Professional Documents
Culture Documents
Siri Ya Kurudi Tena-A5
Siri Ya Kurudi Tena-A5
Aliyekuwa kilema
Aliyekuwa kilema, alipokea muujiza na kuanza alitembea, huko jijini
kutembea wakati wa mkutano ARUSHA (2013) MBEYA
© Haki ya nakala 2013
Nabii B.G. MALISA
Kanisa la Ukombozi Ministries For All Nations.
(UMINA)
P.O. Box 1961 Mwanza, Tanzania.
E- mail: ukombozichurch@yahoo.com
Published by:
Ukombozi Quality Media Publications
P.O.Box 1961 Mwanza, Tanzania
E- mail: ukombozichurch@yahoo.com
Printed by:
UMINA PRINTING PRESS
P.O.BOX 1961
MWANZA- TANZANIA
ISBN: 978–9987–9437– 4 – 6
ii
Yaliyomo:-
Shukurani ……………………………………………………………………………….. v
Utangulizi ………………………………………………………………………………. vi
Sura ya 1
Madhara ya kutokurudi tena …………………………………… …….. 1
Sura ya 2
Hata wakati wa Yesu Kristo kuna baadhi ya watu hawakurudi tena
…………………………………………………………………………………………………… 3
- Kuombewa mara moja haitoshi …………………………… 3
- Kuna roho ambazo huwazuia watu kurudi tena …….. 4
Sura ya 3
Mbinu anazozitumia shetani kuwazuia watu kurudi tena kwenye
kanisa lenye nguvu …………………………………………………………………. 5
- Hofu ya kuhama kanisa…………………………………………… 13
Sura ya 4
Siri ya siku ya Jumapili …………………………………………………………. 14
iii
Neno la faraja.
iv
Shukurani
vi
Sura ya 1
Madhara ya kutokurudi tena
USHUHUDA
Namkumbuka mama mmoja aliyekuwa TASA
kwa miaka 22, alipokuja kuombewa mama yule
kumbe alikuwana majini mahaba yaliyo mfunga
asiweze kuzaa kwamiaka yote hiyo “22”. Baada
ya maombezi Mama huyu alifunguliwa na
akabeba mimba, cha ajabu hakurudi tena
kanisani. Kwa bahati nzuri, siku moja
nilikutana naye mjini, nikamuuliza, “mbona
hukurudi tena kanisani”?
1
Akanijibu, mambo yalikuwa mengi. Akasema,
kweli uliponiombea tu, nilifunguliwa na nika
beba mimba ilipofikisha miezi saba (7), mimba
ilitunga nje ya mfuko wa uzazi. Madaktari
wakaitoa.
- Unapo-ombewa na mtumishi wa
Mungu mwenye nguvu kubwa ya
Mungu halafu ukatoka ukaenda kwa
mtumishi mwenye nguvu ndogo lazima
matatizo yako yatarudi tena. Lazima
ufahamu kuwa watumishi wa Mungu
wanatofautiana kwa viwango vya
upako
2
Sura ya 2
Hata wakati wa Yesu Kristo kuna baadhi
ya watu hawakurudi tena.
Siri kubwa!
Matatizo yanafanana na miti. Mti wenye umri wa miaka 50,
siyo sawa na mti wenye umri wa miezi 2. Ni rahisi sana
kuung‟oa mti wenye umri wa miezi miwili au mwezi mmoja
lakini isiwe rahisi kuung‟oa mti wenye umri wa miaka 50.
Ndivyo ilivyo kwenye matatizo sugu.
USHUHUDA
Mwaka 2008 nilifanya kongamano la uponyaji ndani
ya ukumbi wa shinyanga “guest” jijini Mwanza.
Mama mmoja alikuja akiwa analia machozi kwa
sababu alikuwa TASA kwa miaka zaidi ya 11. Kweli
mama huyu nilimuombea na baada ya miezimichache
alifunguliwa na kupokea muujiza akawa mja mzito
yaani akabeba mimba. Mama huyo nilimpa agizo
kwamba anapaswa kuendelea kuombewa sana na
kufundishwa kwani alikuwa amefungwa sana na
nguvu za giza, lakini yeye alipuuza na HAKURUDI
TENA!!
5
Sura ya 3
Mbinu anazozitumia shetani kuwazuia watu
kurudi tena kwenye kanisa lenye nguvu.
6
2. Mbinu nyingine anayoitumia shetani kuwafanya
watu wasirudi tena ni hii; SHETANI HUWAFANYA
WATU WAONE KWAMBA KANISA LIKO MBALI
SANA. Hii ni mbinu kubwa sana anayoitumia shetani
kuwafanya watu wasirudi tena. Watu wanatafuta pesa
kutoka mbali. Kuna watu wanaishi MUSOMA na kila siku
wanakwenda MWANZA kufanya biashara, na wala
hawalalamiki kwamba Mwanza ni mbali! Kwenye masuala
ya PESA watu huwa hawaangalii umbali.
7
USHUHUDA
Baba mmoja aliyekuwa ameathirika kwa UKIMWI, baba
huyu hakukata tamaa. Hakuacha kuhudhuria kwenye
ibada na kwenye maombezi kila alipoambiwa aende
kupima damu yake, alikuta damu ina virusi vya ukimwi.
Yule baba hakukata tamaa bali aliendelea kuhudhuria
kanisani na kuhudhuria maombezi. Siku moja baba huyo
alienda kupima tena ikiwa ni mara ya kumi (10) Bado
majibu yalikuwa mabaya lakini alipokwenda mara ya 11
alishangazwa na majibu kwani alikuta damu yake ni
“NEGATIVE” yaani alipona.
Kama angekata tamaa mara ya kwanza au mara ya pili au
mara ya tano au mara ya kumi asingepona. Hili ndilo
tatizo la watu wengi kushindwa kupokea miujiza yao kwa
sababu ya kukata tamaa mara ya kwanza tu!
4. VIONGOZI WA DINI
Viongozi wa dini ndiyo walio msumbua sana Yesu Kristo
alipokuwa duniani. Hao ndiyo waliomuua Yesu, ndiyo
walio lisumbua kanisa la Mitume kule Yerusalemu.
Ulipokuwa unasali kwenye dini zao, walishindwa
kukusaidia ndiyo maana ulikuwa umefungwa na
majini, mizimu,umaskini, magonjwa na laana za kila
aina, sasaiweje leo umefunguliwa kwenye kanisa la
Ukombozi halafu wakwambie umepotea?
Soma LUKA 22:1 - 2
8
Ibilisi anaweza kuwatumia viongozi wa dini kule
ulikokuwa unasali wanaanza kukufuatilia kwa vitisho na
kukukatisha tamaa ili uache wokovu/ usiende kwenye
kanisa lenye nguvu. Wanaweza kukuambia, „yaani wewe
umeacha dini yako nzuri; dini ya baba zako,
umepotea; hilo kanisa uliloenda ni la mashetani,
wachawi, n.k
Viongozi hawa hutumia kila mbinu ili kukufanya uiache
imani ya wokovu wanatumia mafundisho ya uongo
wakiwa ni mfano wa watu wanaokusaidia kumbe lengo ni
kukuangamiza.
5. NDUGU ZA UONGO.
Hii ni mbinu nyingine kubwa sana anayoitumia shetani ili
kuwarudisha watu wengi kwenye dhambi. Wengi
wamekatishwa tamaa na hawa wanaoitwa ndugu za
uongo.
“Kwa kuwa ijapokuwa mna walimu kumi elfu katika Kristo, walakini
hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu
kwa njia ya Injili.” 1WAKORINTHO 4:15
10
6. SAUTI ZA SHETANI
IWAKORINTHO 14:10; “Yamkini ziko sauti za namna nyingi
duniani, wala hakuna moja isiyo na maana.”
Shetani anaweza kutumia sauti za ki-geni ili akurudishe
nyuma na uache wokovu. Shetani hutumia sauti
zisizosikika katika masikio ya kawaida.
“Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala
hakuna moja isiyo na maana” 1WAKORINTHO 14:10
Shetani ni roho isiyo-onekana kwa macho ya kawaida,
kwa hiyo ili akudanganye atatumia sauti kwenye
ulimwengu wa roho.
Wakati wa Yesu
Shetani alikwenda kumjaribu Yesu Kristo, pale
alipomwambia,
“Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe
Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya
yawe mikate.” MATHAYO 4:3
Ushuhuda
Dada mmoja aliamini kwamba mtumishi mmoja wa Mungu
siyo mtumishi wa kweli wa Mungu bali anatumia nguvu za
giza eti kwa sababu alimuota usiku yupo kifua wazi.
Nilijaribu kumsaidia kwamba, asijenge msingi wake kwenye
NDOTO na MAONO na hatimaye aliweza kufunguka
13
Lazima ukubali kupandwa kwenye kanisa moja!
Hakuna mti unaoweza kuzaa matunda kama haujapandwa,
kwenye udongo na mizizi yake kwenda chini ya udongo. Mimi
sijawahi kuona mti upo hewani na umezaa matunda, hii
haiwezekani!!
Ndivyo ilivyo, kuna kupandwa ki- roho. Biblia imefundisha siri
hii.Soma ZABURI 92:13
“Waliopandwa katika nyumba ya BWANA Watastawi
katika nyua za Mungu wetu.”
Watu wengi wanakwenda kwenye makanisa kwa ajili ya
kuombewa tu, hawataki kupandwa kwenye hayo makanisa.
Wengi wanakuja kwenye kanisa letu la Ukombozi kwa ajili ya
kuombewa tu na wala hawako tayari kupandwa kwenye kanisa
letu ndiyo maana hawapokei muujiza wowote. Kama umetoka
kwenye dini yako na ukaja kanisani kwetu ili kuombewa, hii
inamaanisha huko uliko toka kwenye dini yako hakukuwa
na MSAADA; sasa kwa nini usikubali kupandwa kwenye
kanisa letu?
15
Wengi wanauliza maswali, “kwa nini kanisa la
Ukombozi wana chukua muda mrefu sana
kushinda kanisani yaani siku yote ya Jumapili
wanaimalizia kanisani.”
16
Mimi huwa nashangaa kwa nini Mungu huwa
tunampa muda mdogo namna hii? Ambaye yeye ndiye
chanzo cha Baraka zetu. Tunaona nyakati za zamani
watu waliofanikiwa sana na kuwa na afya na utajiri ni
kwa sababu walimpa Mungu nafasi kubwa sana ya
“kumuabudu”.
17
Mfano mzuri wa Yesu Kristo Bwana wetu alichukua
muda mrefu sana kwenye ibada zake. Kuna siku moja
aliwafundisha watu kwa muda wa siku 3 usiku na
mchana. Soma MATHAYO 15:32 Hapa Yesu Kristo
alikaa na watu hawa wanaume na watoto pia wanawake
kwa siku 3 na palikuwa “nyikani”yaani jangwani. Yesu
hakuangalia kuna wake za watu au kuna watoto Yesu
hakujali kama wana njaa. Hii ndiyo siri ya miujiza
aliyokuwa nayo Yesu Kristo. Siri ilikuwa ni kumpa
Mungu BABA muda mrefu wa kutosha wa kumuabudu.
18
Kama wanaume wetu, tunawapa muda wa kutosha/ wake
zetu tunawapa muda wa kutosha na kama biashara tunatoa
masaa karibu 60 kwa wiki kwa nini Mungu tusimpe hata
masaa 10 tu kwa wiki?
SIRI KUBWA
19
MAMBO YA KUZINGATIA ILI TUUKULIE WOKOVU