Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 48

MAMA YANGU NI JINI

Kimeandikwa na

IRENE MWAMFUPE NDAUKA

Tunapatikana kwenye namba hizi;


0655 207520

Barua pepe; oshani@yahoo.com

HUTOLEWA NA KUSAMBAZWA
NA A $ S DESIGNING
SIMU: 0713 335560
0788 943433
DAR ES SALAAM
TANZANIA

ONYO

Hahiruhusiwi kuchapa kitabu hiki au kunakiri chochote kutoka kwenye


kitabu hiki bila idhini ya mwandishi. Hatua kali zitachukuliwa kwa
atakayekiuka onyo hili.

1 mama YANGU NI JINI


UTANGULIZI
Baada ya kutoka masomoni nje ya nchi, Damas Ndomba anapata msiba
mzito wa kumpoteza mwanamke wa maisha yake aitwaye Jennifer.
Kutokana na utata wa kifo hicho, Damas anashindwa kuamini, lakini
anapelekwa makaburini kutembelea kaburi la mahabuba wake, Jennifer.
Huko wanakutana na mauzauza .
Hali hiyo inamchanganya na kuamua kurudi nyumbani. Anamsumulia
mama yake mzazi ambaye ndiye kiini cha mkasa huu. Mama yake
anacheka kusikia hayo mauzauza hali inayomshangaza Damas.
Sasa endelea mwenyewe...

2 mama YANGU NI JINI


Naitwa Damas Ndomba, ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika
familia ya mzee Ndomba wa Mbeya, Ruvuma. Nimejitolea kwa ridhaa
yangu kutangaza mkasa huu baada ya kufuatilia mikasa mingi kwenye
magazeti. Nilipoambiwa kuwa, picha yangu haitatumika kwenye gazeti,
nilikubali kuweka wazi kisa hiki ambacho naweza kusema sehemu
kubwa kimejaa misisimko badala ya majonzi.
Lakini mbaya zaidi kwa sasa kila ninapokumbuka tukio zima, nashikwa
na woga hali iliyonifanya nioe haraka ili niwe naishi na mwenzangu
ndani ya nyumba,” ndivyo anavyoanza kusimulia, Damas Ndomba.

KISA KINAANZA AGOSTI, 2007, NJOMBE-IRINGA

Nilikuwa mfanyakazi kwenye ofisi moja ya Serikali Wilaya ya Njombe,


mkoani Iringa (kwa sasa Njombe ni mkoa). Naweza kusema kwa
akili nilizojaliwa na Mungu, wakuu wangu wa kazi walinipenda sana,
wakawa wanasema ikitokea nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi, mimi
nitapewa kipaumbele.
Kauli hizo kutoka kwa mabosi wangu zilizidisha ari yangu ya kuchapa
kazi kwa bidii nikiwa sitaki utani wala vitendo vya kupoteza muda.
Kweli, miaka miwili baadaye, yaani mwaka 2007 nilichaguliwa au
niseme nilipendekezwa kwenda kusoma miaka miwili nchini Sweden
kwenye Chuo Kikuu cha Trust (University of Trust) ambacho kipo kwenye
Jiji la Stockholm ambalo pia ndiyo mji mkuu wa Sweden.
Nilifurahi sana kwa uteuzi na mapendekezo hayo. Wakati huo nilikuwa
sijaoa, niliishi peke yangu. Barua yangu ya utauzi wa kwenda kusoma,
ilinielekeza kuwa, natakiwa kujiandaa kwa wiki mbili tu, mpango wa
tiketi na viza ya kusafiria vilikuwa vinashughulikiwa na ofisi. Nikiwa
ndani ya maandalizi ya safari, nikapokea taarifa kutoka kwetu kijijini
kwamba, mama yangu mzazi anaumwa sana. Yupo hoi.
Nilitaka kuamini kwamba, huenda Mungu hakupenda mimi nisafiri,
maana kama mama anaumwa tena yu hoi, mimi nitasafirije? Si watu
watanishangaa! Ilibidi nifunge safari kwenda kijijini kumwona mama.
Lakini pia, nilisema kama nitakuta anaendelea vizuri, basi ningetumia
muda huo kuwajulisha kuhusu safari yangu ya Ulaya.
Nilikwenda kijijini. Na kweli nilimkuta mama anaumwa, lakini

3 mama YANGU NI JINI


nikaambiwa hali yake kwa siku mbili zile haikuwa kama awali, siku tatu
nyuma. Alikuwa anaendelea vizuri. Nilimwambia baba kuhusu safari
yangu, akaunga mkono na kunitakia safari njema na masomo mema pia.
Akaniambia anaamini mama atakuwa sawa zaidi hivyo nisiwe na wasiwasi
wowote.
Mdogo wangu wa kiume aitwaye Henry, aliniambia nikirudi kutoka
masomoni atapenda kuja Njombe kuishi na mimi ili kubadili mazingira.
Yeye kule kijijini alikuwa mkulima na alikuwa hataki kubadili tasnia hiyo
ambayo ilikuwa ikimzeesha haraka na kuanza kuonekana kama yeye
ndiyo mkubwa kwangu.
Baada ya siku tatu, nilirudi Njombe kujiandaa na safari ambapo zilibaki
siku tano tu kuondoka kuelekea nichini Sweden.
Siku ya safari yangu nilisindikizwa na msichana mmoja wa ofisini kwetu,
anaitwa Yasinta. Yasinta alipenda kuniita kaka na mimi nikawa namwita
dada. Kwa sababu wote tunatoka mkoa mmoja wa Ruvuma. Basi, wakati
nakwenda kupanda basi Njombe ili kuelekea Dar es Salaam, Yasinta
aliniambia:
“Kaka Damas, naamini Mungu kwamba, utakaporudi kutoka masomoni,
utakuwa si mtu wa kawaida. Sijui kwa nini naamini hivyo.”
Mimi niliguna tu halafu nikaingiza akilini maneno ya dada Yasinta.
Moyoni nikawaza:
“Au nitakuwa mtu mkubwa kazini nini? Lakini sawa, kwa jinsi mabosi
wangu wanavyonipenda na hivi ninavyokwenda kusoma, lazima
watanipandisha cheo na mshahara pia. Tena huenda nikapewa na
nyumba ya kulipiwa na ofisi.”
Niliingia Dar es Salaam saa kumi na mbili jioni. Nikafikia katika hoteli
moja ya Harare Inn kwa vile safari ilikuwa saa kumi na moja alfajiri ndiyo
nilitakiwa kuondoka nchina Tanzania.
Usiku wa siku ulikuwa mgumu sana kwangu. Nasema ulikuwa mgumu
sana kwani nilimkumbuka sana mama yangu, hasa kuhusu ugonjwa
wake. Picha yake kichwani kwangu ilikuja ile ya siku naondoka kijijini.
Nakumbuka mama akiwa kitandani, aliniambia:
“Damas mwanangu, nitakuombea sana kwa Mungu. Yeye ni mwema
atakujalia. Ukinikuta hai ni mapenzi yake, usiponikuta pia ni mapenzi yake.
Kwa sababu sisi binadamu tulitoka kwake hivyo hivyo kama tulivyotoka,
hatuna budi kutudi. Hakuna anayetoka halafu asirudi.”
Moyoni niliazimu kuwa, nikifika Sweden, lazima nihakikishe naifuatilia
kwa karibu hali ya mama yangu.
4 mama YANGU NI JINI
Mwishowe nilipitiwa na usingizi mzito sana. Sasa nikiwa usingizini,
nikaota ndoto hii; nimefika salama nchini Sweden. Halafu nikarudi salama
Tanzania. Siku moja nikalala Njombe, kesho yake nikaenda nyumbani,
kijijini, Mbinga kuwasalimia wazazi wangu. Nilimkuta mama amenenepa
sana. Amenawiri sana. Ana afya njema baada ya kupona ugonjwa wake.
Nilifurahi sana kwani hata yeye mama aliponiona alifurahi kama
nilivyofurahi mimi.
Mama: “Mwanangu Damas, umerudi salama?”
Mimi: “Nimerudi salama mama, vipi hali yako?”
Mama: “Mwanangu mimi naendelea vizuri kama unavyoniona.”
Wakati najibizana na mama, alinifuata ili kunilaki huku akiachia tabasamu
pana lililomfanya aonekane kama bado msichana.
Ghafla nikashtuka kutoka katika ndoto hiyo. Jasho jembamba
lilinichuruzika licha ya kwamba kipindi hicho Dar kulikuwa na kibaridi.
Moyoni nikasema:
“Hii ndoto siyo bure. Kijijini hakuna usalama hata kidogo. Hii ndoto ni
ujumbe kwangu.” Niliangalia saa ilikuwa saa kumi alfajiri. Nikajiandaa
haraka haraka na kutoka.
Nilichukua taksi kunipeleka uwanja wa ndege. Sasa nikiwa njiani, nikawa
nawaza kuhusu ile ndoto. Nilijiuliza kwa nini nimuote mama ana afya
njema na amenawiri wakati nilimwacha akiwa mgonjwa?
Nilianza kufuatilia kumbukumbu za ndoto zangu, kwamba mara nyingi
nikiota vipi inakuwa vipi! Lakini sikupata jibu kwani nilijifunza kwamba,
kuna wakati naota kinyume na ndoto, wakati mwingine naota sawasawa.
Hutegemeana na siku ninayoota.
Nilimwambia Mungu anisaidie na safari yangu amsaidie na mama,
apone haraka, nimkute salama salimini au bukheri wa afya.
Mawazo yakahamia katika hali inayonikabili. Kwamba, nakwenda
kutengana na watu niliuowazoea. Watanzania wenzangu. Pia, nilijua
nakwenda kuikosa nchi yangu pendwa ya Tanzania. Mwisho nilimkumbuka
sana mpenzi wangu aitwaye Jennifer ambaye siku naondoka Njombe,
yeye alikuwa kwao, Kyela, Mbeya.
Nilifika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo
niliulizia taratibu zote kwani nilitakiwa kuondoka nchini na usafiri wa
Shirika la Ndege la Scandinavia (Scandinavia Air Ways).
Niliingia ndani ya ndege mapema sana. Katika maisha yangu, huwa
sipendi tabia ya kujipa hofu na wasiwasi, hasa kwenye maswala ya

5 mama YANGU NI JINI


kusafiri, iwe kwa basi au treni. Pia niseme ukweli kwamba, ilikuwa mara
yangu ya kwanza mimi kupanda ndege. Sikumbuki vituo mbalimbali
ambavyo ndege yetu ilipitia, ila kikubwa ni katika Jiji la Athens nchini
Ugiriki wengine hutamka Greece.
Saa kumi na moja ya alfajiri iliyofuata, tuliingia kwenye mji mkuu wa
nchi ya Sweden, Stockholm. Mwenyeji wangu alikuwa uwanjani hapo
kunipokea. Niliambiwa mwenyeji wangu atakuwa amevaa kikaratasi
kifuani kilichoandikwa Mr Humphrey Thomas-Trust University. Hivyo
ndivyo wanavyofanya wenzetu Wazungu.
Nilipomuona nilimfuata na yeye akaniuliza kama mimi ndiye Mr
Damas Mn’domba. Alishindwa kulitamka sawasawa jina la Ndomba.
Nilimwambia ni mimi. Akachukua nafasi hiyo kujitambulisha tena jina lake
na anakotokea licha ya kwamba karatasi la kifuani lilielekeza kila kitu.
Alinipokea begi moja katika mawili niliyobeba, tukaingia ndani ya gari
na kuondoka. Njiani aliniuliza swali moja tu ambalo niliamini lilikuwa
likimsumbua akili kwa muda mrefu sana.
“Mji Mkuu wa Tanzania ni Dodoma au Dar es Salaam?” (Aliuliza kwa
Kiingereza).
“Dodoma,” nilimjibu.
Akaniuliza kama nina uhakika. Nikamwambia kwa asilimia mia moja.
Safari yetu iliishia kwenye nyumba ambayo niliandaliwa kuishi hapo kwa
kipindi chote nasoma.
Kifupi nilikuwa nimeshafika nchi ya Sweden. Nchi yenye baridi kali
kuliko eneo lolote la Tanzania. Yaani Njombe haifui dafu kwa Sweden. Au
niseme nchi zote za Scandinavia ambazo ni tano, yaani Sweden, Denmark,
Holland (Uholanzi), Norway na Finland. Katika maisha yangu ya miaka
miwili nchini humo, jua nililiona mara zisizozidi kumi na tano.
Sweden kijiografia ipo Kaskazini kabisa mwa dunia, hivyo kulifanya
jua kuonekana kwa saa nane tu, tena mwonekano wake ni kama
unavyoonekana upinde wa mvua (rainbow). Jua nchini Sweden halipiti
utosini mwa kichwa cha binadamu kama ilivyo huku nchi za Afrika
Mashariki.
Basi, wiki moja baada ya kuanza masomo, nilianza kukumbuka nyumbani
Tanzania kwa ujumla wake. Lakini hususan kijijini kwetu, Mbinga. Na
hasahasa mama yangu mzazi, binti Ngomeleki. Nilichukua simu na kupiga
namba za baba lakini hakupatikana. Nilifuatilia majira ya kijiografia
nikagundua kuwa, muda huo nyumbani ilikuwa usiku mwingi.

6 mama YANGU NI JINI


NAANZA KUUGUA UGONJWA WA HOMA
YA NYUMBANI (HOME FEVER)
Wazungu wanasema mtu akiwa nje ya kwao, hasa kwa umbali wa nchi
au mkoa, hupatwa na ugonjwa unaoitwa Home Fever ambapo muda
mwingi mtu unajisikia mnyonge, unaonewa na au unahisi hupendwi na
wengine wanaokuzunguka kwa wakati huo.
Hii ndiyo hali ambayo ilinikumba mimi kwa siku za awali za kuwepo
nchini Sweden, baadhi ya wenyeji wangu walisema nitafute girlfriend
(demu) ambaye ni mwenyeji. Atakapokuwa bize na mimi kwa muda
mwingine atakuwa amenitibu tatizo langu au ule ugonjwa wangu.
Kweli, nilimtongoza msichana mmoja wa Kisweden (Swedish) anayeitwa
Julian. Huyu Julian, baba yake ndiye Msweden aitwaye Johnson, mama
yake ni Mmarekani, anaitwa Angeline. Huyu alikuwa akiishi mtaa wa pili
kutoka kwenye nyumba niliyokuwa nikiishi mimi. Nilikutana naye kwa
mara ya kwanza kwenye Pub inayoitwa Cool & Hot.
Uhusiano wetu ulinoga zaidi baada ya kuniambia kwamba, mwaka
2005 aliitembelea Tanzania na alipanda Mlima Kilimanjaro japo hakufika
kileleni. Pia aliniambia alitembelea Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro
Creater.
Nilifurahi zaidi aliponisimulia historia ya Ngorongoro Creater ambyao
mimi mwenyewe mwenye nchi nilikuwa siijui. Kwa mazingira hayo tu,
nilijikuta nakuwa nusu nyumbani Tanzania, nusu ugenini. Kwa kweli
nilimaliza au niseme nilipona Home Fever.
Siku moja nikiwa nakula mchana, simu yangu iliita. Nilipoangalia namba,
ilionesha call tu, hivyo nikajua ni ya nyumbani Tanzania. Nikaipokea.
Niliposema haloo, upande wa pili nikasikia sauti ikiongea Kiswahili,
sauti yenyewe kama ya mama yangu mzazi, binti Ngomeleki ikisema,
‘hujambo mwanangu Damas?’ Lakini kabla ya kujibu, nikawa najiuliza
kama kweli ni mama au la! Simu ile ikakatika. Nilipoipiga mimi haikuwa
hewani!
Nilibaki na maswali kibao. Nilijiuliza Ni kweli ile ilikuwa sauti ya mama
yangu mzazi niliyemwacha Tanzania anaumwa? Nilipata jibu kwamba,
kweli sauti ni yenyewe lakini ni katika mazingira gani aongee yeye mama
anayeumwa. Kwani kwa njia yoyote ile angetakiwa kuanza kuongea
mwenye simu kwa kujitambulisha kisha aje mama.
Aidha, nikataka kujiridhisha tena kama kweli ile ni namba ya nyumbani
Tanzania. Niliikagua upya. Cha ajabu sikuona namba iliyoingia (received

7 mama YANGU NI JINI


call). Nilishtuka kidogo, lakini baadaye nikakumbuka kwamba, namba
ikiwa call tu inawezekana isionekane kabisa.
Maisha ya masomo yaliendelea, uhusiano wangu na Julian ulipamba
moto kiasi kwamba, alisema nikirudi nchini Tanzania nije naye kwani
alitokea kuipenda sana nchi yetu. Pia, alinipenda sana mimi.
Kifupi ni kwamba, wanaume wa Kiswahili wanapendwa sana na
wanawake wa Kizungu. Kisa eti siyo wazito vitandani. Wanamudu
mambo!! Wanasema kuwa, wanaume Wazungu hawawezi kimudu
kitandani kwa nusu saa, labda awe amekunywa madawa. Wanaume wa
Kiswahili wana uwezo wa kudumu kitandani kwa mchana kutwa.
Basi, miaka miwili ya masomo ilikatika, nikahitimu masomo yangu.
Nilijiandaa kwa ajili ya kurudi nyumbani Tanzania. Nakumbuka Julian
alilia sana katika kipindi chote cha maandalizi ya mimi kuondoka ingawa
tulikubaliana kwamba, baada ya mimi kuondoka, itapita miezi miwili tu
naye atafuata.
Siku naondoka, Julian alikuja na baba yake uwanja wa ndege ambapo
kwa mara ya kwanza, mzee huyo ndiyo alinifahamu kwa macho. Lakini
mama yake alikuwa akinijua vizuri sana.
Tulisalimiana na mzee huyo, akasema amefurahi sana kumwona kwa
sura mwanaume anayemnyima usingizi binti yake. Kwangu ilikuwa aibu
kubwa hata uso wangu ulisinyaa kusikia hayo kutoka kwenye kinywa cha
baba mkwe, lakini kwa wenzetu, ni kitu cha kawaida sana.
Wakati nakwenda kwenye ndege, Julian alilia sana, baba yake
akamkumbatia akimbembeleza. Hatua zangu tano mbele, baba yake
aliniita, akanipa mkononi dola za Amerika (USD) 1200 (kama shilingi
milioni mbili kwa wakati huo). Nilimshukuru sana.

MAAJABU YANAANZA TANZANIA

NIlifika jijini Dar es Salaam baada ya saa 47 za kuwa angani na vituo


mbalimbali. Nililala kwenye hoteli ileile. Kesho yake nilipanda basi
kwenda Njombe ambako ningeripoti kazini nikiwa natokea masomoni
Ulaya. Mabosi kazini walikuwa wanajua kuhusu kurejea kwangu kutoka
masomoni.
Asubuhi nyingine nilikwenda ofisini ambako wafanyakazi wenzangu,
wakiwemo mabosi walinipokea kwa nderemo na shamrashamra za hali
ya juu, maana miaka miwili nilikuwa sipo Tanzania.
8 mama YANGU NI JINI
Kiasili mimi ni maji ya kunde, lakini kazini walinishangaa sana. Walisema
nimekuwa mweupe sana tena nimenawiri. Miongoni mwa waliyosema
hivyo ni dada, Yasinta. Ni kweli kabisa, nilikuwa numetakata. Baridi ya
Sweden inatakatisha ngozi tofauti na baridi ya Makambako au Mbeya.
Kwa muda wa kama nusu saa nilikuwa nikisalimiana na wenzangu
tu, mwishowe bosi wangu wa idara aliyeniunganishia safari akanitaka
nikapumzike kwa siku tatu ndipo nianze kazi rasmi na kwamba, nitapokea
barua ya kunifahamisha majukumu yangu mapya.
Nilifurahia sana ruhusa hiyo kwani ukweli ni kwamba, nilichoka sana.
Pia, niliona itakuwa nafasi yangu ya pekee ya kuwa na mpenzi wangu
Jennifer ambaye nilimmisi sana. Mpaka hapo, Julian kama alikuwa
anaanza kutoka moyoni mwangu.Sasa, ile natoka tu getini naangalia
kulia na kushoto, nikamwona mama yangu mzazi binti Ngomeleki. Moyo
ulilipuka liipu!!
“Haa! Mama! Shikamoo mama,” nilimsalimia.
“Marhaba mwanangu, za siku?”
“Nzuri mama. Vipi wewe hali yako mama?”
“Namshukuru Mwenyezi Mungu, umerudi lini mwanangu?”
“Mimi nimeingia jana mama.”
Kitu kimoja kilinishtua! Mama hajawahi kufika Njombe hata siku moja.
Hapajui Njombe. Hapajui kazini kwangu. Sasa alifikaje?
“Umekuja na Henry mama?” Nilimuuliza. Henry ni yule mdogo wangu
wa kiume niliyemtaja awali. Ingawa na yeye pia hajawahi kufika Njombe.
Niliamini amekuja na Henry kwa vile amesomasoma kidogo, hivyo
angweza kufika Njombe na kuulizia kwani licha ya kutowahi kufika lakini
alikuwa anajua nafanya kazi idara gani ya serikali.
“Hapana, nimekuja mwenyewe,” alijibu mama na hivyo kunichanganya
zaidi. Kwani wakati namuuliza kama amekuja na Henry, macho yangu
yalikuwa yakiangaza huku na kule nikiamini nitamwona huyo Henry.
“Haa! Mama...kuanzia Mbinga nyumbani?” Nilimuuliza kwa hamaki
isiyokuwa na umakini wowote.
“Eee! Kwani unadhani mimi sijiwezi? Najiweza mwanangu. Siwezi
kushindwa kufika hapa Njombe.”
“Mh! Nani amekupa ramani ya kufika mpaka hapa?”
“Mdogo wako,” mama alijibu kwa kujiamini.
“Henry?” Nilimuuliza.
“Henry ndiyo.”
9 mama YANGU NI JINI
“Alikupa ramani ya kufika mpaka hapa ofisini au stendi?”
“Mpaka stendi tu,” mama alinijibu pasipokuwa na shaka yoyote.
Moyoni nilikubali kwamb, Henry angeweza kumpa ramani mama
mpaka stendi tu. Si kiasi cha kumwambia kondakta wa basi huyu mama
yangu anashukia Stendi Kuu ya Njombe, lakinin siyo mpaka ofisini tena
getini!
“Sasa mama nani amekuleta hadi hapa ofisini? Na mbona upo peke
yako?”
“Nilipofika stendi nilianza kuulizia.”
“Kuulizia jina langu au la ofisi?” Nilimpiga maswali mengi mama ili
ukweli ujulikane amewezaje kufika ofisini kwangu?
‘La kwako.”
Nilimsikiliza mama kwa umakini mkubwa, maana sikuamini kama
angeweza kunipata kwa kutumia kuniulizia kwa jina.
“Ikawaje sasa?”
“Kuna msichana anaitwa Jennifer, akasema anakufahamu.”
“Jennifer!”
“Eee...na wewe unamjua?”
“Namjua mama.”
“Basi huyohuyo mwanangu, anasema alikuwa Kyela, Mbeya ndiyo
amerudi.”
Niliamini kwa asilimia mia moja sasa kwani Jennifer ni mpenzi wangu,
wakati nasafiri kwenda masomoni alikuwa Kyela. Lakini nilishtuka
kusikia mpaka nimerudi ndiyo na yeye amerudi. Miaka miwili!!
“Sasa yuko wapi?”
“Tulipofika hapa getini, kakutana na kaka yake yuko mbio mbio,
alipomuuliza akasema baba yao mdogo amegongwa na gari amekimbizwa
hospitali kwa matibabu kwakuwa hali yake ni mbaya sana.”
Kusema ukweli kwa maneno hayo kulikuwa na sababu ya Jennifer
kumwacha mama na yeye kuondoka na kaka yake kwenda kushughulika
na hali ya mgonjwa.
Nilimchukua mama hadi nyumbani. Nyumba ni ile ile niliyokuwa naishi
mwanzo, ila kulikuwa na mtumishi mwingine alihama wakati sipo, kule
kazini wakasema vyumba vyake viwili nitavichukua mimi, kwa hiyo
nitakuwa na vyumba vya kulala vinne, sebule moja, stoo, jiko, bafu na
ua mkubwa.
Nilimwonesha mama chumba chake, nikamuonesha jiko, stoo, choo
10 mama YANGU NI JINI
na bafu. Kisha nikaondoka kwenda hospitali kumwona Jennifer na kaka
yake ambaye najua ni Simon kwa vile namfahamu.
Nilipofika, niliangaza huku na kule lakini bila mafanikio, nikaenda
mapokezi na kuulizia kama kuna mtu amepelekwa pale kwa ajali ya
gari.
“Ajali ya gari kugongwa, kugonga au kupinduka?” mtu mmoja wa
mapokezi aliniuliza.
Kabla sijajibu alitokea daktari mmoja ambaye tunafahamiana sana.
Anaitwa John. Kwanza alishtuka kuniona.
“Macho yangu au?” aliuliza.
“Ni mimi dokta.”
“Umerudi lini bwana wakati juzi tu nilikuwa na Sanga akasema
hujarudi.”
“Nimerudi jana, lakini sijaanza kazi rasmi.”
“Oke, leo lazima tukukaribishe kwenye kikao.”
“Hilo ndilo la maana.”
“Sasa una nini, unaumwa au?”
na, nasikia Jennifer kaja na kaka yake hapa, wana ndugu yao kagongwa
na gari.”
“Khaa! We Damas, kwani hujui habari za Jennifer?”
“Una maana gani dokta?” nilimuuliza huku moyo wangu ukipata
mshtuko.
“Ha! Kweli hujui lolote?”
“Sijui dokta. Amini sijui.”
“Kwanza hebu niambie, umesema kuna ndugu wa Jennifer ana matatizo,
habari umepewa na Jennifer mwenyewe au? Kwanza unamzungumzia
Jennifer gani, shemeji yangu au kuna mwingine?”
“Dokta John, we niambie tu unachojua kuhusu Jennifer shemeji
yako.”
“Damas, unajua siamini, kwani huna mawasiliano naye?”
“Sina, nilipokuwa Sweden nimekuwa nikimpigia simu hadi nikachoka,
nikaacha.”
“Mbona alifariki dunia kwenye ajali ya basi iliyotokea Barabara ya
Tukuyu -Mbeya.”
“Kweli John?”
“Yes! Na tulimzika hapa hapa Njombe.”
Nilijikuta nikiishiwa nguvu, miguu ilianza kushindwa kusimama huku
11 mama YANGU NI JINI
nikitamani kukaa mahali popote pale.
“Pole sana Damas. Lakini ni mwaka mmoja na nusu sasa.”
Mara alitokea Jackson, kaka wa Jennifer ambaye ndiye niliamini amekuja
hospitali na Jennifer.
“Shemeji vipi, za siku, za safari?”
Niliitikia salamu zake zote huku tukikumbatiana, nikamtambulisha kwa
Dokta John ambaye alikiri anamfahamu.
“Pole na matatizo shemeji, eti Jennifer alifariki dunia kwa ajali ya gari, ni
kweli shemeji?”
“Ha! Ina maana huna habari shemeji?”
“Niitoe wapi? Na wewe hapa umekuja kwa tatizo gani kwani?”
nilimuuliza.
“Kuna baba yetu mdogo kagongwa na gari leo.”
“Umemleta wewe hapa?”
“Hapana, nilipigiwa simu na dada mmoja, ndiyo nikaja.”
“Umekuja na nani?”
“Peke yangu, kwani vipi shemeji?”
Muda wote namuuliza shemeji maswali haya, Dokta John naye alikuwa
ananitumbulia macho asijue kinachoendelea.
Ilibidi niwachukue wote, yaani Dokta John na shemeji Jackson na kwenda
kukaa nao pembeni, nikawaleza kilichotokea mpaka kikanifanya na mimi
nikafika hospitalini hapo.
“Ha! Mama. Shikamoo mama.”
“Marhaba, za siku mwanangu?”
“Nzuri mama. Vipi wewe hali yako?”
“Namshukuru Mungu. Umerudi lini?”
“Mimi nimeingia jana mama.”
“Umekuja na Henry mama?”
“Hapana, nimekuja mwenyewe.”
“Ha! Mama, kuanzia Mbinga?”
“Eee, kwani unadhani mimi sijiwezi kiasi cha kushindwa kufika huku
Njombe?”
“Mh! Nani amekupa ramani?”
“Mdogo wako.”
“Henry?”
“Henry ndiyo.”
12 mama YANGU NI JINI
“Alikupa mpaka hapa ofisini au mpaka stendi ya Njombe?”
“Mpaka stendi.”
“Sasa mama nani amekuleta hadi hapa ofisini, mbona uko peke yako?”
“Nilipofika stendi, nilianza kuulizia.”
“Kuulizia jina langu au la ofisi?”
“La kwako.”
“Ikawaje sasa?”
“Kuna msichana akasema anakufahamu, anaitwa Jennifer.”
“Jennifer!”
“Eee, na wewe unamjua?”
“Namjua mama.”
“Basi huyo huyo, anasema alikuwa Kyela, Mbeya ndiyo amerudi.”
“Sasa yuko wapi?”
“Tulipofika hapa getini, kakutana na kaka yake yuko mbio mbio,
alipomuuliza akasema baba yao mdogo amegongwa na gari amekimbizwa
Hospitali ya Kibena kwa matibabu kwakuwa hali yake ni mbaya sana.”
Nilipofika hapo, Dokta John na shemeji Jackson wakashtuka sasa maana
walianza kupata picha ya tatizo.
“Ina maana basi kuna Jennifer feki, si ndiyo?” alihoji Dokta John.
“Ndiyo maana yake,” akadakia shemeji Jackson.
Mimi nilibaki kimya tu, nilipumua kwa nguvu huku nikizungusha macho
pale tulipokaa. Hata sijui nilikuwa naangalia kitu gani.
Nilivuta picha na kuichangamsha akili yangu ili kujua kama ni kweli
kuna Jennifer feki au kuna msichana tu alinijua mimi na Jennifer ndiye
aliyekutana na mama akataka kunichezea akili zangu kwa njia ile?
“Unajua Bw. Damas, kinachonishangaza mimi ni kitu kimoja tu,” sauti ya
Dokta John ikanirudisha mahali pale baada ya kuwa katika mawazo kwa
muda.
“Kitu gani ndugu yangu?”
“Afadhali ungekuja hapa hospitali halafu usimkute hata huyu shemeji
yako, ungesema kuna msichana mwingine amekuchezea, lakini sasa ni
kweli umemkuta shemeji yako na kweli kuna baba mdogo amegongwa
na gari, si ajabu hiyo?”
“Ndiyo hapo sasa,” aliitikia shemeji Jackson huku akionekana kuumiza
kichwa kutaka kujua nini ni nini.
Nilichoamua, nilimwomba shemeji Jackson twende akanioneshe kaburi
la marehemu Jennifer, naye bila hiyana akasimama.
13 mama YANGU NI JINI
Tulimwacha Dokta John akirudi ofisini kwake, sisi tukaenda makaburini.
Lengo langu lilikuwa ni kujiridhisha kwamba kweli Jennifer alifariki dunia
na kaburi lake liko.
“Hili ndilo kaburi lake shemeji,” shemeji Jackson aliniambia.
“Daa! Jennifer, umekufa kweli au uko hai mpenzi wangu? Nilipanga
makubwa kwako baada ya kutoka masomoni. Kalale pema mke wangu,”
nilisema huku nikilia.
Mara upepo mkali ulivuma pale kaburini kiasi cha kutupa hofu, nikajikuta
nashindwa kusimama, hata shemeji Jackson pia alikaa na kushikilia
mti mdogo pembeni ya kaburi jingine. Upepo ulipotulia, nilimwamuru
shemeji tuondoke eneo lile haraka sana. Tukiwa njiani akaniuliza:
“Shemeji, ina maana inawezekana mdogo wangu Jennifer amekufa kifo
cha muruweruwe?”
“Shemeji hata mimi nimeshangaa sana. Si kawaida. Mambo yote pale
kaburini hayakuwa ya kawaida. Kuna kitu.”
“Khaa! Sasa mbona tangu kifo chake hadi kuzikwa, hatukuona maajabu
yoyote?”
“Unajua shemeji haya mambo ya marehemu marehemu huwa yanaibuka
muda mrefu baada ya kuzikwa.”
“Kweli ee?”
“Ndiyo.”
Wakati huo tulikuwa tunaingia kwenye makazi ya watu. Niliagana na
Jackson nikimwambia akawaambie ndugu zake kilichotokea kwenye
kaburi la Jennifer.
Nilipofika nyumbani, nilimkuta mama sebuleni, nikamsalimia.
“Haya za huko?” aliniuliza.
“Nzuri tu mama.”
“Ni kweli kuna mtu kagongwa na gari huko?”
“Ni kweli mama, lakini…”
“Lakini nini sasa?” mama alihoji huku akikaa sawasawa.
Nilimsimulia mama kila kitu kilichotokea kula makaburini, akacheka
sana mpaka nikashtuka.
“Sasa mwanangu Damas, toka lini makaburini kukakosa vituko? Lile
ndiyo eneo lake. Ukienda usiku ndiyo kabisa. Hukumbuki yale makaburi
ya kule kijijini, si hayaishi maajabu.”
Ni kweli kabisa, makaburi ya kule kijijini yalikuwa na matukio mengi
sana kiasi kwamba, wazee waliwahi kuweka amri ya watoto kutopita njia
14 mama YANGU NI JINI
yake usiku maana yalikuwa kwenye eneo ambalo kuna njia ya kutoka kijiji
chetu kwenda kijiji kingine.
“Kwa hiyo mama inawezekana ni mauzauza ya kweli lakini kwa sababu
ni kaburi?”
“Ee! Hapo unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unaepuka jambo lolote
linalomhusu huyo Jennifer.”
“Ni kweli mama. Halafu mama nina wazo moja.”
“Lipi hilo Damas?”
“Eee, nafikiria baba naye aje huku Njombe, mtapumzika hapa hadi
mtakapotaka wenyewe.”
“Ni sawa, lakini baba yako hawezi kukubali hata siku moja.”
“Kwa nini mama?”
“Sijui mwenyewe, hata hii safari yangu hakuipenda, anasema tunakuja
kukupa wakati mgumu bure huku.”
“Aaah! Sasa mama mimi si mtoto wenu, mnadhani mnatakiwa kumpa
wakati mgumu nani?”
“Sijui mwenyewe baba yenu.”

******************

Usiku wa saa nne baada ya kula, nilimuaga mama nakwenda kulala,


akasema yeye hana usingizi sana kwa kuwa amekuwa akishinda kulala
mchana kutwa.
Nikiwa kitandani niliwaza kitu. Kitu chenyewe ni hiki:
“Hivi baba alijuaje akimruhusu mama kuja Njombe ataniona mimi wakati
nilikuwa masomoni nje ya nchi? Je, mfano sasa asingenikuta ingekuwaje,
angerudi? Halafu baba ni mwelewa sana, ni kweli alimkubalia mkewe
aje mwenyewe sehemu asiyoijua kwa mategemeo ya kuulizia tu kwa
watu? Mh! Labda mama alimtoroka baba au alilazimisha kuondoka bila
mawasiliano mazuri na baba, nitajua tu,” nilimaliza kuwaza.

MDOGO WANGU ANAKUJA NJOMBE, MAUZAUZA YANAPAMBA MOTO

Mwezi mmoja baadaye nikiwa nimeshaanza kazi, siku hiyo akaja dada
mmoja ambaye aliajiriwa kwa kazi ya kwenda kununua vifaa mbalimbali
vya ofisi (purchasing) akaniambia kuna mgeni wangu mapokezi anaitwa
Henry.
15 mama YANGU NI JINI
Nilitoka mbio ili nikamlaki Henry ambaye ni mdogo wangu, nilimkuta
amekaa kwenye benchi la wageni, mkononi ameshika begi.
Aliponiona alisimama, akanikaribia, tukakumbatiana na kuulizana hali
pamoja na habari za safari kisha nikampeleka nyumbani.
Cha ajabu, tukiwa njiani tunakwenda, sikumuuliza habari za nyumbani
atokako wala yeye hakuniambia nyumbani kukoje au mama anaendeleaje
baada ya kufika kwangu.
Nilisukuma mlango, sebuleni alikaa msichana wa kazi, anaitwa Sekindole.
Huyu ni mwenyeji wa Kijiji cha Kidamali, Iringa, nilizoea kumwita Segito
kwa sababu nilijua ni mhehe, halafu mwanamke.
“Segito kuna mgeni, mpokee begi,” nilimwambia nikikaa kwenye kochi
kubwa.
Henry naye alikaa kwenye kochi dogo akiwa ameshapokelewa begi lake
na Segito.
Usoni, Henry alionesha alikuwa na mambo mengi ya kuzungumza na
mimi, lakini alikuwa akisita.
“Segito,” nilimwita msichana.
“Abee kaka.”
“Mama yuko wapi?”
“Amelala.”
“Aaa, sasa sikia.”
“Abee kaka,” aliitikia Segito akija sebuleni na kupiga magoti pembeni
yangu.
“Huyu mdogo wangu anaitwa Henry, kaja kutoka nyumbani. Mtengee
maji ya kuoga, mpe chakula kisha utamuonesha chumba kile cha mwisho
atapumzika kidogo mpaka mimi nitakaporudi, sawa?”
“Sawa kaka.”
Nilisimama ili kurudi kazini huku nikimpa Segito maelekezo mengine:
“Halafu mama akiamka aje sebuleni kusalimiana na mgeni.”
“Sawa kaka.”

MCHUMBA WA ZAMANI AIBUKA, MAMA ABARIKI NDOA

Nikamuaga Henry ili nirudi kazini. Nikiwa njiani sina hili wala lile, nilisikia
nikiitwa:
“We Damas…Damas wewe.”
Niligeuka kwa mshtuko, kumbe alikuwa msichana mmoja anaitwa
16 mama YANGU NI JINI
Salome anatoka kwenye ukoo unaoitwa Mangula. Niliwahi kuwa na
uhusiano naye, nilipokutana na marehemu Jennifer nikambwaga, lakini
pia kwa sababu alikuwa machepele f’lani.
“Za siku Damas?”
“Nzuri Salome, vipi za siku na wewe?”
“Nzuri, za safari, za Ulaya?”
“Salama, nimerudi salama.”
“Nasikia umerudi na mwanamke wa kizungu?”
Niliishia kucheka kwani haikuwa kweli, lakini nilishtuka jambo moja,
alipendeza na kuvutia kuliko wakati akiwa na mimi.
“Nasikia umeolewa, ni kweli?”
“Wala sina huo mpango Damas, mimi mume wangu ni wewe tu, najua
Jennifer hayupo basi nafasi yangu ipo palepale.”
Maneno yake yalinifanya nishawishike kupanga naye muda wa kukutana
na mahali gani ili tuongee kwa kirefu, akakubali, tukaachana mimi
nikaendelea na safari ya kwenda kazini.
Hatua kama saba toka niachane naye, niligeuka kumwangalia lakini
sikumuona, nikajua aliingia kwenye vichochoro.
Nikiwa kazini, muda mwingi niliwaza kuhusu Salome. Kwamba ni
mwanamke anayeweza kuchukua nafasi ya maisha yangu kwa kuwa
mke. Niliamini ametulia kwani hata mwonekano wake ulionesha hivyo.
Nikaamua kujipa moyo mi mwenyewe kwa kupania kwamba lazima
nimuoe Salome.
Basi, nilipotoka kazini nilikwenda kwenye baa ambayo tulipanga kukutana
na Salome, sikutaka kumpigia simu licha ya kwamba tulibadilishana namba
ya simu. Lengo langu kujua yeye alikuwa na nia na mimi moyoni mwake?
Ile nakaa tu, simu ya Salome ikaingia, nikaipokea na kumjulisha
nimeshafika, nimeshakaa. Akasema anakuja ndani ya dakika saba tu.
Ikawa hivyo kweli, alifika akiwa amevaa tofauti na alivyovaa awali, safari
hii alipendeza sana.
Salome alionekana amekuwa mpya kwa tabia na mwonekano, alijionesha
ni mwanamke mtulivu, mwenyewe kujiheshimu.
Siku hiyo tuliongea mengi sana na msichana huyo, hadi ikafika mahali
nikamwambia nia yangu ya kumuoa, akakubali bila kuzuizi huku akisisitiza
kuwa, hata nilipomwacha mara ya kwanza aliamini kisa ni Jennifer lakini
alijua kuna siku tutarudiana kwa sababu siku zote ndoto zake mimi kuwa
mumewe.
17 mama YANGU NI JINI
Basi, kwa jinsi nilivyotokea kumpenda sana kwa mara nyingine,
nilimsimulia kuhusu mama kuwepo nyumbani, akanitaka tuongozane
hadi huko akamsalimie na kumfahamu pia.
Tulifika nyumbani na kukuta msichana wa kazi, Segito, akatupokea mimi
na Salome mpaka sebuleni, baada ya salamu nilimuuliza aliko Henry,
akasema alikwenda kulala.
Mara mama alitokea kabla sijamuulizia…
“Mama vipi, ulilala?”
“Eee, ndiyo naamka”
“Pole sana mama yangu. Huyu anaitwa Salome.”
“Aaa, hujambo mwanangu?”
“Sijambo mama, shikamoo.”
“Marahaba.”
“Habari za safari, habari za nyumbani?”
“Kwema tu.”
“Mama.”
“Abee.”
“Huyu ni mchumba wangu, ndiye ambaye natarajia kumuoa.”
Mama alimkazia macho Salome kisha akasema:
“Nimebariki, lakini msichezeane.”
“Hakuna kuchezeana mama,” Salome alimjibu.
Pia nilimwita Segito na kumtambulisha kwa Salome, Salome naye
nikamtambulisha kwa Segito.
Nilimuuliza mama kama amekutana na Henry, akaonekana kushtuka,
lakini niliona ni sawa kushtuka kwani hakujua kama amefika.
“Ngoja nimwamshe,” nilisema nikitoka kwenye kochi kwenda chumbani
kwa Henry. Nilimwamsha Henry nikimwambia mama anataka kumsalimia,
akatoka kitandani akionekana kuchoka sana.Lakini nilipofika sebuleni,
mama hakuwepo, alibaki Salome tu.
“Yuko wapi mama?”
“Ameingia ndani,” alisema Salome.
Nilimtambulisha Salome kwa Henry, wakasalimiana na palepale Salome
alianza kumwita Henry shemeji. Nilisimama, nikamsimamisha na Salome,
tukaenda chumbani tukimwacha Henry pale sebuleni.
Kule chumbani nilimwonesha Salome chumba kilivyo, akafurahi sana
akisema anatamani awe mama mwenye nyumba kuanzia siku hiyo,
nikambusu. Tulipotaka kutoka, alishika tumbo akisema linamkata ghafla,
18 mama YANGU NI JINI
nikashangaa. Nilimwomba akae kitandani hadi litulie kwanza, akafanya
hivyo na mimi nilikaa jirani yake.
Baada ya dakika tano akasema limetulia, tukatoka mpaka sebuleni.
Nilimuuliza Henry kama mama alitoka, akasema wameshasalimiana,
amerudi chumbani kwake anasema anajisikia kuchoka.
“Oke, haina shida, mimi namsindikiza shemeji yako.”
“Sawa kaka.”
Salome alimuaga Henry tukatoka. Tulitembea kwa kushikana
mikono, njiani Salome aliniambia nienda naye hadi nyumbani kwake,
nikamkubalia.
Salome alipanga kwenye nyumba yenye sebule na chumba kimoja,
lakini vidogo sana, baadhi ya vitu alivibebanisha kutokana na udogo wa
vyumba.
“Hapa lazima uhame Salome,” nilimwambia.
“Sasa baba si niko chini yako, wewe ndiyo utanipangia siku ya
kuhama.”
Kifupi tuliongea mambo mengi sana na Salome, tukapigana mabusu
mazito mazito. Nilitumia kama masaa matatu pale, mpaga giza liliingia,
nikarudi nyumbani.
Nilikuta Henry amelala akimwambia Segito anahisi maumivu ya kichwa,
lakini alishakunywa dawa. Mama pia alilala, hata hivyo wote walishakula
chakula cha usiku.
Niliingia chumbani kwangu, nikatoa nguo na kuvaa taulo kisha nikaenda
kuoga. Niliporudi nilikaa sebuleni kuangalia tivii kisha nikaenda kulala.
Usiku nilijikuta nina mawazo kuhusu mama na Henry, kwamba
kibinadamu nilitakiwa nikae nao kwa pamoja na kuongea mambo mengi
ya kijijini walikotoka, Henry ndiye angeweza kunipa mwanga kuhusu
safari ya mama.
“Itabidi asubuhi nifanye hivyo kabla sijaenda kazini,” nilisema moyoni,
nikapitiwa na usingizi, nikalala.
Usiku niliota ndoto bado niko nchini Sweden, Henry kanipigia simu,
nikaipokea:
“Shikamoo kaka.”
“Marahaba Henry, za huko, mbona kama unalia?”
“Kaka, mama amefariki dunia?”
“Ha! We Henry, unathubutu vipi kumsingizia mama kitu kikubwa kama
hicho? Una akili kweli wewe?”
19 mama YANGU NI JINI
“Kama ni kweli.”
“Alikuwa anaumwa?”
“Ndiyo kaka.”
“Nini?”
“Tatizo lake ni lile lile ulilomwacha nalo.”
“Ha! Mnazika lini? Maana mimi sidhani kama nitaweza kuwahi mazishi,
kuna muda wa kuandaa safari kutoka huku kuja huko.”
“Mimi nimekutaarifu kaka ili ujue huna mama,” simu ikakatika kwa
ghafla, baada ya hapo sikumpata tena hewani. Nililia sana, nikaishiwa
nguvu. Kuanzia hapo niliichukia Sweden. Ghafla niliamka, machozi
yalikuwa bado usoni, nikajifuta nikiamini nipo Sweden kwenye chumba
amacho nilikuwa nakitumia, lakini nilipoangaza kulia na kushoto
nikagundua niko Njombe na ile ni ndoto tu, nikanyoosha mkono juu
kumshukuru Mungu ingawa nilijiuliza tafsiri ya ndoto ile ni nini, sikupata
jibu.

***
Asubuhi niliamka, nikaenda kuoga, nilipotoka nilikutana na Segito.
“Mama na Henry wameamka?”
Nilimuuliza Segito kabla hata ya kumjulia hali. Mapigo ya moyo wangu
yalibadilika kila sekunde moja ilipoondoka kwenye dunia. Kilichonishtua
zaidi ni kuona Segito hajibu nilichomuuliza licha ya kuamini kwa asilimia
mia moja kuwa alisikia nilichomuuliza.
“We Segito, si naongea na wewe au hunisikii?” nilirudia huku safari hii
nikitoa sauti yenye ukali na mamlaka kidogo.
“Mmh, kaka samahani,” Segito alishtuka sana huku akijitahidi kukaa
sawa na kunijibu:
“Henry aliamka kaka, akaja sebuleni, lakini akarudi tena chumbani.
Mama yeye sijamuona,” alisema Segito huku akiondoka kwenda
kuendelea na shughuli zake.
“Karudi chumbani?”
“Ndiyo kaka.”
“Oke, mimi najiandaa niende kazini.”
“Sawa kaka.”
Wakati wote huo kumbukumbu ya ile ndoto ilizidi kujirudia akilini
mwangu mfano wa sinema kali ya kusisimua kutoka kwa Mel Gibson.
Akili ikazidi kuchanganyikiwa, kwa mara ya kwanza nikajikuta nikiingiwa
20 mama YANGU NI JINI
na wasiswasi mkubwa.
“Lakini waswahili wanasema ndoto huja baada ya shughuli nyingi,
sasa kwa vyovyote vile ile ni ndoto tu baada ya kuwaza sana,” nilisema
moyoni.

MAZITO ZAIDI YAIBUKA, YASHANGAZA

Nilirudi chumbani kwangu, nikaanza kujiandaa kwenda kazini. Nilifungua


kabati na kuchagua nguo za kuvaa kwa siku hiyo. Automatiki nilijikuta
nikivaa suruali nyeusi, shatio jeusi, viatu vyeusi, soksi nyeusi, mkanda
mweusi.
Inawezekana ilikuwa siku ya kushangaza sana kwangu kwani nilikumbuka
nimevaa sare ya rangi wakati najiandaa kutoka nyumbani.Nilitoka
nikitembea kwenye korido kwa mwendo wa madaha, kufika sebuleni
nilimkuta mama amekaa.
“Haa! Shikamoo mama angu.”
“Marhaba mwanangu, umeamkaje?”
“Mungu amenilinda mama. Nilimuuliza Segito akasema hujaamka.”
“Mh! Huyu binti naye muongo, si alikuja hapa sebuleni akaniamkia, sasa
sijaamka kivipi?”
Wakati mama anasema hayo, Segito alitokea.
“We Segito,” nilimwita.
“Abee kaka.”
“Wewe si uliniambia mama hajaamka, ila Henry ndiyo kaamka, karudi
chumbani kwake?”
“Ha! Mimi sijamuona mama, nilimuona Henry tu.”
“Wewe Segito utakuwa mwongo sasa. We huwa unamwamkia Henry
shikamoo?” mama alimuuliza.
“Hapana, namwambia habari za leo.”
“Sasa mbona uliniamkia shikamoo.”
“Ha! Mi sikumbuki, ninachojua alikuwa Henry.”
“Haya, kamwamshe Henry,” nilimwamuru Segito, lakini kabla hajageuza
na kuondoka, mama alisema:
“Ngoja niende mimi.”
Nilikaa kwenye kochi nikitafakari jambo hili.
“Hivi ni kweli Segito amwone mama, halafu ajue ni Henry? Mbona
21 mama YANGU NI JINI
haviingiliani hata kidogo. Au mmoja wao anazungumzia jana, mwingine
leo?”
Mara, Henry alikuja, lakini bila mama.
“Mama yuko wapi?” nilimuuliza.
“Amekwenda uani kama sikosei, shikamoo.”
“Marhaba. Vipi, ulishaamka kumbe?”
“Ndiyo.”
Nilimuuliza hivyo baada ya kumwona usoni hana dalili kwamba ndiyo
anaamka.
“Ulishakuja sebuleni?”
“Hapana.”
“Ha! Wewe kaka Henry, hujaja hapa mpaka nikakusalimia za leo, ukajibu
nzuri?” alisema Segito.
“Sijaja mimi, ndiyo kwanza nimeamshwa na mama sasa hivi.”
“Segito,” niliita.
“Abee kaka.”
“Punguza uongo.”
“Kaka, mimi namaanisha.”
“Sasa unamaanisha mbona mwenyewe anakataa na mama pia
alishakwambia Henry hajaamka?”
“Basi kaka, naomba samahani sana.”
“Ee, usiwe mtu wa kufikirifikiri,” nilisema.
Niliwaaga kwamba nakwenda kazini, wakaitika wote na kunitakia kazi
njema. Lakini nilipotoka umbali f’lani nikakumbuka nimesahahu kitu
muhimu sana, nikarudi. Niliingia chumbani kwangu, nikakichukua na
kutoka. Ile nakanyaga sebuleni tu, nyuma yangu Henry anakuja.
“Shikamoo kaka,” alinisalimia, sikumwitikia, nikatoka. Nikiwa nageuka
ili kufunga mlango, nikamwona anafikicha macho huku akielekea kukaa
kwenye kochi kubwa.
“Huyu Henry naye bwana, kaiga tabia zote wa Kingoni, kila saa shikamoo,
kila saa shikamoo. Akitoka kuoga shikamoo, akinywa chai akimaliza
shikamoo,” nilisema moyoni wakati nakaribia ofisini kwangu.
Nilifanya kazi kichwa kikiwa na mzigo wa mawazo, mojawapo ni jinsi
nitakavyomuoa Salome. Mwanamke ambaye niliamini ni kila kitu kwangu
kama ataingia ndani ya nyumba.
Lakini ghafla kichwani nikakumbuka Yale mazungumzo ya pale
nyumbani:
22 mama YANGU NI JINI
“Haa! Shikamoo mama angu.”
“Marhaba mwanangu, umeamkaje?”
“Mungu amenilinda mama. Nilimuuliza Segito akasema hujaamka.”
“Mh! Huyu binti naye muongo, si alikuja hapa sebuleni akaniamkia,
sasa sijaamka kivipi?”
“Hivi inawezekana kabisa mmoja wao alijichanganya?”
Mara nikawaza kitu kingine.
“Shikamoo kaka.”
“Huyu Henry naye bwana, kaiga tabia zote wa Kingoni, kila saa shikamoo,
kila saa shikamoo. Akitoka kuoga shikamoo, akinywa chai akimaliza
shikamoo.”
Hapo ndipo kwenye kiini cha tatizo sasa, akili zilifanya kazi na kubaini
kuwa kuna jambo zito lilijificha. Kwanza nilikumbuka kuwa, Henry
aliyeniamkia mara ya pili alionekana ametoka usingizini, yule wa mara ya
kwanza alishaamka muda mrefu.
“Mh!” niliguna kwanza nikiwa nashangaa.
“Au mle ndani mna Henry wawili, wa mama na wa kwangu?”
Niliazimia moyoni kuwa nitakaporudi jioni nitafanya upelelezi kubaini
kitu, lakini siku hiyo nilikosa nguvu na ari ya kufanya kazi.Saa tisa na robo,
Salome alinipigia simu na kuniuliza nitatoka muda gani?
“Karibu natoka, kwani vipi?”
“Nimeuliza tu.”
“Lakini siko sawa leo mke wangu Salome.”
“Kwa nini baba? Kuna nini tena?”
“Nitakueleza tukikutana.”
“Ni kuhusu kazi?”
“Hapana.”
“Ni nini sasa mume wangu jamani? Unaniweka roho juu.”
“Nitakwambia.”
“Oke sawa, basi baadaye.”
“Sawa.”
Baada ya kukata simu ya Salome, nilifungafunga makabrasha yangu
na kutia kwenye begi nikasimama ili kuondoka zangu. Kwenye korido
nilikutana na bosi wangu:
“Damas.”
“Ndiyo mkuu.”

23 mama YANGU NI JINI


“Nahisi kama una safari nyingine nje ya nchi.”
“Kweli bosi?”
“Yeah! Safari hii huenda ukaenda Jakata, Indonesia au Kuala Lumpur,
Malaysia.”
“Bosi nadhani nitafurahi sana kwa hilo. Namwomba Mungu litimie kwa
asilimia mia moja.”
“Usijali... usijali Damas,” alijibu bosi huyo.

NDANI YA NYUMBA NAISHI NA WATU WASIYOKUWA BINADAMU

Nilipofika nyumbani, nilimkuta Segito amekaa nje.


“Vipi wewe?”
“Salama tu.”
“Mbona umekaa nje?”
“Nilitaka kwenda dukani, Henry akasema nimtume yeye, nimemkatalia
sana lakini akang’ang’ania, akaenda sasa umepita muda mrefu sana
hajarudi.”
“Ulimtuma nini?”
“Sikumtuma kaka, yeye ndiye aling’ang’ania.”
“Sawa aling’ang’ania, alikwenda kununua nini?”
“Sabuni ya kufulia na kuogea.”
“Basi atarudi, ingia ndani.”
Segito alisimama, akaingia ndani akinitangulia mbele kwenda ndani. Ile
anafungua mlango mkubwa tu, akashtuka sana:
“Haa! Wewe, umepitia wapi?”
“Nani, Henry?” niliuliza kwa mshtuko mkubwa.
“Eee. Si huyu hapa.”
“Nimepitia wapi, mimi nimepitia hapo hapo, wewe nimefika ndani
hukuwepo, ulikwenda wapi kwani?”
“Nilikwenda wapi wakati nilikuwa nakusubiri nje.”
“Aaa. Nje mbona sikukuona. We kuna sehemu ulikwenda.”
“Hakuna Henry, sijaenda mahali.”
Mimi nilimkazia macho Henry, nikamshangaa sana kwa jinsi alivyokazania
kwamba alipita kuingia ndani wakati Segito anakataa. Na mimi namjua
Segito si mtu wa kutoka kwenda kuzurura hovyo.
Niliamua kukaa kimya, nilifikia kwenye kochi kubwa, Henry naye
24 mama YANGU NI JINI
akakaa.
“Henry,” niliita.
“Naam.”
“Mama yuko wapi?”
“Amelala.”
“Kamwamshe kisha na wewe uje hapa.”
“Sawa.”
Alisimama, akaondoka. Baada ya dakika mbili walikuja wakiwa
wameongozana.
“Mama shikamoo.”
“Marahaba mwanangu pole na kazi.”
“Asante mama.”
“Vipi, umerudi salama?”
“Ndiyo kwanza nimeingia mama, nimerudi salama.”
“Sawa, mimi nilipumzika kidogo.”
“Sawa, basi nenda kaendelee kupumzika mama.”
“Haya mwanangu, baadaye,” alisema mama huku akisimama na kutoka
kwenda ndani kwake.
Pale sasa nikabaki mimi na Henry, nilikuwa nikimkazia macho anaangalia
pembeni, nikaangalia pembeni ananikazia macho.
Baadaye akasimama, akaondoka. Nilimwangalia anavyotembea,
nikakataa yule si Henry mdogo wangu.
“Kwani Henry anatembea vile?”
“Mbona kama anatembea hana vidole miguuni?”
“Mh! Hapa kwa Henry bwana pana mchezo. Halafu kwa kawaida
nikiongea na Henry mdogo wangu hawezi kusema naam tu, angesema
naam kaka. Hawezi kusema, ndiyo, angesema ndiyo kaka.”
Baada ya dakika kumi, niliingia chumbani, nikabadili nguo na kuvaa
bukta, nilipotoka nilimkuta Henry naye amebadili nguo amekaa sebuleni.
“Shikamoo kaka.”
“Hivi wewe una nini?”
“Kwa nini kaka?”
“Kwa nini kaka? Yaani unaleta mambo ya Songea huku siyo?”
“Kaka sijakuelewa mbona?”
“Utanielewaje, angalia sana,” nilisema nikiingia chumbani kwa hasira.
Nilifikia kitandani kwangu na kujilaza, nikawa namtafakari huyu Henry.
25 mama YANGU NI JINI
“Yaani yeye kila saa shikamoo. Kila saa shikamoo, anadhani hapa ni
Songea.”
Lakini kuna sauti kwa mbali ikaniambia:
“Una hakika huyu ndiye Henry uliyemkuta wakati unarudi kutoka
kazini?”
“Mh! Halafu kweli. Huyu anatumia sana neno kaka mwisho, yule
hatumii. Inawezekana mawazo yangu yako sawa, kuna Henry wawili ngoja
nikambane kama ni yule yule, nitamuuliza kama alipata hizo sabuni.”
“Henry,” niliita kwa sauti wakati nakwenda sebuleni.
“Naam,” sauti ilitokea sebuleni.
Nilipofika sebuleni, nimkuta amekaa kwa utulivu kabisa:
“Henry.”
“Naam.”
Kwanza hii itikia yake ya ‘naam’ bila kaka mbele nikaingiwa na wasiwasi,
lakini nikajipa matumaini kuwa pengine kaamua tu.
“Ulizipata hizo sabuni ulizotumwa na Segito?”
“Ndiyo.”
“Mama bado amelala?”
“Ndiyo.”
“Hebu nenda kamwamshe mara moja.”
Henry alisimama, akaondoka. Wakati akitembea nilimkazia sana macho.
Alionekana ni Henry wa kweli, lakini pia niliingiwa na wasiwasi kwamba
siye, kwa hiyo nikawa kati kwa kati.
Mara, mama alikujua akitembea kwa kujikongoja.
“Vipi mama?”
“Ah! Leo siko vizuri sana.”
“Pole sana, nini zaidi unakisikia?”
“Mwili wote huu.”
“Henry yuko wapi sasa?”
“Sijui, mi ameniambia unaitwa na kaka, basi akatoka. Labda yupo
chumbani kwake.”
“Henry,” niliita kwa sauti ya juu ili kama alikuwa chumbani asikie.
Sasa hapa napo palitokea utata kwani kama nilisikia sauti mbili
zinazofanana zikiitika.
“Naam.”
Nyingine...
“Naam kaka.”
26 mama YANGU NI JINI
Halafu nikasikia kama milio ya milango miwili kwa mpigo ikifunguliwa.
“Mh! Mama! Mbona..?”
Kabla sijamaliza kusema, mama licha ya kwamba alisema anajisikia
vibaya, nilimuona akinyanyua mguu mmoja kisha akakanyaga chini kwa
nguvu.
“Mama vipi?”
“Miguu imekufa ganzi.”
Mara akatokea Henry.
“Vipi, ulikwenda kulala?”
“Hapana,” alisema akikaa kwenye kiti.

MCHUMBA WANGU AINGILIA KATI


KUUPATA UKWELI WA MAMA NI JINI!

Mara, mlango mkubwa uligongwa, nikasimama kufungua. Alikuwa


Salome.
“Yaani umefanya vizuri sana kuja.”
“Kwa nini?”
“Nilikuwa nawaza nije kwako bila kukupigia simu, kumbe na wewe
unawaza kuja kwangu bila kunipigia simu.”
Salome alicheka huku akienda kumsalimia mama, kisha Henry halafu
akaja kukaa jirani na mimi.
“Mambo baby?”
“Poa tu, vipi wewe?”
“Niko bomba, kukumisi tu.”
“Hunishindi mimi sweet.”
Tuliongeaongea pale kisha nikamruhusu mama akalale, Henry naye
akaondoka, akarudi chumbani kwake huku nikimkazia macho.
“Damas,” aliita kwa mshtuko Salome.
“Eee.”
“Vipi? Mbona unamkazia macho hivyo mdogo wako?”
“Nitakwambia Salome.”
“Tena umenikumbusha, uliniambia kuna kitu kinakutatiza sana.”
“Yes!”
“Kitu gani, si tuko wawili tu. Niambie.”
“Twende chumbani nikakwambie.”
27 mama YANGU NI JINI
Tulisimama hadi chumbani, nikamtaka Salome akae kitandani ili nianze
kumpa ei tu zedi. Nilifanya hivyo mara baada ya yeye kukaa.
Nilimsimulia kila kitu na mara zote katika simulizi zangu, nilipofika eneo
la Jennifer, Salome alishtuka sana. Mwishowe akaniuliza:
“Ina maana mpaka sasa hivi hujapata jibu baba?”
“Sijapata Salome. We unahisi nini?”
“Sihisi kitu, ila naamini kuna mchezo unaendelea Damas. Umeshawasiliana
na kijijini kwenu siku za karibuni?”
“Kule naona baba hana simu maana hayupo hewani kitambo. Kama ni
mama ni huyu ninaye.”
“Kwani Damas ina maana kwa Henry ndiyo unatia shaka, lakini kwa
mama hapana?”
“Yes. Kwa mama hakuna kitu, ila kwa huyu dogo.”
“Sasa unataka kufanyaje ili ujue ukweli?”
“Mh! Sijui.”
Salome alijiinamia kwa muda kisha alipoinua kicha akasema:
“Sikiliza Damas.”
“Nakusikiliza mama.”
“Kesho nije nishinde hapa, kuanzia asubuhi hadi jioni, nitaujua ukweli
tu, lazima.”
“Salome.”
“Abee.”
“Please, kama hakuna shida naomba ulale hapa, kesho ushinde hapa, ili
ufanye upelelezi wako kwa kina.”
“Sawa, hakuna shida, nitafanya hivyo, mimi kule sina mtoto, sina
anayeniuliza niko wapi, mume wangu ni wewe.”
Kuanzia hapo tulianza mkakati wa kuujua ukweli wa Henry kama wapo
wawili au ni kujichanganya kwangu tu. Salome alitoka akisema anakwenda
kuungana na Segito katika mapishi ya jioni, mimi nikalala nikisoma gazeti.
Baada ya nusu saa tu, Salome akarudi haraka sana.
“Baba nikwambie kitu?”
“Nini tena Salome jamani?”
“Madai yako yana ukweli.”
“Kwa nini unasema hivyo Salome?”
“Dada kaniambia, wifi unajua huyu Henry mimi simwelewielewi.
Nikamuuliza kafanyaje? Akasema kuna wakati anakuwa mpole, kuna
wakati anakuwa mcharuko. Halafu anaweza kutoka amevaa kaptula,
28 mama YANGU NI JINI
baada ya muda akatoka amevaa suruali.”
“Loo! Salome umeona?”
“Nimeona baba.”
“Sasa hapo tatizo si mama.”
“Ni Henry,” Salome alidakia akiwa amekaa jirani na mimi.
“Kwa hiyo unaonaje?”
“We unaamini nini?” aliniuliza Salome.
“Mimi naamini kwamba, humu ndani kuna Henry wawili.”
“Kwa maana gani, mmoja ni jini au?”
“Inawezekana au haiwezekani, lakini hoja ni kwamba kuna Henry
wangapi?.”
“Wawili.”
“Eeee, wawili. Ndiyo maana nilikwambia vile. Halafu pia, ndiyo maana
wana tabia mbili tofauti. Kuna Henry ana heshima sana, halafu yupo
ambaye hana heshima.”
“Haa! Sasa si hatari?”
“Hatari sana.”
“Sasa ina maana wote wanalala chumba kimoja?”
“Salome, nina uhakika kuwa wanalala vyumba viwili tofauti. Ushahidi
ni kwamba, leo kabla hujaja, nikiwa na mama sebuleni niliita Henry.
Pakatokea utata.
“Utata gani?”
“Nilisikia sauti mbili zinazofanana zikiitika naam, lakini nyingine ikapitiliza,
ikamalizia na kaka.”
“Una maana mmoja aliitika naam kaka?”
“Eee. Halafu nikasikia kama milio ya milango miwili kwa mpigo
ikifunguliwa.
“Mh! Mbona makubwa mume wangu. Mama akasemaje?”
“Kikubwa yeye nilimwona akipiga mguu chini, akasema umekufa ganzi.”
“Mmh! Kweli?”
“Eee.”
“Sasa alikuja Henry gani?”
“Naamini alitokea Henry wa uongo maana wa ukweli anapenda kumalizia
na neno kaka, wa uongo hatumii hili neno.”
“Mfano.”
“Mfano alipokuja nilimuuliza ulikwenda kulala? Akajibu hapana,
29 mama YANGU NI JINI
angekuwa yule wa ukweli angejibu hapana kaka ndiyo na wewe ukafungua
mlango ukaingia.”
“Kwa hiyo Henry yule niliyemkuta ndiye feki?”
“Haswa.”
“Ase hapa dear aje mganga wa kienyeji. Inawezekana wote ni feki.”
“Sasa mganga wa nini?”
“Ndiyo atatufumbulia hili fumbo.”
“Salome.”
“Abee mume wangu.”
“Katika maisha yangu mimi na wewe isitokee hata siku moja ukaenda
kwa waganga wa kienyeji, mimi na hayo mambo mbalimbali.”
“Sasa tutafanyaje dear?”
“Tumwangalie Mungu.”
“Unaamini yeye anaweza?”
“Salome, kwake hakuna linaloshindikana.”
Salome aliniaga, akarudi jikoni aliko Segito, mimi nikabaki peke yangu.
Baada ya dakika kumi mbele, mlango uligongwa, nikajua si Salome maana
yeye angeingia tu, nilisimama kwenda kuufungua mlango.
“Kaka samahani sana, nataka kuongea na wewe mambo fulanifulani,”
Henry alisimama mbele yangu na kusema hivyo.
“Sasa hivi?”
“Itakuwa vyema sana.”
“Mama yuko wapi?”
“Mama gani?”
“Khaa!” wakati nimeshangaa, mara nilisikia kizunguzungu, nikashika
mlango ili nisianguke huku nimefumba macho. Henry akanishika mkono
hadi sebuleni, nikakaa. Hapo Salome hakujua kinachoendelea.
“Pole sana,” aliniambia Henry. Nilifumbua macho nikamwona Henry,
lakini amevaa tofauti na vile alivyosimama mlangoni na kuongea na
mimi.
“Ulikuwa unasemaje Henry?”
“Ah! Mimi sina usemi sana, ila nilitaka nikuombe ruhusa nikatembee
kunyoosha miguu.”
“Sasa hivi?”
“Ndiyo.”
Nilipomkazia macho, alihisi aibu, akakimbiza macho pembeni. Mara
akatokea mama.
30 mama YANGU NI JINI
“Kumbe mmekaa hapa?”
“Ndiyo mama, umeamka?”
“Eee, lakini moyo wangu leo unapenda sana kula nyama lakini isiive
sana.”
“Mama mbona umekuwa ukipenda nyama isiyoiva sana, una nini?”
“Sina tatizo.”
Wakati naongea na mama hivyo, Henry alisimama na kusema:
“Kama hivyo basi,” huku akifungua mlango mkubwa na kutoka zake.
“Haya sawa.”
Mama naye muda huohuo aliomba kurudi chumbani kwake, naye
nikamruhusu, wakati anasimama na mimi nikasimama kwenda chumbani
huku nikimwita Salome.
“Dear, mambo yanazidi kunoga.”
“Kwa nini?”
“Si umekutana na mama akienda chumbani kwake?”
“Hapana, nimekutana na Henry tu.”
“Na Henry?”
“Ndiyo. Kwani kuna nini, we niambie na mimi nitakwambia kitu.”
Nilimsimulia Salome tangu mlango ulipogongwa, nilipofungua, Henry
alichosema na alivyotumia neno kaka. Pia nikamsimulia nilivyoshikwa
na kizunguzungu ghafla, Henry alivyonishika na kunipeleka sebuleni,
lakini akiwa amevaa nguo nyingine. Nikamsimulia na mama alivyokuja
na hamu yake ya kula nyama isiyoiva sana.
“Haya, wewe mwenzangu kwako umeona nini?” nilimuuliza Salome.
“Mh! My dear sasa nakubali kuna kitu katika hawa akina Henry,” alisema
Salome huku akiniangalia kwa macho yaliyojaa wasiwasi mkubwa.
Nilianza kuhisi kwamba, huenda Salome akaamua kuondoka zake
kurudi kwake hasa alipobaini kwamba, Henry alishatoka nje lakini yeye
alikutana naye kwenye korido mle mle ndani.
Mimi kwa wasiwasi nilipandisha miguu juu ya kitanda kwani niliamini
Henry anayetuchezea anaweza kuwa chini ya kitanda.
“Sasa mume wangu, huoni kuwa hata kumuona Henry wa ukweli
itakuwa kazi?”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu Henry mbaya atakuwa akiingilia yeye na uliniambia
kwamba kuna wakati uliita, zikaitika sauti mbili na milio miwili ya mlango

31 mama YANGU NI JINI


ikifunguliwa, lakini mwisho wa siku alijitokeza Henry mbaya.”
“Ni kweli Salome, yaani hata sijui iweje!”
“Sasa sikia, wakati mimi niko na dada kule jikoni, aliniambia kitu.”
“Kitu gani mke wangu?”

“Alisema kuwa, yeye anaamini huyu mama si mama yako mzazi.”


“Si mama yangu mzazi?”
“Ndiyo.”
“Kwa kigezo gani?”
“Yeye anajua kwa undani zaidi, ila alisema kuwa, kuna siku alimsikia
mama akimuuliza Henry, sasa nadhani ni huyo Henry asiyetakiwa kwamba
anawakumbuka watoto wake waliopo New Delhi, India.
“Akaniambia Henry alimuuliza mara ya mwisho kwenda ni lini, akamjibu
hata kuja kwake pale alikuwa ametokea huko.
“Lakini Akaniambia wewe ulimwambia yule ni mama yako mzazi
ametokea kijijini kwenu Songea, sasa akashangaa ni kwa nini aseme
alikuwa India halafu wewe useme ametoka Songea.
“Lakini pia kingine kinachomtia wasiwasi ni kwamba, kuna wakati Henry
anamlalamikia ni kwa nini anapenda kumtengea ugali ulioliwa upande
mmoja, kama anataka si wale wote.
“Lakini yeye Segito akijitetea, Henry hamwelewi, sasa akasema hajui
chakula hicho huwa anaanza kula nani? Kuna siku alikitenga chakula
akiamini hakijaliwa, yeye akakaa na mama jikoni, lakini cha kushangaza,
Henry alipokwenda kula alikikuta kimeliwa upande.”
“M! Salome.”
“Abee.”
“Mambo ni mazito kumbe kuliko nilivyokuwa nikifikiria. Lakini mbona
Segito hajanisimulia chochote siku yoyote?”
“Labda anaogopa.”
“Anaogopaje jambo zito kama hilo?”
“Lakini Damas, mimi nahisi tatizo si kwa Henry tu.”
“Kwanini unaamini hivyo?”
“Naamini hivyo kwa sababu ya maneno ya Segito. Mimi Naamini na mama
naye achunguzwe, ana mambo yake ambayo pengine wewe huyajui tu.”
“Salome.”
“Nakusikiliza.”
“Unataka kuniambia mama yangu mzazi naye si yule mama yangu mzazi
32 mama YANGU NI JINI
wa kule nyumbani Ruvuma?”
“Simaanishi hivyo Damas.”
“Noo, kwa kauli yako Salome inaonekana wewe humwamini huyu
mama, kama una mawazo hayo naomba yaondoe maana ni potofu.”
“Damas.”
“Naam.”
“Unahisi naweza kuwa namkandamiza mama?”
“Mimi kwa upande wangu nashawishika sana kuamini hivyo, sijui ni
kwa nini?” nilisema huku nikiwa nasimama na kwenda kuushika mlango,
nikaufungua na kutoka kuelekea sebuleni.
Nilimwacha Henry chumbani. Nilijua alikuwa amejisikia vibaya kwa kile
kile kitendo changu cha kumshutumu kuhusu mama.
“Mama,” niliita kwa sauti ya juu nikiwa nakaa kwenye kochi dogo ambalo
huwa nalipenda sana kulikalia. Japo niliita mama, lakini aliyetokea ni
Salome:
“Mume wangu,” aliita.
“Nini?” Nilimwitikia hivyo.
“Usiniitikie hivyo mume wangu, nisamehe sana kama nitakuwa
nimekukwaza kwa mane no yangu lakini mimi nilisema vile kwa sababu
ulishanisimulia matatizo ya hapa kwako na mimi nikaona nianze
kukuchunguzia ili tujue kiini cha matatizo.”
Kabla sijamjibu mama alitokea.
“Karibu mama.”
“Haya.”
Wakati mama anakaa, nilimwamuru na Salome naye akae.
“Hivi mama, kule kijijini naweza kupata kiwanja nikanunua?”
Nilimuuliza kwa lengo la kumjua tu Kama kweli ni mama yangu na
ametoka nyumbani kijijini.
“Kwa nini usipate kama una pesa?”
“Sasa kwa pale nyumbani, kwa wapi panaweza kuwa na kiwanja?”
Nilimwona mama akikunja sura kwa swali langu hilo lakini na mimi
nilimkazia macho kwa muda. Wakati fulani nilimwangalia Salome, naye
akaonesha kujiamini zaidi.
“Wewe kama unataka kiwanja, wasiliana na mdogo wako,” akimaanisha
Henry.
“M! Mama kama wewe hujui unadhani Henry atakuwa anajua nini?”

33 mama YANGU NI JINI


“Yeye ndiye mzururaji kule kijijini, anaweza kujua wapi pana kiwanja
cha kuuza,” alisema mama akiwa anasimama kuondoka.
“Sasa mama mbona unaondoka?”
“Si nimekujibu, ongea na mdogo wako bwana, mi miguu inaniuma sana
leo.”
Baada ya mama kuondoka, nilimwangalia Salome ambaye naye alikuwa
akiniangalia mimi kwa macho yanayonisuta.
“Salome mke wangu.”
“Abee.”
“Mh! Hapa kwa mama kuna kitu kabisa, wala hakuna ubishi juu ya
hilo.”
“Niseme nini baba?” Salome aliniambia, mara akatokea Henry kutokea
ndani alikoelekea mama.
“Wewe umerudi muda gani?”
“Wapi?”
“Wewe si ulisema unakwenda kutembea kidogo?”
“Aaa, kaka mimi nipo mbona, ila kweli nilitoka ila nimerudi muda tu.”
“Henry.”
“Nakusikia kaka.”
Nilimwangalia Salome ambaye alinikodolea macho pima.
Moyoni niliamini Henry huyu ndiye mdogo wangu baada ya kutumia
neno kaka wakati tukiwasiliana.
“Hebu nipishe niongee na shemeji yako kwanza.”
Henry aliondoka, nikabaki na Salome tukitazamana kwa muda.
“Umeona mume wangu?”
“Nimeona Salome, Lakini huyu sasa ndiye Henry wa ukweli.”
“Kwa kuwanametumia neno kaka?”
“Ee, tofauti na yule aliyeondoka kwenda kutembea.”
“Dear, hapa home kwako sipo, tena mimi naamini hapa hakuna Henry
nduguyo, wote ni ishu nzito.”
“Khaa! Salome mbona unageuka tena?”
“Sigeuki Damas, moyo unanishuhudia kuwa wewe hapa zaidi ya Segito
hakuna mwingine mwenye dhamira njema na wewe.”
Mh! Sasa inakuwaje?”
“Wewe fanya juu chini uhakikishe unawasiliana na kijijini kwenu.”
“Ili niwaambieje Salome?”
“Damas, wewe mtu mzima sasa, si unaulizia kama mama yupo pale,
34 mama YANGU NI JINI
ulizia na Henry.”
“Je, nikiambiwa hawapo?”
“Ndiyo utajua tatizo liko wapi my Dear?”
“Mh! Mbona kama naogopa my Dear.”
BABA NAYE AJA NYUMBANI KWANGU, MAAJABU YAONGEZEKA

Wakati tukiendelea kuongea na Salome, hodi ilipigwa mlangoni, mimi


nikashtuka.
Nilisimama, nikaenda kufungua mlango huku nikiuliza ni nani.
“Kevela.”
Kevela ni dereva wetu ofisini.
“Kuna nini mzee Kevela?”
“Kuna mgeni Bwana Damas.”
“Mgeni, nani?” nilihoji huku nafungua mlango.
“Haaaa!” nilishtuka na kuhamaki. Alikuwa baba yangu mzazi.
Hakuwa na mzigo, ila Kevela yeye alishika begi mkononi.
“Baba.”
“Mzee Bwana kaja mjini saa nyingi, alikuwa anafanya kazi ya kukutafuta,
akakutana na mzee Mangula, ndiyo ikawa nafuu yake, akanipigia
nikamfuata kwa Mangula.”
Mangula ni mwanasheria wetu kazini. Si Mangula baba wa Jennifer.
Wakati huo baba alishaingia ndani na kufikia kwenye kochi ambalo
nilimwelekeza mimi kukaa pale.
Baada ya kukaa tu na Mzee Kevela kuondoka, mimi nilianza
utambulisho.
“Baba.”
“Naam.”
“Huyu anaitwa Salome, ni mchumba wangu. Salome.”
“Abee.”
“Huyu ni baba yangu mzazi.”
“Haya, za huko baba?”Salome alimsalimia zaidi.
“Huko salama mama, ingawa si sana.”
“Kwa nini baba?” Salome alimuuliza kwa kudakia.
“Misiba mingi tu.”
“Ipi hiyo baba?” mimi nilimuuliza kwa haraka sana.
Aliniangalia kwanza kwa macho yaliyojaa maswali na huruma kisha kabla
35 mama YANGU NI JINI
hajanijibu, akaniuliza:
“Wewe umerudi lini Tanzania?”
“Nina mwezi mmoja sasa, si ndiyo Salome?”
“Ee,” Salome alijibu huku akimwangalia baba kwa macho yaliyojaa woga
wa hali ya juu.
“Baba, misiba gani?” mimi nilikazania kutaka kujua.
“Yule mzee Komba, pale jirani na kilabu cha pombe za kienyeji...”
“Baba yake Galus?” nilimuuliza baba ili kumwonesha kwamba mzee
Komba namjua vizuri.
“Ee, alifariki dunia. Halafu mama ake Yosefa naye alifariki, Yosefa
mwenyewe yuko hoi kitandani, wa leo au kesho.”
Taarifa hizo za baba bado hazikunisaidia na matatizo yaliyopo pale
nyumbani. Nilimwangalia Salome, nikamuona anapanua kinywa kutaka
kusema jambo, lakini ghafla akajishika koo na kukohoa kwa nguvu zote.
“Vipi dear?” Nilimuuliza.
Salome aliendelea kukohoa huku akiwa bado ameshika koo lake.
Alionekana kama mtu aliyepaliwa na maji au chakula.
“Imekuwaje tena?” baba aliniuliza akiniangalia kwa umakini.
Hali ya Salome ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba ilibidi niite taksi ili
kumkimbiza hospitali kwa matibabu.
Wakati natoka sikuongea tena na baba wala hakuna mtu mwingine wa
ndani aliyejua kama baba amekuja.
Nikiwa njiani ndiyo nikakumbuka, lakini nikasema kwa vile na yeye
ameiona hali halisi hakuna neno.
Lakini nilikuwa najiuliza kisa cha tatizo la Salome.
“Au yule pia siyo baba yangu mzazi? Sasa labda Salome pale alitaka
kumuuliza swali ambalo lingemshinda kujibu ndiyo maana akasababisha
Salome kupaliwa?” Nilijiuliza mwenyewe.
Hospitali madaktari walimshughulikia Salome kwa utaalam wao wote,
lakini mwisho walisema hawaoni kiini cha tatizo, lakini wakamchoma
sindano.
Niliamua kurudi naye nyumbani. Tukiwa njiani, Salome akafungua kinywa
kuongea:
“Dear, ungenurudisha kwangu, sirudi kwako.”
Nilishtuka kwa sentensi hiyo, nikajua kwa vyovyote vile, Salome alihisi au
kuona kitu zaidi ya tatizo lake. Ni kwa nini akuogope nyumbani kwangu?
“Salome mke wangu?”
36 mama YANGU NI JINI
“Abee.”
“Kwani kwangu kuna nini?”
“Sweet niwaishe kwangu nitakwambia.”
“Nakuwaisha mama, ila ungeniambia ingekuwa vizuri zaidi.”
“Tukifika tu nitakwambia.”
“Oke, nitakukumbusha tukifika tu.”
“Lakini baba nakiona kifo kiko jirani yangu sana,” aliniambia Salome,
nikaogopa.
“Umekionaje?”
“Nikiangalia mbele nakiona.”
Nilianza kuogopa nikimkumbuka mpenzi wangu, Jennifer ambaye
alikufa, lakini nikajaambiwa na mama alikutana na msichana huyo na
ndiye aliyemleta kazini kwangu.
“Salome hutakufa bali utaishi na utayasimulia matendo makuu ya Mungu
aliyokutendea,” nilimwambia kwa ujasiri.
Tulipofika kwake, ile anakaa tu, nikumuuliza kisa cha kukataa kwenda
kwangu na kung’ng’ania kwake:
“Damas.”
“Naam.”
“Uko tayari nikwambie?”
“Niko tayari mke wangu.”
Salome alionekana kusita kuniambia huku akinitazama kwa wogawoga,
lakini baadaye akasema:
“Umesema yule ndiye baba yako mzazi?”
“Ndiyo. Kwani vipi Salome?”
“Mh! Hapana Damas.”
“Salome.”
“Abee.”
“Una maana gani, pale umemsikia akiwataja watu wa kijijini kabisa, leo
useme siye?”
“Damas inategemea.”
“Na nini?”
“Sikiliza ushauri wangu Damas.”
“Upi?”
“Niliyokwambia.”
“Lini?”
37 mama YANGU NI JINI
“Kumbuka.”
“Sikumbuki ndiyo maana nimekuuliza.”
“Damas, nenda nyumbani kwenu, kuna mambo mazito sana kule.”
“Salome, mbona unanitisha mpenzi wangu, si uweke wazi tu kama
Mungu amekujalia wewe maono.”
“Sikiliza Damas, yule baba yako wakati nataka kumuuliza kitu, sura yake
iligeuka, akawa kama mnyama wa porini usoni na ndipo ghafla nikajikuta
siwezi hata kutoa sauti na kuanza kukohoa.”
“Ha! Mbona mimi sikuona Salome, siyo kwamba unamzushia baba?”
“Damas, nielewe ninachokwambia, yule si baba yako.”
“Sasa ni nani?”
“Ni jini.”
“Salome unanitafuta ugomvi, una maana mimi nitakuwa naishi na majini
wangapi ndani, Henry mmoja ni jini, haya baba naye ni jini? Ina maana ile
nyumba yangu ni ya majini siyo?”
“Ndyo, nina wasiwasi hata na mama yako.”
“Salome unakwenda mbali sasa, uko ni mbali sasa.”
“Damas, hata kama unaumia lakini pokea ukweli. Huo ndiyo ukweli.”
Nilivuta pumzi kwa kasi kisha nikazitoa na kutulia kwa muda.
“Salome.”
“Bee.”
“Leo umetamka maneno mazito sana, lakini anyway, sasa nitawezaje
kukutii wewe wakati wote ninao nyumbani, Henry, mama na baba wote
wako kwangu.”
“Hao siyo. Wewe nenda kwenu ukaone hali halisi.”
“Mh! Haya sawa, nitakwenda d, lakini pale nyumbani nitagaaje?”
“Usiage.”
“Si watanitafuta?”
“Damas, hapa Njombe na Songea pana umbali gani, unaweza kwenda
ukarudi, si ndyo?”
“Oke, nimekupata mke wangu.”
Nilijiinamia kwa muda nikikumbuka mambo fulani kuhusu Henry, mama
na hatimaye baba:
“Hivi mama, kule kijijini naweza kupata kiwanja nikanunua?”
“Kwa nini usipate kama una pesa?”
“Sasa kwa pale nyumbani, kwa wapi panaweza kuwa na kiwanja?”

38 mama YANGU NI JINI


Mama anakunja sura kwa swali langu, mimi nilimkazia macho kwa
muda.
“Wewe kama unataka kiwanja, wasiliana na mdogo wako.” (Henry).
“M! Mama kama wewe hujui unadhani Henry atakuwa anajua nini?”
Huku akisimama: “Yeye ndiye mzururaji kule kijijini, anaweza kujua wapi
pana kiwanja cha kuuza.”
Nilishtuka ghafla kama nilikuwa usingizini, moyoni nikakiri kweli kuna
tatizo katika hawa wazazi wangu. Lakini nikapata wazo, kwamba kabla
ya kwenda nyumbani, Songea niende kwanza kwa mganga wa kienyeji
ambaye ni mtaalam wa kweli akaniangalizie maisha yale.
Sikumwambia Salome kuhusu mawazo yangu hayo, nikakaa naye
mpaka akawa ‘nomo’, niliondoka naye kurudi kwangu nikimwambia
asimuulize baba swali lolote wala asiwe na wasiwasi ila atakachotakiwa ni
kumwangalia kwa kumwibia ili tuweze kupata mambo mengi zaidi.
“Sawa,” alisema.
Tulipofika nyumbani, baba hakuwepo sebuleni. Nikajua mama alitoka,
wakakutana kwa hiyo alimpeleka chumbani kwake na kumwandalia
maji ya kuoga.
Nilimwita Segito, alipokuja nikamuuliza kama amemuona baba
yangu.”
“Mh! Mimi muda mwingi nilikuwa jikoni kaka, sijamuona.”
Nilimwangalia Salome ambaye naye alinikazia macho
kunishangaa.
“Ina maana hujui kama kuna mgeni alikuja hapa?”
“Nilisikia ukiongea na watu muda fulani lakini sikufuatilia, mi nilijua
ulitoka nao.”
“Mama?”
“Yupo kwake.”
“Mwite.”
Sagito aliondoka kwenda kumwita mama, baada ya dakika mbili alikuja:
“Unasemaje Damas.”
“Mama ulishalala?”
“Ndiyo,” alijibu kwa mkato wakati si kawaida yake.
“Mgeni?”
“Mgeni gani?”
“Ah! Mama, baba si amekuja?”

39 mama YANGU NI JINI


“Baba ‘ako gani?”
“Nina baba wangapi mimi?”
“Si mzee Ndomba.”
“Ndiyo huyo huyo ninayemzungumzia.”
“Si yupo kijijni.”
“Yupo kijijini wakati kaja leo.”
“Kaja wapi?”
“Si hapa.”
“Sasa yuko wapi?”
“Mh! Mama ina maana hujamuona baba?”
Salome akaingilia kati kwa kusema:
“Sasa my love, mama anahusika na nini? Baba kaja yeye hajui,
tumeondoka kwenda hospitali yeye pengine pia hajui.”
“Nani alikwenda hospitali?” akahoji mama.
“Haya sasa, si unaona? Mama hata hajui kama tulikwenda hospitali,”
alidakia Salome, akaendelea:
“Sikia mama, muda si mrefu kuna mfanyakazi mwenzake Damas alikuja
na baba, akasema ndiyo ameingia kutoka kijijini.”
“Ndiyo mkampeleka hospitali?”
“Hapana, mimi niliugua ghafla,” Damas akanikimbiza hospitali, baba
tulimwacha hapa.”
“Labda amekwenda kulala chumbani kwa mtoto wake, Henry.”
Wakati mazungumzo yakiendelea, Segito alikuwa amesimama,
nikamtuma akamwite Henry. Kuondoka kwake hakukutupa nafasi ya
kuongea kwani ukimya ulitawala mpaka aliporudi Segito.
“Anakuja.”
“Oke, wewe kaendelee na shughuli zako.”
Segito anaondoka, Henry anatokea akiwa anafunga vifungo vya shati.
“Naam.”
Ile itikia yenyewe nikajua siye Henry mdogo wangu, maana yule
angesema ‘naam kaka.’
“Baba uko naye huko kwako?”
“Ndiyo,” alijibu huku akifikicha macho ili kuona sawasawa.
“Khaa! Sasa kwa nini usimwamshe mama, si ndiyo mwenye jukumu la
kumpokea mumewe, akamwandalia maji ya kuoga na kumwonesha pa
kulala?”
40 mama YANGU NI JINI
“Mimi sikujua.”
“Hukujua kama?”
“Kama mama ndiyo mwenye jukumu.”
“Sasa si ndiye mumewe.”
“Samahani.”
Aliposema ‘samahani’, nilimwona Salome akigeuza shingo kuniangalia,
tukakutana macho.
Nilijua Salome aliniangalia vile kwa sababu Henry huyu aliniambia
‘samahani’, angekuwa Henry yule tunayemjua sisi angesema, ‘samahani
kaka.’
“Basi nenda kwamwamshe baba,” nilimwambia, akageuka na
kuondoka.
Huku nyuma, Salome alitingisha kichwa kwa ishara ya kusikitika
huku akisema maneno ya chini kwa chini ambayo haikuwa rahisi mimi
kuyasikia, ilibidi nimuulize:
“Unasemaje dear?”
“Mh! Siwezi kusema hapa, ila nina mengi,” alininong’oneza.
“Twende chumbani basi,” nilimwambia huku mimi nikiwa bado nimekaa.
Lengo langu yeye ndiyo atangulie kusimama na kuondoka.
Alisimama ndani ya sekunde kadhaa, akaenda na mimi nikasimama
kumfuata:
“My dear, unachelewa bure, utakuja kuumia mume wangu, hapa huna
ndugu wewe, huna mama, huna baba wala mdogo wako, nenda kijijini
even tomorrow (hata kesho),” Salome aliniambia.
Nilimkumbatia na kumwambia:
“Haiwezekani kabla sijaenda nikaenda kwa mganga akaniangalizia
kwanza?”
“Una amini?”
“Katika nini?”
“Mambo hayo?”
“Itabidi niamini.”
“Basi tutakwenda wote.”
“Hayo maneno,” nilisema tukatoka kurudi sebuleni. Hakukuwa na mama
wala Henry.
Nilimwita Segito.
“Naam kaka.”
“Mwite mama na Henry.”
41 mama YANGU NI JINI
Segito aliondoka, aliporudi akawa anaonesha uso wenye hofu na
wasiwasi.
“Vipi, wako wapi?” nilimuuliza.
“Nimegonga sana milango, hawajafungua…”
“Khaa! Mara hii?” aliuliza Salome akionesha uso wenye wasiwasi
mkubwa.
Mara tulisikia milio ya milango, kama inafunguliwa na kama inafungwa.
“Si hao?” nilisema mimi. Segito aliondoka, akachukua kama dakika kumi
huku mimi na Salome tukiwa tumekaa sebuleni.
Sijui nini kilitokea, ila ninachokumbuka ni kwamba, nilishtuka usiku
wa manane nikiwa chumbani, nilipoangalia pembeni yangu sikumwona
Salome.
Nilivuta kumbukumbu na kubaini kuwa, mara ya mwisho mimi na
Salome tulikuwa sebuleni tukisubiri ujio wa mama, baba na Henry ambao
walifuatwa na Segito.
Mbali na hapo, nikavuta picha na kukumbuka hata mazungumzo ya
Segito kwetu mara ya mwisho:
“Nimegonga sana milango, hawajafungua…”
Salome: Khaa! Mara hii?
Mara milio ya milango…
“Si hao?”
Segito anaondoka.
“Mh!” nilijikuta nikiguna baada ya kumbukumbu hiyo.
Nilikurupuka kutoka kitandani, nikajiangalia nilivyo, nilikuwa sijavua
nguo, nikatoka. Lakini ile nakaribia kushika kitasa cha mlango, nikakiona
kikizungushwa. Kwanza nilishtuka, nikajua maajabu yanaanzia pale,
nikarudi mbio kitandani huku nimeukazia macho mlango kuona nani
ataingia au nini kitaingia.
Nilianza kuona miguu, nikazidi kutumbua macho, ikawa inazidi kuingia
huku mapigo yangu ya moyo yakienda kwa kasi ya ajabu.
Nilishtuka kuona ni Salome. Aliingia akiwa anaonekana kushangaa:
“Dear, ikawaje tena?” aliniuliza, uso ulikuwa umemvimba kwa usingizi.
“Na mimi nashangaa sana baby.”
“Kwani ilikuwaje?”
“Sijui, nimeshtuka niko kitandani peke yangu, tena nilikuwa sijavua nguo,
nataka kutoka ndiyo nikaona mlango unafunguliwa, kumbe wewe.”
“Sasa Damas, ina maana kuna mtu alikuleta huku wewe mimi akanipeleka
42 mama YANGU NI JINI
jikoni?”
“Ha! Ina maana umejikuta upo jikoni?”
“Eee. Nimetokea jikoni. Yaani Damas lazima kuna kitu tu.”
Nilikaa kitandani na kujiinamia kwa muda kisha nikamuuliza Salome:
“Kwani mara ya mwisho si tulikuwa sebuleni?”
“Ndiyo.”
“Tulikuwa tukifanyaje?”
“Si tulikuwa tunamsubiri mama, Segito alikwenda kumwita.”
“Hakurudi?”
“Nani sasa?”
“Segito.”
“Sijui, si ndiyo nimeamka mimi najikuta niko jikoni!”
“Da! Panda ulale mke wangu, mambo mengine tutayajua asubuhi.”
“Hapana mume wangu, hatuwezi kulala, tuondoke usiku huuhuu
tukalale kwangu, asubuhi sana tudamkie kwa mganga wa kienyeji. Hii hali
inaashiria kifo.”
“Kwa maana gani?”
“Damas, usipende kuulizauliza, hapa pana hatari baba, mwisho wa siku
mmoja wetu atakufa, amini usiamini.”
Tuliondoka na Salome, hatukufunga mlango ila tuliurudisha tu, tukaanza
kutembea kwa tahadhari.
Mbele kidogo, Salome alinishika mkono kisha akauminya kama
anayeniambia kitu, nilimwangalia naye akainamisha uso, nikaangalia
pande zote lakini sikuona kitu.
Tulipofika mbele kabisa, akaniambia:
“Ulimuona?”
“Nani?”
“Henry.”
“Hapana, alikuwa kwa wapi?”
“Si tumempita pale.”
“Sasa kwa nini hukuniambia palepale?”
“Alikuwa uchi wa mnyama.”
“Uchi wa mnyama? Ina maana mchawi?”
“Sijui.”
Tulifika nyumbani kwa Salome, tukafikia kulala licha ya kwamba tulikuwa
tumechoka sana kwa mazingira yaliyojitokeza kwangu.
43 mama YANGU NI JINI
***

Ilikuwa asubuhi ya saa kumi na mbili na nusu, Salome aliniamsha,


nilipoamka nikagundua yeye alishaamka maana alikuwa amesimama
sakafuni:
“Damas, unajua maajabu yanatufuata mpaka huku?”
“Mpaka huku?”
“Ndiyo. Nimekuta mlango uko wazi, au hatukuufunga jana usiku?”
“Tuliufunga, si hata wewe ulisimama wakati naufunga?”
“Ndiyo nakumbuka.”
“Sasa imekuwaje ukawa wazi?”
“Si ndiyo hapo.”
Mara mlango ukagongwa.
“Atakuwa nani?” nilimuuliza kwa mshtuko Salome.
“Mh! Sijui, labda jirani,” na yeye aliniambia huku akienda kufungua.
Ghafla alirudi mbio huku akipiga kelele.
Nilimuuliza nini kilimpata akaniambia amemwona Henry.
“Sasa dear Henry ndiyo anakutia hofu hivi?”
“Amepajuaje hapa?”
Swali hilo kidogo na mimi lilinifungua akili kwani ni kweli kama Henry
alipajuaje pale wakati hakuwahi kufika hata siku moja.
Niliamka na kutoka nje, nikaenda mlangoni, lakini sikumkuta Henry.
“Darling.”
“Abee.”
“Una uhakika ulimwona Henry au mawazo yako tu?”
“Uhakika baby,” Salome aliniambia huku akija kwa wasiwasi.
“Mbona hayupo baby?”
“Nimemuona kabisa, tena tulipokutana macho akatabasamu.”

SAFARI YA KIJIJINI NA MAKABURI YA WAZAZI WANGU

Niliwaza kwa muda mrefu juu ya suala lile huku midomo ikinitetemeka
kwa woga. Nilianza kuhisi mauti mbele yangu.
“Salome.”
“Abee,” aliitika akitetemeka.
“Kifo kinanijia. Hii hali itaniua.”
44 mama YANGU NI JINI
“Si ndiyo maana nilikwambia uende nyumbani.”
“Mimi nadhani hakuna hata haja ya kwenda kwa waganga, niende tu
nyumbani Songea.”
“Itakuwa vizuri Damas.”
“Sasa kule nyumbani nimwache Segito na wewe au?”
“Hapana Damas, tutakwenda wote Songea.”
“Halafu mama tunaenda naye au?”
“Walio pale nyumbani tunawaacha wote. Ilimradi tuwaachie pesa za
matumizi tu.”
Tulijiandaa, tukaenda nyumbani na Salome, nikamwachia maagizo
Segito lakini sikumwambia nakwenda wapi, ila nilimwambia nitakuwa
sipo kwa siku mbili.Nikiwa sebuleni, nilimuuliza kama mama ameamka,
akasema aliamka akaniulizia, kisha karudi tena kulala, nikamwomba
akaniamshie.
Mara, mama alitokea akiwa anatembea kwa kujikongoja.
“Shikamoo mama.”
“Marhaba.”
“Vipi baba, kaamka?”
“Jamani, mbona sijui kama baba yako amekuja?”
“Basi mama. Sasa wewe kapumzike.”
Mama aligeuka na kuondoka, nikamuita Segito. Nilimuaga nikimwachia
pesa za matumizi. Nilimpigia simu bosi mmoja wa ofisini kumwomba
ruhusa ya dharura, lakini sikumwambia naondoka nje ya mji wa Njombe.
Tulipata basi la kwenda Songea, sikumbuki muda gani tuliingia. Pale
tukapanda basi jingine la kwenda kijijini. Tulifika saa kumi na moja
jioni. Wakati tunashuka na Salome, nilihisi ugeni, lakini baadhi ya watu
niliwafahamu, nao walinifahamu wakaja kunipokea.
“Za siku bwana Damas?”
“Nzuri tu,” tulisalimiana. Wa shikamoo niliwaamkia, wa marhaba
waliniamkia.
Nje nyumbani, alikaa mzee mmoja simfahamu, lakini nilipomwakia tu,
nikasikia sauti ya mdogo wangu Henry ikisema:
“Ha! Kaka.”
Alikuja mbio na kunikumbatia. Mimi na Salome tulishtuka sana. Wakati
tunasalimiana na Henry, wale walionipokea walishaondoka wakisema
watakuja kunisalimia vizuri kesho yake.
“Habari za Ulaya kaka?”
45 mama YANGU NI JINI
“Nzuri Henry. Huyu ni nani?” nilimuulizia yule mzee sasa.
“Tunaishi naye hapa kaka, muda mrefu. Alitokea Nyasa.”
“Sawa. Vipi mama, vipi baba?”
Henry aliangusha kilio palepale.
“Vipi Henry?” nilimuuliza kwa hofu kuu…
Henry aliendelea kuangua kilio kiasi cha kushindwa kuongea mpaka
Salome naye akaingilia kati kumbembeleza…
“Shemeji nyamaza, jikaze we ni mwanaume, kaka yako ni mgeni hapa
mpe maelekezo.”
Nilimgeukia yule mzee sasa…
“Eti, kuna nini kinaendelea hapa nyumbani?”
“Mama yako alishafariki dunia…”
“Aaaash,” nilishtuka nikishika kichwa na hapohapo machozi yalianza
kunitoka.
Yule mzee akanishika mkono na kunikalisha kwenye kiti kingine ambacho
ni imara zaidi kuliko kile nilichokalia kwanza.
“Nyamaza mjukuu wangu,”yule mzee alisema.
Nilijikaza nikatulia kidogo maana hata Salome aliniomba ninyamaze.
“Na baba?”
Safari hii alijibu Henry kwa haraka sana.
“Baba naye arobaini yake ilikuwa wiki iliyopita.”
Hapo nilijikuta nimeanguka chini na kupoteza fahamu.
Nilipokuja kurudiwa na fahamu, mwili ulikosa nguvu hata baada ya
kuzinduka, nilijikuta nikihisi kifo nakijua tofauti na zamani. Lakini akili
kichwani zilikuwa zikijichanganya na ile hali niliyoiacha nyumbani
kwangu, Njombe.
“Kwa hiyo Henry, mama alikufa siku zilezile nilivyosafiri?”
“Ndiyo kaka. Kama wiki moja baada ya wewe kuondoka.”
“Na baba naye alikuwa akiumwa nini?”
“Baba yeye alishikwa na tumbo, akalalamika kwa siku mbili akafariki
dunia.”
Mwanaume ni mwanaume, nilijikaza yakaisha yote.
Mimi na Salome tulikwenda makaburini kwa msaada wa Henry na mzee
mmoja mtani wetu. Baadaye tuliporudi nyumbani, nilikaa na Salome tu
na kujadili mambo fulani:
“Ina maana ni kweli wale nyumbani hakuna mama wala Henry, si ndiyo
46 mama YANGU NI JINI
sweet?”
“Hakuna hata baba pale.”
“Sasa tukirudi watatuambia nini?”
“Hatutawakuta.”
“Kweli?”
“Kwa vyovyote vile.”

MAMA JINI, BABA JINI, MDOGO WANGU JUNI, WOTE WATOWEKA

Baada ya kukaa nyumbani siku saba, tuliondoka kurudi Njombe. Tulimpa


Henry nauli na pesa za matumizi baada ya mwezi mmoja aje Njombe
nikimwachia maelekezo ya nini cha kufanya kabla ya kuja na wapi atafikia
ili anipate kirahisi.
Tulifika Njombe saa tisa alasiri, kiu yangu au shauku yangu kuu ilikuwa
kufika nyumbani ili tukaone nini kiliendelea.
Nyumba ilikuwa kimya, hakukusikika redio wala watu wanaoongea kwa
lolote lile. Salome ndiye aliyebisha hodi.
“Nani?” aliuliza Segito.
“Sisi.”
Segito aliposikia sauti zetu alikuja mbio kufungua mlango, akatukaribisha
ndani.
Wote tulifikia sebuleni huku macho yetu na Segito yakigongana kwa
maswali kila wakati licha ya kwamba tulikuwa tukisalimiana.
“Dada,” aliita Salome.
“Abee.”
“Mama yuko wapi?”
“Aliondoka mbona.”
Mimi na Salome tukaangaliana.
“Na Henry?” mimi niliuliza.
“Waliondoka wote, siku ileile mlipoondoka nyiye na wao wakasema
wanaondoka, hawakusema wanakwenda wapi.”
“Baada ya siku hiyo unaishije humu ndani?” salome alimuuliza.
“Niko salama kabisa dada.”
Salome alimruhusu Segito akaendelee na shughuli zake, tulipobaki
wawili nikasema:
“Hivi Salome, ina maana muda wote niliishi na mama jini siyo?”
47 mama YANGU NI JINI
“Ndiyo maana yake. Na siyo mama tu, baba na mdogo wako wote ni
majini.”
“Namtaja mama yangu ni jini kwa vile ndiye wa kwanza kunitokea. Kuna
uwezekano hata Henry na baba alikuwa yeye mwenyewe,” nilisema.
“Kabisa darling.”
“Mh! Sikuwahi kufikiria, kumbe ningejua niliporudi toka masomoni
ningeenda nyumbani.”
“Ilikuwa vigumu sasa, si mama alikuja, baadaye akaja Henry, ungekwenda
kufanya nini? Huoni ulipobaini kuna maswali mengi juu ya mama,
umekwenda umejua kila ktu,” alisema Salome.
Ni kweli mke wangu. Lakini nawaza je, haya yote yaliyotokea yana
uhusiano wowote na marehemu Jennifer au?”
“Acha kurudisha mawazo nyuma mume wangu, tuangalie mbele,”
alisema Jennifer, tukakumbatiana.
Kuanzia siku hiyo, nilianza kuwa makini sana na wageni, makini na hata
marafiki. Niligundua wengi tunaishi na watu siyo tukiamini ndiyo. Tuwe
makini sana.
Baadaye, Henry alikuja Njombe, nikamfungulia biashara ya duka
anaendelea nayo. Salome ana watoto wangu wawili. Segito aliolewa na
dereva wa Lori.

MWISH0.

48 mama YANGU NI JINI

You might also like