Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

Tarehe 15/9/21

Y9 lesson8
Malengo
- kujuwa waliohudhuria kipindi
- Kupima uwezo wa kusoma na kufahamu yaliyosomwa kwa kujibu
maswali

Zoezi 3
Utasoma habari kuhusu hatari ya moto, kisha jibu maswali yanayofuwata kwa
kiswahili
Ruhee Jivani Y9S
HATARI YA MOTO

Bibi Asha ni mwanamke mzuri. Ana mume mrefu. Ana watoto watano. Lakini
pichani tunaona watoto watatatu. Mtoto mkubwa ni Juma; mtoto mdogo ni Hadija.
Mtoto wa katikati ni Maria.Maria na Hadija ni wanene kidogo. Juma si mnene, ni
mwembamba. Yeye ni mrefu pia. Juma na baba yake ni warefu. Maria na Hadija,
wao ni wafupi.
Watoto wana vitu vingi. Wana kalamu, karatasi, viti, deski, na vitabu. Hivi ni
vyao. Lakini kiberiti si chao. Hawana kiberiti. Mama yao ana kiberiti. Yeye ana
kiberiti kwa sababu yeye ni mtu mkubwa, ni mtu mzima. Kwa hiyo, kiberiti ni
chake. Lakini ni watoto na wao wanataka kiberiti. Wanataka kucheza na kiberiti.
Sasa watoto wawili wana kiberiti. Wasichana, ambao ni wanene kidogo, wana
kiberiti. Wao ni Maria na Hadija. Hawa wanacheza na kucheka. Sasa wanawasha
moto.

Lakini Maria na Hadija wanafanya makosa. Wana kiberiti cha mama. Kiberiti si
chao, ni cha mama yao. Wao ni wajinga. Moto ni hatari. Si kitu cha kuchezewa na
watoto. Juma anautazama moto. Yeye ni hodari. Anajua hatari yamoto.
Sasa Juma anazima moto. Ana maji rnkebeni. Anatia maji motoni. Yeye ni mlinzi
wa watoto. Lakini watoto wanalia. Wao wanapenda moto. Wanapenda kiberiti pia.
Wanalia sana.
Juma anasema, “Kiberiti ni chenu? La, si chenu; ni kiberiti cha mama. Ni chake.
Ninyi mna kalamu, karatasi, viti, deski, na vitabu. Lakini kiberiti si chenu. Kiberiti
na moto ni vitu hatari sana.”
Sasa Maria na Hadija wanaogopa moto. Moto ni hatari. Sasa wanajua hatari ya
moto. Mzazi wao ana kiberiti; watoto hawana kiberiti. Wana vitu vingine. Watoto
wafupi wana karatasi, kalamu, deski, na viti, Sasa hawa wanachora picha.
Wanafurahi. Tena wanacheza

1. Mume wake Bi Asha ni mfupi au mrefu?


(1marks)
Ana mume mrefu.
2. Bi Asha ana watoto wangapi?
(2marks)
Ana watato watano.
3. Maria na Hadija wakoje: wanene au wembamba?
(1marks)
Maria na Hadija ni wanene kidogo.
4. Watoto gani wanawasha moto?
(2marks)
Maria na Hadija.
5. Kiberiti ni cha nani?
(2marks)
Mama yao ana kiberiti.
6. Nani anaelewa hatari ya moto?
(2marks)
Juma
7. Kwa nini watoto wa kike wanalia?
(2marks)
Wanapenda moto. Wanapenda kiberiti pia.
8. Taja majina ya watoto wa Bi Aisha ambao wanapatikana katika ufahamu?

(2marks) Maria
Hadija
Juma
9. Mtoto mdogo wa Bi Aisha anaitwa nani?
(2marks)
Hadija
10. Ni nani aliye zima moto? Taja vile alivyouzima?
(3marks)
Juma anazima moto. Ana maji mfukoni.

You might also like