Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

ANZA SIKU NA BWANA

SOMO: AHADI ZA MUNGU

#0008

2 Wakorintho 1:20

[20]Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin;
Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

Kwa habari za AHADI ZA MUNGU

#1Ahadi zote za Mungu ziko ndani ya Kristo Yesu. Huwezi kupokea ahadi ya Mungu Nje ya Kristo Yesu.

Mtu ambaye hajampokea Kristo hawezi kupokea ahadi yeyote ya Mungu “ Uponyaji, kufunguliwa,
Amani, Furaha, Mafanikio ”

Kwahiyo haujamwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako hauna kigezo chochote cha
kupokea ahadi za Mungu.

Ndio maana sio sawa Mtu kupokea Uponyaji halafu ukamkataa Yesu. Lazima kwanza Akubali kuwa
Yesu ni Bwana !

#2Ahadi Zote za Mungu katika Yesu Kristo Yesu NI NDIYO

Maana yake chochote alichokisema Mungu unapaswa kukipokea kama Mtoto MCHANGA, bila maswali
na wasiwasi na mashaka.

Ahadi zake katika Kristo ni NDIYO

maana yake Chochote anachosema Mungu kwa habari za maisha yako ni NDIYO
Unapaswa kuwa na jibu Moja tu

“ NDIO BWANA ”

Akisema “ Mathayo 8:17 ”

Yeye mwenyewe alitwaa udhaifu wetu

aliyachukua magonjwa Yetu

Hupaswi kuwa na maswali, wala haupaswi kuingiza Elimu yako ya Darasani na Ya kimaisha

Mungu akisema

Unapaswa kuwa na Jibu Moja tu

“ Ndiyo Bwana Ninaamini kabisa bila maswali - Kuwa Sipaswi kuwa mgonjwa, kwasababu
umeyachukua Magonjwa yangu ili mimi nisiwe nayo ”

KINACHOLETA SHIDA KWENYE MWILI WA KRISTO

1. Usomi “ Elimu ya Darasani ”

2. Elimu ya Maisha na Kijamii inayotokea kwenye mazingira aliyokulia

3. Ukubwa wa Jambo analopitia ukilinganisha na urahisi unaosemwa na Neno la Mungu.

Neno la Mungu

liko juu Sana sana sana ya ELIMU YA DARASANI. Elimu ya Darasani ni elimu ya chini sana
kulingamisha na Neno la Mungu. Hiyo ni mitizamo ya Watu kwa kutumia akili zao za kibinadamu
wanajaribu kubashiri masuluhisho ya matatizo fulani.

Neno la Mungu ni zaidi ya Maandishi

huo ni UZIMA, AFYA, UTAJIRI NA MAFANIKIO.


#3Ahadi za Mungu katika Kristo Yesu ni AMIN.

Maana yake na IWE KWANGU

Ahadi za Mungu sio kwa ajili ya wachungaji, Waalimu, Wainjilisti na Mitume. Ahadi za Mungu ziko
ndani ya Kristo Yesu, na Kama Mtu amemwanini Yesu kama Bwana Na Mwokozi wa maisha yake Ahadi
za Mungu ziko kwa ajili yake, na zinapaswa kutimia katika maisha yake.

unapoiona Ahadi ya Mungu juu ya Afya au Uchumi, au Ndo “ Unapaswa kusema na iwe kwa kwangu ”
bila maswali- ukijua ndivyo Mungu anavyotaka iwe.

Neno la Mungu linasema

Isaya 1:19

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

Kwahiyo Ahadi za Mungu ziko kwa ajili yako na zinapaswa kutimia kwenye maisha yako, na kwahizo
uungu utaanza kudhihirika kwenye maisha yako.

watu wengi wamekubali Elimu ya dunia na Akili zao ndogo walizonazo kwa habari ya maisha, na
wameziacha ahadi za Mungu ambazo tayari ziko ndani yao ambazo zitawapelekea kuishi maisha huru
kabisa.

UNATAKA KUISHI MAISHA BORA

Jua ahadi za Mungu juu ya maisha yako

Tambua kwamba ziko tayari kwa ajili yako kwasababu zimekamilika ndani ya Kristo Yesu

ziamini na zipe kipaumbele cha kwanza katika maisha yako

Ziishi nazo zitakupa kuishi maisha ya Kiungu.

God Bless you, na Uwe na wakati mwema

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa kristo.

Kwa maoni, ushauri na msaada zaidi

whatsap +255 768522999.

harrisonhumphrey25@gmail.com

Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

You might also like