Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

ANZA SIKU NA BWANA.

#0002

UMUHIMU WA IBADA

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, BWANA
ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

ZAB. 91:1-2

Watu wengi inawezekana huwa wanajiuliza ni kwanini tunahudhulia ibada kanisani au kwingineko
zinakoitishwa na wanaishia kutokupata majibu yaliyo sahihi katika ufahamu wao.

Fahamu kuwa, Kusudi la Mungu kukuumba wewe ni ili wewe umfanyie ibada! Mungu anapenda sana
Ibada, anahitaji ushirika na wewe kila saa kila wakati, na ndiyo anatafuta waabuduo halisi ili wamuamudu
katika roho Na kweli. Kwa nini anatafuta waabudio? Kwa sababu inawezekana waliokuwepo na
hawatoshi au hakuna kabisa

Siku za leo Watu wapo busy kutafuta pesa na ukiwauliza mbona hata Ibadani huonekani anasema yuko
busy na Kazi, Hivi Umeshawahi jiuliza maisha ya Ibrahimu ambaye alikuwa ni tajiri na Sidhani kama
wewe unamfikia hata Robo lakini alimjengea Mungu madhabahu (Alimuabudu Mungu) iweje wewe huna
hata Ng'ombe Kumi unajifanya uko busy?

Rudisha Ibada mpendwa.

Ukiona una muda wa kazi tuu na huna Muda wa Mungu ujue umetekwa na Upendo wako kwa Mungu
umepoa na unajipenda mwenyewe. Na Biblia iko wazi

Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa
wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana,
wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,

2 Timotheo. 3:1-2

Ayubu Alikuwa ni Mtu tajiri, mwenye Mali nyingi, kasome Ayubu yote utaona, lakini kuwa na Mali Na
ubusy alikuwa nao hakuacha Ibada, Wewe unanini hadi uwe na Excuse kwenye Ibada, Ungekuwa na Mali
zaidi ya Ayubu si ungepotea kabisa?

Rudisha Ibada, Mahusiano yako na Mungu yakue. Shetani anakutenda kwa akili, shituka na rudisha Ibada

Kwa nini urudishe Ibada? Kwa sababu Mungu ndiye anayekupa NGUVU YA KUPATA UTAJIRI

Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye
imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. KUM. 8:18

Huwezi kufanikiwa Kama umeacha ibada, ili ufanikiwe ni Lazima ung'ang'ane na Anaye toa nguvu za
huo Utajiri unaoutafuta.

Rudisha ibada mpendwa.


Unapoacha Ibada na kuwa busy na Kazi, ni sawa na kutwanga Maji kwenye Kinu, kwa sababu ndiye
anayebariki Kazi ya mikono yako, kama huna mahusiano Mazuri, nani ataibariki, nani atailinda kazi
yako?

Rudisha Ibada mpendwa.

Mtu mwingine anasema, mbona wapo Wasio na Mungu alafu wamefanikiwa? Ni kweli unaweza weza
ukasema wamefanikiwa, Je, unajua Siri ya mafanikio yake? Je, itawasaidia nini wakiupata ulimwengu
wote na kuukosa uzima wa Milele? Nawe itakusaidia nini ukapata Mali zote ila ukaikosa raha ya Uzima
wa milele?

Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

Marko. 8:36

Rudisha Ibada.

Kumbuka ili ufanikiwe Kimungu, Lazima Namba moja awe ni MUNGU.

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Mathayo. 6:33

Pia BIDII NI MUHIMU katika mafanikio yako.

Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.

Mithali. 10:4

Yapo mengi yatakayo Kufanya ufanikiwe Ila hayo juu niliyoyasema ni ya Muhimu (Key points).

Nisikuchoshe Sana, Nikuache ukitafakari

KUMBUKA MUNGU ananafasi kubwa katika Mafanikio yako, hivyo kama uliacha ibada Kwa sababu
ya kutafuta Utajiri, RUDISHA IBADA.

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap +255 768522999.
harrisonhumphrey25@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la
Mungu*

You might also like