Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

AHADI ZA WANAO FANYA HARUSI

CHRISTELLE :

Mupenzi wangu Imani , Naagana nawe leo kwa kuhakikisha ninavyo kupenda na kuwa nimeachana na
wazazi wangu kabisa ili kama lilivyo Neno la Mungu katika biblia , naambatana nawe na kukaa nawe
kuanzisha mimi na weye , yetu jamaa .

Tangu hivi Sasa tunaanza maisha ya pamoja katika ndoa .

Nitakuheshimu na kukutii Sana maisha yangu yote , mufano wa Kanisa la Kweli mbele za Kristo

Nimekubali kuwa msaadaidizi wako wa maisha yote ( kwa mwili , roho katika kumuheshimu Muumba
wetu Yesu Kristo.)

Kwa Neema yake Kristo , ambae ame nipa wewe leo Uwe mume wangu , nita kutunza na pamoja
naweye tutawapenda wana wetu , kuwatunza wote na kuwalea Sawasawa na Maandiko ya biblia .

Chéri Imani, Mbele za Mungu , mbele ya Kanisa lote , machoni pa wazazi na mbele za Watu wote ,
ninaagana nawe kama Nitakuwa Mwaminifu katika ndoa yetu .

Niko tayari kwa musamaha na kukuchukuliya Mara yote .

Nitakuheshimu Sana na kukusikiya katika kila lililo njema machoni pake Mungu .

Tangiya saa hii , ninakuwa wako walote na weye wangu pasipo kuchangiya n'a mwengine mutu
yeyote . kifo cha Uzee ndicho kitakacho tutenganisha

(1+1=1) Amen

IMANI i:
Chérie Christelle

Mbele za Mungu na kwa ushahidi wa Kanisa nawa hawa Watu wote , Naagana naweye kuwa Tangu Sasa
wewe ndiwe muke wangu .

Nitazidi kukupenda na kukutunza .

Nitakuwa Mwaminifu kwako na kwa kanisa na zaidi kwa Mungu wetu .

Naagana nawe kuwa mimi na weye tangiya leo tunakwama mwili moja .

Weye wangu mimi wako .

Byangu njoo byako , byako njoo byangu .

Neema yake Kristo iwe nyingi kwetu mimi na weye n'a wazao wetu , katika maisha yetu yote, katika
imani, tumaini na upendo katika Yesu Kristo.

Kati wanawake wote duniani, sikumuona na hatakuwaka wakunitenganisha nawe Ila kifo cha uzee katika
Imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Amen .

You might also like