UCHAMBUZI WA KITABU Mindset Saikolojia Mpya Ya Mafanikio - Sehemu

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 28

SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.

ME/SOMAVITABUTANZANIA

UCHAMBUZI WA KITABU; Mindset


(Saikolojia Mpya Ya Mafanikio – Sehemu
Ya Pili)
SEHEMU YA PILI; ATHARI ZA MITAZAMO KWENYE MAFANIKIO.
Karibu kwenye sehemu ya pili ya uchambuzi wa kitabu Mindset: the new
psychology of success kilichoandikwa na Carol S. Dweck. Kitabu hiki
kinatufundisha aina mbili za mitazamo tuliyonayo na jinsi inavyoathiri
mafanikio tunayopata kwenye maisha.
Kwenye sehemu ya kwanza tumejifunza kwa kina kuhusu aina mbili za
mtazamo ambao watu tunakuwa nao, mtazamo mgando (FIXED MINDSET) na
mtazamo wa ukuaji (GROWTH MINDSET). Kisha tukaingia ndani zaidi kwenye
kila mtazamo na kisha kuona jinsi mitazamo hiyo inavyoathiri uwezo ambao
mtu anakuwa nao na matokeo ambayo anayapata kwenye maisha.
Kwenye sehemu ya pili tunakwenda kuona jinsi mitazamo ambayo watu
wanayo inavyokuwa na madhara kwenye michezo, biashara na mahusiano.
Kwenye michezo tutaona jinsi mitazamo inavyowatofautisha wanaoshinda na
wanaoshindwa, kwenye biashara na kazi tutaona mitazamo inavyowajenga au
kuwabomoa viongozi na kwenye mahusiano tutaona jinsi mitazamo
inavyochangia kuimarika au kuvunjika kwa mahusiano.
Karibu kwenye sehemu hii ya pili, tuyaone madhara ya mtazamo na hatua za
kuchukua ili kujijengea mtazamo sahihi utakaokuwezesha kufikia mafanikio
makubwa kwenye chochote unachofanya.

MICHEZO; MTAZAMO WA WASHINDI.


Kila mtu huwa anaamini mafanikio kwenye michezo yanatokana na kipaji
ambacho mchezaji anacho. Hata wale ambao ni wataalamu kwenye eneo la
michezo, wamekuwa wanaamini wanaofanikiwa ni wale wenye kipaji na
mchezo husika na kama mtu hana kipaji basi hawezi kufanikiwa.
Vipaji vimekuwa vinaaminiwa sana kwenye michezo kiasi kwamba timu kubwa
na makocha wamekuwa wanatafuta na kuwinda wachezaji wenye vipaji,
wakiamini kwa kuwa na wachezaji wa aina hiyo, kushinda mataji itakuwa rahisi.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Lakini tunaporudi kwenye dunia ya kawaida, tunapoangalia baadhi ya


wachezaji ambao waliweza kufikia mafanikio makubwa, hawakuwa na vipaji
kabisa kwenye michezo hiyo. Mwanzoni walionekana ni watu ambao hawana
nafasi ya kufanikiwa kwenye michezo waliyoingia.
Mfano mzuri ni aliyekuwa mpiganaji Muhammad Ali, hakuwa na mwili
unaoendana na upiganaji. Kwa vipimo vya kipaji kwenye upiganaji, Muhammad
Ali alionekana kutokuwa na nafasi ya kufanikiwa, hakuwa na uzito sahihi,
ukubwa wa kifua na hata ngumi ya kutosha. Na hata alipoingia kwenye
upiganaji, mtindo wake ulikuwa wa tofauti na wa hasara kwake, kwa sababu
ulimpa mshindani wake nafasi nzuri ya kumshinda.
Mchambuzi mmoja aliwahi kumwelezea Muhammad Ali kama mtu aliye
kwenye reli na treni inakuja, lakini badala ya kuondoka kwenye reli hiyo,
anaikimbilia treni.
Pamoja na kukosa kila aina ya kipaji ambacho alipaswa kuwa nacho ili
afanikiwe kwenye mchezo wa masumbwi, Muhammad Ali aliweza kufikia
mafanikio makubwa kwenye mchezo huo, kwa sababu alijua nguvu yake
ilipokuwa, ambayo ni kwenye akili yake. Akihojiwa kuhusu pambano moja
aliloshinda lakini akionekana kupigana tofauti Muhammad Ali alieleza
kilichomwezesha kushinda ni kumjua vizuri mshindani wake. Kabla ya
pambano, alisoma kila kitu kuhusu mchezaji huo, aliangalia mapambano yake
ya nyuma na hata kufuatilia mahojiano yake. Kwa njia hiyo alijua jinsi akili ya
mshindani wake inavyofanya kazi na kuona udhaifu ulipo ili kuweza kuutumia
vizuri.
Mchezaji mwingine ambaye aliweza kufikia mafanikio makubwa kwenye
michezo licha ya kukosa kipaji alikuwa Michael Jordan. Tangu akiwa mdogo
hakuonekana kuwa na kipaji cha mpira wa kikapu. Akiwa shule ya sekondari
aliondolewa kwenye timu ya shule kwa sababu alionekana hawezi. Akiwa chuo,
alipenda sana kuwa kwenye timu ya kikapu lakini hakupewa nafasi.
Kwa jinsi Michael Jordan alivyokuja kufikia mafanikio makubwa kwenye mpira
wa kikapu na kushinda mataji mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote,
unaweza kusema makocha wa shuleni na chuoni walifanya makosa makubwa
kutokumpa nafasi. Lakini ukweli ni kwamba hakuwa na kipaji na wala
hakuweza kucheza vizuri kipindi hicho.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Jordan alipokosa nafasi ya kucheza kwenye timu ya chuo, alionekana kukata


tamaa, lakini mama yake alimwambia kama anataka kweli kucheza mchezo
huo, lazima ajijengee nidhamu ya hali ya juu. Jordan alisikia alichoambiwa na
mama yake, alikuwa akiondoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi na
kwenda kufanya mazoezi kabla muda wa shule haujafika. Alitumia muda
mwingi kwenye kufanya mazoezi na alifanyia kazi maeneo yote aliyokuwa na
madhaifu.
Kocha wa timu ya chuo aliona jinsi Jordan alivyokuwa anajituma na kuwa bora
kila siku na hapo alimpa nafasi. Lakini bado miaka ya awali kwenye mchezo
hakuwa vizuri, timu yake ilipoteza mashindano mengi lakini yeye hakukata
tamaa. Hata baada ya kushindwa, aliendelea kufanya mazoezi makubwa na
kwa muda mrefu. Hali hiyo ilimfanya kuwa bora zaidi na kusaidia timu yake
kushinda.
Hii ikawa ndiyo tabia ya Jordan, hata alipokuwa kwenye kilele cha mafanikio,
hakusahau kuweka juhudi kubwa kwenye mazoezi. Alikuwa akifanya mazoezi
kama vile mchezaji mchanga. Mmoja wa makocha wake amewahi kumwelezea
Jordan kama jiniazi ambaye kila wakati anakazana kukuza ujiniazi wake.
Jordan mwenyewe amekuwa akieleza kwamba anachoamini ni mafanikio
yanatokana na uimara wa akili na roho na siyo mwili peke yake.
Kilichomwezesha kufanikiwa licha ya kuonekana hana kipaji cha mchezo wa
kikapu ni uimara wa akili na roho yake, ambao ulimsukuma kujenga uimara wa
mwili kupitia mazoezi na hatimaye kuwa bora.
Mifano ni mingi na kwa kila aina ya mchezo, wale wanaofanikiwa sana siyo
wanaoanza wakiwa na vipaji, bali wanaoanza wakiwa kawaida na kuweka
juhudi kubwa kwenye kukuza uwezo wao na kuweza kufanikiwa.

Athari za mtazamo kwenye michezo.


Kwa mifano tuliyoiona, tunaona jinsi ambavyo mitazamo watu waliyonayo
inaathiri mafanikio wanayoyapata.
Kwenye michezo iko wazi, mtu anawekwa kwenye kundi la ana kipaji cha
mchezo fulani au hana. Kama ana kipaji anapewa nafasi ya kufanikiwa na kama
hana kipaji basi hapewi nafasi.
Kuwa au kutokuwa na kipaji kunawagawa watu kwenye makundi mawili,
wenye mtazamo wa ukuaji na wenye mtazamo mgando.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Wenye vipaji wanakuwa na mtazamo mgando, wakiamini vipaji vinawapa


uwezo na hivyo hakuna namna wanaweza kubadili hilo. Wasio na vipaji
wanakuwa na mtazamo wa ukuaji, wakijua kwamba wanaweza kufanikiwa
iwapo wataweka juhudi kubwa.
Kinachotokea ni wasio na vipaji wanafanikiwa sana huku wenye vipaji wakiishia
kuwa kawaida. Mtazamo walionao unakuwa na athari kubwa kwenye
mafanikio wanayopata.
Mitazamo hii imekuwa inajengwa na mategemeo ambayo jamii imekuwa nayo.
Kwa kila mchezaji aliyefanikiwa, amekuwa anasifiwa kwa kipaji alichonacho na
hilo kuwafanya wengine waone kama hawana vipaji hawawezi kufanikiwa.
Lakini unapoangalia maisha ya wale waliofanikiwa kwenye kila aina ya
michezo, siyo vipaji pekee, bali juhudi kubwa zimechangia mafanikio yao.
Mwandishi Malcolm Gladwell amekuwa anaeleza kwamba jamii imekuwa
inawatukuza washindi kama watu wa tofauti, ambao walizaliwa na vipaji vya
juu. Wakati ukiangalia wengi, walikuwa wa kawaida kabisa kabla hawajafikia
ushindi, kilichowafikisha kwenye ushindi ni juhudi kubwa walizoweka na
kujijengea uwezo ambao hawakuwa nao awali.
Kwa kifupi tunaweza kusema mtazamo wa jamii kwenye mafanikio ya michezo
ni mgando, huku mtazamo wa wale wanaofanikiwa kwenye michezo hiyo
ukiwa wa ukuaji.

Kipaji kinapokuwa laana.


Kuna wachezaji ambao wanaanza wakionekana kuwa na kipaji kikubwa
mwanzoni, wanapewa matumaini ya kufanya vizuri na kufanikiwa sana kwenye
michezo waliyopo, lakini kinachotokea ni wanashindwa vibaya, tena na wale
ambao walionekana hawana kipaji kabisa kwenye michezo hiyo.
Kipaji kimekuwa laana kwa wengi kwa sababu kinawafanya wawe na mtazamo
mgando. Kwa kuambiwa wana kipaji ambacho wengine hawana, wamekuwa
hawajisukumi kuweka juhudi na kujiendeleza. Wao wanaamini tayari uwezo
wanao na hawahitaji kufanya mazoezi sana kama wale wasio na kipaji.
Hali hiyo inawaingiza kwenye mtazamo mgando, hawajifunzi, hawakazani kuwa
bora na kwa jinsi michezo ilivyo, mchezaji asiyeweka juhudi kwenye kujifunza
na mazoezi, hawezi kufanikiwa.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Hivyo picha ambayo imekuwa inaonekana kwenye michezo ni hii, wale wenye
vipaji vikubwa wamekuwa wanaishia kuwa kawaida, huku wanaoanza bila
vipaji wakifanya makubwa. Kwa wengi kuanza na kipaji kunakuwa kikwazo cha
kufikia mafanikio makubwa, yote ni kwa sababu ya mtazamo mgando ambao
wenye vipaji wanakuwa nao.
Wale wenye vipaji, kwa kudanganywa na ukuu ambao vipaji hivyo vinawapa
wamekuwa hawaoni umuhimu wa kuweka kazi kujiendeleza ili waweze
kufanikiwa na hilo ndiyo linawazuia kufanikiwa.

Mtazamo na tabia.
Athari ya mtazamo kwenye mafanikio ya michezo inatokana na tabia ambayo
mchezaji anakuwa amejijengea.
Tabia ndiyo inayowatofautisha wale wanaofanikiwa na baadaye kushindwa na
wale wanaofanikiwa na kubaki kwenye ushindi huo.
Kwenye michezo, hata wale wenye vipaji na wasioweka juhudi kwenye
kujiendeleza, kuna wakati vipaji vyao huwawezesha kushinda, lakini huwa
hawadumu kwenye ushindi huo.
Iko hivi, kila mchezaji kuna wakati huwa anakutana na ugumu. Hata mchezaji
mwenye mafanikio makubwa kiasi gani, huwa hapati ushindi kwenye kila
mchezo.
Kila mchezaji huwa anashindwa kwenye baadhi ya mashindano, kushinda huko
ndiyo kunakowatofautisha wale wanaofikia mafanikio makubwa na kudumu
nayo na wale wanaopotea.
Wale wanaoanza wakiwa na vipaji na kuwa na mtazamo mgando,
wanaposhindwa kwenye shindano moja, huwa wanajiona hawawezi tena,
wanakata tamaa na hawaweki tena juhudi kwenye mashindano mengine.
Wale wanaoanza bila ya vipaji na wenye mtazamo wa ukuaji, wanaposhindwa
kwenye shindano moja, wanajifunza makosa waliyofanya na wanaenda
kufanya mazoezi zaidi ili waweze kushinda mashindano yanayofuatia.
Wachezaji wengi wanaofanikiwa wamekuwa wakieleza kilichowawezesha
kufanikiwa ni uimara wa akili zao, kuweza kuendelea kujisukuma licha ya
kukutana na ugumu ambao uliwaangusha na kuwakatisha tamaa wengine.
Wachezaji wote wanaofikia ushindi wa juu, wanajua kabisa kwamba
hawajazaliwa na uwezo wa kipekee kwenye michezo yao, wanajua juhudi
JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

wanazoweka kwenye mazoezi ndizo zinawapa ushindi na huwa hawaachi hilo


maisha yao yote wanapokuwa kwenye michezo hiyo.
Mmoja wa makocha maarufu kwenye mpira wa kikapu John Wooden amewahi
kunukuliwa akisema; “Naamini uwezo unaweza kumfikisha mchezaji kileleni,
lakini kitakachomfanya abaki kwenye kilele ni tabia yake. Ni rahisi kuzoea na
kuacha kuweka juhudi ukishafika kileleni, inahitaji tabia kumfanya mtu
aendelee kuweka juhudi kwenye mazoezi hata baada ya kuwa mshindi.”
Wachezaji wenye mtazamo wa ukuaji, wamekuwa wakifanikiwa kwa sababu
wana tabia ya kujifunza na kufanya mazoezi bila ya kujali wako kwenye hatua
gani. Kwao kujifunza na kufanya mazoezi ni kitu endelevu na wanachofurahia
kufanya kila siku. Iwe wanashinda au wanashindwa, kujifunza na mazoezi ni
kitu endelevu.
Mtazamo wa ukuaji unawajengea wachezaji wanaofanikiwa imani kwamba ili
kufanikiwa, mtu anapaswa kuweka juhudi kubwa kwenye kujifunza na mazoezi
bila ya kujali yupo kwenye hatua gani.

Mtazamo kwenye kushinda na kushindwa.


Wale wenye mtazamo wa ukuaji, wanaposhindwa huwa wanachukulia kama
kitu cha kuwaamsha na kuwahamasisha kuweka juhudi zaidi.
Hili linaelezewa vizuri na kauli ambayo Michael Jordan amewahi kuitoa,
akisema; “Nimekosa zaidi ya mashuti elfu 9, nimepoteza michezo zaidi ya 300.
Mara 26 niliaminiwa na kupewa nafasi ya kuipa ushindi timu yangu, lakini
nilishindwa kufanya hivyo.”
Unaweza kufikiria ni kwa namna gani mtu anayekiri kufanya makosa mengi na
makubwa kiasi hicho ameweza kufikia mafanikio ya juu kabisa kwenye mchezo.
Na jibu liko wazi, kila alipokosea, kila aliposhindwa alienda kujifunza na
kufanya mazoezi zaidi na hilo lilimfanya awe bora zaidi.
Wale wenye mtazamo mgando, kushindwa ni kiama, wanaposhindwa kwenye
shindani au mchezo mmoja, wanajiona hawana tena uwezo. Na kwa sababu
hawaamini kwenye kujifunza na mazoezi, hawakazani kuwa bora zaidi,
wanakata tamaa na hawafanikiwi.
Mtazamo mgando pia huwafanya wachezaji kuwa na wivu, pale wao
wanaposhindwa huku wengine wakifanikiwa, wanawaonea wivu wale

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

wanaofanikiwa na kuwaombea mabaya. Hali hii huwafanya wasiwe tayari


kushirikiana au kujifunza kutoka kwa wengine.

Ushindi ni mchakato.
Wale wanaofikia ushindi kwenye michezo na kubaki kwenye kilele cha ushindi
kwa muda mrefu wamekuwa wanajua kitu kimoja muhimu, ushindi ni
mchakato na siyo tukio.
Hivyo huwa wanaumiliki mchakato wa wao kufika na kubaki kwenye kilele cha
ushindi. Hilo ndiyo limekuwa linawawezesha wengi kubaki kwenye kilele cha
mafanikio kwa muda mrefu, licha ya umri wao kwenda.
Ni kwa sababu wanaujua mchakato na kuufuata kila wakati, bila ya kujisahau
kwa kuona mafanikio yao yanawapa nafasi fulani.
Kinachowafanya waufuate mchakato ni kwa sababu wanaufurahia. Wengine
wanapowaangalia washindi wanavyofanya mazoezi magumu kila siku,
wanaona kama wanajitesa, lakini wao wanakuwa wanafurahia hali hiyo, kwa
sababu wanajua ndiyo kinachowafanya wakae kwenye kilele cha ushindi.
Wenye mtazamo mgando na ambao hawakai kwenye kilele cha ushindi kwa
muda mrefu, huwa hawachukulii ushindi kama mchakato. Huwa wanaona ni
kitu ambacho tayari wameshapewa, ni wao kukichukua tu.
Kwa mtazamo huu hawaweki juhudi kwenye kujifunza au mazoezi na hilo
hupelekea wao kufanya vibaya. Wanapofanya vibaya, huwa hawaangalii wapi
wanakosea, badala yake wamekuwa wanatafuta nani wa kumlaumu. Kwa kuwa
tayari kutupa lawama kwa wengine, hawajifunzi na hivyo wanazidi kupotea.

Mchango wa timu.
Japokuwa wachezaji wengi wenye mafanikio makubwa huwa wanaelezewa
wenyewe, lakini wote hawajafika kwenye mafanikio yao peke yao.
Wamesaidiwa na timu ambazo wamekuwa nazo katika michezo wanayofanya.
Hakuna mchezaji yeyote ambaye ameweza kufikia mafanikio makubwa yeye
peke yake, hata kwa michezo inayohusisha mchezaji mmoja kama golf au
ngumi, bado mchezaji anahitaji kuwa na kocha wa kumfundisha na kumpa
miongozo mbalimbali.
Wenye mtazamo mgando na wa ukuaji wanatofautiana kwenye timu.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Wale wenye mtazamo mgando huwa hawapo tayari kushirikiana na timu,


huwa wanajiona wana kipaji cha juu na hivyo wanaweza kufanya makubwa
peke yao na hilo limekuwa kikwazo kwao.
Wale wenye mtazamo wa ukuaji wamekuwa wakithamini sana mchango wa
timu, wanajua hawana vipaji vikubwa hivyo ushirikiano wa wengine unahitajika
kwenye mafanikio yao. Wanakuwa tayari kujifunza yale wanayofundishwa na
kushirikiana na wengine na hilo linawafikisha kwenye mafanikio.
Mtazamo mgando unamfanya mchezaji ajione tayari anajua na anaweza kila
kitu na hilo linaathiri ushirikiano wake na wengine.
Kikubwa kabisa tunachojifunza kuhusu athari za mtazamo kwenye michezo ni
tabia, akili na roho vina mchango mkubwa kwenye mafanikio kuliko kipaji.
Kuwa na mtazamo wa ukuaji kunawasukuma wachezaji kujifunza, kufanya
mazoezi na kuwa bora zaidi, huku mtazamo mgando ukiwafanya wachezaji
kuamini kwenye vipaji walivyonavyo na kutokuweka juhudi kwenye kujifunza
na mazoezi.
Hivyo wale wanaoanza bila ya vipaji vikubwa wamekuwa wanafanikiwa sana
wanapokuwa na mtazamo wa ukuaji, huku wale wanaoanza na vipaji vikubwa
wakishindwa pale wanapokuwa na mtazamo mgando.
Uwe una kipaji au la, mafanikio yako kwenye mchezo wowote ule
yanategemea zaidi mtazamo wako kuliko kipaji.

Hatua za kuchukua.
Je kuna michezo yoyote ambayo umekuwa unaipenda lakini unajiambia huna
kipaji nayo? Hiyo siyo sababu ya kushindwa kufanikiwa kwenye michezo hiyo,
kama kuna mchezo unaoupenda sana, jijengee mtazamo wa ukuaji na nenda
kaweke juhudi kwenye mchezo huo, utafanikiwa.
Je kuna mchezo uliokuwa una kipaji nao ulipokuwa unaanza lakini baadaye
ukaona huwezi tena? Hapo umekutana na laana ya kipaji, ambayo ilikuzuia
usiweke juhudi. Unaweza kufanikiwa kwenye mchezo huo ukiwa na mtazamo
wa ukuaji na kuweka juhudi.
Tabia ni hitaji muhimu kwenye mafanikio ya michezo na tabia nzuri zinatokana
na mtazamo wa ukuaji. Je ni tabia zipi unazohitaji kujijengea ili uweze
kufanikiwa kwenye mchezo wowote uliopo au unaotaka kuingia?

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Wachezaji wanaofanikiwa huwa wanafurahia mchakato na siyo matokeo, je


wewe ni kipi unachofurahia kwenye mchakato wa mchezo unaoshiriki au
unaotaka kuingia?
Muhimu; unaweza kutumia dhana hizo kwenye maeneo mengine na siyo
michezo tu, mfano uandishi, muziki na hata sanaa nyingine. Wengi wamekuwa
wanaamini hawana vipaji lakini ukiangalia wanaofanikiwa, siyo kwa sababu ya
vipaji bali juhudi. Kama umekuwa unataka kuandika au kuongea lakini
unajiambia huna kipaji, futa kabisa hiyo dhana, badala yake weka juhudi
kwenye kujifunza na kufanya mazoezi na utafanikiwa.

BIASHARA; MTAZAMO NA UONGOZI.


Kila kampuni huwa inapitia changamoto mbalimbali, baadhi ya kampuni huwa
zinavuka changamoto hizo na kufanikiwa, huku nyingine zikishindwa kuvuka na
kufa. Kinachotofautisha kampuni zinazofanikiwa na zile zinazokufa ni aina ya
watu walio ndani ya kampuni hizo.
Kampuni huwa inajenga mtazamo wake kulingana na mtazamo wa walio ndani
ya kampuni hiyo. Na hili huanzia kwenye uongozi wa kampuni.
Kampuni nyingi zimekuwa zinaamini kwenye vipaji, kujiri watu wenye vipaji
maalumu na uwezo mkubwa na kuamini hao wataiwezesha kampuni
kufanikiwa. Hivi ndivyo makampuni mengi makubwa yanavyofanya, kwenda
kwenye vyuo mbalimbali na kuchagua wale wenye ufaulu mkubwa kwa
kuamini wataweza kufanya vizuri kazi zao na kuiwezesha kampuni kufanikiwa.
Lakini kinachotokea ni kampuni inajikuta ina watu wengi ambao wana
mtazamo mgando, ambao wanaamini uwezo wao ni wa juu na una ukomo
hivyo hawajisukumi kujifunza na kuweka juhudi.
Mbaya zaidi ni pale watu hao wanapokutana na changamoto, hawazipokei na
kujifunza ili wawe bora zaidi, badala yake wanatafuta namna ya kuzikimbia au
kutoa lawama kwa wengine. Hali hiyo ndiyo imekuwa inapelekea makampuni
makubwa kuanguka pale yanapokabiliana na changamoto. Yanakuwa yamejaa
watu ambao wana mtazamo mgando na wasio tayari kuweka juhudi.
Kama ambavyo tumeshajifunza, watu wenye mtazamo mgando huwa
hawakubali madhaifu yao na kujifunza, badala yake hukazana kuonesha uwezo
walionao. Hivyo kampuni iliyo na viongozi na wafanyakazi wenye mtazamo
mgando inaweza kufanikiwa kwa kiasi, lakini haiwezi kudumu kwenye

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

mafanikio hayo kwa muda mrefu. Hiyo ni kwa sababu watu hawajifunzi wala
kuweka juhudi ili kuwa bora zaidi.
Kampuni yoyote ambayo haiwezi kukubali makosa yake na kuyarekebisha,
haiwezi kudumu muda mrefu.

Uongozi na mafanikio.
Kwenye kitabu cha Good to Great kilichoandikwa na Jim Collins alilinganisha
makampuni ambayo yameweza kufikia mafanikio makubwa na yale
yaliyoshindwa, kisha kuja na vitu vinavyotofautisha makampuni hayo. Kimoja
kikubwa kilikuwa ni uongozi.
Uongozi wa kampuni zilizofanikiwa ulikuwa tofauti kabisa na wa kampuni
zilizoshindwa. Kwenye kampuni zilizoshindwa, kiongozi ndiyo alikuwa kila kitu,
alionekana ni anayejua kila kitu na kila mtu kumsujudu. Aina hiyo ya uongozi
iliamini zaidi kwenye vipaji kuliko juhudi. Hivyo kilichotokea ni kampuni
kushindwa kukabiliana na changamoto na kufa.
Kwenye kampuni zilizofanikiwa, kiongozi hakuwa kila kitu, hakuonekana kuwa
anajua kila kitu na hivyo alizungukwa na washauri wazuri, ambao aliwaamini.
Waliamini kwenye juhudi kuliko vipaji na hivyo waliajiri watu kwa kigezo cha
juhudi na siyo kipaji.
Kwa mtazamo wa nje, viongozi wa kampuni zilizoshindwa walionekana wana
mafanikio makubwa, kwa sababu wanakuwa wamejijengea sifa kubwa, lakini
kampuni zao ziliishia kuanguka. Huku viongozi wa kampuni zilizofanikiwa
wakionekana ni wa kawaida kwa sababu hawajengi sana sifa zao, lakini
kampuni zao zilifanikiwa sana.
Kwa tabia hizo tu, tunaona wazi madhara ya mtazamo kwenye uongozi na
mafanikio. Kampuni zinazofanikiwa zina viongozi wenye mtazamo wa ukuaji,
huku kampuni zinazoshindwa zikiwa na viongozi wenye mtazamo mgando.
Kwenye kitabu cha Collins, ameonesha zaidi tabia hizo, mfano kwenye
makampuni yanayoshindwa, viongozi huwa wanajiona wako juu ya kila mtu
kwenye kampuni, huwa wanachukua mafanikio ya wengine na kuyafanya kuwa
yao na huwashusha wengine ili kuonesha mamlaka waliyonayo. Lakini kwenye
kampuni zilizofanikiwa hali ni tofauti kabisa, viongozi hawajioni wakiwa juu ya
kila mtu, kwani huheshimu na kujali michango ya wengine, hawachukui
mafanikio ya wengine na kuyafanya yao na hawakazani kuwashusha wengine ili
waonekane wako juu.
JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Hapa tunaona jinsi mtazamo ulivyo na nguvu, wenye mtazamo mgando


wanaamini uwezo wao una ukomo na hivyo hawapo tayari kuwapa wengine
nafasi. Lakini wenye mtazamo wa ukuaji wanajua uwezo hauna ukomo, juhudi
zinaweza kuongeza uwezo na hivyo wanakuwa tayari kuwapa wengine nafasi
bila kuona ni hatari kwao.
Viongozi wenye mtazamo mgando hupenda kuzungukwa na watu
wanaowatukuza na wasiowakosoa kwa namna yoyote ile, hivyo hata
wanapokosea, hakuna anayewaambia na hilo huwapeleka kwenye matatizo
makubwa.
Viongozi wenye mtazamo wa ukuaji hupenda kuzungukwa na watu wanaoweza
kuwahoji na kuwakosoa, hilo linawafanya waone mapema pale wanapokosea
na kuweza kurekebisha kabla tatizo halijawa kubwa.
Viongozi wenye mtazamo mgando huwa wanajenga kampuni
zinazowategemea wao kwa kila kitu, hivyo hata kampuni hizo zinapofanikiwa,
huwa haziwezi kudumu kwenye mafanikio hayo kwa muda kwa sababu hazikui.
Na pale inapotokea kiongozi hayupo, basi kampuni inaanguka kwa sababu
haijaengwa kwenye misingi ya kuweza kwenda bila ya kiongozi husika.
Viongozi wenye mtazamo wa ukuaji huwa wanajenga kampuni ambazo
haziwategemei kwa kila kitu. Wanaweka misingi sahihi ya kuiwezesha kampuni
kuendelea hata kama wao hawapo, hivyo mafanikio yanayopatikana huwa
yanadumu, hata pale kiongozi anapoondoka.
Viongozi wenye mtazamo mgando huwa wanajali sifa zao binafsi na huzilinda
hata kama kampuni inaingia kwenye matatizo. Viongozi wenye mtazamo wa
ukuaji huweka maslahi ya kampuni mbele na siyo sifa zao binafsi.
Viongozi wenye mtazamo wa ukuaji huwa wanatengeneza timu bora
inayowazunguka na wanawaendeleza viongozi wengine kuwa bora zaidi na
kuweza kuendesha kampuni hata kama wao hawapo.
Viongozi wenye mtazamo mgando huwa hawatengenezi timu inayojitegemea,
badala yake hujiona wana kipaji na uwezo mkubwa hivyo hawahitaji timu,
wanachohitaji ni watu wa kuwasaidia kutimiza maono yao. Huwa hawaendelezi
wengine kuwa viongozi wazuri. Kwa njia hiyo wanajenga kampuni ambayo
haiwezi kuendelea bila uwepo wao, na hata wanapoendelea kuwepo, bado
kampuni haiwezi kufanya vizuri kwa sababu haipati mchango bora kutoka kwa
wengine.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Mfano wa mtazamo mgando na madhara yake.


Mwandishi anatupa mfano wa kiongozi wa kampuni kubwa ambaye alikuwa na
mtazamo mgando na ambao ulipelekea kampuni yake kufa licha ya kufanya
vizuri awali.
Mfano huo ni wa Lee Iacocca aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya
magari ya Chrysler Motors. Kabla ya kwenda kampuni ya Chrysler, Iacocca
alikuwa kwenye kampuni ya magari ya Ford na aliweza kufanya makubwa
kwenye kampuni hiyo. Alitegemea angepata nafasi ya kuwa mtendaji mkuu,
lakini hakupewa na baadaye akaondolewa kabisa kwenye kampuni hiyo.
Kwa hasira alienda kwenye kampuni shindani ya Chrysler na kuweka juhudi
kubwa. Alipofika alikuta kampuni hiyo ikiwa kwenye changamoto kubwa na
ikikaribia kufilisika. Lakini yeye aliweka juhudi kubwa na kuiokoa kampuni hiyo.
Aliajiri watu wapya na kuja na aina mpya za magari huku akihakikisha kampuni
inapata fedha za kujiendesha. Ndani ya muda mfupi hali ya kampuni ilibadilika,
ikatoka kwenye kuelekea kufa na kuanza kwenda vizuri.
Haikuchukua muda, kampuni ya Chrysler ilianza kuingia tena kwenye matatizo
na sasa yalikuwa matatizo makubwa zaidi. Matatizo hayo yalitokana na
mtazamo mgando aliokuwa nao Iacocca.
Baada ya kufikia mafanikio ya awali ya kuiokoa kampuni, Iacocca alitumia
muda mwingi kwenye mambo yanayojenga sifa na jina lake kuliko yale
yanayoijenga kampuni. Hivyo sifa yake ilizidi kukua huku kampuni ikiwa
inaingia kwenye matatizo.
Wakati soko la magari likiwa kwenye ushindani mkali kutokana na ujio wa
magari ya Japan, kampuni ya Chrysler ilifanya utafiti wa kina na kuja na
mapendekezo ya namna bora ya kukabiliana na ushindani huo, kwa kuja na
aina bora zaidi za magari yanayoweza kushindana na magari ya Japan sokoni.
Lakini Iacocca hakukubaliana na mapendekezo hayo, aliendelea kusisitiza
kampuni izalishe magari ambayo tayari yapo sokoni.
Iacocca alitupa lawama zake kwenye magari ya Japan na kuitaka serikali ya
Marekani kutoza kodi kubwa kwenye magari hayo ili yasiendelee kuteka soko
la Marekani. Iacocca alishauriwa mara nyingi kwamba suluhisho siyo kuzuia
magari ya Japan, bali kutengeneza magari bora yanayoweza kushindana na
hayo ya Japan sokoni. Lakini mtazamo wake mgando haukuwa tayari kupokea
mapendekezo na ushauri huo.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Iacocca pia hakutengeneza timu ambayo ingeweza kumsaidia, aliwafukuza


wale wote waliomhoji na kumkosoa huku akishindwa kuwatambua na kuwajali
wale waliojituma kwa ajili ya kampuni. Alijali zaidi mambo yake binafsi na hata
wakati kampuni imeingia tena kwenye matatizo, bado aliendelea kujilipa kiasi
kikubwa huku wafanyakazi wakiwa kwenye hali ngumu.
Baada ya Iacocca kuonekana ni mzigo, bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya
Chrysler walimwondoa kwenye uongozi huku wakimpa marupurupu mazuri.
Kiongozi aliyemrithi aliendesha kampuni vizuri kitu kilichompa Iacocca wivu na
kuanza mikakati ya kumpindua. Mapinduzi yake yalishindwa na hilo likaweka
doa zaidi kwenye sifa yake. Kile alichokuwa anakazana kukijenga, yaani sifa
yake binafsi akaishia kuharibu kabisa.
Kilichopelekea Iacocca ashindwe licha ya kuanza vizuri ni mtazamo mgando. Ni
kweli alipenda biashara ya magari na alikuwa na mawazo mazuri yaliyoleta
matokeo makubwa, lakini alipenda kuonekana yeye ndiyo kila kitu na
kuzungukwa na watu wanaomtukuza, kitu kilichopelekea anguko lake. Na hata
pale mtazamo wake mgando ulipokuwa kikwazo kwake bado hakukubali
makosa yake, badala yake alitoa lawama kwa wengine.
Iacocca alipatwa na ugonjwa ambao mwandishi anauita CEO disease ambapo
mkurugenzi anatengeneza kampuni inayowatukuza badala ya kukua yenyewe.
Anazungukwa na watu wanaomsifia na kukubaliana naye kuliko wanaomkosoa
na kumwonesha madhaifu yake. Hii ni sifa kubwa ya wenye mtazamo mgando.

Akili kubwa inapokuwa kikwazo.


Kwa mifano na tafiti nyingi mwandishi anatuonesha kwamba pale kiongozi wa
juu wa kampuni anapokuwa na akili kubwa, basi huwa ni kikwazo kwenye
ukuaji wa kampuni.
Wengi wenye sifa hiyo huwa na mtazamo mgando, kwa kujiona wanajua kuliko
wengine na hivyo kutokusikiliza au kupokea ushauri.
Pia kwa akili kubwa wanayokuwa nayo, wale wanaowazunguka huwa
wanawaogopa na kuhofia kutoa mapendekezo yao kwa kuwa yataonekana siyo
ya maana.
Hali hiyo huchochea mtazamo mgando wa viongozi na kushindwa kuona kile
wanachopaswa kuona.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Viongozi wa aina hii hutumia muda na nguvu kubwa kujenga sifa zao kuliko
kujenga kampuni. Na pia huwa tayari kuua kampuni kulinda sifa zao, kuliko
kuweka pembeni sifa zao na kuisaidia kampuni kukua.

Siyo kwa makusudi.


Ukiangalia viongozi wote ambao wameangusha kampuni ambazo walikuwa
wanaziongoza, kwa nje unaweza kufikiri walifanya kwa makusudi. Lakini
unapoangalia kwa ndani unagundua siyo makusudi, ila tu wanashindwa kujua
udhaifu wao ambao ni mtazamo mgando.
Viongozi wote wanaanza wakiwa na nia njema, ya kuiwezesha kampuni
kufanikiwa na kufanya makubwa. Wanakuwa ni watu wenye uwezo mzuri na
walishaonesha mafanikio kwenye nafasi nyingine za chini walizokuwa nazo.
Kwa nafasi hizo za chini, waliweza kufanya vizuri kwa sababu maamuzi yao
hayakuwa ya mwisho. Wanapokuja kupewa uongozi mkuu na maamuzi yao
kuwa ndiyo ya mwisho, ndipo udhaifu walionao unapokuwa kikwazo kwao.
Viongozi hao wanajikuta njia panda inayowataka kufanya maamuzi muhimu
kwa ajili ya kampuni, hujikuta wakifanya maamuzi yanayotunza sifa zao badala
ya yale yanayoiwezesha kampuni kukua zaidi.
Wanapojikuta kwenye changamoto, badala ya kuzitatua wanalalamika na
kulaumu wengine, wanatafuta njia za mkato za kuondokana na matatizo hayo
au kuyaficha, kitu ambacho huzalisha matatizo zaidi.
Viongozi hao wanakuwa kwenye sekta yenye ushindani mkali, lakini wao
wanaishi kwenye dunia yao ya kipekee, inayotukuza sifa zao na kuwaona wao
ndiyo kila kitu. Kwa mtazamo wao na nafasi wanayokuwa nayo wanaona
hawawezi kushindwa, huwa wanaona wanastahili kupewa sifa kwa makubwa
waliyofanya na nafasi waliyonayo.
Kwa udhaifu walionao, wanajikuta wakifanya mambo mengi ya kutunza sifa
zao na siyo ya kukuza kampuni. Sifa zao zinawapa upofu wasione kampuni
ikianguka, huku wale wanaowazunguka wakiwa hawana msaada kwa sababu
wametengenezwa kusifia, kusikiliza na kufuata maagizo na siyo kushauri kilicho
sahihi.
Kwa kuwa na mamlaka makubwa kwenye nafasi zao, viongozi hao hujikuta
wanayatumia vibaya kitu kinachopelekea kushindwa zaidi. Wengi hujiona kama
wafalme kwenye kampuni zao na wengine kwenye kampuni hizo wakiwa

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

watumishi wao. Wale walio chini yao na hujifunza njia bora ya kwenda nao na
kuwa watu wa kujipendekeza ili wasifukuzwe, kitu kinachoficha matatizo na
kuyapa nafasi ya kukua zaidi.

Madhara ya mtazamo wa kiongozi.


Kutokana na mtazamo mgando ambao kiongozi anakuwa nao, watu
wanajifunza jinsi ya kwenda naye ili wasipate changamoto. Kwa njia hiyo, wale
wanaomzunguka wanakuwa watu wa kusifu na kujipendekeza. Na wale ambao
hawaendi kama kiongozi anavyoenda huishia kufukuzwa au kuondoka
wenyewe.
Kwa namna hii kampuni nzima inakuwa na mtazamo na madhaifu kama
aliyonayo kiongozi na hilo ndiyo linapelekea kampuni kushindwa.
Badala ya watu kujifunza na kuweka juhudi ili kampuni iweze kupiga hatua, kila
mtu anaanza kufikiria ni jinsi gani atamfurahisha kiongozi ili asiingie kwenye
matatizo. Hali hiyo huanzia kwa kiongozi na baadaye kusambaa kwa kila mtu
kwenye kampuni.
Hali hii hupelekea uthubutu na ubunifu kuondoka kwenye kampuni na hivyo
kukosa nguvu ya kushindana na makampuni mengine.
Kwa viongozi wenye mtazamo wa ukuaji, mambo ni tofauti kabisa, eneo la kazi
linakuwa sehemu ya kujifunza na kukua zaidi. Watu wanapewa nafasi
kulingana na mchango wao na siyo kujipendekeza. Mawazo mbadala
yanapewa nafasi na kujaribiwa, kitu kinacholeta uthubutu na ubunifu kwenye
kampuni. Kila mtu anafurahia kile anachofanya na kampuni inanufaika.
Kiongozi mwenye mtazamo wa ukuaji anaifanya kampuni nayo kuwa na
mtazamo wa ukuaji na hilo linafanya kampuni ifanikiwe. Kiongozi mwenye
mtazamo mgando anaifanya kampuni iwe na mtazamo mgando na kupelekea
kampuni kushindwa.

Mfano wa mtazamo wa ukuaji kwenye uongozi.


Mwandishi anatupa mfano mwingine wa kiongozi aliyekuwa na mtazamo wa
ukuaji na ambao uliweza kusaidia kampuni yake kufanya vizuri.
Kiongozi huyo ni Jack Welch aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya
General Electric. Licha ya mafanikio makubwa ambayo Welch aliyapata,
hakuwahi kulewa sifa na kuacha kupambana ili kampuni yake ifanikiwe zaidi.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Wakati anachukua nafasi ya uongozi wa kampuni, ilikuwa kwenye hali mbaya


na mtazamo mgando. Lakini alifanya mabadiliko makubwa na kuondoa
mtazamo mgando na kujenga utamaduni wa ukuaji na ushirikiano kama timu.
Welch aliweka kipaumbele kwenye ukuaji wa watu, kuanzia kwake binafsi na
kwa wafanyakazi wote wa kampuni. Alitambua udhaifu aliokuwa nao na
aliufanyia kazi ili usiwe kikwazo kwake na kwa kampuni pia.
Welch aliwatambua na kuwathamini wafanyakazi ambao walifanya vizuri na
kuisaidia kampuni na hilo lilitengeneza mazingira ya wengine nao kujitoa ili
kampuni ipige hatua zaidi.
Badala ya kuwa mtu wa lawama kama walivyo viongozi wenye mtazamo
mgando, yeye alikuwa mtu wa shukrani.
Welch hakujipa sifa za mafanikio ya kampuni yeye binafsi, bali alipeleka sifa
hizo kwa wafanyakazi wake, ambao aliwaita mashujaa walioiwezesha kampuni
kufanikiwa.
Hapo tunaona jinsi viongozi wenye mtazamo wa ukuaji walivyo tofauti kabisa
na wale wenye mtazamo mgando.

Kufuata mkumbo.
Kuna hali huwa zinajitokea kwenye kundi ambapo watu wanakuwa wanafikiria
kitu kimoja, hakuna anayehoji wala kukosoa pale mambo yanapoonekana
hayaendi vizuri. Wanasaikolojia wanaita hali hii groupthink na imekuwa chanzo
cha matatizo makubwa kwenye taasisi nyingi.
Kufikiri kwa kufuata mkumbo huwa kunachochewa zaidi na mtazamo mgando.
Pale taasisi inapokuwa na kiongozi ambaye anachukuliwa kuwa na uwezo
mkubwa na kuwa mwenye mtazamo mgando, kila mtu anaweka imani yake
kwa kiongozi huyo na kuona kila analofanya kuwa sahihi.
Mwandishi anatupa mfano wa jinsi hali hii ya kufikiri kwa kufuata mkumbo
ilivyowahi kuwa na madhara kwenye uvamizi wa siri uliopangwa na Marekani
ili kumpindua Castro wa Cuba (Bay of Pigs invasion).
Hilo lilikuwa tukio la kushindwa kwa aibu kwa taifa hilo kubwa dhidi ya taifa
dogo na uchunguzi unaonesha kilichopelekea uvamizi huo kushindwa ni watu
kuacha kufikiria kwa usahihi na kufuata mkumbo.
Chanzo kikuu cha kushindwa kwa uvamizi huo ilikuwa ni kiongozi wa wakati
huo, Rais Kennedy ambaye alikuwa amejijengea sifa ya kufanya mambo mengi
JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

kwa usahihi. Watu walimwamini sana na kuona ana maono makubwa na yaliyo
sahihi, ambayo hayapaswi kuhojiwa wala kukosolewa.
Hivyo alipopendekeza uvamizi wa Cuba, japo mpango haukuwa sahihi,
washauri wake wote walikubaliana naye. Yeye alifikiri wanakubaliana naye kwa
sababu mpango ni sahihi, kumbe wanakubaliana naye kwa sababu ya imani
waliyonayo kwake.
Kilichotokea ni uvamizi kushindwa vibaya kwa sababu ya watu kufuata
mkumbo kwenye kufikiri.
Mwandishi anatushirikisha kiongozi mwingine ambaye alijua madhara ya
kufikiri kwa mkumbo na kuzuia hali hiyo isiwe kikwazo kwake. Huyu alikuwa
waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill, ambaye alitengeneza kitengo
maalumu ambacho kazi yake ilikuwa kumpa habari zote mbaya na kuonesha
madhaifu na makosa ya kila mpango.
Kwa kuwa na watu aliowapa kazi hiyo, Churchill alijua kila kinachoendelea kwa
uhalisia wake na siyo kwa kudanganywa na wale wanaojipendekeza kwake.

Tukutane tukiwa tumelewa.


Changamoto ya kufuata mkumbo haijaanza leo, tangu enzi na enzi imekuwa
ndiyo chanzo cha mambo mengi kushindwa, hasa vita au mapambano makali.
Maandiko ya Herodotus ya karne ya tano kabla ya Kristo alieleza kwamba watu
wa Persia walikuwa na njia ya kuepuka madhara ya kufikiri kwa mkumbo.
Kila walipofikia maamuzi wakiwa na akili timamu, walikubaliana kwenda
kulewa kwanza, kisha kuja kuyajadili tena maamuzi hayo.
Kwa njia hii, waliweza kuona udhaifu wa maamuzi hayo, maana wengi
wakishalewa huwa wanaondoa aibu na kuongea ukweli ulio ndani yao.
Njia bora ya kutumia kuepuka kufikiri kama kundi kwenye zama zetu ni kujenga
mtazamo wa ukuaji kwa watu wote. Pale watu wanapokuwa na mtazamo wa
ukuaji, wanaona wazi madhaifu na kuyafanyia kazi.
Kwenye mazingira ya myazamo wa ukuaji, kiongozi naacha kuonekana kama
mungu asiyekosea na badala yake anaangaliwa kama binadamu mwenye
madhaifu yake. Hiyo inawapa watu nafasi ya kuhoji na kuangalia udhaifu uliopo
kwenye kila mpango kabla haujatekelezwa.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Lakini pia mazingira ya mtazamo wa ukuaji yanawafanya watu kuwa huru


kuomba msaada kwa wengine na kujifunza na kutokuona aibu kuuliza kile
wasichojua au ambacho hawana uhakika nacho.
Mtazamo wa ukuaji unakuwa na manufaa kwa kiongozi na hata wafuasi wake,
kwa sababu wote wanakuwa wazi na huru kujifunza na kuchukua hatua sahihi
kufanikiwa. Hawafanyi ili kulinda sifa zao, bali wanafanya ili kupiga hatua zaidi.

Motisha kwa wafanyakazi.


Viongozi wamekuwa wanatafuta njia ya kuwapa motisha wafanyakazi wao,
lakini njia nyingi zilizozoeleka zimekuwa hazileti matokeo mazuri.
Kumekuwa na njia ya kutoa zawadi kwa mfanyakazi bora, lakini bado hiyo
imekuwa haitoi motisha ya kutosha kwa wengi kwa sababu inachochea
mtazamo mgando.
Wale wanaopata zawadi hiyo wanajiona wana uwezo au kipaji fulani huku
wanaokosa wakijiona hawawezi.
Viongozi pia wamekuwa wanatafuta wataalamu wa kutoa mafunzo kwa
wafanyakazi wao ili wawe na hamasa ya kujituma kwenye majukumu yao,
lakini hamasa hizo zimekuwa zinadumu kwa muda mfupi tu.
Njia nyingi za kutoa motisha kwa wafanyakazi zimekuwa hazifanyi kazi kwa
sababu ya mtazamo mgando ambao unakuwa unaanzia kwa viongozi.
Wengi huwa wameshawagawa kabisa wafanyakazi kwenye kundi la wenye
uwezo na wasio na uwezo. Wakishawagawa wafanyakazi hivyo, wanakuwa
hawana imani kwamba wasio na uwezo wanaweza kubadilika na kufanya
makubwa.
Kwa mtazamo huo hawajisumbui kuwashauri na hata kuwafundisha na
kuwafuatilia kwa ukaribu, kwa sababu wamekata tamaa na watu hao. Na kwa
wale wenye uwezo pia hawawasaidii kupiga hatua zaidi. Hali hiyo inawaharibu
wote, wenye uwezo na wasio na uwezo.
Njia ya kuondokana na hili ni kwa viongozi kuanza kwa kuwa na mtazamo wa
ukuaji, badala ya kuona uwezo wa wafanyakazi wao kuwa wenye ukomo,
waone kwamba uwezo huo unaweza kuboreshwa zaidi, iwapo watapata
mafunzo sahihi na kufuatiliwa kwa karibu.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Uzuri ni kwamba mtazamo wa ukuaji unaweza kufundishwa kwa yeyote, hivyo


kuanzia kiongozi anaweza kujifunza na kuwa na mtazamo wa ukuaji na kisha
kulipeleka hilo kwa wafanyakazi wake.
Mwandishi anatushirikisha mafunzo yaliyowahi kutolewa kwa viongozi ili
kuwasaidia kubadili mtazamo wao na wa wafanyakazi wao pia. Mafunzo hayo
yaliweka msisitizo kwenye maeneo manne;
Moja ni kujua kwamba uwezo wa mtu hauna ukomo, unaweza kuendelezwa.
Mbili ni kufikiria maeneo ambayo walikuwa na uwezo mdogo ila wameweza
kuukuza.
Tatu ni kuangalia wafanyakazi wao na kuona maeneo gani wanaweza
kuyaboresha kisha kuwaandikia namna ya kuwa bora kwenye maeneo hayo.
Nne ni kukumbuka nyakati ambazo waliamini watu hawawezi kufanya vitu
fulani ila wakaweza.
Kwa kufanya mambo hayo manne, viongozi waliweza kubadili mtazamo wao na
kuwasaidia wafanyakazi wao kujiendeleza na kukuza uwezo wao. Baada ya
mafunzo, viongozi hao walishuhudia mabadiliko makubwa kwao wenyewe na
kwa wafanyakazi wao pia.
Walikuwa tayari kuwafundisha na kuwaongoza wafanyakazi wote na waliweza
kuona jinsi wafanyakazi walivyokuwa tayari kujifunza na kuweka juhudi kukua
zaidi.
Kwa zoezi hili, tunajifunza haya muhimu;
Kwanza ni mafanikio ya kampuni hayategemei kupata na kuajiri watu wenye
vipaji, bali kupata watu wenye mtazamo wa ukuaji na kuwasaidia kukua zaidi
kupitia mafunzo na hamasa.
Mbili ni mtazamo wa ukuaji ni hitaji la kwanza kwa kiongozi na watu wake ili
kampuni iweze kufanikiwa.

Jinsi ya kujenga mazingira yanayochochea mtazamo wa ukuaji.


Ili kujenga mazingira yanayochochea mtazamo wa ukuaji kwenye kampuni au
taasisi yoyote, kila kiongozi anapaswa kufanya yafuatayo;
1. Kuweka ujuzi kama kitu ambacho mtu anaweza kujifunza na kuwa bora zaidi.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

2. Kuweka utayari wa kujifunza na uvumilivu kuwa msingi mkuu wa taasisi


badala ya kuangalia tu vipaji.
3. Watu kupewa mrejesho unaowaonesha namna wanavyoweza kujifunza na
kuwa bora zaidi na siyo kuwakatisha tamaa kwamba hawawezi.
4. Viongozi kuwa chanzo cha kujifunza kwa wale walio chini yao.
Kazi ya kitengo cha rasilimali watu kwenye taasisi yoyote ni kuamini kwamba
uwezo wa watu unaweza kukuzwa zaidi na kuwasaidia kwenye hilo. Hiyo ndiyo
njia pekee kampuni inaweza kukua na kufanikiwa zaidi.

Viongozi wanazaliwa au kutengenezwa?


Kumekuwepo na mvutano kwa miaka mingi iwapo viongozi wazuri wanazaliwa
au kutengenezwa yaani kulelewa kuwa viongozi. Wengi waliamini kuna watu
wanazaliwa wakiwa na kipaji cha uongozi na ambaye hana hicho basi hawezi
kuwa kiongozi mzuri.
Lakini kwa tuliyojifunza mpaka sasa kuhusu mtazamo, tunaona wazi kwamba
viongozi wazuri siyo tu wanatengenezwa bali pia wanajitengeneza wenyewe.
Pamoja na malezi wanayoweza kupata na kuwajenga kama viongozi, kwa
sehemu kubwa wanakuwa wamejijenga wao wenyewe.
Na viongozi wote bora, wana mtazamo wa ukuaji na siyo mtazamo mgando.
Kwa mtazamo wao wa ukuaji wanakazana kuwa bora zaidi na hilo ndiyo
linawawezesha kuwa viongozi bora.
Kila kiongozi huwa anapata nafasi ya kujifunza kwenye kile anachofanya, lakini
baada ya kujua yale ya msingi, wengi huridhika na kufanya kazi zao kwa
mazoea. Hili linawazuia wasikue zaidi. Lakini wale wenye mtazamo wa ukuaji,
wanaojua wanaweza kuwa na kufanya zaidi, wanaendelea kujifunza na kuwa
bora zaidi.

Ifanye taasisi kuwa na mtazamo wa ukuaji.


Kama una biashara au kampuni yako au kama wewe ni kiongozi kwenye eneo
lako la kazi, unaweza kuwa bora zaidi kama utakuwa na mtazamo wa ukuaji na
hatimaye kufanya mtazamo wa taasisi nzima kuwa wa ukuaji.
Njia ya uhakika ya kufanya hivyo ni kuanzia kwenye kuajiri, badala ya kutafuta
vipaji, tafuta watu walio tayari kujiendeleza kisha wasaidie waweze
kujiendeleza. Watu hao hata kama wanaonekana wa kawaida mwanzoni, kiu
yao ya kujiendeleza itawasukuma kufanya makubwa zaidi.
JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Katika kusifia na kutoa zawadi kwa wafanyakazi, weka mkazo kwenye juhudi na
siyo uwezo au kipaji, pale mtu anapoonesha juhudi ambazo ni za tofauti,
atambuliwe na kupewa sifa au zawadi. Hilo litawafanya wengine nao kuwa
hivyo.
Pale taasisi inapokuwa ya mtazamo wa ukuaji, inapata manufaa mengi, baadhi
ni;
1. Wafanyakazi kuwa waaminifu zaidi kwa kampuni na kuwa tayari kujitoa kwa
maendeleo ya kampuni.
2. Wafanyakazi kumiliki kile wanachokifanya na hivyo kukifanya kwa ubora
zaidi.
3. Wafanyakazi kushirikiana vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
4. Wafanyakazi kukaa kwenye taasisi kwa muda mrefu, huku wakiendelea
kuwa bora hivyo taasisi haiingii gharama kuajiri watu wapya kila wakati.
5. Taasisi kupata viongozi wengi na wazuri kutoka ndani ya wafanyakazi wake.

Hatua za kuchukua.
Je eneo lako la kazi lina mtazamo wa ukuaji au mtazamo mgando? Je wale
wanaokuzunguka wanakuhukumu au kukusaidia uwe bora zaidi? Je wewe
mwenyewe umekuwa unajichukuliaje kwenye kazi zako? Unakua zaidi au
umeganda pale pale? Anza kwa kujijengea mtazamo wa ukuaji kuhusu kazi
yako na eneo lako la kazi, kwa kutumia fursa za kujifunza na kufanya kwa ubora
zaidi.
Kama wewe ni kiongozi kwenye eneo lako la kazi au biashara yako, je
unawachukuliaje wale walio chini yako? Je unawaona ni watu wenye uwezo
ulio na ukomo au watu wanaoweza kukua zaidi? Je huwa unapenda wakuone
uko juu na wao wako chini yako? Huwa unapokeaje pale aliye chini yako
anapokupinga au kukukosoa? Unaona anahatarisha nafasi yako? Kama
kiongozi, anza kujijengea mtazamo wa ukuaji ili uweze kuongoza watu wako
vizuri.
Angalia njia zipi unazoweza kutumia kuwaendeleza wafanyakazi wako. Angalia
kila mmoja na changamoto zake kisha weka mpango wa kumsaidia kuwa bora
zaidi.
Unaepukaje kufikiri kwa mkumbo kwenye eneo lako la kazi? Je watu wanatoa
maoni yao kwa kufikiri wenyewe au wanaungana na kile ambacho wengine
JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

wanafikiri? Tengeneza mpango mzuri wa kufanya maamuzi ambao utakuwa


huru kwa kila mtu kutoa mawazo yake na siyo kufuata kundi. Chagua watu
ambao watakuwa wanatafuta madhaifu na makosa kwenye kila maamuzi
yanayofanyika ili yaonekane mapema na kufanyiwa kazi. Kuwa na njia ya siri ya
kutoa maoni ambapo wale wenye mawazo mbadala wanaweza kuyatoa bila
kuwa kwenye hatari ya kukosolewa au kupingwa na wengine.

MAHUSIANO; MTAZAMO KWENYE MAPENZI.


Mahusiano ni eneo jingine ambalo limekuwa linaathiriwa sana na mtazamo
ambao watu walio kwenye mahusiano wanao. Kudumu au kuvunjika kwa
mahusiano kunategemea sana mtazamo ambao watu wanao.
Na kama tulivyojifunza mpaka sasa, mtazamo mgando ndiyo chanzo cha wengi
kushindwa. Na hata kwenye mahusiano, wale wanaoingia kwenye mahusiano
wakiwa na mtazamo mgando, mahusiano hayo huishia kuvunjika.
Lakini wale wanaoingia wakiwa na mtazamo wa ukuaji, mahusiano yao hukua
zaidi.
Wote tunajua hakuna mtu aliyekamilika, hivyo unapokuwa kwenye mahusiano
ya aina yoyote ile, yule unayejihusisha naye anakuwa hajakamilika, anakuwa na
mapungufu na changamoto wake.
Wale wenye mtazamo mgando, huona wale walionao kwenye mahusiano
hawawi kama wanavyotaka wao na hawapo tayari kwenda nao kama walivyo
na hilo hupelekea mahusiano kuwa na migogoro na kuvunjika.
Lakini wale wenye mtazamo wa ukuaji, huwa wanajua wenza wao wana
mapungufu yao lakini kwa kuwa wanajua kila mtu ana nafasi ya kuwa bora
zaidi, huwapa muda wa kujiboresha huku wakiwachukulia jinsi walivyo, hilo
hupelekea mahusiano kudumu na kuwa bora.
Hapa mwandishi anatushirikisha jinsi mtazamo unavyoathiri mahusiano na
hatua za kuchukua ili mahusiano yako yasiathiriwe na mtazamo ulionao.

Mtazamo mgando na kulipa kisasi.


Pale mahusiano yanapovunjika kwa sababu yoyote ile, wenye mtazamo
mgando huwa wanaona kama wamehukumiwa na kuchukuliwa kama watu
ambao hawafai na hawapendwi au kukubalika, hivyo kinachotokea ni wao
kutafuta njia za kulipa kisasi.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Watu hawa huwa hawawezi kuwasamehe wale walikuwa nao kwenye


mahusiano na yakavunjika, iwe ni ya kimapenzi, ndoa, kazi au biashara. Hujiona
wameumizwa na kuonewa hivyo nao hutafuta nafasi ya kulipa maumivu hayo
na kufanya hivyo pale fursa inapojitokeza.
Mwandishi anatushirikisha utafiti uliowahi kufanywa kwa wale waliotalikiana
na wenye mtazamo mgando, aligundua wengi walikuwa na nia ya kulipa visasi
kwa wenza wao. Mmoja alisema mwenza wake alimfanya ajione hana thamani
na kila siku anatafuta njia ya kumfanya alipe hilo. Mwingine akaeleza
akiambiwa achague yeye kuwa na furaha au mwenza aliyeachana naye awe na
maisha ya hovyo, atachagua mwenza huyo kuwa na maisha ya hovyo.
Tunaona jinsi mtazamo mgando ulivyo na nguvu na unavyoweza kuharibu
maisha ya mtu, anaona ni bora akose furaha lakini amuone mwingine akiteseka
kwa sababu tu hawakuweza kuendelea pamoja.

Mtazamo wa ukuaji na msamaha.


Kwa watu wenye mtazamo wa ukuaji, pale mahusiano yao yanaposhindwa na
kuvunika, lengo lao kuu huwa ni kusamehe. Hawa hujua njia sahihi kwao kuwa
na maisha bora ni kusamehe, hata kama wengine waliwakosea wao.
Kwenye utafiti, mmoja alisema; mimi siyo mtakatifu na hivyo najua kwa amani
ya akili yangu napaswa kusamehe na kusahau. Aliniumiza lakini bado nina
maisha ya kuishi, itakuwa ujinga kuacha kuishi maisha yajayo kwa kukumbuka
yaliyopita. Namtakia maisha yenye heri na mimi niwe na maisha yenye heri pia.
Kwa mtazamo huu wa ukuaji, watu huwa hawajioni kama wamehukumiwa na
kuwekwa kwenye kundi la wasiofaa au kupendwa. Kwa mtazamo huu
wanajifunza na wanapoingia kwenye mahusiano mengine, wanakuwa bora
zaidi. Hawabaki kuishi maisha ya nyuma, badala yake wanayapokea na kuyaishi
maisha yajayo.

Ubaya wa mtazamo mgando kwenye mahusiano.


Unapokuwa na mtazamo mgando halafu ukaingia kwenye mahusiano, hapo
unakuwa na mtazamo mgando kwenye vitu vitabu.
Kwanza kabisa unakuwa na mtazamo mgando kwako binafsi, kwa kuona uwezo
wako una ukomo na hauwezi kubadilika.
Pili unakuwa na mtazamo mgando kuhusu mwenza wako kwa kuona vile alivyo
ndivyo atakavyokuwa milele, hawezi kubadilika.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Tatu unakuwa na mtazamo mgando kuhusu mahusiano yenyewe, kwa kuona


jinsi yalivyo ndivyo yatakavyoendelea kuwa, hayawezi kubadilika na kuwa bora
zaidi.
Kwa njia hii, mtazamo mgando unakuwa ni mzigo mzito kwenye mahusiano.
Kwa wenye mtazamo mgando, mahusiano ni kama bahati, kama yataenda
vizuri basi yalipangwa kwenda vizuri, kama yatavunjika basi hayakupanga
kuwa.
Kwa namna hii wengi wenye mtazamo mgando huwa hawajifunzi hata pale
mahusiano yanapovunjika, kwa sababu wanaona siyo sababu yao, bali ni kitu
ambacho kilipangwa au hakikupangwa.
Utawasikia wengi wanasema, ilipangwa tuwe pamoja au haikupangwa tuwe
pamoja, hivyo ndivyo mtazamo mgando unawafanya wayachukulie mahusiano.
Kwa wenye mtazamo chanya, mambo huwa tofauti, kwa sababu huona wao
binafsi, wenza wao na mahusiano yao yanaweza kufanywa kuwa bora kuliko
yalivyo sasa.

Matatizo makuu ya mtazamo mgando kwenye mahusiano.


Mtazamo mgando huwa una matatizo makuu mawili kwenye mahusiano.
Tatizo la kwanza ni kuwazuia watu wasiweke juhudi kwenye kujenga
mahusiano yao. Wenye mtazamo mgando huwa wanaamini kama mahusiano
yamepangwa kuwepo, basi hayahitaji kazi, kama inabidi mtu aweke kazi
kujenga mahusiano hayo basi anayalazimisha. Wanaamini kwenye hadithi
zinazoishia na wakaishi kwa raha mustarehe, kwamba changamoto zozote
kwenye mahusiano ni kiashiria kwamba hayakupaswa kuwepo. Hili ndiyo
hupelekea wasiweze kudumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu.
Tatizo la pili ni kuwafanya watu waone tabia walizonazo watu hazibadiliki na
hivyo kuwa kikwazo kwa mafanikio. Pale inapotokea watu wanashindwa
kuelewana kwenye mahusiano, wenye mtazamo mgando huona ni kiashiria
kwamba mahusiano hayo hayawezekani, kwa sababu hakuna anayeweza
kubadilika. Inapotokea changamoto za mahusiano wenye mtazamo mgando
hutupa lawama kwa wenza wao au hata kwao wenyewe au kwa mahusiano
yenyewe. Lawama hizi ndizo zinazopelekea mahusiano kuvunjika, kwa sababu
mtu anakuwa hayupo tayari kuboresha mahusiano hayo. Pale wenye mtazamo
mgando wanapoona udhaifu wa wenza wao, hukata tamaa na kuona hakuna

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

namna mahusiano hayo yanaweza kwenda kwa hali hiyo, kwa sababu
hawaamini madhaifu hayo yanaweza kuboreshwa.

Mahusiano ni fungu la matatizo.


Mtaalamu wa mahusiano Daniel Wile anaeleza kwamba kuchagua mwenza
kwenye mahusiano ni kuchagua fungu la matatizo. Hakuna mtu ambaye hana
matatizo. Hivyo ili mahusiano ya dumu, ni kila mtu kujua matatizo na madhaifu
ya mwenzake na kukubaliana kujenga mahusiano ambayo hayataathiriwa na
vitu hivyo.
Mshauri wa mahusiano Aaron Beck huwa anawaambia wale wanaoenda kwake
kwa ajili ya ushauri wa mahusiano kamwe kutokuwa na fikra kwamba wenza
wao hawawezi kubadilika, kwa sababu fikra hizo ndizo zinazovunja mahusiano.
Pamoja na mtazama wa ukuaji kumfanya mtu aamini mwenza wake anaweza
kuwa bora zaidi ya alivyo sasa, haimaanishi anaweza kumlazimisha mwenza
wake kubadilika. Bali mwenza anapaswa kutaka kubadilika yeye mwenyewe,
kuamua kweli kwamba atabadilika na kuchukua hatua za mabadiliko.
Kitu kikubwa cha kuepuka kwenye mahusiano ni kupeleka lawama kwa
mwenza wako pale mahusiano yanapokuwa na changamoto. Badala yake
mnapaswa kulielewa tatizo linalopelekea changamoto hizo na kwa pamoja
kusaidiana kutatua tatizo hilo ili kuondoa changamoto hizo za mahusiano.

Mahusiano ya urafiki.
Mahusiano ya urafiki ni mahali ambapo watu hupata nafasi ya kusukumwa ili
kuwa bora zaidi na pia kusifiwa kwa hatua nzuri wanazopiga.
Marafiki wanapeana ushauri mzuri wa hatua sahihi za kuchukua na pia
wanasifiana kwa yale matokeo ambayo mtu ameyapata.
Ili mahusiano ya urafiki yawe bora, sifa zinapaswa kutolewa kwenye juhudi
ambazo mtu ameweka na siyo kwa uwezo ambao anao. Kama tulivyoona, mtu
anaposifiwa kwa juhudi anaendelea kuweka juhudi zaidi. Lakini akisifiwa kwa
uwezo, anaona uwezo huo una ukomo.
Mahusiano ya urafiki yanaathiriwa sana na mtazamo mgando ambapo marafiki
huwasifia wenzao ili tu kutokuwaumiza na hilo limekuwa haliwasaidii.
Ushauri maarufu kwenye mahusiano ya kirafiki umekuwa huu; utawajua
marafiki zako wa kweli unapokuwa na shida. Na hii ni kweli, wale

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

watakaosimama na wewe wakati wa matatizo, ni wale waliojitoa kweli kwa ajili


yako.
Lakini ipo njia nyingine ya kuhiji urafiki wa kweli, na njia hiyo ni wakati mambo
yako ni mazuri, je marafiki zako watafutahia hilo? Unaweza kuwa na marafiki
ambao wanakuwa na wewe wakati una shida, lakini unapofanikia kuliko wao
wanapatwa na wivu na hilo kupelekea mahusiano yenu kuharibika.
Hivyo unapowapima marafiki, usiangalie tu wakati una shida, bali pia angalia
wakati ambao umefanikiwa kuliko wao, je bado watafurahia na kuwa pamoja
na wewe?
Mtazamo wa ukuaji utakusaidia sana kwenye mahusiano ya urafiki, kwanza
utakuwezesha kuwa na marafiki zako pale wanapokuwa na matatizo ukijua
wanaweza kuwa bora zaidi. Na hata pale wanapofanikiwa kuliko wewe,
hutaumia kwa sababu unajua hata wewe utafanikiwa pia.
Kadhalika kwa wewe kuwa na mtazamo wa ukuaji, unawavutia marafiki ambao
pia wana mtazamo wa ukuaji.

Uonevu kwenye mahusiano (Bullying)


Mahusiano mengi, hasa ya watoto mashuleni huwa yamejawa na uonevu.
Huwa kunakuwa na wale wanaojiona ni muhimu zaidi na wanaowaangalia
wengine kama ambao siyo wa muhimu na kuwaonea.
Kinachopelekea watu kuwaonea wengine ni mtazamo mgando. Mtazamo huo
unawafanya wajione wao wako juu ya wengine na hivyo wanapoona kuna mtu
mwingine anayeweza kuwa juu kuliko wao, wanamuonea ili asiwe juu. Lengo ni
kuwashusha wengine ili wao wabaki juu.
Kwa kuwaonea wengine, mtu anajiona yuko juu yao na hilo linamlisha hitaji
lake la kuthibitisha kwamba uwezo wake ni wa juu kuliko wa wengine.
Kitu kingine anachopata waoneaji ni sifa kutoka kwa wengine, kwa kuonea
wengine, huwa wanasifika na kuogopwa na wengi, kitu kinachothibitisha
uwezo wao na kuwafanya wajisikie vizuri.
Mtazamo mgando pia una athari zaidi kwa wale wanaoonewa. Wale
wanaoonewa na wenye mtazamo mgando, huwa hupanga namna ya kulipa
kisasi kwa wale wanaowaonea. Na hili hufanya mahusiano yazidi kuwa
mabovu.

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

Na wale wanaoonewa na kujenga roho ya kulipa visasi, ndiyo ambao huja


kufanya matukio mabaya kwa wengine.
Wale wenye mtazamo wa ukuaji wanapoonewa, huwa wanajua tatizo siyo lao,
bali la wale wanaowaonea. Kwa njia hiyo hujua nana bora ya kuepuka
mahusiano yenye uonevu na kuondokana na matatizo zaidi.
Wenye mtazamo mgando huwa wanawanyanyasa wengine, na wale wenye
mtazamo mgando wanaponyanyaswa huwa wanapanga kulipa kisasi, hali hiyo
huwapelekea kuwa na sonona na hata kujiua au kusababisha machafuko zaidi.
Kuondokana na hali hizi za uonevu kwenye mahusiano, kwa watoto ni
kuwajengea mtazamo wa ukuaji, wale wanaoonea wanapokuwa na mtazamo
wa ukuaji, wanaona kuna njia nyingi za kupata sifa badala ya kuonea wengine.
Pia wale wanaoonewa wanapokuwa na mtazamo wa ukuaji, hawachukulii
uonevu huo kama tatizo lao binafsi, bali tatizo la wale wanaowaonea. Kwa
watu wazima, ni kuepuka mahusiano na wale ambao ni waonevu hasa
wanapokuwa na mtazamo mgando na kutokuwa tayari kubadilika wao
wenyewe.

Hatua za kuchukua.
Unajisikiaje pale unapokataliwa na wengine au mahusiano kuvunjika? Je huwa
unaona kama umeumizwa sana na kupanga kulipa kisasi? Au unakuwa tayari
kusamehe, kusahau na kusonga mbele huku ukijifunza na kuwa bora zaidi?
Kumbuka mahusiano uliyowahi kuwa nayo na yakavunjika na kukuumiza sana,
fikiria ulichukuliaje hali hiyo kipindi inatokea, kwa mtazamo mgando au
mtazamo wa ukuaji? Jiulize sasa ni kipi ulijifunza kwenye mahusiano hayo. Na
kama bado hujamsamehe yeyote ambaye mahusiano yenu yamewahi
kuvunjika, chukua hatua ya kuwasamehe sasa na kujifunza ili kuwa bora zaidi
kwenye mahusiano yako mengine.
Tengeneza picha ya mahusiano bora ya kimapenzi kwako, unapenda yaweje?
Je unapenda mahusiano ambayo mnaendana na kukubaliana kwa kila kitu,
mahusiano ambayo hayahitaji kuweka kazi ili kuyajenga? Kama hii ndiyo picha
uliyonayo basi tambua una mtazamo mgando kwenye mahusiano. Badilika na
kuwa na mtazamo wa ukuaji, ukijua kila mahusiano yana changamoto zake na
ili yawe bora lazima kazi iwekwe.
Inapotokea changamoto kwenye mahusiano, huwa unakimbilia kutoa lawama?
Hicho ni kiashiria cha mtazamo mgando, acha sasa kutoa lawama na angalia

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007
SOMA VITABU TANZANIA WWW.T.ME/SOMAVITABUTANZANIA

tatizo liko wapi na hatua gani za kuchukua kwa pamoja ili kuondokana na
changamoto hiyo.
Je umewahi kuwa kwenye mahusiano ambayo ulikuwa unaonewa? Je
ulichukuliaje hali hiyo, uliona unastahili na kupanga kulipa kisasi au uliona
anayekuonea ana matatizo yake binafsi? Kuanzia sasa, pale mtu mwingine
anapokuonea bila sababu yoyote, jua ana matatizo yake binafsi na kubwa
kabisa ni mtazamo mgando alionao, hivyo epuka kabisa watu wa aina hiyo.
Huu ni mwisho wa sehemu ya pili ya uchambuzi wa kitabu cha MINDSET
ambapo tumeona madhara ya mtazamo kwenye michezo, uongozi na
mahusiano. Kwenye sehemu ya tatu tunaona jinsi mtazamo unavyojengwa
tangu utotoni na jinsi ya kubadili mtazamo wako kwa hapo ulipo sasa. Usikose
uchambuzi huo wa sehemu ya tatu na ya mwisho ya kitabu hiki.
Umejifunza mambo muhimu sana kupitia uchambuzi huu wa kitabu. Sasa kazi
ni kwako kwenda kuyaweka kwenye matendo ili uweze kupiga hatua na
kufanikiwa kwenye maisha yako.
Kuendelea kupata chambuzi za kina za vitabu na vitabu vilivyochambuliwa,
jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, kwa kufungua
www.t.me/somavitabutanzania
Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na
mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na
upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua;
https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

JIUNGE KUPATA UCHAMBUZI WA VITABU TUMA UJUMBE KWA TELEGRAM NAMBA 0678 977 007

You might also like