Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 13

Rozari Takatifu Ya Mama

Bikira Maria

Mwongozo wa kusali Rozari


Sala, Matendo ya Rozari na Litania ya Bikira Maria
ROZARI YA MAMA MARIA

JINSI YA KUSALI ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika


taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba
ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu, Amina”.

Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama
mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika

1
ROZARI YA MAMA MARIA

nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia


zetu sisi wenyewe, nk) .

Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba


Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo,
zikiambatana na Salamu Maria tatu.

Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:


“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana
utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu
washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee
matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa
mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au;

“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,…..


Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e
Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na
sasa na siku zote, na milele, Amina.

2
ROZARI YA MAMA MARIA

Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa


milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji
huruma yako zaidi.

Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.

Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha


hapo juu.

Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…,


“Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama
muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda
ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya
makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe
kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na
Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.

3
ROZARI YA MAMA MARIA

MATENDO YA ROZARI TAKATIFU

MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria


kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie
unyenyekevu.

Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.


Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.

Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu


atujalie moyo wa ufukara

Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu


atujalie usafi wa moyo.

4
ROZARI YA MAMA MARIA

Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe


Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.


Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.

Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.


Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.

Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.


Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.


Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu


atujalie kuwapenda Yesu na Maria.

MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie


kugeuka watakatifu.

Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie


kwenda mbinguni.

5
ROZARI YA MAMA MARIA

Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe


Mungu atujalie bidii katika dini yetu.

Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe


Mungu atujalie kufa vizuri.

Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.


Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.

MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)

Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe


Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.

Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.


Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya
enjili.

Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe


Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.

Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie


neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.

Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia.


Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya
wengine.

6
ROZARI YA MAMA MARIA

LITANIA YA BIKIRA MARIA

 Bwana utuhurumie

 Bwana utuhurumie

 Kristo utuhurumie

 Bwana utuhurumie

 Bwana utuhurumie

 Kristo utusikie

 Kristo utusikilize

 Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie

 Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie


7
ROZARI YA MAMA MARIA

 Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie

 Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie

 Maria Mtakatifu ………. utuombee

 Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee

 Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee

 Mama wa Kristo ……… utuombee

 Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee

 Mama Mtakatifu sana ……… utuombee

 Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee

 Mama mwenye ubikira ……….. utuombee

 Mama usiye na doa ……….. utuombee

 Mama mpendelevu ………. utuombee

 Mama mstajabivu ………. utuombee

 Mama wa Muumba ………. utuombee

 Mama wa Mkombozi ………….. utuombee

 Mama wa Kanisa……….. utuombee

8
ROZARI YA MAMA MARIA

 Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee

 Bikira mwenye heshima ………….. utuombee

 Bikira mwenye sifa ………….. utuombee

 Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee

 Bikra mweye huruma ………….. utuombee

 Bikra mwaminifu………….. utuombee

 Kioo cha haki ………….. utuombee

 Kikao cha hekima ………….. utuombee

 Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee

 Chombo cha neema ………….. utuombee

 Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee

 Chombo bora cha ibada ………….. utuombee

 Waridi lenye fumbo ………….. utuombee

 Mnara wa Daudi ………….. utuombee

 Mnara wa pembe ………….. utuombee

 Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee

9
ROZARI YA MAMA MARIA

 Sanduku la Agano ………….. utuombee

 Mlango wa Mbingu ………….. utuombee

 Nyota ya asubuhi ………….. utuombee

 Afya ya wagonjwa ………….. utuombee

 Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee

 Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee

 Msaada wa waKristo ………….. utuombee

 Malkia wa Malaika ………….. utuombee

 Malkia wa Mababu ………….. utuombee

 Malkia wa Manabii ………….. utuombee

 Malkia wa Mitume ………….. utuombee

 Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee

 Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee

 Malkia wa Mabikira ………….. utuombee

 Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee

 Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee

10
ROZARI YA MAMA MARIA

 Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee

 Malkia wa amani ………….. utuombee

 Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za


dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.

 Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za


dunia,…………..Utusikilize ee Bwana

 Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za


dunia,…………..Utuhurumie.

 Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi


za Kristo.

Tuombe

Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na


mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu
Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za
milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.

11
ROZARI YA MAMA MARIA

MWANDISHI: Melkisedeck Leon Shine

Copyright © All Rights Reserved, Ackyshine

Tembelea katoliki.ackyshine.com Kupata majarida mengine

12

You might also like