_

_*Luka 8 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake
kulikoma.*_

_*Luka 8 45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana
mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.*_

_*Luka 8 46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.*_
_*Luka 8 47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka
mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.*_

_*Luka 8 48 Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.*_

: 👆🏾👆🏾 _Hakuna Jambo ambalo Yesu alilifanya bila kusudi wakati wa ujio wake wa kwanza, Na katika kila
tukio YESU alikusudia 1. KUMFUNUA BABA, NA 2. KUJIFUNUA YEYE NI NANI._

[: _Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12 hakuwahi kujua kwanini WAGANGA NA WATAALAMU
wa dawa hawakupata ufumbuzi wa tatizo lake HADI SIKU ALIPOKUJA YESU NA KISHA MWANAMKE
KUGUSA PINDO LA VAZI LA YESU. Tukienda katika agano la kale na kisha unabii tutaona ni aina gani ya
kutokwa damu kulimtokea huyu mwanamke._

_*"Mambo ya Walawi 15 25 Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika
majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za
kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu
najisi.*_

_*Mambo ya Walawi 15 26 Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama
kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa
kwake.*_

: Biblia ya KING JAMES VERSION inasema kuwa "ALIKUWA NA TATIZO LA DAMU"

_*KJV Luke 8

43 And a *woman having an issue of blood twelve years, which had spent all her living upon physicians,
neither could be healed of any,*_

_*Na katika Walawi 15:25 inasema KUHUSU KUTOKWA DAMU YA HEDHI AU "Menstrual blood" ambayo
ilifikia mahali ilikuwa NJE YA MAJIRA YA KAWAIDA KWA MWANAMKE KWA MIAKA 12.*_

: 👇🏽👇🏽

KJV Leviticus 15

25 And if *a woman have an issue of her blood many days out of the time of her separation, or if it run
beyond the time of her separation; all the days of the issue of her* uncleanness shall be as the days of
her separation: she shall be unclean.

: 👆🏾👆🏾 _Swali, nini Yesu alikusudia kufundisha, Na kujifunua Yeye kuwa NDIYE ALIKUJA KUKOMESHA
KUTOKWA KWA DAMU YA MWANAMKE huyu?*_.
: _*Note: Kabla ya Mwanamke huyu kuponywa, Alianzia kuponywa BINTI ALIYEKUWA NA UMRI WA
MIAKA 12,*_.

_"Luka 8 :42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye *ni mwana pekee, umri wake amepata miaka
kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.*_

_Swali ni, Kwanini MIAKA 12? na kwanini wote NI WANAWAKE? hakuna jambo alilolifanya Yesu pasipo
kusudi_

_*POINT ZIFUATAZO ZIWEKENI KICHWANI*_.

1. *Wote ni wanawake.*

2. *Wote miaka 12 ya tatizo*.

3. *Mmoja suala la kutokwa DAMU*.

4. *Mmoja Tatizo la Kuzimia kwa muda mrefu* (KJV Luke 8

42 For he had one only daughter, about twelve years of age, and *she lay a dying.* But as he went the
people thronged him.

: 5. *aliyekomesha tatizo ni YESU naye "ALIKUFA BADALA YA yule binti na pia ALITOKWA DAMU
msalabani badala ya yule mwanamke aliyetokwa damu kwa miaka 12.*

: 👆🏾👆🏾 _*Matukio haya yalitokea kama vivuli, na upande wa pili yalikuwa na maana zifuatazo*_.

_*01. Mwanamke ni kivuli cha KANISA (Mwanzo 3:15).*_...

👇🏽👇🏽

[: _*"Mwanzo 3 :15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao
wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.*_

: 👇🏽👇🏽

: _*Nyoka aliwakilisha SHETANI, na Mwanamke (Eva) aliwakilisha KANISA LA MUNGU na wafuasi wote
watakaoshika Amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu!*_.👇🏽👇🏽
: _*Ufunuo wa Yohana 12 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao
wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya
mchanga wa bahari.*_

👆🏾👆🏾 _Joka, shetani alimkasirikia MWANAMKE na kufanya vita juu ya UZAO WAKE WAZISHIKAO AMRI ZA
MUNGU NA USHUHUDA WA YESU, swali Hawa wafuasi wataitwaje zaidi ya kuitwa KANISA LA MUNGU
maana kanisa ni watu!*_

_*Point ya 2. Tatizo la kutokwa Damu ilikuwa kivuli cha TATIZO LA KANISA TANGU ANGUKO EDENI
lilikuwa LINAISHI KAMA MGONJWA ALIYETOKWA DAMU MIAKA YOTE kwa kutoa KAFARA ZA WANYAMA
kila siku na Kila mwaka na wengine WALIANZA KUTAFUTA SULUHISHO LA DHAMBI kwa waganga na
masanamu ili waishi maisha ya amani na dhambi bila KUTOA KAFARA ZA WANYAMA LAKINI KANISA
LILIPASWA KUENDELEZA KAFARA ZA WANYAMA hadi KUJA KWAKE (MASIHI/KRISTO) ambaye alikuwa
ametabiriwa (KUKOMESHA TATIZO LA KUMWAGA DAMU YA WANYAMA TENA NJE YA MAJIRA, maana
yake Mwanamke (Kanisa) lilikuwa LINATOKWA DAMU kwa miaka Mingi HADI KUJA KUGUSA PINDO LA
KRISTO aliyekuja katika ubinadamu, Ndiyo maana YESU ALIPOGUSWA, NGUVU ZAKE ZILIMTOKA.*_

[: _*"Waebrania 10 2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha
kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?*_

_*Waebrania 10 4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.*_

: _*"Waebrania 10 9

ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe
la pili.

_*Waebrania 10 10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara
moja tu.*_

_*Waebrania 10 11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara
nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.*_

_*Waebrania 10 12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata
milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;*_

: 👆🏾👆🏾 _Kristo ALIKUJA KUKOMESHA kanisa lisiendelee KUTOKWA DAMU, na pia KANISA kuondolewa
katika hali ya MAUTI( Kama binti aliye lala kama mfu kwa miaka 12.*_

: _*Pia YESU HAKUJA KUTOA DAMU ya wanyama BALI ALIKUJA KUKOMESHA dhabihu ya wanyama KWA
KUJITOA YEYE KAMA KONDOO, na kisha Baada ya KUJITOA kama kondoo AKACHUKUA JUKUMU KAMA
KUHANI TENA kwa wakati maalumu, tutarudi kwenye DANIEL 8, tujue NINI MAANA YA MWANAMKE
ALIYETOKWA DAMU KWENDA KWA WAGANGA kwa miaka 12, Ambapo ndipo tutagundua kwanini
"WALIOANGUSHA NA KUPAKANYAGA PATAKATIFU WALIKUWA WAPAGANI na kwanini HATA
PATAKATIFU palihitajika kutakaswa maana mwanamke(KANISA) alikuwa bado anatokwa damu NA NJIA
YA UPONYAJI WA TATIZO ILIKANYANGWA NA WAGANGA Tena kwa gharama kubwa!*_.

[: 3. _*Kwanini miaka 12?*_.

: _*Tuchukue miaka 12 × (siku 360), utapata kuwa mwanamke alimwaga damu kwa SIKU 4,320*_.

: (kulingana na mwaka wa Kibiblia ambao una siku 360 tu, maana Ufunuo 11-2-4, miezi 42=1260).

*Biblia inasema kuwa YULE MWANAMKE aliponywa rasmi mwaka huo huo wa 12 au siku 4320 wa
kutokwa kwake damu,* nini maana ya haya?😇

_Turudi kwenye Danieli sura 8 kisha tutaziunganisha kwa pamoja._.👇🏽👇🏽

: _*"Danieli 8 1

Katika mwaka wa tatu wa *kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi,* naam, mimi
Danieli, baada ya hayo yaliyonitokea hapo kwanza.

_*Danieli 8 2 Nami naliona katika maono; ilitukia, nilipoona, nalikuwako huko Shushani ngomeni, katika
wilaya ya Elamu; nikaona katika maono, nami nalikuwa karibu na mto Ulai.*_

_*Danieli 8 3 Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume,
mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile
iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.*_

[: 👆🏾👆🏾 _Kipindi hiki Danieli na waebrania wengi walikuwa utumwani bado, na utumwa wao ULIDUMU
KWA MIAKA 70, wakati huo YERUSALEMU ukiwa umevunjwa NA NEBUKADNEZA na HUDUMA YA
UPATANISHO ILIKUWA IMEKOMESHWA maana watu wa Yuda hawakuwa na mahali pa kutolea kafara
tena huko utumwani Babeli, kwa miaka 70, maono yalimtokea Danieli AKAONYESHWA WANYAMA
wafuatao!
1. *Kondoo dume!*.

*Danieli 8: 5-8 (KONDOO DUME, na maana yake iko kwenye Danieli 8:21).*

: 👇🏽👇🏽

*"Danieli 8 20 Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na
Uajemi

_Tuzingatie kwa umakini ni nini wanyama hawa walikifanya ili tujue ni yupi ALIYEPAKANYAGA
PATAKATIFU NA KUKAHITAJIKA KUTAKASWA, baada ya NYAKATI ZA JIONI NA ASUBUHI 2300 na zitaenda
kukutana na tukio la mwanamke aliyetokwa damu miaka 12, maana MWANAMKE ALIPONA KUTOKWA
DAMU LAKINI HAKUSAFISHWA UNAJISI WAKE maana kanuni ya MWANAMKE ALIYETOKWA NA DAMU
alipaswa baada ya DAMU KUKOMA, alipaswa kufanya utakaso pia.*_

_"Mambo ya Walawi 15 28

*Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia
siku saba, na baadaye atakuwa safi.*

Mambo ya Walawi 15 29

*Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa
hema ya kukutania.*
Mambo ya Walawi 15 30

*Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi,* na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; *naye
kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.*

: 👆🏾👆🏾 _*Mwanamke aliyetokwa Damu miaka 12, Baada ya kuponywa tatizo kulikuwa na hatua ambazo
YESU ALIENDELEA NAZO BILA yule mwanamke kujua, LAKINI YESU ALITEKELEZA kama mfumo ulivyokuwa
zamani, SADAKA YA KUTEKETEZWA akawa Yeye binafsi na Kisha HATUA INAYOFUATA ILIKUWA YESU
AWE KAMA KUHANI amfanyie Mwanamke yule UPATANISHO KWA AJILI YA KUTOKA DAMU YA UNAJISI
KWAKE.*

_Turudi Danieli 8:_

_*"Danieli 8 5 Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa
dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.*_

_*Danieli 8 6 Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama
karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake.*_

_*Danieli 8 7 Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume,
akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali
akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume
katika mkono wake.*_

: _Beberu aliwakilisha Nini? Biblia inajibu kuwa aliwakilisha UFALME WA UYUNANI!*_

_*Danieli 8:21 Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa
iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.*_

_*Danieli 8 :22 Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne,
falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.*_

_*Uyunani iligawanyika toka kuwa na MFALME MMOJA wakawa wafalme WANNE lakini si kwa nguvu
kama zake yuke wa Kwanza.*_.👇🏽👇🏽

: *katika UFALME WA UYUNANI, hapa ndipo chimbuko la kuwa na WAFALME WA KASKAZINI NA


KUSINI NA MAGHARIBI NA MASHARIKI, ILA kilichotokea Ni kwamba Wafalme wa Mashariki na
Magharibi WALIANZA UGOMVI MMOJA AKAMPIGA MWENZAKE NA KUMTAWALA, NA YEYE AKAJA
KUPIGWA NA MFALME WA KASKAZINI AKATAWALIWA ndipo zikabaki PANDE 2 TU, KASKAZINI NA
KUSINI, na kilichofanya ijulikane kaskazini na kusini Ni wapi NI BAADA YA HUO UFALME WA UYUNANI
KUGAWANYIKA PANDE NNE, KITUO CHA KATIKATI YAO ILIKUWA NI PALESTINA ambayo SI MBALI NA
YERUSALEMU.*_
_*"hapo katikati yalipita Mambo mengi na Wafalme wa Uyunani walirithishana wengi tu hakuwa
Mmoja, Baba akifa anamwachia MWANAE, Hadi ujio wa Ufalme namba 3. RUMI YA KIPAGANI.*_

: 👇🏽👇🏽_*Danieli 8, Inasema katika ufalme wa huyu BEBERU kuna kitu kilimtokea*_👇🏽👇🏽

Danieli 8 8

Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; *na badala yake
zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.*

Danieli 8 9

Na katika moja ya pembe hizo *ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa
magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.*

Danieli 8 10

Nayo ikakua, *kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota,
ikazikanyaga.*

Danieli 8 11

Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, *ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya
daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.*

_Pembe ndogo ILIINUKA JUU YA MNYAMA HUYO HUYO BEBERU kuonyeshwa kwamba iliinukia katika
eneo lile lile ambalo UYUNANI ILITAWALI.

_*Linganisha pia na Danieli 11:16,(Rumi ya Kipagani ilimpiga Mfalme wa KASKAZINI WA UYUNANI, Rumi
ya kipagani ndo ikatawala KAMA MFALME WA KASKAZINI TENA, na eneo la kaskani hiyo Ni SYRIA,
GREECE, MECADON, CIlICIA, MTO FLATI, HADI BABELI*_

: _*Swali ni nani ALIYEPAKANYAGA PATAKATIFU NA KWELI YA MUNGU?*_

: Danieli 8 12

*Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo
ikaiangusha kweli hata chini;* ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.

Danieli 8 13
Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, *Haya
maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata
lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?*

Danieli 8 14

Akamwambia, *Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu
patakapotakaswa.*

: 👆🏾👆🏾 _Pembe ndogo NDIYO (MFALME MWENYE USO MKALI AJUAYE MAFUMBO).*_👇🏽👇🏽

Danieli 8 22

Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne
zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.

Danieli 8 23

Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, *mfalme mwenye uso mkali,
afahamuye mafumbo, atasimama.*

Danieli 8 24

Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha
kustaajabisha watu, na kufanikiwa, *na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na
watu watakatifu.*

Danieli 8 25

*Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake;
naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa
wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.*

Danieli 8 26

*Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo;
maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi.*

:
Baada ya Pembe zile za Uyunani, na RUMI YA KIPAGANI ilifuatia RUMI YA KIDINI ambayo ilirithishwa
NGUVU ZA MAMLAKA NA KIJESHI juu ya dunia nzima na Hiyo ndiyo INAFANANISHWA NA MFALME
MWENYE USO MKALI, aliyefanya Vita na watakatifu na kupakanyaga patakatifu na kuondoa SADAKA YA
KUTEKETEZWA YA DAIMA NA KUPAANGUSHA PATAKATIFU na ili kutakaswa kwa patakatifu ZINGEPITA
NYAKATI ZA JIONI NA ASUBUHI 2300! Tujue ni Miaka ipi hizi *FALME ZILITAWALA NA tutaona RUMI YA
KIDINI(Upapa) uliiangusha kweli na KUPOTOSHA HUDUMA YOTE YA UPATANISHO KWA MIAKA MINGI?*

Danieli 8,
1. *KONDOO DUME (umedi na uajemi 539-331 BC),*.

2. *BEBERU (UYUNANI - 331 BC.-168, .*.

3. *Rumi ya kipagani (168 BC- 476 A.D) KISHA PEMBE NDOGO (538 A D -1798 A.D).*.

_*Patakatifu paliangushwa na RUMI YA KIDINI, (pembe ndogo) Sio na Kondoo dume, Na hivyo
TUJIULIZE NI LINI RUMI ILIPAANGUSHA PATAKATIFU, Ni tangu kabla ya UJIO WA KRISTO Rumi ya
kipagani aliikuta Yesu IKIWA INAFANYA VITA NA WAYAHUDI na kuwatia chini ya kongwa la utumwa.*.

*70 A.D Rumi ya kipagani ilivunja MJI NA HEKALU LA YERUSALEMU, mwaka 68 A.D Mfalme NERO
ALIANZA KUWAUA MITUME Hata mtume PAULO akiwa mtume wa kwanza kuuliwa na Rumi, ukiachana
na Stefano aliyeuawa na wayahudi waloikataa injili, na KISHA RUMI YA KIDINI ILIKUBALI MATAKWA YA
RUMI YA KIPAGANI NA KWELI IKAANGUKA, ibada za KIPAGANI, MAOMBEZI KUPITIA WAFU( makabuli ya
watakatifu, Ibada ya JUA, Ibada ya Shanga, ibada ya MSAMAHA KUPITIA MARIA (BADALA YA KRISTO
KAMA MPATANISHI (hii ndiyo HUDUMA YA SADAKA YA DAIMA iliyofanyika kuanzia siku ya Sabato ya
siku ya 7 hadi juma zima watu walipaswa kuishi kwa toba na msamaha kupitia KRISTO, lakini RUMI
ILIONDOA, NA KWELI IKAANGUSHWA.*_

: _*Huu ULIKUWA MWENDELEZO TU WA KUNAJISIWA KWA PATAKATIFU PA DUNIANI NA MBINGUNI


maana BABERI NAYO ILILIVUNJA HEKALU LA YERUSALEMU kwasababu ya maovu ya watu wa
Yerusalemu. Na hivyo, DHAMBI + UHARIBIFU + KUINGIZWA KWA MAFUNDISHO YA KUPOTOSHA
HUDUMA YOTE YA PATAKATIFU NA RUMI ilihitajika KUJULIKANA NA LINI PATAKATIFU
PANGETAKASWA.*

_*"Na Mungu alitafuta sasa NI NANI ATAENDA KUPATAKASA? NA ATATUMIA DAMU YA NANI?*_.....
_Biblia inasema!👇🏽👇🏽

_*"Kama vile huduma ya Kristo ilipaswa kuwa na sehemu mbili kuu, Kila moja ikichukua kipindi cha
muda na ikiwa na mahali maalumu katika patakatifu pa Mbinguni, Hivyo hudumu ya mfano ilikuwa na
sehemu mbili, HUDUMA YA KILA SIKU NA HUDUMA YA KILA MWAKA, na kwa kila moja chumba chake
katika hema kilitengwa. (Counsels for the Church. uk.347. 6).*_

_*Huduma ya kila siku(Daima) ilifanyika kila SABATO, au maarufu kama UPATANISHO WA KILA SIKU
uliokuwa ukianza upya kila Siku ya Sabato ndipo mikate ya wonyesho ilibadilishwa na kuwekwa mipya na
PIA ILIKUWA SABATO ZA KILA MWAKA, ambazo zilikuwa upatanisho wa kufunga mwaka.*

BAADA YA WAKRISTO KUHAMISHWA TOKA SABATO YA SIKU YA 7 hadi KUANZA KUABUDU JUMAPILI
(siku ya jua) hata ufahamu wa Upatanisho wa daima ULIKANYAGWA, na katika siku za mwisho ni
marudio tu,
_*"Kama vile Kristo katika kupaa kwake alionekana katika uwepo wa Mungu kuwasilisha damu yake kwa
niaba ya waaminio wanaotubu, ndivyo kuhani katika huduma yake ya kila siku(daima) alinyunyiza damu
ya dhabihu katika patakatifu kwa niaba ya mwenye dhambi." (Counsels for the church. uk.347.7).*_

_*Swali, BAADA YA RUMI KUPOTOSHA HUDUMA YOTE YA PATAKATIFU, Hatua ambazo MUNGU
Alizifanya ili KUREJESHA MSINGI HUO, Biblia inasema INGECHUKUA NYAKATI ZA ASUBUHI NA JIONI
2300.*👇🏽

: _*Gabrieli malaika Akaja kumfafanulia DANIELI KUWA KUTAKASWA KWA PATAKATIFU KUTAANZA KWA
KUJENGWA UPYA KWA YERUSALEMU maana UTAKASO WA PATAKATIFU ULIPASWA UANZE KWA
KAFARA YA DHAMBI YA KUTEKETEZA, sasa KAMA HEKALU limevunjwa je, Watatakasia wapi, NA
ANAYEKUJA KUKOMESHA DAMU YA WANYAMA apate kujulikana.

_*"Danieli 9 21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi
hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.*

Danieli 9 22

*Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.*

Danieli 9 23

*Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa
sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.*

Danieli 9 24

*Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, *ili kukomesha
makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia
muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.*

_Gabriel alikuja kufafanua HATUA ZA UTAKASAJI ZITAKAVYOKUWA NA MUDA WA KUANZA, Kama


utakaso wa HEMA ENZI ZA HARUNI Zilianza kwa KUTOA SADAKA YA UJUMLA KWANZA ndipo huduma
iliendelea ndivyo pia YESU ALIANZIA KUFA MSALABANI,_.

Get Ready! 🦙🐑: _*Gabrieli anasema, MAJUMA 70 yameamriwa juu ya WATU WAKO, NA JUU YA MJI
MTAKATIFU,

01. *KUKOMESHA MAKOSA.*

02. *KUISHIRIZA DHAMBI.*


03. *KUFANYA UPATANISHO KWA AJILI YA UOVU.*.

04. *KULETA HAKI YA MILELE.*.

05. *KUTIA MUHURI MAONO NA UNABII.*.

06. *KUMTIA MAFUTA ALIYE MTAKATIFU*.

👆🏾👆🏾Hapa ndipo tutapata ukweli wa wazi. tupumzike, na tuombe, Mungu atupe kiu ya kujua kutakaswa
maisha yetu kabla ukuta haujaandikwa "MENE MENE TEKEL NA PERES" Mungu atubariki na atulinde
usiku huu.

You might also like