Professional Documents
Culture Documents
Imba Wimbo Wetu0001
Imba Wimbo Wetu0001
MBELE YA KUENDA
(Descente du drapeau) Kiro chante p.4
Mbele ya kuenda
Tushushe bendera !
Ikashuke ndani ya roho amini
Iko nguvu, furaha,
Na Baraka kwa wakiro !
2
37
Ulie katika……………………..
(Ao : ulie mu inchi ya…………….)
Mwito wetu kwa Kristu Mfalme !
Mfalme!
Tumfuate, tumsifu popote Mfalme
Waaskari wake wema
Tutalia popote na nguvu
Kama Kristu ni Mfalme wetu.
Tipige tarumbeta (trompette) za Mfalme :
Zilie kitumaini.
Sisi wakiro, tayari kweli
Kwa Mfalme wetu, Kristu !
KATIKA UMOJA
(Collections pilote) Kiro chante p.12
Na dunia nzima
Mipaka yaondoshwe,
Umoja ubakie !
MAMA MWEMA
(Noble Dame) Kiro chante p.6
KUJA NDUGU
(Viens, ami, prends place dans la ronde)
Kiitikio
6
37
Tukionya uaminifu,
Marafiki watakuja ;
Tutazidi pamoja
Mapigano kwa Mfalme !
Tuonye, marafiki,
Uhodari katika vita !
Utashi wa uaminifu
Kumpigania Kristu mfalme !
NDIYO CHEFU
Kiro chante p.14
Namtumainia chefu :
Ni rafiki mu mapigano.
Ataonyesha mfano :
Hataweza kujifanya mtumwa !
Kiitikio
8
37
Wewe ulinitolea
Maisha yako ya kijana.
Sababu sikupoteza
Uhodari wangu wa roho.
MUONE WANA-NGOMA
(L’écuyer chante) Kiro chante p.15
Muone wana-ngoma
Wenzetu wema.
Tunapendana sana
Twaimba popote.
Kiitikio
Mutazame pennon zetu,
Halihi, halihe, haliho !
Kundi letu linafurahi :
Hali, halihe, haliho !
Mucheze bila woga,
Wenzetu wema.
Tufuate mwendo mwema
Pamoja na Savio !
TWAJUA WANA-NGOMA
(Voyez les écuyers) Kiro chante p.17
Twajua wana-ngoma
Wakati wa mwendo
Walia na kusema :
“siwezi kufuata !”
Lakini kila Kiro
Apima kufuata.
Kiitikio
Donn, donn, donn, diridonn
bis
Donn, donn, diridonn
Lakini mwana-mkuki
Azani : « ni nzuri. »
Anajikaza kabisa ;
Siwezi kumfuata.
Mikulu yake mirefu ;
Lakini nguvu ni wapi ?
Muone mwana-ngao
Wakati wa mwendo.
Acheka siku zote
10
37
Hajui hatari.
Na kila mtoto ndugu
Anayempenda sana.
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha !
Nyimbo zetu zaleta furaha
Ha ha ha ha ha ha ha !
Tutaingia misituni
Wana-ngao wa Kiro.
Tutacheza pale vema
Na furaha kabisa.
Ee we, rafiki ukipenda
Kuingia ku Kiro
Utasema mbio sana
Sitatoka kabisa.
Tunaporudi mangharibi
Tutachesa zaidi.
Kila siku kwetu nzuri
Inajaa furaha.
Sababu ya furaha hii
Ni usafi wa roho
Wote wanaweza kuja
Na kupata furaha.
WAKATI VIJANA WAKIIMBA
Kiro chante p.20
Wakati vijana wakiimba
Pamoja nami na wewe,
Bendera yetu yatukokota
Katika mwendo njiani.
Kiitikio
Najua vijana hodari
Karibu bendera yetu
bis
Watabaki wamini popote
Wengine wakituacha.
Wakati wakiro watembea
Kwa nguvu ya uaminifu,
Wachefu wetu watatuonya
Mifano yao popote.
RAFIKI HODARI
12
37
Kiitikio
Unipe mkono,
Popote njiani.
Tutaimba na furaha,
Tataimba na furaha
Rafiki, na furaha
Twende kwa ushindi,
Juani na pa baridi
Kwa kristu wetu mfalme !
Nampenda Rafiki: ni mwamini !
Na moyo wake ni ngao nzuri,
Tayari kulinda inchi yetu,
Atashindana na kicheko kweli. (bis)
MISITU YATUITA
(Déjà sont revenus) Kiro chante p.23
Kiitikio
Kamata mfuko na vitu vyako.
Katika furaha twendeni porini.
Usiogope rafiki :
Wakiro wako hodari.
Maua yananuka kando yetu.
Uzuri wao musangae.
Angalieni : Mungu yuko mwema.
Atutolea mwanga na yote !
Yetu daima :
Yarukokota, yataonyesha
Mwendo wetu
Katika maisha yote.
Bendera, peperuka!
Tutakufuata.
Tupo tayari wote
Kukupigania.
Kristu atatulinda
Katika vita !
TUKITOKA NA NGOMA
(Écoutez notre joie) Kiro chante p. 25
Kiitikio
Ona jua juu,
Na wakati mzuri,
Na kicheko chetu
Midomoni mwetu.
Tunapenda kucheza na marafiki
Na watoto wamini wa kundi letu.
Kwa wakiro maisha mazuri sana
Na ujana ni mfano wa furaha.
KUJENI MBIO
(Allons les gars…) Kiro chante p.26
Kiitikio
Nia yet(u) ni moja tu kwetu,
Ni nia ya kila Kiro !
Kumtum(i)kia Kristu Mfalmewe,
Vitani kuona hodari !
Tazama mwendo wa Kiro,
Sangaa nguvu yake.
Katika njia za inchi
Waimba heri wao (bis)
Wengine wakitufuata
Wataona furaha nasi
Fuateni wote watoto
Mpaka ushindi mkubwa (bis)
TUFUATE BENDERA
(Ami, la route est devant nous) Kiro chante p.29
Bendera inatangulia
Wakiro wafuata.
Upepo inacheza nayo
Tupende bendera.
SISI WAKIRO
(Pleins d’allégresse) Kiro chante p.30
Kipwa inapokaribia
Twasikia nguvu ;
Nguvu kubwa ya damu
Inatukokota inje.
Kiitikio
Twendeni wote wakiro
Fuateni bendera.
Wakiro wanapenda
Kuimba njiani ;
Twataka kundi lifike
Katika furaha.
Don Bosco awe mulinzi wetu
bis
Katika mwendo.
Tukirudi mangharibi
Twaonyesha kicheko.
Tukichoka kabisa
Hata moja halalamiki.
Mvua inatupigilia
Sawa fimbo kali
Hatuoni uchungu
Tunavumilia yote.
TUONGEZE MWANGA
(Plus de joie) Kiro chante p .32
NJIA YA WA KIRO
(La route que suivent…..) Kiro chante p.32
Njia ya wakiro
Ni njia nzuri sana.
Njia ya urafiki na furaha
Njia nzuri !
Kuja wewe rafiki,
Uunge kundi letu.
Njia ya wakiro
Ni njia nzuri sana.
Nyimbo za wakiro
Zinapanda hewani.
Nyimbo za urafiki wa jamaa
Nyimbo nzuri.
Imba wewe pia
Pamoja na wakiro.
Nyimbo za wakiro
Zinapanda hewani.
Tabnia ya Kiro
Tabia nzuri sana.
Tabia ya uwema na furaha
20
37
Tabia nzuri!
Usingoje rafiki
Kuunga kundi letu.
Tabia ya Kiro
Tabia nzuri Sana.
JUA LIKO JUU YETU
Kiro chante p.33
Jua liko juu yetu,
Ndege zinaruka.
Vipepeo na vidudu
Vinamsifu Mungu
Sisi pia tutaimba
Nyimbo zetu za aksanti !
Kiitikio
Sifu Kristu Mfalme wetu !
Beba bendera na furaha.
Kuja kwetu na ushindi,
Mwana-ngao wa Kristu !
Na wakati wa baridi
Mutaona Kiro !
Wakipita kwenu mbio
Na bendera mbele !
Wanapenda kujikaza
Kwa mapashwa ya vijana !
KESHO TUTAONDOKA
(Demain nous partirons) Kiro chante p.34
Na wakiro !
Kule adui atungojea ;
Ataka kutupiga na nguvu.
Strophe 1
Nyama, ndege, vidudu,
Nzige nyingi tena,
Zaimba bila neno
Mufalme Mwenyezi.
3
Inchi yetu………………..
Twakupenda kweli.
Kwa sababu wakiro
Watabaki kwako.
JUA LIKIANGAZA
Kiro chante p.37
Jua likiangaza vizuri
Maua yachanua porini.
Fungua vyepesi roho,
Moyo wako.
Uzuri huo usitupwe.
Kiitikio
Tembea njiani
23
37
Kiitikio
Tukimweshimu mlinzi wa Kiro
Tutamfwata katika mwendo
Hatutamwogopa adui
Savio atatukinga. bis
Fuateni furaha ya Savio
Mapendo na urafiki
Mutaona uzuri wa Kiro
Mukifuata mifano yake. bis
TUKITEMBEA
Kiro chante p.39
24
37
Tukitembea tunafurahi
Tunapoimba watu watusangaa.
Misitu, milima yajibu nyimbo
Uzia ukiwa hatusimami.
Kiitikio
Maisha mazuri
Katika ujana.
bis
Bendera yetu
Yapiga zamu !
Tukichukua bendera zetu
Katika wimbo : nguvu na furaha.
Tusiwe na woga, twendeni mbio
Kushinda dunia kwa Kristu Mfalme.
WAKIRO WAIMBA
(Les bandes Kiro que de joie) Kiro chante p.40
25
37
Kiitikio
Kicheko usoni na kusudi bora
Ukarimu utatuongoza
Na tutafana na Don Bosco
Tukifurahi, tukifurahi,
Tutashinda wote, tutashinda wote
Kwa kicheko chetu. bis
Juni valle…
Waingia…
Vijana musikie
Katika furaha aminifu
Munapashwa kukokota
Wengine wengi bis
Juni valle…
Munapashwa…
WATU WOTE KUJENI
(Admirez le Kiro) Kiro chante p.44
Tunapenda kutembea
Tukiimba nyimbo.
Tunajua kama leo
Ni wakati mzuri.
Kiitikio
Tembea Kiro,
Bila mashuruli.
Beba bendera
Kwa Kristu !
Kama mfuko uko mzito
Tusionye uchungu.
Moyo wetu utabaki
Na furaha daima.
Mangharibi tukirudi
Tunachoka sana.
Siku ilikuwa nzuri
Twimbe tena pamoja.
KUJA NASI RAFIKI
(Viens avec nous) Kiro chante p.46
Vuteni makasia
Na nguvu ya wimbo.
Mtumbwi wetu ukifika
Tutasahau teso.
Kiitikio
Ohe rafiki (Ohe rafiki)
Twende rafiki (Twende rafiki) bis
Funga nguo ya mtumbwi
Bendera juu kabisa.
Imbeni wote wakiro
Nyimbo zenu za furaha
Tukiziimba vizuri
Tutajulisha Kiro.
Zamani mu Italia
Padri mmoja alifika,
Kwa watoto waliokuwa
Na hatari kubwa sana.
Leo pia anakuja
Akalinde watoto
Weusi na weupe
Wamupende Mungu mwema.
Kiitikio
Don Bosco utupe baraka yako
31
37
TEMBEA NJIANI
(Quittant les rues de nos cités) Kiro chante p.50
Wa Kiro tusisahahu
Kicheko nyumbani.
Popote tunapitamo
Tulete furaha.
Na uhorari wa Kiro
Ni kitu cha ajabu.
Wapata uzuri wote
Karibu na Kristu.
Kiitikio
Trala tralalalala
Trala tralalalala lalalala
Tralala tralala lala !
Sikia msemwa wa kwanza ; ni : tralala…
Habadiliki kabisa ; ni : tralala…
WANA-NGOMA, WANA-NGAO
(Vois la route) Kiro chante p.52
Wana-ngoma, wana-ngao,
Wana-mkuki wa Kiro,
Tutakuja, tutashinda
Tukipiganiamo.
Kiitikio
Holai, holao,
Holai lai lai lai lao bis
(1° fois : hilalala !)
Marafiki, twatembea,
Tunaimba na furaha,
Kila siku ni zawadi
Mungu mwema kabisa !
Marafiki tukicheza
Na wenzetu wa Kiro,
Kila moja atasema
Kiro : kundi nzuri mno !
Na kiisha tukirudi
Kwa wazazi nyumbani,
Bila shaka watesema :
Mtoto ni muzuri, oh !
Rafiki utabeba
34
37
Kiitikio
Katika vita tuwe hodari
Twataka kushinda.
Hodari wakiro,
Musiache kupigana.
Rafiki utashinda
Adui, adui mu vita.
Popote utaonyesha
Uwema, uwema wa Kiro.
Rafiki utumaini
Daima, daima kwa Kristu.
Sababu unafahamu
Uwezo, uwezo wa Mfalme.
Rafiki usisahau
Imara, imara ya Kiro.
Wakiro watatolea
Maisha, maisha kwa Mfalme.
BANS CHANTES
1. Bravo, bravo, bravo,
Bravissimo !
Bravo, bravo, bravissimo!
Kiro chante p.15
2. Brabrabra bravo !
Brabrabra bravo!
Bravo, bravo, bravo, bravo !
Kiro chante p.16
Wana-ngao kujeni
Kuonyesha nguvu !
Wapenda kucheza
Na kufanya mzaha !
Na wale wakubwa,
Wana-mkuki wetu !
Marafiki wamini,
Wacheza nguvu !
Wachefu wa Kiro,
Hodari sana !
Hawachoki kabisa
Wakichunga mchezo !
Munajua jamaa
Ya Kiro yetu !
36
37
Mukitaka kufuata
Mutapata heri.
37