Litania Ya Bikira Maria

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

LITANIA YA BIKIRA MARIA

Bwana Utuhurumie Bwana Utuhurumie


Kristo Utuhurumie Kristo Utuhurumie
Bwana Utuhurumie Bwana Utuhurumie
Kristo Utusikie Kristo Utusikilize

Baba wa mbinguni Mungu, Utuhurumie.


Mwana, Mkombozi wa
dunia, Mungu Utuhurumie
Roho Mtakatifu, Mungu Utuhurumie
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja Utuhurumie

Maria Mtakatifu Utuombee


Mzazi Mtakatifu wa Mungu Utuombee
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa Mabikira Utuombee
Mama wa Kristo Utuombee
Mama wa Kanisa Utuombee
Mama wa huruma Utuombee
Mama wa neema ya Mungu Utuombee
Mama wa matumaini Utuombee
Mama Mtakatifu sana Utuombee
Mama mwenye usafi wa moyo Utuombee
Mama usiye na doa Utuombee
Mama usiye na dhambi Utuombee
Mama mpendelevu Utuombee
Mama Mstaajabivu Utuombee
Mama wa shauri jema Utuombee
Mama wa Muumba Utuombee
Mama wa Mkombozi Utuombee
Bikira mwenye utaratibu Utuombee
Bikira mwenye heshima Utuombee
Bikira mwenye sifa Utuombee
Bikira mwenye enzi Utuombee
Bikira mwenye huruma Utuombee
Bikira amini Utuombee
Kioo cha haki Utuombee
Kikao cha hekima Utuombee
Sababu ya furaha yetu Utuombee
Chombo cha neema Utuombee
Chombo cha heshima Utuombee
Chombo bora cha ibada Utuombee
Waridi lenye fumbo Utuombee
Mnara wa Daudi Utuombee
Mnara wa Pembe Utuombee
Nyumba ya dhahabu Utuombee
Sanduku la Agano Utuombee
Mlango wa mbingu Utuombee
Nyota ya asubuhi Utuombee
Salama ya wagonjwa Utuombee
Kimbilio la wakosefu Utuombee
Mfariji wa wenye uchungu Utuombee
Msaada wa Wakristo Utuombee
Malkia wa Malaika Utuombee
Malkia wa Mababu Utuombee
Malkia wa Manabii Utuombee
Malkia wa Mitume Utuombee
Malkia wa Mashahidi Utuombee
Malkia wa Waungama Utuombee
Malkia wa Mabikira Utuombee
Malkia wa Watakatifu wote Utuombee
Malkia uliyeumbwa pasipo
dhambi ya asili, Utuombee
Malkia uliyepalizwa mbinguni Utuombee
Malkia wa Rozari Takatifu Utuombee
Malkia wa familia Utuombee
Malkia wa Amani Utuombee

Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye dhambi za ulimwengu – Utuhurumie

Mwanakondoo wa Mungu
uondoaye dhambi za ulimwengu- Utuhurumie

Mwanakondoo wa Mungu
uondoaye dhambi za ulimwengu- Utuhurumie

K. Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu


W. Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Ee Bwana Mungu, twakuomba utujaalie sisi
watumishi wako tuwe siku zote na afya ya roho na
mwili; na kwa maombezi matukufu ya Maria
Mtakatifu, Bikira daima, tuopolewe katika
mashaka ya sasa, tupate na furaha za milele. Kwa
njia ya Kristo Bwana wetu.

KUMBUKA

Kumbuka, Ee Bikira Maria mwenye rehema,


haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu
aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba shime kwako,
akitaka umwombee. Nami kwa matumaini hayo,
nakukimbilia, ee Mama, mkuu wa mabikira;
ninakuja kwako, nasimama mbele yako mimi
mkosefu, ewe Mama wa Neno wa Mungu,
usiyakate maneno yangu, bali uyasikilize kwa
wema na unitimizie. Amina.
SALAMU MALKIA

Salamu Malkia, Mma mwenye huruma; uzima,


tulizo na matumaini yetu salamu. Tunakusihi
ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia
tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye
machozi. Haya basi, mwombezi wetu, utuangalie
kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa
ugeni huu utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa
tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu,
Bikira Maria.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu

W. Tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:

Ee Mungu, makimbilio na nguvu yetu, uwaangalie


kwa wema watu wanaokulilia; na kwa maombezi
ya Bikira Maria Mtukufu asiye na kosa, Mzazi wa
Mungu na ya Mtakatifu Yosefu, mume wake, na
ya watakatifu Petro na Paulo Mitume wako, na ya
watakatifu wote; usikilize kwa huruma na wema
sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na
kwa uhuru na utukufu wa Kanisa, Mama
Mtakatifu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo
Bwana wetu. Amina.

You might also like