Jifunze Kutengeneza Bidhaa Za Viwandani

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 65

YALIYOMO

UTANGULIZI

SEHEMU YA KWANZA

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutengeneza

Sabuni

Sababu ya sabuni kujikata au kujitenga.

Vifaa vya usalama na vitendea kazi.

Kazi za malighafi.

Sabuni ya maji kanuni ya kwanza.

Sabuni ya maji kanuni ya pili.

Sabuni ya maji kanuni ya tatu

Sabuni ya maji kanuni ya nne

Sabuni ya maji ya caustic solution

Sabuni ya kuoshea vyombo

Sabuni ya chooni
PILI

Hair shampoo

Shampoo ya alovera na asali

Shampooo ya tango

Shampoo ya alovera

Sabuni ya kunawia

Jiki za rangi

Jiki za kawaida

Sabuni ya maji ya kuogea

Window cleaner

Sabuni ya kuoshea magari

After shave

TATU

Mafuta ya mgando

Mafuta ya kurefusha nywele

Mafuta ya mgando ya rika zote

Mafuta ya nazi ya mgando

Udi wa kuogea

Ubuyu wa vipande

Ubuyu wa Zanzibar
NNE

Chaki

Kanuni ya kuchanganya caustic soda na maji

Mold au vifyatulio vya sabuni

Sabuni za mche /kipande

Sabuni za magadi

Sabuni za magadi kanuni ya pili

TANO

Aina za batiki

Batiki za kuchovya(tie and dye)

Batiki za mshumaa

Batiki za kublich

Batiki za kuprint

Batiki za kufinyanga

SITA

Sabuni ya unga

Siagi ya karanga

Body lotion

Lotion ya limao

Whitening & softening body serum

Coffee body scrub

Sugar scrub

Scrub yenye exfoliant zaid ya moja


SABA

Scrub isiyotumia maji

Scrub inayotumia maji

Kazi ya baadhi exfoliant

Tiles & sink cleaner

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTENGENEZA SABUNI

1. Vaa gloves ,mask na viatu vigumu kabla hautaanza kutengeneza sabuni

2. Pima kemikali kwa kipimo maalumu usikadirie

3. Weka mbali na watoto kemikali

4. Weka chumba maalumu kemikali usiweke chumba cha kulala viumbe hai.

SABABU YA SABUNI KUJIKATA AU KUJITENGA

1. Kuzidi kwa chumvi

2. Kuzidi kwa pafyumu

3. Uvivu wa kukoroga

4. Kupitwa kwa wakati kwa kemikali

5. Kuzidi kwa soda ash

Ili kuepuka tatizo hili fuata vipimo na taratibu zilizoelezwa kwenye makala hii.

VIFAA VYA USALAMA NA VITENDEA KAZI


VIFAA VYA MSINGI KATIKA UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAGADI NA TIBA

KIPIMIO
KAZI YA MALIGHAFI

SABUNI YA MAJI | ( kanuni ya kwanza )

Mahitaji

1. Sulphonic Acid -Lita 1 2. Sless -500g

3. Soda Ash- 500g 4. Glycerine -250g

5. Cde -200g 6. Alka 2 _100g

7. Sodium Sulphate -300g 8. Rangi _2g

9. Perfume 50g 10. Maji_ 17.5

11. Dm dmh -40mls 12. Ph Inayotakiwa 6_8

Malighafi.
Hatua Za Utengenezaji

Chukua ndoo weka sulphonic acid kwenye chombo cha kukorogea koroga soda ash light
kwenye maji lita moja na nusu mimina kwenye sulphonic acid koroga

Weka sless kwenye mchanganyiko wako anza kukoroga.

Weka maji kidogo kidogo lita 10 lita kumi zilizobakia korogea alka tu kisha mimina kwenye ndoo
yenye mchanganyiko ule wa mwanzo

Weka Cde,Ongeza Glycerine Koroga

Weka Rangi Na Perfume

Weka Dm Dmh /Nu-Care

Pima Ph

Weka Kwenye Vifungashio Na Fungasha

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA

MAJI (kanuni ya pili

MALIGHAFI

1. Sulphonic acid -Lita moja

2. Siles au ungarol-lita moja

3. Soda ash-vijiko 15 vya chakula

4. CMC-VIJIKO 6 vya chakula


5. Maji Lita 30

6. Grisalini -vijiko 8

7. Pafyumu -kijiko 1-2 vya chakula

8. Rangi- kijiko kimoja

9. Chumvi ya mawe kilo moja Ila usiweke yote

10. Dm dmh –vijiko 5 vya chakula

Vifaa vya kutengenezea

1. Jaba au ndoo 2. Mwiko mkavu

3. Gloves 4. Mask

5. Overral

Kuwa makini kuna baadhi ya kemikali hatari kwa afya

HATUA ZA UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI

1. Chukua ndoo au Jaba unaweka sulphonic acid Na Siles unakoroga kuelekea upande mmoja
2. Weka soda ash Na cmc koroga kuelekea upande mmoja

3. Weka Maji Lita 30 koroga kuelekea upande mmoja kwa dakika 5

4. Weka grisalini,pafyumu Na rangi koroga kuelekea upande mmoja

5. Weka DM dmh na chumvi ambayo uliiloweka kwenye Maji weka kidogo kidogo huku ukipima
uzito upendao ,ukishamaliza hapo funika Sabuni yako iache ipoe povu lote lishuke ndipo uanze
kupaki kwenye Vifungashio

NB: Usiache bila kufunika pafyumu yako itaruka nakuisha kabisa.

SABUNI YA MAJI (kanuni 3)

MALIGHAFI

1. Caustic soda solution-1ltr 2. Maji _20lita

3. Sulphonic acid_lita 2 4. Dm dmh-50 mls

5. Rangi ya Sabuni ya maji-5mls 6. Manukato -5mls

7. Chumvi gram 1000 ( usiweke yote )

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua Kilo 1 Ya Caustic Soda Na Maji Lita 3 Koroga Kisha Ziache Zipoe Kwa Muda Wa Siku
mbili

2. Chukua sulphonic acid changanya na maji Lita 10 ukikoroga ongeza maji Lita 20
3. Koroga Hadi vipande vyeupe vitoweke Kisha weka chumvi ,rangi na manukato koroga kwa
dakika 5

4. Pima kwa pH isome 6-8

5. Baada ya hapo weka kwenye vifungashio

SABUNI ZA MAJI (kanuni ya nne)

Malighafi

Maji liter 30 au 40

1. Sulfonic acid 1 litre 2. Sles / Ungarol 1 litre

3 Soda ash light ½ kg 4. Gryceline ¼ litre

5. Ethanol 50ml 6. Cdea 50ml

7. Chumvi 1½ kg 8. Alka 2 /cmc 125 gram

9. Perfume 50ml 10. Rangi gram 5

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Andaa maji lita 40 chota Lita 3 kisha weka kando.

2. Chukua sles tia ktk ndoo koroga tia chumvi kijiko kimoja kuyeyusha sless vizuri, koroga hadi
upate cream Kama lotion iwe soft kabisa.

3. Chukua Sulfonic acid mimina ktk ndoo yenye sless kisha koroga vizuri na utie maji lita moja ili
kulainisha mchanganyiko huo kisha koroga, ongeza soda ash ambayo uliiloweka ktk maji robo
lita itie humo ktk mchanganyiko huo koroga vizuri ikianza kuleta ugumu anza kutia maji nusu
Lita kisha koroga upate cream soft kabisa
4. Baada ya kupata cream soft endelea kutia maji lita moja moja hadi yaishe huku ukikoroga
kuelekea upande mmoja pia maji tia upande katika ndoo na sio kumwagia katikati ya ndoo,
ongeza chumvi kilo 1½ ile uliyoloweka koroga vizuri kabisa ilete uzito dakika 20

5. Baada ya kutia chumvi na kukoroga vizuri saana ( ukorogaji mzuri wa muda mrefu hufanya
sabuni iwe nzuri na isiwe na wingu) ongeza cdea koroga.

6. Chukua alka 2/ cmc tia katika maji Lita 3 uliyotenga koroga vizuri upate uji mzito kisha
miminia katika sabuni yako koroga vizuri kwa dakika 20 upate uzito zaidi ( usiloweke tigna na
kuiacha itaganda na kuharibika.)

7. Tia gryceline kisha koroga,tia rangi kiasi ukitazama isizidi na kukolea saana, iwe rangi kiasi ili
kuleta mvuto pia utakoroga kuelekea upande mmoja ili kuepusha povu kukuzuia kuona ndani, hii.
( Loweka rangi katika maji kiduchu ikoroge ndipo uitumie)

8. Tia ethanol 50ml na DM DMH Koroga vizuri Funika sabuni yako iache kwa iive kisha utaitia
pafyum yako na kuifungasha tayari kwa matumizi.

UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAJI

(kanuni 5)

MALIGHAFI

1. Sless- ½ ( 500gm) 2. Sulphonic acid -1 kg

3. Caustic soda- 60gm 4. Soda ash- 125 gm

5. CMC/ALKA 2-80gm 6. Tigna- 250gm


7. Gryceline-250 ml 8. Ethanol- 50mls

9. Chumvi -500 g 10. Rangi-10gm

11. Perfume- 50mls 12. Maji -25

MAANDALIZI

1. Chukua caustic soda 60gm loweka katika maji ya 1000ml.

2. Chukua soda ash 125gm loweka kwenye maji ya 1000mls.

3. Chukua Foaming booster 80gm loweka kwenye maji ya 1000mls

NB: Viache kwa muda wa masaa mawili.

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua sless na sulphonic acid mimina kwenye jaba lako lisilo na maji kisha koroga kwa
muda wa dk 5 hadi vichanganyike vizuri.

2. Chukua caustic soda uliokuwa umeiloweka katika maji 1000mls mwaga katika mchanganyiko
wa awali kisha koroga kwa muda wa dk 5

3. Chukua soda ash iliokuwa imelowekwa katika maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko
wako kisha endelea kukoroga kwa muda wa dk 3 hadi 5

4. Chukua booster iliokuwa imelowekwa kwenye maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko
wako wa awali kisha koroga vizuri kwa muda wa dk 5
5. Chukua Tigna ichanganye kwenye maji uliyo yaandaa 22000mls sawa na lita 22 ikologe kwa
dk1 ichanganyikane vizuri kisha mimina hayo maji ambayo ni mchanganyiko na Tigna katika
mchanganyiko wa awali.

Kisha utaendelea kukoroga mpaka pale utakapo ona uzito.

BAADA YA SABUNI KUWA NZITO.

6. Weka gryceline koroga kwa dk 1

7. Weka DM DMH/ethanol koroga kwa dk1

8. Weka industrial salt kisha koroga kwa dk 1

NOTE: Hapo sabuni yako itakuwa imekamilika kwa 90% kisha ifunike vizuri.

SIKU INAYOFUATA

1. Weka perfume kisha koroga kidgo

2. Weka rangi kisha koroga kwa dk 3

NOTE: Baada ya hapo sabuni yako itakuwa tayari sasa kupeleka sokoni.

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI MULTIPURPOSE KANUNI 5

Malighafi

1. Maji lita 25-30

2. Nitrosol 250

3. Ladi water lita 1

4. Sulphonic acid lita 1


5. Sless nusu lita

6. Dm Dmh mls 40

7. Pefume mls 50

8. Glycerine mls 100

JINSI YA UTENGENEZAJI

1. Chukua jaba weka maji kasha weka nitrosol koroga hadi iyeyuke

2. Weka ladi water kasha koroga weka sulphonic acid kisha koroga

3. Weka sles kasha koroga weka DM DMH koroga

4. Weka perfume,glycerine na rangi kasha koroga

5. Anza kuweka kwenye vifungashio tayari kwa kupeleka sokoni

DISINFECTANT LIQUID SOAP (Sabuni ya kudekia/kusafishia nyumba/chooni.

Hii ni aina ya sabuni ambayo hutumika kusafishia au kudekia mazingira ya nyumbani. Sabunii hii
huuwa vijidudu (Germs) na Bacteria wazungukao sehemu za nyumba zetu, kama vile jikoni,
chooni, sebuleni na maeneo mengine. Sabuni hii ni rahisi kutumia pia ni rafiki kwa matumizi ya
nyumbani. Pia huondoa madoa au uchafu sugu kwa haraka zaidi.

MAHITAJI

1) LABSA/Sulphonic acid - ½ Lita 2) Maji – 19 Lita

3) Boric acid – 100g 4) Borax – 100g

5) Rangi – 1Tbsp 6) Perfume(Lavender) – 100ml

7) Alka tu – 100g 8) Citric acid- 20g/

9) DM DMH-50MLS

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Weka maji lita 19 katika ndoo/Jaba kisha weka Alkatu 100g kisha koroga kwa dk 10 h adi 15.

2. Ongeza Sulphonic acid ½ Lita kisha koroga vizuri.

3. Chukua Boric acid 100g na Borax 100g tia katika jagi lenye maji lita 1 koroga vizuri na kisha
tia katika jaba letu endelea kukoroga kwa dakika 10.

4. Chukua rangi kiasi kidogo koroga pembeni katika maji kidogo, koroga vizuri kisha tia katika
ndoo au Jaba la Sabuni na endelea kukoroga.

5. Weka DM DMH na endelea kukoroga.

Ongeza perfume ya Lemon/Dettol au Lavender 100ml kisha koroga vizuri na acha kwa saa 24
au zaidi kisha fungasha peleka sokoni.

HAIR SHAMPOO

Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu
bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye
nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo
zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea.

MAHITAJI /MALIGHAFI

1. Sless Lita moja na nusu 2. CDE-250 MLS

3. Glycerine -500 MLS 4. Citric acid - 12 g

5. Rangi - 5gm 6. Perfume - 30-40 MLS

7. Maji Lita 20 8. Ph.5_ 7

9. DM DmH 40 MLS 10. Chumvi 300gm sio lazima

VIFAA

MZANI NDOO YA PLASTIKI

GLOVES MASK

BUTI MWIKO WA KUKOROGEA

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua ndoo weka sless peke yake KOROGA mpaka iwe kama cream ,weka maji kidogo
kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga

2. Weka CDE na glycerine KOROGA kwa dakika tatu

3. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja

4. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi
weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga

5. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako.
MAMBO YA KUZINGATIA

1. Koroga kuelekea upande mmoja.

2. Rangi uweke kwenye maji hata nusu Lita Kisha Anza kuitumia

3. Katika kuboresha bidhaa yako unaweza kuongeza vionjo mbalimbali Ila lazima viwe
vimefanyiwa utafiti

Mfano wa vionjo

Alovera, Asali, Tango, Tangawizi

Pia viwe asilimia 2-5 Sawa na 200mls – 600mls

SHAMPOO YA ALOVERA NA ASALI

MAHITAJI /MALIGHAFI

VIFAA

Mzani

Ndoo Ya Plastiki

Gloves Mask

Buti

Mwiko Wa Kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua ndoo weka sless peke yake KOROGA mpaka iwe kama cream

2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga

3. Weka CDE na glycerine KOROGA kwa dakika tatu

4. Weka alovera na asali Kisha koroga vizuri

5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja

6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi
weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga

7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako
SHAMPOO YA TANGO

MAHITAJI /MALIGHAFI

1. Sless Lita moja na nusu 2. CDE-250 MLS

3. Glycerine -500 MLS 4. Citric acid - 12 g

5. Tango_600 MLS 6. Rangi - 5gm

7. Perfume - 30-40 MLS 8. Maji Lita 20

9. Ph.5_ 7 10. DM DmH 40 MLS

11. Chumvi 300gm sio lazima

VIFAA

Mzani, Ndoo Ya Plastiki, Gloves, Mask, Buti, Mwiko Wa Kukorogea

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua ndoo weka sless peke yake koroga mpaka owe cream

2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga

3. Weka CDE na glycerine koroga kwa dakika tatu

4. Weka juisi ya tango Kisha koroga vizuri

5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi
weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga

7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako

SHAMPOO YA ALOE VERA

Hii ni shampoo yenye virutubisho lishe vya aloe vera. Miongoni mwa vitamin zinazopatikana
katika mmea huu ni vitamin B12 na B14 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa nywele. Hulainisha
nywele kwa kuzuia ngozi kukauka, kuponya michubuko, kuzipatia nywele rangi yake na kuzuia
nywele kujisokota.

MAHITAJI (LITA 10)

a) Maji -lita 10. b) Uice soft ya aloe vera -200ml.

c) Cde -200ml. d) Gryceline – 100ml.

e) Sless –nusu lita f) Perfume – 20ml.

g) Rangi (kijani) –10ml h) Cmc/ akla 2 -100gm.

i) Dm dmh-50 mls. j) PH 5-7

JINSI YA KUTENGENEZA.

1. Pima maji lita 10 kwa kutumia measuring cylinder na mimina kwenye chombo cha
kuchanganyia

2. Chukua sless 1kg, gryceline 100ml, formaline 10ml, perfume 20ml na cde 200ml.Kisha
vichanganye pembeni bila maji hadi vichanganyikane vizuri hadi sless iyeyuke kabisa.weka
cmc/ alka 2 100gm kisha koroga tena vizuri hadi iyeyuke vizuri.
3. Weka juice yako ya aloe vera na koroga tena vizuri.

4. Malizia kwa kuweka rangi yako 10gm (kadiria) na weka DM DMH koroga tena hadi ishike
vizuri.

5. Pima PH acha povu lishuke tayari kwa matumizi.

ANTI BACTERIAL HAND WASH/ SABUNI YA KUNAWIA

MAHITAJI

1. Sless Lita 1 na nusu 2. Cde 250mls

3. Chumvi 500 gm 4. Glycerine 250 MLS

5. Rangi 5gm 6. Perfume-30had 40mls

7. Maji Lita 20 8. DM DMH MLS 40

10. IPA 50 MLS 11. Ph - 6-8

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Koroga slesa ponda ponda mpka iwe Kama cream

2. Ongeza maji yenye chumvi (sodium sulphate) koroga

3. Weka cde koroga

4. Ongeza glycerine endelea kukoroga

5. Weka rangi koroga

6. Weka perfume ,ongeza DM DmH

7. Pima pH inatakiwa iwe 6-8,.Iache sabuni ishuke povu anza kufungasha.


DAWA YA MADOA KWA NGUO ZA RANGI.

Mahitaji.

1. Hydrogen peroxide 500- 1kg

2. Chumvi 1kg

3. Soda ash 1kg

4. Culcium Hypoclorite 1kg

5. Maji 25L.

Utengenezaji

2. Tenga maji Lita 25 tia hypoclorite korogo iyeyuke yote, tia soda ash koroga dakika 10

3. Ongeza chumvi na hydrogen peroxide koroga vizuri funika acha kwa saa 24 kisha fungasha.

NB. Jaribu bidhaa yako kabla hujauza.

DAWA YA KUONDOA MADOA (jiki)

Malighafi

1. Maji lita 10

2. Breach//sodium hypochlorite nusu kilo

3. Soda ash-robo kilo

JINSI YA KUTENGENEZA

1. Mimina maji katika chombo cha kutengenezea weka breac/ sodium hypochlorite taratibu
katika maji na ukoroge kwa dakika tano (5) ongeza soda ash na ukoroge kwa dakika 10 mpaka
ichanganyike vizuri

2. Acha ipoe kasha chuja weka kwenye vifungashio


SHOWER GEL(sabuni ya kuogea )

Hii ni Sabuni ya maji ambayo iko maalumu kwa ajili ya kuogea

MAHITAJI

1. Sless - kutakatisha na kuongeza povu

2. Cap b-kuongeza povu, inaongeza uzito na nzuri kwenye ngozi

3. Chumvi - uzito na kutunza

4. Glycerine -moisturizer

5. Citric acid -kuweka ph, vitamin C, kutunza

6. Rangi - mvuto

7. Perfume - harufu

8. Maji kibebeo Cha shower gel


9. Ph.kupima asid na base

10. Dm dmh - kutunza isiharibike

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua chombo Cha plastiki WEKA siles koroga iponde ponder Hadi iwe Kama cream

2. Weka maji yenye chumvi(chumvi koroga pembeni kwa kipimo kile like Cha sodium Sulphate)

3. Weka maji Lita mbili mbili huk u ukiendelea kukoroga kidogo kidogo

4. Weka Capb na endelea kukoroga

5. Weka Glycerine endelea kukoroga

6. Weka citric acid ,ongeza rangi na perfume alafu koroga

7. Weka Dm DmH Kisha koroga,pima pH iache ikitulia Anza kuweka kwenye vifungashio

Mambo ya kuzingatia

1. Inashauriwa pafyumu isowe Kali Sana iwe imepoa

2. Unaweza kuweka vionjo ili kufanya ipendeze na kuteka soko

3. Unaweza kuweka matunda ,Castro Oil, Olive Oil

Vitu hivi viwe vimefanyiwa utafiti na kujiridhisha na sababu za kuviweka

4. Usisahau kuweka preservative ili shower gel isioze

5. Kama unaweka malighafi za mafuta Ni vizuri kuweka emulsifier mf polysobate

Kama unaweka malighafi za mafuta ratio iwe 2% Hadi 5% sawa MLS 200 Hadi 600mls

WINDOW & GLASS CLEANER

Hii ni bidhaa ambayo hutumika kwa matumizi ya kusafishia vioo na vyombo mbalimbali aina ya
glass. Huenda vioo vya madirisha au magari, watu wengi huwa wanamiliki vitu ambavyo vina
material ya vioo na hawajui jinsi gani ya kusafisha hivyo vioo punde baada ya kuchafuka.
Hii ni bidhaa nzuri ambayo mara nyingi hutumika katika kusafishia madirisha ya vioo au kifaa
chochote ambacho kimetengenezwa kwa material ya kioo,

MALIGHAFI ZITUMIKAZO KATIKA KUTENGENEZA

WINDOWS CLEANER

1. Sabuni ya maji

2. Vinegar ( ACETIC GRACIAL ACID )

3. Maji safi

JINSI YA KITENGENEZA WINDOWS CLEANER

1. Utakuwa na maji lita kumi kama unataka kutengeneza lita kumi.Chukua sabuni yako lita moja
kisha mimina katika chonbo chako ulicho aandaa ili utengeneze windows cleaner.

2. Chukua vinegar ( acetic gracial acid ) lita moja kisha uta mimina katikas chombo ambacho
uliweka sabuni yako ya maji.. Kisha utakoroga mpaka utakapoona kuwa imekuwa vzuri kabisa.
So povu litatokea jingi sana so unaweza ukaicha kwa kipindi flani hivi ( takribani dakika 5 )
mpaka utakapoona kuwa povu limetoka loteee.

Na hapo inakuwa umeweza kutengeneza windows cleaner kwa njia nyepesi kabisa.

SABUNI YA KUOSHEA MAGARI

Sabuni ya maji ya ya kuoshea magari ni moja ya sabuni pendwa sana mijini kutokana na
urahisishaji wake ktk kuoshea magari pamoja na ubora wake.Sabuni ya maji ya kuoshea magari
haipaswi kuwa na kemikali ili isipaushe magari na kupoteza ule mng'ao wa magari.Sabuni hii
itaacha gari yako ktk mng'ao mzuri sana, pia haitapauka kutokana na malighafi hizi ambazo
hazina kemikali.
Mahitaji:

1. Sless/ ungarol 1½kg =

2. Cocamidopropyl betaine ¼L

3. Isopropyl Alcohol/ Ethanol 200ml

4. Grycleline ¼L

5. Coconut oil 100ml

6. Perfume 25ml

7. Color 20g

8. Salt 100g

9. Tigna/CMC 125g

10. Maji 20L.

KAZI ZA MALIGHAFI

1. Sles -Kuweka povu, kuondoa uchafu, kuweka utelezi.

2. Cocamidopropyl betaine - Kuongea povu, utelezi, mng'ao wa sabuni na ulaini/ smoothly.

3. Isopropyl Alcohol/ Ethanol -Kitunza sabuni, husaidia kulegeza uchafu mgumu utoke.

4. Grycelin-Huleta ulaini, utelezi, huzuia gari isipauke.( Mafuta)

5. Coconut oil-Hulainisha sabuni, huacha gari ktk hali ya unyevu unyevu isipauke na kuwa kavu.

6. Pafyum- Harufu

7. Rangi -Muonekano.

8. Tigna /CMC-Uzito, povu, utelezi.

9. Chumvi- imetumika kusaida kuyeyusha sless, pia kutunza sabuni & kuongezea uzito.

10. Maji 20L.


HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Pima sless 1½ kg ktk jaba/ ndoo yako, tia chumvi 100g pamoja koroga kwa dakika 20 upate
rojo laini kama lotion.

2. Tia maji Lita 4 koroga dakika 15 kuelekea upande mmoja, ongeza maji Lita 6 koroga dakika
15.

3. Ongeza maji lita 7 koroga dakika 15- 20.

4. Tia Grycelin koroga dkk 3, ongeza cdea koroga dkk 15.

5. Tia coconut oil koroga dkk 3, ongeza Isopropyl Alcohol/ Ethanol koroga dakika 5.

6. Tenga maji Lita 3 yaliyobakia, tia tigna koroga upate uji mzito, tia kaika sabuni yako koroga
dkk 15 funika acha kwa saa 24.

7. Baada ya saa 24 tia pafyum 25ml koroga dkk 5

8. Tia rangi 20g iliyoloa maji koroga dkk10 kisha fungasha tayari kwa matumizi.

Mtaji Tsh 24,000/= tu, sabuni Lita moja Tsh 3,000/=

AFTER SHAVE

MAHITAJI

1. Ethanol- 200ml 2. Glycerine- 50ml

3. Menthol- 1tbsp 4. Colour

5. Perfume- 10ml

UTENGENEZAJI

1. Pima kiasi cha Ethanol na uyeyushe Menthol ndani ya chombe chenye Ethanol.

2. Koroga vizuri mchanganyiko huo.

3. Ongeza Glycerine na ukoroge.


4. Ongeza tena Ethanol katika mchanganyiko wako na ukoroge tena vizuri.Ongeza perfume na
rangi kisha koroga vizuri.After shave itakuwa tayari kwa matumizi.

MATUMIZI: hutumika baada ya kunyoa(ku shave). mfano ukisha nyoa ndevu una paka hii after
shave kuzuia kutokwa na vidonda au mapele.

MAFUTA YA MGANDO

Mafuta ya mgando ni mojawapo ya vilainishi vya ngozi vinavyoipa ngozi mwonekano wa kuvutia
na nyororo.

Mahitaji.

1) Micro wax 0.5kg.

2) White oil 0.5 Lita.

3) Glycerine ya kiwandani 20ml.

4) Perfume 25ml.

5) Rangi tone mbili.

6) Jiko lenye moto.

7) Sufuria.

8) Vifungashio.

Jinsi ya kutengeneza

1. Washa jiko lako moto kiasi na ubandike sufuria.

2. Weka micro wax nusu kilo ndani ya sufuria na subiri iyeyuke.

3. Weka white oil nusu Lita na koroga vizuri.

4. Weka perfume 25ml. na koroga tena.

5. Shusha mafuta yako na subiri yapoe kiasi {usiache yakapoa sana }


6. Malizia kwa kuweka glycerin yako 20ml{mafuta yakiwa chini} kisha koroga tena vizuri.

7. Weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi.

NB: Mafuta haya yanaviwango vya TBS hivyo yafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote
{Mtoto mdogo hadi mzee }

Mtaji wa mafuta ya mgando Lita 1.

1. Microwax ½ kg Tsh 3000/=

2. White oil ½ kg Tsh 3000/=

3. Grycelin ¼ litre Tsh 1500/= tumia 20ml tu.

4. Perfume 50ml Tsh 3,000/= tumia 10ml tu.

5. Rangi (optional) Tsh 1000/= tumia tone 2.

Jumla Tsh 11,500/= tu

Utatoa mafuta 1000ml sawa na vichupa 20 vya 50ml kila kichupa uza Tsh 1,500 hadi 2000, vifaa
kama Grycelin, rangi, pafyum, vitabaki.

MAFUTA YA KUREFUSHA NYWELE

1. White Oil 1 lita

2. Micro Wax 1 lita

3. Olive Oil vijiko 11 vya chakula

4. Castrol Oil ½lita

5. Majani ya Mvuje 10

6. Majani ya Rosemary Kichane 1

7. vitunguu Swaumu 6 punje


8. Vitunguu maji 3 vyekundu

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Yeyusha White Oil+Micro Wax kwa njia ya double boil.Ikiyeyuka weka Castrol Oil na uipue.

2. Chemsha Olive Oil Vijiko 6+Vitunguu swaumu+Vitunguu maji (Unaweza kusaga kabla) Kisha
chuja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa Awali.

3. Chukua tena Olive Oil Vijiko 5+Mvuje +Rosemary Chemsha Kisha uchuje na uchanganye
kwenye mchanganyiko wa Awali.Koroga vyema.

4. Weka Rangi ya Mafuta (Kijani/njano hupendeza zaidi) Weka Perfume, koroga. Yakipoa
mimina katika package ulizoziandaa yaache yagande Kisha tayari kwa matumizi.

MAFUTA YA MGANDO KWA RIKA ZOTE(WATOTO HADI WAZEE)

MAHITAJI

1. White oil - 2 lita

2. Micro wax - 1 kg

3. Pure coconut oil -¼ lita

4. Gryceline - 50mls

5. Perfumu (sio lazima)- 25ml

6.Rangi (sio lazima) - tone 2

7. Aloe vera gelly - 200mls.


VIFAA

Jiko lenye moto, SufuriaIfungashio, Mwiko/kijiko cha kukorogea

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Washa jiko lako moto na ubandike sufuria.

2. Weka micro wax ndani ya sufuria na subiri iyeyuke,Kisha weka white oil lita 2 na koroga
vizuri.Kisha ongeza coconut oil na Aloe vera gelly kisha koroga vizuri.

3. Weka Gryceline na uendelee kukoroga, weka perfume na koroga tena.Shusha mafuta yako na
subiri yapoe (usiache yakapoa sana kwani yataganda kabla hujaweka kwenye vifungashio)

4. Weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi.

NB: Mafuta haya yanafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote.(watoto hadi wazee)

MAFUTA YA NAZI YA MGANDO

Mahitaji

1. White Oil 1 litre

2. Micro Wax 1 Litre

3. Pure Coconut Oil ¼ litre

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua sufuria weka jiko weka maji chukua nyingine ndogo kwa kutumia njia ya double
boil,Weka vyote jikoni viyeyuke.
2. Vikishayeyuka na kuchanganyikana,ipua na uache yapoe.Yakishapoa mimina katika package
ulizoziandaa yagande Kisha tayari kwa matumizi.

NB. Haya anaweza kutumia mtoto wa kuanzia miaka miwili na kuendelea.

UDI WA KUOGEA

UDI huu hutumika kuweka kwenye maji ya kuogea.Maji yanakuwa na harufu nzuri mno, badala
ya kuweka hiriki, au mchaichai weka Udi unukie siku nzima.

MAHITAJI

1. Soap base (Transparent) - 120g

2. Cocoa butter- 30ml

3. Essential oil- 15ml

4. Rangi- 5ml/kijiko cha chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

1. Weka sufuria jikoni kisha weka vipande vya soap base na cocoa butter na acha viyeyuke.

2. Vikisha yeyuka zima jiko.

3. Weka essential oil ( perfume) na changanya vizuri.

4. Kama utahitaji kuweka rangi zaidi ya moja basi gawa mchanganyiko wako kila mmoja weka
rangi unayotaka.

5. Mimina kwenye mold kugandisha


6. Kwa muda wa saa 24 na kuendelea zitakuwa zimeshaganda.

7. Pack kwenye vifungashio vyako tayari kwa matumizi.

NB: Kikopo huuzwa Tsh.1000 I nategemeana na eneo ulilopo.

UTENGENZAJI WA UBUYU WA VIPANDE

Mahitaji

1. Unga wa Ubuyu -kilo moja

2. Sukari-kilo moja Na nusu

3. Radha-nusu kijiko cha chakula

4. Rangi-vijiko 2-3

5. Maji –nusu Lita

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chemsha Maji jikoni weka sukari koroga mpakaiyeyuke kisha weka radha Na rangi koroga

2. Uache mkorogo wako uchemke had uanze kunata nata anza kuweka unga wa Ubuyu huku
ukisonga kama ugali Na kuzidi kuongeza unga mpaka uishe

3. Ukisha changanyika vizuri anza kumimina kwenye chombo cha plastiki ulichoanza kupaka
mafuta ya kula ili usigande ukikauka tandaza vizuri kisha uache ukauke

4. Ukikauka anza kukata vipande uvitakavyo wewe kwa ajili ya kuuza au kula
NB: weka maji zaidi ya robo lita kwa ajili ya akiba kama maji yatakuwa machache unaweka ya
akiba hayo.

UBUYU

MAHITAJI

1. Sukari vikombe 2

2. Maji vikombe 2

3. Nusu kikombe unga wa ubuyu

4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe

5. Kijiko ¼ cha pili pili ya unga

6. Kijiko ¼ cha chumvi

7. Kijiko ¼ cha iliki ya unga

8. Rangi nyekundu au yeyote utakavyopenda.

JINSI YA KUPIKA

1. Katika sufuria, weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe
juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo
lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.
Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo
linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri
kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.

4. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika
ubuyu.

5. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.

CHAKI

Chalk ni bidhaa ambayo imebuniwa kwa ajili ya matumizi ya shule, vyuo n.k

Chalk zinatofautiana kutokana na malighafi inayotumika, Rangi aina ya chokaa, Gypsum


iliyotumika kutengenezea Isiyo na dust

(dustless)

CHALK No.1

Chalk ambayo malighafi yake ni CHOKAA.

Malighafi

1. Chokaa nyeupe 1kg

2. Maji 1lita
3. Rangi kama unahitaji iwe ya rangi

4. Foil paper (mould)

5. Moto.

6. PLASTER OF PARIS (P.O.P)

Hii ni malighafi muhimu sana, na ndio malighafi kubwa inayotakiwa kwa kiwango kikubwa sana
katika utengenezaji wa chaki hizo tunazozizungumzia. Kitaalamu au kisayansi zinaitwa
“Calcium carbonate”. Hii inatengeneza uji mzito na kukauka kwa haraka sana pale
inapochanganywa na maji.

HATUA ZA KUTENGENEZA

1. Chokaa kilo moja na iwe imechekechwa na kupata unga ulio safi, Maji lita moja, Rangi ya
chakula 10 mls.Mchanganyiko huu uchanganywe kwa pamoja na upate uji mzito, koroga kwa
muda wa dakika 15.

2. Weka mchanganyiko wako katika mould ya fowl paper zikate ziwe na shape ya saizi ya chaki
unayotaka ,Weka juani chaki zako mpaka zikauke Zikikauka, toa kwenye foil paper tuziingize
jikoni kama tunavyochoma vyungu na matofali ili kuhahakikisha imeiva ukiishika inaacha vumbi
mkononi na ikidondoka inakatika vipande vingi.

KANUNI ZA KUCHANGANYA CAUSTIC SODA NA MAJI KWA USAHIHI

KANUNI YA KWANZA

1. Caustic Soda Kilo 25 Maji Lita 80

2. Caustic Soda Solution Lita 10 Mafuta Lita 20

Kama Unatumia Hydrometer Unapima Baume 30


NUNI YA PILI KWA VIPIMO VIDOGO 1.CAUSTIC SODA KILO MOJA MAJI LITA 3

CAUSTIC SOLUTION LITA MOJA MAFUTA LITA 2KA

Kwa kutumbukiza hyrometer kwenye caustic solution tupate baume 30 kama itakuwa
imepungua ongeza

Caustic soda kisha koroga kupima tena kama imezidi ongeza maji kisha pima tena

NB: Vipimo hivi kwa wanaotumia hydrometer hata wale wasiotumia hydrometer wanatumia
kutengeneza sabuni.

MOLD NA VIFYATULIO VYA SABUNI

Kuna mold za aina nyingi zipo za chuma ambazo ukihitaji kumwagia mchanganyiko wako
unapaka grisi.

Kuna mold za mbao ambazo ziko ndogo kwa ajili sabuni za tiba za vipande pia zipo kubwa za
sabuni ya mche au magadi

Pia aina ya tatu kuna mold zinaitwa silicon mold kwa ajili ya sabuni za tiba za kuogea

Namna ya kudesign mold inategemea na vipimo vyako vya sabuni ambayo unataka iwe

Mfano mold ya sabuni za magadi urefu wa mche huo ndio uwe upana wa mold urefu na kimo
unakadiria ila upana tu uwe unafanana na mche wa sabuni ambao ulionao kama sampo.
Mfano wa mold mbalimbali

ZA MCHE/KIPANDE SABUN

MAHITAJI
1. Mafuta Lita 20 (mawese,mise)

2. Caustic solution Lita Lita 10

3. Sodium silicate robo Lita

4. Rangi gram 25-30 sio lazima

5. Pafyumu MLS 50 sio lazima

Mfano wa sabuni ya mche

HATUA ZA UTENGENEZAJIHATU

1. Vaaa gloves chukua chombo Cha plastic weka mafuta na pia chukua ndoo weka caustic
solution changanya na sodium silicate koroga ukimaliza
2. Chukua mchanganyiko wenye caustic solution + sodium' silicate nenda kaweke kidogo
kidogo kwenye mafuta huku ukiendelea kukoroga weka rangi na pafyumu koroga

3. Kama unatumia mold ya chuma weka grisi kwenye mold au Kama unatumia mold ya mbao
weka nailoni Anza kumwagia mchanganyiko wako na uache uakuke kwa masaaa kadhaa
ukikauka Anza kukata tayari kwa kupelekea sokoni.

JEDWALI LA KANUNI

SABUNI ZA MAGADI (gwanji)

Ni moja ya sabuni ambazo zinapendwa Sana na kuweza kuteka soko kwa kiasi kikubwa sana.

MAHITAJI
1. Mafuta ya mise Lita 20

2. Caustic solution Lita 10

3. Sodium silicate robo Lita

4. Rangi ya Sabuni 30 gram

Mfano wa sabuni ya Magadi

HATUA ZA UTENGENEZAJI

Mafuta Caustic Sodium Rangi

solution silicate

1 Lita 5 Lita 2.5 Mls 50 5 gm

2 Lita 10 Lita 5 Mls 100 10 gm


3 Lita 20 Lita 10 Mls 200 20 gm

4 Lita 40 Lita 20 Mls 400 40 gm

1. CHUKUA NDOO YA PLASTIKI WEKA MAFUTA PIA

Chukua ndoo nyingine Pima caustic solution Lita 10 yenye BAUME 30

2. Chukua caustic solution weka sodium' silicate kuroga kwa muda wa dakika 2-3 ukimaliza
Anza kumimikia mchanganyiko wa caustic solution na sodium silicate kwenye mafuta huku
ukiwa unakoroga koroga kwa muda Hadi mchanganyiko uchanganyike vizuri

3. Chota uji wako kiasi Kama Lita mbili Hadi tatu weka pemben Pima rangi yako Anza
kuchanganya na uji ule mdogo ulioutenga pembeni.

4. Chukia mchanganyiko wako mweupe Anza kumimina kwenye kibao Cha kufyatulia kidogo na
Kisha unamimina wa rangi ya bluu kiasi unakuwa unafanya hivyo Hadi mchanganyiko wako
wote uishe wa bluu na mweupe uki maliza chukua mti anza kuchoza zig zag au nane juu ya
kibao Cha kufyatulia ukimaliza acha ukauke

5. Ukikauka Anza kukata sabuni yako kwa kufuata ukubwa ambao utakuwa unauhitaji

I ZA MAGADI

MAHITAJI

SABUN
1. Caustic Soda kilo 3 na gram 400

2. Mafuta ya mise lita 20

3. Sodium Silicate robo Lita

4. Maji lita 10

5. Rangi ya bluu vijiko 3

6. Mold ya kufuatilia

Jinsi ya kutengeneza

1. Pima maji Lita 10 Weka Caustic soda 3kg na gram 400 kwenye maji yako Lita 10 kisha
koroga vizuri hadi iyeyuke iache kwa masaa 24.

2. Chukua caustic solution yako uliyoikoroga kiasi cha 10 lita weka sodium silicate koroga
kuelekea upande mmoja.

3. Pima mafuta ya mise/mbosa 20 lita na mimina kwenye caustic solution yako kisha koroga
vizuri. Na haraka haraka.

4. Chota huo uji kiasi ( lita 2 hadi 3} kisha weka rangi yako kwenye ule uji uliouchota pembeni na
koroga vizuri hadi rangi ikolee.

5. Mimina kiasi chako cha uji usio na rangi kwenye mold au box la kugandishia.Anza kumimina
uji wako wenye rangi pembeni ya mold/box lako la kugandishia kuzunguka.

6. Chukua mti wako wa kukorogea na chora namba 8 kwenye uji wako ulioumimina kwenye
mold au box kwa kutumia mti wako wa kuchanganyia hadi yatokee mawimbi ya rangi yako.

NB: Hifadhi uji wako sehemu yenye kivuli na uache wazi ili ugande.sabuni yako inakauka baada
ya masaa 4 hadi 6 tayari kwa kukata.

BATIKI ZA AINA MBALIMBALI

Batiki ni nini?

Ni nguo au kitambaa cha pamba asilimia 100 kilichotiwa rangi kwa kuchora, kugonga, kuchovya,
kunyunyiza au kuchubua.
Historia ya Batiki.

Batiki ilikua kama vazi lililoundwa au kubuniwa nchi za China na India, lakini kutokana na ukuaji
na technolojia inavyozidi kukua ikasambaa mpaka kuingia hapa nchini kwetu na kushika hatamu.
Hivi inavyokwenda wabunifu wengi wameweza kubuni kila aina ya mitindo mpaka kuipa sifa ya
kuingia katika mitindo maalum ya Kitaifa.Ili iwe batiki lazima kuwe na aina fulani ya muundo bila
hivyo itasomeka ni nguo ya kawaida tu.Batiki hutengenezwa kwa kutumia malighafi
kadhaa.Malighafi hizi zote ni hatari na zinatakiwa kutumiwa na kutunzwa kwa uangalifu na mtu
anaetumia basi lazima azijue hatari na jinsi ya kujilinda nazo. La sivyo anaweza kupata madhara
makubwa na hatimae hata kupata vilema au matatizo ya kudumu au hata kifo.

AINA ZA BATIKI

1. Batiki za kuchovya tie and dye

2. Batiki za mshumaa

3. Batiki za kuprint

4. Batiki za kubabua(kublich)

5. Batiki za kufinyanga

BATIKI ZA KUCHOVYA (TIE AND DIE)

Ni aina ya nguo au vazi la asili linayotengenezwa kwa mikono kwa kuweka picha michoro na
urembo mbalimbali.kwa hapa tanzania batiki soko lake kubwa na watu wengi wamejikita
kufanya ujasiriamali huu unawaingizia kipato kikubwa na kuweza kumudu maisha yakitanzania

BATIKI ZA TIE AND DIE

Ni aina ya batiki ya kukunja mikunjo kwa kutumia mkono vilevile tie ni neon la kiingereza lenye
maana ya funga na die ni neno la kiingereza lenye maana chovya hivyo basi ni batiki za kufunga
mikunjo na kuchovya.
Malighafi

1. Cautic soda vijiko vitatu vya chakula

2. Sodium hydrosulphet vijiko vitatu vya chakula

3. Rangi vijiko viwili hadi vitatu vya chakula.

VITENDEA KAZI:

Meza, kitambaa cha pambe, kalamu, uzi, sindano, mkasi, kamba, sufuria kijiko kikubwa, ndoo au
beseni, jiko, vibanio, maski na gloves.

AINA ZA TIE AND DYE.

1. Kushona- chora mchoro wowote ushone, halafu vuta na uzi kwa nguvu.

2. Kufanya- loweka kitambaa kisha tandika kwenye mkeka au nailoni, anza kuvuta kwa
kufinyanga, kisha mwagia dawa.

3. Funga uzi na kamba-kunja mkunjo wowote funga na kamba, tumbukiza kwenye dawa.

4. Kutumia blichi (jiki)- tandika kitambaa kwenye meza halafu mwagia blichi yako uliyoiweka
kwenye chupa na kutoboa mfuniko kwa ajili ya kutoa blich yako kama urembo

Baadhi ya hizi zinaweza kuchanganywa na kupata rangi kama ifuatavyo Red +blue=purple
yellow+blue =green yellow+orange=chungwa green+red=brown=udongo=green dark orange
+blue=combat-rangi ya jeshi
JINSI YA KUTENGENEZA.

1. Chemsha maji ya moto

2. Pima malighafi ya kwanza hadi ya tatu, weka vyote kwenye beseni.

3. Weka maji ya moto lita 2_3, koroga kwa dakika tatu,

4. Chovya kitambaa kwenye rangi acha kwa dakika 15 ili vipoe na kuingia rangi vizuri

5. anika kisha ukimaliza fua na upige pasi, tayari kwa kwenda sokoni

BATIKI ZA MISHUMAA

Mahitaji
1. Vitambaa vya batiki

2. Sponji

3. Rangi vijiko 3

4. Sodium hydrsulphate vijiko 3 vya chakula

5. Caustic soda vijiko 3 vya chakula

6. Mshumaaa

7. Sufuria kubwa

8. Beseni

9. Meza

10. Jiko

11. Mti mrefu

VIFAA KINGA

Gloves

Miwani

Viatu vigumu

Brush

Kiziba pua (barakoa)

koti

Kazi za madawa

A. Sodium
Kazi ya sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje kama itachanganywa na caustic soda.

Madawa haya yana kazi moja ila ikikossekana moja nyingine haifanyi kazi.

B. Mshumaa

Kazi yake ni kuweka nembo ktk nguo na ktk vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye
urembo wa tembo, twiga ,matunda au urembo wowote anaohitaji mtengenezaji.

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Weka mshumaa jikoni ili uweze kuyeyuka ukiyeyuka anza kukonga mshumaa kwenye
kitambaa chako hakikisha unagonga mbalimbali kuruhusu kuweka mshumaa wa pili baada ya
kuweka rangi ya kwanza acha mshumaa wako ukauke.

2. Uwekaji rangi,Chemsha maji ya moto yachemke sana Kisha pima Lita 3hadi 4 pima caustic
vijiko 3, pima sodium vujiko 3 changanya na maji Moto tia rangi kijiko 2-3

Baada ya hapo pima maji lita 6 ya baridi Kisha changanya na mchanganyiko wa madawa awali
kusudi yapoe yawe vuguvugu.

Tumbukiza vitambaa vinee vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuza geuza ili viingie rangi
kwa dkk 20 Kisha suuza kwa maji ya baridi anika

3. Baada ya kukauka weka rangi ya kwanza chukua kitambaa chako chemsha mshumaa anza
kugonga ua lingine kwenye kile kitambaa chemsha maji ongeza sodium hydrosulphate vijiko na
rangi na caustic vijiko 3 koroga ongeza maji lita 5 anza kuchovya vitamba vyako viache kwa
dakika 20 kisha suuza anika vikikauka nenda katoe mshumaa
Namna Ya Kutoa Mshumaa

Chemsha maji yachemke kabisa Kama ya kupikia ugali Kisha tumbukiza kimoja kimoja jikoni ili
kuondoa mshumaa ktk kitambaa, Geuza kwa mti mrefu Kisha suuza kwa maji baridi anika
kivulini na kabla hakijakauka vizuri piga pasi ili kuimarisha rangi.

BATIKI ZA KUBABUA / KUBLICH

Katika kutengeneza batiki za kubabua tunatumia kutengeneza kwa kutumia jiki na kumwagia
kwenye kitambaa au kutumia sponji kuweka ua ambalounalihitaji

Mahitaji

1. Kitambaaa

2. Sodium/calcium hypochlorite vijiko 5

3. Maji nusu lita

4. Sponji au spry container

JINSI YA UTENGENEZAJI
1. Chukua chombo weka maji kisha weka sodium hypochlorite kisha tikisa au koroga hadi
iyeyuke

2. Chukua kitambaa chako tandika chini au kwenye meza anza kunyunyiza yale maji yako yenye
sodium hypochlorite kitaanza kubabuka ukimaliza 3. Chukua kitambaaa kifue na kianike

BATIKI ZA KUPRINT

Hizi ni batiki ambazo unatumia rangi na screen kwa ajili ya kutengeneza batiki hizi

Mahitaji

1. Vitambaa

2. Rangi ya kuprint

3. Screen yenye michoro

4. Spatula ya kuwekea rangi kwenye screen

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua kitambaa tandika kwenye meza au sakafu chukua screen yenye michoro anza
kuweka alama sehemu unazohitaji kuweka

2. Anza kuweka rangi kwenye screen huku ukifuta na kusambaza kwa kutumia spatula.

3. Baada ya hapo anika kivulini ikikauka chukua kitambaa laini weka juu ya batiki anza kupiga
pasi ukimaliza tayari kwa kupeleka sokoni.

BATIKI YA KUPRINT
BATIKI ZA KUFINYANGA

Batiki hizi ni moja ya batiki rahisi kuliko zote hizi kwanza mchanganyiko wake unaandaliwa
kama tie and dye za kuchovya.

MAHITAJI

1. Kitambaa

2. Sodium hydrosulphate vijiko 3

3. Caustic soda vijiko 3

4. Rangi vijiko 3

5. Maji lita 3

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Chukua vitambaa vyako weka kwenye maji kisha kamua viwe na umajimaji kwa mbali anza
kufinyanga kwa kuvuta vuta kwa pamoja ukishamaliza
2. Chukua sufuria weka jikoni weka maji lita 3 yakichemka ipua chukua chombo cha plastiki
weka sodium hydrosulphate ,caustic soda na rangi kisha weka maji yale ya motokisha koroga
ukimaliza

3. Anza kumwagia kidogo kidgo kwenye batiki zako ukimaliza acha zipoe kwa dakika 15 kisha
kunjua kupata batiki anika kivulini ikikauka piga pasi fua tayari kwa kupeleka sokoni.

SABUNI YA UNGA

MAHITAJI:

1. Soda ash 3.3kg.

2. LABSA 650mls.

3. Sodium sulphate 750grams.

4. Nansa 10grams.

5. STPP 750grams.

6. Optical Brightener 20grams

7. Perfume 20ml.

8. Rangi ukipenda{kadiria}

JINSI YA KUTENGENEZA:

1. Pima Soda ash 3.3kg, Mimina Sulphonic acid/LABSA 750grams kisha changanya vizuri.

2. Mimina Sodium sulphate 750grams kisha changanya vizuri. Mimina Nansa 10grams kisha
changanya tena vizuri.

3. Weka Sodium Trip polyphosphate {STPP} 750grams kisha changanya vizuri.


4. Weka Optical brightener 20grams kisha changanya tena vizuri.Weka rangi ukipenda {kadiria}

5. Weka perfume 20mls kisha changanya vizuri.Anika kivulini ikauke vizuri kisha weka kwenye
vifungashio tayari kwa matumizi,

NB: Rangi ya sabuni ya unga si sawa na rangi ya sabuni ya maji na ya sabuni ya maji si sawa na
ile ya Sabuni ya mche

SIAGI YA KARANGA

MAHITAJI

1) Karanga kg 1/4

2) Asali kijiko 1.5 cha chakula

3) Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha chakula

4) Chumvi 1/2 kijiko cha chai (k ama peanut zake hazijakua roasted na chumvi )

5) Chupa yenye mfuniko ya kigae ( kwa kuhifadhia peanut butter yako )

NAMNA YA KUTAYARISHA

1) Ondoa maganda karanga zako

2) Osha vizuri then weka zikauke vizuri

3) Zioke katika oven dakika 30-35 minutes, moto 350F

4) Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1
acha kidogo saga hadi iwe laini

5) Ongeza asali, chumvi na mafuta saga hadi iwe laini... 6) Hifadhi katika chupa yako then weka
kwenye friji tayari kwa matumizi.
LOTION AND CREAM

Malighafi

1. White oil lita 1

2. Stearic acid gramu 100

3. CSA gram 250

4. Cetal alcohol gram 250

5. Pola wax gramu 250

6. Lactic acid mls 100

7. Cetrimide mls 100

8. Salicylic acid gram 50

9. Methyl paraben gram 40

10. Propyl paraben gram 10

11. Glycerine ml 100

12. IPA -150-200 ml

13. Bee wax/ shea butter – gram 50 (sio lazima)

14. Pafyumu – mls 40


15. Kojic acid gram 10 -30 (sio lazima kwa ajili ya weupe zaidi)

KAZI ZA MALIGHAFI

1. CSA –uzito ,ngozi kung,arisha

2. Cetal alcohol –uzito ,kungarisha

3. Pola wax –kiunganishi ,kufanya kuwa nyeupe ,emulsifier

4. Bee wax –kungarisha ngozi

5. White oil- kulainisha malighafi

6. Lactic acid –kutakatisha

7. Proply paraben –kuhifadhi

8. Methly paraben-kuhifadhi

9. Centrimide –kutoa michirizi kwenye ngozi

10. Salicylic acid –kutoa chunusi

11. Grycerine –kurainisha

12. IPA- kuondoa chunusi ,ubaridi

13. Stearic acid –kungaridha ngozi

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1. Weka maji lita moja jikoni pima centrimide iache iyeyuke weka salicylic acid iache iyeyuke
kabisa koroga kisha ipua weka pembeni

2. Chukua sufuria nyingine weka white oil (unaweza kuweka alovera oil /mafuta ya alizeti) kisha
weka stearic acid ikiyeyuka pima CSA weka kwenye sufuria, weka cetal alcohol iache iyeyuke
vizuri weka pola wax.

3. Weka menthly parabene na propyl paraben (ukiwa na bee wax unaweka wakati huu)

4. Chukua maji lita mbili weka kwenye mchanganyiko ule wa mwanzo kwenye beseni

5. Zima jiko chukua mchanganya wa pili anza kuchanganya na mchanganyiko wa mwanzo kisha
koroga weka maji kisha endelea kukoroga vizuri

6. Weka IPA na grycerine weka kisha koroga vizuri

7. Weka lactic acid kisha koroga weka pafyumu

Kumbuka

1. Rangi unaweka kwenye white oil

2. Vitamin c gram 50 /mls 50 unaweka kwenye mchanganyiko wa kwanza

3. Ukitaka iwe cream acha maji lita 8 ukitaka lotion weka maji hadi lita 15

LOTION YA PARACHICHI

Lotion hii kwaajili ya kuifanya ngozi iwe ya asili( Natural soft skin).

Na haichubui hata kidogo.

MAHITAJI

1. Parachichi zilizoiva vizuri- 3 au 4

2. Almond oil - 100mls/kichupa 1

3. Vitamin E - matone 4 / ya vidonge

4. Shea butter - mls 250

5. Aloe vera velly - 50mls

6. Rose water - kijiko 1

7. Preservative - kijiko 1 cha chai

UTENGENEZAJI

1. Chukua parachichi menya kisha saga kwenye blenda mpaka upate juice nzito na laini kabisa.
(smooth juice).
2. Kisha yeyusha shea butter na itie kwenye rojo au juice la parachichi na ukoroge vizuri
mchanganyiko huo.

3. Baada ya hapo tia Almond oil kichupa kimoja au 100 mls na kisha endelea kukoroga.

4. Tia Aloe vera gelly 50mls kisha endelea kukoroga.

5. Chukua vitamini E (for skin) dondoshea matone 4 au unaweza tumia ya vidonge 4 na ukoroge
vizuri.

6. Tia rose water kijiko 1 na ukoroge.

7. Weka essential oil (perfume) uipendayo kijiko 1 na ukoroge vizuri.

8. Mwisho utaweka Organic preservative ili kuifanya lotion yako ikae kwa muda mrefu bila ya
kuharibika.

9. Weka katika vifungashio tayari kwa matumizi.

MATUMIZI:

Lotion hii ni kwaajili ya kung'arisha na kuifanya ngozi iwe soft.(soft natural skin).

-Lotion hii ni nzuri kwa wenye ngozi kavu itawafanya ngozi zao kuwa na unyevu nyevu. (very
soft).

LOTION YA LIMAO(LEMON

Lotion hii ni nzuri kwa wenye sura au ngozi yenye mafuta.Huondoa chunusi, mabaka na kuifanya
ngozi yako ipendeze.

MAHITAJI

1. Micro wax -½ kg

2. White oil - ½ au 1 lita

3. Paraffin wax - ½ kijiko

4. Rangi - kijiko 1 cha chai

5. Perfume - kijiko 1

6. Limao – 10
7. Flavour(lemon) -Vijiko 3 vya chai

NB: PARAFFIN WAX - Unaweza kuongeza kama utahitaji lotion yako isiwe nzito.

UTENGENEZAJI

1. Chukua sufuria kubwa ya maji weka jikoni.Maji yakianza kuchemka chukua sufuria nyingine
ikalishe juu ya maji.(double boiler).

2. Weka micro wax kisha iache iyeyuke,

3. Weka parrafin wax kisha nayo iache iyeyuke kabisa.

4. Kisha weka white oil na baada ya hapo anza kukoroga taratibu kwa dakika kadhaa.

5. Kamua malimao yako upate juice.Kisha mimina juice hiyo ndani ya mchanganyiko wako na
ukoroge vizuri.

6. Weka rangi 10 gm au kijiko 1 na ukoroge kwa dk 3 hadi 5

7. Weka ladha/ Flavour vijiko 5 vya chai

8. Weka Perfume ya Lemon na koroga vizuri.

9. Weka preservative kijiko 1 cha chai na ukoroge vizuri.

10. Fungasha na upeleke sokoni.

WHITENING & SOFTENING BODY SERUM

Hii ni kwaajili ya kung'arisha.

MAHITAJI

1. Mafuta ya nazi(pure) - 50mls

2. Vitamin E - vijiko 2

3. Almond Oil- vijiko 2

4. Rose water - vijiko 4/ 40mls

5. Preservative- 10 mls

6. Carot - 1 au 2
7. Manjano - kijiko 1 cha chakula

8. Maziwa - 30mls/ vijiko 3

9. Alóe vera gelly - 10mls

10. Gryceline - nusu kijiko/ 5mls

11. Asali - kijiko 1

12. Perfume - 10 mls

HATUA ZA UTENGENEZAJI

1 Andaa chombo chako(Bakuli) safi na kavu. Weka Almond oil, Vitamin E, na Gryceline kisha
changanya vizuri mchanganyiko wako kisha weka kando(pembeni).

2 Chukua chombo kingine (Bakuli) kisha weka maziwa, asali, rose water na Aloe vera gelly kisha
koroga vizuri mpaka vichanganyikane vizuri.

3 Kwenye mchanganyiko wa hatua ya pili(wa maziwa) tia manjano, preservative, kisha koroga
vizuri na weka pembeni.

4 Chukua mafuta ya nazi ya asili kabisa ambayo hayajachakachuliwa yaweke katika sufuria
kisha weka jikoni yapate moto alafu tia karoti iliyosagwa kaanga mpaka karoti ibadilike rangi
iwe ya brown na mafuta yawe ya Orange. Kisha zima moto na epua.

5 Chukua bakuli lenye maji tumbukiza sufuria yenye mchanganyiko wa mafuta ya nazi na karoti
itumbukize ielee uku mfuta yakipoa ila yasipoe sana.

6 Chukua kitambaa safi chuja mafuta ya nazi yatengane na mafuta ya karoti.

7 Kisha chukua bakuli lenye Almond oil, Gryceline na vitamin E mimina kwenye mchanganyiko
wa mafuta ya nazi na karoti kisha koroga vizuri kwa dk 5 hadi 10.

8 Chukua bakuli lenye mchanganyiko wa maziwa, asali, rose water na Aloe vera gelly changanya
au mimina kwenye bakuli kenye mchanganyiko wa awali( hatua ya saba) kisha koroga vizuri kwa
dk 10-15.

9 Kisha chukua Essntal perfume tia alafu koroga vizuri.

10 Baada ya hapo weka katika vifungashio tayari kwa matumizi.

COFFEE BODY SCRUB (1kg )


Sasa hii ni jinsi ya kutengeneza coffee scrub bila kutumia sugar (sukari) endapo utataka
kutengeneza emulsifying coffee sugar scrub maji hayahusiki. Hivyo hatutakuwa na kitu kinaitwa
water phase.

MAHITAJI

1. (Waterphase) 2. Maji 820g

4. Cap B 100g 5. sles 20g

3. Xgum 6g

Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel .

MAHITAJI

(Oil Phase)

1. Stearic acid 5g 2. Cetyl alcohol 30g

3. Coconut oil 20g 4. Salicylic acid 1.5g

5. Coffee powder 2g 6. Potassium sorbate 5g

Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro (usiweke salicylic acid coffee powder potassium
sorbate.

JINSI YA KUTENGENEZA.

1. Chukua sufuria kubwa weka maji kiasi na weka jikoni.

2. Kisha chukua sufuria mbili ndogo zenye malighafi na uziweka ndani ya sufuria kubwa jikoni
zielee katika maji yanayochemka.

3. Weka vipima joto katika sufuria zenye malighafi hakikisha hazigusi sufuria.

4. Joto likisoma 75°c zima jiko na chukua malighafi za sufuria moja uchanganye na za kwenye
sufuria nyingine kwa pamoja.

5. Kisha weka kwenye blenda na uanze ku blend. Joto likipungua weka botanical powder
( Coffee powder) na uchanganye vizuri kwa blenda.
6. Joto likishuka zaidi chini ya 40°c au iwe nyuzi 40°C utaanza kuweka potassium sorbate na
salicylic acid na uchanganye vizuri kwa kutumia kijiko au spatula na sio blenda.

Mpaka hapo Scrub itakuwa tayari, utaipack vizuri tayari kwa matumizi.

SUGAR SCRUB

(Mfano wa Pili wa Scrub)

Ukisikia emulsifying, maanake hazihusishi maji (hakuna water phase / hakuna malighafi zenye
asili ya maji. Unatengeneza kilo moja ambayo ni sawa na gram 1000 za scrub

MAHITAJI

1. Cocoa butter 200g 2. Mango butter 100g

3. Cetyl alcohol 100g 4. Ewax 100g

5. Avocado oil 440g 6. Orange oil 40g

7. Germa 10g 8. Lemon essential oil 30g

9. Sukari 1000g

Note: Sio lazima itumie butter nilizotumia na mafuta niliyotumia unaweka kuweka mengine
kulingana na matakwa yako scrub isaidie nini kwenye ngozi.

UTENGENEZAJI

1. Weka vyote kwenye sufuria kasoro essential oil germa na sukari

2. Bandika sufuria yenye maji kiasi kubwa kuliko ya mwanzo jikoni. Tumbukiza sufuria yenye
malighafi iwe inaelea. Acha malighafi ziyeyuka dakika 20 (uwe na saa), kisha epua

3. Peleka kwenye freezer acha igande mpaka uone Tabaka limejitengeneza dakika 20 .

4. Changanya kwa kutumia blender /hand mixer spidi kubwa hadi uone imekuwa
nzitonzito(heavy) na laini(soft)dakika 10

5. Weka essential oil ,germa kisha changanya vizuri kwa kutumia kijiko kisafi cha plastic au
spatula na sio hand mixer.
Pack kwenye vifungashio vyako tayari kwa matumizi au kupeleka sokoni.

SCRUB YENYE EXFOLIANT ZAIDI YA MOJA NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA . PIA
SITATUMIA MAJI (SCRUB ITAKUWA EMULSIFYING )

EXFOLIANT NINAZOCHAGUA NI manjano na mchele. Nitahakikisha niko na fine powder zake

Mahitaji kutengeneza kilo moja ya scrub

1. Shea butter 100g 2. Cocoa butter 200g

3. Cetyl alcohol 100g 4. Ewax 100g

5. Olive Oil 440g 6. Orange Oil 40g

7. Germa 10g 8. Clove essential Oil 30g

9. Manjano 500g 10. Mchele 500g

UTENGENEZAJI

1. Chukua sufuria kubwa weka maji kiasi na weka jikoni.

2. Chukua sufuria nyingine weka malighafi zote isipokuwa exfoliant, Germa(preservative), na


essential oil.Hivi havita ingia jikoni.

3. Weka sufuria hiyo yenye malighafi ndani ya maji kwenye sufuria kubwa iliyopo jikoni na acha
ielee juu ya maji mapaka malighafi ziyeyuke.(dk 20)

4. Epua mchanganyiko wako na weka katika freezer, mchanganyiko ugande na kutengeneza


tabaka kisha utaitoa.(huchukua dk 20)

5. Kisha utaitoa katika freezer na uta blend mpaka mchanganyiko wako uwe mzito na laini.(dk
10)

6. Ukishakuwa laini utaweka zile malighafi zingine ambazo ni Germa, essential oil, na exfoliant
yako.- Changanya vizuri kwa kutumia kijiko cha plastic au Spatula na sio mixer au blenda tena.

Mpaka hapo itakuwa tayari, weka kwenye vifungashio, weka lebo na peleka sokoni.
NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA PIA NITATUMIA MAJI SCRUB HII ITATAKUWA NA
VIPENGELE VIWILI WATERPHASE NA OIL PHASE EXFOLLIANT

NILIZOCHAGUA KUTUMIA ni nyanya na tango Hakikisha una unga wa nyanya na tango


MAHITAJI (kutengeneza kilo moja) waterphase (kipengele cha maji na malighafi zenye asili ya
maji)

1. Maji 820g 2. Xgum 6g

3. Cap B 100g 4. Sles 20g

Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel kipengele cha pili oil phase mahitaji.

1. Citric acid 5g 2. Cetyl alcohol 30g

3. Coconut oil 6g 4. Salicylic acid 1.5g

5. Tango 8g 6. Nyanya 8g

7. Potassium sorbate 5g

Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro salicylic acid exfoliant zako ambazo ni tango na
nyanya preservative yako ambayo ni potassium sorbate.

JINSI YA KUTENGENEZA

1. Kwanza kabisa hakikisha una exfolliant zako kwenye mfumo wa unga unga (powder)

2. Weka malighafi zote zenye asili ya maji katika sufuria moja.

3. Kisha chukua malighafi zenye asili ya mafuta (Oil phase) na weka katika sufuria nyingine.

4. Kisha utachukua sufuria nyingine kubwa utaweka maji kiasi kidogo na utabandika jikoni.

5. Kisha utatumbukiza sufuria zako mbili zenye malighafi ndani ya sufuria kubwa lenye maji.

6. Weka vipima joto ndani ya hizo sufuria zenye malighafi( Hakikisha hazigusi sufuria)

7. Joto likifika 75°C ipua na changanya malighafi zako katika chombo kimoja.

8. Joto likiwa chini ya 40°C utaweka Exfolliant na preservative na utachanganya tena vizuri.

Mpaka hapo Scrub yako itakuwa tayari.Weka katika vifungashio, weka Lebo na upeleke sokoni.
Active ingredient: hapa tuna maanisha zile kemikali ambazo zinachangia kwenye kutibu
matatizo ya ngozi. Kwa mfano SALICYLIC ACID hutibu chunusi.

KAZI ZA BAADHI YA EXFOLIANT:

1. NYANYA - Hutumika kuondoa au kupunguza makunyanzi au mikunjo usoni au katika ngozi.

- Hulinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua.

2. TANGO - Kuondoa chunusi na madoa.

3. COFFEE - Huondoa michirizi.

- Kufanya ngozi kuwa laini.

4. MANJANO - Kung'arisha ngozi na kuondoa makovu.

5. MCHELE - Husaidia sana kwa watu wenye ngozi za mafuta (Hubalance mafuta yaliyozidi)

- Hung'arisha

- Kuleta rangi moja.

Kwahyo utachagua Exfolliant yyte kulingana na mahitaji yako.

TILES & SINK CLEANER

Malighafi

1. Sless ¼ kg

2. Hydrocloric acid 6 lt

3. Rangi njano kiasi

4. Perfume 50 MLS

5. Maji Lita 20

UTENGENEZAJI:
1. Weka sless katika ndoo yenye ujazo wa zaidi ya Lita 20 kisha koroga ongeza chumvi kidogo
Kama gram 150 tu ili isaidie kuyeyusha sless kisha koroga vizuri Hadi kupata creamy na Kisha
tia maji kidogo kidogo huku ukikoroga kuelekea upande mmoja, endelea kuongeza maji kidogo
kidogo Hadi maji yaishe huku unakoroga.

2. Weka hydrocloric acid yote kidogo kidogo Hadi iishe huku unaendelea kukoroga .

3. Chukua rangi iloweke kando kisha koroga na itie kidogo kidogo kadiria rangi isizidi iwe kiasi
kidogo tu.

4. Mwisho tia pafyum koroga vizuri na acha kwa saa 24 Kisha fungasha peleka sokoni.

5. Mtumiaji ahakikishe anavaa gloves na miwani wakati wa kutumia hii dawa ya kunga' risha
sink , rashia eneo husika kisha sugua kwa sabuni baada ya dakika 60-90.

Naamini kitabu hiki kitakuwa kimekusaidia sana katika kujifunza mambo mbalimbali ambayo
yataharakisha safari yako ya mafanikio. Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza kwa bidii ili
upate matokeo makubwa zaidi. Kumbuka kuwa una uwezo mkubwa sana ndani yako na kama
ukiamua kuufanyia kazi basi hakuna kitu ambacho kitakuzuia. Nakutakia mafanikio katika ndoto
yako

You might also like