Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

MO DEWJ BACKGROUND

Ni bilionea ambaye ametambliwa kuwa ni miongoni mwa mabilionea


wa umri mdgo zaid barani afrika.

Ni mfanya biashara na mwanasiasa ambae pia amewekeza katika


kandnda pia shughuli za hisani. Ni mnyenyekevu na mara nyingi
haandamani na wa linzi kama ilivo wa watu mashuhuri.

Mo Dewji ni nani?

Mo alizaliwa tarehe 8 Mei mwaka 1975, ikiwa na maana kwamba kwa


sasa ana miaka 43.

Alizaliwa eneo la Ipembe, Singida maeneo ya katikati mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes, ana


utajiri wa dola bilioni 1.5.

Ni wa pili miongoni mwa watoto sita wa Gulamabbas Dewji na Zubeda


Dewji.

Alisomea elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Arusha na baadaye


akasomea elimu ya sekondari katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika
(IST) jijini Dar es Salaam.

Alihamishiwa Marekani kwa masomo zaidi ya sekondari katika jimbo la


Florida mwaka 1992.

Alisomea chuo kikuu cha Gerogetown jijini Washington DC na kuhitimu


mwaka 1998 akiwa na shahada ya kwanza katika biashara ya
kimataifa na fedha, na masuala pia ya dini. Miongoni mwa watu
mashuhuri waliosomea chuo kikuu hicho ni rais Bill Clinton, rais wa
zamani wa Ufilipino Gloria Arroyo, Mfalme wa Jordan Abdullah na
wachezaji wa NBA kama vile Allen Iverson na Patrick Ewing.

Baada ya kufuzu, alirejea Tanzania na kuanza kushiriki katika


usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited
(MeTL) iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.

Alihudumu kwa miaka miwili kabla ya kuwa afisa mkuu mtendaji wa


kampuni hiyo, wadhifa ambao ameendelea kuushikilia hadi sasa.
Mo ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia miongoni mwa
matajiri wa umri mdogo zaidi Afrika.

Kampuni ya METL, kwa mujibu wa Forbes, ilifanikiwa kwa kununua


viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa
bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa
kisasa wa menejimenti.

METL ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za


matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina
mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa
mwaka.

Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni


kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75
ya hisa zote.

Kwa mujibu wa tovuti yake, METL inaendesha shughuli za uagizaji na


usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo,
vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji
baiskeli.

Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha
kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

METL ina shughuli zake katika nyingi barani Afrika na ina malengo ya
kujipanua zaidi katika maeneo zaidi.

Inaendesha shughuli zake Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi,


Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji
na Zambia, ambapo huajiri watu zaidi ya 28,000.

Shughuli za MeTL huchagia 3.5% ya jumla ya pato la taifa (GDP) la


Tanzania.

Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia


mwaka 1999 hadi mwaka 2014 kutoka $30 milioni hadi $1.3 bilioni
kilikuwa ni 200%.

Lengo la kampuni hiyo ni kuongeza mapato ya taifa lake hadi $5bn


kufikia mwaka 2020, pamoja na kuwaajiri watu 100,000.
Mo Dewji ameorodheshwa wa 17 kwenye orodha ya mabilionea barani
Afrika na wa 1561 duniani kwenye orodha ya mabilionea mwaka 2018.

Wakati mmoja kampuni yake ilianzisha Mo Cola kushindana na Coca


Cola.

Wakfu wa hisani
Dewji ni Mtanzania pekee aliyesaini mkataba mwaka 2016 wa kutoa
kwa wahitaji nusu ya mali yake.

Mo Dewji Foundation ndio asasi ambayo aliianzisha mwaka 2014 ili


kutekeleza nia yake hiyo na kazi yake kubwa ni kusaidia watanzania
wasiojiweza kwa upande wa afya, elimu na maendeleo jamii.

Kujiingiza katika siasa


Mbali na biashara na shughuli za jamii Mo Dewji amewahi kuwa
mwanasiasa na mwaka 2005 mpaka 2015, Mohamed Dewji alikuwa
mbunge wa Singida Mjini.

Alijiingiza katika siasa mara ya kwanza mwaka 2000 ambapo alishinda


uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo, wakati huo
akiwa na miaka 25, lakini akazuiwa kuwania kwa madai kwamba
alikuwa bado mdogo wa umri.

Alistaafu kutoka kwenye siasa baada ya kuhudumu mihula miwil

Tuzo
Mwaka 2012, alitawazwa Kiongozi Mdogo Duniani kwa Kiingereza
Young Global Leader (YGL) wakati wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu
wa uchumi Duniani (WEF).

Mwaka 2015, alitajwa kuwa bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika na


jarida la Forbes na baadaye akatawazwa Mtu Mashuhuri wa Mwaka wa
Forbes.
Mwaka uliopita, alishinda tuzo ya Afisa Mkuu Mtendaji bora wa Mwaka
Afrika katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu watendaji wa Afrika.
Familia: Mke wake na watoto

Mke wa Dewji huitwa Saira, aliyekuwa wanapendana tangu utotoni, na


wamejaliwa watoto watatu Nyla, Abbas na Mahdi. Alifunga ndoa
mwaka 2001. Mo na mke wake walikutana Shule ya Kimataifa ya
Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.
Klabu ya Simba SC

Dewji pia ni mpenzi wa michezo na amewekeza katika klabu ya mpira


ya Simba Sports Club inayocheza katika Ligi Kuu ya Tanzania ambapo
ni mfadhili mkuu kwa sasa.

Amekuwa akifadhili ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Sababu ya kurejea Tanzania kutoka Marekani

Mo Dewji alisomea Marekani na mpango wake ulikuwa kusalia na


kufanya kazi huko.

Ilikuwaje mwishowe akajipata Tanzania?

Mwezi Septemba, aliandika kwenye Instagram sababu iliyomfanya


kurejea, ambapo anasema ni ushauri wa babake pamoja na kugundua
kwamba kulikuwa na fursa nyingi Tanzania.

Ujumbe aliouandika 10 Septemba, 2018 ndio huu:

"Nilipomaliza masomo yangu ya shahada nikiwa nchini Marekani


niliamua kubaki huko na kufanya kazi. Nilitumia muda na nguvu nyingi
kazini lakini pesa ambayo niliipata haikukidhi kufanikisha malengo
yangu.

"Ndipo Baba yangu akanishauri nirejee nyumbani Tanzania na


nilipofatilia kwa kipindi hicho niligundua kwamba Tanzania kuna fursa
nyingi za kibiashara na hapo ndipo nilipoamua kurudi na kujiunga
katika biashara ya familia.

Muhimu kufahamu ni kwamba mafanikio sio lazima uende kuyatafuta


nje ya nchi, hapa hapa nchini kwetu kuna fursa ambazo ukifanyia kazi
utafanikiwa. Unafikiri kwanini baadhi ya watu wanapenda
kuishi/kufanya kazi nje ya nchi?"

Nukuu muhimu za Mo Dewji

Mara kwa mara, hutoa ushauri, na pia huwa hafichi upendo wake kwa
klabu ya Simba FC ambayo ndiye mdhamini wake mkuu.

1. Ijumaa wiki iliyopita, aliandika: "Kila jambo unaloogopa, Mungu ana mpango wake. Mungu ni mkuu
kuliko hofu uliyonayo. Ana mamlaka na maisha yako ya baadae. Kuwa na imani."
2. Kuhusu urafiki na mikopo, kauli yake hii: "Hamna kitu kinaua urafiki kama mikopo!"
3. Kuhusu utajiri na umaskini, aliweka nukuu hii aliyoitoa kwingine pengine kwenye Twitter majuzi: "Walio
fukara hujaribiwa kwa umaskini, sisi nao hujaribiwa kwa kupewa zaidi ya tunavyovihitaji."
4. Ana ushauri pia kuhusu kufanikiwa maishani: "Vitu vingi katika maisha vinaweza kujaribu kukuondoa
kwenye malengo yako lakini usipoteze mwelekeo. Mipango inaweza kubadilika lakini kamwe sio mwisho
wa safari!"
5. Kuhusu kuwezeshwa kwa wanawake: "Kwenye Uislamu, mwanamke hahitaji kuwezeshwa na mwanaume,
wameshawezeshwa na Mungu."
6. Kuhusu kuwa mfano bora kwa watoto: "Mtoto wako atafata mifano yako, sio ushauri wako. Hata
tunapofikiri hawatuoni, wanatuona. Hata tunapofikiri hatulei,

You might also like