Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 112

MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MWANGA
wa
Kwa Shule Za Upili

Duncan M. Were Lutomia


(Mhariri)

i
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

© Duncan M. Were Lutomia


Tel: +254724018681
Email: weredan88@yahoo.com

Haki zote zimehifadhiwa; hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kuchapa au


kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini ya mwandishi.

Kimechapishwa mara ya kwanza 2017

ISBN 978-9966-100-13-9

Mpangilio na Uchapishaji

Double Shasa Limited


P.O Box 667-50100, Kakamega
Perus Abura road, Opposite Kenya Power Oice
Tel: +254 709 746 650
Website: www.doubleshasa.com
Email: doubleshasaltd@gmail.com

Ingawa kila juhudi imefanywa kuhakikisha kuwa kitabu hiki kimeboreshwa zaidi, makosa machache yanaweza kutokea.
Hivyo basi usisite kutufahamisha ili tufanye marekebisho.

ii
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Yaliyomo
Shukrani…………………………………………………….................….….…. iv
Dibaji…………………………………………………………….................….… vi
Sura ya kwanza
Mapisi ya ushairi wa Kiswahili…………………………………................…….. 1
Dhana ya ushairi……………………………….………………..............………. 3
Sifa za ushairi…………………………………..…………………..............……. 3
Umuhimu wa ushairi………………………………………………............….… 3
Changamoto za ufundishaji na usomaji wa ushairi……………….................…. 4
Jinsi ya kutatua changamoto hizi……………………………………..............… 4
Sura ya pili
Istilahi mbalimbali zinazotumika katika ushairi…………………….................. 5
Sura ya tatu
Migao/kategoria kuu za ushairi……………………………………...............….. 8
Mashairi ya jadi…………………………………….………………................…. 8
Mashairi huru………………………………………………………...............…. 9
Sura ya nne
Bahari za mashairi………………………………………………….............….. 11
Sura ya tano
Uhakiki wa mashairi…………………………………………….............…….. 26
Sura ya sita
Idhini/uhuru wa kishairi…………………………………………...........……. 31
Sura ya saba
Mkusanyiko wa mashairi……………………………………………............… 34
Msururu wa maswali ya KCSE tangu 2008- 2016
KCSE 2016..................................................................................................... 66
KCSE 2015……………………………………………………………........… 70
KCSE 2014……………………………………………………………........… 72
KCSE 2013…………………………………………………………….......…. 74
KCSE 2011…………………………………………………………….......…. 76
KCSE 2010……………………………………………………………........… 79
KCSE 2009……………………………………………………………............ 80
KCSE 2008…………………………………………………………...........…. 83

Majibu ya mitihani ya KCSE………………………………………............... 84

Marejeleo………………………………………………………………....… 102

iii
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shukrani
Natoa shukrani za dhati kwa wazazi wangu Silas Were na Pamela Adhiambo,
kwa kuenzi masomo, mke wangu Wanjiru, kwa uvumilivu wake, Dkt. George
Lutomia na mwandani Binti Elvera Tumaini, ushauri walonipa ulinifaa pakubwa.
Jamii ya Shule ya Upili ya Wasichana ya St.Mary’s Mumias, hususan Mwalimu
Mkuu Bi. Kwendo Adema Rosemary. Sitowasahau Bw. Ofunya Charles Wangatia,
Mkuu wa Idara-Shule ya Upili ya Wasichana ya St. Mary’s Mumias na Bw. Issa
Barasa- St. Peter’s Mumias Boys, kwa kukubali kupitia na kukihakiki kitabu hiki,
na wengine wote mlochangia katika kukifanikisha kitabu hiki, Karima awajalie!

Ningependa pia kutoa shukrani jazili kwa makampuni ya uchapishaji ya Oxford


University Press, Acacia Stantex, Vide-Muwa, Longman, Phoenix na Kenya
Literature Bureau kwa kunukuu kazi kutokana na machapisho yao.

iv
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Tabaruku
Toleo hili ni tunu maalum kwa mamangu Pamela Adhiambo.

v
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Dibaji
Kwa miongo kadhaa iliyopita, waandishi wengi wa vitabu vya Kiswahili
wamekuwa wakishughulikia kipengele cha sarui na kusahau kazi za kifasihi,
ushairi ukiwa mojawapo. Kuikia leo hii, ushairi haujatiliwa maanani mno licha
ya kuwa ni sehemu mojawapo inayotahiniwa katika hadhi ya kitaifa katika
karatasi ya tatu. Utanzu wa ushairi umepitia mabadiliko mengi tangu uanze
kufanyiwa utaiti.
Vipo vitabu ambavyo hutumiwa katika kufundishia ushairi wa Kiswahili katika
shule za sekondari, ingawaje ni dhahiri shahiri kwamba bado pana haja ya
kitabu ambacho kitaoana na kazi za waandishi wengine ili kukidhi mahitaji ya
wanafunzi katika udurusu wao wanapojiandaa kufanya mitihani ya kuhitimu
masomo ya sekondari.
Mwanga wa Ushairi kwa Shule za Upili ni kitabu ambacho kimeandikwa ili
kuziba mwanya ulioshamiri katika ufunzaji na ujifunzaji wa ushairi. Kitabu hiki
kinaangazia masuala yote muhimu yanayohitajika katika uwanja huu wa ushairi.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa utaalamu wa kutosha ili kuwawezesha wanafunzi
kufanya maandalizi bora wanapojitayarisha kwa mtihani wa Kiswahili hasa
ushairi katika KCSE. Kitabu hiki vilevile ni cha kipekee kwa kuwa kinashirikisha
maswali na majibu ya mitihani ya K.C.S.E tangu mwaka wa 2008-2016, hivyo
basi kumpa mtahiniwa nafasi bora zaidi ya kujiandaa vilivyo kabla ya mtihani.
Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitachangia pakubwa katika kuendeleza
ubunifu wa kutunga mashairi na vilevile kuboresha usomi na ufundishaji wa
ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.

Duncan M. Were
Idara ya Kiswahili
Shule ya Upili ya Wasichana ya St. Mary’s, Mumias
Januari, 2017

vi
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MWANGA WA USHAIRI
Uga ninaufungua, niruhusu ukumbini,
Kishairi nafungua, walio bara na pwani,
Ushairi kuangua, na kutopendwa barani,
Ugumu wake ni upi, ushairi kutopendwa?

Kwa waja walohoia, katika enzi za kale,


Ushairi kuiia, kwa kogofya kina wale,
Mabingwa wakajiia, shairi kuzikwa mle,
Ugumu wake ni upi, ushairi kutopendwa?

Nawatunuku diwani, ashiki wa mashairi,


Bidii iso kifani, kuukuza ushairi,
Na wengi wanothamini, na kuenzi ushairi,
Ugumu wake ni upi, ushairi kutopendwa?

Tama nalifunga buku, tarifa yangu yakoma,


Wengi ninawatunuku, si bakuli si hazama,
‘Shairi kwenea huku, ‘frika na dunia nzima,
Ugumu wake ni upi, tuipende ushairi!

Limetungwa na Hawa Wakhayanga


Kidato cha 4 (2017)
Shule ya Upili ya Wasichana ya St. Mary’s Mumias

vii
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Limenikubali Liwe hai

Penzi Kivumvu Letu Maadui

Moyoni Hakiniandami Penzi Niwakwepe

Furaha Daima nitambimbirisha Letu

Nina Wahasiri

Nimekwepa Penzi

Manung’uniko Kote

Silalamiki Nidatie

Kamwe Mtetezi

Moyoni Wangu

Kinyongo Kweli

Sina Kesharudi

Naapa Nitulie

Mimi

Karibuni wapenzi wa ushairi


Limetungwa na:
Nancy Muthini (Kidato cha 4) 2016
Shule ya Upili ya Wasichana ya St. Mary’s, Mumias

viii
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

1
DHANA YA USHAIRI
Shabaha

Kuikia mwisho wa kidato cha nne, mwanafunzi aweze:

a. Kusoma kwa kina na kuelewa mashairi mbalimbali


b. Kuchanganua, kuchambua na kuhakiki kazi ya ushairi
c. Kujibu maswali kwa ufasaha kwa kutumia lugha ya kishairi
d. Kuwa mbunifu na kuweza kutunga shairi lake kwa kuzingatia kaida
zinazotawala utunzi wa mashairi

MAPISI YA USHAIRI WA KISWAHILI


Si bayana ni lini hasa utanzu wa ushairi ulipoanza ingawaje imebainika kuwa
ndio utanzu mkongwe na ulio na historia ndefu kati ya tanzu nyinginezo za
fasihi. Tarehe kamili ya kuchimbuka kwa ushairi ingali imegubikwa katika utata.
Utanzu huu wa ushairi unakisiwa ulitokana na nyimbo za hapo jadi. Utanzu
wa ushairi umepitia matapo/vipindi vinne katika kukua na kusambaa kwake.
Vipindi hivi kama wanavyoeleza Kitula King’ei na Amata Kemoli, katika Diwani
yao ‘Taaluma ya Ushairi’ ni kama vifuatavyo:
a) Tapo/Kipindi cha urasimi mkongwe
Dhana ya urasimi huwa na maana ya mkusanyo wa mikondo ya kiikra au
kimtazamo ambayo chanzo chake ni sanaa na utamaduni wa Wayunani na
Warumi. Matapo ni vipindi mbalimbali vya kihistoria ambavyo fasihi au sanaa
kwa jumla imevipitia. Pia huweza kuelezwa kama mikondo au makundi makuu
ya kinadharia ambayo yametawala katika fasihi au sanaa katika nyakati maalum.
Katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa ushairi ulianza kuandikwa.
Upande wa mashairi kimaandishi mshairi aliyejulikana sana ni Muyaka bin
Haji (1776-1970). Ingawa kuna malenga wengine wa kipindi hiki, mashairi yao
bado hayajakusanywa na kuwekwa katika vitabu. Mashairi yanayotambulika
mno katika tapo hili ni pamoja na Utenzi wa Hamziya ambao uliandikwa
na Sayyid Abdarus, Utenzi wa Al-Inkishai wake Sayyid Abdalla, Utenzi wa
Tambuka ulioandikwa na Mwengo na Utenzi wa Mwanakupona. Utenzi huu wa
Mwanakupona ndio wa kipekee uliotungwa na mwanamke na ulioacha athari
kubwa katika wakazi wa Pwani Kaskazini hasa katika maisha yao kindoa.

1
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Katika kipindi hiki pia, nyingi ya mashairi yalikuwa yenye maudhui ya kidini
hasa dini la Kiislamu. Watunzi wengine wa kipindi hiki ni Bwana Mataka, Ali
Koi, Muhammad Kijumwa na Hemedi Abdallah.
b) Kipindi cha utasa (1885-1945)
Huenda kipindi hiki killitwa hivi kwa sababu maandishi machache yaliandikwa
wakati huu.Huu ulikuwa ni wakati wa vita vya dunia, na mataifa mengi
yakigawana Afrika. Sheria za utunzi wa mashairi zilianza kutozingatiwa.
c) Kipindi cha urasimi mpya (1945-1960)
Mashairi yaliyotungwa katika kipindi hiki aghalabu yalikuwa yanafuata kanuni/
arudhi. Washairi waliotawala kipindi hiki ni Amini Abedi, Shabaan Robert,
Mathias Mnyampala miongoni mwa wengine mashuhuri. Wao walikuwa na
itikadi kuwa ili utungo uitwe shairi, sharti liweze kuimbwa, hivyo lazima liwe
na urari wa vina, mizani inayolingana pamoja na masuala mengine ya kiarudhi.
Kipindi hiki pia kilishuhudia washairi chipukizi wapya kuanza kuibuka.
d) Kipindi cha sasa (1967 kuendelea)
Hiki ni kipindi cha leo hii ambapo pana mgogoro kati ya wanamapokeo na
kundi nyingine la wanamapinduzi.Wanamapokeo wanashikilia mitazamo ya
jadi kuwa shairi lazima lifuate arudhi, nao wanamapinduzi wanapinga suala hili.
Kulingana na wao, muhimu ni ujumbe ambao shairi linabeba bali si muundo wa
shairi. Mashairi mengi wanaotunga wanamapinduzi ni mashairi huru. Washairi
wa kipindi hiki ni pamoja na Euphrase Kezilahabi, Kithaka wa Mberia, Alamin
Mazrui, Mugyabuso Mulokozi kati ya wengineo.
Mwandishi Kezilahabi pia ametoa maoni sawa na haya kuhusu hatamu
mbalimbali ambazo Ushairi wa Kiswahili umepitia. Naye vipindi hivi ameviita
muhula katika Diwani yake. Kezilahabi anaeleza kuwa katika muhula wa
sasa, uhuria umetawala. Idadi ya washairi imeongezeka, idadi ya mashairi pia
imeongezeka na ubora wa mashairi kuimarika. Katika kipindi cha sasa, ushairi
umekuwa sanaa ya umma na mambo yafuatayo yanabainika wazi:
 Mashairi huru ni mengi
 Mashairi yanahusisha drama/maigizo
 Ushairi wa vijana unaosaili yaliyopo katika jamii
 Ushairi umebadilika kuendana na hadhira, hivyo basi unachanganywa
na ngoma
 Ushairi umeendelea katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEKNOHAMA)

2
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Dhana ya Ushairi
Wanafunzi wengi hushindwa kueleza maana ya ushairi. Dhana ya ushairi
inaweza kufafanuliwa kwa njia kadhaa.
Ushairi ni mojawapo wa utanzu wa fasihi andishi unaoelezea mawazo mazito
kuihusu jamii na ulio na mpangilio mahsusi wa maneno yenye mtiririko, lugha
ya mkato na urembo fulani wa aina yake.
Ni sanaa inayotambulishwa na mpangilio maalum wa vifungu ambao una
mdundo maalum na aghalabu hutumia lugha ya mkato.
Shairi ni utungo wa kisanaa ambao hutumia lugha teule na kushirikisha
mpangilio maalum wa maneno ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa. Ni tungo
za kishairi zenye maudhui maalum yanayomhusu mwanadamu na tabia zake.
Sifa za ushairi
Sifa ni upekee fulani unaojitokeza katika kazi yoyote ile. Ushairi huwa na upekee
wa aina yake ukilinganishwa na kazi nyinginezo za fasihi. Hivyo basi utanzu wa
ushairi huwa na sifa kuu zifuatazo:
 Hutumia lugha teule na ya mkato.
 Hutumia tamathali tofauti tofauti za usemi.
 Sio lazima ufuate kaida za kisarui.
 Lugha iliyotumiwa huweza kuibua hisia, yaani hugusa moyo wa
anayesoma.
 Huwa na mpangilio maalum kuanzia kwa vina, mizani, mishororo na
beti.
 Huweza kukaririwa ama kuimbwa
 Huelezea mambo yanayohusiana na imani za watu katika jamii.
Umuhimu wa ushairi
Mashairi huwa na umuhimu anuwai katika jamii. Baadhi yazo ni pamoja na:

 Kukuza usanii wa lugha.


 Kuelimisha jamii kuhusiana na masuala fulani.
 Kuburudisha wasomaji.
 Kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu katika jamii.
 Kukuza utamaduni.
 Kuhamasisha na kuzindua watu mfano kuhusu kazi.

3
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Changamoto za ufundishaji na usomaji wa ushairi


Utaiti unaonyesha kuwa kuna changamoto nyingi katika ufundishaji na
usomaji wa ushairi. Changamoto hizi huenda ikawa ndizo huchangia kudorora
kwa matokeo ya wanafunzi katika somo la ushairi. Hebu tuangazie baadhi ya
changamoto hizo:
 Wanafunzi wengi wana mtazamo hasi kuwa ushairi ni dhana ngumu.
 Kuna baadhi ya walimu ambao pia wana mtazamo hasi kuhusu ushairi.
 Walimu kutojiandaa vyema katika somo hili.
 Upungufu wa vitabu teule vya ushairi katika shule zetu.
 Walimu kutowapa wanafunzi wao mazoezi ya kutosha ya ushairi.
 Walimu kutotambua mashairi yanayoendana na viwango vya
wanafunzi, kilugha na kimaudhui.
 Istilahi zinazotumiwa katika ushairi ni nyingi sana.
Ni vipi changamoto hizo zitatatuliwa?
 Wanafunzi na baadhi ya walimu wabadilishe mtazamo wao kuhusu
ushairi na waichukulie kama masomo mengine
 Ufundishaji wa ushairi ulioratibiwa.
 Kutoa ufafanuzi sahili kuhusu dhana ya ushairi na sifa zake.
 Mashairi mepesi na ya kuwavutia wanafunzi yateuliwe.
 Usomaji wa ushairi mara kwa mara ili kupevusha viwango.
 Wanafunzi washiriki utunzi wa mashairi mepesi.

4
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

2
ISTILAHI ZA USHAIRI
Istilahi mbalimbali zinazotumika katika ushairi
Tumeeleza chini ya sifa za ushairi kuwa utanzu huu huwa na upekee fulani. Hili
vilevile linadhihirika tunapoangazia istilahi za kishairi. Mwanafunzi bora ni
yule anayeweza kutumia istilahi za kishairi anapochambua na kuyajibu maswali.
Istilahi za kishairi ni misamiati bainifu ambazo hutumika kurejelea masuala ya
ushairi. Istilahi hizi ni kama zifuatazo:
Mizani – ni idadi ya silabi au sauti zinazotamkika katika kila mshororo wa
ubeti. Mashairi mengi ya arudhi aghalabu huwa na mizani 16 ingawaje huwa
siyo lazima. Rejelea mifano inayofuata inayoonyesha mizani katika mshororo.
Ku ru ki a si ku zu ri, ma ne no mu si ru ki e, (mizani 16)
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16
Mu ta ku ja zu sha sha ri, ma ko nde mu ya bu gi e, (mizani 16)
Vina – ni silabi za mwisho wa kila kipande cha mshororo. Huainishwa kama
vina vya ndani/kati ama vina vya nje/mwisho. Vina huweza kufanana ama
kutofautiana. Iwapo shairi lina vipande ziadi ya viwili, vina huainishwa kutegemea
vipande kwa mfano vina vya ukwapi, vina vya utao, vina vya mwandamizi na

• Huleta mdundo, ridhimu na hata burudani kwa msomaji.


vina vya ukingo. Vina huwa ni muhimu kwa sababu zifuatazo:

• Hutambulisha na kupambanua utanzu wa ushairi kwani vina


hutumika tu katika mashairi.
Hebu tazama mfano unaofuata.
Kurukia si kuzuri, maneno musirukie,
Mutakuja zusha shari, makonde muyabugie,
Mukimbie kwa ghururi, kama kuku mukimbie,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.

Wasemapo majabari, maneno musirukie,


Hasa walio jeuri, kamwe musikurubie,
Ndondi zitawaaziri, na kwa Mola mutubie,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
(Abedi K.A)
Katika mfano huo, vina vya ndani ni ‘ri’ ilhali vina vya nje ni ‘e’
5
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kipande (vipande) – ni kijisehemu katika mshororo. Mshororo huweza kuwa


na kipande kimoja, vipande viwili, vitatu au hata vinne.
Ukwapi – ni kipande cha kwanza katika mshororo.
Utao – ni kipande cha pili katika mshororo.
Mwandamizi – ni kipande cha tatu katika mshororo.
Ukingo – ni kipande cha nne katika mshororo.
(ukwapi) , (utao) , (mwandamizi) , (ukingo)
, , ,
, , ,
, , ,
Mshororo (mishororo) – ni mstari au sentensi moja katika ubeti. Mistari
hii inapowekwa pamoja hujumlisha ubeti. Ni kigezo hiki ambacho hutumika
kuainisha aina za mashairi. Mfano wa hapo juu ni shairi la mishororo minne
katika kila ubeti.
Mwanzo –ni mshororo wa kwanza katika ubeti. Pia huitwa fatahi ama
kifungua.
Mloto – ni mshororo wa pili katika ubeti.
Mleo – ni mshororo wa tatu katika ubeti.
Mshata (mishata)- ni mshororo katika ubeti wa shairi ambao haujakamilika
haswa kimaana na hutegemea mwingine unaofuata ili kupasha ujumbe.
Idadi ya mizani pia huweza kuwa si kamilifu ikilinganishwa na mishororo
mingine.
Sifa za mishata
• Huweza kuishia kwa alama za mdokezo.
• Huwa fupi
• Huwa na mizani michache ikilinganishwa na mishororo mingine
• Haikamiliki kimaana yaani haitoi ujumbe kamili.
• Humhitaji msomaji kuwaza jinsi ya kuukamilisha.
• Humlazimu msomaji kusoma mshororo mwingine ili kupata ujumbe.
Mistari kifu/toshelezi- ni mishororo inayojitosheleza kimaana bila
kutegemea mishororo mingine. Vilevile idadi ya mizani huwa kamili katika
mishororo yote.
Kibwagizo/kiitikio/mkarara/kipokeo – Aghalabu huwa ni mshororo wa
mwisho katika ubeti ambao umerudiwarudiwa katika beti zote.

6
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Mfano ufuatao unaonyeesha mwanzo, mloto, mleo na kibwagizo.


Imezukapo hatari, hii leo nikwambie, (mwanzo)
Msemaji mhodari, uhodari ajitie, (mloto)
Kapambana na jabari, la kufanya asijue, (mleo)
Maneno musirukie, wasemapo majabari. (kibwagizo)
Kabla hayajakiri, jitu limgeukie,
Likamzaba hodari, naye mbio akimbie,
Likamkazia shari, na mbio asizijue,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
(Abedi K.A)

• Huwa ni kiini cha shairi yaani hubeba maudhui.


Umuhimu wa kibwagizo

• Kupitia kwa kibwagizo tunaweza kupata kichwa cha shairi iwapo

• Husisitiza ujumbe wa shairi.


hakikutajwa.

• Huonyesha mwisho wa ubeti.


Kiishio/kimalizio- mshororo wa mwisho katika ubeti. Mshororo wenyewe
huwa ni tofauti katika beti zote.
Ubeti (beti) – ni jumla ya mishororo iliyowekwa pamoja na ambayo
hujitosheleza kimaana na hubeba hoja ama ujumbe na hubainishwa na kuwepo
ama kutokuwepo kwa kanuni kuu za utunzi wa tungo.
Shairi lililonukuliwa hapo juu lina beti mbili. Kila ubeti una mishororo minne.
Utoshelezo - ni ile hali ya mtunzi kuandika ujumbe ambao unaeleweka
kinagaubaga na ambao unaweza kujisimamia kivyake katika kila ubeti wa shairi.
Yaani kila ubeti hutoa taarifa yake kikamilifu pasi na kutegemea ubeti mwingine
kukamilisha ujumbe uliokusudiwa.
Arudhi - ni sheria au kanuni zinazotawala utunzi wa mashairi. Suala hili la arudhi
haswa hujitokeza sana katika mashairi ya jadi. Kanuni hizi ni kama vile: urari
wa vina, mpangilio maalum wa beti, mishororo sawa katika kila ubeti, mizani
inayojitosheleza katika kila mshororo, vipande sawa katika kila mshororo n.k.
Muwala- ni kule kutiririka kwa mawazo au ujumbe na hata fani kutoka
hatua moja hadi nyingine katika shairi. Ujumbe hufululiza vyema kwa njia ya
kueleweka kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
Bahari- ni mikondo tofauti tofauti ya mashairi kutegemea jinsi shairi lenyewe
lilivyoundwa. Bahari za mashairi zimejadiliwa kwa kina katika sura tofauti.
Diwani- hurejelea mashairi mengi yaliyokusanywa katika kitabu kimoja.
Malenga- ni neno ambalo hutumiwa kuashiria mtunzi wa mashairi.
Manju- ni mwimbaji wa mashairi.

7
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

3
KATEGORIA ZA MASHAIRI
Migao/Kategoria kuu za mashairi
Mashairi huweza kugawika katika kategoria mbili kuu:
1) Mashairi ya jadi
2) Mashairi huru
Mashairi ya jadi.
Mashairi haya pia huitwa mashairi ya kimapokeo au ya kiarudhi. Aina hii ya

• urari wa vina
mashairi hufuata kaida za utunzi wa mashairi. Kanuni hizi ni kama vile:

• mpangilio maalum wa beti


• mishororo sawa katika kila ubeti
• mizani inayojitosheleza katika kila mshororo
• vipande sawa katika kila mshororo n.k.
Malenga wanaoshikilia msimamo huu huitwa wanamapokeo. Mashairi
yasiyofuata sheria hizi hujulikana kama guni. Mfano wa shairi la kiarudhi ni
kama lifuatalo.
Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini
Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?
Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
Naja nije rudi papo, panigedeme mgando
Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo
Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
(Limenukuliwa)
Tunaainisha shairi hili kama la jadi kwa sababu:
• Lina urari wa vina; ubeti wa 1 vina ni……...‘ni’…….......‘ndo’
ubeti wa 2 ........................‘pi’................‘ndo
ubeti wa 3 ........................‘po’...............‘ndo’
8
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI



Lina mishororo sawa (minne) katika kila ubeti


Mizani inajitosheleza katika kila mshororo (mizani 16)


Vipande ni sawa (viwili, yaani ukwapi na utao) katika kila mshororo
Lina beti tatu zinazojitosheleza.
Mashairi huru/za kisasa
Ni kategoria ya mashairi yasiyozingatia kanuni za utunzi. Hii ina maana ya
kwamba kanuni zilizoorodheshwa chini ya mashairi ya kimapokeo siyo lazima
zifuatwe. Aghalabu mashairi haya huzingatia maudhui kwa kina. Kila malenga
huwa na mtindo wake tofauti wa kuwasilisha kazi yake. Wanaoshikilia msimamo
huu nao huitwa wanamapinduzi. Mashairi haya pia huitwa mapingiti/mavue/
masivina/zuhali/za kimapinduzi. Hebu tazama shairi lifuatalo.
Nimeyaandika maneno haya
kwa niaba ya,
Mamilioni wasio malazi
Wazungukao barabarani bila mavazi
Wabebao vifurushi vilivyo wazi,
… milki yao ya maisha.
Kwa niaba ya:
Maelfu wanaovuma bila haki
Wiki baada ya wiki
Leo sumu au spaki
Leo kamba au bunduki
Na kwa wale wanasubiri kunyongwa
Kwa niaba ya
Vijana walio mtaani
Wale mayatima na maskini
Wazungukao mapipani
Kila pembe mjini
Kuokota sumu kutia tumboni
Kujua bila kujua
’ili kupata kuishi.
Kwa niaba ya:
Wakongwe wasiojiweza
Walao chakula kilichooza
Wachukuao choo wakijipakaza
Pole pole wakijiangamiza
Katika vyumba vyao
Baridi na giza
Kwa saba hawan watazama
Wala wauguza

9
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Mbona tukasema kuwa shairi hilo ni huru? Ni kwa sababu;


• Halina urari wa vina
• Mizani si sawa katika mishororo yake
• Idadi ya mishororo katika beti ni tofauti

• Huwa hayazingatii idadi sawa ya mishororo katika beti.


Sifa za mashairi huru

• Aghalabu huwa hayana urari wa vina.


• Hayana idadi maalum ya vipande katika mishororo.
• Huwa hayana idadi sawa ya mizani katika mishororo.
• Nyingi yazo huwa na kipande kimoja tu.
• Hutumia mistari mishata.
• Hayana kibwagizo bali huwa na kituo.
• Hutumia takriri kwa wingi.

10
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

4
BAHARI ZA MASHAIRI
Mojawapo wa maswali yanayotahiniwa katika ushairi ni kueleza bahari ya
shairi. Je nini maana ya bahari? Bahari za mashairi ni neno ambalo hutumiwa
kurejelea zile mikondo mbalimbali za mashairi kwa kutegemea sura ya shairi
lenyewe. Bahari ni aina mojawapo ya tungo za mashairi ambazo huainishwa
kwa mujibu wa sifa zake. Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa
vigezo mbalimbali ambavyo vimeangaziwa hapa chini. Vigezo hivyo ni kama
vifuatavyo:
 Kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti
 Kulingana na idadi ya vipande katika mshororo
 Kulingana na vina
 Kulingana na mpangilio wa maneno
 Kulingana na mizani
Kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti
Aina za mashairi
Mashairi huwa ni ya aina mbalimbali. Ili kueleza shairi ni la aina gani, kigezo cha
idadi ya mishororo katika kila ubeti ndicho hutumiwa. Kwa kuzingatia kigezo
hiki, tunapata aina zifuatazo za mashairi.
Tathmina/umoja – ni shairi lenye mshororo mmoja kaika kila ubei.
Mashairi ya aina hii hayapaikani kwa wingi. Vielelezo vifuatavyo vinaashiria
aina hii ya shairi.
1._________________________, _________________________
2._________________________, _________________________
3._________________________, _________________________
4._________________________, _________________________
5._________________________, _________________________
Tathnia/uwili – ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti. Mashairi
haya ingawaje yapo, lakini pia kwa uchache. Tazama vielelezo vifuatavyo;
1_________________________, _________________________
_________________________, _________________________
2_________________________, _________________________
_________________________, _________________________
3_________________________, _________________________
_________________________, _________________________
11
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

4_________________________, _________________________
_________________________, _________________________
Mfano huo unaonyesha shairi la beti nne, mishororo miwili katika kila ubeti na
kisha vipande viwili katika kila mshororo.
Tathlitha/utatu/wimbo – ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti.
Shairi la aina hii wakati mwingine pia huitwa wimbo. Tazama shairi lifuatalo;
1. Wakale metenda mengi, milele ya kukumbuka,
Walioanzisha misingi, ambayo yaaminika,
Waleo hutupingi, baadhi tungekenka.

2. Wakale metuongoza, njia zilizo nyooka,


Ukulima walianza, mvua zinapoika,
Waleo twajipoteza, kuiaga wasioigika.

3. Wakale wenye makelele, ya kukabili mashaka,


Walovumbua mchele, ubwabwa leo twabwika,
Si wa kale walolele, mithili ya wana paka.

Malenga wa Vumba
B. Amana Uk.63,O.U.P 1982

Tarbia/unne – ni shairi lenye mishororo minne kaika kila ubei. Mashairi


mengi ambayo yametungwa huwa ni ya aina hii. Mfano ni kama ufuatao;
Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki,
Kwa kweli haaminiki, hila ameicha ndani, la wazi ni unaiki,
Ukweliwe haaiki, njama zake zi moyoni,usimwone ni raiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake,ni hatari kama nyoka.
Wengine watakuua,wakiona una pesa,hata zikiwa kidogo,
Hizo kwao ni maua,hupupiwa zikatesa,wakizifuata nyago,
Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo,


Mtu akiwa mtukutu, tanuna mtimani,kwalo lako tekelezo,
Tamko lake “Subutu”, kuondoa tumaini, na kukuulia wazo
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
(Limenukuliwa)

12
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Takhmisa/utano – ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti.


Rejelea mfano ufuatwao;
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!
(Abdilatif Abdalla)
Tasdisa/usita – ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti. Tazama
shairi linalofuata ambalo pia wakati mwingine hujulikana kama tashlita.
Ewe hisia!
Umeniamshia ndoto niloisahau zamani
Umelimsha mwangu moyoni
nyimbo ya kale
na mdundo usomvutia
ila hayawani wa mwangu rohoni.
Tulia sasa tulia.
Hebu tulia ewe hisia ulo mtimani.
Nakataa katu kusisimka
kwa sauti yako laini
Kwani njia zetu ni panda
daima hazioani
Umesubutu vipi kuniita
kutoka mwako ngomeni
ulimosahauliwa tangu zamani
Basi yawache maombolezi yako yaso maoni,
yawateke hao mashujaa wa kale
watu walo kaburini.
(Limenukuliwa)
Katika shairi hili, kuna beti tatu. Kila ubeti una mishororo sita.
Tasbia/usaba – ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti. Tazama
mfano wa hapa chini.
1________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
13
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Naudi/unane – ni shairi lenye mishororo minane katika kila ubeti.


1________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
Telemania/utisa – ni shairi lenye mishororo tisa katika kila ubeti.
1________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
Ukumi – ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti. Pia shairi hili
huitwa ushuri.
1________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________

14
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Soneti- ni shairi lenye mishororo kumi na minne katika kila ubeti.


1________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
________________________, ________________________
Kulingana na idadi ya vipande katika mshororo
Kipande ni kijisehemu katika mshororo. Mshororo huweza kuwa na
kipande kimoja, vipande viwili, vitatu au hata vinne. Kutokana na kigezo
hiki, tunapata bahari zifuatazo za mashairi.
a) Utenzi
Ni bahari ambapo shairi huwa na kipande kimoja katika kila mshororo. Mengi
ya mashairi haya huwa ni marefu sana. Mashairi haya aghalabu huwa na mizani
zisizozidi 12 katika mshororo na huzungumzia maswala mazito kama vile siasa,
dini na ndoa. Mfano wa utenzi ni kama vile Utenzi wa Mwana Kupona. Mfano
wa utenzi ni kama ufuatao:

Nina machache mabwana,


Kwa nudhumu nitanena,
Na wala shaka hayana,
Napenda kuyaandika.

Sababu tumezidia,
Kuacha ya asilia,
Kazi ilotimilia,
Ambayo imetukuka.

Iwapo kazi hupati,


Usipotewze wakati,
Rudi shamba kata miti,
Na magugu kuyakata.

15
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Haraka tukaze kamba,


Tukimbilie mashamba,
Tukaipande migomba,
Na mimea ya nafaka.

Ukishajijua wazi,
Kuwa wewe huna kazi,
Yapunguze matembezi,
Kuzurura ni mashaka,.

Haya sahibu mwendani,


Sizurure mitaani,
Litie jembe mpini,
Uwache kuhangaika.

Ni kalamu mfukoni,
Suti na tai shingoni,
Twautaka ukarani,
Mashamba twayaepuka.

Tunapokaa mezani,
Shamba atalima nani,
Kisha tutakula nini,
Inataka kukumbuka.

Ni bure wanaosema,
Kudharau ukulima,
Na hali dunia nzima,
Ukulima wasiika.
(Limenukuliwa)
b) Mathnawi
Ni bahari ambapo shairi huwa na vipande viwili katika kila mshororo yaani
ukwapi na utao. Shairi lifuatalo linaonyesha mfano wa bahari hii ya shairi.
KILA MCHIMBA KISIMA
1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,
Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
16
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,


Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima,
Upate njema daraja, duniani na kiyama,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
(Musa Mzenga)

c) Ukawai
Ni bahari ambapo shairi huwa na vipande vitatu katika kila mshororo yaani
ukwapi, utao na mwandamizi. Tazama mfano ufuatao.
HAKI
1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
Watukoroisha, tusikuandame, kila penye kitu,
Mbona watugwisha, miba ituchome, kwenye huu mwitu,
Tutokwe na utu!
2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa,
Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
Haki twashangaa!
3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,
Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,
Usifanyekatu!
(Suleiman A. Ali)

4. d) Bantudi/Tuo
Ni bahari ambapo shairi lina vipande vinne katika kila mshororo yaani ukwapi,
utao, mwandamizi na ukingo. Hebu tazama vielelezo vifuatavyo vinavoonyesha
mfano wa bahari hii ya shairi.
(ukwapi) (utao) (mwandamizi) (ukingo)
______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________

______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________
______________,________________,_______________, _______________

17
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kulingana na vina
Vina ni silabi za mwisho wa kila kipande cha mshororo. Huainishwa kama vina vya
ndani/kati ama vina vya nje/mwisho. Vina huweza kufanana ama kutofautiana.
Kutokana na kigezo hiki, bahari zifuatazo za mashairi zinadhihirika wazi.
a) Mtiririko
Katika bahari hii, shairi huwa na vina vya kati/ndani na vilevile vina vya nje
ambavyo havibadiliki katika utungo mzima. Hii ina maana kuwa vina vya ndani
vinafululiza katika beti zote na vilevile vina vya nje pia vinafululiza katika beti
zote. Shairi lifuatalo linaelezea mfano wa shairi katika bahari hii.
Ndege akiwa angani, usiseme wangu mie
Mngoje atuwe chini, na ndipo mgombanie
Lakini yupo hewani, tama isikwingie
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Ndege apaa angani, sigombee kivulie
Mnapigana machoni, mwagombea uzurie
Mwalizana kama nyani, matunda mwagombeae
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Shika awe mkononi, ndipo ukajivunie
Umshikapo mwilini, chukua kajifugie
Kama utavyo moyoni, kufuga ama mwachie
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
(Mathias Mnyapala)
b) Ukara
Bahari hii ya shairi huwa na vina vya kipande kimoja ambavyo havibadiliki
katika utungo mzima, lakini vina vya kipande kingine vinabadilika kutoka ubeti
hadi mwingine. Hebu tazama vielelezo vifuatavyo.
_________________________sa, ________________________ta
_________________________sa, ________________________ta
_________________________sa, ________________________ta

_________________________sa, ________________________la
_________________________sa, ________________________la
_________________________sa, ________________________la

Katika hicho kielelezo cha hapo juu, vina vya ndani ambavyo ni ‘sa’ ndivyo
havibadiliki lakini vina vya nje vinatofautiana kutoka ubeti hadi ubeti. Zingatia
mfano huu wa pili hapa chini ambapo sasa vina vya kati vinabadilika kutoka
ubeti hadi ubeti ilhali vina vya nje havibadiliki.
18
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

1. Wakale metenda mengi, milele ya kukumbuka,


Walioanzisha misingi, ambayo yaaminika,
Waleo hutupingi, baadhi tungekenka.

2. Wakale metuongoza, njia zilizo nyooka,


Ukulima walianza, mvua zinapoika,
Waleo twajipoteza, kuiaga wasioigika.

3. Wakale wenye makelele, ya kukabili mashaka,


Walovumbua mchele, ubwabwa leo twabwika,
Si wa kale walolele, mithili ya wana paka.
Malenga wa Vumba
B. Amana Uk.63,O.U.P 1982
c) Ukaraguni
Ni bahari ya shairi ambalo vina vyake vya ukwapi, utao, mwandamizi au ukingo
huwa vinabadilika baina ya beti, yaani vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi
mwingine. Hii ina maana ya kuwa vina vya ndani na vya nje huwa ni tofauti
katika beti zote. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha mfano wa shairi katika bahari
hii.
MAISHA UHUSIANO MWEMA
Maisha kwa mwanadamu, ma’na yake ni kuishi,
Tangu siku ya Adamu, hadi ile ya mazishi,
Maisha hutugharimu, kupata kila utashi,
Maisha uhusiano, mwema katika jamii.

Tuko katika maisha, yaliyo na kila tabu,


Tuko tunayaendesha, tofauti na mababu,
Yote tunayadumisha, kila mtu kwa wajibu,
Maisha uhusiano, mwema katika jamii.

Tuko kwenye hali ngumu, ya uchumi kimaisha,


Ni wachache wanadamu, nuru wamefanikisha,
Baadhi ubinadamu, nadra kutuonyesha,
Maisha uhusiano, mwema katika jamii.
(Charles Mloka, Diwani ya Mloka.)

19
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kulingana na mpangilio wa maneno


Kwa kuzingatia kigezo hiki cha mpangilio wa maneno, kunaibuka bahari
zifuatazo za mashairi.
a) Kikwamba
Katika shairi la bahari hii, neno moja huchukuwa nafasi maalum katika ubeti.
Neno lenyewe hujirudiarudia. Linawezakuwa mwanzoni mwa mshororo,
katikati au hata mwisho ilimradi neno hilo limechukuwa nafasi fulani katika
mshororo. Pia linaweza kuwa neno la kwanza katika mishororo yote ya ubeti
ama utungo wote mzima. Sasa tazama mfano ufuatao unaoonyesha mfano wa
shairi katika bahari hii.
NIMO
Nimo ndimo mi nilimo, simo simostahili,
Nimo niwajibikamo, simo mwenye ujahili,
Nimo nikusudiamo, simo wanamodhalili,
Nimo na nitakikamo, simo nami kwa thakili,
Nimo kwa kina na kimo, simo kwa wasiobali,
Nilimo ndimo.

Nimo nimuchunguamo, simo mnamodekezwa,


Nimo nimuikirimo, simo nilimodumazwa,
Nimo haki munyimwamo, simo mnamotukuzwa,
Nimo namo msimamo, simo mnotumbuizwa,
Nimo nayo yaliwamo, simo mwa kuteterezwa,
Nilimo ndimo.
(Mahiri Mwita)
Katika mfano wa juu, neno ‘nimo’ limetumika kutanguliza mishororo yote
katika beti zote mbili.

Tazama mfano huu wa pili.


Mke_________________________ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________

Mke________________________ _ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________
_____________________________ , _____________________________
20
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kielelezo hicho nacho kinaashiria neno moja ambalo ni ‘mke’ limetumika


kutanguliza mshororo wa kwanza katika kila ubeti katika utungo mzima. Mfano
huo pia unaashiria bahari ya kikwamba.
b) Pindu/nyoka/mkufu
Katika bahari hii ya shairi, kina cha kibwagizo, ama kipande kizima, ama
mshororo mzima wa mwisho wa ubeti mmoja unachukuliwa ili kuwa mwanzo
wa ubeti unaofuata. Zingatia vielelezo vifuatavyo vinavyoonyesha mfano wa
bahari hii ya shairi.
___________________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, ____________________mzigo

Mzigo______________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, _____________________beba

Beba_______________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, ____________________cheza

Kulingana na hicho kielelezo, neno la mwisho katika mshororo wa mwisho wa


kila ubeti ndio umetumika kutanguliza mshororo wa kwanza wa ubeti unaofuata.
Tazama mfano huu wa pili wa kielelezo tofauti lakini bahari sawa.
___________________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, kila jogo anapowika asubuhi

Kila jogo anapowika asubuhi, ________________________


___________________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, mwanamke anapaswa kuamka

Mwanamke anapaswa kuamka, ________________________


___________________________, ________________________
___________________________, ________________________
___________________________, heri shuguli za kukamilika
Kulingana na mizani
a) Msuko
Ni bahari ya shairi ambalo huwa na kituo au kibwagizo kifupi kikilinganishwa
na mishororo iliyotangulia. Idadi ya mizani ya mshororo huo huwa ni chache

21
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

mno ikilinganishwa na mishororo mingine. Shairi la hapa chini ni mfano bora


wa bahari ya msuko.
Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?
Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo
Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo
Naandika!
Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo
Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!
Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo
Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo
Naandika!
Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo
Naandika!
(Limenukuliwa)
b) Kikai
Mashairi katika bahari hii huwa na mikondo mingi. Huwa na mizani sita kwa
nane, nne kwa nane au nane kwa tano.
6a, 8b au 4a, 8b au 8a, 5b
6a, 8b 4a, 8b 8a, 5b
6a, 8b 4a, 8b 8a, 5b
6a, 8b 4a, 8b 8a, 5b
Bahari nyinginezo za ushairi
 Sakarani
Huwa ni mchanganyiko wa bahari mbalimbali katika shairi moja. Kwenye ubeti
mmoja, kunakuwa na bahari tofauti, kwa mfano ubeti wa kwanza ni wa aina ya
tathlitha, ubeti wa pili ni wa takhmisa n.k. Hebu tutazame kielelezo kifuatacho.
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________

22
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________, _________________________
__________________________
__________________________
__________________________
__________________________
__________________________
__________________________
Hapa, ubeti wa kwanza una mishororo mitatu, ubeti wa pili una mishororo
mitano, ubeti wa tatu mishororo ni minne ilhali ubeti wa nne una mishororo
sita. Hivyo basi kuna bahari mbalimbali katika utungo mmoja.
 Ngonjera
Ni shairi la majibizano. Tofauti na tungo nyinginezo, ngonjera hukaririrwa,
haziimbwi. Ngonjera hutambuliwa kwa kuwepo kwa wahusika wanaojibizana
katika utungo. Pia huambatana na vitendo. Kwa mfano, ubeti wa kwanza mzazi
akazungumza kisha ubeti unaofuata mwanawe akamjibu. Zingatia shairi hili.
Babu: Jina hili limevuma , mjini shambani pia
Gazetini wanasema, mara nyingi hutokea
Nashindwa pa kutuama , makelele yamejaa
Ukimwi ninauliza , kitu hiki kitu gani?
Bibi: Sihangaike bwanangu, jambo hilo kutuhusu
Dunia ina mizingu, shika yanayotuhusu
Mambo mengi chunguchungu, ni vigumu kudurusu
Ukimwi nimesikia, kila mtu yuataja
Babu: Nikifungua radio, matangazo yazagaa
Kenya nayo hata hio, Tanzania yaongea
Jihadhari na kinoo, Ukimwi ukisambaa”
Ukimwi ninauliza, Kitu hiki kitu gani?
Bibi: Jambo umeshikilia , Ukimwi sijui nini?
Shika njia kimbilia , Uliza wanake nini?
Mashaka yamezidia , Waweweseka ndotoni?
Nyuma tusijiachie , mashaka kujiwekea
Babu: Ni vyema tuutambue, twende kwa wanaojua
Akili watufumbue, tufahamu ya dunia.
Nyuma tusijiachie, mashaka kujiwekea.
Ukimwi ninauliza, kitu hiki kitu gani?

23
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Bwana afya: Sijidanganye mzee, ukimwi hauna dawa.


Na mabingwa waendee, kufanyiza na daawa.
Wataushidwa umee, ukukate kama buwa.
Ni ugonjwa wa hatari , jiepushe na ukimwi
(S . KUVUNA)
 Malumbano
Ni shairi lenye mjadala juu ya jambo fulani, yakiwa ya kupinga, kuunga mkono,
kuonya au kusifu. Huwa ni mashairi ya mafumbo, kwa hivyo kwa njia ya kishairi,
malenga kadhaa hufumbiana ama kujibizana. Aghalabu huwa ni mashairi
mawili.
 Masivina
Ni bahari la shairi lisilo na urari wa vina katika mishororo yake. Hii ina maana
kuwa vina vyake vyote aidha vya kati au vya nje vinatofautiana baina ya
mishororo. Vielelezo vifuatavyo vinaelezea mfano wa bahari hii ya shairi.
Matapeli
salamu naanza mimi, niwajuvye walimwengu
Muyatege masikiyo, uneni pate lipuka
Pia mutiye manani, asilani musipuze
Kina matapeli ndugu, hutokea kama njozi.
Wanooitwa matapeli, hao watu walaghai
Wonapo pato unalo, kukupoka hutamani
Wataja kufanya zuzu, japo wewe mashuhuri
Kina matapeli ndugu, hutokea kama njozi.
(Kuvuna S)
 Taabili
Ni shairi ambalo limetungwa kwa nia ya kumsifu mtu aliyeaga dunia.
 Mandhuma
Ni bahari ya shairi ambalo upande mmoja (ukwapi) hueleza hoja au huuliza
swali na kisha upande wa pili (utao) hutoa jibu au suluhu ya swali hilo.
 Kisarambe
Ni shairi ambalo haswa limejikita kwa maudhui ya kidini. Huweza kuitwa pia
kasida.
 Mavue
Ni aina ya mashairi yasiyofungika na sheria zozote za kiarudhi kama vile
utoshelezi wa vina na mizani.
 Sabilia
Ni shairi ambalo halina kibwagizo bali huwa na mstari wa kituo/kiishio/
kimalizio.

24
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Togoo
Ni aina ya shairi ambalo limetungwa kwa kusudi la kusiia uzuri wa mahali, mtu
au kitu fulani.
 Kumbukizi
Ni aina ya shairi ambalo huwakumbusha watu kuhusu matukio mahsusi katika
jamii. Matukio haya yaweza kuwa ya kihistoria, kidini au hata kishujaa. Kwa
mfano ujio wa Rais wa Marekani nchini Kenya, ujio wa Papa Mtakatifu (2015)
ni matukio ya kihistoria.

25
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

5
UHAKIKI WA MASHAIRI
Uhakiki wa mashairi (Namna ya kuchambua mashairi)
Ili kuyachambua mashairi, ni lazima kuzingatia mambo muhimu yafuatayo;
 Dhamira
 Maudhui
 Muundo
 Lugha
a) Dhamira
Mara si haba, wanafunzi hukumbana na swali hili…‘Eleza dhamira ya shairi hili.’
Dhamira ni lengo kuu ambalo malenga huwa nalo anapoitunga kazi yake. Lengo
la mtunzi linaweza kuwa kuelimisha jamii, kuikosoa jamii, kutahadharisha,
kufariji, kuhamasisha n.k Maneno mengine ambayo huweza kutumika badala
ya dhamira ni kama vile lengo, nia, kusudi, azma.
b) Maudhui
Suala la maudhui ni muhimu sana katika uchambuzi wa mashairi na hata kazi
nyinginezo zozote za fasihi. Maudhui ni ujumbe mkuu unaowasilishwa katika
kazi ya fasihi. Maudhui huweza kuwa kama vile ya ndoa, migogoro, elimu,
matabaka, ukengeushi n.k
c) Muundo
Ni kawaida vilevile wanafunzi kuulizwa…‘Eleza muundo wa hili shairi.’
Muundo ni mjengo, umbo au sura ya shairi. Umbo hubainishwa kwa kuonekana
bayana kama alivyoandika mtunzi. Mwanafunzi anapolijibu swali hili anastahili
kuangalia shairi na kuandika tu anayoyaona. Hastahili kuikiria kwa kina ili
kuandika anayoyaona.
Ili kueleza muundo wa shairi, mwanafunzi anafaa kuzingatia mambo
yafuatayo;


Je shairi lina beti ngapi?


Je shairi lina mishororo mingapi katika kila ubeti?


Je shairi lina vipande vingapi katika kila mshororo?
Je shairi lina vina vya kati na vya nje, na kuna urari wa vina au
la?
26

MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI


Je idadi ya mizani ni ngapi katika kila kipande au mshororo?
Shairi lina kibwagizo au kituo? Iwapo lina kibwagizo, basi nakili
kibwagizo moja kwa moja
d) Lugha
Matumizi ya lugha na viambajengo vyake ni muhimu sana katika kufanikisha
uchambuzi bora wa mashairi. Jinsi malenga mmoja anavyotumia lugha ni tofauti
sana na jinsi malenga mwingine atakavyoitumia. Kipengele hiki huchunguza
jinsi mtunzi ametumia tamathali za usemi. Lugha pia huendeleza maudhui ya
shairi. Tamathali hizi ni pamoja na;
 Tashbihi/mshabaha- ni mbinu ya lugha ambapo vitu viwili
hulinganishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Kwa ufupi,ni ulinganisho
isiyo wa moja kwa moja kwa kutumia vilinganishi kwa mfano: mithili
ya, kama, ja na sawa na. Tazama mfano huu:
Juma ni mrefu mithili ya/ja mlingoti.
 Uhaishaji/uhuishi/tashihisi- ni mbinu ambayo vitu visivyo na uhai
hupewa sifa za kibinadamu. Mfano: Kaburi likammeza mzima mzima.
 Misemo na nahau- ni kauli fupifupi ambazo hutumika kutoa maana
nyingine pasi na maana iliyotumika. Misemo huwa haitumii vitenzi
kwa mfano: mkono birika- mchoyo, mkono mrefu-mwizi n.k. Nahau
hutambulishwa kwa matumizi ya vitenzi kwa mfano: kula kalenda-
fungwa jela, chungulia kaburi- karibia kifo n.k
 Takriri/anafora- mbinu ya kurudiarudia neno,tukio au mawazo Fulani.
Takriri huweza kuwa za aina mbalimbali kama vile
Takriri sauti- sauti fulani hurudiwarudiwa.
Takriri neno- neno/kifungu cha maneno fulani hurudiwarudiwa,
Takriri mawazo- mawazo fulani hurudiwarudiwa.
Takriri muundo/usambamba ambapo muundo fulani wa
kisintaksia hurudiwarudiwa. Malenga hutumia takriri hususan
kusisitiza ujumbe.
 Maswali balagha/mubalagha- huwa ni maswali yasiyohitaji majibu.
 Tanakuzi- pia huitwa ukinzani. Hapa mawazo yanayokinzana hutumiwa
pamoja katika sentensi moja. Kwa mfano; baada ya dhiki faraja, mpanda
ngazi hushuka, nazama nakuibuka.
 Tanakali za sauti- mbinu hii pia hujulikana kama onomatopeia.
Maneno yanayoiga sauti au hali fulani hutumika. Mfano kuanguka
majini chubwi.
 Methali- huwa ni misemo ya hekima na ambayo maana yake imefumbwa.
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya
methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa
zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema
27
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi


kuwa kitambulisho chake. Mbinu iliyotumika katika uundaji wa istilahi
hizo za majina ni ile ya kuunganisha viambishi awali vya maneno
yanayopatikana katika kila kikundi. Majina hayo yanayopendekezwa ni

 Ukimea- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali kama anwani.


kama yafuatayo:

 Ukimemo- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali moja.


 Ukimenu- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali nusu.
 Ukimembi- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali mbili (au

 Ukimeka- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali kama kauli.


zaidi)

 Ukimeki- Ushairi wa Kiswahili unaotumia methali kama kibwagizo

 Ukimeso- Ushairi wa Kiswahili uso methali.


(au kiishio)

 Chuku/udamizi- ni mbinu ya kutilia chumvi suala fulani kwa ajili ya


kusisitiza ujumbe fulani.
Tasida- ni matumizi ya lugha ya adabu ili kuicha makali ya lugha.
Mfano kujifungua mtoto badala ya kuzaa, kuenda haja badala ya kuenda


chooni.
Kinaya- hapa mtunzi huleta dhana ya kinyume cha matarajio. Kwa
mfano badala ya kiongozi alichaguliwa kutetea maslahi ya watu wake
akawa wa kwanza kuwanyanyasa. Kuna aina kadhaa za kinaya kama vile
kinaya cha kiusemi na kinaya hali. Kinaya cha kiusemi ni hali ambapo
maana inayokusudiwa huwa kinyume cha kile kinachosemwa. Katika


kinaya hali matokeo huwa kinyume cha matarajio.
Jazanda- matumizi ya lugha iche au ya mafumbo. Msomaji huhitajika
kuwaza maana kamili iliyokusudiwa. Kwa mfano paka na panya kwa
maana ya watawala na watawaliwa, Mdudu hatari kurejelea ugonjwa wa


UKIMWI.
Tabaini- matumizi ya neno “si” pamoja na maneno kinzani. Kwa mfano:


Alikuwa si wa maji si wa dawa.
Utohozi- mbinu ya kuswahilisha maneno yasiyo ya lugha ya Kiswahili.


Mfano “school”- skuli, “Class”- klasi
Sitiara/sitiari- huu ni ulinganisho wa vitu au hali mbili kwa njia ya
moja kwa moja kwa sababu vitu hivi vina sifa au tabia sawa. Mfano:
Mwalimu mkuu ni simba, Maria ni twiga.
 Taashira/Ishara - mbinu ambapo mtunzi hutumia lugha ya ishara
kuwakilisha ujumbe fulani. Kwa mfano mvi kuashiria mtu mzee.
 Taswira- ni mbinu ambapo mtunzi hutoa maelezo ambayo huibua
picha ya kitu au hali fulani akilini mwa msomaji. Kuna aina kadha za
taswira kama vile:
Taswira mnuso/harufu- k.m rihi ya maua

28
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Taswira mguso- k.m kumpapasa, kumbusu miguu


Taswira usikivu- k.m anasikiliza ndege
Taswira ya mwendo- k.m yeye kuendelea kwa furaha
 Nidaa/siahi- hutambulishwa na matumizi ya alama hisi (!) ambayo
mtunzi hutumia kudhihirisha hisia fulani kama vile furaha, huzuni,
mshangao n.k
 Majazi- mbinu ya mwandishi kuwapa wahusika ama mahali majina
yanayoshabihiana na tabia, vitendo au hali zao.
Masuala mengine muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Anwani/kichwa cha shairi
Maswali mengi huwahitaji wanafunzi kulipa shairi anwani mwafaka. Je, ni vipi
mwanafunzi ataweza kulijibu swali hili? Uteuzi wa anwani huzingatia urudiaji
wa maneno fulani katika shairi lote au pia kibwagizo. Hivyo basi mwanafunzi
anaweza kulipa shairi anwani kwa kuzingatia ni maneno yapi yaliyorudiwarudiwa
au kwa kutumia maneno katika kibwagizo.
Anwani pia yaweza kubuniwa kutokana na maudhui yanayojitokeza kwa wingi
katika shairi. Anwani ya shairi huwa kama ufupisho au muhtasari wa yale
yaliyomo katika shairi. Hivyo basi mtu yeyote anayesoma kichwa cha shairi
fulani huweza kukisia kile ambacho shairi hilo linazungumzia hata bila ya
kulisoma shairi lenyewe. Kwa ufupi, kichwa cha shairi humpa msomaji taswira
ya kijumla ya mambo yanayozungumziwa katika utungo wenyewe.
Falsafa ya mwandishi
Huu ni msimamo wa mwandishi kuhusu maudhui tofauti tofauti aliyoyajadili
katika utungo wake. Msimamo wa mwandishi unaweza kuwa analiunga mkono
jambo fulani au analipinga jambo fulani. Hili litadhihirika wazi jinsi anavyoeleza
maudhui yake.
Nafsineni
Huwa ni anayezungumza katika shairi. Wakati mwingine huwa ni mtunzi
mwenyewe anayezungumza au wakati mwingine akamtumia mhusika fulani
kupasha ujumbe wake.
Nafsi nenewa/hadhira lengwa
Huwa ni anayeelekezewa ujumbe. Ujumbe katika shairi au hata kazi yoyote ya
fasihi huwa inamlenga mtu au kundi fulani la watu. Walengwa hawa ndio nafsi
nenewa ama hadhira lengwa, kwa mfano wanafunzi, wazazi au wananchi.
Lahani/Toni ya shairi
Mwanzoni mwa kitabu hiki tulieleza kuwa shairi hutumia lugha teule, yenye
mnato na iliyojaa hisia. Toni ni hisia ambazo huibuka kutokana na yale
anayosema mzungumzaji katika shairi. Mzungumzaji huweza kuibua hisia za
kuchekesha, kulalamika, kubeza, furaha, huzuni n.k

29
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Mandhari na wakati
Mandhari ni mazingira au muktadha au mahali ambapo shairi fulani hutungiwa.
Mandhari na wakati huenda sambamba. Kutokana na maudhui ya shairi,
tunaweza kubaini ni wapi na ni lini shairi lilitungwa. Mifano ya mandhari ni
kama vile Pwani, mjini, shuleni n.k. Hivyo basi mandhari na wakati husaidia
kuendeleza maudhui ya shairi. Kwa mfano katika shairi la Mnazi na Vuta n’
kuvute, mandhari ni ya Pwani.
Uhusika katika ushairi
Mashairi pia huweza kuwa na wahusika haswa tukirejelea ngonjera na
malumbano hivyo basi ni muhimu kulitilia maanani suala hili. Wahusika huwa
kama sauti ya mwandishi maanake ni kupitia kwao ambapo mtunzi hueleza
mawazo yake bayana.
Tasnifu
Haya ni maelezo mafupi ambayo mwandishi wa kazi ya fasihi huyatoa kuhusu
maudhui na dhamira yake katika utungo.
Lugha ya nathari/Lugha tutumbi/mjalizo
Hili ni swali ambalo aghalabu halikosi kwenye maswali ya ushairi. Mwanafunzi
ataulizwa...Andika ubeti fulani katika lugha ya nathari. Lugha ya nathari ni
lugha ya kawaida. Huwa ni maandishi mfululizo. Ubeti uandikwe kwa aya moja
ama kwa njia ya kiinsha bali si ya kishairi. Mishororo igeuzwe iwe sentensi za
Kiswahili sanifu zinazozingatia kanuni za lugha. Sehemu zilizorudiwarudiwa
ziandikwe mara moja tu. Usitumie lugha ya mshairi.

30
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

6
UHURU WA KISHAIRI
Idhini/Uhuru wa kishairi
Kazi za sanaa huhitaji ubunifu wa hali ya juu. Hali hii hupelekea wakati mwingine
watunzi kuenda kinyume na kaida za matumizi ya lugha kimaksudi. Jambo hili
huibua dhana ya uhuru wa kishairi. Uhuru wa kishairi ni idhini au ruhusa ya
mwandishi kutunga shairi kwa namna fulani bila kuzingatia kanuni za kisarui.
Uhuru wa kishairi huhusisha yafuatayo:
1) Mazida – uhuru huu humruhusu mtunzi kuyarefusha maneno fulani.
Mazida husaidia kuleta utoshelezo wa idadi ya mizani katika kipande
au mshororo na pia urari wa vina.
2) Inkisari – huu ni uhuru wa mshairi kuyafupisha maneno fulani. Kama
ilivyo katika mazida, inkisari pia husaidia kutosheleza idadi ya mizani
na kuleta urari wa vina.
3) Tabdila – ni uhuru wa mshairi kubadilisha herui au hata sauti ya neno
bila kubadili maana ya neno hilo. Kwa mfano daraza badala ya darasa.
Tabdila husaidia kuleta urari wa vina katika kipande cha mshororo.
4) Kuboronga/kuinyanga/Kubananga sarui – pia huitwa miundo
ngeu/ukiushi wa kisintaksia/ukiushi wa kimiundo. Huu ni uhuru wa
mshairi kutofuata kanuni zinazotawala sarui. Kusudi la kufanya hivi ni
kuleta urari wa vina katika mishororo. Kwa mfano, kunapopambazuka
kila, amka mwanadamu badala ya kila kunapopambazuka,
mwanadamu amka
5) Kikale – ni matumizi ya msamiati wa kale, kwa mfano, nyuni badala ya
ndege, mgunda badala ya shamba n.k
6) Vilugha/vilahaja – ni matumizi ya msamiati wa lahaja za Kiswahili
badala ya Kiswahili sanifu.
7) Utohozi – kutohoa ni kuswahilisha msamiati wa lugha nyingine na
kuwa Kiswahili. Kwa mfano, klasi badala ya class, eropleni badala ya
aeroplane, deski badala ya desk n.k.

Mfano wa shairi lililochambuliwa kikamilifu


Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
31
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Dunia ingetatana, na kizazi katikati,


Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Peleleza utaona, hayataki utaiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)
Maswali na majibu yake
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
LAU HAKUNA MAUTI

 Mtiririko – vina vya kati vinafanana na vya mwisho pia vinafanana


b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza

katika shairi lote


Vya kati vya mwisho
na, ti,
na, ti,
na, ti,
ti, na.

32
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Mathnawi – lina vipande viwili – utao na ukwapi


c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
(i) Inkisari –kwazawa, ńgekuwa, ńgetutafuna, nanena,
sitokwenda
(ii) Tabdila – Sharuti badala ya sharti
(iii) Kuboronga sarui – mauti kawa hakuna – ikiwa hakuna mauti,
– katika wote wakati – katika wakati wote
(iv) Lahaja (ya kimvita) – hatuwati (hatuwachi)
– yaoleni (yaoneni)
d) Eleza umbo la shairi hili.
(i) Beti 8
(ii) Mishororo 4 katika kila ubeti
(iii) mizani 16 katika kila mshororo
(iv) vina vya kati vya mwisho
na, ti,
na, ti,
na, ti,
ti, na.
(v) vipande viwili – utao na ukwapi
(vi) Lina kibwagizo “lau hakuna mauti, vipi tungelisongeni?”

 Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi


e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.

 Mwenyezi Mungu anajua kupanga


 Baadhi ya watu wafe na baadhi wazaliwe
 Bila kifo tungesongamana/jaa sana

 Subuhana
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.

 Rabana
 Jabaruti
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi

 Balagha
hili

 Tashbihi
- k.v Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
- ikawa kama ya kuti

 Takriri - si ati ati


- Kama ukosi na shati

 - Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

33
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

7
MKUSANYIKO WA MASHAIRI

Shairi 1, Abedi K.A


Maneno musirukie

Kurukia si kuzuri, maneno musirukie,


Mutakuja zusha shari, makonde muyabugie,
Mukimbie kwa ghururi, kama kuku mukimbie,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
Wasemapo majabari, maneno musirukie,
Hasa walio jeuri, kamwe musikurubie,
Ndondi zitawaaziri, na kwa Mola mutubie,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
Hii nayo ni kiburi, lisemwalo murukie,
Yafaa mujihadhari, gumzo mulisikie,
Musije watu hasiri, magumi yawashukie,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
Imezukapo hatari, hii leo nikwambie,
Msemaji mhodari, uhodari ajitie,
Kapambana na jabari, la kufanya asijue,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.
Kabla hayajakiri, jitu limgeukie,
Likamzaba hodari, naye mbio akimbie,
Likamkazia shari, na mbio asizijue,
Maneno musirukie, wasemapo majabari.

Maswali
a) Onyesha mpangilio wa vina katika ubeti wa nne.
b) hibitisha matumizi ya pindu katika shairi hili
c) Taja, ueleze na utoe mfano wa mbinu zozote mbili za uhuru wa ushairi
zinazodhihirika katika shairi hili.
d) Toa mifano miwili ya uradidi katika shairi.
e) Kuna madhara gani kwa mtu anayerukia maneno?
f) Fafanua dhamira ya mshairi

34
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 2, Abdilatif Abdalla


KIBARUWA
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!
Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.
Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-
Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!
Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani1

Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao


Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”

35
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
a) Eleza dhamira ya shairi hili.
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia
mshairi
c) Kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu
ya kimuundo.
d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu
vibarua.
e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari.
f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba.

36
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 3, Said A. Mohamed


1. Dharau ije kwa bezo mtu kumkata pua
Iwile kama fumizo ghafula kuja muua
Dharau ni angamizo kwa wale wasotambua
Mtu humkata pua!
2. Dharau ije kwa mzo mja humuuangamiza
Kwa ufanyae vikwazo dharau ishakuweza
Kama vile mtelezo dharau hukubwatiza
Mja humuangamiza!
3. Dharau ni mwambuzo kidonda inaambuza
Kipele cha mkwaruzo machozi huja kuliza
Yazidipo matatizo mguu ukipoteza
Kidonda inaambuza!
4. Dharau kwa kazi twezo hwenda ukaipoteza
Haikupi kishikizo wewe na kazi kucheza
Malipo yako na tuzo kazini hukufukuza
Hwenda ukaipoteza!
5. Dharau mfwatilizo inangoja kumaliza
Haiwi haiwi hizo kuwa kutakutimiza
Dharau si ya chetezo kinga haitapatiza
Inangoja kumaliza!
6. Dharau si maliwazo kukaa ‘kizungumza
Na nyakati zipitazo wewe uli ukichuza
Dharau ni fumanizo ghala huja kupaza
Dharau si maliwazo!
7. Dharau ni mabwagizo maisha kudidimiza
Hukuvunjia uwezo kutenda na kufanyiza
Na mingi kwako mizozo kote imekuzingiza
Dharau ni mabwagizo!
8. Dharau ni maapizo laana ya kuapiza
Hupungukiwa mawazo na watu hukupuuza
Muokwako matutizo na kuzama na kuviza
Dharau ni maapizo!
9. Dharau ni matelezo Chini yatakubwagiza
Na hakuna mazuizo telezi ukiteleza
Purr chini kunasazo kuinuka hutaweza
Dharau ni matelezo!
10. Dharau ni hitimizo wasia wangu chukua
Ninafunga beti hizo kumi niloziambua
Ikimbie ndugu guzo dharau inaumbua
Dharau ni hitimizo!
(Kutoka: Stadi za Lugha, Kitabu cha 3, Said A. Mohamed, OUP, uk. 31 – 32)
37
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka
b) Shairi hili ni la bahari gani. Toa sababu.
c) Fafanua dhamira za shairi hili
d) Onyesha muundo wa shairi hili
e) Taja na ueleze tamthali tatu za lugha zilizotumika katika shairi hili
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi
i) fumanizo
ii) mwambuzo

38
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 4, Said Karama


Sahiba umenisema , kwa mchana na laili,
Munaondoa lazima, muenendo wa kiasili,
Kujenga ulipohama, mtu huaje aili,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe,kupewa usikubali,
Haiwi mtu mwanawe,na pia asimjali,
Ulikataa mwenyewe, kwa ghadhabu na ukali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Ndipo wewe ushukiwe, ukajifanya mkali,
Na sitaki uambiwe, mtu asije kwa hili,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Kwani ulihama wewe, kugura hapo mahali,
Enenda sinisumbuwe, siniudhi yangu hali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Na hili langu ujuwe , kwangu hili ni jamali,
Siachi ninga kwa mwewe, wala siwezi badili
kupewa usikubali, wajatoka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Na hapa ndiyo mwishowe, tamati shairi hili,
Kaa usinizuzuwe, nasuburi ilihali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Maswali
a) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili.
b) Mwandishi anadhamiria nini katika shairi hili?
c) Hili ni shairi la aina gani? Eleza
d) Ni methali gani inayoaiki maelezo katika ubeti wa kwanza?
e) Ni nini maana ya kifungu “Kupewa usikubali, wajataka usipewe“
f) Andika ubeti wa mwisho katika lugha nathari.
g) Bainisha maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
i) Sahiba
ii) Laili

39
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 5, Oncharo P. Wyclife


SHAIRI LA A
Falaula ngalijua, singalikuwa kijana,
Kwa sababu sikujua, kajipata mvulala,
Mengi mambo nikajua, nikashinda wasichana,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Mwili wangu kabadilli, toto hadi utu uzima,
Sauti yangu kabadili, nikajiola mzima,
Kakiuka maadili, dunia nikaizima,
Kweli ujana moshi, ukienda haurudi.
Masikiongu katonga, herini nikavalia,
Nywele yangu nikasonga, na mikufu kuvalia,
Video pia runinga, tazama bila tulia,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Malaika kapata, moyo wangu kapambika,
Jina lake kaloreta, mie wangu malaika,
Penzi langu kalipata,mambo mengi katendeka,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Moyongu kausumbua, nilipomtia mboni,
Penzi lanisumbua, aingiapo moyoni,
Sautiye kazindua, yatoa nyoka pangoni,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Penzi lake kalionja, kwangu likawa asali,
Nikawa kionjaonja, kuliwasha kawa kali,
Vitabungu nikakunja, navyo kavitupa mbali,
Kweli ujana ni moshi , ukienda haurudi.
Mzigo kabebesha, ukamwachisha skuli,
Mashakani kaniingisha, nikawa sasa silali,
Kulisaka suluhisho, likawa sasa ghali,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Majuto nikayapata, kwa matendengu awali,
Mifano nikaipata, Yakimwagika yazoli.

40
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Petro Lubale Wa Akungwi


SHAIRI LA B
Mhariri nipe fursa, niichue jambo hili,
Nipige wengi msasa, nakusihi tafadhali,
Ukweli wajue sasa, wamakinike ki hali,
Samaki pale barini,kweli huwa si mmoja.
Nawajuza mahawara, pale walipo hakika,
Si ya neni kihasira, ukweli nautamka,
Wayaepuke madhara, wazidi kumakinika
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.
Dunia imegeuka, waja leo wana shani,
Wazidi kuhangaika, watatizika moyoni,
Utesi umeshazuka, mashambani na mijini,
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.
Mahaba yakigeuka, hakika huwa ni dhiki,
Ugomvi uje kuzuka, uharibu uraiki,
Wakosane washirika, wapigane kila mwezi,
Samaki pale barini, kweli si mmoja.
Lakini sasa tengeni, vigogo niwasaili,
Iwapo ni hayawani,mpungufu kiakili,
Unisamehe sabini, kwa kosa moja kwa kweli,
Samaki pale barini kweli huwa si mmoja.
Hakika huwa si vyema, kibaya kukimiliki,
Mchongaji nayasema, natangaza uhakika,
Mtu mate huyatema, iwapo hayamezeki,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.
Nafumbua fumbo wazi, mnielewe vizuri,
Nafasili ya mapenzi, yalokumbwa nazo zari,
Yaloitinika wazi, hapo ndipo nashauri,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.
Maswali
a) Linganisha shairi la A na B kwa upande wa maudhui.
b) Eleza muundo wa shairi la A
c) Toa mifano ya uhuru wa utunzi uliotumiwa katika shairi la B.
d) Andika ubeti wa nne wa shairi la A katika lugha nathari.
e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi haya.
i) Nikajiola
ii) Mzigo kambebesha
iii)Shani
iv) Zari
41
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 6, Muhammed Seif Khatib


MWANAMKE
1. Namwona yu shambani,
Na jembe mkononi,
Analima,
Mwanamama,
Mavuno si yake,
Ni ya mume wake.
2. Namwona viwandani,
Pia maoisini,
Yu kazini,
Hamkani,
Anabaguliwa,
Na anaonewa.
3. Namwona yu nyumbnai,
Mpishi wa jikoni,
Yaya yeye,
Dobi yeye,
Hakuna malipo,
Likizo haipo.
4. Namwona kitandani,
Yu uchi maungoni.
Ni mrembo
Kama chombo,
Chenye ushawishi,
Mzima utashi.
5. Namwona mkekani,
Yuwamo uzazini,
Apumua,
Augua,
Kilio cha kite,
Cha mpiga pute.
6. Kwa nini mwanamke,
Ni yeye peke yake,
Heshimaye,
Haki anakosa,
Kwa kweli ni kosa

42
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
(a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua dai hili kwa kutoa mifano
minne.
(b) Eleza umbo la shairi hili
(c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
(d) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima utoe mifano miwili
ya jinsi ilivyotumika
(e) Onyesha mifano miwili ya ubabadume inayojitokeza katika shairi hili
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika shairi:
(i) mzima utashi
(ii) maungoni

43
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 7, E. Kezilahabi
Dhamiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kuikia yote nimekula.
Ninaona majani mengi mbele yangu
Lakini siwezi kuyaikia: kamba, kamba.
Oh! Nimefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuiikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.
Kamba isiyoonekana haikatiki.
Nami sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
Aliharibu na mbwa aliuma watu.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
Lakini lazima nitamke kwa nguvu “Hapa nilipo sina uhuru!”
Maswali
a) Lipe shairi kichwa mwafaka
b) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia.
c) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru?
d) Eleza maana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
“Kamba isiyoonekana haikatiki.”
e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili.
f) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza
katika shairi hili.
g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi.

44
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 8, Mohammed seif Khatib


WASAKATONGE
1. Wasakatonge na juakali
Wabeba zenge ya maroshano,
Ni msukuma mikokoteni,
Pia makuli bandarini,
Ni wachimbaji wa migodini,
Lakini maisha yao chini
2. Juakali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapa kazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopazi wa majaani,
Lakini bado ni maskini.
3. Wasakatonge na juakali
Wao huweka serikalini,
Wanasiasa madarakani,
Dola ikiwa mikononi,
Wachaguliwa na ikuluni,
Lakini wachaguaji duni.
4. Juakali na wasakatonge
Wao ni wengi ulimwenguni,
Tabaka lizilo ahueni,
Siku zote wako matesoni,
Ziada ya pato hawani,
Lakini watakomboka lini?
Maswali
a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa” fafanua rai hii kwa kutoa mifano
minne
b) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe
mifano miwili ya jinsi ilivyotumika
c) Eleza umbo na shairi hili.
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya mjalizo.
e) Onyesha mifano miwili ya maadili yanayojitokeza katika shairi hili.
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi
(i) Manamba
(ii) Tabaka lisilo ahueni

45
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 9, E. Kezilahabi
KISU MKONONI
Wakati miaka inaibwa mmoja mmoja,
Kurudi nyuma, kusimama, kupunguza mwendo
Siwezi, kama gurudumu nitajiviringisha
Mtelemko mkali huu
Lini na wapi mwisho sijui
Mbele chui mweusi, nyuma mwanga
Nionako kwa huzuni vifurushi maelfu ya dhambi
Kisu! Maisha kairi haya
Kama kutazama nyuma na mbele
Ni kufa moyo mzima!
Sasa kama Simba - Mtu shauri nimekata
Ya nyuma sana nisijali, ya mbele sana niyakabili
Kwa ujasiri na uangalifu nitazunguka
Nikifuata kamba kama ng’ombe aliyefungwa,
Kila mpigo wa moyo wangu
Huu mpigo muziki wa maisha
Maswali
a) Hili ni shairi la aina gani?
b) Taja sifa mbili za shairi la aina hii.
c) Eleza toni ya shairi hili.
d) Eleza ujumbe wa mtunzi kwa kifupi
e) Kwa kutolea mifano taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika shairi hili.
f) Mhusika katika shairi hili ana matatizo gani?
g) Ni kwa namna gani mhusika katika shairi ananuia kutatua matatizo yake?
h) Mtunzi ana maana gani anaposema
(i) Wakati miaka inaibwa mmoja mmoja
(i) Kama simba – mtu shauri nimekata

46
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 10, Duncan M, Were


BURIANI DHARWESH
Jumanne, Disemba, Elfu mbili kumi na tano
Habari za simanzi kotekote zikaenea
Huzuni mioyoni mwa kila aliyemjua
Wote tulimfahamu mtangazaji alobobea
Ahmed Dharwesh jina lake tulozoea
Fikra zako akilini mwetu hazitopotea
Tabasamu lako kwenye runinga litasalia!
Angani, nyumbani kwake tulielekea
Kikowani makaburini mwili wake tukaupokea
Maisha safari, mwisho wake twaisherehekea
Makiwa! Jamii kwa jumla tulikutegemea
Huzuni tele mioyoni ila twakuombea
Akulaze mahala pema Manani alokuwekea
Anapowalaza wema wengi walojiondokea
Siamimi leo hii tumempoteza mwenzi
Mdau katika lugha tunayoienzi
Kazi, dini na hata mapenzi
Alitufundisha na kutuondolea ushenzi
Katuonyesha mwanga zaidi ya kurunzi
Daima mioyoni mwetu tutakuenzi
Salama usairi, akuhifadhi pema Mwenyezi
Nne beti naika tamati
Hakika kila nafsi itaonja mauti
Tumelia wengi tunapofunga msikiti
Tulosalia Allah atufariji kila wakati
Familia nayo aingilie kati
Awalinde hata na kina banati
Kwaheri ya kuonana mwandani wa dhati
(Shairi la mwandishi)
Maswali
a) Taja na ueleze bahari tatu za shairi hili?
b) Eleza ujumbe wa mshairi.
c) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
d) Je unadhani kwamba aliyeaga alikuwa akifanya kazi gani? Eleza
e) Andika ubeti wa tatu katika lugha tutumbi.
f) Eleza hisia za mwandishi kuhusu aliyefariki.
g) Jamii rejelewa anayotoka aliyeaga ni ya dini gani? hibitisha
h) Taja majina matatu aliyotumia mshairi kurejelea Mungu.
i) Taja na ueleze mifano miwili ya uhuru wa kishairi aliyotumia malenga.
47
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 11, Muhammed Seif Khatib


1. Fahali la dunia, 2. Fahali la dunia
Ndani ya zizi lake, linatesa, Latumia mabavu, laoneya,
Linaminya, Lasakama,
Linanyonya, Laandama,
Kwa kinyama, Kina mama,
Linaoneya. Linatesa.

3. Fahali la dunia, 4. Fahali Ia dunia,


Lisilo na huruma, linatesa, Limeota pembe, laoneya,
Linapiga vindama, Limehama zizi,
Na wengine wanyama Laranda duniani,
Tena bila huruma, Mashariki na Kusini,
Laoneya: Linatesa,

5. Fahali Ia dunia, 6. Fahali Ia dunia,


Kwa kiburi, linatesa, Lidhibitiwe, lisitese,.
Linajigamba, Dunia unganeni,
Linatamba, Pamoja shikaneni,
Kuwa mwamba, Unyonge kataeni,
Linaoneya. Semeni basi,
(Kutoka: Diwani ya Wasakatonge, Muhammed Seif Khatib, OUP, Dar es Salaam, uk. 45)

Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka
(b) Eleza muundo wa shairi hili.
(c) Onyesha maovu yanayoendelezwa na anayerejelewa.
(d) Huku ukitoa mifano miwili eleza uhuru wa kishairi alioutumia msanii.
(e) Mshairi anatoa ushairi gani katika shairi?
(f) Andika ubeti wa 3 katika lugha nathari.
(g) Eleza maana za maneno haya kama yalivyotumika katika shairi.

(i) Lasakama
(ii) Limeota pembe

48
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 12, Euphrase Kezilahabi


KWA WALIMU WOTE
Sikilizeni wimbo huu:
Nilipokuwa mtoto niliitwa Chacha
Kwa matamshi yangu ya sasa
Nilipokuwa kijana niliitwa Chaupele
Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele
Nilipokuwa mwalimu nikaitwa Bure.
Huu utakuwa wimbo wako
Utakapostaafu urudipo nyumbani
Umelewa kangara na nyayo zako
Zikishindwa kulenga njia nyembamba vijijini.
Utakuwa kichekesho cha watoto
Watakaokuita, Ticha! Popote upitapo.
Kumbuka mwalimu utakapostaafu.
Mijusi watataga mayai ndani ya viatu
Vyako vilivyokwisha visigino .
Na ndani ya sidiria chakavu
Zilizoshikizwa kamba kwa pini:
Mende watazaliana ndani ya chupa tupu
Za marashi na za bia.
Na manyigu yatajenga ndani ya koia
Zilizosahaulika kutani
Utakapokufa nge watazaliana
Chini ya jiwe juu ya kaburi lako,
Na mlevi fulani akipita atapenga
Na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke
Mwanzo na mwisho wako ndio huo.
Lakini wakati ungali hai
Unaweza kubadilisha mkondo wa maji.
Lakini kwanza tuzungumze wewe na mimi.
Acha mioyo yetu izungumze.
Baada ya kunyanyaswa.
Na kisha nusu mshahara,
Utafundisha tena nyimbo kuwasifu viongozi?
Utafundsha tena ngonjera?
Utapeleka tena wanafunzi asubuhi
Wakajipange barabarani kusubiri
Mgeni aikaye saa kumi, na apitapo
Apunga tu mkono kuwatia kichaa cha shangwe
Na huku nyuma mwasambaa na njaa?
49
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Tazama hilo rundo la madatari mezani


Utalimaliza kwa mshahara mkia Wa mbuzi?
Tuzungumze. Ninyi na mimi.
Acha mioyo yetu izungumze.
Mkiwa waoga na kujikunja kama jongoo
Mtawekwa kwenye vijiti na kutupwa
Nje ya ua, nä ndani mtawaacha
Wacheza ngoma wakitunga nyimbo mpya.
Sikilizeni walimu.
Anzeni kufundisha hesabu mpya:
Mjinga mmoja kujumilisha na wezi ishirini.
Ni sawa ná sifuri.
Fundisheni historia mpya:
Hapo zamani za sasa
Hapakuwa na serikali.
Sikilizeni kwa makini.
Umoja hatuna:
Twasambaratika kama nyumbu.
Tulichonacho ni woga, .
Na kinachotuangusha ni unaiki.
Lakini tusikate tamaa kama mbuni.
Tukiupata umoja bado tunayo silaha.
Kura.
(Euphrase Kezilahabi: Dhifa)
Maswali
a) Eleza dhamira ya mshairi kuwahusu walimu.
b) Ni dhiki zipi mbili zinazowakumba walimu baada ya kustaafu?
c) Taja mapendekezo ya masuluhisho ya dhiki zinazomkumba mwalimu.
d) Taja na kutolea mifano mitatu ya tamathali zilizotumika katika shairi hili.
e) Eleza maana ya mshororo ufuatao kama ulivyo katika shairi.
“Hapakuwa na serikali”
f) Kwa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza katika
shairi hili.

50
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 13, Maina Alfred Mainah


Nyanya
Nakuita mjukuu, karibia nikwambize,
Ni jambo lilo nafuu, keti chini nikujuze,
Imi ndimi jungu kuu, wasia usikilize,
Wishipo ukufae, hishima ujijengee.
Mjukuu
Nasikia niko wima, haya nyanya unipashe,
Rai yako ni daima, ni mwenge kwangu uwashe,
Uangaze mbele nyuma, udumu usizimishe,
Nayo hamu kusikiza, nijuze uliyo nayo.
Nyanya
Weye ni mwana wa kike, tena umebalegheya,
Nakutaka ukumbuke, tohara kuisongeya,
Jamali hino jivike, ja wenzio kupambiya,
Nataka wende jandoni, ukajivumie mema.
Mjukuu
Sijakupinga uneni, nilivyoishi nyanyangu,
Nisikutie huzuni, kwa hini yangu mikungu,
Kuwa leo maishani, halifai hili fungu,
Nalo lisitendwe kwangu, imi siendi jandoni.
Nyanya
Tohara kitu cha ghali, ni tunu kwa mwanamke,
Tena tendo la halali, toka insi tuumbike,
Wewe ungaliko mwali, uwoga sijigubike,
Uenende na rikalo, wasikucheke wenzako.

Mjukuu
Nyanyangu wanifahamu, toka mwangu utotoni,
Wewe kwangu u mkimu, wa nasaha duniani,
Ela taasubi kamu, chungua wako uneni,
Imepitwa na wakati, na masomo ya kisasa.

Nyanya
Naona nimekwelewa, usemayo mjukuu,
Ni kweli tumechelewa, na dhana yenye mafuu,
Naenda uloamuwa, kwa mamako ninukuu,
Tohara za wanawake, zina madhara makuu.

51
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka kwa shairi ulilolisoma.
b) Fafanua umbo la ubeti wa pili.
c) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
d) Eleza bahari mbili za shairi hili.
e) Malenga alikuwa na lengo lipi alipolitunga shairi hili?
f) Jadili maudhui makuu yanayojitokeza katika shairi.
g) Fafanua msimamo wa mjukuu kuhusu tohara ya wanawake.

52
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 14, Mturi wa Ngolya


Liwalo liwe na liwe, mii kwangu si ajabu,
Nasema hili mujuwe, kila jambo na sababu,
Usotaka utendewe, kwa mwenzio sijaribu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.
Utungaji ni hekima, werevu wa kuratibu,
Twapimana kwa kusema, kwa kulenga si nasibu,
Juu ya yote heshima, hung’aa kama dhahabu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.
Tunene yenye ujuzi, kila tunapohutubu,
Tuweke mbali ufyozi, na tukosapo tutubu,
Kama haya huyawezi, basi ni mtu wa gubu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na adabu.
Mambo tukiyasanifu, tuwe na utaratibu,
Hoja zenye takilifu, hazijengi zaharibu,
Sio mana kujisifu, bora nikutaadabu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na adabu.
Elimu kitu azizi, inatimiza wajibu,
Alo nayo kwa wenyezi, huwa hakosi thawabu,
Ila usipomaizi, yaweza kukughilibu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.

Kwa hoja ilo kweli, kupinga sina sababu,


Nilionalo batili, silijongei karibu,
Asilani sikubali, kundini sinihesabu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.
Semi za kutukanana, mkota naona aibu,
Ni ujinga wa ujana, ama kukosa adabu,
Chambilecho ni laana, na kutubu ni wajibu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.
Neno moja maraiki, nimeona aghalabu,
Kila mshiriki chuki, hawezi kujirekebu,
Na daima atabaki, na moyowe wa kisebu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.

53
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kila lililo na ila, siwi nalo uraibu,


Ni desturi na mila, lilipo najitanibu,
Mana lisilo aula, amelilani Wahabu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzi.
Ninawaaga malenga, ninakifunga kitabu,
Musidhani ni muoga, kwayo niliyohutubu,
Kila mjuzi wa kunga, kunena hili wajibu,
Na tulumbe na adabu, kwa hekima na ujuzu
Maswali
a) Anwani gani inafaa shairi hili?
b) Eleza umbo la shairi hili.
c) Nakili utao wa mloto wa ubeti wa sita.
d) Taja na ueleze bahari ya shairi hili kwa kigezo cha mpangilio wa vina.
e) Taja nafsi neni.

54
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi 15, Alamin Mazrui


NIGUSE
Nitokapo kizuizini
Nitamwomba yoyote mwendani
Aniguse
Taratibu
polepole
Lakini
Kwa yakini!
Niguse tena
Unijuze tena
Unifunze tena
maisha yalivyo
maisha yaonjavyo
ladha yake ilivyo
Nipo hapa nimekukabili
Niguse tena tafadhali!
Niguse!
Niguse!

(Alamin Mazrui “Chembe Cha Moyo” 1988:1)

Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu

b) Eleza ujumbe wa shairi hili.

55
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 16, TIMOTHY AREGE


VIDATO VYA MAISHA
Vidato
vya
maisha
mithili
ya
sarafu;
kipo
kichwa
nao
wa
pili
upande.
Kuna
kupanda
na
kushuka,
kupenda
na
kuchukia,
kufaulu
na
kushindwa.
Leo
utapanda
kesho
washuka.
Ni
kawaida
ya
maisha;
mdundo
wa
moyo,
burudani
ya
nafsi!
Maswali
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
(b) Zibainishe tamathali za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
(c) Shairi hili ni mfano wa shairi picha.Kwa nini?
56
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 17, MWALAA MRANGA NYANJE


‘SIKATI TAMAA
Huchi kunikaa
Nisiye angaa
Nyumba wala taa
Sina cha kuvaa
Kila kuking’aa
Mimi hushangaa
Hukosi angaa
Kwangu kusambaa
Huna haya njaa
Hebu nikataa
Maisha jukwaa
‘sikati tamaa

Maswali
(a) Shairi hili ni la aina gani?
(b) Ni nani mzungumzaji katika shairi hili?
(c) Eleza taswira inayochorwa na mzungumzaji katika shairi hili.
(d) Eleza toni ya shairi hili na uonyeshe inavyochangia kuupitisha ujumbe wa
shairi.

57
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 18, MWALA MRANGA NYANJE


SIONDOKI
Eti
Niondoke!
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu!
Nimesaki; licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki.
Mimi
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki.
Hapa
Siondoki
Mimi nipahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki.
Haki
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki.
Kamwe
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki.
Sendi
Nende wapi?
Si’hapa kitovu change!
Niondoke hapa kwangu
Wangwana na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki.
Katu
Siondoki
Sihitaji karatasi
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki.
58
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
(a) Chambua maudhui ya shairi hili.
(b) Kuna uhusiano gani kati ya muundo wa shairi hili na maana yake.
(c) Shairi la aina hii linaitwaje?
(d) Eleza muundo wa shairi hili.
(e) Toa mifano ya mishata katika shairi hili.

59
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 19, ABDALLA SAID KIZERE


KIBURI
1. Ikiwa umeumbika, kwa uzuri ulotimu,
Au umetajirika, pesa nyingi tasilimu,
Kiburi ukajivika, vazi lenye uhasimu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
2. Mola mwenye madaraka, ndiye mwenye kurehemu,
Kukupa na kukupoka, ndiye kaziye Karimu,
Humpa anayaetaka, jamii ya wanadamu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
3. Waringa na hekaheka, wenzio kuwashutumu,
Kwa kuziona fanaka, Mola alokukirimu,
Wazimu ukakushika, ukawa huna fahamu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
4. Kwanza ziondowe taka, nduguzo kuwahasimu,
Usiipige mipaka, wazazi kuwalaumu,
Zinduka ndugu zinduka, wewe sio marehemu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
5. Kiburi ni mbaya shuka, kuivaa ni haramu,
Yapendeza kukumbuka, msemo wenye kudumu,
Mpanda ngazi hushuka, alacho kikawa sumu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
6. Na mwanadamu yataka, bonge lake kuhitimu,
Wazee walotamka, maneno yalo muhimu,
Kulonama huinuka, laini huwa kigumu
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.
7. Kituoni nimeika, nazikomesha nudhumu,
Yatosha naloandika, kiburi ni jahanamu,
Ashikae atashika, asoshika si lazimu,
Kiburi kwa mwanadamu, si kitu chema kiburi.

Maswali
(a) Kwa nini msanii alilitunga shairi hili?
(b) Taja mambo mawili yanayoweza kupelekea kiburi mintaarafu ubeti wa
kwanza?
(c) Nini sababu ya mtunzi kunadi kuwa kiburi hakifai?
(d) Fafanua muundo wa shairi hili.
(e) Yanakili majina ya Mwenyezi Mungu yaliyodhukuriwa shairini.
(f) Tambua methali mbili alilozidokeza mtunzi.
60
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 20, SAID HAMADI LUNGO


TAMAA
1. Viumbe wa siku hizi, tamaa zimewashika,
Mtu japo ana kazi, ya cheo na madaraka,
Atafanya uchafuzi, kuharibu mamlaka,
Apoteze uazizi, Mungu alomtunuka,
Cheo na kupanda ngazi, awe ni mwenye kushuka.

2. Na ajili ya kutenda, hutongewa ni tamaa,


Tamaa zimemshinda, moyoni zimemjaa,
Akitaka kujilinda, roho yamwambia twaa,
Heshima akaivunda, kwa kutenda yasofaa,
Jinale akaliponda, akarudi kuduwaa.

3. Tamaa dunia nzima, sasa imeshika zamu,


Siyo kwa wenye kusoma, wala wasiyo elimu,
Watu wamekuwa nyama, kwa kutaka darahimu,
Tarajia ni kuchuma, jingine hawafahamu,
Mara huwa wamezama, na lengohalikutimu.

4. Haya niliyoyatunga, siyo mambo ya kubuni,


Siku hizi kila janga, hutangazwa radioni,
Kuna wezi wa mapanga, wangiao majumbani,
Wengineo hujikonga, kuwadhuru insani,
Ili wapate faranga, tamaa zao nyoyoni.

5. Wengine hufanikiwa, bahati ikiwa nzuri,


Wakenda wakachukuwa, kama vyao kwa shuari,
Na kwengine huuawa, wakachimbiwa kaburi,
Wakabaki kufukiwa, pasipo na dua nzuri,
Na yote yasingekuwa, tamaa zimewaghuri.

6. Nilipoika unasi, natia kadi tamati,


Najua mtu hakosi, tamaa kila wakati,
Lakini zisitughasi, zikatupa tasliti,
Na nyendo za Ibilisi, hazikosi tafauti,
Kupata siyo kwa kasi, kupata kuna wakati.

61
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
(a) Beti hizi zimekusudiwa nini?
(b) Nakili
(i) Utao wa mloto wa ubeti wa pili
(ii) Ukwapi wa mleo wa ubeti wa tano
(c) Yaorodheshe matendo manne yanayoonyesha tamaa.
(d) Taja hasara zinazomkabili mja mwenye tamaa.
(e) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
(f) Fafanua bahari tatu za shairi hili.
(g) Idhini ya kishairi humruhusu msanii kuitumia lugha pasi kujali sana.
hibitisha kwa kurejelea vipengele viwili kati ya vifuatavyo mintaarafu shairi
hili.
(i) Inkisari
(ii) Tabdila
(iii) Kuboronga sarui
(h) Andika ubeti wa tatu kwa lugha mjalizo.
(i) Eleza msamiati ufuatao kufungamana na shairi.
(i) Uazizi
(ii) Akaivunda
(iii) Dua
(iv) Kasi

62
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

SHAIRI 21, OMARI SULEMANI KIZILIZALA


MWANANGU NAKUUSIA
1. Mwanangu sogeza kiti, nataka kuhadithia,
Uchao kijizatiti, nguvu zangu zapungua,
Leo napenda uketi, ili nikupe wasia,
UBISHI si kitu chema, mwanangu nakuusia.
2. Penye watu katikati, usipende kujitia,
Ubishi ukasharutu, jambo kulikazania,
Utayapata mauti, dunia kuikimbia,
UKAIDI si mzuri, mwanangu nakuusia.
3. Usifanye tashtiti, yangu ukayachukia,
Haya ninayokunuti, moyonimo yakingia,
Adui hafurukuti, u bukheri wa aia,
KIBURI si kitu chema, mwanangu nakuusia.
4. Tazama huno umati, unaoushuhudia,
Wote ni wa Jabaruti, ndiye alotuumbia,
Usijione simati, wengine kuwachukia,
DHARAU si jambo zuri, mwanangu nakuusia.
5. Mungu amekupa noti, utakavyo watumia,
Waliokosa bahati, ‘kawa wawasinzilia,
Unapokufa janati, huwezi kwenda ingia,
USHARI kitu kibaya, mwanangu nakuusia.
6. Utembeapo sukuti, matusi kuyatumia,
Sijione madhubuti, umeshinda mabondia,
Wengi sasa mahayati, wameihama dunia,
UZINZI si kitu chema, mwanangu nakuusia.
7. Ukiwaona banati, makwao wametulia,
Kwa makini wameketi, na waume wa sharia,
Kijifanya asherati, mwisho utaangamia,
WIZI ni kitu kibaya, mwanangu nakuusia.
8. Wizi ukiushatiti, heshima hukuvunjia,
Magereza ya mabati, ndiko unakoishia,
Nawe walala tiyati, na kazi zenye udhia,
MARINGO si kitu chema, mwanangu nakuusia.

63
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

9. Una kazi ya shiti, kwa taimu waingia,


Wendapo hupigi buti, una gari watumia,
Ukajiona u seti, fukara wawaringia,
KILA JAMBO LINA MWISHO, mwanangu nakuusia.
10. Japo chifu umeketi, wasikizwa na raia,
Kisema hili sitati, watu wakuitikia,
Kipenda jambo sharuti, watu watakukimbia,
URAFIKI UNA MWISHO, mwanangu nakuusia.
11. Pata raiki wa dhati, awe msai wa nia,
Kutwa moja haipiti, bila kukutembelea,
Nduguzo’kiwasaliti, mwisho utakuja lia,
NA UHAI UNA MWISHO, mwanangu nakuusia.
12. Sijione katikati, starehe zakujia,
Kila nchi umeketi, pembe zote za dunia,
Kuna siku ya mauti, raha utazikimbia,
KUJISIFU si vizuri, mwanangu nakuusia.
13. Penye na mwingi umati, nawe ukihudhuria,
Katikati usiketi, watu wakakuzingia,
Patatokea hilati, wote watakulalia,
MAJUMBA USIRINGIE, mwanangu nakuusia.
14. Ukazimiliki noti, majumba kujijengea,
Ukayatia mabati, fanicha za kuvutia,
‘Kawacheka wa makuti,si kazi kuteketea,
SIWARINGIE WATOTO, mwanangu nakuusia.
15. Umejaliwa bahati, watoto kujizalia,
Waume na banati, popote wawatumia,
Kaita washerati, kizazi walokosea,
SIRINGIE MADARAKA, mwanangu nakuusia.
16. Kazini uwe ‘meketi, wengine wakusiia,
Ama u mueka noti, wenzio wawachukia,
Siku ya kupata shoti, huna wa kukutetea,
SHIKA SANA MAMBO HAYA, yote nalokuusia

64
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Maswali
(a) Eleza aina ya shairi hili.
(b) Shairi hili ni la bahari gani? Kwa nini?
(c) Fafanua umbo la shairi hili.
(d) Pendekeza anwani nyingine ya shairi hili.
(e) hibitisha kuwepo kwa matumizi ya udhini ya ushairi katika shairi hili.
(f) Ni vipi sharia za utunzi/arudhi zilivyotumika kwa mujibu wa hili shairi.
(g) Eleza mbinu tatu za lugha alizotumia mshairi.
(h) Ni maudhui yapi yanayojitokeza katika shairi hili?
(i) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.

65
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MSURURU WA MASWALI NA MAJIBU YA MITIHANI YA


KITAIFA YA KCSE TANGU 2008-2016
KCSE 2016
Shairi la 1
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Kilio cha Lugha


Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia

Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa


Hamna nami imani, wala kupanga siasa
Mwasema sayansini, siku ningalitosa
Mwanambia nikotosa, kuiva sijaika

Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu


Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.

Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza


Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza


Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao


Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

66
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia


Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia

Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote


Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi


Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha

Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya


Lugha takuwa imara, ukabila tutainya
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana


Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.

(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu (Alama 2)


(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
(Alama 4)
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
(d) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
(Alama 3)
(f) Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3)
i. nasongwa
ii. kuriaria
iii. adinasi

67
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi la 2
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili

Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi

Punde natumbukia katika shimo


Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghala nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka

Jambo moja nakukumbukia: Mungu


Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!

Kitu kimoja nakiamini


Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitaika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
68
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

(a) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)


(b) Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2)
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka”
katika ubeti wa tatu? (Alama 2)
(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea
mifano mwafaka. (Alama 10)
(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2)
(f) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu

69
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2015
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.

Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi za maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa,kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …

Na mimi kubaki kujiuliza


Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)

a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (alama 1)


b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa
katika shairi hili. (alama 2)
c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili. (alama 3)
70
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (alama 2)


e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili: (alama 3)
i. tashhisi
ii. kinaya
iii. tashbihi
f) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
g) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
h) Changanua muundo wa shairi hili. (alama 3)

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

T. Arege: Mwili
Leo kitaka niike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.
a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 4)
b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 8)
c) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili? (alama 1)
e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande. (alama 2)
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari. (alama 3)

71
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2014
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
1 Ngakua na mato, ya kuonea 6 Kwa yangu mabega, nikathubutu
Ngalisana kito,cha kuchezea Ngabeba maiga, yalo matatu
Kilicho kizito, cha kuelea Bila hata woga, kwenye misitu
Kikamuenea, akivae. Simba tembo chatu, sinitishie.
2 Makusudi yangu,ngaliandaa 7 Miti yenye pindi,na jema umbo
Ngainyanga chungu, cha mduwaa Ngajenga ulindi, mwema
Ngatia vitangu,vinavong’aa wimbombo
Ili ziwe taa, kwa apikae. Fundi aso fundi, penye kiwambo
Moyo wenye tambo, apekechae.
3 Mkungu wa tano, wa mduwara
Ulo bora mno, kisha imara 8 Singaajiri, ngachimba mimi
Ulo na maono, kuwa ni dira Kisima kizuri, cha chemchemi
Kwenye barabara, itindiae. Maji ya fahari, ya uzizimi
Jua la ukami, siyaishae
4 Ngaomba Baraka, kwake Rabana
Punje za nafaka, kila aina 9 Tamati nafunga, kwa kuishia
Chunguni kuweka, kwa kulingana Mato ndo malenga, kanikimbia
Hajaangu suna, yule alae. Nahofu kutunga, mabeti mia
5 Ngafanya bidii, kwenda mwituni Asije chukia, ayasomae.
Sio kutalii, kukata kuni
Ya miti mitii, huko jikoni
Isio na kani,ni iwakae.
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 2)
(b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa
kishairi aliotumia mshairi. (alama 4)
(c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(d) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
(e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 6)
(f) Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (alama 2)

72
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.


T. Arege: Watafuta Riziki
1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.
2. Watafuta riziki, wahaingaikao mijini
Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini
Japo hawasikii, hawakosi kujiamini
3. Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii
Kamwe hawajidhiki, tama za moyo kutii
Bali huaiki, kupingana na ulaghai
4. Watafuta riziki, pato ambalo la halali
Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali
(a) Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili. (alama 5)
(b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi
hili. (alama 6)
(c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza
mahitaji ya kiarudhi. (alama 6)
(d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama 3)
(i) idadi ya mishororo katika beti.
(ii) mpangilio wa vina
(iii) mpangilio wa maneno

73
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2013
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,
Ni wakati utanena.
Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipazao nao,
Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao,
Haupandiki mgomba, wana nyemi, isadi wa hadhi zao,
Eti ni kwa raha zao.
Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,
Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa?
Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,
Waama sina makosa
Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,
Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo,
Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,
Kwalo sichafuki moyo
Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika,
Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itaika,
Kwa shangwe na njerejere, kila mtu, mdomo utafumuka,
Akiri amejibika.
(Mwalaa M. Nyanje)
(a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa.
(alama 2)
(b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika
shairi hili. (alama 5)
(c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili. (alama 2)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(e) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5)
(f) Bainisha matumizi mawili ya tafsida katika shairi hili. (alama 2)

74
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.


1. Huno wakati muti, vijana nawausia, 5. Wawapi leo madume, anasa walopapia?
Msije juta laity, mkamba sikuwambia, Wamepita ja umeme, leo yao sitoria,
Si hayatti si mamati, vijana hino dunia, Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

2. Japo aula kushufu, na machoni vyavutia, 6. Nambie faida gani, nambie ipi idi?
Dunia wana dhaifu, waugua nisikia, Upatayo hatimani, waja wakikufukia,
Vijana nawasarifu, falau mkisikia, Ilakufa kama nyani, kasoroyako mkia,
Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula. Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

3. Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria, 7. Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia,
Msije andama baa, makaa kujipalia, Ujifanye kama kwamba, u jiwe huna hisia,
Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria, Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

4. Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia, 8. Vyatiririka tiriri, vina vyanikubalia,


Wajimwaie uturin na mapoda kumichia, Alo bora mshairi,pa tamu humalizia,
Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia, Nahitimisha shairi, dua ninawapigia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia,


Wakinge wanarika, na anasa za dunia,
Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
(Mwalaa M.Nyanje)
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
(b) Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza
mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 8)
(c) Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze
pande hizo. (alama 2)
(d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (alama 3)
(e) Bainisha toni ya shairi hili. (alama 3)

75
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2011
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
KUJITEGEMEA
1 Nchi ni ile ambayo, imekita ardhini 3 Twaishije tujihoji, wanachi humu nchini
Siyo ile iombayo, ghaibu na majirani Kila tunachohitaji, kupatakwe ugenini
Taratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneni Hiyo ni tete haviji, tongo tupangusaneni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

2 Chumo lote na mitaji, leo lirao maganjani 4 Kuomba wataalamu, ni mwendo hauh’ngani
Bepari na wanyonyaji, wasalie maguguni Tupate wa humu humu, wajuzi wa kila fani
Shime utekelezaji, vingine havifanani Mbele washike hatamu, kwa mapimo na makini
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

5 Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imani 6 Vote hatuyatimizi, alotimiza ni nani


Tushiriki kila kazi, na mambo yalomkini Lakini tuwe maizi, tusizurure mijini
Mikopo ina kinyezi, si kitu cha tumaini Tukamshabihi kozi, kipanga au kunguni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

7 Shujaa itakiwavyo, aonekane vitani


Nasisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani
‘Kutegeniea’ vilivyo, kondo tujiamueni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

Boukhet Amana: Malenga wa Mrima


Mwinyihatibu Mohammed
Oxford University Press
1977
(a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)
(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (alama 2)
(c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili
kujitegemea. (alama 3)
(d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika
shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)
(e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi:
(alama 2)
(i) Ghaibu
(ii) Tukamshabihi.

76
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

HAKI
1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
Watukoroisha, tusikuandame, kila penye kitu,
Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu,
Tutokwe na utu!
2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa,
Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
Haki twashangaa!
3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,
Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,
Usifanyekatu!
4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza,
Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza,
Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
Kambi yatuviza!
5. Haki buna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
Tukiifatia, hatuiki mbali, wengi tunaganda,
Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
Haki yatuponza!
6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,
Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika,
Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatuika,
Kwetu nimashaka!
7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa,
Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
Nandio ya sasa!
8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
Haki wauliwa!
9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
Hatuna ashiki,kuvutalahaja,haki ituvae,
Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
Haki tamati!
(Suleiman A. Ali) Malenga Wapya

77
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

(a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama2)


(b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)
(c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)
(d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi
katika shairi hili. (alama 6)
(e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(f) Mshairi ana maana gani kwa kusema:
(i) Kambi yatuviza
(ii) Kuweza tukisi. (alama 2)

78
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2010
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Dhamiri yangu
Dhamiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kuikia yote nimekula.
Ninaona majani mengi mbele yangu
Lakini siwezi kuyaikia: kamba, kamba.
Oh! Nimefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuiikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.
Kamba isiyoonekana haikatiki.
Nami sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
Aliharibu na mbwa aliuma watu.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
Lakini lazima nitamke kwa nguvu
“Hapa nilipo sina uhuru!”

(E. Kezilahabi)
(a) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia. (alama 4)
(b) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru? (alama 2)
(c) Eleza rnaana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
“Kamba isiyoonekana haikatiki.” (alama 2)
(d) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili.
(alama 4)
(e) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata
yanavyojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
(f) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (alama 4)

79
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2009
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!
Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.
Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-
Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!
Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani1
Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”
a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
(alama 4)
c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya
kimuundo mshairi (alama 4)
d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu
vibarua. (alama 4)
80
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari (alama 4)


f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba (alama 2)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:
Kila Mchimba Kisima
Musa Mzenga
1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,
Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,
Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima,
Upate njema daraja, duniani na kiyama,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama
Ya kukutia harija, hasara kukuandama,
Usione afuwaja, mwanza ajue heshima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe
4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema,
Si ari ya mwenginewe, kumuonya kwa lazima,
Mtu hufunza mwanawe, Kwanza ajue heshima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema,
Kusudi nikuongowe, uepukwe na tujuma,
Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama,
Kila mchimba kisima, bundi hungia mwenyewe
6. Hii si heri ujuwe, matusi kuigandama,
Hadhi usiniuzuwe, hamithilishwa na nyama,
Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
7. shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema
Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima,
Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
8. Yakupasa uchunguwe, kila jambo kulipima
Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama
La kuwaka ulijuwe, pia lipi la kuzima,
Kila mchimba kisima hungia mwenyewe.

81
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

a) Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 4)


b) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na
utoe mifano. (alama 6)
c) Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili (alama 4)
d) Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4)
e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi:
i) afuwaja
ii) taaluma (alama 2)

82
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2008
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
WASAKATONGE
1. Wasakatonge na juakali
Wabeba zege ya maroshani,
Ni msukuma mikokoteni,
Pia makuli bandarini,
Ni wachimbaji wa migodini,
Lakini maisha yao chini
2. Juakali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapa kazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopasi wa majaani,
Lakini bado ni masikini.
3. Wasakatonge na juakali
Wao huweka serikalini,
Wanasiasa madarakani,
Dola ikawa mikononi,
Wachaguliwa na ikuluni,
Lakini wachaguaji duni
4. Juakali na wasakatonge
Wao ni wengi ulimwenguni,
Tabaka lisilo ahueni.
Siku zote wako matesoni,
Ziada ya pato hawaoni,
Lakini watakomboka lini?
(Mohammed Seif Khatib)
(a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua rai hii kwa kutoa mifano minne.
(alama 4)
(b) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe mifano
miwili ya jinsi iiivyotumika. (alama 3)
(c) Eleza umbo la shairi hili. (alama 5)
(d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari. (alama 4)
(e) Onyesha mifano miwili ya maadiii yanayojitokeza katika shairi hili.
(alama 2)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Manamba
(ii) Tabaka lisilo ahueni (alama 2)

83
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MAJIBU YA MITIHANI YA KCSE


KCSE 2016
Shairi la 1
(a) Tarbia- mishororo minne katika kila ubeti

 Maimamu kuidharau lugha


(b)

 Wengi wanaigiza kizungu kuliko Kiswahili


 Kiswahili kutupwa baada ya uhuru
 Kuwa na upungufu wa msamiati
 Msamiati umeombwa ili kuikuza lugha
(c) Yafaa kuelewa Imamu na Maamuma walipokuwa vijana Kiswahili ki-
likuwa sawa. Baada ya kupata elimu wanakidharau na huo ni kuwa
mtumwa.
AU
Kila mmoja aelewe, mlipokuwa vijana mlikitumia Kiswahili.
Baada ya kusoma, mmeanza kukidharau, na kwa kufanya hivi,
mnafurahia utumwa.
(d) Toni ya huzuni/uchungu- kuhuzunishwa na dharau

 Inkisari- msamiatiwe
(e)

 Utohozi- risavuni
 Mazida- Huria
 Tabdila- maa- mama
 Kilugha/lahaja- kiimanya
(f) Nafsineni ni mwanalugha/mtetezi/mkereketwa wa lugha
(g)
(i) nasongwa- nasumbuliwa/dhulumu/sikitika/nabanwa
(ii) kuriaria- kuzurura/kurandaranda
(iii) adinasi- binadamu/insi/mahuluki

84
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi la 2
(a) Toni ya kuhimiza/matumaini/matarajio
(b) Msairi/mwenye matumaini katika maisha
(c) Kuwa tayari kupambana na misukosuko utakayokutana nayo
(d)
 Taswira- miinuko
 Tasihisi- azma kunihimiza
 Tanakuzi- zama na kuibuka
 Taashira- barabara- maisha, miinuko- ugumu
 Jazanda/stiari- barabara
(e) Nafsineni ni Mcha Mungu- dini
(f)
 kuruba- mahangaiko/mateso
 barabara yenye ukungu- misukosuko

85
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2015
Shairi la 1

 Mwenye tumaini/tama- kubwa hamu


a)

 Mwenye bidii- alfajiri na mapema, kutokwa na jasho


 Anayeyafurahia mandhari- anapotembea anasikiliza videge…
 Mtulivu- kuna siri gani inayomliwaza?
 Aliyedhulimiwa- soko la dunia lamkaba koo.
 Anayesagika kwa kazi ngumu kuwafaida wenye tama- ayalimia

 Aliyeridhika- kuna jambo gani linalomridhisha.


matumbo ya waroho.

(zozote 4x1=4)

 Inkisari- babuze- babu zake


b)

 Kuinyanga sarui/miundo ngeu ya kisintaksia- kubwa hamu- hamu


kubwa (2x1=2)

 Taswira mnuso/harufu- rihi ya maua


c)

 Taswira mguso- kumpapasa, kumbusu miguu


 Taswira usikivu- anasikiliza ndege
 Taswira ya mwendo- yeye kuendelea kwa furaha
(3x1=3)
d)

 Kudadisi hali/kushangaa- kuna siri gani inayomliwaza? Kuna jambo


Maswali ya balagha yametumiwa:

 Kuonyesha hali ya kinyume, kutokubaliana na jambo- furaha ya mtu ni


gani linalomridhisha?

 Kuzindua- furaha ya mtu ni furaha gani, katika dunia inayomhini?


furaha gani, katika dunia inayomhini?

(2x1=2)

 Tashhisi- umande kumbusu, miti kumpapasa


e)

 Kinaya- mkulima anafurahi ilhali dunia inamhini


 Tashbihi- kama mtu aliye na kubwa hamu
(3x1=3)

 Toni ya uchungu- furaha ya mtu ni furaha gani katika jamii


f)

 Toni ya kuajabia/kushangazwa na jambao- kuna jambo gani


inayomhini?

 Kuhuzunisha/kusikitisha/kuhurumia
linalomridhisha?

(kutaja 1, kueleza 1 1x2=2)


86
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Mtetezi wa haki/mtu aliyezinduka/anayelalamikia dhuluma ya


g) Nafsineni ni:

 Mtu anayemtazama mkulima akipita


wanyonge

(yoyote 1x1=1)

 Shairi lina beti tatu


h)

 Kila ubeti una idadi tofauti ya mishororo na beti nyingine


 Kila mshororo una kipande kimoja
 Shairi halina mpangilio maalum wa vina
 Idadi ya mizani katika mishororo inatofautiana
 Mshororo wa mwisho katika kila ubeti ni tofauti/ kituo/kimalizio/
kiishio (zozote 3x1=3)
Shairi la 2: Mwili

 Dhamira ya mwandishi ni kuonyesha kuwa kazi ni shughuli muhimu


a)

 Kuonyesha kuwa ipo haja ya kuipa afya kipaumbele kwa kuvikataa


ila haiwezi kuzingatiwa zaidi ya afya.

 Kuonyesha dhuluma wanazofanyiwa wafanyakazi vitisho pamwe


vitisho vya wenye kazi/waajiri.

 Kuukosoa uongozi dhalimu- kufutwa sikawi


kelele.

 Kuzindua wafanyakazi
(4x1=4)

 Shairi linatumia Kiswahili sanifu


b)

 Kuna matumizi ya sitiari/jazanda- si gurudumu mwili


 Uhaishaji- ugonjwa umepewa sifa ya kutenda mwili kuudhili
 Matumizi ya nahau- viraka kuutia (ub 3)
 Urudiaji wa maneno/takriri- kila ubeti unaisha kwa neno mwili
(kutaja 1, mfano 1, 4x2=8)

 Hasira- si gurudumu mwili


c) Toni ya:

 Ukali- sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili. Kufutwa sikawi,

 Machungu- ila wauma mwili


nitakita, kidete nao mwili

 Kukashifu- vitisho pamwe kelele, ninavicha


 Kulalamika- sihofu kupata mawi, sitajuta
(kutaja 1, mfano 1 yoyote 1x2=2)

87
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

d) Mwenye kazi/mwajiri (1x1=1)


e) Ukawai-vipande vitatu katika kila mshororo.
(kutaja 1, kueleza 1, 1x2=2)
f) Mimi kwa hakika ninaithamini kazi kwa akili na mwili/isipokuwa siamini
kwamba inafaa kuteseka kwa kila hali. Hasa ugonjwa unapohusika kutumia
nguvu hakuwezi kunitisha/siwezi kuogopa kutumia nguvu kujitetea. (al 3)

88
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2014
Sauti ya kiza

 Shairi linazungumzia tatizo la upofu mf. ngakua na mato.


a)

 Kwamba mtu anayepatwa na tatizo la upofu huwa hawezi kufanya

 Nafsineni inasikitikia hali yake ya kutomudu kujifanyia mambo kwa


mambo ambayo zamani alizimudu bila tatizo.

sababu ya upofu. (yoyote 2x1=2)

 Inkisari- imetumika ili kudumisha ulinganifu wa mizani. Mf.


b)

 Tabdila- imetumiwa ili kuleta urari wa vina mf. mduwaa- mduara,


ngaliandaa- ningaliandaa, ngalifanya- ningalifanya, ngatia- ningalitia

 Kuboronga/kuinyanga sarui ili kutosheleza urari wa vina mf. maksudi


apikae- apikaye

yangu ngaliandaa (zozote 2x2=4)


c) Ningetumia miti iliyoinda na yenye umbo nzuri/kutengenezea kijiti
kwenye tundu la wimbombo/kupekechea moto kwa ufundi
mkuukiwambono/ningekuwa fundi stadi katika upekechaji wa moto.
Tanbihi- wimbombo ni kipande cha mti kilichotobolewa tundu na
kinachotumiwa kupekechea moto. Ulindi ni kijiti kinachopekechwa kwenye
wimbombo ili kutoa moto.
d) Toni ya huzuni/ya kuomboleza/ya masikitiko
Mshairi anahuzunishwa na analalamikia hali yake ya upofu isiyomruhusu
kujifanyia mambo mengi.
(kutaja al. 1, kueleza al. 1)
e)


Urudiaji wa sauti mf. ubeti wa 1 – msatri wa mwisho kila ubeti


Urudiaji wa silabi ra ra ra /a, a, a, /ngu, ngu, ngu n.k


Urudiaji wa maneno ulo- ubeti wa 3, mato ubeti wa 1, 9
Usambamba/urudiaji wa vishazi/urudiaji wa miundo sawa ya
mistari mf. ngaliinyanga chungu, cha mduwaa.
(Kutaja al. 1, mfano al. 1 za kwanza 3x2=6)
f) Kipofu/mtu asiyeona. Ubeti wa 1 anasema, ngakua na mato.
(Kutaja al.1, kueleza al. 1)
Watafuta riziki

 Hodari wa kufanya kazi/wenye bidii/wakulima hodari


a)

 Wenye kujiamini
 Waliopuuzwa/hawana makubwa (hawasikiki)
 Hawana tamaa
 Wenye kupinga ulaghai/wa kweli
89
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI



Wenye ndoto haizimiki


Hawahini/ huwapa watu haki yao/ waaminifu


Wazalendo
Wanaohangaika/ wanaoteseka kupata/ wanaosumbuka
(za kwanza 5x1=5)

 Tashbihi- kama watanga na ropini- kuonyesha jinsi walivyojitolea (bidii)


b)

 Uhaishaji/tashhisi- tamaa za moyo kutii, kupigana na ulaghai- hapa

 Nahau/msemo- ndoto haizimti. Hawapotezi tumaini- kuonyesha


tamaa za moyo na ulaghai vimepewa uwezo wa kutenda.

 Taswira- kutwa kile na hiki kama watanga na njia- kuonyesha watu


hawafaidiki kwa wasichokifanyia kazi.

 Sitiari/jazanda- ndoto haizimiki kumaanisha hawapotezi tumaini.


wanaoshughulika kufanya kazi kuiendeleza nchi.

 Taashira- watokwa jasho vijijini- bidii


 Kinaya- japo wasikia hawakosi kujiamini- kuonyesha kutokata tamaa.
(kutaja 1, mfano 1 za kwanza 3x2=6)
c)
 Mazida- vinyuani badala ya vinywani ili kutosheleza mahitaji ya idadi

 Kuinyanga sarui/kuboronga lugha/miundo ngeu/ukiushi wa


ya mizani.

kisintaksia/ukiushi wa kimiundo mf. tamaa za moyo kutii badala ya


kutii tamaa za moyo. La haramu jasho hawali badala ya hawali jasho la
haramu. Ya kesho kuwa hali njema badala ya hali kesho kuwa njema.

 Udondoshaji wa maneno (kuacha maneno) mf. pato ambalo la halali


Imetumika kuleta upatanisho wa vina.

badala ya pato ambalo ni halali. Imetumika ili kutosheleza idadi ya

 Utohozi- mf.wiki
mizani/kupunguza idadi ya mizani

(kutaja al. 1,kutaja al. 1,za kwanza 3x2=6)


d)
 Tathlitha/wimbo/utatu- mishororo mitatu katika kila ubeti
 Ukara- vina vya kati/ndani vinafanana katika shairi zima, vya nje

 Kikwamba- kila ubeti unaanza kwa kirai/maneno watafuta riziki.


vinatofautiana

(3x1=3)

90
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2013
Shairi la 1
a) Mzungumzaji (nafsineni) anasingiziwa ugumba hasa kwa kutoshiriki
mapenzi nje ya ndoa. (1x2=2)

 Kuiga rika; hususan kushiriki ulevi pamoja na kufukuza wasichana.


b)

 Mzungumzaji kupakwa tope (kuaibishwa) kwa kuwa yeye ni gumba.


 Wamsemao kudai kwamba anatamani kuwa kama wao.
 Eti kuwa ugumba na ukapera ni kosa.
 Kuharibu maisha kwa ujana.
 Kusingiziwa atapenda (atatamani) hali za wamsemao.
 Watu kueneza uvumi kuwa yeye ni gumba. (za kwanza 5x1=5)

 Viishio hivi ni vifupi na hivyo vinatoa ujumbe kwa namna iliyo


c)

 Viishio hivi vinaunga ujumbe wa kila ubeti/vinasisitiza ujumbe wa


madhubuti.

 Viishiovinachimuza/kuonyesha/kubainisha dhamira au mwelekeo wa


shairi.

mshairi kuhusu hali ya vijana kujiingiza katika mahusiano yasiyofaa.


d) (yoyote 1x2=2)
Ni jambo gani ambalo linamkasirisha Mungu ambalo halikubaliki
kanisani? Je ni mtu kuwa kahaba na mwenye vioja ama mtu
aliyezaliwa akiwa tasa? Kuwa gumba au kapera si kosa na wala haliwezi
kuwa kosa. Kwa kweli mimi sina makosa. (4x1=4)
e)
 Kila ubeti una mistari minne
 Mistari mitatu ya kwanza ina vipande vitatu ilhali wa nne una kipande

 Vina katika kila kipande vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi


kimoja.

 Kiishio kimefupishwa.
mwingine.

 Kila mstari una mizani 20 isipokuwa kiishio chenye mizani 8


 Shairi lina beti 5
(zozote 5x1=5)

 Mbio za wasichana- uasherati/uzinzi/uzinifu


f)

 Haupandiki mgomba- hana uwezo wa kujamiana.


(2x1=2)

91
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Shairi la 2

 Shairi hili ni wasia kwa vijana; unawaonya dhidi ya kushiriki mapenzi.


a)

 Linashauri kuwa wanaovutia machoni wanaugua na hivyo wanaweza

 Zinaa hii haichagui wala kupendelea yeyote. Hata wenye nguvu au


kuwaambukiza maradhi yasiyotibika.

 Vijana wajikaze kuhakikisha kuwa hawaingii kwenye mtego wa kushiriki


warembo wamesalimu amri. (ubeti 4)

 Wapo watakaowasema wenye kujitunza lakini hilo lisiwafanye


mapenzi.

kutetereka. (zozote 4x1=4)

 Tabdila- kubadili miendelezo ya maneno pasi na kubadili idadi ya


b)

mizani. Mf. nisikia badala ya nisikie. Limetumiwa hivi ili kukidhi

 Inkisari- kufupisha maneno. Imetumiwa ili kuleta ulinganifu wa mizani.


mahitaji ya vina.

Mf. sikuwambia- sikuwaambia, jepusheni- jiepusheni, ngawa- ingawa,


waone- uwaone, ngia- ingia, walopapia- waliopapia, watalokwamba-

 Kuboronga sarui/miundo ngeu ya kisintaksia- ni mpangilio wa maneno


watakalokwamba.

katika tungo kutofuata utaratibu wa kisarui wa lugha ya Kiswahili.


Mf. yaugua nisikia- nisikie yaugua, si mlango nyumba nzuri- nyumba
nzuri si mlango, makaa kujipalia- kujipalia makaa, madhara kukadiria-

 Mazida- vyang’aria badala ya vyang’ara.


kukadiria madhara, mapoda kumichia- kumichia mapoda.

 Utohozi- Sitoria- history


Mazida na utohozi zimetumiwa kuleta urari wa vina.
(kutaja al. 1, mfano al.1 za kwanza 4x2=8)

 Vijana (ubeti 1-8)


c) Pande mbili ambazo mshairi anasema nazo ni;

 Mungu (ubeti 9) (2x1=2)

 Hutumiwa kusisitiza wazo au kumfanya msomaji kushawishika na


d)

mtazamo wa msanii. Kwa mfano ubeti wa 6, mshairi anamshawishi

 Hutumiwa kuzindua. Ubeti wa 5 anamzindua msomaji kuona kuwa


msomaji kwamba hakuna faida ya kuingilia anasa.

 Humfanya msomaji kulidadisi jambo linaloibuliwa. Katika ubeti wa


hata wenye nguvu huangamizwa na zinaa.

sita msomaji atavuta ikra kuhusu ‘faida’ ya kuingia kwenye anasa ya

 Hutumiwa kusuta watu au kukashifu jambo. Ubeti wa 5 unawakashifu


kumuua. Kwa kulidadisi hili ataona kuwa hamna faida na hivyo kujirudi.

waliopapia anasa na kuwatahadharisha wasomaji kwa kuonyesha kuwa

 Maswali ya balagha ambayo yanalenga msomaji wa kazi ya fasihi


hatima ya anasa ni kifo.

hunuiwa kumfanya kulitafakari jambo hivyo kujifunza kwalo.


(zozote 3x1=3)
92
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Toni ya huzuni/kusikitika- anasikitikia madhara yatakayowapata


e)

wanaoingilia zinaa kwa kauli kama vile ‘wawapi leo madume, anasa

 Toni ya kunasihi au kushawishi- anawasihi vijana kuepuka zinaa. Mf


walopapia?’ ubeti 5

 Kukejeli/kudharau/stihizai/bezo
anawaambia, ‘kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia.’ Ubeti 7

 Uchungu- anaonea uchungu tabia ya vijana.


(kutaja al. 1,kueleza na kutoa mfano al. 2, yoyote 1x3=3)

93
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2011
Kujitegemea
a)Umuhimu wa nchi kujitegemea/tatizo la mikopo na uombaji. (alama2)

 Ni tarbia/unne
b)
(alama 1)

 Manthnawi- vipande viwili katika kila mshororo


Sababu lina mishororo minne katika kila ubeti (alama2)

 Ukara- lina vina vya ndani vinatofautiana na vya nje vinafanana/urari


(alama 1,2)

wa vina.

 Kupata wataalamu wa ndani ya nchi kuendesha mambo-ubeti 4


c)

 Wananchi washiriki kufanya kazi/za aina yoyote-ubeti 5


 Wananchi wawajibike ubeti 2
 Kuepukana na mikopo maana haina faida-ubeti wa 5
 Kujiepusha na uzembe-ubeti wa 6,2
 Wananchi wasitegemea vitu bure ubeti 6
 Kuzingatia uongozi;wenye manufaa
 Wananchi waache kutegemea vya ugenini/kujihoji
 Wananchi wasaidiane-ubeti 3

 Inkisari/ufupisho- mbinu ya kufupisha maneno.


d)
(alama 2)
Mifano
-wanachi-ub3
-kupatakwe-ub3
-pamwe-ub 5
-yalomkini-ub 5
-alotimiza-ub 6
-wongozi-ub 5
-twambizanani-ub l

 Kuboronga sarui
AU
(alama 2)
-twaishije tujihoji
-tongo tupangusaneni
-mbele washike hatamu
-shujaa itakiavyo
-kondo tujiamueni.
e) Shughuli zote za kiuchumi ziko mikononi mwa wananchi na wakoloni
pamoja na wanyonyaji wametengwa kando bila kitu kwa hivyo ni muhimu
kufanva bidii maana hakuna njia nyingine ya kujiendeleza kwa kuwa daima
mwombaji wa heshima. Kila siku kuzembea na kukaa/kusubiri kupewa/
kusaidiwa. (Hoja4xl=4)

 Ulaya, ng’ambo,nchi za nje,nchi za mbali, ugenini


f)

 Kufananana, kuwa kama


(alama2xl=2)

94
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Haki
a) Ukosefu wa haki ulimwenguni/jinsi haki inavyokosekana maishani
(alama 2xl=2)

 Shairi la tarbia-mishororo minne


b)

 Msuko-mshororo wa mwisho umefupishwa


 Ukawai- mpangilio wa vipande vitatu katika kila mshororo
 Sabilia -halina kibwagizo
(Tuza; kutaja 1; maelezo 2 jumla 3)

 Tashihisi -haki inazungumziwa kama binadamu/haki inapewa wasifu


c)

 Takriri /Uradidi-neno haki


wa kiumbe.

 Siyahi/nidaa- mwisho wa kila ubeti


 Ritifaa- kuzungumza na haki kana kwamba ni binadamu
(Tuza yoyote moja, kutaja l, mae!ezo 2, jumla 3)

 Matumizi ya msamiati usiokuwa wa kawaida k.m machumi- ubeti 2


d)

 Inkisari- mbinu ya kufupisha maneno au kuyahademi k.m waloteuliwa


–ubeti 4 badala ya

 Msamiati wa kilahaja “tukiifatia” ubeti 5


walioteuliwa, ilotoweka, itavyopatika.

 Tabdila- kunaienea, hakukumbukae


 Kuboronga sarui- siyo hao mabwana, na vikubwa visa
 Utohozi- ‘tukisi’- busu (Tuza hoja zozote 3x2=6)

e) Haki haifanyiki au haipatikani mahati penye mambo au visa vingi/watu


hawataki kufanya lolote la haki mradi watapata pesa/sisi tunapata shida
kubwa ila wao wako sawa/haya ndiyo ya leo au siku hizi.
AU
Watu wanapopatwa na shida/mkasa/taabu/visanga hawatendewi haki. Ili
kutendewa haki au kusaidiwa ni lazima walipe pesa/hongo. Wakati wa shida
hawahurumiwi, hakuna utu/ hawajali/hawana hisia na huu ndio mtindo wa
kisasa/na hivyo ndivyo ilivyo siku hizi. (Hoja 4xl=4)

 Mahali tulipo panatuumiza/panatutesa/panatudunisha/panaturudisha


f)

 Kuweza kuikiri/kusema/kubusu/kutetea
nyuma
(al 2)

95
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2010
Dhamiri yangu

 Kufugwa
a)

 Kunyimwa uhuru
 Alipofungwa pameharibika
 Angependa kuhama lakini hawezi
 Kuna majani mengi mbele yake lakini hawezi kuyaikia - chakula
 Analalamikia upungufu wa chakula/njaa/sahani imeenda mbali
(4 x 1 = 4)

 Amekwisha zoea hali yake


b)

 Hapendi kuonekana tofauti, Hataki kuukosa utu kwa sababu amefungwa


katika kamba ya ufu/hana misimamo yake, analazimishwa na sheria,

 Hataki kuleta madhara kama walivyofanya mbuzi na mbwa


dini, itikadi n.k

 Aweze kupata kisingizio au sabbau ya kulalamika (Yoyote 1 x 2 = 2)

c) Ni dhamini katika nafsi yake ambayo ameshikilia ambayo haionekani kwa


macho ndiyo iliyomfunga/hajafungwa na yeyote, amejifunga na nafsi yake.

 Tashbihi - kama mbuzi, kama mbwa


d)

 Isitari/sitiari/jazanda - sahani ya mbingu, kamba isiyoonekana

 Tasida/tauria – nimekwisha pachafua


- mti wa utu

 Takriri/uradidi/marudio/kusiiza - kamba, kamba


 Nidaa/Siyahi - Oh!

 Tashihisi/Uhuishi/uhaishaji
- uhuru!
- Dhamiri imenifunga
- Sahani kwenda mbali

 Taswira - kamba fupi/mbuzi kuzunguka


- Mti wa utu

 Tanakuzi - anataka kufunguliwa lakini tena hataki


- mbwa kusukuma sahani mbali

 Kinaya – nasmhukuru aliyenifunga (Zozote 2 x 2 = 4)


e) Mishata- Mishororo ambayo maana yake inakamilika katika mshororo

 Nami kwa mbaya bahati, katika


unaofuata mf.

 Uhuru kupigana, sahani ya mbingu


 Nimepiga teke na nigusapo kwa mdomo.
 Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena.
 Nami sasa sitaki ikatike maana.
96
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba


(Zozote 2 x 2 = 4)
f) Nimefungwa kama mbwa na kwa bahati mbaya katika kutaka kuondoka
pale nimeipiga teke sahani ya mbingu ambayo imeenda mbele na siwezi
kuiikia. Na pale nilipofungwa ni pachafu ila siwezi kupatoka.

AU
Mshairi analalamika kufungwa kwake kama mbwa. Katika harakati zake
za kupigania uhuru na kufanikiwa kuupata alichotaka hata akizidisha bidii.
Mahali alipofungwa amepachafua na hawezi kupaondoka. (alama 4)

97
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2009
Kibaruwa
a) Maisha ya wafanyakazi na vibarua shambani ni duni na ilhali wanaofaidika ni
wengine. (al.2)

 Tabdila- mvuwa, kibaruwa


b)

 Lahaja- mte, kutipuza, mtilizi


 Mazida- tisiya
 Inkisari- Ikajinamiya, lingiapo (kutaja 1, mfano 1 zozote 2x2=4)

 Tamathali mf.
c)

- Tashisi/uhaishaji/uhuishi- ndege watumbuiizao, upepo uvumao kwa


ghadhabu,mito itiririkayo
kwa furaha.
- Ritifaa- waulize ndege kwa nyimbo, iulize na mito
- Taswira- maji itiririkayo, upepo mkali wa ghadhabu uvumao

 Mbinu ya kimuundo mf.


- Takriri- iulize, waulize,uulize (kutaja 1, kueleza 1, yoyote 1x2=2)

- Usambamba/takriri- urudiaji kimuundo


- Kipande kimoja
- Mizani ni sawa katika kila mshororo- 19 (kutaja 1, kueleza 1)

 Jasho la vibarua linafaidi wengine


d)

 Wale wanaonyonya vibarua wajue kwamba wanafanya lisilostahili


 Vibarua wenyewe wazinduke (mshairi anauliza maswali ya

 Jamii nayo ijue vibarua wananyonywa


kuchochea,ya kutafuta mwelekeo)

 Wanaotarajiwa kushughulikia haki za vibarua hawajali


 Vibarua wanafanyishwa kazi nyingi kwa malipo duni
 Wanadharauliwa na kutukanwa (zozote 2x2=4)
e) Swali ni kwamba ni nani anayelima na kupalilia mashamba? Mimea
inayopatikana mashambani ikazaa kwa wingi kutokana na juhudi za
mkulima ambaye ni kibarua. Mwishowe ni nani anayepata utajiri wa
mali hiyo yote akajilimbikizia, akanona na kuwa kama ana mimba hata
akaongeza magari na kujipatia starehe kama kuwabadilisha wanawake.
Swali hili liulizwe ili kubainisha ni nani hasa anayefanya kazi hiyo.
(al. 4)

 tajiri au mwenye shamba


f) Kibarua manamba ni jina la:

 mfanyikazi shambani (tazama matumizi ya herui kubwa)

98
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

Kila mchimba kisima

 Tendo litendwe kwa hekima kulingana na kauli tunazotoa


a)

 Ukitenda la faraja utafaidika


 Mtu anayetoa kauli au kutenda mabaya anajiletea maangamizi au

 Mtu humfunza mwana ndipo mwana awe na heshima ili yeyr kama
kujivunjia heshima

 Ni vyema kutenda wema ndipo mtu hupata heshima na baraka


mzazi asilaumiwe

 Ni vyema kubainisha matendo mazuri na maovu (zozote 4x1=4)

 Mtu binafsi- kauli zenye upendo humfurahisha mtu binafsi


b)

 Jamii- kuonyana na kuelekezana ni muhimu.


- kalima yenye upendo kufurahisha mtima- ubeti wa 1

 Mtoto- ni jukumu la mzazi kumfunza mtoto wake maadili

 Mzazi- nisipokwambia wewe, hukufunza kila jema- ubeti wa 5


- mtu hufunza mwanawe, kwanza ajue heshima- ubeti wa 4

(kutaja 1, mfano 1, hoja 3x2=6)

 Kama kimalizio cha ubeti


c)

 Msisitizo/ukariri wa ujumbe wa mshairi au kama dhamiri yake


 Mtu binafsi, jamii, mzazi au watoto wasipotenda mema watapatwa na
athari za maisha (hoja 2x2=4)

99
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

KCSE 2008
Wasakatonge

 Wanajamii wanajishughulisha katika kazi mbalimbali ili kuboresha


a)

 Vibarua (manamba, wachapakazi, mayaya, madobi, matopasi)


maisha yao lakini maisha yao ni duni.

 Viongozi serikalini wamepewa nyadhifa hizo za hadhi lakini hawajibiki


wanaoajiriwa wanafanya kazi kwa bidii lakini mishahara yao ni duni.

 Tabaka la chini ndio walio wengi katika jamii na ndio tegemeo la jamii
kunyanyua hali za waliowachagua

 Haijulikani mateso ya walio wengi yataika kikomo lini (zozote 4x1= 4)


lakini wanaishi maisha ya mateso mengi.

 Kinaya
b)

i) Wasakatonge ndio wengi lakini hawana sauti


ii) Makuli, mayaya, matopasi, wachapakazi nk ni maskini
iii) Wasakatonge wafanyao kazi kwa mateso mishahara yao ni duni
iv) Wapelekao watu serikalini hawashughulikiwi na walowachagua
v) Wazalishao mali hawana chochote bado ni maskini ( manamba, ma-

 Taswira
dobi, mayaya, wachapakazi)

i) Wabeba zenge ya marashani


ii) Wasukuma mkokoteni
iii) Makuli bandarini
iv) Wachimbaji migodini
v) Manamba mashambani
vi) Wachapakazi viwandani
vii) Matopasi wa majaani
viii) Wanasiasa madarakani

 Takriri
ix) Mayaya na madobi wa nyumbani (siku zote wako matesoni)

i) wasakatonge
ii) Juakali
iii) Lakini
iv) Wao
v)
 Ulingunuzi/ulinganushi
Ni

- wachimbaji migodini lakini maisha-yao ni ya chini


- wachapakazi viwandani lakini maskini

 Kipande kimoja
c)

 Shairi lina kituo/kimalizio


 Mizani hailingani katika kila ubeti
100
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

 Beti 4
 Mishororo 6 kila ubeti/ tasdisa / usita au kila uneti una kichwa au

 Mshororo wa kwanza vina vinabadilika (li na – nge)


kijichwa / anwani na kila ubeti una mishororo mitano

 Mishororo mitano ina vina vinavyofanana (ni)


 Mishororo wa kwanza katika kila ubeti unapindapinda (pindu)
 Neno lakini limetumiwa mwanzo wa kila kituo- kikwamba
d) Watu wa tabaka la chini/ndio huwapa nyadhifa viongozi/ kutolana na
nyandhifa hizo viongozi hupata mali au uwezo wa kiuchumi/ wale
waliowachagua maisha yao ni ya kusikitisha.

 Kufanya kazi kwa bidii


e)

 Kuwajibika – kwa umma katika kushiriki kuwachagua viongozi


 Viongozi wanastahili kuadilika kwa kunyanyua hali za umma na kujali
hali ya wafanyikazi
f)

 Manamba- vibarua, wafanyikazi


 Tabaka lilisilo ahueni – watu maskini/wasio na hali nzuri kiuchumi/
walalahoi

101
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

MAREJELEO
Abedi, K.M. (1954) Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri.
Nairobi: Kenya Literature Bureau.
Arege, T. (2013) Tunu ya Ushairi. Nairobi: Oxford University Press.
Arege, T. (2016) Fani ya Ushairi kwa shule za Upili. Nairobi: Oxford
University Press.
Kezilahabi, E. (1973): “Diwani ya Massamba”, katika MULIKA Na. 13.
Dar es Salaam: TUKI.
Kitula, K na Amata, K. (2001) Taaluma ya Ushairi. Nairobi: Acacia Stantex
Publishers.
Khasiani, D. (2014) Mwongozo wa KCSE Fasihi. Nairobi: Vide- Muwa Publishers
Limited.
Mohamed, S.A. (1980) ’Sikate Tamaa. Nairobi: Longman Publishers.
Mulokozi, M.M. na Kahigi, K.K. (1973) Mashairi ya Kisasa. Dar es Salaam:
Tanzania Publishing House.
Mutali, C.S. na Mbugua, D. (2004) Uhakiki wa Mashairi. Nairobi: JB Publishers.
Walibora, K. (2007) Malenga wa Karne Mpya. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

102
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

103
MWANGA WA USHAIRI KWA SHULE ZA UPILI

104

You might also like