Professional Documents
Culture Documents
Lesson 2 Zoezi
Lesson 2 Zoezi
Zoezi
PAA NA BUIBUI
SIKU moja baba na mama yake Juma waliuchoma moto msitu uliokuwa karibu na nyumba yao.
Buibui mmoja akamwambia paa, 'Tafadhali, rafiki yangu, nichukue juu ya pembe zako ili
msiteketee katika moto huu. Siku moja na mimi nitakusaidia vile vile; watu wamesema,
'Ukimfaa mwenzio kwa jua, naye atakufaa kwa mvua.''
Paa akamwambia, ' Ha, ha, ha, mdudu mdogo kama wewe utawezaje kunisaidia mnyama
mkubwa na mwenye nguvu kama mimi ? Unanidanganya tu.' Lakini halafu paa akakubali
kumchukua juu ya pembe yake.
Baadaye Ali na Mwangi, wawindaji, wakaja katika msitu ule. Paa alikuwa amejificha kwa mbali
kidogo. Mara Ali akaona alama za nyayo za paa. Akamwambia Mwangi, 'Mwangi eh, naona
mwanzo wa alama za nyayo za paa ; hayuko mbali.'
Buibui akasema, ' Sasa wakati wa kukulipa fadhili zako umefika, Bwana Paa.' Basi buibui
akauzungusha uzi mahali pale alipokuwapo paa. Kisha akauzungusha mwingine juu ya zile
alama za nyayo zilizokuwa karibu na paa. Ali na Mwangi walipoona ule uzi, wakasema, ' Ah,
bila shaka amepitia njia nyingine.' Basi wakaenda zao moja kwa moja bila ya kuzidi kumtafuta
paa yule.
Basi kama wenzetu wakitusaidia wakati wa shida au dhiki, nasi hatuna budi kuwasaidia
wapatwapo na mambo kama hayo. Wadogo nao huweza kuwasaidia wakubwa.
MAZOEZI
Baba na mama yake Juma waliuchoma moto msitu uliokuwa karibu na nyumba yao.
3. Paa alijibuje ?
Yeye akacheka na kusema, vipi mdudu mdogo kama unamlinda mnyama mkubwa kama
mimi.
4. Ali na Mwangi walikuwa watu gani ? Walifanyaje?
Buibui akauzungusha uzi mahali pale alipokuwapo paa. Kisha akauzungusha mwingine
juu ya zile alama za nyayo zilizokuwa karibu na paa.
IV. Andika majina ya wazee wako, rafiki zako na miji minne yoyote. Tunga sentensi utumie
majina hayo.
V. Andika sentensi utumie majina ya wanyama wenye pembe tu katika hawa wafuatao:
asali, ndovu, buibui, mishale, wadogo, wawindaji, moto, shimo, sumu, maziwa.
1. Ali na Mwangi walikuwa wawindaji hodari.