Fursa Sequip - 2024

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

FURSA YA ELIMU BILA MALIPO

ELIMU YA SEKONDARI KWA UFADHILI WA MRADI WA SEQUIP - AEP


Secondary Education Quality Improvement Project – Alternative Education Programme

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Mkoa wa Dar es Salaam kwa


kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Ilala na Manispaa za Kigamboni,
Ubungo, Kinondoni na Temeke; tunawatangazia wananchi wote fursa ya
Elimu ya Sekondari bila malipo kwa wasichana wenye umri baina
ya miaka 13 hadi 21; waliokatisha masomo yao walipokuwa shule za
sekondari za serikali; kutokana na sababu mbalimbali kama vile ujauzito,
uhaba wa usafiri, migogoro ya kifamilia, magonjwa, ndoa za utotoni,
ugumu wa maisha, kuhamahama, mila na desturi kandamizi n .k.

Elimu hii inatolewa kupitia Mfumo wa Elimu ya Sekondari kwa Njia Mbadala katika vituo vifuatavyo:-
NA. JINA LA KITUO MAHALI KILIPO MANISPAA NA. JINA LA KITUO MAHALI KILIPO MANISPAA
1 MBEZI INN Mbezi Inn Sekondari Ubungo 6 N.C.I TEWW - Makao Makuu Ilala

2 CHAMAZI Chamazi Sekondari Temeke 7 KITUNDA Kitunda Sekondari Ilala

3 MBAGALA Mbagala Sekondari Temeke 8 KINYEREZI MPYA Kinyerezi Mpya Sekondari Ilala

4 TURIANI Turiani Sekondari Kinondoni 9 KIWALANI S / M Kiwalani Ilala

5 KIDETE Kidete Sekondari Kigamboni

Fomu za udahili zinapatikana Ofisi ya Mkufunzi Mkazi (M) D’Salaam na


pia katika Vituo vya Mradi wa SEQUIP vilivyobainishwa hapo juu.
(Muone Mratibu –“Coordinator” wa Kituo cha SEQUIP au Mkuu wa Shule).

Mlengwa atakapofika kituoni atapewa FOMU YA UDAHILI ambayo


ataijaza kisha atakabidhi fomu na picha zake (Passport size) MBILI
(zikiwa na jina lake kamili nyuma); katika kituo alichochagua kusomea.
Fomu zijazwe na kurejeshwa mapema kabla ya tarehe 05/01/2024.

SIMU kwa maelekezo zaidi: 0754341933, 0754599291, 0787876170, 0717085649 au 0745841451

N.B. Wahitaji wengine wa Elimu ya Sekondari ( wa kiume na wa kike wenye


umri wowote) ambao hawakidhi vigezo vya kufadhiliwa na mradi wa
SEQUIP; wataruhusiwa kusoma, ila kwa kuchangia gharama nafuu.
WAHI MAPEMA NAFASI ZA UFADHILI NI CHACHE
Imetolewa na Mkufunzi Mkazi – TEWW – Mkoa wa Dar Es Salaam

You might also like