Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

TİKA PROGRAM YA KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO AÇSAP

Kama sehemu ya programu maalum zilizofanywa na TİKA na Wizara ya Afya ya Jamhuri ya


Uturuki, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya nchi inayopokea Programu ya Msaada wa
Afya ya Mama na Mtoto (AÇSAP) imetekelezwa kwa mafanikio katika nchi nyingi na kwa
sasa inaendelea ili kuongeza asili ya matokeo ya rasilimali watu katika sekta zote chini ya
uratibu wa Miradi ya elimu ya TİKA
Awamu ya kwanza ya mpango ni pamoja na:
1. Karibu Mtoto
2. Ufufuaji wa Maisha ya mtoto mchanga (Neonatal Resuscitation)
Mafunzo ya Ufufuaji wa Maisha ya mtoto mchanga inachukuliwa kuwa jambo muhimu zaidi
la uzoefu uliofanikiwa ambao Uturuki imepata katika kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Kwa kuchukua hatua muhimu katika dakika chache za kwanza baada ya kuzaliwa,
inawezekana kupunguza vifo vya watoto wachanga. Ili kujifunza hatua hizi muhimu ambazo
wafanyikazi katika chumba cha kujifungulia watatumia kama timu kwa njia ya utaratibu,
moduli ya mafunzo ya siku tatu, ambayo inakubalika kama kiwango cha kawaida
ulimwenguni kote, lazima itekelezwe kwa umakini zaidi.
Kabla ya mafunzo ya vitendo katika mbinu za kufufua Watoto wachanga zilizotolewa na
waganga wa Kituruki kwa washiriki Pamoja na wataalamu neonatolojia wan chi husika,
wakunga na wauguzi, mtihani wa kuwapima kiwango unasimamiwa ili kutathmini maarifa na
ujuzi wao. Hii inaruhusu udhibiti wa ufanisi na uwezo wa kujifunza wa mafunzo. Washiriki
wanaofaulu mitihani mwishoni mwa kozi wanastahili kupokea vyeti.
Sanjari au mfululizo na mafunzo haya, programu za mafunzo juu ya:
1. Uchunguzi wa kusikia kwa watoto wachanga
2. Uchunguzi wa Macho wa Mtoto mchanga (retinopathy)
pia hutolewa na wataalam kutoka Uturuki kwa wataalamu husika katika eneo hilo.
Baadaye, kikundi cha wataalam wanaohudhuria Mafunzo ya Utunzaji Baada ya Kufufua
ambayo yatatekelezwa ndani ya nchi wanachaguliwa kushiriki katika Mafunzo ya Mwalimu
wa Ufufuo wa Watoto Wachanga nchini Uturuki.
Inatarajiwa kuwa wataalam wanaopata Mafunzo ya Wakufunzi nchini Uturuki watashajihisha
programu za mafunzo zitakazoandaliwa katika nchi iliyopokea mafunzo hayo pamoja na nchi
jirani, kwa ushiriki na ufuatiliaji.
Lengo la mpango huo, ambao utatekelezwa kwa muda mrefu, kulingana na matarajio ya nchi
mpokeaji, ushiriki, ufuatiliaji, na shauku, ni kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto
wachanga katika nchi nzima inayopokea mafunzo hayo.
Picha kutoka nchi ambazo programu ya mafunzo inatekelezwa

You might also like