Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

MKATABA WA KUKODISHA CHUMBA

Mimi……..……………………………………………..…nimekodi chumba kwenye nyumba No. H/MB 219c iliopo Mbweni,Zanzibar.


Kwa kiasi cha Tsh…………………….………..…cha malipo ya muda wa miezi…………sawa na Tsh…………………..…………kwa mwezi
MASHARTI YA MKATABA

1. Haikubaliki kwa mkodishwaji kukodisha chumba baada ya kukabidhiwa wala kumkabidhi umiliki wa kodi mtu mwengine
pasipo na makubaliano na mkodishaji.
2. Siruhusa kwa mpangishwaji kufanya aina yoyote ile ya vitendo vya kihuni kwa mujibu ya maadili ya kizanzibari ndani na
nje ya sehemu aliyopangishwa.
3. Ni wajibu wa mpangishwaji kutoa taarifa kabla ya mwezi mmoja kuisha mkataba wa awali kuhusu kuendelea na
kuongeza muda au kurejesha chumba ikiambatana pamoja na kulipa kodi ya mkataba mpya vilevile na mkodishaji
analazimika kutoa taarifa mwezi mmoja kabla kwa mkodishwaji kuhusu kupokea kodi mpya au kutokupokea tena baada
ya kumaliza muda wa mkataba wa mwanzo.
4. Kodi ya kuendelea kwa mkataba mpya ilipwe siku 15 kabla ya mkataba mpya kuanza.
5. Iwapo mpangishwaji hatoongeza muda wa mkataba mpya basi atalazimika kukabidhi chumba kwa mkodishaji kwa
mujibu wa muda wa mkataba ulioandikwa.
6. Mpangishwaji atumie vipaza sauti vyake kwa sauti ya kumtosheleza yeye chumbani pasipo kukera wengine kwa kutumia
sauti kubwa.
7. Haikubaliki kupika kwa jiko la mkaa na kuni ndani ya chumba
8. Mpangishwaji atagharamika mwenyewe kwa uharibifu wowote atakaofanya.
9. Ni wajibu kwa mpangishwaji kutunza chumba ikiwemo kufanya usafi wa ndani na nje ya sehemu aliyopangishwa na
kutunza vifaa vya ndani ya chumba.
10. Takataka zote zinahifadhiwa sehemu maalumu na wajibu wa mpangishwaji kuchangia kwa pamoja pesa za wanaobeba
taka.
11. Ni wajibu kwa mpangishwaji kuchangia kwa pamoja pesa za umeme utakapohitajika (hairuhisiwi kutumia jiko la umeme).
12. Haikubaliki kwa mpangishwaji kubadili wanawake/wanaume tofauti (kugeuza guest house).
13. Idadi ya mwisho ya wapangishwaji ni watu wazima wawili kwa chumba.

TAHADHARI: Endapo kama mpangishwaji ataenda kinyume na masharti ya mkataba huu basi kutakuwa na
haki ya lazima kwa mkodishaji kumtowa mkodishwaji ndani ya chumba tena pasipo na fidia yoyote kutoka
kwa mkodishaji.
MKODISHAJI MKODISHWAJI
JINA……………………………………………………… ………………………… JINA………………………………………………………………….……………..
SIMU: ………………………………………………………….. SIMU:...……………………………………..................
NAMBA YA NIDA …………………………………..…….. NAMBA YA NIDA……………………………………….

SAHIHI……………………………… SAHIHI…………………………………

MASHAHIDI
SHAHIDI UPANDE WA MKODISHAJI SHAHIDI UPANDE WA MKODISHWAJI
JINA……………………………………………………… …………………........... JINA………………….…………………………………………….……………….
SIMU: …………………………………………………………. SIMU: ……………………………………………………….
NAMBA YA NIDA…………………………………………. NAMBA YA NIDA……………………………………….
SAHIHI………………………………… SAHIHI……………………………….

Muda wa kuanza mkataba ………..…/…………/20…….


Muda wa kumaliza mkataba ……..…./…..……/20.……

You might also like