Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

MKATABA WA UPANGISHAJI

Mkataba huu unafanywa leo tarehe ……. Mwezi wa ………..mwaka


………

KATI YA
(jina la mpangishaji)

MKATAB
A WA
NYUMBA 2020
2020
MKATABA WA NYUMBA BAINA YA MPANGISHAJI MKATABA
NA MPANGAJI, UKIONYESHA MAKUBALIANO YA
MUDA ATAKAO KUWEPO NA SHERIA
ZINAZOTAKIWA KUFATWA KIPINDI CHOTE CHA
MKATABA.

………………………………………………………………wa S.L.P
…………..
ambaye katika mkataba huu atajulikana kama MPANGISHAJI

NA
(jina la mpangaji)
…………………………………………………….WA S.L.P
……………………………….
ambaye katika mkataba huu atajulikana kama MPANGAJI.

Na kwa vile MPANGISHAJI ana nia na yuko tayari kupangisha nyumba


yake iliyopo katika Wilaya ya ………….. Mkoa wa…………….

KWA HIYO MKATABA HUU UNASHUHUDIA YAFUATAYO:

1. Kodi itakayolipwa na mpangaji kwa mpangishaji katika mkataba


huu wa upangaji ni shilingi za kitanzania TSH ……………. kwa
mwezi ambazo zitalipwa kwa kipindi cha muda sahihihi wa
makubaliano.
2. Wajibu na majukumu ya mpangaji katika mkataba huu ni kama
ifuatavyo:
(a) Kulipa kodi yote iliyotajwa katika mkataba huu kadri ya
makubaliano.
(b) Wakati wote wa ukaazi katika nyumba, kutunza na kuweka
mazingira yote ya nyumba (ndani na nje) katika hali ya usafi
wakati wote na kuhakikisha utunzaji wa vifaa vyote vya
nyumba ikiwamo milango, vitasa, madirisha, mabomba, nyaya
za umeme, rangi na mazingira kwa ujumla yawe katika hali
nzuri wakati wote.
(c) Kumruhusu mpangishaji au wakala wake atakaye mteua
kuingia katika nyumba kwa ajili ya ukaguzi na au kufanya
matengenezo.
Kuingia huko katika nyumba lazima kuwe kwa wakati na muda
unaokubalika hasa wakati wa mchana na lazima kuwe na taarifa
kutoka kwa npangishaji itakayokuwa imetolewa kwa mpangaji
kwa muda muafaka.
(d) Kutokubadilisha mandhari ya nyumba, kuongeza au kupunguza
Chochote kisichohamishika pasipo kuomba na kupatiwa idhini
ya kimaandishi na mpangishaji.
(e) Kutumia nyumba inayohusika na mkataba huu kwa makazi tu
na kutoruhusu au kuweka kitu chochote ambacho kitasababisha
kero, usumbufu, au kuwa chanzo cha uharibifu wa nyumba na /
au mazingira ya nyumba au nyumba za jirani.
(f) Kutokufanya biashara ya aina yeyote katika nyumba, na
kutokuifadhi vitu vya kulipuka km petrol,diesel na gesi.
(g) Kulipa ankra zote zitokanazo na matumizi ya umeme na maji
na kuhakikisha wakati wote haachi deni lolote litokanalo na
matumizi tajwa katika kipindi chote cha ukaazi.
(h) Kutokupangisha nyumba inayohusiana na mkataba huu au
sehemu yeyote ya nyumba kwa mpangaji mwengine. Mpangaji
atakapoondoka anatakiwa kukabidhi nyumba kwa mpangishaji
au mwakilishi wake atakayemwarifu.
(i) Mkataba huu utakapokoma au kwisha kipindi chake na
Mpangishaji akaaka kuokuendelea na mkataba, Mpangaji
atatakiwa kukabidhi nyumba kwa mpangishaji ikiwa katika hali
nzuri pamoja na vifaa vyote vya nyumba ikiwemo
milango,vitasa,madirisha,mabomba,nyaya za umeme. Kama
alivyokabidhiwa mwanzoni mwa mkataba.
Mpangaji atatakiwa kulipa na/kufidia uharibifu wowote
utakaotokana na matumizi mabaya na yasiyo ya kawaida au
sahihi katika nyumba.
Ikiokea mpangaji kuvunja sheria tajwa hapo juu, Mpangishaji
anauwezo wa KUSITISHA MKATABA na kurudisha kodi
iliyobaki katika kipindi cha mpangaji.

3. Wajibu na majukumu ya Mpangishaji katika Mkataba huu ni kama


ifuatavyo:
(a) Kuhakikisha kwamba mpangaji anakaa kwa amani na
anafurahia nyumba na eneo linaloambatana nalo bila
kubughudhiwa kwa namana yeyote na mpangishaji au
mwakilishi wake kwa kipindi chote cha mkataba huu.
4. Kwa sharti kwamba inakubalika na kutamkwa na pande zote mbili
kuwa :
(a) Kama kutakuwa hakuna ukiukwaji wowote wa mkataba huu na
Mpangaji ametoa taarifa kwa Mpangishaji miezi (3) kabla ya
mkataba huu kufika kikomo kukusudia kuuendeleza mkatab
huu, na kama mpangaji ataridhia, mkataba huu utatiwa saini
tena kwa kipindi kipya na pande zote mbii kwa masharti
yaleyale au tofauti na yaliyofikiwa kwenye mkataba huu.
(b) Ikitokea Mpangaji amekatisha mkataba kabla ya kipindi
kilichokubaliwa kwenye mkataba kwisha, mpangishaji
atamrudishia nusu ya fedha itakayokuwa imebaki kwenye
mkataba.

Kwa kuridhia na kuthibitisha dhamira zetu, pande zote mbili zimeafikiana


vipenfele vyote vya mkataba huu na kuweka saini.
(JiNA mpangishaji) (saini)

………………………………………………………….
……………………………………..
(JiNA mpangaji) (saini)

…………………………………………………………..
……………………………………..
Tarehe……….Mwezi ………….mwaka………..

You might also like