Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

ANZA SIKU NA BWANA.

#0001

SOMO: TOBA ,MSAMAHA NA KUVUKA NGAMBO

Mathayo 8: 18 Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo.

Marko 5: 21 Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia
mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.

Yoshua 1: 11 Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa
maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana,
Mungu wenu, mpate kuimiliki.

Zaburi 107: 29 Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi yake yakanyamaza.

MAOMBI

1.MUOMBE MUNGU AKUONGEZEE KIWANGO CHAKO CHA IMANI KATIKA KUVUKA YALE
UNAYOPITIA KATIKA MAISHA YAKO

2.HARIBU KILA HILA ZA SHETANI ZINAZOZUIA ILI USIVUKE PALE MUNGU


ALIPOKUSUDIA KATIKA MAISHA YAKO

3.OMBA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ZIJAE KWA WINGI NDANI YAKO ILI UWEZE
KUJIOMBEA KWA MUDA MREFU

4.OMBA KIBALI CHA MUNGU KICHANUE NA KUSTAWI KATIKA KILA UNACHOPITIA


KATIKA MAISHA YAKO

NINYI KILA MSIMAMAPO NA KUSALI, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu
aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye
mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11;25, 26).

Maombi yako hayajibiwi mara nyingi kwa sababu ya wewe kutosamehe wengine. Kwa maneno mengine
Yesu alitaka tufahamu kuwa, tusipojifunza kusamehe wengine waliotukosea, tutabaki na dhambi mbele
za Mungu.

Maana yake nini basi?

Maana yake, kutokusamehe kunahesabiwa kuwa ni kosa mbele za Mungu, na ni dhambi inayotutenga na
uso wa Mungu, ili tusijibiwe maombi yetu toka kwa Mungu.

Kutokusamehe ni uasi, Dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4) Dhambi ni kuasi maagizo ya Mungu.

Kama Mungu ameagiza kwa kinywa cha Kristo, kuwa kabla hatujaomba lo lote, ni lazima tusamehe
kwanza; inakuwaje basi, wewe unataka ujibiwe maombi yako kabla hujamsamehe mwenzako ?
Na kwa kutokusamehe umeasi agizo la Mungu, na kufuatana na waraka wa kwanza wa Yohana 3:4
umehesabiwa kuwa umetenda dhambi.Kwa hiyo unahitajiwa utubu juu ya kutokusamehe!

Tuna uhakika kuwa wewe unayesoma hayo umewahi kuisema 'Sala ya Bwana' iliyoandikwa katika kitabu
cha Mathayo, Sura ya 6:9-15.

Hatujui kama unaelewa uzito wa maneno yaliyomo katika sala hiyo. Walio wengi wanaisema kwa sababu
wameikariri, lakini si kwamba wameielewa maana yake.

Katika sala hiyo, kuna maneno yanayohusu mambo ya kusamehe:

"Utusamehe deni zetu (makosa yetu) kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu (walio tukosea).
(Mathayo 6:12)

Tafakari hili neno 'kama'

Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe waliotukosea.Hii ina maana ya kwamba
kipimo kile unachokipimia katika kuwasamehe wengine ndivyo na Mungu atakavyotumia kipimo hicho
hicho kukusamehe wewe mambo uliyomkosea.Sasa elewa kwamba hakuna kusamehe kukubwa, wala
kusamehe kudogo. Kutokusamehe ni kutokusamehe. Na kusamehe ni kusamehe. Mizani yake inapima
kitu kizima, haipimi msamaha kidogo kidogo.

Yesu alilifafanua jambo hili aliposema:-

"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali
msiposamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu." (Mathayo 6:14,15).

Kumbe kupitia somo hili tunaona msamaha ulivyo na nguvu katika maisha ya mwamini wa Kristo.

SAMEHE NA ANZA MAISHA YAKO UPYA

Ni mimi ndugu yako; Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa Kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap +255 768522999.
harrisonhumphrey25@gmail.com

Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

You might also like