Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 54

KITIVO CHA THEOLOJIA

IDARA YA UTAFITI

NINI CHANZO CHA WAKRISTO KURUDI NYUMA


KIIMANI KATIKA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE?
ENEO LA UTAFITI NI WILAYA YA KIGAMBONI MKOA
WA DAR ES SALAAM, TANZANIA.

NA

ANNIE OSCAR BWANALI

RIPOTI YA UTAFITI WA SHAHADA YA KWANZA YA


THEOLOJIA KATIKA UONGOZI WA KIKRISTO NA
MAENDELEO YA JAMII

2023
NINI CHANZO CHA WAKRISTO KURUDI NYUMA
KIIMANI KATIKA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE?
ENEO LA UTAFITI NI WILAYA YA KIGAMBONI MKOA
WA DAR ES SALAAM, TANZANIA.

NA

ANNIE OSCAR BWANALI

RIPOTI YA UTAFITI INAYOWASILISHWA KWAAJILI YA


KUHITIMU SHAHADA YA KWANZA YA THEOLOJIA KATIKA
UONGOZI WA KIKRISTO NA MAENDELEO YA JAMII

2023
UTHIBITISHO

Aliyetia sahihi hapa chini, anathibitisha kuwa amesoma utafiti huu unaosema “Nini

Chanzo cha Wakristo kurudi nyuma kiimani katika makanisa ya Kipentekoste? Eneo la

Utafiti ni Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania” na anapendekeza

ikubaliwe na Chuo cha New Life Academy of Leadership kwa ajili ya kutimiza sehemu ya

masharti ya kutunukiwa Digrii ya Theoloji katika Uongozi wa Kikristo na Maendeleo ya

Jamii katika Chuo cha New Life Academy of Leadership.

…………………………….

Msimamizi

Tarehe: Thursday, August 24, 2023

i
HAKIMILIKI

Hairuhusiwi kuiga au kunakili kwa namna yoyote sehemu yoyote ile ya utafiti huu kwa

njia yoyote kama vile, kielektroniki, kurudufu nakala, kurekodi au njia yoyote nyingine

bila ya idhini ya mwandishi au Chuo cha New Life Academy of Leadership kwa niaba.

ii
TAMKO LA UTAFITI

Mimi, Annie Oscar Bwanali, nathibitisha kuwa utafiti huu ni kazi yangu halisi na

haijawahi kuwasilishwa katika Chuo Kikuu kingine chochote kwa ajili ya kutunukiwa

shahada kama hii au nyingine yoyote.

_______________________

Saini

Tarehe: Thursday, 24 August 2023

iii
SALAMU

Kazi hii iwafikie familia yangu.

iv
SHUKRANI

Kukamilisha kazi hii mpaka katika hatua hii iliyofika ni jambo la kumshukuru sana

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya

njema na akili timamu katika kipindi cha mwaka mmoja nilichotumia katika kusoma

shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Uongozi wa Kikristo na Maendeleo ya Jamii

katika Chuo cha New Life Academy of Leadership.

Pia, namshukuru msimamizi wangu wa kazi hii kwa kunisimamia vizuri tangu katika

uandishi wa pendekezo la utafiti, uandishi wa ripoti ya utafiti kama ilivyo hivi sasa.

Namshukuru sana kwa kunitia moyo kila mara nilipokwama na kutokuiona njia yeye

aliniongoza na kunishauri.

Nawashukuru pia familia yangu ilikuwa bega kwa began na mimi mpaka kukamilisha kazi hii

ya utafiti.

v
IKISIRI

Mada ya utafiti huu ni kutathmini chanzo cha Wakristo kurudi nyuma kiimani katika

makanisa ya Kipentekoste: Eneo la Utafiti ni Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es

Salaam, Tanzania. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni kujua kwanini watu

wanahama makanisa. Ili kukamilisha malengo haya mahususi, data za utafiti zilikusanywa

kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Utafiti umepata matokeo

yanayoonesha kuwa watu wengi wanahama makanisa na kuacha wokovu kwasababu

kutokana na watu kukosa majibu ya ahadi walizoahidiwa kabla ya kuokoka. Utafiti

umependekeza kuwepo na mafundisho endelevu ya kuukulia wokovu baada ya watu

kuokoka ili wasirudi nyuma kiimani, pia kuwepo na ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa

wale waliookoka ikiwezekana kujua mahitaji yao ya kiroho na kimwili ili ikiwezekana

yajibiwe, pia kufanyike maombi ya mara kwa mara kwaajiri ya watu wapya waliookoka.

vi
YALIYOMO
UTHIBITISHO..........................................................................................................i

HAKIMILIKI............................................................................................................ii

TAMKO LA UTAFITI............................................................................................iii

SALAMU.................................................................................................................iv

SHUKRANI..............................................................................................................v

IKISIRI..................................................................................................................... vi

YALIYOMO...........................................................................................................vii

SURA YA KWANZA...............................................................................................1

UTANGULIZI..........................................................................................................1

1.1 Utangulizi............................................................................................................1

1.2 Chimbuko la Utafiti.............................................................................................1

1.3 Kauli ya Utafiti....................................................................................................5

1.4 Malengo ya Utafiti...............................................................................................6

1.4.1 Lengo kuu la Utafiti..........................................................................................6

1.6 Umuhimu wa Utafiti............................................................................................6

1.7 Mipaka ya Utafiti.................................................................................................7

1.8 Mpangilio wa Utafiti...........................................................................................7

SURA YA PILI.........................................................................................................8

MAPITIO YA NYARAKA.......................................................................................8

2.1 Utangulizi............................................................................................................8

2.2 Maana ya Maneno Muhimu.................................................................................8

2.3 Mapitio ya Nyaraka...........................................................................................11

SURA YA TATU....................................................................................................15

vii
MBINU ZA UTAFITI.............................................................................................15

3.1 Utangulizi..........................................................................................................15

3.2 Mtindo wa Utafiti..............................................................................................15

3.3 Eneo la Utafiti...................................................................................................16

3.4 Sampuli na Usampulishaji.................................................................................16

3.5 Aina ya Data Zilizokusanywa............................................................................16

3.5.1 Data za Msingi................................................................................................17

3.5.2 Data za Upili...................................................................................................17

3.6 Mbinu za Kukusanyia Data...............................................................................17

3.6.1 Upitiaji wa Nyaraka........................................................................................17

3.6.2 Dodoso...........................................................................................................18

3.6.3 Mahojiano.......................................................................................................18

3.7 Vifaa vya Utafiti................................................................................................18

3.8 Uchambuzi wa Data..........................................................................................19

3.9 Uzingatiaji wa maadili.......................................................................................20

SURA YA NNE......................................................................................................21

UWASILISHAJI, UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA UTAFITI...........................21

4.1 Utangulizi..........................................................................................................21

4.2 Matokeo ya Utafiti.............................................................................................21

SURA YA TANO...................................................................................................38

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO.......................................................................38

5.1 Utangulizi..........................................................................................................38

5.2 Hitimisho...........................................................................................................38

5.3 Mapendekezo.....................................................................................................40

viii
MAREJEO..............................................................................................................42

VIAMBATANISHO...............................................................................................43

ix
SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

1.1 Utangulizi

Sura hii inawasilisha utangulizi wa utafiti huu. Vipengele vilivyomo ndani ya sura hii ni

chimbuko la utafiti, kauli ya utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa

utafiti na mipaka ya utafiti na mpangilio wa utafiti.

1.2 Chimbuko la Utafiti

Mithali 1:32-33 Biblia mahali hapo inasema; “Maana kurudi nyuma kwao wajinga

kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye

atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.” Ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa

sio wakristo wote wanaopata neema ya kuzaliwa mara ya pili au kuokoka wanapata neema

vilevile ya kuukulia wokovu, wengine wanarudi nyuma na hata kufa kiroho kutokana na

sababu mbalimbali, wote tunafahamu kuwa ziko sababu mbalimbali za kwanini,

watu wanarudi nyuma na hatimaye kufa kiroho, lakini katika somo hili tutajaribu

kuchambua chache kati ya hizo.

Luka 8:13 Biblia inasema “Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea

lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa

kujaribiwa hujitenga.” Ni muhimu kufahamu kuwa mara baada ya kuokolewa kila mtu

aliyeokoka anapaswa kuhakikisha kuwa analifanyia kazi neno la Mungu na kujijengea juu

ya msingi huu, kila mmoja anapaswa kuota mizizi na sio tu kuota lakini kuhakikisha kuwa

mizizi yake inashuka chini sana, tatizo kuu la wakristo wengi sana wako katika kundi hili

linalotajwa na Yesu Kristo kama watu au mioyo inayolipokea neno la Mungu kwa furaha

lakini hawana mizizi, hawaendelei mbele wanadumaa na hatimaye kuiacha imani, Hawa

1
pia wanaweza kufananishwa na mtu aliyejenga nyumba yake kwenye Mchanga Mathayo

7:24-27 “.Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu

mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja,

pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu

ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu

mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja,

pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”

Unaweza kuona tatizo kubwa la wapendwa wengi sio tu kulitendea kazi neno lakini hata

kulielewa hawalielewi,wako wakristo ambao hata hawajui kwanini wanatoa sadaka, kwa

nini wanahudhuria ibada katika kanisa wanalohudhuria, kwa nini wanaomba, kwa nini

wanene kwa lugha? Na wakikutana na changamoto ndogo tu wanakwazika na

kuchanganyikiwa, Hwawezi kuitetea imani, Hawana ujuzi wala uzoefu katika kutembea na

Mungu ni wakristo ambao hawawezi kusema Mungu amezungumza name na wakikusikia

kuwa unasema umezungumza na Mungu wanashangaa, hawana ushuhuda wao wenyewe.

Mkristo mwenye Misingi imara anapaswa kusimama mwenyewe haijalishi hata kama mtu

aliyekuingiza katika ukristo amehama imani na kujiunga na imani potofu, yeye anaendelea

kusimama kwa gharama yoyote, wazazi ndugu jamaa au rafiki wa karibu hawezi

kubadilisha msimamo wa mtu mwenye mizizi, utashangaa kuona mtu aliyeokoka hajui

hata tofauti ya Mashahidi wa Yehova na hata wasabato yeye kila aina ya fundisho na imani

na kila aina ya upepo wa Elimu unamzoa tu!

Mkristo mwenye mizizi kamwe hawezi kuyumbishwa na jaribu la aina yoyote,taarifa

mbaya kuhusu kiongozi wako wa kidini haiwezi kuwa sababu yaw ewe kuiacha imani,

unaweza kuwepo kanisani lakini kama mimani yako haijajengwa kwenye misingi na

haijaota mizizi ni rahisi kujikuta matatani, Dhambi za kiongozi wako wa kidini

2
zinauhusiano gani na wokovu wako?uwapo duniani je unafikiri unaweza kumuacha Yesu

kwa sababu ya dhambi ya kiongozi wako?mkristo anayeweza kumuacha Yesu kwa sababu

ya tatizo la mtumwingine huyo hana misingi wala hajaota mizizi hajakomaa.

Mkristo aliyesimama vema ni yule ambaye amesimama hawezi kutikiswa na kurudi nyuma

kwa wengine Yohana 6:66-69 “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake

wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je!

Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani?

Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe

ndiwe Mtakatifu wa Mungu.” 

Wanafunzi wa Yesu wenye msimamo kama Petro hawakuweza kuacha kuandamana na

Yesu kwa sababu walitambua kuwa Yesu anao uzima wa milele, Mtu ambaye hajajengwa

kwenye msingi na hana mizizi kwake ni rahisi kukata tamaa, ni vigumu kwake kupokea

neno gumu na kusonga mbele kwao ni rahisi kukwazika tu na kungung’unika na kurudi

nyuma Biblia haitutii moyo kumfuata kiongozi awaye yote anapokuwa amekengeuka

badala yake inatutia moyo kumfuata Yesu au kumfuata kiongozi kama anamfuata Yesu

pale anapokengeuka sisi tunasonga mbele na Yesu tu, tukimuombea yeye au kumuacha na

ukengeufu wake Paulo mtume alisema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo 1

Wakoritho 11:1 “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.” Ukiwa kiongozi wa

kiroho ni rahisi sana washirika wako kukutii katika jambo lolote utakalowaamuru,

wanakutii wanakuheshimu wanakusikiliza, lakini ni muhimu kuwafundisha washirika wetu

kumfuata Yesu na sio mtu au dhehebu, wengi tumewaharibu washirika katika makanisa

kwa sababu ya kuwaaminisha katika Dhehebu na katika mtu, badala ya Yesu na kuwafanya

kuwa wanafunzi wa neno la Mungu, sisi watumishi wa Mungu ni binadamu na

tunauwezekano mkubwa sana wa kufanya dhambi tena kubwa na za aibu tu, hivyo ni

3
lazima ieleweke wazi kuwa kama tutawaambia washirika wetu kutenda jambo ambalo sio

la kibiblia basi wawe na uwezo wa kusema hapana kubwa, na kama tutafundisha fundiso

lisilo la kibiblia pia wawe na uwezo wa kutuambia Mchungaji, Mwinjilisti, Nabii, Mtume,

Mwalimu na kadhalika je hili fundisho ni la msingi wa kibiblia?

Pasipo kuwajenga washirika katika kuwa wanafunzi wa Yesu kumepelekea baadhi ya

watumishi wanafikia ngazi hata ya kuoga na mshirika kwa madai kuwa ni oga takatifu,

wengine wameweza kuwaibia wakristo mali zao zote kwa kisingizio cha kumtolea Bwana,

haya na mauchafu mengine mengi yanaweza kufanyika kwa sababu wakristo wengi

wamedumaa kiroho na hawataki kujijenga juu ya msingi na kuota mizizi mikali katikia

imani hivyo wanazolewa na kila mbwembwe za kila upepo wa kila elimu hata zile zisizo

na uungu ndani yake!

Nikwa sababu kama Hizi Paulo alisema mnifuate mimi kama ninavyomfuata Kristo hii ni

kwa sababu Paulo mtume alikuwa na uhakika wa mwenedo na tabia yake katika Kristo,

alikuwa mwaminifu, wakristo ni lazima wajifunze neno la Mungu na kuwa na mizizi na

kuwa ma misingi imara ya kutokuyumbishwa na aina yoyote ya ukiroho wa mtu, kumbuka

kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ya kiroho anaweza kukengeuka na kurudi nyuma, Je

hatusomi katika maandiko kuwa Haruni aliruhusu makutano kuabudu sanamu Hapo Musa

alipokuwa mlimani kuomba? Musa alipokawia mlimani je Israel wote hawakugeuka na

kushindwa kusimama katika zamu yao  na kuabudu miungu ya sananu huku wakisema

kuwa ndio mungu aliyewaokoa katika mikono ya Farao huko Misri? Ni wazi kuwa watu

hawa walikuwa hawajajengeka katika imani, walikuwa hawana msingi na walikuwa

hawana mizizi katika ujuzi wao binafsi na Mungu kumbuka kuwa Mungu si wa mkumbo,

kila mmoja anapaswa kujijengea uzoefu binafsi katika kuwa na uhusiano wako na Mungu

bila kufuata mkumbo. diraelimu.blogspot.com

4
Wengi wa walioabudu sanamu chini ya uongozi wa Haruni walikuwa ni watu waliofuata

mkumbotu, wengi wa walioangamizwa jangwani walikuwa ni watu walionung’unika kwa

sababu ya taarifa za wapelelezi, kumi waliokosa imani na hawakuwajali wawili waliokuwa

na imanikwa Mungu, wengi pia wa waliomfuata mkumbo wakati Yesu anasulubiwa na

kupiga kelele wakisema asulubiwe asulubiwe hawakuwa na msimamo wao thabiti bali

walikuwa watu walifuata umati au mkumbo, kufuata mkumbo katika kutenda uovu ni

tatizo kubwa sana kwa wakristo wa nyakati za leo hebu komaa kiroho, hebu kataa

kudumaa, hebu kubali kuongozwa na neno na uote mzizi ya ujuzi wako mwenyewe

mfanye Mungu kuwa Mungu wako na neno lake kuwa neno lako, usikubali kwenda kwa

mkumbo Muombe Mungu akupe neema ya kusimama kwa miguu yako na uwe mkristo

mwenye mizizi iliyozama sana chini katika imani.

1.3 Kauli ya Utafiti

Kanisa la kwanza ambalo lilikuwa la mitume pamoja na waliookoka baada yao lilidumu

katika misingi minne ukisoma kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume 2:42 inasema

“Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika na katika kuumega

mkate na kusali” na nyongeza yake ni Matendo ya Mitume 4:32 ambayo inasema “Na

jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja

aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe bali walikuwa na

vitu vyote shirika. Ukiangalia mistari utagundua ya kwamba kanisa lilidumu katika imani

maana watu hawakuweza kurudi nyuma kiimani wala kuacha wokovu waliimarika

walipata mafundisho sahihi, walijibiwa mahitaji yao, walipata amani ya moyo maana yake

waliridhika. Ili kwasasa imekuwa tofauti ndio maana kunatokea kurudi nyuma kwa imani

za Wakristo na kuacha wokovu. Hivyo basi utafiti huu umekusudia kutathmini chanzo cha

5
Wakristo kurudi nyuma kiimani katika makanisa ya Kipentekoste: Eneo la Utafiti ni

Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania.

1.4 Malengo ya Utafiti

1.4.1 Lengo kuu la Utafiti

Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini chanzo cha Wakristo kurudi nyuma kiimani katika

makanisa ya Kipentekoste.

1.4.2 Malengo Mahususi

Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi yafuatayo;

i. Kutambua dhana ya kurudi nyuma kiimani.

ii. Kutathmini sababu za Wakristo kuhamahama makanisa.

iii. Kupendekeza jinsi ya kudumu katika imani.

1.5 Maswali ya Utafiti

Utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo;

i. Ipi dhana ya kurudi nyuma kiimani?

ii. Zipi ni sababu za Wakristo kuhamahama makanisa?

iii. Zipi ni njia za kudumu katika imani?

1.6 Umuhimu wa Utafiti

Utafiti huu una umuhimu sana katika kanisa. Kwa upande wa taaluma, utafiti huu utakuwa

ni rejeleo muhimu kwa wahadhiri, walimu na wanafunzi wanaosoma na kujifunza taaluma

za Theolojia. Wahadhiri na walimu watautumia utafiti katika kuandaa maandalio ya somo

na kukuza utafiti zaidi katika uwanja wa maswala yahusuyo imani na namna ya

6
kuwaimarisha Wakristo makanisani ili wasirudi nyuma kiimani. Wanafunzi wa taaluma ya

Theolojia watautumia utafiti huu katika kujisomea na kuandaa mapendekezo ya utafiti

ambao wataufanya baadae. Kwa upande wa kanisa utafiti huu utasaidia kulijulisha kanisa

namna sahihi ya kuwasaidia watu wanaookoka makanisani ili wasirudi nyuma kiimani na

kuwapa mafundisho sahihi. Mambo haya yatawanufaisha wasomaji wote watakaosoma

utafiti huu katika maisha yao ya kila siku.

1.7 Mipaka ya Utafiti

Utafiti huu unafanywa kwa lengo la kutathmini chanzo cha Wakristo kurudi nyuma

kiimani katika makanisa ya Kipentekoste: Eneo la Utafiti ni Wilaya ya Kigamboni Mkoa

wa Dar es Salaam, Tanzania, lakini kulingana na malengo ya utafiti huu ilionekana kuwa

eneo hilo moja linatosha. Utafiti huu ulichukua miezi mitatu ili kukamilika.

1.8 Mpangilio wa Utafiti

Utafiti huu una jumla sura tano ambapo sura ya kwanza inahusu utangulizi na usuli wa

tatizo la utafiti, sura ya pili inahusu mapitio ya kazi tangulizi na mkabala wa kinadharia na

sura ya tatu inahusu mbinu za utafiti. Sura ya nne inahusu uwasilishaji, uchambuzi na

mjadala wa data za utafiti na sura ya tano ni hitimisho na mapendekezo.

7
SURA YA PILI

MAPITIO YA NYARAKA

2.1 Utangulizi

Sura hii inazungumzia mapitio ya nyaraka zinazohusiana na utafiti huu.

2.2 Maana ya Maneno Muhimu

Mkristo: Kwa tafsiri kutoka kamusi ya Webster mkristo ni “mtu mwenye kukiri imani

ndani ya yesu kama kristo au dini yenye msingi wa mafundisho ya yesu.” Ijapokuwa huu

ni mwanzo mwema wa kufahamu mkristo ni mtu gani, kama maelezo mengi ya kidunia

yalivyo, inapungukiwa na uhalisi wa kibiblia juu ya Maana kamili ya ukristo au mkristo.

Neno mkristo limetumika mara tatu katika agano jipya (Matendo 11:26; Matendo 26:28; 1

Petro 4:16). Wafuasi wa yesu kristo waliitwa kwa mara ya kwanza “wakristo” antiokia

(Matendo 11:26) kwa sababu tabia zao, matendo yao na hotuba zao zilikuwa kama za

Kristo. Ilitumika kiasili na watu wasiookoka wa Antiokia kama jina la kimajazi

kuwadhihaki wakristo hao. Ina maana sawa na “Kuwa mmoja wa kundi la kristo” au

“mfuasi wa kristo,” ambayo imefanana na tafsiri ya Neno hili katika kamusi ya Webster.

Kwa bahati mbaya, neno mkristo limepoteza kwa kiwango kikubwa usawa wa matumizi

yake na Linatumika mara kwa mara kumaanisha tu mtu mwenye dini au pengine muadilifu

kinyume cha Mfuasi halisi wa yesu kristo aliyezaliwa mara ya pili. Watu wengi

wasioamini na kuwa na tumaini ndani ya yesu kristo hujichukulia tu kuwa ni wakristo kwa

sababu wanahudhuria ibada za kanisa ama wanaishi katika taifa la kikristo. Lakini, kuenda

kanisani, kuwahudumia wale wasiobahatika maishani au kuwa mtu mzuri haviwezi

kukufanya kuwa mkristo. Kama muinjilisti mmoja alivyosema, “kuenda kanisani

hakufanyi mtu kuwa mkristo sawa na mtu kuenda gereji hakumfanyi kuwa gari.” Kuwa

8
mshirika wa kanisa anayehudhuria ibada kila mara na kutoa kwa ajili ya kazi za kanisa

hakuwezi kukufanya wewe kuwa mkristo. Biblia inatufundisha ya kwamba matendo yetu

mema tunayoyatenda hayawezi kutufanya tukubalike mbele za Mwenyezi Mungu. Tito 3:5

inatuambia ya kwamba “si kwa matendo ya haki tuliyoyatenda, ila kwa huruma zake

alituokoa kwa kutuosha na kutufanya upya kwa roho Mtakatifu.” Kwa hivyo mkristo nimtu

aliyezaliwa mara ya pili na Mungu (Yohana 3:3; Yohana 3:7; Petero wa kwanza 1:23) na

aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya yesu kristo. Waefeso 2:8 inatuambia ya

kwamba “Kwa neema mmeokolewa kupitia imani wala si kwa ajili yenu wenyewe bali ni

kipawa cha Mungu.” Mkristo wa kweli ni mtu aliyetubu dhambi zake na kuweka imani na

tumaini lake ndani ya Yesu kristo pekee. Imani yao haimo ndani ya kufuata dini ama

kanuni Fulani za uadilifu ama miongozo ya kusema fanya hiki na usifanye kile. Mkristo

wa kweli ni mtu aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya utu wa Yesu kristo na

kukubali ya kwamba alikufa msalabani kwa fidia ya dhambi zetu na akafufuka tena siku ya

tatu kupata ushindi dhidi ya kifo ili awape uzima wa milele wote wamwaminio. Yohana

1:12 inatuambia ya kwamba “wote waliomwamini aliwapa uwezo kuwa wana wa mungu,

kwa wale waliaminio jina lake.” Mkristo wa kweli ni mwana wa Mungu halisi, sehemu ya

jamii halisi ya mungu na aliyepewa maisha mapya ndani ya kristo. Alama ya mkristo wa

kweli ni upendo kwa wengine na utiifu kwa neno la Mungu (Yohana wa kwanza 2:4;

Yohana wa kwanza 2:10).

Imani: Waebrania 11: 1 inatuambia kuwa imani ni "Basi imani ni kuwa na hakika ya

mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana." Labda hakuna sehemu

nyingine ya maisha ya Kikristo ni muhimu zaidi kuliko imani. Hatuwezi kununua, kuuza,

au kuipa marafiki zetu. Kwa hiyo imani ni nini jukumu gani imani inahusika katika maisha

ya Kikristo? Neno hili linafafanua imani kama "Imani katika, kujitolea, au kuamini mtu

fulani au kitu, hasa bila uthibitisho wa kimantiki." Pia inafafanua imani kama "kuamini na
9
kujitolea kwa Mungu." Biblia ina mengi zaidi ya kusema juu ya imani na jinsi ni muhimu.

Kwa kweli, ni muhimu sana kwamba bila imani hatuna nafasi na Mungu, na haiwezekani

kumpendeza (Waebrania 11: 6). Imani ni kumwamini Mungu mmoja, Mungu wa kweli,

hata bila kumwona Yeye. Imani inatoka wapi? Imani sio kitu tunachojishughulisha

wenyewe, wala si kitu ambacho tunazaliwa nacho, wala imani nkuwamatokeo ya bidii

katika kujifunza au kufuata kiroho. Waebrania 2: 8-9 inafanya wazi kwamba imani ni

zawadi kutoka kwa Mungu, sio kwa sababu tunastahili, tumeipata, au tunastahili kuwa

nayo. Sio kutoka kwetu; ni kutoka kwa Mungu. Haipatikani kwa nguvu zetu au mapenzi

yetu ya bure. Tumepewa tu na Mungu, pamoja na neema yake na huruma, kulingana na

mpango Wake takatifu na kusudi, na kwa sababu hiyo, Yeye anapata utukufu wote. Mungu

alifanya njia ya kutofautisha kati ya wale ambao ni wake Yeye na wale ambao sio wake, na

inaitwa imani. Kwa urahisi tu, tunahitaji imani ili kumpendeza Mungu. Mungu anatuambia

kwamba inampendeza Yeye kuwa tunamwamini hata ingawa hatuwezi kumuona. Sehemu

muhimu ya Waebrania 11: 6 inatuambia kwamba "Anawapa thawabu wale wanaomtafuta

kwa bidii." Hii sio kusema kwamba tuna imani kwa Mungu tu kupata kitu kutoka kwake.

Hata hivyo, Mungu anapenda kuwabariki wale wanaomtii na waaminifu. Tunaona mfano

kamili wa hili katika Luka 7:50. Yesu anahusika katika majadiliano na mwanamke

mwenye dhambi wakati anatupa maelezo ni kwa nini imani inastahili sana. "Imani yako

imekuokoa; nenda kwa amani." Mwanamke aliamini kwa Yesu Kristo kwa imani na

akampa thawabu kwa ajili yake. Hatimaye, imani ni chombo kinachotuwezesha hadi

mwisho, kwa kujua kwa imani kwamba tutakuwa pamoja na Mungu milele. " Naye

mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini;

na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa

imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu" (1 Petro 1: 8-9). Mifano ya imani; Waebrania

sura ya 11 inajulikana kama "sura ya imani" kwa sababu ndani yake matendo makuu ya

10
imani yanaelezwa. Kwa imani Abeli alitoa sadaka ya kupendeza kwa Bwana (mstari wa 4);

Kwa imani Nuhu alijenga safina wakati ambapo mvua haijulikani (mstari wa 7); Kwa

imani Ibrahimu alitoka nyumbani kwake na kutii amri ya Mungu ya kwenda penye hajui,

kwa hiari alimtolea mwanawe pekee (8-10, 17); Kwa imani Musa aliwaongoza wana wa

Israeli kutoka Misri (mstari wa 23-29); Kwa imani Rahabu alipokea wapelelezi wa Israeli

na akaokoa maisha yake (mstari wa 31). Wengi wa mashujaa wa imani wanatajwa "ambao

kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa

vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu

baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya

wageni."(mstari wa 33-34). Kwa wazi, kuwepo kwa imani kunaonyeshwa kuwa wa hatua

(kitendo). Imani ni jiwe kuu la Ukristo; Bila kuonyeshe imani na uaminifu kwa Mungu

hatuna mahali pamoja naye. Tunaamini katika kuwepo kwa Mungu kwa imani. Watu

wengi wana wazo lisilo wazi, lisilojumuishwa kuwa Mungu ni nani lakini hawana heshima

inayofaa kwa nafasi yake iliyoinuliwa katika maisha yao. Watu hawa hawana imani ya

kweli inayohitajika kuwa na uhusiano wa milele na Mungu anayewapenda. Imani inaweza

kushindwa wakati mwingine, lakini kwa sababu ni zawadi ya Mungu, iliyotolewa kwa

watoto Wake, hutolewa nyakati za majaribu na mateso ili kuthibitisha kuwa imani yetu ni

halisi na kuimarisha na kutujenga. Ndiyo maana Yakobo anatuambia kuchukulia kuwa

"furaha safi" kwa sababu kujaribiwa kwa imani yetu hutoa uvumilivu na kukua, kutoa

ushahidi kwamba imani yetu ni halisi (Yakobo 1:2-4).

2.3 Mapitio ya Nyaraka

Wengine wanarudi nyuma kwa sababu ya kute nda zambi ya mwili: Citoyen Bumani

alifanya hivi. Alikuwa amekaa pamoja na mke wake kwa miaka 15 na alishiriki ndani ya

kazi ya Mungu kanisani vilevile. Alikuwa tu namna ya Wakristo wote, lakini alifurahia

11
wanawake zaidi. Alipenda kuwaambia maneno matamu na kugusagusa miili yao. Halafu

siku moja ilimpasa kufanya safari kwa ajili ya bwa na wake wa kazi na kule katika mji

mwingine ali anguka. Tangu siku ile anafikia nyumba ya Mungu siku moja moja tu. Hana

furaha tena nyumbani mwake kama mbele. Watu hawajui nini imetokea na kwa sababu

gani roho yake ni baridi naye hakai na furaha pamoja na watu. Anakusudi kuficha za mbi

yake, lakini hana salama rohoni.

Watu wengine wanafanana na mwana mpotevu katika Luka 15: Tuwaze juu ya citoyen

Bulabanga. Alipata nguvu nyumbani mwa Wakristo na aliokolewa mwaka mmoja mbele

ya kuingia kazi ya askari. Alifurahi sana siku alipoondokea nyumba ya wazazi wake na

hakuwa chini ya amri yao tena. Alikusudi kutimiza mapenzi yake yote. Askari wenzake

hawakuweza kujua ya kwamba yeye ni Mkristo. Alishiriki ndani ya zambi zao zote . . .

lakini kule ndani zamiri yake ilimshitaki naye hakuwa na furaha hata kidogo.

Wakristo wengine huacha njia ya Bwana kwa sababu ya kujifunza zaidi: Mfano ni Citoyen

Kularaba aliyekuwa mwenye akili nyingi. Nyuma ya kumaliza chuo ya Biblia alikwenda

kwa chuo cha elimu nyingi. Alitaka sana kuendelea na alijifunza elimu ya asili ya mambo

yote na vitu vyote. Nyuma ya mwezi mmoja tu alipata shaka rohoni juu ya imani yake kwa

sababu ya mafundisho aliyopata pale. Hakuwaka tena kwa Bwana. Aligeuka mtu wa

kasirani na roho yake ilijazwa mashaka na maulizo.

Wakristo wengine wanarudi nyuma kwasababu ya ulevi: Alianza kunywa malofu nusu

nusu tu wakati alipokuwa nyumbani mwa watu wengine, lakini alikunywa zaidi saa

alipokuwa na masumbuko nyumbani au wakati kazi ilipoongezeka kupita kipimo. Sasa

pombe inamtawala kabisa. Anapata haya kubwa kila mara anapowaza juu ya kanisa na

rafiki zake Wakristo. Halafu anakunywa chupa kingine cha pombe kwa kulalisha dhamiri

yake.

12
Wakristo wengine wanarudi nyuma kwa sababu wameoa hasiyeamini: Tubakori alikuwa

msichana wa furaha aliyependa Bwana sana. Alipasha rafiki zake zote habari za Mwokozi

wake. Kijana mmoja alipatana naye kwa kumwoa na nyuma ya majuma machache kijana

huyu alisema kwamba ameamini Kristo vilevile. Leo Tubakori anafikili mume wake

hakuamini kweli kweli. Yeye na mume wake ha washiriki pamoja ndani ya ma neno ya

Mungu na nyumba yao ni nyumba ya ma gomvi tu. Watoto wao hawajui kutii. Mume wake

anamwambia Tubakori ya kwamba hampendi na hapendi watoto wake. Kila mangaribi

nyuma ya kazi anakwenda kukaa pamoja na rafiki zake, akiacha Tubakori peke yake

nyumbani na huzuni na machozi. Tubakori alijaribu kufuata Bwana kwa miaka michache

nyuma ya kuolewa, lakini sasa ameacha.

Wakristo wengine wanarudi nyuma kwa sababu ya kazi yao: Hawafanyi zambi kubwa sana

lakini wanaacha kazi yao kula saa zao zote hata hawana saa tena kwa jamaa yao wala kwa

Mungu. Hawaweki saa kwa kusoma Biblia na kwa maombi na wanakutana pamoja na

Wakristo wengine kuabudu Mungu siku moja moja tu. Masumbuko ya maisha ya sasa

yamepunguza nguvu yao ya roho na kuwaacha zaifu sana kwa maneno ya Mungu. Tamaa

na mapendo ya mali yamewashinda. Wakristo wanarudi nyuma kwa njia mbalimbali

kabisa. Wengine wanapata hasara na halafu roho zao zinageuka baridi. Hawakubali ya

kwamba mambo haya ni mapenzi ya Mungu kwa maisha yao. Hawafahamu ya kwamba

taabu yao itageuka baraka kwao nyuma, hivi wanakasirika na kupoa rohoni. Wengine

wanakataa kusamehe watu wengine ambao waliwaumiza. Wanakaa na roho nguvu, bila

rehema. Basi Mungu Baba hawezi kusamehe watoto wake wanaokataa kusamehe ndugu

zao (Mathayo 6:14-15).

Wakristo wengi wanarudi nyuma kwa sababu ya magomvi madogo madogo nyumbani

mwao. Mume na mke hawakai tena na salama na mapendo pa - mo ja. Inawashinda

13
kusemezana vizuri, na hawa - ombi tena pamoja. Wao wawili wanakataa kukubali ya

kwamba wameanguka. Roho zao ni ngumu ka - ma chuma na hawafahamu ya kwamba

wao wawili walikuwa wamekwenda mbali na Bwana. Kwa nini watu wanarudi nyuma?

Kwa sababu ya zambi. Wanaasi maagizo ya Mungu, wanaacha tamaa ya mwili

kuwatawala, wanapenda mali na vitu vya dunia hii kupita Mungu, wanakataa kusamehe

wenzao, vivi hivi. Unashangaa kusikia ya kwamba waamini wanaweza kwenda mbali na

Mungu hivi?

Tukumbuke kwamba watu wa Mungu wa zamani walirudi nyuma vilevile: Daudi alirudi

nyuma kwa sababu ya tamaa ya mwili. Alizini na kuua mtu (2 Samweli 11:1-27). Mungu

aliokoa Noa toka garika, lakini nyuma yake Noa alishindwa na ulevi (Mwanzo 9:20-21).

Loti alirudi nyuma kwa sababu ya kazi yake. Alitafuta heshima na utajiri katika mji wa So

- domo (Mwanzo 13:7-11; 19:1-28). Watu hawa wote walitubu na kurudi karibu na

Mungu. Walikuwa na upatano mzuri naye tena. Basi kila mwamini wa kweli aliyeacha njia

ya Bwana anaweza kurudi karibu naye vivyo hivyo kama akitubu na kuacha dhambi zake.

14
SURA YA TATU

MBINU ZA UTAFITI

3.1 Utangulizi

Katika sura hii tumefanya uwasilishaji wa mbinu na vifaa vya utafiti ambavyo

vimetusaidia kupata data ambazo zitatuwezesha kukamilisha malengo mahususi ya utafiti

wetu. Mbinu za utafiti ni jumla ya kanuni, taratibu, sheria na miongozo ambazo hufuatwa

hatua kwa hatua katika kukamilisha utafiti uliokusudiwa kufanyika (Babbie, 1999). Hivyo,

katika utafiti huu vipengele ambavyo vimetumika ni usanifu wa utafiti, eneo la utafiti,

sampuli na usampulishaji. Vipengele vingine ni aina za data zilizokusanywa, mbinu za

kukusanyia data na mbinu za kuchambulia data.

3.2 Mtindo wa Utafiti

Mtindo wa utafiti ni kipengele muhimu katika kutoa picha kamili ya namna utafiti

ulivyofanyika tangu mwanzo hadi mwisho. Mtindo wa utafiti ni ramani inayotoa taswira

kamili ya namna utafiti ulivyofanyika tangu katika kukusanya data mpaka kufanya

uchambuzi wa data (Kothari, 2008). Utafiti huu umetumia mbinu ya mbinu ya case study.

Hii ni mbinu ya kuteua eneo moja maalumu ambalo ndilo lililofanyiwa utafiti na kutoa

data ambazo ndizo zimejibu maswali ya utafiti wetu. Hivyo, katika utafiti huu wilaya ya

Kigamboni ndiyo iliyochanguliwa kwaajili ya kufanyiwa utafiti wa kutathmini chanzo cha

Wakristo kurudi nyuma kiimani katika makanisa ya Kipentekoste. Mbinu hii ni nzuri kwa

sababu inamfanya mtafiti kutumia muda mfupi na kuweza kupata data nyingi ambazo

zinajibu maswali ya utafiti kwa uhakika (Yin, 1994).

15
3.3 Eneo la Utafiti

Eneo la utafiti ni mahali ambapo utafiti umefanyika ili kukusanya data za utafiti kwa lengo

la kukamilisha malengo mahususi ya utafiti (Kothari, 2008). Eneo la utafiti katika utafiti

huu ni Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania.. Eneo hili limeteuliwa

kwa sababu ndipo zinapopatikana taarifa zilizokamilisha utafiti huu.

3.4 Sampuli na Usampulishaji

Sampuli ni wawakilishi ambao wanateuliwa kutoka katika kundi kubwa la watafitiwa ili

kutoa data ambazo zitawakilisha kundi zima (Robson, 2007). Sampuli ya utafiti huteuliwa

kwa sababu si jambo rahisi kwa mtafiti kuweza kutafiti watafitiwa wote wanaopatikana

katika sehemu au eneo fulani wote kwa ujumla wake na akaweza kukamilisha malengo ya

utafiti wake. Sampuli ya utafiti huu ni jumla ya watu 20 ambao ni washirika 15, viongozi

wa kanisa 4 na Mchungaji 1. Hata hivyo, sampuli haiwezi kupatikana bila ya kufanyika

kitendo cha usampulishaji. Usampulishaji ni kitendo cha kuteua sampuli ambayo

itawakilisha watafitiwa wote wanaolengwa katika utafiti unaotarajiwa kufanyika

(Cresswell, 2000). Katika utafiti huu tumetumia mbinu ya usampulishaji lengwa katika

kupata sampuli ya watafitiwa. Usampulishaji lengwa ni aina ya usampulishaji ambapo

mtafiti huteua sampuli yake akiwa na imani kwamba sampuli hiyo ndiyo inayoweza

kumpatia data za utafiti. Hivyo, mtafiti alikuwa na imani kuwa idadi ya watu 20 iliweza

kumpatia data alizozihitaji na kuweza kukamilisha malengo mahususi ya utafiti wake. Data

zilizokusanywa katika utafiti huu zilihusu kutathmini chanzo cha Wakristo kurudi nyuma

kiimani katika makanisa ya Kipentekoste.

3.5 Aina ya Data Zilizokusanywa

Utafiti huu umekusanya data za aina mbili ambazo ni data za msingi na upili. Lengo la

kukusanya data za aina mbili ni kufanya malengo ya utafiti yaweze kukamilika.

16
3.5.1 Data za Msingi

Data za msingi ni aina ya data za utafiti zinazokusanywa kwa mara ya kwanza na

hazijawahi kukusanywa na mtafiti mwingine yeyote yule kwa minajili ya utafiti kama huu

uliofanywa na mtafiti huyu wa sasa (Furlong, 1984). Data za msingi kwa jina lingine

hujulikana kama data ghafi yaani data ambazo hazijawahi kufanyiwa kazi. Katika utafiti

huu data za msingi zilikusanywa kwa kutumia mahojiano, dodoso na uchunguzi.

3.5.2 Data za Upili

Data za upili ni aina ya data ambazo tayari zilikwishakukusanywa na watafiti wengine kwa

ajili ya kukamilisha malengo ya utafiti wao (Yin, 1994). Data hizi hukusanywa kwa lengo

la kujazilishia data za msingi ilikuzifanya zisionekane kuwa mpya kabisa. Data za upili

kwa kawaida hukusanywa katika vitabu, makala, tasinifu, magazeti na makala

zinazopatikana katika tovuti na wavuti. Hivyo, data za upili katika utafiti huu zilikusanywa

katika maktaba pamoja na mitandao.

3.6 Mbinu za Kukusanyia Data

Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu za upitiaji wa nyaraka, mahojiano,

dodoso na uchunguzi. Mbinu hizi mbili zimewezesha kupatikana kwa data za utafiti kama

zilivyochambuliwa na kuwasilishwa katika sura ya nne ya utafiti huu.

3.6.1 Upitiaji wa Nyaraka

Upitiaji wa nyaraka ni mbinu ya kukusanya data za upili ambazo kama ilivyosemwa hapo

awali hizi ni data za kujazilishia data za msingi. Upitiaji wa nyaraka ni mbinu ya

kukusanya data kwa mtafiti kutafuta machapisho ambayo yanahusiana na mada ya utafiti

wake na kisha kuyasoma machapisho hayo ili kupata data ambazo alizitumia kushadadia

hoja zinazojitokeza kutoka katika data za msingi (Babbie, 1999). Mbinu hii ni nzuri kwa

17
sababu iliwezesha kupatikana kwa data ambazo ziliusaidia utafiti wetu kutokupwaya kwa

sababu ulipewa misingi imara na data za hizo za upili. Nyaraka zilizopitiwa kupitia mbinu

hii ni tasinifu, vitabu, makala, majarida, magazeti, vipeperushi na makala pepe katika

wavuti na tovuti.

3.6.2 Dodoso

Utafiti ulitumia mfumo wa maswali binafsi ambao ulitumiwa kwa wakristo. Maswali yana

faida katika suala la uchumi, ukosefu wa upendeleo wa mhojaji na uwezekano wa

kutotajwa (Kidler, 1981). Maswali yalikuwa yaliyofichwa na yaliyowazi ili kuongeza

uhalali wa majibu. Kutoka katika njia hii, mtafiti alipata majibu ya maswali aliyoyaandaa.

3.6.3 Mahojiano

Utafiti ulitumia mahojiano ili kupata taarifa kutoka kwa viongozi wa kanisa na mchungaji.

Hii inajumuisha mahojiano ya kina ya ana kwa ana. Maswali kiongozi yamelenga katika

malengo ya utafiti yaliyoandaliwa hapo kabla. Ratiba ya mahojiano iliwekwa kwa

kukubaliana na anayehojiwa ili kumuwezesha kujiandaa kufanyiwa mahojiano na mtafiti.

3.7 Vifaa vya Utafiti

Vifaa vya utafiti ni jumla ya vitu na zana zote ambazo zimetumika katika zoezi zima la

ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti tangu unaanza mpaka mwisho wa utafiti huo.

Data za utafiti huu zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia vifaa mbalimbali kama

ifuatavyo:

Kalamu na Karatasi; kalamu na karatasi ni vifaa muhimu sana katika kusaidia kukamilika

kwa utafiti wa aina yoyote ule uwao. Katika utafiti huu vifaa hivi vilitumika katika

kuchukua madondoo kutoka katika mahojiano na kuyaweka madondoo hayo katika daftari

ambalo ndilo ndani mwake mna makaratasi ya kuandikia. Data hizo zilizokusanywa

18
zilihifadhiwa vizuri katika daftari hilo mpaka wakati wa kuandika andiko la utafiti

ulipofika.

Kompyuta; kifaa hiki kimetumika katika kukusanya na kuchambua data za utafiti kwa

namna mbili. Kwanza kilitumika katika kukusanya data za upili kwa kusoma makala pepe

zinazopatikana katika wavuti na tovuti. Pili, kifaa hiki kilitumika katika kuchapa kazi hii

na kuifanya kuonekana hivi ilivyo hivi sasa.

Simu ya Mkononi; kifaa hiki kilitumika katika kuweka miadi ya kukutana na msimamizi

wangu wa utafiti kwa ajili ya kupatiwa maelekezo ya namna ya kuboresha kazi yangu. Pili,

simu hiyo hiyo ilitumika katika kupewa maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa

msimamizi juu ya namna bora ya kuifanya kazi yangu iwe nzuri na ikamilike kwa wakati.

Wakati mwingine msimamizi alinipigia simu kuniuliza mbona sipeleki kazi yangu kwake

na muda alionipatia wa kufanya marekebisho ukiwa umekwisha. Pia kifaa hiki kilisaidia

kuwasiliana na wahojiwa kupanga eneo la kufanyia mahojiano na kilitumika kurekodia

mahojiano ili kumrahisishia mtafiti katika uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa. Hivyo,

kwa namna moja au nyingine kifaa hiki kilitoa msaada mkubwa wa kuweza kukamilisha

data za utafiti huu.

3.8 Uchambuzi wa Data

Uchambuzi wa data ni kitendo cha kupanga, kuchagua, kulinganisha na kutolea maelezo

data zilizokusanywa ili ziweze kujibu maswali ya utafiti uliokusudiwa. Uchambuzi wa data

ni zoezi lililo na umuhimu mkubwa katika utafiti kwani bila ya uchambuzi wa data ripoti

au tasinifu ya utafiti haiwezi kuandikwa na kutoa matokeo yaliyotarajiwa (Young, 1984).

Kimsingi, zipo mbinu na mikabala mbalimbali ya uchambuzi wa data lakini katika utafiti

huu tulitumia mkabala wa kimaelezo. Huu ni mkabala ambao hutumika kuchambua data za

utafiti kwa kuzitolea maelezo ya kina kwa mwelekeo ambao unasaidia kutimiza lengo kuu
19
la utafiti. Data za utafiti huu ziliwasilishwa kwa njia ya madondoo na kisha kuchambuliwa

kwa madondoo hayo kwa kutolewa maelezo ya kina yaliyoweza kujibu maswali ya utafiti

wetu kwa namna iliyokusudiwa.

3.9 Uzingatiaji wa maadili

Katika mwanzo wa kukusanya taarifa, mtafiti alipata ruhusa/kibali kwa msimamizi wa

chuo ambacho kilimsaidia kuendelea na utafiti hasa katika zoezi la ukusanyaji wa taarifau.

Kwa nyongeza, kila swali lilijumuisha barua ya utambulisha ambayo ilihitaji ushirikiano

kwa wahusika wanaotakiwa kujibu maswali. Waliojibu walihakikishiwa ya kwamba

majibu yao yatakuwa ya siri yatatumika kwaajiri ya utafiti tu na si vinginevyo. Waliojibu

walihakikishiwa ulinzi binafsi na wanamamlaka ya kukataa au kukubali kufanyiwa

mahojiano.

20
SURA YA NNE

UWASILISHAJI, UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA UTAFITI

4.1 Utangulizi

Sura hii inahusu uwasilishaji, uchambuzi na mjadala wa data za utafiti ili kufanikisha lengo

la utafiti huu. Uwasilishaji na uchambuzi wa data za utafiti umefanywa kwa kuzingatia

malengo mahususi ya utafiti.

4.2 Matokeo ya Utafiti

Dhana ya kurudi nyuma: Maneno kurudi nyuma, katika mazingira ya Kikristo, yana maana

ya kuondoka mbali na Kristo badala ya kuenda kwake. Aliyerudi nyuma ni mtu ambaye

anaenda njia mbaya, kiroho. Anadidimia badala ya kuendelea. Aliyerudi nyuma alikuwa

kwa wakati mmoja ameonyesha kujitoa kwa Kristo au aliweka kiwango fulani cha tabia,

lakini hajawahi rejea kwa njia za zamani. Kurudi nyuma kunaweza kujionyesha kwa njia

kadhaa, k.m., kuacha kanisa, kupoteza juhudi katika Bwana, kutembea mbali na huduma

au familia, au kurudi katika tabia za kale.

Watu wengine hutumia maneno kurudi nyuma kumaanisha kuwa mtu amepoteza wokovu

wake. Hata hivyo, mtu aliyeokoka ako salama katika Kristo (Yohana 10: 28-29). Mungu

hatatupa watoto wake nje ya familia yake hatutatumia maneno hayo hivyo. Badala yake,

tunapozungumza juu ya kurudi nyuma, tunamaanisha kwamba mtu anazidi kuwa baridi

katika Kristo. Hali ya kurudi nyuma iliyorejeshwa inaweza kuonyesha kwamba mtu

hakuwahi kamwe kuokolewa ili aanze-katika hali hiyo, aliyerudi nyuma anaonyesha tu

rangi zake za kweli. Lakini pia inawezekana kwa watoto wa Mungu kurudi nyuma, kwa

muda.

21
Bibilia inatumia maneno kuanguka mbali badala ya kurudi nyuma, lakini wazo ni sawa.

Katika Bibilia "kuanguka" inaweza kumaanisha mambo mawili tofauti. Katika mfano

mmoja, mtu huyo anaokolewa lakini anapata muda wa kujiuliza maswali ambayo tunaweza

kuiita "mgogoro wa imani." Kwa upande mwingine, mtu huyo hakuwahi kamwe

kuokolewa lakini anajifanya tu kama mtu aliyeokolewa. Tutaita hii kuchukua Ukristo kama

"gari la mtihani."

Katika Marko 14:27 Yesu anawaambia wanafunzi wake, "Ninyi nyote mtaanguka."

Alichomaanisha ni kwamba, wakati alipokamatwa, watapata shida ya imani, tukio la

maisha la kushangaza ya kwamba watakimbia kutoka kwa Yesu na kuuliza msingi wa

imani zao. Ilikuwa usiku wa kosa, usiku wa kuwakumbusha kwao. Lakini hii ilikuwa hali

ya muda. Siku tatu baadaye, Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na akaonekana kwa

wanafunzi. Imani na matumaini yao yalirejeshwa, imara zaidi kuliko hapo awali.

Mtume Paulo anatuambia jinsi ya kushughulika na mwamini mwezetu ambaye anarudi

nyuma: "Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni

upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe

mwenyewe"(Wagalatia 6: 1). Yakobo anakubaliana: "Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu

amepotelea mbali na kweli. . . mtu anapaswa kumleta mtu huyo "(Yakobo 5:19). Aliyerudi

nyuma ametembea kutoka mahali ambapo anapaswa kuwa na ana "kushikamana" katika

dhambi, lakini kanisa litafanya kazi kumrejesha na kumrudisha katika njia ya haki.

Kuna matukio katika maisha, kama kifo cha mpendwa, ambacho kinaweza kutufanya

tuulize Mungu. Hii ni sawa, ili mradi tuende kwa Mungu na maswali hayo badala ya

kuyatumia kama sababu za kuishi katika uasi. Matokeo ya mgogoro wa imani ni mara

nyingi kwamba tunamjua Mungu zaidi kwa karibu kuliko hapo awali. Wakati wa

22
majaribio, tunapaswa kuingia ndani ya Neno, kuomba kwa uvumilivu (Luka 18: 1), na

kuzungukwa na wale ambao imani yao ni imara.

Tunaona aina nyingine ya "kuanguka" katika Waebrania 6: 4-6 na Luka 8:13. Waebrania 6

inaelezea mpotofu, mtu ambaye "aliwahi onja tu uzuri wa neno" (mstari wa 5) na baadaye

analikataa. Katika Luka 8:13 Yesu anafananisha upotofu na udongo wenye mwamba-

baadhi ya watu huanguka au kurudi nyuma kwa sababu "hawana mizizi." Katika kila fungu

hili, mtu huonekana kwa nje kuwa Mkristo, angalau kwa muda, lakini hajajitolea kwa

Mungu. Mtu kama huyo anaweza kuhudhuria kanisa, kusoma Bibilia yake, kusikiliza

muziki wa Kikristo, na kutembea na marafiki wakristo. Anapenda mazingira hayo yote

mazuri na urafiki mzuri ambao kuwa karibu na Wakristo hutoa. Lakini moyo wake

haujabadilika; yeye hajawahi kuzaliwa tena. Hatimaye, anarudi nyuma au kuanguka.

Alikuwa amechukua Ukristo kama gari la mtihani na akaamua kuwa hakuwa anunue.

Wokovu huja kwa njia ya kukiri halisi wa Yesu kama Bwana kwa moyo unaoamini katika

kifo cha Yesu na ufufuo (Warumi 10:9-10). Ikiwa mtu aliyeokolewa ya kweli hurudi

nyuma-yaani, anarudi tena katika mitazamo na tabia za kiroho za uharibifu-kurudi iyo

nyuma itakuwa ya muda mfupi. Adhabu ya Bwana itamrudisha (angalia Waebrania 12:4-

13). Mchungaji Mzuri atamtafuta mwana-kondoo aliyepotea (Luka 15:3-7).

Ikiwa mtu ambaye hakuwahi okolewa lakini anaweka tu kurudi nyuma ya uzuri-yaani,

anaacha matone na kuonyesha rangi yake ya kweli-hali yake ya mwisho itakuwa mbaya

kuliko ya kwanza (Waebrania 10:26-31). Tunawezaje kuwaambia aina moja ya kurudi

nyuma kutoka kwa nyingine? Hatuwezi daima, isipokuwa tu kupewa wakati, na hata hivyo

hatujui muda gani Mungu atachukua katika kurejesha aliyerudi nyuma. Mungu pekee

ndiye anayeweza kuona moyo.

23
Sababu zinazosababisha wakristo kuhamahama makanisa: Wachungaji wengi wanapoona

watu wanahama makanisani kwao hukimbilia kusoma 1 Yohana 2:19 inayosema

“Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu,

wangelikaa pamoja nasi.” Huu mstari hauzungumzii watu ambao wanaondoka kanisa moja

kwenda kanisa lingine! Unazungumzia watu ambao kwa nje wanaonekana wamepokea

neema ya wokovu lakini kwa ndani hajapoke! Kwa hiyo tusihukumu kupitia msitari huo.

Hata hivyo ukiachilia mbali kwamba siku hizi watu wamekuwa na masikio ya utafiti, yaani

hawawezi kutulia sehemu moja, ni wazi kwamba kuna sababu zinazosababisha hayo yote

yatokee! Kwa ujumla utafiti umebaini sababu zifuatazo;

Inawezekana kutokana na watu kukosa majibu ya ahadi walizoahidiwa kabla ya kuokoka

Tangu zamani ni watu wachache sana wanaoenda kanisani pasipo kupitia changamoto

nyingi katika maisha yao. Watu wengi wanaposikiliza mikutano ya injili na jinsi watumishi

wa Mungu wanavyowaahidi kwamba ukimpokea Yesu kristo mambo yako yatakuwa safi.

Sasa mara wanapokaa kanisani kwa muda wa mwaka mmoja wanaona hali zao zinazidi

kuwa mbaya, basi huamua kuondoka.

Mtumishi wa Mungu unapoona watu wanaanza kuondoka kanisani na kuelekea kanisa

lingine, haijalishi wewe uko katika kiwango gani, hao bado hawajapata majibu ya maswali

yao au zile ahadi walizoahidiwa siku ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi

wa maisha yao. Hili nalo wewe kama mtumishi wa Mungu liweke kwenye kumbukumbu

kwamba lazima ugundue hitaji la mioyo yao na ahadi walizoahidiwa mara ya kwanza ni

zipi.

Watu kujisikia kubadilisha mazingira ya kuabudu: Kuna watu wengine ambao hawapendi

kuzoeleka mahala fulani. Wakionekana kwamba wameanza kuzoeleka huhama mapema

sana. Watu kama hawa nimewaita mimi “wageni ziku zote” kwa maana ya kwamba

24
wanapenda sana kubakia kuwa wageni popote pale wanapokuwa. Ukiangalia kwa undani

zaidi kinachowasumbua watu wa namna hiii ni kwamba wanapenda sana kupokea misaada

kutoka kwa watumishi wa Mungu au kwa waumini wa sehemu husika. Wanatumia

mwavuli wa upya wao kujipatia vipato. Kama ambavyo Paulo alimwambia Timotheo kuwa

“wanadhani utauwa ni njia ya kupata faida”

Udhaifu wa mahali mtu alipokuwa anaabudu unaweza kuchangia mtu kuhamia sehemu

nyingine: Udhaifu ndani ya ibada husababisha watu wengi sana kuhama makanisa na

kuelekea sehemu nyingine ambako roho zao zinaweza kuridhika kumwabudu Mungu. Hata

hivo hoja hii tunaweza kuiweka kwamba; kwa kutegemea na hitaji la mwabudu anaweza

kuhama kanisa kwa sababu anadhani zile ibada za mahali hapo haziendani pamoja naye.

Watu ndani ya makanisa kwa kawaida wako tofauti tofauti. Kuna wengine wanapenda sifa

ya muda mrefu, na kuna wengine wanapenda sifa ya muda mfupi tu. Kuna mwingine

anataka kuomba kwa muda mrefu, na mwingie anataka kwa muda mfupi tu. Kuna

mwingine anataka kuomba kwa sauti kuu na kulia huku kuna mwingine anaona hiyo ni

kero kwake, anaumiza kichwa kwa nini mwenzake anafanya hivyo. Kwa sababu hiyo

ndiyo maana unakuta mtu badala ya kuendelea kugugumia hapo hapo anaamua kuchomoka

peke yake na kuelekea sehemu nyingine.

Siku hizi kuna ibada za kitume na kinabii, haijulikani imeanzia wapi na imeishia wapi, sasa

kama mtu akihamia kwako na wewe huna wito (kama inavyodaiwa) wa kitume-basi ujue

mtu huyo hawezi kutulia. Vivyo hivyo hata wewe unapokuwa unaenda kwenye kanisa la

kitume (kama inavyodaiwa), huwezi kwenda kuingia viutaratibu vyako hapo. Kaa tulina!

Mwabudu Mungu kwa uzuri wake. Taratibu za ibada zote zimeandaliwa kwa lengo la

kuwaongoza watu wamwabudu Mungu katika hali ya uzuri na utakatifu, sidhani kama

25
kuna kanisa ambalo huandaa utaratibu unaoenda kinyume na matakwa ya waabuduo.

Kama ikitokea hivyo, basi hilo siyo kanisa la kweli.

Nia Ya Kutafuta Uongozi Ndani ya Makanisa: Kama tujuavyo kwamba kanisa linakuwa na

uongozi, na ule uongozi ni watu ndio wanaowachagua. kama mtu alienda kwenye kanisa

fulani kwa nia ya kupata uongozi, anapokuwa hajapewa uongozi alioutaka, ni dhahiri

kwamba atahama tu. Tangu zamani hata tunaposoma historia tunaona kwamba watu

mbalimbali walipokosa uongozi mahali fulani waliamua kuhamia makanisa mengine.

Kwamba, nia ya watu wa namna hii ni kuongoza na wala siyo kuongozwa, kwa kifupi wao

hawana karama ya kuongozwa (kama ipo) na wala hawajawahi kuota ndoto ya kuongozwa

hata siku moja. Wao wakikaa katika kanisa kazi yao kubwa ni kukosoa uongozi uliopo

madarakani na kutaka wao ndio wachaguliwe kuwa viongozi.

Ushawishi kutoka kwenye makanisa mengine na kuahidiwa mambo makubwa: Kuna

wakati mwingine inatokeaa kwamba makanisa mengine labda yanatumia vyombo vya

mziki, ilhali katika kanisa lako bado unategemea mikono tu au wenzio wanatangaza

kwenye runinga, wewe hujui hata hiyo runinga ikoje. Sasa mtu anapokutana na watu wa

kundi fulani huanza kuelezea mafanikio ya kanisa lao, naye hushawishika kabisa na

kujiona kwamba ile sehemu anayosali siyo salama kabisa. Kuna wengine hutumia

umaarufu wa wachungaji wao kuwashawishi watu kuhama makanisa. Unakuta mtu

anamweleza kwamba “unajua mchungaji wetu yuko hivi na hivi” sasa mtu huyu

anapolinganisha anamwona mchungaji wake hana hizo sifa, basi huamua kuhama kabisa.

Kukosa ushirikiano katika kanisa jipya ambalo amehamia: Watu huondoka kanisa wakati

wanapokosa ushirikiano ndani ya kanisa husika. Hii ni moja ya sababu ambayo inaweza

kutumika kama sababu ya watu kuja kanisani lakini pia wakati huo huo ikawa sababu ya

watu kuondoka.

26
Mafundisho fulani fulani: Mojawapo ya sababu ya kuwepo kwa madhehebu mengi ni

tofauti za kimafundisho ndani ya kanisa. Kwa hiyo siku hizi ni vigumu sana

kuwaunganisha watu wakawa kitu kimoja kwa sababu kuna tofauti katika mafundisho,

ingawa wakati mwingine tofauti hizo zinaweza kutatuliwa na kutatua changamoto kadhaa

lakini hili limekuwa tatizo kubwa.

Kushindwa kuelewana na watumishi wa Mungu wa mahali fulani: Kuna watumishi

wangine ambao kwa asili ni watata tu, yaani wao hawaelewani na watumishi jirani na

makanisa yao. Watu wanapokuja kusali kwako wakati mwingine siyo kwamba kule

walikuwa wamehama, lakini kwa sababu wewe huna mahubiri zaidi ya kuwasema

watumishi wengine tu, hii inakujengea chuki wewe na waumini wa kanisa hilo.

Waumini wanapoona kwamba ninyi wenyewe hamuelewani, wao huchukua huo mwanya

kupenya na kwenda kwenye makanisa mengine. Hivi mchungaji unajua kwamba hiyo kazi

unayofanya ni kazi kubwa sana mbele za Mungu ambayo kwayo unapaswa kusimama

vizuri pasipo kutikisika?

Kutokujua nini maana ya kuokoka: Ama kwa kushindwa kufundishwa vizuri, ama kwa

sababu ya uzembe wao wenyewe, kuna wakristo ambao mpaka leo hawajui maana ya

wokovu nini katika maisha yao. Wanadhani kwamba wanapokuwa wameokoka shida na

matatizo mbalimbali ya dunia hii yanakoma.

Kushindwa Kutimiza Vigezo vya Kanisa Husika: Siku hizi watu wanapenda sana kujua

mkazo wa kanisa husika. Ni jambo la muhimu sana kwa sababu bila kujua mafundisho ya

msingi ya kanisa husika watu watu huingia katika matatizo makubwa. Lakini huja yangu

hapa ni kwamba kuna waumini mbalimbali ambao huhamia makanisa fulani tu kwa sababu

yanafundisha mambo ambayo wao wanayapenda.

27
Wachungaji kushindwa kuona upande wa waumini wao: Kumekuwepo na kasumba ya

wachungaji kusubiri waumini waje kanisani bila kujua kile ambacho kwa wiki nzima

wamekuwa wakifanya. Wachungaji wanapaswa kukumbuka kwamba kwa muda wa wiki

nzima waumini wanakuwa wanahangaika kujitafutia maisha, hivyo basi ni lazima

mchungaji ajue upande wa waumini wao. Kumekuwepo na kasumba ya wachungaji wa

aina mbalimbali kuhodhi muda wa waumini wao kwa kigezo cha kwamba wanamtumikia

Mungu. Unaweza kushangaa watu wanakuja kanisani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi

mpaka saa kumi na mbili jioni. Halafu kesho yake tena alfajiri kuna ibada ya maombi kila

siku, halafu pia mtu huyohuyo anapaswa kwenda kufanya kazini kila siku. Sasa watu

wengine wanaona isiwe sababu ya kushindwa kuelewana na wachungaji wao, wanaamua

kuhamia makanisa mengine. Kuwepo na ratiba za ibada kila siku ni vizuri sana lakini

mchungaji anapaswa kujua kwamba si waumini wote wanaweza kuja, na pindi

wanapokuwa wameshindwa kuja wasionekane kwamba wao siyo watii.

Ubinafsi wa Waumini: Mojawapo ya tatizo kubwa ambalo linakabili kanisa kwa leo ni

ubinafsi wa waumini kanisani. Watu wengi hushindwa kukaa katika kanisa moja na

kuendelea kuzunguka makanisani kwa sababu mioyo yao imejaa ubinafsi na hawataki

kushirikiana na waumini wengine. Watu wanapaswa kutambua kwamba katika maisha ya

Kikristo ni maisha ya ushirikiano na uhusiano. Mtu anapokuwa amekaa katika kanisa moja

anakuwa amejenga uhusiano wa waumini wengine pia.

Changamoto ya Matoleo: Katika makanisa ya leo kipaumbele cha kwanza kimekuwa ni

matokeo. Kwa sababu hiyo watu wengine wamekuwa wakihama makanisa kwa sababu ya

matoleo mengi kanisani. Unaweza kushangaa kanisani, ibada ya Jumapili inakuwa na

matoleo zaidi ya saba, na kila matoleo hayo unapaswa kutoa; kwa mfano unapaswa kutoa

matoleo ya sadaka ya kawaida, ujenzi, zaka, shukrani, kumtunza mchungaji, kusindikiza

28
kwaya, ununuzi wa vyombo, pamoja na michango mingine midogomidogo. Nakumbuka

kanisa langu la zamani, viongozi wa ibada walikuwa wanatumia muda wa zaidi ya masaa

mawili wakiomba michango ndani ya ibada. Tena wengine mpaka wanafanya na minada

kanisani kwa ajili ya kuuza vitu. Hivyo basi, kuna wakati mwingine watu wanahama

makanisa kwa sababu ya kuogopa kwamba watatoa nini kwenye ibada. Wanaogopa

kuaibishwa na wachungaji wasaka tonge. Wanaogopa kudhalilika mbele ya waumini

matajiri ambao wana pesa za kutosha.

Unadhifu ndani ya kanisa: Kuna watu wengine ambao huhama makanisa kwa sababu ya

unadhifu ulio ndani ya kanisa hilo. Hapa ninaamisha kwamba kuna wakati mtu anaingia

kanisani anakuta watu wote wamevaa nguo za maana (suti na nguo za gharama kubwa).

Halafu wakati huo yeye akijiangalia amevaa mitumba ambayo gharama yake haizidi elfu

tano. Moja kwa moja mtu wa namna hii anakata tamaa ya kuingia ndani ya kanisa hilo na

kuendelea kusali hapo. Mara kwa mara huduma yangu imekuwa ikishutumiwa kwa kuwa

na watu wanaovaa nguo za gharama kubwa na kusababisha watu wengine kuogopa kuingia

ndani ya kanisa. Kuna siku niliwahi kuwaambia kwamba ni lazima waangalie mavazi yao

ili yasiwazuie wengine kuingia ndani ya kanisa kwa hofu ya kusemwa vibaya.

Majungu ndani ya Kanisa: Watu wengi sana wamekuwa wakihama makanisa kwa sababu

na majungu ndani ya kanisa wanalosali. Ingawa kwa kweli sababu hii inawalenga hasa

Wakristo wachanga ambao bado hawana mizizi ya neno, lakini ni muhimu kuijua.

Majungu huharibu mioyo ya watu wachanga na hatimaye huamua kuhama. Majungu

maana yake ni kumsengenya ni kusemana kwa kusengenyana. Yaani mtu anamsema

mwenzake sehemu nyingine bila kibali chake. Jambo analosemwa huyo mtu si lazima liwe

na uongo, hata kama ni la ukweli lakini kwa sababu hakuna kibali kutoka kwake kwamba

mlizungumzie jambo hilo, basi mnapokuwa mnalizungumzia mnakuwa mnapiga majungu.

29
Madhara ya majungu ni kuagamiza ushirika kati ya muumini mmoja na mwingine na

mwishowe watu kuamua kutengana. Nadhani kitu kinachoweza kuharibu mwili wa Kristo

kuliko vitu vingine vyote ni uvumi wa majungu. Majungu husabababisha watu waanze

kulaumiana ndani ya kanisa na kushindwa kutekeleza majukumu ya kikanisa. Majungu

huleta uchonganishi ndani ya kanisa na kuwafanya watu waishi kwa hofu. Biblia inasema

kuwa "Mtu asiye na uaminifu hueneza mgongano, na mchongezi hutenganisha marafiki wa

karibu" (Mithali 16:28). Kama kanisa, tunahitaji kuwa makini sana na maneno kutoka

upande fulani fulani. Tusiwe wepesi wa kuyashabikia maneno hayo. Hata hivyo kumbuka

kwamba majadiliano na mazungumzo husema mengi juu ya tabia ya mtu. "Kinywa

huzungumza" (Mathayo 12:34). Maovu na majadiliano maovu ya watu wasiomcha Mungu

hufunua hali ya mioyo yao. Maneno yaliyosemwa yana nguvu sama. Maisha na kifo

vinaweza kuamuliwa kwa maneno yetu. Maneno pia yanaelezwa kama silaha na mishale

(Zaburi 57:4, 64:3, Yer 9:8). Yakobo anaelezea uwezo wa ulimi kama mwendo wa meli au

cheche ambacho huweza kuwasha msitu kwa moto (Yakobo 3:2-12).

Dhambi za Watumishi: Ama kwa hakika hakuna mtu asiyetenda dhambi hapa duniani!

Kila mtu anaamini hilo kwa sababu ya anguko la mwanadamu pale Edeni. Dhana hii ya

dhambi haipo miongoni mwa waumini kwamba mchungaji au mama mchungaji anaweza

kutenda dhambi. Ikitokea kwamba mmojawapo kati ya watu hawa amefanya dhambi, basi

watu huwa wanakata tamaa kabisa na kuamua kuhamia kwenye makanisa mengine

ambako wanaamini kwamba watumishi wa Mungu wa mahali hapo hawawezi kutenda

dhambi. Ni kweli mchungaji ni mwanadamu kama walivyo wengine, lakini linapokuja

suala la dhambi basi, lazima tujiangalie mara mbili mbili. Ninaamini kwamba dhambi zote

ni sawasawa mbele za Mungu lakini naamini kwamba kuna dhambi moja ambayo

mchungaji akiifanya kwa namna yoyote ile watu hawawezi kumsamehe na kumruhusu

kuendelea kuwa mchungaji wao! Dhambi hiyo ni “uzinzi.” Mchungaji ukifanya uzinzi
30
kanisani na watu wakajua, hata kama ukiwaeleza na kuomba msamaha hawawezi kukubali

kubaki na wewe. Kwa hiyo ni lazima kuwa makini sana. Mchungaji Lee Jae Chul

alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi kwa watumishi wa Mungu alisema alisema hafikirii

kama kuna mtumishi wa Mungu anaweza kufanya hivyo. Yule aliyemuuliza swali alimpa

mfano wa mfalme Daudi aliyezidi na Bathsheba, yeye alijibu kwamba “Daudi alikuwa

hafai kuwa mchungaji ila alikuwa anafaa kuwa mfalme tu”

Mchungaji kushindwa kujitathimini mwenyewe: Watumishi wa Mungu mara kwa mara

huwa tunashindwa kujitathimini utumishi wetu. Kuna wakati mwingine tunatumika kwa

mazoea mazoea tu. Unakuta mchungaji maisha yake hayana tofauti na watu wa kawaida.

Ninamkumbuka mhubiri mmoja aliwahi kusema “mchungaji siyo mtu.” Katika ufafanuzi

wake walisema kuwa mchungaji lazima ajitofautishe na watu wa kawaida. Kanisa haliwezi

kukua zaidi ya mchungaji alivyo. Kama mchungaji ni dhaifu kanisa lazima litakuwa

dhaifu. Watu wengi hawapendi kuona mchungaji wao akiwa dhaifu. Udhaifu tunaousema

hapa hauna maana ya kwamba mchungaji hawezi kufanya dhambi.

Jinsi ya kudumu katika Imani bila kuhamahama: Yesu anasema nasi, “kaeni ndani yangu

nami ndani yenu” ambapo tunaona mawili, Yesu kukaa ndani yetu na sisi kukaa ndani ya

Yesu. Katika sehemu iliyopita tumeona Yesu kukaa ndani yako, kwamba ni kumpokea

Yesu ndani ya moyo wako; yaani “kuokoka”. Leo tunaona Yesu kukaa ndani yako; yaani

“maisha ya wokovu”.

Yesu anasema, mkikaa ndani yangu “mtazishika amri zangu”. Kuzishika amri za Yesu

ndiyo kuishi katika wokovu. Kwa hiyo ukiweza kuishi kwa kuzishika mari za Yesu

unakuwa umeishi maisha ya wokovu tunayoyazungumzia. Tumeona kwamba unapookoka,

Yesu anakuwa ameingia ndani yako na sasa tunakwenda kujifunza maisha katika wokovu

ambayo kwa lugha nyingine tunaita kukaa ndani ya Yesu. Maisha ya wokovu ni maisha ya

31
hapa duniani tangu mwanadamu anapookoka hadi atakapokufa (hatima ya maisha ya

duniani). Baada ya maisha ya wokovu ni maisha ya milele ambapo tutaishi pamoja na

Baba katika ufalme wake Mbinguni. “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia

sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye

pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi,

kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha

enzi” (Ufunuo 3:20-21).

Bwana Yesu ni wa kwanza, anabisha hodi, ukifungua mlango (ukimruhusu aingie) yaani

ukimwamini na kumkiri… anaingia ndani yako na kufanya makao. Atakula pamoja nawe,

nawe pamoja Naye (kila utakachokuwa unafanya, atakuwa pamoja nawe), katika mawazo

yako yupo nawe, katika matendo yako yupo nawe, na kila sehemu utakapokuwepo Yeye

yupo nawe. Akiisha ingia kwako inakupasa nawe ukae ndani yake, yaani uyaishi maisha ya

wokovu kikamilifu kwa uangalifu mkubwa. “Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa

Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa,

ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu

uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa

kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao.

Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.” 1

Yohana. 3:8-10

Yesu akikaa ndani yako nawe unapokaa ndani ya Yesu, unakuwa umeruhusu utatu wote

mtakatifu kukaa nawe. Kwasababu hiyo, unakuwa na utukufu wa mbinguni, na mtembeo

utakao tembea ni mtembeo wa kimbingu, maana akikaa ndani yako anayeishi sasa siyo

wewe bali yeye aliye ndani yako na laiye ndani yako ni ufalme wote wa Mbinguni. Biblia

inasema katika Wagalatia 2:20 kwamba; “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai;

32
wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilionao sasa katika mwili ninao

tena katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwaajili

yangu.”

Na kwasababu umefanyika mwana wa Mungu aliye hai, unakuwa na tabia maalum ya

Mungu. Mungu wetu ni mtakatifu, kwa hiyo watoto wake waliozaliwa naye wanapaswa

kuwa watakatifu. “…Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao

wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na

Mungu…”

Maisha ya wokovu ni kupambana ili kudumu katika utakatifu. Utakatifu ni kutokutenda

dhambi. Na kwasababu umeshatolewa kwenye ule utu wa kale, yaani kuishi kimwili na

ukawa mfu kimwili na kuanza kuishi kiroho, vivyo hivyo unapaswa uenende kwa namna

ya rohoni. Paulo katika waraka wake wa pili kwa Timotheo anasema “nimevipiga vita

vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda” 2Timotheo 4:7. Unaona hapa

sasa, maisha ya wokovu ni maisha ya vita. Vita ni mapambano. Siyo maisha ya starehe na

raha, bali ni maisha ya kusimama imara. Shetani kila kukicha anapambana kuiteka Imani

yetu, sisi tunapaswa kuilinda hii Imani. Haya maisha ya wokovu ni maisha ya utakatifu.

Mtu anapookoka anakuwa mtakatifu (bila dhambi) na hivyo baada ya kuokoka mtu

anapaswa kupambana kuishi katika utakatifu, na haya ndiyo maisha katika wokovu. “Basi

kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina

na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa;

mkizidi kutoa shukrani. Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na

madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya

awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Kolosai 2:6-8).

Mbinu kuu nne za kudumu katika wokovu:

33
Neno la Mungu: Ili kuishi maisha ya wokovu kwa ushindi unapaswa kusoma, kulishika na

kulifuata neno la Mungu. Biblia inasema “ni kwa jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa

kuitii na kulifuata neno” Zaburi.119:9, 2Timotheo.3:16-17 Biblia inasema “kila andiko

lenye pumzi ya Mungu linafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na

kwa kuwaongoza na kuwaadibisha katika haki… ili mtu wa Mungu awe kamili, aweze

kukamilishwa apate kutenda kila tendo lililo jema.”

Tumepata kusema kwamba maisha ya wokovu ni mapambano, maisha ya wokovu ni vita.

Silaha yetu kubwa katika hiyo vita ni neno la Mungu. Biblia inasem ahivi “Neno la mungu

li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” (Waebrania 4:12). Yoshua mwana

wa Nuni alipokabidhiwa kundi la wana wa Israel alifikishe nchi ya ahadi, alipewa maagizo

na Mungu. Aliambiwa, “kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari

maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno

yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapofanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi

sana”. Baada ya kufuata masharti hayo, Yoshua alikuja kuwa na mafanikio sana na ushindi

mno. Tumesoma kuwa alivuka maji ya mto Jordan na pia aliangusha ukuta wa Jeriko na

kuiteka miji yote ng’ambo ya Jordan. Hatimaye Yoshua anasema, “Mimi na nyumba yangu

tutamtumikia Bwana Mungu wetu, nyinyi chagueni hii leo mtakaye mtumikia” kwa maana

ameiona siri ya ushindi alionao utokanao na Neno kukaa ndani yake. Neno la Mungu

likikaa ndani yako, utaishi maisha wokovu kwa ushindi siku zote. Utayaishi maisha ya

wokovu bila kutetereka na kutikisika, utayaishi maisha ya wokovu bila kuyumba na

kuzimia moyo. Hatimaye utaurithi ule uzima wa milele ambayo ndiyo ahadi

tunayoishindania.

34
Roho mtakatifu: Ili kuishi kwa ushindi maisha ya wokovu, tunahitaji sana msaada wa Roho

mtakatifu. Biblia inasema Basi nasema, “enendeni kwa Roho, wala hutazitimiza kamwe

tamaa za mwili” (Wagalatia 5:16), ukiendelea kusoma Biblia inasema, kwa maana mwili

hutamani ukishindana na roho…hata hamwezi kufanya mnayoyataka, lakini mkiongozwa

na Roho mtakatifu hampo chini ya sharia tena… ukisoma Yohana 14:25. Roho mtakatifu

anatufundisha na kutukumbusha kuenenda sawasawa na Neno la Mungu. Unapaswa

kulisoma Neno kila mara, kuliweka ndani yako Neno na kulitenda Neno; Roho mtakatifu

ni mwalimu, anakufundisha Neno, ni msaidizi anakusaidia kuliweka ndani yako na

anakukumbusha kuenenda sawasawa na Neno la Mungu. Petro Simon, mwanafunzi wa

Yesu alikosa kuwa na ujasiri kuenenda na kukiri wokovu hata akamkana Yesu mara tatu…

Lakini alipokuwa pamoja na kanisa la kwanza pale ghorofani Jerusalem, Roho mtakatifu

alishuka na kuwajaza wote wakanena kwa lugha nyingine… Petro alipata ujasiri mkubwa

sana akahubiri na kumkiri pamoja na kumshuhudia Yesu Kristo mbele ya wayahudi

maelfu, wakabatizwa hapo watu takriban wanaume 3,000.

Maombi: Maombi ni silaha nzito sana ili tuwe na ushindi katika maisha yetu ya wokovu.

Maombi hupenya pasipopenya silaha yoyote ile. Maombi ni silaha katika ulimwengu wa

kiroho. Shetani anapambana nasi kila saa ili sisi tushindwe kuishi maisha ya wokovu.

Biblia inasema, “kesheni mkiomba, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi lakini mwili ni

dhaifu”, Mathayo. 25:41; Efeso 6:18, “Kwa sala zote na maombi, mkisali kila wakati

katika Roho, mkikesha katika jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”

Maombi yanatuweka katika uwepo wa Mungu, yanatufanya tuishi tukiwa tumekaa na

Mungu kila wakati. Katika maisha ya wokovu maombi yanatufanya kuzidi kukaa katika

ulimwengu wa roho na kuishi kiroho. Ndiyo maana Bwana Yesu alitusihi kukesha katika

kuomba, Paulo naye ansema “ombeni bila kukoma” 1Thesalonike 5:17 anasema dumuni

katika kuomba… Kolosai 4:2 Kutokana na maombi Mungu ametuahidi mambo mengi


35
mazuri sana. Mathayo.7:7-11, Luka.18:1-8, Yohana.6:23-27. Biblia inasema, “hata

walipokwisha kumwomba Mungu, mahala pale walipokusanyika pakatikiswa, wote

wakajaa Roho mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri”, Matendo. 4:31. Pia Biblia

inasema, “…huu ndiyo ujasiri tulionao, tukiomba kitu chochote katika mapenzi yake

atusikia, kama tunajua atusikia basi tunazo zile haja tumwombazo…” (1Yohana 5:13-15).

Kusanyiko/Kanisa: Ili tuwe na ushindi katika maisha ya wokovu, ni muhimu sana kuwa

washirika. Neno la Mungu linasema, “Kwakuwa walipo wawili watatu, wamekusanyika,

kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”, Mathayo 18:20 Bwana Yesu

alipowatuma wanafunzi wake kwenda kuhubiri injili, aliwapanga wawili wawili na siyo

mmoja mmoja. Biblia inasema “Basi baada ya hayo, Bwana Yesu aliweka na wengine

sabini, akawatuma wawili wawili waende kila mji na kila mahala alipokusudia kwenda

mwenyewe. Akawaambia mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache…” Luka

10:1-2 Kama isingekuwa ni umuhimu wa ushirika Bwana Yesu asingewatuma

wawiliwawili, kwamaa anasema “mavuno ni mengi na watenda kazi ni wachache”.

Aliwatuma wawili wawili kwasababu kila walipo wawili watatu au shirika kwa jina lake

na Mungu yupo mahala hapo.

Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri. Wala tusiache

kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya

hivyo, kwa kadri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia” (Waebrania 10:24-25), pia ukisoma

Yakobo. 5:16. Biblia inasema “ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana

mpate kuponywa…” Neno la Mungu linazidi kuweka bayana umuhimu wa ushirika katika

maisha yetu ya wokovu. Tunaona tena ni katika makusanyiko, mfano kusanyiko la

Yerusalem walipoomba kwa bidii ndipo Roho mtakatifu alishuka, wanafunzi na kanisa la

kwanza wakaanza kunena kwa lugha mbalimbali. Mungu alishuka kwa nguvu kubwa sana.

36
Kuwepo katika ushirika kwa jina la Mungu kunakufanya kukaa katika uwepo wa Mungu

maana yupo mahala hapo.

37
SURA YA TANO

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

5.1 Utangulizi

Sura hii inatoa hitimisho na mapendekezo ya utafiti mzima. Sura hii inatoa ufupisho wa

mambo yote muhimu yaliyowasilishwa katika utafiti huu ili mtu anaposoma sura hii

anapata picha kamili ya utafiti mzima.

5.2 Hitimisho

Utafiti huu umegundua kwamba Wakristo wanarudi nyuma kiimani kwasababu mbalimbali

zikiwemo kukosa misingi au mizizi: Luka 8:13 Biblia inasema “Na wale penye mwamba

ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini

kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.” Mkristo mwenye Misingi imara

anapaswa kusimama mwenyewe haijalishi hata kama mtu aliyekuingiza katika ukristo

amehama imani na kujiunga na imani potofu, yeye anaendelea kusimama kwa gharama

yoyote, wazazi ndugu jamaa au rafiki wa karibu hawezi kubadilisha msimamo wa mtu

mwenye mizizi, utashangaa kuona mtu aliyeokoka hajui hata tofauti ya Mashahidi wa

Yehova na hata wasabato yeye kila aina ya fundisho na imani na kila aina ya upepo wa

Elimu unamzoa tu. Mkristo mwenye mizizi kamwe hawezi kuyumbishwa na jaribu la aina

yoyote,taarifa mbaya kuhusu kiongozi wako wa kidini haiwezi kuwa sababu yaw ewe

kuiacha imani, unaweza kuwepo kanisani lakini kama mimani yako haijajengwa kwenye

misingi na haijaota mizizi ni rahisi kujikuta matatani, Dhambi za kiongozi wako wa kidini

zinauhusiano gani na wokovu wako?uwapo duniani je unafikiri unaweza kumuacha Yesu

kwa sababu ya dhambi ya kiongozi wako?mkristo anayeweza kumuacha Yesu kwa sababu

ya tatizo la mtumwingine huyo hana misingi wala hajaota mizizi hajakomaa. Mkristo

aliyesimama vema ni yule ambaye amesimama hawezi kutikiswa na kurudi nyuma kwa

wengine Yohana 6:66-69 “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake


38
wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je!

Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani?

Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe

ndiwe Mtakatifu wa Mungu.” 

Kuwa debe tupu: 1Wakoritho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika,

kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.” Mkristo ambaye ni debe

tupu ana maisha hatarishi shetani atatafuta kila namna ili aweze kuhakikisha kuwa

anakujaza mambo yatakayokufanya uwe wa kawaida na kukurudisha nyuma, utajaa kila

namna ya udunia ambayo hujawahi hata kuwa nayo kwa sababu, huna kitu, lazima mkristo

awe mtu aliyejaa kitu na sio debe tupu.

Kuupenda ulimwengu: 2Timotheo 4:10 “Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu

huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda

Dalmatia.” Kama mtu akikipenda kitu uko uwezekano mkubwa wa kukifuata, Dema

aliupenda ulimwengu akaacha kufuatana na Paulo mtume anauendea ulimwengu, binti

akimpenda kijana anaaacha wazazi wake na kuambatana na yule kijana kupenda kuna enda

na nguvu ya kufuata au kuambatana.

Uchungu: Waebrania 12: 14-15 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo

utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu

asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na

watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo”.

Maisha ya dhambi: Wakristo wanaoishi katika maisha ya dhambi pia hawawezi kufurahia

kanisa ambalo linakaza kukataza dhambi, hawawezi kujisikia salama kuweko mahali

ambako dhambi zinakemewa,wanaweza kusema sihitaji kumsikia muhubiri huyu mwenye

mahubiri ya kizamani,sitaki kumsikiliza Mchungaji yule na mambo yake ya kuvuana nguo

39
hawataki kukemewa wanahitaji jumbe za kuwatia moyo tu ukianza kunyoosha

wanakuchukia kama uko safi hutaogopa kukemewa ni muhimu kukubali kukemewa,

kurudiwa na kuonywa hali hii ndio itakayotupeleka kwenye uzima. 

Uongo: Uwongo ni dhambi, watu wengi sana hujifunza kusema uongo tangu utoto,

tunapookoka biblia inatutaka tuache kabisa uongo na kuambiana ukweli, Mwanzo 37:31-

35 “Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika

damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii;

basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Akaitambua, akasema, Ndiyo

kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.

Kuasi: Dhambi moja tu katika biblia inafananishwa na uchawi, dhambi hii ni dhambi ya

kuasi, kuasi kwa ufupi ni kushindana na kupinzana na kupingana na mamlaka iliyoko,

wakati wote vikundi vya aina hii vinavyopigana na serikali kwa sababu ya madai kadhaa

kama mfano hapa Afrika vimepewa jina la waasi, Hali kadhalika watu waliomtii Mungu

huitwa wana wa kutii na kinyume chake watu wanaomuasi Mungu huitwa wana wa

kuasi (1Petro 1:14). 

Uzembe/ ujinga/upumbavu: Biblia ina maneno magumu sana kwa mtu aliyerudi nyuma

anu kudumaa kiroho, hakuna maneno ya kutia moyo kwa mkristo anayemuacha Yesu,

watu wengi sana wanapoishi maisha ya dhambi hujifikiri kuwa wao ni wajanja lakini biblia

inamuita mtu anayerudi nyuma kama mjinga na mpumbavu mimi naita uzembe, Mithali 1:

32.

5.3 Mapendekezo

Utafiti huu umetathmini kutathmini chanzo cha Wakristo kurudi nyuma kiimani katika

makanisa ya Kipentekoste: Eneo la Utafiti ni Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es

Salaam, Tanzania. Kutokana na utafiti, Mtafiti amekuja na mapendekezo yafuatayo kwa

40
namna moja ama nyingine, kama yatazingatiwa yatasaidia kanisa. Kwa hiyo imetupasa

kuyaangilia zaidi ya hayo yaliosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana ikiwa lile neno

lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa uasi ulipata ujira wa haki, sisi je!

Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? (Waebrania 2:1-3). Kuna mifano ya

kibiblia ya makanisa ya mara moja yenye nguvu ambayo yalimalizikia kwa kurudi nyuma.

Katika Ufunuo, tunasoma juu ya kanisa la Efeso likiumiza Kristo kwa kujiweka mbali na

upendo wao wa kwanza (Ufunuo 2:4). Vilevile, kanisa la Laodikia liliporudi nyuma kwa

kujiweka katika hali ya joto (3:15), na kanisa la Sarde likageuka kifo cha kiroho (3:2).

Paulo anawaonya waumini wa Galatia kwamba walikuwa wamepotea kutoka ushindi wa

msalaba wa Kristo na walikuwa wamegeuka nyuma kwa kazi za mwili (tazama Wagalatia

1:6-7).

Paulo anaonya hivi, "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na

hekima bali kama watu wenye hekima" (Waefeso 5:15). Unawezaje kujilinda dhidi ya

kuludi nyuma kutoka kwa Kristo na kukataa "wokovu mkubwa"? Paulo anatuambia

"tujali" kwa mambo tuliyoyasikia. Kusoma kasi kwa njia ya Neno la Mungu kunaweza

kuwa na hisia moja ya kufanikiwa, lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba "kusikia" yale

unayosoma na masikio ya kiroho. Fikiria juu ya Neno ili ulisikie moyoni mwako.

Paulo anasema, "Jitathmini wenyewe kwamba mmekuwa katika imani. Jaribu mwenyewe.

Je, hamjui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?" (2 Wakorintho 13:5).

Utafiti umependekeza kuwepo na mafundisho endelevu ya kuwasaidia wakristo kudumu

katika imani. Kwa hiyo kwa kuhitimisha utafiti huu mapendekezo yaliyotolewa

yanatokana na mtazamo wa mtafiti. Hii inamaanisha mtu mwingine aweza kuona tofauti,

kanisa linasisitizwa kutazama mapendekezo.

41
MAREJEO

Bible Society of Kenya. (1992). Biblia. Habari Njema. Nairobi: Bible Society of Kenya.

Bible Society of Tanzania. (1997). Biblia. Maandiko Matakatifu. Dodoma: Bible Society

of Tanzania.

Creswell, J. W. (2009). Research Design: Qualitative, Quantitative, and Mixed Methods

Approaches, Los Angeles: SAGE Publications.

Kothari, C. R. (2008). Reserch Methodogy: Methods and Techiniques, New Delhi: New

Age International Publising Ltd.

Yin, R. K., (1994). Case Study Research: Design and Methods, (2 nd eds.) Thousand Oaks

Calif: SAGE Publishers.

42
VIAMBATANISHO

Kiambatisho A: MWONGOZO WA DODOSO

Naitwa Annie Oscar Bwanali, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha New Life Outreach

Academy of Leadership nachukua Shahada ya Theolojia katika Uongozi wa Kikristo na

Maendeleo ya Jamii. Hojaji hii ina maana ya kujazwa na wahojiwa. Ninatarajia ushirikiano

wako, pia, majibu yako yatahifadhiwa kwa siri na yatatumika hasa kwa kusudi moja la

kufanya utafiti huu.

1. Jina la Mtafitiwa (Hiari):.........................................................................

2. Jina la Kanisa.........................................................................................

3. Nini maana ya Mkristo?

4. Je, umeshawahi kuhama kanisa? Ndiyo ( ) Hapana ( )

5. Nini maana kuhusu Imani?

6. Nini maana ya kurudi nyuma kiimani?

7. Je umeshawahi kufikiria kuacha imani? Ndiyo ( ) Hapana ( )

8. Je umeshawahi kushuhudia mshirika kanisa kwako akihama kanisa?

Ndiyo ( ) Hapana ( )

9. Zipi ni sababu za Wakristo kuhamahama makanisa?

10. Zipi ni njia za kudumu katika imani?

Asante kwa ushirikiano wako

43

You might also like