Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 7

MASWALI YA BEMBEA

Kwa majibu piga simu 0729125181


1. Anwani bembea ya Maisha inaafiki tamthiliya hii. Jadili kwa kutoa hoja ishirini (alama 20)

2. Kwa kurejelea tamthilia hii eleza namna mila na desturi zinavyoweza kuzua migogoro katika jamii.

(alama 20)

3. A. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali.

"La! Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani

Kwa majibu piga simu 0729125181


akijua itamfaa tena. Kinacholelewa hakina budi kulea."

a) Fafanua muktadha wa mancno haya. (alama 4)

b) Taja mbinu nne zilizotumika hapa. (alama 8)

c) Eleza sifa nne za mnenaji (alama 8)

4. A. Soma dondoo kisha ujibu maswali.

"Kumbuka, mrina haogopi nyuki. Marehemu mamangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi

mwanadamu wala hazipotei bure — humalizwa tu na mabuu. Mwanangu, usifanye hofu. Nikujuavyo

mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. yote yana kikomo ati! Ipo

siku haya yote yatapita. Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki

safl kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi

zilizopigwa pasi zikanyooka."

a) Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)

b) Fafanua sifa moja ya mnenaji inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)

c) Fafanua mbinu zilizotumika (alama 8).

d) Onyesha kuwa msemewa hakuingia bahari ambayo si yake (alama 6)

5. Soma dondoo kisha ujibu maswali.

Eti alama! My foot! Eti ameshuka nafasi darasani lakini akapandisha alama...

Kwa majibu piga simu 0729125181


a) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)

b) Jadili sifa tano za mnenaji. (alama 10)

c) Tathmini umuhimu wa mnenaji katika tamthilia. (alama 8)

6. Soma dondoo kisha ujibu maswali.

“Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli,: Hata wahudumu wenyewe hawana mlahaka mwema. Amri na

vitisho kama askari. Unashindwa kama UUguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu

ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini

ya kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka katika sala”.

a) Changanua mtindo wa dondoo kwa kurejelea hoja tano. (alama 10)

b) Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. (alama 10)

7. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali.

‘...wanajikuta katika vuta n'kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo

pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na
mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani,

ushirikiano, upendo, kutanabahi, na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara.. ."

a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)

b) Hakiki mtindo wa dondoo hili. (alama 2)

c) Fafanua mitikiso saba inayotishia mahusiano ya kijamii ya tamthilia hii. (alama 14)

Kwa majibu piga simu 0729125181


Kwa majibu piga simu 0729125181
Kwa majibu piga simu 0729125181
22. Mwandishi wa Bembea ya Maishaameipa uzito mbinu rejeshi. Eleza. (alama 20)

23. Soma dondoo hili na ujibu maswali.

"Mtu anaishi na wanawe ambao wiki nzima anawaona wakiwa usingizini; wamelala
fofofo.. .Nyumba ni

ya yaya."

i. Weka maneno haya kwenye muktadha wake. (alama 4)

ii. Fafanua maudhui yanayojitokeza kwenye dondoo. (alama 2)

iii. Fafanua manufaa saba ya mazingira ya dondoo hili. (alama 14)

24. Soma dondoo hili kisha ujibu maswali.

‘Maisha yetu ni mfano wa mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo haina budi kuoza kwanza ndipo
ioteshe mche

upendezao. Mche huo wa asili ya mbegu iliyooza, hatimaye hutoa zao la mbegu nyingi ajabu.
Ukitazama

vizuri, mbegu ile haifi bali huchukua mkondo mwingine wa maisha. Huchukua umbo)ipya
lipendezalo

hasa ikiwa itakuwa imeangukia ardhi nzuri.. -Sasa rudini msaidie kuzalisha mbegu nyingi nzuri.
Nyinyi

Kwa majibu piga simu 0729125181


mmebahatika kuwa mbegu nzuri istahiliyo kupandwa."

Hakiki ukweli wa maneno haya kwa kurejelea Bunju,Neema na wahudumu hospitalini. (alama
20)

25. Bembea ya Maisha ni tamthilia inayohimiza mshikamano wa kijamii. Jadili. (alama 20)

26. Mwanamke anaonyesha maumbo mbalimbali, mazuri na mabaya.

27. Elimu ni mafundisho aali yatolewayo darasani au katika jamii. Jadili kwa kurejelea tamthilia
ya Bembea

ya Maisha (alama 20)

28. “Imani na itikadi huthaminiwa sana na jamii ya watu”. Jadili ukweli wa kauli hii kwa
kurejelea tamthilia

ya bembea ya Maisha (alama 20)

29. Mwandishi wa tamthilia hii ameshughulia sana suala la Mabadiliko katika jamii. Fafanua
(alama 20)

30. Eleza jinsi mwandishi watamthilia ya Bembea ya maiisha alivyofanikiwa kutumia ishara
katika kazi (alama 20)

Kwa majibu piga simu 0729125181

You might also like