Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 59

12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Mengineyo

MAARIFA SHOP
MAARIFASHOP ni mtandao unaokupa maarifa mengi ya kukuwezesha kushinda changamoto nyingi za kiuchumi na maisha kwa ujumla. Kumbuka
maandiko yanasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa"

Home Motisha wa Kazi nani Anapaswa Kutoa? Vitabu Wajasiriamali Kaya na Uchumi Ufunguo wa Pesa

Kiongozi AfyaYetu Biashara

Ufunguo wa Pesa Umependa Makala?

Pesa Yako ni Ishara ya Nini? KamaUnajua


Usisome Hapa About Me

MUSHONGI
View my complete profile
"Pesa ni Mwakilishi Shughulika na Anayewakilishwa" ~ CYPRIDION MUSHONGI

WEKA E-MAIL KUPATA MAKALA


BURE

Subscribe to our mailing


list

* indicates required
Email Address

*
First Name

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 1/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Last Name

Subscribe

Popular Posts

Fahamu Mambo Sita


Kuelekea Kwenye
Mabadiliko Chanya
“Njia nzuri na ya pekee ya
kuweza kusaidia maskini
ni kutokuwa mmoja wapo” 1. Acha
kuamini yale uliyodhania ni kweli:
Bahati mbaya, k...

Unaposikia Uwekezaji
Katika Hisa Unapata
Picha Gani?
“Mtu anayeuza hisa ni
sawa na mtu anayeuza
kuku wakati anapenda mayai” ~
Cypridion Mushongi Neno "hisa"
limekuwa maaru...

UZIO WA MJI NANI


ANAFUNGUA LANGO
LAKE?
Pesa ni kitu gani mpaka karibu kila mtu anaitafuta? Kama pesa inatafutwa na kila “Mahitaji ya lazima ni
machache lakini vitu
mtu, lazima kujiuliza wapi hasa inapatikana. Je? Ni kweli wote tunafahamu
tunavyovitaka havina kikomo” ~
sehemu au mahali inapopatikana? Kama mahali pesa ilipo hapajulikani tutawezaje Cypridion Mushongi Wengi tunafahamu
kuipata? Maswali yote haya yanahitaji majibu kwanza kutoka kwa kila mmoja wetu nyumba nyingi zina uzio wa ...
ambaye anazitaka pesa kwa dhati.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 2/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Fanya Mambo 5 Leo


Maswali yote haya pia ndiyo yanatoatafsiri halisi ya kwanini kila mmoja Kufaidi Nguvu ya Fikra
Zako
anakwambia kuwa anahangaika kutafuta pesa, wengine wanakwambia siku hizi
Fanya Mambo 5 Leo
kuwa wanapambana. Yote haya yanaonyesha dhahiri kuwa kuna vita ndani kwa Kufaidi Nguvu ya Fikra
ndani katika fikra, akili na nafsi zetu juu ya wapi pesa itapatikana. Zako Fikra zetu kutoka ndani ya akiri
zetu ndiyo kila kitu. Fikra ndilo dirisha
unalotumia ...
Uzoefu unaonyesha kwamba mahali pesa ilipo bado hapajulikani kwa waliowengi.
Kutokana na hali hii, wengi suala la kutafuta pesa linabaki kuwa suala la UNAPOAMUA KUANDIKA HISTORIA
kubahatisha na kubangaiza. Kutafuta pesa kwa kubangaiza kumekuwa ndiyo hali YA MAISHA YAKO USIKUBALI MTU
MWINGINE AKUSHIKIE KALAMU
ya maisha ya kila siku kwa waliowengi. Kwakuwa maisha ni safari ambayo
unasafiri muda mrefu kabla ya kufika
Wakati ukiendelea kutafuta majibu ya maswali hapo juu, ni vizuri kutambua unakokwenda au kufikia maisha ya
ndoto yako. Wakati ukiendelea na sa...
mambo makuu muhimu juu ya pesa; Moja ni kwamba, pesa halisi inapatikana
ndani yetu; Pili, pesa yote unayoiona ni ISHARA tu ya kitu fulani kilichofanyika. Mafanikio Yako
Yamejificha Ndani ya
Thamani
Pesa inakuwaje ISHARA na kupatikana ndani yako?
Mafanikio Yako
Yamejificha Ndani ya
Nguvu ya hisia ikichanganyika na matamanio ndani ya akili, inaachia nguvu ya Thamani Kadiri utakavyozidi
kutengeneza thamani nyingi kwaajiri ya
ubunifu wa vitu na huduma mbalimbali.
watu wengine, ndivyo utakavyoz...

Baada ya hapo akili yako inakusukuma ili ukamilishe kazi ya kubadilisha huo
ubunifu uliopo katika hali ya wazo kuwa vitu halisi ambavyo mwisho wake
Blog Archive
hukuletea pesa.
▼ 2023 (4)
Ndiyo maana tunasema PESA ni ishara ya nguvu ya ubunifu ulionao katika hali ya ▼ March (1)
kuonekana kwa macho. Kwahiyo, pesa tunatembea nazo mawazoni mwetu, UZIO WA MJI NANI
tunalala nazo usingizini, tunakuwa nazo kila mahali tunapokua. ANAFUNGUA LANGO
LAKE?

Kazi tunayo moja tu nayo ni kuzitoa huko ndani yetu. Ili tuweze kuzitoa pesa ndani ► January (3)
yetu tunahitaji kuendelea kujifunza namna bora ya kuzitoa nje, maana zikikaa
► 2021 (3)
tutakufanazo.
► 2020 (12)

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 3/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

► 2018 (8)
Binadamu ukishapata kile unachohitaji na ukawa na uhuru wa kuchagua upate nini ► 2017 (36)
na uache nini ndiyo unapata kuishi maisha ya furaha na kuridhika pia.
► 2016 (41)
► 2015 (38)
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba wewe umejaliwa nguvu ya ubunifu ndani yako
na hiyo ndiyo hazina ya pesa uliyonayo. Kwahiyo, unatakiwa kuwa mtu mwenye
matumaini na kuhakikisha hofu na mashaka havina nafasi kwako.
JAZA E-MAIL KUPATA MAARIFA

Habari njema ni kwamba leo hii kuna idadi ya watu wengi sana ambao tunakaribia
kuwa watu bilioni tisa hivi.
WATEMBELEAJI WETU
Watu wote hawa wako tayari kulipa pesa ili kukidhi mahitaji yao. Unachotakiwa
kufanya kama wewe ni kukidhi mahitaji ya asilimia ndogo sana ya watu wote 92,303
walioko hapa duniani.

Kwahiyo, ukiona umepata pesa ujue kuwa hiyo ni ishara inayoonyesha nguvu ya MAARIFASHOP
ubunifu ndani yako.
Search

Wengi wanaofikiri hawana pesa siyo kwamba hawana nguvu ya ubunifu


tunayosema BALI ni kwamba hawajachukua muda wao kutambua kuwa nguvu
hiyo ipo lakini pia hawajachukua hatua ya kuibadilisha nguvu hiyo kuwa vitu halisi
vyenye thamani na ambavyo vinaweza kuuzika kwa watu wengine tukapata pesa.

Kila wakati tuzame zaidi katika kutafiti na kufuatilia hitaji hasa la jamii tunayoweza
kuifikia na katika hitaji lao hilo tuone pesa kwa macho yetu ya rohoni.

Tukishaona kwa macho ya ndani tuanze kufanyakazi ya kuitoa ndani kwa maana
ya kufanyakazi kwa vitendo ili kukidhi hitaji lililopo kwenye jamii husika.

Kazi ya nguvu ya ubunifu ikishakamilika, watu wenye uhitaji wataleta pesa kwako
na utaanza kuikusanya kwenye kapu, hapo ndio itaanza kuonekana kwa watu
wengine.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 4/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Baadae, utaanza kusikia watu mtaani wakisema fulani amezipata pesa, sijui
amezitoa wapi wakati wao ndio wamezileta kwako….hivyo ndivyo maisha
yanavyokwenda.

Mpendwa msomaji wa makala hii litafakari sana suala hili la kuitoa nje pesa iliyoko
ndani kwani ni rahisi kuutokomeza umaskini moja kwa moja.

Najua unapenda kufuata njia za mkato lakini ukweli ni kwamba ukae ukijua kuwa
pesa inayopatikana kwa njia za mkato inadumu kwako muda mfupi sana na wakati
mwingine njia inayotumika siyo rahisi kuitumia wakati mwingine.

Kwahiyo, wakati ukiendelea na njia zako za mkato anza taratibu kufuata kidogo
kidogo njia hii ya nguvu ya ubunifu ili kutengeneza mfereji wa pesa zitiririkazo kuja
kwako bila kikomo.

Kwahiyo endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali


yatakayokuwezesha kuitoa nje pesa iliyoko ndani yako.

Kupata mafunzo ya kila siku na makala mpya kwa njia ya whatsap bonyeza
neno MAFUNZO.

Kama unapenda kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza kiungo


hiki; NITUMIE MAKALA kisha sajiri barua pepe yako.

Umuhimu wa Kutafuta Pesa Bila Sababu ni Huu

“Unashindwa kupata pesa nyingi kwasababu unatafuta pesa


kulingana na shida unazotegemea kupata siku zijazo” ~
Cypridion Mushongi

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 5/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye aliwahi kuniuzia


kiwanja siku za nyuma. Baada ya mwaka mmoja tangu rafiki huyo
aniuzie kiwanja, tulikutana mjini Bukoba na hapa aliniuliza juu ya mpango
wangu wa kukiendeleza kiwanja hicho. Jibu langu kwake lilikuwa...
“kwasasa sina pesa, ngoja kwanza nijipange”.

Jibu hili la kwamba mimi sina pesa halikumridhisha sana, ndipo


akaniambia maneno mazito tena kwa lugha ya kihaya! “Amahela Geija
Omubyemba!” Tafsiri isiyo rasimi kwa maneno haya ni kwamba “pesa
uja wakati wa matatizo na shida”.

Shida na matatizo yanayozungumziwa hapa ni kama vile kuugua au


kuuguliwa, kupatwa na msiba, harusi, kesi mahakamani, kudaiwa, karo

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 6/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

za shule, ndoa kuvunjika n.k.

Tulipoachana nililazimika kuandika maneno yale kwenye kitabu changu


cha kumbukumbu za kila siku. Wakati nikiendelea kundika nilizidi
kutafakari kwa kina, juu ya jambo hili la pesa kupatikana wakati wa
matatizo na shida. Nilizidi kujiuliza ni kwanini pesa ipatikane tu wakati
tunapopatwa na shida au matatizo?

Bilashaka, maneno ya rafiki yangu huyu, yalilenga kunikumbusha kuwa,


pindi nikiamua kwa dhati kuanza ujenzi, kwa vyovyote vile pesa
itapatikana tu!.

Ukichunguza kwa kina, utagundua kuwa watu wengi ambao ni maskini


ndani ya fikra zao, hawana na hawafikirii kuwa na pesa nyingi. Maisha ya
maskini ni kana kwamba wakati ambao hakuna shida au matatizo, haoni
haja ya kutafuta pesa!

Kwahiyo, kama hakuna shida, mara nyingi watu wengi uchagua


kutokuwa na pesa. Kwa maana nyingine ni kwamba, watu wa namna hii
wanapopatwa na shida, ndipo uanza kuona umuhimu na ulazima wa
kutafuta pesa.

Kwa watu wa namna hii hasa maskini, shida na matatizo ndivyo


vinakuwa sababu kubwa na kichocheo cha mtu kutafuta pesa kwa
namna yoyote hile. – Pesa upatikana kwa muda mfupi!.

Katika hili tunajifunza mambo mengi, lakini mojawapo ni kwamba “watu


wengi tunashindwa kupata pesa nyingi kwasababu hatujafikia hatua ya
kutafuta pesa bila sababu zinazotokana na shida.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 7/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Ukitafuta pesa baada ya kusukumwa na mahitaji ya matatizo pamoja na


shida, basi ujue fika kuwa zikishapatikana zitatumika mara moja kwaajili
ya kuondoa shida ambayo ndiyo ilikutuma uzitafute.

Matatizo na shida vikiisha na pesa inaisha. Pesa ikishaisha na wewe


unaedelea kuishi maisha yako ya siku zote. Maisha ambayo umezoea
kupata pesa ndogondogo basi!.

Matatizo mengine yanapoibuka ndipo unaanza upya kujituma tena


kutafuta pesa ili kukabiliana na shida zilizo mbele yako.

Imaonekana bila kuwepo sababu maalum na hasa inayotokana na


shida/matatizo ya wakati huo, wewe hauko tayari kutafuta pesa.
Kwahiyo, ni sawa na kusema “hakuna shida hakuna haja ya pesa”. Kwa
maana nyingine ni kwamba, wakati ambao siyo wa shida, kutafuta pesa
ni usumbufu. "Mtindo wa maisha ya namna hii ni hatari sana kwa maisha
yako".

Watu wengi wanashindwa kupata pesa nyingi kwasababu, wanatafuta


pesa kulingana na shida au matatizo wanayotegemea kupata siku zijazo.
“Haya ni majanga”!
Watu waliofanikiwa (matajiri) mara nyingi utafuta pesa bila sababu
zitokanazo na shida. Unapotafuta pesa bila sababu ya matatizo na shida
unakuwa na wakati mzuri wa kufikiria na kuendeleza miradi mikubwa na
yenye tija kwa watu wengi. Hii ina maana unatulia na kutafuta pesa bila
kukurupuka -Yawezekana ndiyo maana matajiri wana pesa nyingi.

Ikumbukwe kuwa, kila kitu afanyacho binadamu anakuwa na sababu.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 8/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Lakini, jiulize, wewe unatafuta pesa kwasababu gani? Aina ya sababu


ndiyo itakufanya ama upate pesa nyingi au upate pesa kidogo sana.

Sababu ya maskini kutafuta pesa ni kumaliza shida/dharura, majanga


aliyonayo. Lakini, watu matajiri utafuta pesa ili kuzidi kupata vitu vingi na
utajiri kwa ujumla.

Kwahiyo, ndoto, malengo, sababu, dhamira n.k. ya kutafuta pesa ndizo


zinatofautiana kati ya mtu na mtu. Kwa maana hiyo, wewe ndiye wa
kubadilisha malengo na sababu ya kutafuta pesa.

Mpaka hapa ni kwamba, kama wewe ni mmojawapo wa watu


wanaotafuta mafanikio, ni lazima uwe mtu wa kutafuta pesa bila ya
kusukumwa na sababu zitokanazo na shida/matatizo. Jitahidi kujituma
sana kutafuta pesa ikiwezekana jitume kuliko yule atafutaye pesa
kwasababu ya shida na matatizo.

Sasa umeyajua haya! Ni lazima tuanze pamoja kutafuta pesa bila sababu
zitokanazo na shida/matatizo.

Hatujachelewa hata kidogo tuanze leo.

Kwa maoni zaidi au ushauri jiunge NA mtandao huu kwa kubonyeza


neno hili: MAARIFA SHOP.

Siri ya Faida Kuwa Bora Kuliko Mshahara Imefichuka

“Lengo la biashara yoyote ni kutoa suruhisho ya matatizo


ya watu-kwa FAIDA” ~ Paul Marsden

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 9/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Pesa ambayo huwa tunapata mara zote utoka kwenye mifumo mikuu
miwili ambayo ni “mfumo wa mshahara” na “mfumo wa FAIDA”. Kati ya
mifumo hiyo, mfumo wa mshahara ndio unaotegemewa na kuaminiwa na
watu wengi. Lakini pia ndio mfumo ambao unazalisha maskini wengi, na
ni mfumo ambao watu wake uhangaika sana kutafuta pesa ya kujikimu.

Watu ambao huwa wanafanikiwa kupata uhuru wa kipato au pesa ni wale


ambao wanapata pesa yao nyingi kutoka kwenye mfumo wa faida kuliko
wale wanaotegemea pesa kutoka kwenye mfumo wa MSHAHARA.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 10/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kwa wale wote ambao tunapata pesa kutoka kwenye “mfumo wa


mshahara”, biashara yetu kubwa ni ya “KUUZA MUDA” kama ulivyo.
Kama unamiliki mfumo wa faida, unaweza kuwekeza pesa yako tena na
tena katika mfumo huo huo na hatimaye kupata pesa nyingi.

Mfumo wa mshahara unakupatia pesa mara moja kwa kipindi Fulani


kilichopangwa. Mfano kwa waajiriwa wegi serikalini pamoja na
makampuni makubwa ya binafsi, pesa inatoka mara moja kwa mwezi nje
ya hapo hupati kitu hata kama una shida kiasi gani hakuna namna.

Wakati huo huo, mfumo wa faida unakuwezesha wewe kupata pesa kila
siku. Unapoweza kupata mapato (pesa) kila siku inakusaidia kufikia
ulinganifu wa mapato na matumizi.

Ukweli ni kwamba, watu wengi tunaopata pesa yetu kutoka kwenye


mfumo wa mshahara tunakabiliwa na tatizo sugu la kutokuwa na
ulinganifu wa mapato na matumizi yetu. Kutokuwepo kwa ulinganifu wa
mapato na matumizi ndiko kunasababisha watu wengi kutumia zaidi
kuliko mapato yao halisi.

Mfumo wa mshahara unatufanya tupate pesa mara moja kwa mwezi na


wengine kama wakulima ni baada ya miezi miezi 4 hadi 6. Mfumo huu wa
kupata pesa mara moja baada ya kipindi kirefu ndio unatufanya watu
wengi kukabiliwa na mzigo wa madeni yasiyoisha.

Hali hii ndiyo inatufanya wengi hasa waajiriwa kushindwa kupata mitaji
ambayo ingetuwezesha kuingia kwa urahisi kwenye “mfumo wa faida”.
Kwa maana nyingine ni kwamba tayari tumejenga tabia au utamaduni wa
kula bila ya kuwa na pesa.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 11/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kitu kinachoitwa mshahara au ujira huwa siyo cha kudumu, muda


wowote kinaweza kukoma. Inatosha kusema kwamba, maisha ya
mshahara yanakutaka usiugue/usiuguze, usisafiri n.k.

Kwa maana nyingine ni kwamba ukisimama kufanya kazi, pesa nayo


inakatika hapo hapo. Pesa yako itakoma au kushuka kama utakuwa
unaumwa. Pale utakapostaafu, pesa yako itapungua..ingawaje unataka
pesa nyingi hasa pale unapostaafu

Hatahivyo, kama utajikita na kuegemea zaidi upande FAIDA , badala ua


mfumo wa mshahara basi ataweza kutengeneza pesa wakati akiwa
amesinzia au huko kwenye gym n.k. Endapo akiugua bado atatengeneza
pesa nyingi. ukistaafu, pesa yako itaendelea kama kwaida.

Maisha ya mshahara siyo rafiki kwa maana hayatoi mwanya kwako


wewe kuweza kufanya shughuli au mambo yale unayoyapenda. Mfumo
wa mshahara unatumia zaidi ya asilimia 90 ya muda wa mwajiriwa.

Kama mwajiriwa huna udhibiti wowote wa mshahara wako wa kila mwezi.


Wale wanaokulipa ndio wanaojipangia wakate ushuru kiasi gani bila hata
ya kukuuliza.

Siku zote waajiri wako wanakata pesa yao kwanza, alafu wanakupangia
kiasi utakachotumia kuendesha maisha ambayo wao wanaona ni
muhafaka kwako. Kimsingi maisha yako yote yanadhibitiwa hadi unakosa
kuifurahia dunia hii yenye maziwa na asali.

Kwa ufupi ni kwamba mfumo wa mshahara unakusaidia tu! wewe upate


kuishi LAKINI mfumo wa faida unakusaidia wewe kutajirika…jambo
ambalo ni zuri zaidi.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 12/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Uzoefu umeonyesha kuwa hakuna mtu yeyote ambaye huwa anatajirika


kwenye mfumo huu wa mshahara. Labda wanamichezo au wanariadha
wachache wenye majina makubwa. Wengine ni wakurugenzi wa
makampuni makubwa ambao pamoja na kuuza muda wao, pia, utajiri
wao mkubwa unatoka kwenye mfumo wa faida kupitia mikataba yao, kwa
mfano kuwekeza na kupewa kiasi fulani cha hisa za makampuni
wanayoyaongoza.

Njia pekee ya kupata ukombozi na uhuru wa kipato ni kila mara wewe


kutenga kiasi fulani kutoka kwenye mshahara wako, ili kuwekeza pesa
hiyo kwenye “mfumo wa faida” kama biashara ya hisa, ardhi ya
kukodisha, nyumba ya kupangisha, biashara ya kushirikisha rafiki zako
taarifa za bidhaa au huduma (jenga mtandao) n.k. hapo utakuwa tayari
kwenye mfumo wa faida.

Ili kupata usalama na uhuru wa kipato, ni wakati muhafaka sasa wa


kutoka kwenye “mfumo wa kuuza muda” ili upate pesa yako na kwenda
kwenye “mfumo wa faida”.

Ewe mtanzania, muda wa kuanza jitihada za kuingia na kupata pesa


kutoka kwenye mfumo wa FAIDA ni leo. Ni muda muhafaka pia wa
kuanza kujiuliza maswali magumu. Kwa mfano: inabidi ujiulize; utakuwa
wapi miaka 10 ijayo, endapo utaendelea kukaa kwenye mfumo wa
mshahara?, je? Ukiendelea kufanya biashara ya kuuza MUDA, utaacha
miaka 10 ipite bila kutimiza malengo yako?

Kuna mengi ya kuzungumza kuhusu jinsi ya kuhama kutoka kwenye


mfumo wa mshahara kwenda kwenye mfumo wa faida. LAKINI nimeona

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 13/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

ni vizuri wewe msomaji wa MAARIFA SHOP, … ukatoa maoni yako juu a


dhana hizi mbili yaani MSHAHARA na FAIDA……Endelea kutoa maoni
juu ya hili…

Unajua Kwanini Pesa ni Ngumu Kupatikana?

“Kutokuwa na pesa ni chanzo cha mabaya mengi”


~George Bernard Shaw.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 14/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Binadamu ili apate kufahamu kitu fulani lazima picha iliyoko kichwani
ilingane na kufanana na kitu unachotafuta. Endapo picha zikipishana
lazima itakuwa vigumu sana kupata hicho unachotafuta. Mara nyingi, tizo
hili la kupishana kwa picha linatokea zaidi kwa vitu vingi ambavyo siyo....
halisi, kama vile PESA. Katika suala la pesa, watu wengi wanapicha
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 15/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

ambayo haiendani na uhalisia wa pesa yenyewe. Kwa maana nyingine ni


kwamba pesa, siyo kitu halisi tofauti na inavyochukuliwa na watu wengi.
Kitu ambacho siyo halisi, mara nyingi huwa hakioneani kwa urahisi
mpaka utumie macho ya ubongo ndipo unaweza kukiona. Kwa maana
nyingine ni kwamba pesa ni kitu ambacho akionekani kwa macho, na ni
kitu ambacho SIYO HALISI.
Watu wengi wanadhania kuwa pesa ni kitu halisi, ndiyo maana wakiona
zile noti na silver wanadhani wameona pesa…hapo kila mmoja utakuta
anafukuzia ufukuzia noti lakini bila mafanikio yoyote.

Inatosha kusema kuwa katika utafutaji wetu wa pesa tuko katika makundi
makuu mawili ya watu. Kundi la kwanza ambalo ndilo la wengi ni lile
linaloichukulia pesa kuwa ni kitu halisi na mara nyingi hawa wanatumia
HISIA zaidi katika kufanya maamuzi mbalimbali juu ya utafutaji wake.
Kundi la pili ni lile la watu wachache ambao wanaitambua pesa kama
“kitu ambacho SIYO HALISI ~ ni WAZO” na mara nyingi wanatumia
ukweli katika kupanga na kuchagua njia za kuitafuta pesa.

Mara nyingi kundi ambalo linadhania kuwa PESA NI KITU HALISI,


imekuwa vigumu sana kwao kupata pesa endelevu na wakati mwingine
wameweza kuzikosa kila wanapoweka mtego. Kama usipochukua muda
wako kutafakari juu ya pesa, ni rahisi sana kushawishika na kuona kile
unachokiona kwa macho kama kitu halisi.

Hatari ya kuiona pesa kama KITU HALISI ni pale unapoifunga akiri yako
isiweze kuona na kujua kile kinachosababisha pesa kuingia mfukoni.
Kwakuwa akiri yako itakuwa tayari imejifunga basi mwisho wake ni
kwamba hautajali kuboresha au kuendeleza kile ambacho
kinakuwezesha wewe kupata pesa hiyo unayoifurahia sasa.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 16/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kwa upande mwingine ni kwamba, ukiweza kuitafakari pesa katika


uhalisia wake basi utaipata bila wasi wasi wowote, kwani kila mara
utashikiria sana kile ambacho huivuta pesa kuja kwako.

Nitamjuaje mtu ambaye anaichukulia pesa kama kitu halisi? Ni wazi


kuwa umewahi kuwasikia watu wengi wakisema kuwa pesa ni sabuni ya
roho, pesa ni kila kitu, pesa ni bahati, siri ya kupata pesa aijulikani n.k.
Hisia za namna hii juu ya pesa ndizo zinawafanya watu wengi kupenda
kutumia njia za mkato ilimradi tu wamezipata.

Utumiaji wa njia za mkato katika kutafuta pesa umesababisha madhara


mengi sana kwenye jamii zetu hizi hasa za kitanzania ambazo hazijawa
na mifumo imara ya kijamii. Tumekuwa tukishuhudia wizi wa pesa, watu
wanadhurumiana, watu wamejenga chuki na ndugu na jamaa na
mengine mengi.

Madhara mengine ni ya kiuchumi kama kaya na taifa kwa ujumla…Watu


wengi wanaodhania pesa ni kitu halisi siyo rahisi kwao kuamini katika
kuzalisha vitu na huduma (thamani).
Wengi wanakuwa hapa katikati au mwishoni mwa ule mnyororo mzima
wa uzalishaji. Mwisho wake bidhaa na huduma zinakuwa chache sana
kiasi cha watu wengi kushindwa kuzipata kutokana na bei yake kuwa
kubwa.
Nchi ambayo ina watu wengi wa namna hii, mara nyingi inategemea
sana bidhaa kutoka nje ambazo tumeshuhudia kuwa ni feki (bei rahisi)
jambo ambalo limefanya thamani ya shilingi ya Tanzania kushuka kila
siku.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 17/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Watu wengi wakizidi kuamini kuwa pesa ni kitu halisi, ni wazi kwamba
siku zote wataendelea kuamini kuwa pesa walizonazo ni kidogo na
mwisho kujikuta wakijenga wivu na chuki dhidi ya wale wanaowadhania
kuwa wanazo pesa nyingi.

Falsafa yangu katika hili ni kwamba “Ukidhania pesa ni kitu halisi, basi
ujue kuwa hata njia na mbinu utakazotumia kutafuta zitakuwa
zinafanana na zile za kutafuta vitu halisi”.

Kwa kawaida, upatikanaji wa vitu vyote ambavyo ni halisi huwa ni wa


moja kwa moja; unatumia mchakato mfupi kuvipata. Ukitaka kitu fulani, ni
kiasi cha wewe kunyanyuka na kufuata kilipo. Pia, vitu vyote ambavyo ni
halisi, michakato yake ya kuvipata huwa ni rahisi sana na hauhitaji kufikiri
sana.

Mfano: Ukitaka nyanya moja kwa moja ama utaenda shambani kwako au
utaenda gengeni hayo yakifanyika unapata nyanya kwa dakika chache.
Ukihisi njaa moja kwa moja unatafuta kitu halisi ambacho ni chakula –
ama utakwenda nyumbani au hotelini, michakato hiyo ikifanyika tayari
tatizo lako la njaa litakuwa limekwisha.

Kwahiyo, inaonekana faulo yetu ya kwanza katika kutafuta pesa ni pale


tunapotumia mbinu ambazo ni maalum kwaajiri ya kutafutia vitu halisi.

Vitu ambavyo siyo halisi kama ilivyo pesa, navyo vina utaratibu wake na
mbinu zake katika kuvitafuta. Pia ni vizuri kukumbuka kuwa, pesa yoyote
unayoiona siyo halisi bali ni kitu kilichopewa thamani na binadamu,
japokuwa pesa ni muhimu sana katika maisha lakini akili, afya na
ufahamu wako ni muhimu kuliko PESA. Maana pesa ulipwa baada ya

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 18/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kuzalisha thamani (kutoa vitu na huduma).

Kwa maana nyingine ni kwamba, thamani yoyote ile uzalishwa au


kuendelezwa na wewe binadamu. Wewe ndie unayetoa huduma au
kuzalisha, wewe ndie unayechagua kazi gani ufanye ili upate pesa, hivyo
wewe ni zaidi ya pesa na wewe ndie unayeamua upate pesa nyingi au
kidogo. Lakini yote hayo yatategemea sana wewe kuacha kuiona pesa
kama kitu halisi.

Kwahiyo, inahitajika wewe mwenyewe ufikirie kwa kina hadi ujiridhishe


pasipo shaka lolote kuwa PESA SIYO KITU HALISI. Endapo utakuwa
umekubali wewe binafsi tokea ndani mwako, basi tuungane katika
kufahamu na kujifunza mbinu na njia mpya zinazotumika katika kutafuta
na kupata vitu ambavyo siyo halisi kama PESA. Kwa kujielimisha kila
siku, tutakuwa tumejenga uwezo wetu wa kutafuta na kupata pesa nyingi
bila kuzikosa.

Unadhani Pesa Uliyonayo ni Kidogo au Nyingi?

"Mungu hakupi pesa kidogo au nyingi, anakupa tu kile


kiasi unachohitaji”.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 19/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kwasasa wapo watu wengi wanaodhani kuwa wao wanazo pesa kidogo
na wangependelea Mungu awaongezee. Pia kuna wale wachache
ambao wanadhani wanazo pesa nyingi lakini na hawa wangependelea
Mungu azidi kuwapa pesa nyingi zaidi. Ki-ukweli hakuna pesa kidogo
wala pesa nyingi.

Ukimwambia mtu yoyote kuwa “pesa aliyonayo ni sawa na kiasi


unachohitaji”, anakukatalia kata kata kwasababu, hisia zake zinamtuma
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 20/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kuamini kwamba yeye ana pesa kidogo na mpaka anafikia hatua ya


kulaumu watu wegine anaodhani wana pesa nyingi.

Katikati ya mwezi wa December mwaka 2015 nikiwa kwenye likizo yangu


ya mwaka nilikutana na rafiki yangu ambaye ni Mganda Bw. Sam Mpiira.
Rafiki yangu huyu ni mjasiriamali anayechipukia jijini Kampala-
Uganda.Tukiwa tumekutana kwenye viunga vya hotel ya Speak Resort
Munyonyo, tuliongelea sana juu ya namna tunavyoweza kutajirika na
hatimaye kusaidia watu wengine kutajirika. Katikati ya mazungumzo yetu
alinieleza mojawapo ya falsafa yake kuhusu “KUPATA PESA” na hapa
alisema “Mungu hakupi pesa kidogo au nyingi, anakupa tu kile kiasi
unachohitaji”.

Ukiangalia kwa undani unaona kuwa Falsafa hii inatugusa wengi, na


inatuonyesha umuhimu wa kuacha kulichukulia suala la pesa kuwa la
HISIA, badala yake tuone ukweli juu ya pesa tuliyonayo kuwa ni matokeo
ya fikra na jitihada zile tunazoziweka kila siku basi!. Endapo tukilitabua
hilo basi tutakuwa tumeachana na fikra za kwamba kupata pesa ni
“bahati”.

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa watu wengi bado wana
machungu na wanalalamika kila wakati kwamba wao hawafanikiwi
kupata pesa ya kutosha. Kuwepo kwa hali ya malalamiko juu ya pesa
kidogo kunaonyesha dhairi kuwa ufahamu uliopo ni kidogo, kwasababu
mfumo wa elimu ya darasani hauna ajenda ya kufundisha pesa. Na pia
watu wengi tumefanya utafutaji wa pesa kuwa wa HISIA zaidi kuliko
ukweli ulivyo.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 21/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Ndugu msomaji wa MAARIFASHOP, siri unayotakiwa kuijua leo ni


kwamba, suala la kiasi gani cha pesa huwenacho ni la binafsi zaidi kuliko
unavyofikiria. Hali hii inatokana na uwepo wa mahitaji yanayo tofautiana
kati ya mtu na mtu. Ni vigumu kwangu mimi kufahamu wewe una kiu
kiasi gani ya pesa. Utofauti huu wa mahitaji ya pesa ndio uzaa shauku,
nguvu, motisha na hamasa tofauti linapofika suala la kutafuta pesa.

Kwahiyo, wale ambao ndani ya nafsi zao wana sababu nzito ya kutafuta
pesa ndio wanapata kiasi hicho ambacho kwako wewe uliye na sababu
nyepesi unaona wamepata pesa nyingi. Napenda kurudia tena kusema
kuwa “hakuna aliye na pesa nyingi bali kila mtu anacho kiasi ambacho ni
hitaji lake kwa wakati huo”.

Kwahiyo, kila mtu kabla ya kuanza mchakato wa kutafuta pesa ni vizuri


ukatenga muda wa kutafakari kwanza juu ya maisha yako wewe
binafsi.Tafakari zako zielekeze kwenye vitu vizuri ambavyo ungependa
kuwa navyo maishani au hali ya maisha ambayo unadhani ukiifikia
utajisikia raha na mwenye furaha.

Kwa maana nyingine lazima huwe na picha au ndoto ya maisha mazuri


kwanza kabla ya kuyafikia. Ndoto ya maisha mazuri ndiyo itakayo
kujengea sababu na hamasa ya wewe kutafuta pesa ya kutimiza ndoto
yako. Utaratibu wa namna hii, utakusaidia sana kuachana na
malalamiko. Pia ukiwa na ndoto yako ya maisha mazuri itakuwa vigumu
kuwaonea wivu watu wengine waliotimiza ndoto zao, yaani wale ambao
sasa hivi unadhani wana pesa nyingi.

Kikubwa hapa ni kufikiri, kutafakari, kupanga na kutekeleza kwa vitendo.


Ninaamini kama pesa ndiyo shida yako itapatikana tu japo itachukua

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 22/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

muda. Ni muhimu kutokata tamaa na kuwa mvumilivu.

Kama unadhani ni muhimu kuwa na mawasiliano ya karibu na mtandao


huu wa “MAARIFA SHOP”, ni kiasi cha kubonyeza maneno haya
“KARIBU MAARIFASHOP, -tayari utaanza kupata moja kwa moja mambo
mapya ya mtandao huu.

Njia Mpya ya Kununua Tena Muda Wako Imefahamika

“Falsafa ya matajiri na masikini ni hii hapa: Matajiri wanawekeza


pesa yao na kutumia kiasi kinachobaki, Masikini wanatumia pesa
yao na kuwekeza kiasi kinachobaki” ~ Robert Kiyosaki

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 23/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Hali ya umaskini katika jamii yetu kwa kiasi kikubwa imesababishwa na


watu wengi kuuza muda wao kwa watu wengine. Dunia ya leo bado
inatawaliwa zaidi na kundi la watu ambao biashara yao ya kila siku ni
kuuza muda kwa lengo la kujikimu kimaisha. Katika ulimwengu wa
kutafuta riziki (kipato), tunapata kuona aina kuu tatu za kipato ambazo
ni.....

kipato kutokana na ajira, kipato hai na kipato endelevu au kipato bila


kikomo.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 24/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Karibu asilimia 90% ya watu duniani wanapata kipato chao kutoka


kwenye ajira (mshahara) na kujiajiri (mapato hai). Ni chini ya asilimia
10% pekee ndio wanapata aina ya kipato abacho hakina kikomo –
kikianza kuingia kinaendelea hata kama haupo kufanya kazi. Kwa maana
nyingine ni kwamba, asilimia chini ya 10% ndio matajiri wanaomiliki
asilimia 90 ya utajiri wote duniani.

Kimsingi mapato yanayotokana na kujiajiri (kipato hai) na ajira, yote ni


mapato ambayo tunayapata baada ya “kuuza muda wetu” au
kubadilishana muda (mwajiriwa) na pesa (mwajiri). Kutokana na hali hiyo
ya kuuza na kununua muda, ndiyo maana watu wengi tuliokwenye ajira
au tuliojiajiri mara nyingi hatuna muda wa kufanya vitu tunayovipenda
hata kama vina maana na umuhimu mkubwa kwetu.

Kwa maana nyingine ni kwamba muda mwingi ambao tungeutumia katika


kubuni vitu vipya tunakuwa tumeishiwa tayari kutokana na ukweli
kwamba tumekwisha uza muda huo kwa watu wengine hasa waajiri –
zaidi zaidi tunafanya biashara ya kuuza muda basi!

Kutokana na ukweli wa mambo ulivyo ni kwamba wauzaji wa muda kama


mali tuko wengi sana kuliko wanunuzi (waajiri). Matokeo yake ni kwamba
soko la MUDA linashuka au tuseme bei ya muda inashuka kila kukicha.
Hali hii imetufanya wote wauza muda kuuza kwa bei ya chini ambayo
hailingani na thamani ya kitu tunachokiuza. Leo hii, tunashuhudia
migomo ya kila aina hasa kwa wafanyakazi wa viwandani na
mashambani, hoja yao kubwa ikiwa ni maslahi duni au mishahara
midogo “Kiduchu” isiyoweza kukidhi hata mahitaji ya lazima kama vile
chakula na malazi.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 25/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Nataka kupata MAPATO YASIYO NA KIKOMO lakini siyajui ni kitu


gani:
Unapoongelea suala zima la mapato yasiyo na kikomo ni sawa na wewe
kufunga bomba la maji mtoni, ili kuleta maji nyumbani kwako. Maji
yakishafika nyumbani wewe unayatumia unavyotaka na hayakatiki. Wale
wote wasiofikiwa na mabomba ya maji majumbani mwao, wao
wanachokifanya ni kuchota maji kwa kutumia vifaa kama ndoo, madumu
n.k.

Watu hawa wakishapata maji, wanayatumia na inafika wakati yanaisha.


Mara tu maji yanapoisha, inawabidi wafunge safari tena kwenda kuchota
maji popote yalipo, na mzunguko unakuwa hivyo maisha yao yote.
Ukichota maji yanakuwepo nyumbani, usipochota maji hayapo LAKINI
yule mwenye bomba anaendelea kupata maji masaa yote, hata akiwa
amesafiri maji yapo tu!.

Mfano huu wa maji ni sawa na mfumo wa mapato tunayoyapata. Kwa


maana nyingine ni kwamba, wale wote tunaopata mapato hai au mapato
ya ajira (mshahara), tunafanana kabisa na wale watu wanaochota maji
mtoni kila siku kwa kutumia ndoo, madumu n.k. Kwa mfano: Mapato ya
ajira -unalipwa siku unapofanya kazi, usipofanya kazi haulipwi, ukisafiri
bila ruhusa haulipwi, ukiugua muda mrefu hulipwi n.k.

Kwahiyo, mapato bila kikomo ni mapato anayopata mtu pasipo kuwa na


ulazima wa kushughulika au kufanya kazi kwa wakati huo. Mapato haya
mara nyingi yanatokana na kazi au shughuli uliyokwisha kufanyika
kitambo na kuendelea kupata mapato hayo “kimya kimya”, kutokana na
ukweli kwamba watu wengine wanakuona tu umekaa lakini kumbe wewe

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 26/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

unaingiza pesa nyingi mfukoni.

Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mapato au pesa isiyo na kikomo ni ile


ambayo mtu huipata mara kwa mara, lakini kwa kutumia nguvu kidogo
sana katika kuiendeleza. Mfano; ni pesa itokanayo na haki miliki
kama;k.m. pesa ya mrahaba au “royalties” kutokana na kuuza vitabu,
album au kukodisha hakimiliki; faida benki; kodi ya majengo au mashine;
au pesa kutoka kwenye biashara ambayo haikuhitaji tena wewe kuwepo
moja kwa moja kama “biashara ya kupashana habari au mtandao”. Hii ni
mifano tu ya vyanzo vya pesa isiyo na kikomo. Aina hii ya mapato
inapatikana baada yaw ewe kufanyakazi kwa bidii sana kwa muda fulani
(k.m. miaka 2 hadi 5), baadae unaendelea kupata pesa kwa muda mrefu
bila hata wewe mwenyewe kushughulika tena au zaidi.

Uzuri wa mapato yasiyo na kikomo ni kwamba, unaendelea kupata pesa


kwa muda mrefu baada ya kazi ya uzalishaji au ya awali kukamilika. Hali
hii ya wewe kupata pesa bila kulazimika kufanya kazi tena ndiyo
ukuwezesha wewe kupata MUDA wa ziada na hivyo kupata fursa ya
kuwekeza muda huo kwenye mambo mengine. Uzuri mwingine wa
mapato haya ni kwamba duniani kote hayatozwi kodi kubwa kama
mapato ya aina nyingine.

Kwa wale wote tulio na ndoto ya kupata mafanikio makubwa kimaisha


tunashauriwa kufanya kazi na kuwekeza kwenye miradi inayotuhakikishia
kupata mapato yasiyo na kikomo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba
mapato ya aina hii, ndiyo mapato pekee ambayo ni imara, endelevu na
yanarithishwa kizazi hadi kizazi. Sababu nyingine inayonituma nikushauri
kupata mapato haya ni kwamba, watu wengi waliofanikiwa (matajiri)
duniani, wamejipanga na kujikita katika kupata mapato haya.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 27/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Je? unawezaje kutumia mapato yasiyo na kikomo kununua tena


muda wangu? Je? kununua muda wako tena kuna maana gani? Maana
yake ni kwamba pesa ambayo unatengeneza kwa wiki kutoka kwenye
biashara ambayo ni zaidi ya pesa uliyokuwa ukipata ulipokuwa
ukimfanyia kazi mtu mwingine (mwajiri). Kwa upande mwingine, mapato
bila kikomo yana tabia ya kununua muda wako tena kwakuwa
yanarudisha kwako ule muda au masaa yote uliyokuwa ukiyatumia
kufanya kazi za mwajiri.

Inapotokea biashara yako ikaanza kukupatia kipato kikubwa kisicho na


kikomo na ambacho ni zaidi ya pesa (mshahara) uliyokuwa unaipata
kutokana na kuuza muda wako kwa mwajiri, basi hapo utakuwa
hulazimiki tena kuuza muda wako ili kupata mahitaji na badala yake hayo
masaa yako uliyokuwa ukibadilishana awali na pesa, sasa unaanza
kuyatumia (kuyawekeza) wewe mwenyewe katika kukuza faida na
hatimaye kujijengea mikondo mingi ya kuingiza pesa –hii ndiyo namna ya
kujenga utajiri.

Ukiona biashara au shughuli yako unayofanya inakuletea pesa isiyokuwa


na kikomo, basi ujue kuwa biashara hiyo inaweza kukusaidia kununua
muda wako na hatimaye ukajimilikisha tena muda huo. Kwa mantiki hiyo,
ni wazi kwamba mapato yasiyo na kikomo ndiyo pekee yanaweza
kukuwezesha wewe kurudisha au kununua tena muda wako.

Mwisho nipende kusema kuwa utakapoamua kwa dhati kujifunza undani


wa mapato yasiyo na kikomo utakuwa ni sawa na mtu aliyepata dhahabu
au aliyepata kujua suala nyeti. Kutokana na unyeti wa mapato ya aina hii,
ndiyo maana ninapenda sana watu tuliowengi tuyafahamu na kuyajua

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 28/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kwa undani zaidi.

Tukisha elewa vizuri dhana nzima ya mapato yasiyo na kikomo; ni


matarajio yangu kuwa tutaweza kuhama kutoka mfumo wa biashara ya
kuuza muda (mshahara) kwenda biashara ya kuwekeza muda (faida).
Nakusihi uanze mchakato wa kujifunza hatua wa hatua kupitia makala
nzuri za ujasiriamali na mafanikio nyingi zikiwa zinapatikana hapa
kwenye mtandao wa “MAARIFA SHOP”. Kama unapenda kuwa karibu na
mtandao huu bonyeza KUWA KARIBU.

Kwa mawasiliano zaidi:

WhatsApp: 0788 855 409

E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com

Tovuti: http://maarifashop.blogspot.com

Unataka Kutajirika Anza na Hili

“Uhuru wa kipato upo kwa wale tu waliotayari kujifunza na


kufanya kazi” ~ Robert Kiyosaki

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 29/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Watu wengi wanatafuta utajiri kwa hudi na uvumba, japo wengine


wachache wanapata na waliowengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo
ambalo ni dhairi kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya
kutafuta utajiri katika hatua au vituo tofauti tofauti. Kwahiyo, swali la
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 30/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kujiuliza ni je? Safari yetu ya kutafuta “Utajiri” inapaswa kuanzia...


wapi?.

Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kwamba, UTAJIRI unaanzia


kwenye fikra. Na “fikra ni nguvu pekee inayoweza kuzalisha utajiri wa
kuonekana kutoka kwenye vitu visivyoonekana”.

Kila kitu unachokifanya sasa hivi kimeanza kama wazo kutoka ndani
yako. Hakuna matendo utakayotenda bila kuanzia kwenye fikra
(mawazo).

Kwahiyo, ukiwaza kwa namna fulani, basi ujue kwamba utapata utajiri wa
namna fulani sawa na ulivyowaza mwanzoni kabla ya kupata utajiri huo.
Fikra au mawazo, ndio kitu pekee ambacho huweza kukusukuma
kufanya vitu fulani fulani ambavyo ndivyo huweza kukuletea utajiri.

Utajiri sio dhambi, bali ni sehemu ya maisha, tumeletwa hapa duniani


kuweza kutawala vilivyopo na kama ukiweza kuvitawala vizuri ni lazima
utakuwa tajiri. Unachohitaji ni kuweza kugeuza ndoto yako kuwa kweli.

Wakati ukifanya yote hayo, kumbuka kuwa, wewe ni mtu mwenye


thamani kubwa sana isiyokuwa na mwisho. Hata kama unajiona wewe
sio mtu mbunifu, hata kama ulishashindwa huko nyuma, hata kama
unafikiri umeshajaribu kila kitu ila ukashindwa, jua kwamba bado una
nafasi kubwa ya kupata chochote unachotaka.

Huwezi kuishi maisha unayoyataka, huwezi kuishi maisha yenye uhuru


kama huna utajiri. Huwezi kuinuka na kufikia juu kwenye chochote
unachofanya kama kweli huna uhuru wa kipato.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 31/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Ndio maana ni muhimu sana kwako kuwa TAJIRI. Kwa kawaida


binadamu wote tunazo nia tatu ambazo tunaishi nazo, yaani mwili, akiri
na roho. Nia hizi ndizo utengeneza maeneo muhimu ambayo utuongoza
kuishi ama maisha ya utajiri au maisha ya umaskini.

Maeneo hayo yote matatu ni muhimu sana katika kuishi maisha yenye
mafanikio na furaha. Ni lazima mwili uwe na utajiri, akili iwe ya utajiri na
roho pia iwe na utajiri, hapo ndipo itawezekana wewe kuifikia ndoto yako
ya utajiri.

Lengo la maisha yetu ni maendeleo yaletwayo na utajiri na wala si kitu


kingine. Msingi mkuu wa maisha ni kuendelea kupiga hatua.

Kama kila kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa,
iweje wewe leo uendelee kuwa pale pale miaka yote? Mti unakazana
kukua zaidi ya ulivyo sasa.

Na wewe binadamu pia ni lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa
katika maeneo yote muhimu ya maisha yako.

Katika harakati zako za kutafuta utajiri, lazima kuhakikisha kuwa fikra


zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako
kuzuia akiri yako isirishwe mambo ya umasikini, na ifanye akili yako ibaki
imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au
kuumba .

Kamwe usizungumze: Jitahidi usizungumzie kuhusu matatizo yako ya


zamani ya kifedha kama ulikuwa nayo; usiyafikirie kabisa.Usizungumze
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 32/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kuhusu umaskini wa wazazi wako au ugumu wa maisha yako ya huko


nyuma. Kufanya lolote kati ya hayo ni kujiweka kiakiri katika umaskini
kwa wakati huu ulionao sasa.Weka umsakini na mambo yote
yanayohusiana nao kado au nyuma yako kabisa.

Linda mazungumzo yako: Kamwe usizungumze kuhusu masuala yako


au chochote kile katika namna ya kuvunja moyo au kukatisha tamaa.
Kamwe usikubali uwezekano wa kushindwa au kuzungumza katika
namana inayoashiria kushindwa. Unatakiwa kutozungumza kuhusu
nyakati kuwa ngumu au mazingira ya biashara kama vile una mashaka.

Nyakati zinaonekana kuwa ngumu kwa wale wote walio katika usawa
wakushindana na wenzao. Lakini, wewe unayetafuta utajiri wako
hunabudi kuanza kujifunza maisha yale ambayo unashindana na
malengo yako au ndoto zako basi.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nipende kusema kuwa “Mafanikio ni


mchakato siyo tukio”. Kwahiyo, kama wewe umeweza kujifunza kitu
chochote kipya na cha thamani kutoka kwenye makala hii ni wazi
kwamba tayari umeanza mchakato wa kuelekea mafanikio.

Kitu kikubwa kingine unachoweza kufanya ni kuwashirikisha marafiki


zako wanaopenda kujifunza namna bora ya kufanikiwa na hapa
wanahitaji tu kubonyeza neno “NITUMIE MAKALA MPYA”.

Sababu ya Wewe Kutopata Mtaji Imebainika

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 33/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
“Ukipata pesa na ukaitumia kabla ya kutenga akiba, basi ujue
umelipa watu wengine kwanza na wewe umesahau kujilipa”

Tajiri mkubwa na mashuhuri duniani, Bwana Warren Buffet aliwahi kusisitiza kuwa, kama unataka
kujenga mtaji kutoka kwenye akiba yako binafsi ni sharti ujitahidi kuacha tabia ya “kuweka akiba
baada ya kutumia na badala yake utumie kile kinachobaki baada ya kutenga pesa ya akiba”. Katika
maisha ya umilikaji pesa duniani, kuna makundi ya ina mbili.

Kundi la Kwanza ni la wale wanaoweka akiba ya kile kinachobaki baada ya wao kutumia na kundi la
pili ni wale wanaoweka akiba kabla ya kutumia. Kwa mfumo wetu wa mapato na matumizi ya pesa,
tunaona kuwa kundi la waweka akiba baada ya kutumia ni wengi sana na ndilo kundi la watu ambao
ni walalamikaji juu ya ukosefu wa mitaji ya kufanyia biashara au shughuli nyingine za kiuchumi.

Katika ulimwengu wa biashara, mtaji ndilo suruhisho la uwekezaji wowote wenye tija. Hatahivyo, mtaji
umekuwa ni adimu kuupata na umekuwa ni kikwazo namba moja cha watu wengi kushindwa
kuwekeza na hatimaye kuwa wajasiriamali. Ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa
mitaji, watu wengi wamezidi kuhamasishwa kujiweea akiba binafsi kidogo kidogo kutoka kwenye
mapato wanayopata.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 34/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
Lakini pamoja na kwamba njia hii ya akiba binafsi ni rahisi na ya uhakika, bado suala la kuweka akiba
limekuwa gumu kutekelezeka. Sababu kubwa ya kushindwa kujiwekea akiba ni kwamba watu wengi
tumejenga utamaduni wa “kutumia kwanza na akiba baadae”.

Ukweli ni kwamba, pindi tunapopata pesa, kitu cha kwanza kufanya ni kutumia kwanza kwa lengo la
kumaliza eti shida zilizopo. Hapa kipaumbele kinakuwa ni kumaliza shida na siyo kuweka “akiba”.
Uzoefu umeonyesha kuwa, ukipata pesa na ukaanza kutumia kabla ya kutenga akiba, inakuwa siyo
rahisi kubakiza pesa yoyote kwasababu shida ni nyingi na mahitaji ya wakati huo ni mengi,
ukilinganisha na kiasi cha pesa unachokuwa umepata.

Ukipata pesa na ukatumia kabla ya kutenga akiba, basi ujue umelipa watu wengine kwanza kabla ya
kujilipa wewe. Utamaduni wa kulipa watu wengine kwanza pindi tupatapo pesa umezidi kukua siku
hadi siku na tumeendela kuulithisha kwa watoto wetu. Pesa yoyote unayojilipa kwanza ndiyo hiyo
hugeuka kuwa “akiba”. Tunahitaji kujenga utamaduni wa kujilipa kwanza kabla ya kufikiria kununua
kitu chochote kile pindi tunapoingiza pesa mifukoni mwetu.

Nimeshindwa kujiwekea akiba kwahiyo…. Kwakuwa nimeshindwa kujijengea nidhamu ya kuweka


akiba ili hatimaye nipate mtaji, basi nimeamua kwenda kukopa mtaji ili nianzishe biashara yangu.
Maeneo ambayo watu wengi ukimbilia ili kupata mikopo ni pamoja na ndugu, jamaa na marafiki;
mabenki, n.k.

Hatahivyo, utumiaji wa mikopo kama chanzo cha mitaji, bado haujaweza kuwanufaisha kwa kiwango
walichotarajia. Hii ni kutokana na upungufu mkubwa wa elimu juu ya mtiririko wa pesa (inayoingia na
kutoka) au uelewa mpana juu ya mapato na matumizi ya pesa.

Kukosekana kwa uelewa wa kutosha juu ya utunzaji na utumiaji wa mikopo, wanufaika wengi wa
mikopo, wamejikuta wakigeuka kuwa mawakara wa kudumu wa mabenki ya biashara. Hii ni kutokana
na ukweli kwamba, mikopo mingi imekuwa ikitumika zaidi kununua vitu ambavyo si vya kuingiza pesa
mfukoni (assets), bali vimekuwa ni vitu vya kupeleka pesa nje ya mfuko.

Wapo watu wengi ambao tumeshuhudia wakishindwa kabisa kurudisha mikopo na hapa wakopeshaji
wa pesa, wanalazmika kunadi mali zao na hivyo kujikuta wakifirisika ghafla. Lakini chanzo cha
kushindwa kurejesha mikopo kukosekana kwa nidhamu ya matumizi ya pesa ambayo haikujengeka
huko nyuma. Bila kuwa na nidhamu na tabia ya kujilipa kwanza kutokana na mapato yako binafsi,
huwezi kuwa na nidhamu ya kutumia pesa ya mkopo (ambayo siyo ya kwako) kwa umakini
unaostahili.

Kwahiyo, tabia ya kutenga akiba kabla ya kutumia (kulipa watu wengine), ndio inatuwezesha kujenga
nidhamu ya matumizi stahiki ya pesa yetu binafsi na hata ile ya mkopo.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 35/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Akiba binafsi imeshindikana….! Wengi wetu tunashindwa kabisa kujiwekea akiba binafsi licha ya
kwamba tunapata pesa ya kutosha. Kila wakati tunapopata pesa kitu cha kwanza tunachowazia na
kukipa kipaumbele ni “MATUMIZI” yaani kununua mahitaji (kuwalipa wengine) na pesa inayobaki
ndiyo mara nyingi watu ukumbuka kujiwekea akiba. Haipiti wiki moja, ile akiba tuliyoweka mwanzoni
baada ya kutumia nayo tunaitumia kwa mambo mengi ambayo ufanyika kwa mtindo wa dharura.

Suala la kupenda kutumia haliishii hapo bali watu wengine uenda hatua ya mbele zaidi ambayo ni ya
kutumia vitu kwa mkopo ambapo mtu ulipa pesa baadae baada ya kupata pesa. Unapomkuta mtu
yuko busy anatafuta pesa, husidhani mtu huyo anasukumwa na kutaka kutoka kimaisha laasha! Bali
huyo mtu anatafuta pesa za kulipia madeni ya vitu alivyokwisha tumia siku za nyuma.

Kwahiyo, itoshekusema kuwa mtu huyo alikula bila kufanya kazi, na adhabu yake ni kwamba
matunda yote ya kazi yake, lazima yalipe madeni tu maana hamna namna nyingine.

Unapanga mipango ya kutumia baada ya kupata pesa? Tabia hii ya kutumia kwanza na akiba
baadae ndiyo inawafanya watu wengi kuamini kwamba huwezi kupanga mipango yoyote kabla ya
kupata pesa.

Watu wa namna hii kwa kipindi ambacho hawana pesa wanakaa tu bila kupanga na kufanya
chochote cha maana. Kwa maana nyingine, watu hawa bila kusukumwa na pesa waliyonayo mifukoni
hawawezi kufanya jambo lolote la maendeleo. Hii ni hatari na lazima umaskini huwe halali yako.

Iwapo msukumo wako wa kufanya kitu


chochote unategemea au kusukumwa na
pesa tasilimu uliyonayo mfukoni ni wazi
kwamba ikishapatikana, lengo la kuweka
akiba kwanza haliwezi kupewa kipaumbele
au wakati mwingine haliwezi kufanyika
kabisa.

Matokeo yake ni kwamba kila wakati


utajikuta hubakizi chochote kwasababu kila
mara utakapopata pesa, lazima utaipangia
kulipia mahitaji (lipa wengine) alafu itaisha. Hali hii itakapoendelea na baadae kuwa tabia yako basi
uje kuwa kila wakati wewe utakuwa ni mtu wa kukosa nidhamu ya kujiwekea akiba ambayo ndiyo
ingezaa mtaji wa kutimiza ndoto zako.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 36/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
Waliofanikiwa wanaweka akiba kwanza kabla ya yote: Kwakuwa akiba binafsi ndiyo chanzo cha
uhakika wa kupata mtaji binfsi, ni lazima tuanze kubadilika kwa kuanza kujifunza tabia ya wale watu
waliofanikiwa.

Watu waliofanikiwa, mara nyingi wanapopata pesa yoyote hile, kitu cha kwanza kwao huwa ni
kutenga kwanza asilimia fulani ya pesa kama akiba na baada ya hapo ndipo ufikiria suala la matumizi
mengine. Unapoweka akiba kwanza kabla ya kitu chochote ndipo unaweza kudhibiti tamaa yako, kwa
maana utatakiwa kuwa na nidhamu ya kutumia kulingana na kile kilichobaki.

Kwahiyo, jijengee tabia ya kutanguliza kujilipa kwanza kabla ya kulipa watu wengine; kwani kwa
kufanya hivyo, utapata mtaji wa kutosha na hatimaye kufikia mafanikio makubwa maishani.

Ili kuendelea kupata makala hizi moja kwa moja kupitia e-mail yako bonyeza “KUPATA MAKALA”

UNASHANGAA NINI? PESA YAKO NI SANAMU

Ukitumia macho ya ubongo unaona "Wallet" zetu hazijabeba


pesa, bali vitu tofauti
Ikiwa biashara yako wewe ni kufuga na kuuza kuku, “basi elfu
kumi yako ni kuku”

Ilikuwa siku ya jumanne ya tarehe 30/06/2015, kwenye kipindi cha tuongee


asubuhi kinachorushwa na ITV kila siku mara baada ya kusoma magazeti

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 37/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

asubuhi. Zamu hii, alikuwa akihojiwa kiongozi mmoja wa dini, ambaye alikuwa
akijaribu kuelezea jinsi walivyojipanga katika kuandaa na kukamilisha siku ya
mkesha wa kuombea uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu, na akasisitiza
kuwa maombi yatafanyika mkesha wa 8/8/2015. Katika mazungumzo yake
akagusia jambo moja muhimu kuwa kwa sasa watu wengi wanatanguliza pesa
mbele hata kabla ya kufanya kazi na wengine wanadai walipwe pesa, ndipo
wapige kura za ndiyo kwa wagombea, hasa katika kipindi hiki tunapoelekea
uchaguzi mkuu. Kiongozi huyu, alitumia fursa hiyo kuwahasa watanzania
kujiepusha na tabia ya kupenda kutanguliza pesa mbele. Katika kuweka msisitizo
wa kuonyesha ni kwa jinsi gani pesa siyo kitu halisi; alirejea maandiko kutoka
katika vitabu vitakatifu yanayosema kuwa “Pesa ni Sanamu”. Kitendo cha watu
wengi kushindwa kutambua usanamu uliopo juu ya pesa, ndicho chanzo cha
kuwepo kwa changamoto nyingi zinazotukabili leo hii kama watu binafsi na taifa
kwa ujumla.

Dhana hii ya “pesa ni sanamu” ni muhimu tukaijua na kuielewa vizuri, ili hatimaye
mimi na wewe tupate kujinusuru kwa kutoka kwenye kundi kubwa la watu
wanaotafuta pesa kama “sanamu”. Yawezekana leo hii hatupati pesa ya kutosha
na unaangaika sana, kwasababu fikra na mitazamo yako ni ile ile ya kudhania
kuwa pesa ni kitu halisi kumbe ni “sanamu”. Tafsiri ya neno “pesa ni sanamu”
inamaanisha kwamba, pesa siyo kitu halisi bali ni mfano au kivuli cha bidhaa na
huduma mbalimbali, ambazo hazionekani kwa macho yetu ya kawaida. Kwa
maana nyingine, pesa ni kitu ambacho husimama badala ya bidhaa na huduma
mbalimbali hasa wakati wa zoezi zima la ubadilishanaji vitu kati ya muuzaji na
mnunuzi.

Usanamu wa pesa unatokana na ukweli kwamba, pesa uliyonayo mfukoni


imetokana na wewe kuwapa watu wengine bidhaa au huduma ulizokuwa nazo; na
wao kwa hiari yao wakaamua kukupa vithibitisho ambavyo ni kama stakabadhi
zinazothibitisha uwepo wa makabidhiano ya bidhaa/huduma kati yako na watu
wengine. Kwahiyo, unapoangalia pesa uliyonayo mfukoni ujue una mfano tu wa
vitu vilivyofanya pesa kiasi fulani ije kwako. Kwenye wallet zetu hatuna pesa bali

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 38/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

tuna vitu tofauti tofauti. Mfano: utakuta mtu mwingine kwenye wallet yake
ameweka huduma ya mapambo, usafiri, ufundi, elimu, kuchangia mawazo kwenye
vikao n.k. Wengine wallet zao utakuta bidhaa kama vile chakula, nguo, dawa, jiko,
taa, simu, mafuta n.k. Ukiamua kutumia macho ya ubongo wako utakubaliana na
mimi kuwa, pesa tulizonazo kwenye wallet zetu hazifanani.

Wote tunaweza kuwa na noti ya shilingi elfu kumi za kitanzania, ambazo kwa
macho ya kawaida zinafanana, lakini kwa macho ya ubongo, wallet zetu
hazijabeba pesa bali zimebeba vitu tofauti mtofauti kabisa. Kwahiyo, ikiwa wewe
biashara yako ni kufuga na kuuza kuku basi elfu kumi yako ni kuku; kama wewe ni
mwandishi basi elfu kumi yako ni habari, gazeti au kitabu na ikiwa wewe ni
mshereheshaji basi elfu kumi yako ni ushereheshaji, ualimu, uchoraji n.k. Mifano
hii michache inatuonyesha kuwa, pesa zote tulizonazo hazifanani kabisa,
isipokuwa bidhaa na huduma tunazozalisha ndizo hubadilika na kuwa kitu kimoja
ambacho ni sanamu yaani “pesa” inayoonekana kwa macho yetu ya kawaida.

Kwa wale wote wanaoamini kuwa pesa siyo sanamu, maana yake ni kwamba vitu
vyote vinavyotengeneza pesa waliyonayo, hawawezi kuviona kwasababu macho
yao ya ubongo yamepofuka na hivyo wamebakia kutumia macho ya kawaida peke
yake. Ukiangalia pesa kwa macho ya kawaida (kwa mujibu wa kinachonekana),
kiukweli wewe utaishia tu kuona noti za elfu 10, 5, 2, 1 n.k. ikiwa kuona kwako
kutaishia hapo, basi na wewe ni mmojawapo wa watu hawaoni pesa bali wanaona
“sanamu”. Mtu anayeona sanamu kila wakati, hawezi kujua mahali kitu halisi kilipo
na wala hatajua hiyo pesa ilikotoka. Ndiyo maana inapotokea mtu akapata pesa
na baadae kuishiwa, ni vigumu kuzipata tena kwa haraka kwasababu, anakuwa
tayari ameishasahau zilikotoka. Na kwa yule anayetambua kuwa pesa aliyonayo
kwenye wallet ilitokana na mkusanyiko wa bidhaa na huduma mbalimbali; ni rahisi
sana kwake yeye kuzipata pesa kwa muda mfupi, kwasababu chanzo chake
kinajulikana na kimekuwa kikitunzwa na kuimarishwa mara kwa mara.

Kwenye jamii yetu kwasasa, bado watu wengi wanaishi kwenye ulimwengu wa vitu
vinavyoonekana kwa macho ya kawaida. Tunahitaji kujifunza kutumia macho yetu

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 39/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

ya ubongo katika kuona vitu vinavyoonekana na visivyooekana na hapo ndipo


tutaweza kuiona pesa halisi badala ya sanamu tunayoiona sasa. Ni wakati
muhafaka sasa kwa watu wote wanaotaka mafanikio makubwa kugeukia kile
kinachofanya pesa ije kwenye wallet zao; kwani hicho ndicho kitu halisi. Ni
muhimu, juhudi na maarifa yetu yote yakaelekezwa kwenye kuzalisha thamani
kupitia vitu na huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watu wengine na jamii
kwa ujumla. Na tuyafanye yote haya, huku tukiamini kufanikiwa na hakika
tutafanikiwa.

PESA NYINGI INAPATIKANA HAPA

Unapoamua kuwekeza nguvu kazi yako kwenye shughuli za uzalishaji ndipo


unapata bidhaa.

Unapokuwa na bidhaa/huduma ndipo watu wengine sasa huamua kutoa na


kutuma pesa zao kwako, ili kujipatia bidhaa/huduma husika.

Leo hii watu wengi tunahangaika,


tunanungunika na tunalalamikiana
juu ya kukosekana kwa pesa. Kila
mtu anamtuhumu mwenzie juu ya
hali duni ya maisha. Maisha duni
yametokana na kukosekana kwa
mahitaji. Ili binadamu apate
mahitaji, kwa sehemu kubwa
anahitaji pesa na hii mara nyingi
inatokana na bidhaa au huduma
ambazo umezalisha mwenyewe.
Uzalishaji wa bidhaa au huduma
zilizonyingi unategemea zaidi matumizi ya nguvukazi, ambayo chimbuko lake ni afya
bora. Mtu mwenye afya bora, kwa vyovyote vile ni mtu mwenye kuwa na nguvu
yakutosha kufanya shughuli mbalimbali na hasa za kiuchumi. Nguvukazi hatupewi na mtu

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 40/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

yeyote, bali unakuwanayo kwa kuzaliwa ilimradi, uwe na utaratibu wa kujali afya yako
basi!.

Kwakuwa kila mmoja wetu anamiliki na kuitawala nguvukazi yake mwenyewe, maamuzi
ya kutumia nguvukazi yako kwa mtu mwenyewe. Kuna kundi la watu wanaotumia
nguvukazi yao zaidi kwenye “Uzalishaji Pesa” na kuna wengine wanaitumia zaidi kwenye
shughuli ambazo siyo za uzalishaji wa pesa (Non Income Generating Activities ~ NIGA).
Hapa Tanzania, bado watu wengi wanawekeza nguvukazi kubwa zaidi kwenye shughuli
zisizo za uzalishaji pesa. Shughuli nyingi ambazo siyo za uzalishaji pesa, zinatumia sana
pesa, hali inayopelekea watu wengi kutumia kuliko wanavyozalisha pesa. Kama nguvu-
kazi yetu nyingi inawekezwa zaidi kwenye shughuli ambazo siyo za uzalishaji, basi tujue
kabisa kuwa tutapata bidhaa/huduma kidogo, na hatimaye tunaishia kupata pesa kidogo.

Watu wengi tunataka na tunatamani sana “maisha bora”; maisha ambayo tutakuwa na
uwezo endelevu katika kupata chochote tunachohitaji kama lilivyo kusudio la Mungu
kutuweka hapa duniani. Kwakuwa, maisha bora ndiyo kusudio la watu wengi, basi
inatupasa tubuni mchakato wa maisha bora badala ya hali ya sasa ambayo tumejikita
kwenye shughuli za kutafuta pesa ambazo hazina mpangilio. Kwa sasa ukichunguza
harakati nyingi za kutafuta pesa, unagundua kuwa kila shuguli inajitegemea kiasi kwamba
kukamilika kwa shughuli moja hakuna uhusiano wowote na shughuli nyingine. Jambo hili
la kufanya shughuli ambazo hazina mpangilio maalumu unaolenga kupata maisha bora,
ndiyo linatufanya tukose mwelekeo na hatimaye kushindwa kuyafikia maisha ya ndoto
yetu. Kwahiyo, zoezi la kutafuta pesa na hatimaye maisha bora ni lazima kulifanya kuwa la
ki-mchakato zaidi kuliko ki-shughuli zaidi. Kupitia fikra, utafiti, vitabu na hitoria za watu
waliofanikiwa; nimejifunza kuwa, ili uweze kuyafikia maisha ya ndoto yako (maisha bora)
ni muhimu upitie mchakato maalum. Mfano ni kama huu hapa chini:

AFYA BORA NGUVUKAZI BIDHAA PESA MAHITAJI MAISHA BORA

Ukichunguza mchakato wa kupata pesa hapo juu unaona moja kwa moja kuwa pesa siyo
matokeo ya mwisho ambayo binadamu anayatafuta bali pesa ni sehemu tu ya mchakato wa
maisha bora. Katika mchakato wa kupata maisha bora, pesa ipo katika nafasi ya nne kati ya

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 41/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

vitu sita muhimu ambavyo vinahitajika kupewa kipaumbele kama unataka kufanikiwa.
Mafanikio makubwa yameshindikana kufikiwa na watu wengi, kwasababu ya kutilia
mkazo zaidi kitu kimoja tu! ambacho ni PESA. Michakato yetu mingi ya kutafuta pesa,
haitilii mkazo vitu vingine kama “afya, nguvukazi na bidhaa”. Kwa maana nyingine
tunaweza kusema kuwa hatupati pesa kwasababu mara nyingi mchakato wa kutafuta pesa
na hatimaye maisha bora “tunauanzia katikati”.

Unapopanga mkakati au mchakato wa kutafuta pesa na wakati huo huo ukaacha kuzingatia
na kujali afya yako, basi ujue kuwa uwezekano wa wewe kupata maisha bora ni mdogo
sana. Kumbuka afya bora ndio chimbuko la nguvu ulizonazo ambazo ndio hukupatia
rasilimali “nguvukazi”. Unapoamua kuwekeza nguvu kazi yako kwenye shughuli za
uzalishaji ndipo unapata bidhaa au huduma ambazo hugeuka kuwa pesa. Unapokuwa na
bidhaa/huduma ndipo watu wengine sasa huamua kutoa na kutuma pesa zao kwako, ili
kujipatia bidhaa/huduma husika. Kwahiyo, iwapo utakuwa umezalisha bidhaa nyingi
utapata pesa nyingi na ni pesa hiyohiyo ambayo na wewe utaitoa na kuituma kwa watu
wengine ili kupata bidhaa/huduma na hatimaye kukidhi mahitaji yako mbalimbali.
Unapofikia hatua ya endelevu wa kupata kile unachohitaji kwa muda muhafaka, ni wazi
kwamba unakuwa tayari umefikia maisha bora ambayo ni ya ndoto yako na hapa ndipo
unaanza kupata vitu vile ulivyokuwa ukivipenda lakini ulilazimika kuviacha kwa muda ili
kuruhusu mchakato wako wa maisha bora ukamilike.

Kwahiyo, tunapojiandaa kuanza safari ya kutafuta mafanikio ni lazima tujitahidi kuanza


mchakato wa kutafuta maisha bora, kwa kuanza na ujenzi wa afya bora, ili itupatie
nguvukazi itakayo tuwezesha kuzalisha bidhaa za kuleta pesa nyingi kukidhi mahitaji kwa
kiwango endelevu na hatimaye kufikia maisha bora ambayo ndiyo ndoto yetu.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 42/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

USIBANE MATUMIZI YA KIPATO “TUMIA KIPATO


KUPANUA NJIA ZA KUINGIZA KIPATO”

Yawezekana unaendelea kuishi maisha duni,


kwasababu unaishi kwa “kubana matumizi”; na
hii ni kutokana na ukweli kwamba, tangu tukiwa
wadogo tumefundishwa na wazazi, ndugu jamaa
na marafiki kuwa ili uweze kuwa salama ni “Ishi
Chini ya Uwezo Wako”. Watu wengi wenye
mtazamo huu, mara nyingi wanaotumia njia ya
kubana matumizi kuwa ndiyo suluhisho na njia pekee ya kukabiliana na ugumu wa
wa maisha. Ukweli ni kwamba, kubana matumizi ni utaratibu mzuri lakini
inategemea una malengo gani ya kufanya hivyo. Kutokana na kutotambua ubaya
wa tabia ya kubana matumizi, wengi wamelichukulia kuwa ni utaratibu wa kudumu
badala ya kuwa wa muda tu!.

Watu wameendelea kubana matumizi tangu wanajitabua mpaka wanazeeka.


Unapokuwa mtu wa “kubana matumizi” muda wote, kinachojitokeza ni kwamba
unajenga hofu kubwa ndani yako juu ya kuishiwa pesa kidogo uliyonayo. Akiri
yako yote inaelekezwa kulinda pesa yako isitoke au wengine wanasema eti! Itoke
kwa mpangilio – lakini mwisho wa yote hali inabakia palepale “kuishiwa na
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 43/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kutaabika”. Kwa mtu ambaye amejiwekea utaratibu wa kudumu wa kubana


matumizi, akiri yake inadumaa sana kiasi cha kukubali kuishi maisha duni na
ufukara. Mtu wa namna hii kila anapotafuta na kupata, badala ya kuwaza ni kwa
namna gani atapata kingi zaidi, yeye mara moja unawazia kuishiwa, ndiyo maana
anaanza kuweka nguvu nyingi kubana hicho kidogo kilichopatikana. Mwisho
anatumia kwa kujinyima sana na hatimaye kinaisha ndipo huyo mtu uhanza tena
kutafuta. Kwahiyo, unajikuta umenasa katika mzunguko wa kuishiwa na maisha
yanakuwa ni ya kubangaiza miaka yote.

Kuishi chini ya uwezo wako ni kitu cha


kawaida na mara nyingi ushauri utolewa sana
na wataalam na wasomi wa masuala ya
biashara na uchumi kuwa njia pekee ya
kuendana na hali ni kufanya vitu vilivyo chini
ya au vinanavyolingana na uwezo wako.
Lakini badala ya kulikubali hili bila kulitafakali
ngoja tujiulize ni kwanini wanasema hivi? Au
kwanini imani hii ya kubana matumizi
inatokea? chimbuko la kubana matumizi ni kuazia wakati ule wa zama za kale
ambapo binadamu aliishi kwa kukusanya matunda na kuwinda wanyama. Wakati
huo, watu hawakuwa na fikra za uzalishaji, kwasababu walizoea kula vitu
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 44/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

ambavyo vilijiotea na kukua vyenyewe bila kutegemea akiri na nguvu ya


binadamu.

Kazi ya binadamu wakati huo ilikuwa ni kutafuta na pale vilipopatikana


vilikusanywa kiasi cha kutosha. Baada ya kuvikusanya, binadamu huyo wa kale
alijitahidi sana kuvitunza ili vikae muda mrefu bila kuisha. Kwakuwa vitu hivi mara
nyingi vilikuwa vinatoka mbali sana na makazi yao, ilibidi kujitahidi kubana ili
kupunguza safari za kwenda huko; njiani walipambana na wanyama wakali,
mafuriko, mvua n.k. kwahiyo kila walikuwa wakifkiria safari ilikuwa ni budi wabane
kupunguza hadha za namna hiyo. Sasa wewe unayeishi katika zama hizi za leo,
tayari una uwezo wa kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali, na hivyo
kutotarajiwa kuishi kwa style kama ya enzi za kale. Uhamuzi ni wako kwa maana
kwamba unaweza kuamua kuzalisha vingi na ukatumia kiasi unachoona kinafaa
kukutoshereza mahitaj yako ya wakati huo. Badala ya kila wakati kufikiria kubana
matumizi na mwisho kuishia kuishi katika maisha ya kupata mahitaji chini ya
kiwango chako halisi.

Kuishi chini ya uwezo wako ni sawa a kujiaminisha kuwa suluhisho la kumudu


gharama za maisha ni kupunguza matumizi. Kuishi juu ya uwezo wako ni sawa na
kujiaminisha kuwa pesa ipo nyingi. Hali zote mbili hazifai, bali suluhisho pekee ni
kupanua na kuongeza vyanzo vya mapato. Kila mmoja anaweza kupunguza
matumizi, na kila mmoja anaweza kutumaini na kuomba Mungu kuwa pesa
itakuja, lakini inahitaji ubunifu, maarifa na uelewa, pamoja na ujasiri ili kukuza na
kupanua mapato yako kupitia njia halali. Kimsingi siamini katika kuishi chini ya
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 45/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

uwezo na wala kuishi juu ya uwezo, ninachoamini ni kuishi kwa kupanua na


kuongeza njia za kuleta mapato.
Siamini katika mtazamo wa “ishi chini ya uwezo wako”. Kwa watu walio wengi
pamoja na wale watoa ushauri, huu kwa ujumla ni mtazamo wa kimaskini na siyo
mzuri. Lakini pia, kibaya zaidi ni kwamba ushauri huu wa kuishi chini ya uwezo
unasababisha kuua kabisa dhamira na fikra za ujasiriamali. Ushauri huu
unakufanya usinyae kuwa mdogo. Hali hii inafanya mtu anakuwa na maisha duni
kuliko alivyopaswa kuwa. Hali hii pia inakufanya kuingia katika kundi la watu wa
kawaida au wenye mawazo ya wastani (mediocre). Na kama uliwahi kuambiwa na
wewe mwenyewe kuwazia kwamba unatakiwa kuishi chini ya uwezo wako acha
mara moja. Huu ni wakati wa kukua na kufanya mambo makubwa, ni wakati wa
kuwekeza asilimia kubwa ya kipato chako kwenye vitu vinavyoingiza pesa kwako;
ni wakati wa kuwa mbunifu na kupanua siyo tu njia za kuingiza kipato, bali pia
jitanue kwa kuilisha akili yako ili uweze kufaidika na fursa zilizokuzunguka.

NI VIGUMU SANA KUFANIKIWA KAMA MARA NYINGI UNAITUMA PESA


YAKO KUNUNUA VITU NA KUBAKIA HUKO BILA KURUDI

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 46/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Mara zote ukishakupata pesa (kuingia mfukoni), kinachofuata huwa ni


kuzitumia hata kama ukizitunza kwanza, mwisho wake huwa ni kutumika
kwaajili ya kukidhi mahitaji ya vitu na huduma mbalimbali. Watu wengine
upenda kusema kwamba “pesa ni mzunguko”. Mzunguko wa pesa una
vipengele viwili ambavyo ni “Kuingia na Kutoka”. Kwa lugha rahisi tunaweza
kusema kuwa pesa ina milango miwili, kuna mlango wa pesa kuingia na
kutoka kwako.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 47/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kwa yeyote anayetafuta mafanikio makubwa ni lazima kuangalia milango hii


miwili (kuingia na kutoka) na hapa ndipo kuna tokea makundi mawili ya watu
ambao ni masikini na tajiri. Kwa upande wa maskini tayari wamejenga hofu
kubwa sana na muda wote wana wasiwasi ya pesa kutoka na kupotea.
Kutokana na hofu hii, maskini wengi sana wemejijengea tabia ya kuibana
pesa ikisha ingia mifukoni mwao, huku wakidhani kuwa hilo ni suluhisho la
wao kutoishiwa na pesa. Matokeo yake linapokuja suala la kuwekeza au
kuchangamkia fursa kubwa wanakuwa waoga sana wa kuthubutu kutokana
na hofu ambayo imejengeka kwa muda mrefu ndani ya fikra zao.

Wenzao ambao ni matajiri wao, mara tu pesa inapoingia, kitu cha kwanza
ujiuliza ni kitu gani wanaweza kukitoa ili kuondoa kero kwenye jamii ikiwemo
le iliyowazunguka. Kwahiyo, wao uweza kuiachia pesa yao kutoka lakini kwa
malengo ya kuituma malighafi ambayo pengine ikiunganishwa na mambo
mengine uweza kurudi na bidhaa au Huduma ambayo ni hitaji muhimu
kwenye jamii. Kwa kufanya hivyo, hata wale maskini walioogopa kuiachia
pesa yao mwanzoni, wakati huu uweza kuituma kwa matajiri hao na
mzunguko uendelea hivyo hivyo na mwisho ni umaskini uliokithiri.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 48/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Kama tulivyoona kuwa kuna milango miwili ya pesa kuingia na kutoka.


Mlango wa kwanza ni wa kuingilia (pesa inaingia mfukoni) na wa pili ni wa
kutokea (pesa inatoka nje ya mfuko wako). Pesa ikishatoka nje ya mfuko
wako, kuna mambo mawili ambayo yanatokea; kwanza pesa inaweza
kutumwa mali ambayo iwapo itaongezewa thamani na kutoa bidhaa au
huduma ambayo ikiuzwa tena inarudisha ile pesa iliyotoka mwanzoni na
nyongeza juu (faida) na hii yongeza ni kwasababu ya thamani iliyoongezeka.
Pili pesa inaweza kutoka nje ili kufuata vitu ambavyo kwako wewe unakuwa
ni mtumiaji wa mwisho; kiasi kwamba pesa iliyotumwa vitu vya aina hii,
kamwe haiwezi kurudi hata ungefanyaje.

Watu wengi hasa waajiriwa pamoja na wakulima, huwa pesa zao zikishatoka
kwa mwenyewe, mara nyingi huwa hazirudi kwasababu ya kutumwa vitu
ambavyo wewe ndiye mtumiaji wa mwisho. Sababu kubwa ya waajiriwa
ufanya hivyo ni kwasababu ya kutegemea mshahara mwisho wa mwezi. Hali
hii humfanya mtumishi pamoja na mkulima kuishi maisha ya kawaida sana
ambayo huwa hayabadiliki miaka nenda rudi. Baadhi ya vitu ambavyo pesa
ikitumwa kuvifuata yenyewe hairudi ni vingi sana; mfano: Runinga Redio,
Karo za wanafunzi, gari la kutembelea, n.k.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 49/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

Bila kuingilia mipangilio mbalimbali ya watu walionayo, unaweza kuona


kuwa pindi tu tunapoanza kazi ya kuajiriwa tunaanza vizuri lakini muda mfupi
tu! tunawahi kutekwa na utamaduni wa kupeleka pesa kule ambako huwa
hairudi. Na kwenye jamii tulizomo watu wanahamasishana kufanya hivyo. Na
mpaka sasa watu wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoea, kwamba
unapopata ajira eti unashauriwa na wenzako kununua kiwanja na kujenga
nyumba ya kuishi na vitu vingine vyenye kupeleka pesa bila kurudi.

Watanzania, tunahitaji kubadili tabia pamoja na mtazamo wetu juu ya mapato


na matumizi ya pesa; tunahitaji kujifunza ni jinsi ya kutuma pesa ikarudi
pamoja na vitu. Pia, tunahitaji kuwa na mikakati na mbinu za namna ya
kuifanya iwe nyingi badala ya utaratibu uliozoeleka wa kubana matumizi.
Tukiweza kuyafanyia kazi yote haya hakika tutakuwa tumepiga hatua moja
muhimu sana ya kutufikisha kwenye mafanikio tuyatakayo.

MWANZO WA KUIPATA PESA NI KUIJUA KWANZA!


Je? Na wewe ni mmojawapo wa wanaotafuta pesa? Kama jibu ni ndiyo, hiyo pesa
unajua ni nini? mbali na kufahamu sura tu ya sarafu na noti? Ukiacha hilo, kuna
cha zaidi unachojua kuhusu pesa? Ikiwa jibu ni “hapana” sasa wewe pesa
utazipataje wakati huzijui? Mara nyingi watu husema kuwa, “huwezi kuona kitu
usichokijua”! Mpaka sasa, ufahamu na uelewa uliopo juu ya pesa ni mdogo sana
labda tu! ufahamu uliopo ni wa kujua jinsi pesa zinavyogawanyika na walio wengi
tunafahamu zaidi kutoa na kujumlisha pesa, hasa wakati wa kurudisha chenji kwa
mteja. Ukiacha hilo, taswira kubwa na ndefu iliyopo nyuma ya pesa (noti na
sarafu) haionekani kirahisi kwa watu walio wengi. Ufahamu na uelewa mdogo juu

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 50/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

ya maana pana ya pesa upo kwa watu wengi, na hali hii ni kwa wote waliokwenda
shule na wale ambao hawakwenda kabisa.

Ukweli ni kwamba “Pesa ni kitu chochote kinachowezesha watu kubadilishana vitu


na huduma. Hapa ndo kuna mkanganyiko kwasababu watu wengi mpaka sasa
wanaamini pesa ni kitu halisi na hivyo kusababisha wao kuweza kuiabudu na
kuamini pesa kama inavyoonekana katika hali yake ya noti na sarafu. Mtazamo
wa kuichukulia pesa kama kitu halisi, unawafanya walio wengi kuwekeza nguvu
kubwa Katika kusaka/kutafuta pesa yenyewe kama ilivyo. Lakini wakisha ipata
wanagundua kuwa, hitaji lao siyo makaratasi ya noti bali ni vitu na huduma
mbalimbali hapo ndipo huzipeleka kwa wenye vitu na huduma, huku wakibakia
tupu kabisa.

Katika kutafuta pesa kunakuwa na dhamira tofauti kati ya maskini na tajiri; “Watu
maskini wanawekeza muda na nguvu yao kwa dhamira ya kutafuta pesa lakini
watu matajiri wanawekeza muda, akili na nguvu yao kwa dhamira ya kutafuta “vitu
na huduma”. Kwasababu maskini wengi waliamini kuwa mwisho wa utafutaji wao
ni pesa, basi ndipo ugundua kuwa sio mwisho, kumbe mwisho wao ni kupata vitu
na Huduma (chakula, dawa, mavazi; usafiri, elimu, utaalam, nguvukazi n.k.).
Kwahiyo, pamoja na kutafuta pesa hiyo kwa kutumia nguvu kubwa na muda
mrefu, mtu huyo ujikuta akilazimika kuzipeleka mwenyewe kwa tajiri ambaye
wakati huo ana vitu na huduma fulani fulani. Kwa maana nyingine tunaweza
kusema kuwa watu hawa wanaishi kwa kutafuta pesa na kisha kulipa bill! au
madeni basi.

Mahitaji ya mwanadamu ni mengi sana na hayana kikomo, lakini pamoja na hayo,


mahitaji haya yamegawanyika katika makundi makuu mawili: yaani “Vitu na
Huduma”. Tunaposema “Vitu” inamaanisha vitu halisi na vinavyoshikika kama vile
nguo, meza, komputa simenti, gari, simu, vyombo, spare, vitabu n.k); na
tunaposema “Huduma” ni vitu ambavyo havishikiki navyo ni kama; usafiri, habari,
utaalam, ulinzi na usalama, maombi, ufundi n.k. Kwahiyo, kutokana na ukweli huo

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 51/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

hapo juu, ndiyo maana siku zote pesa itakwenda kule kulipo na vitu au huduma
hakuna sehemu nyingine.

Kutokana na ukweli huu, ni wazi kwamba unapoona pesa imeingia mfukoni


mwako, basi ujue kuna mtu ametuma pesa hiyo kufuata kitu fulani kwako, na
iwapo huna kitu chochote ulichonacho basi hutapata pesa yoyote kwasababu
hakuna kitu cha kufuata kwako. Sasa unachotakiwa kufanya leo ni kuanza kubadili
swali ambalo watu wengi ujiuliza pindi wanapohitaji kupata pesa; swali lenyewe
huwa ni hili hapa: “Nitapata pesa wapi?” na kwa kuwa wengi ujiuliza swali hilo,
ndiyo maana huishia tu! kutafuta pesa bila mafanikio.

Iwapo utaendelea kujiuliza swali la nitapata pesa wapi ndivyo itakavyozidi kuwa
vigumu kupata jibu ambalo litakuongoza kupata pesa. Kwahiyo, mtanzania
mwenzangu ni wakati sasa wa kubadili swali lako kutoka “nitapata pesa wapi?”
kwenda “Pesa itakuja kwangu kufuata nini?”. Na kila mara utakapojiuliza swali la
pesa itafuata nini kwako, basi jibu jibu lake tu! litakuwa ndiyo pesa yenyewe kwa
maana nyingine utaona watu wakibisha hodi mlangoni kwako, kwaajili ya
kukuletea pesa ambayo miaka yote umekuwa ukikimbia huku na huko kuitafuta
bila mafanikio!. Sasa unachotakiwa kufanya ni utafiti katika mazingira yanayo
kuzunguka na maeneo mengine unayoweza kuyafikia ili kutambua mahitaji, kero
na changamoto zilizopo. Matokeo ya Utafiti yatakusaidia kubuni na kuzalisha vitu
au huduma ili kukidhi mahitaji ya jamii husika, na ukifikia hapo ndipo utaona ndani
muda mfupi watu wakituma pesa ili ikafuate vitu na huduma kutoka kwako.

Kwahiyo, uwanja ni wako wewe mtanzania unayetafuta mafanikio, kwani tuna


imani kubwa sana kuwa unaweza kupata pesa nyingi, iwapo utakubatia na
kuifanyia kazi falsafa hii ya “Pesa itakuja kwangu kufuata nini?”.

SIRI YA WALIOFANIKIWA NI KUWEKEZA KWAO ZAIDI KWENYE AINA YA MAPATO


YASIYOKUWA NA KIKOMO (TULI)
Unapoanza safari yako kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni vizuri ukafahamu ni aina gani ya
kipato unachopata kwa sasa? Kwahiyo, ili kuweza kufahamu sifa na aina za vipato, ni muhimu kujua

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 52/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
kuwa zipo aina kuu tatu za vipato ambazo ni: Mapato ya Ajira (mshahara); Mapato Hai (kujiajiri);
Mapato yasiyo na kikomo au Tuli, (Passive Income).
1. Mapato ya Ajira (Earned Income)
Haya ni mapato yanayotokana na kufanya kazi ya kuajiriwa (mshahara), ambayo mtu huyapata
kutokana na ajira yake. Katika aina hii ya kipato, vigezo vya kukuwezesha ulipwe ni pamoja na aina
ya kazi na wadhifa au cheo chako. Pia, mapato haya yanajumuisha mapato yoyote yatokanayo na
ajira binafsi (kujiajiri), biashara ndogondogo na shughuli nyinginezo ambazo unapata kipato kutokana
na juhudi na muda uliotumika. Kwa maana nyingine, ni kwamba kama husiposhugulika au
ukasimama kufanya kazi na kipato kinakoma pale pale.
Ø Uzuri wa Mapato ya Ajira
· Mapato yanaongezeka zaidi kulingana na muda na ukubwa wa shughuli inayofanya
· Hauitaji mtaji kuweza kupata mapato haya
· Mtaji ni nguvu au ujuzi wako mwenyewe
Ø Ubaya wa Mapato ya Ajira
· Uwezi kupata utajiri wa kudumu kwa aina hii ya mapato yanayotokana na mshahara.
Kwasababu mshahara unapata, unakula na unanaisha.......Unapata unakula zinaisha.....
· Siyo mapato endelevu, ukiacha kufanya kazi mapato yanakoma.
· Mapato haya ya ajira yanatozwa kodi kubwa kuliko aina nyingine zote za mapato na
Waajiriwa wanalijua vizuri hili.
Mfano; kwa mtu anayelipwa mshahara wa kiasi cha 1,350,000/- anakatwa kodi hivi:
Aina ya Makato Kiasi (TSh)/Mwezi
Kodi (Income Tax) 260,400.00
Bima ya Afya 40,500.00
Chama cha Wafanyakazi 27,000.00
Mfuko wa Pensheni 67,500.00
Jumla 394,900.00
Sasa, ebu fikiria mtu anakatwa karibu Shilingi 400,000/- kila mwezi, kiasi ambacho kwa mwaka
kinafikia karibu shilling 4,800,000/-. Unaweza kukuta mtu ana biashara yenye mtaji upatao shilingi
million 15, siajabu kukuta analipa kodi kiasi kisichozidi shilingi 500,000/- kwa mwaka.
2. Mapato Hai (Active Income)
Aina hii ya mapato, kwa kiasi fulani inafanana na mapato ya ajira yanayo jumuisha mishahara, kwani
mapato haya yanatokana na kuuza na kununua bidhaa kubwa kubwa kama magari, nyumba, kiwanja
n.k. Mchakato huu ni kwamba, unanunua kitu halafu unakiuza kwa faida, halafu basi. Ili uweze kupata
mapato mengine inakubidi, utafute kitu kingine au ununue kitu kingine haraka ndipo upate tena pesa.
Maana yake ni kwamba lazima uwe kazini (active) muda wote huku ukiendelea kuchakarika ndipo
upate mapato. Kama ilivyo kwa mapato ya mshahara, pindi unapoacha kununua na kuuza vitu,
mapato nayo yanakoma mara moja.
Ø Uzuri wa Mapato Hai
· Mapato haya hayahitaji watendaji kazi wengi ili kufanikisha shughuli ni wewe tu mwenyewe.
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 53/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

· Kodi yake ni ndogo kulinganisha na ile ya mapato ya ajira


· Unapata zaidi kutokana na jitihada zako za kutafuta na uchangamkia fursa.
· Unaweza kufanya na kupata pesa hata pasipokuwa na mtaji. Mfano, unachukua mali (sema
gari), Unamwambia jamaa utamletea pesa yake baada ya siku mbili hivi, kumbe wakati huo
umeisha tafuta mteja tayari unampelekea, unauza unamlipa jamaa wewe unabaki na faida.
Tayari umeisha tengeneza pesa bila hata kuwa na mtaji ~ yaani ni ujanja ujanja tu!
Ø Ubaya Wake
· Inahitaji utaalam na ujanja wa hali ya juu na kufahamika pia, unaweza kupewa vitu feki,
kuzurumiwa, kuibiwa, kupata hasara n.k.
· Unaendelea kushughulika wewe mwenyewe ndipo unapata faida
· Unaweza kupata hasara kutokana na kubadilika kwa hali ya mambo juu ya bidhaa husika.
Mfano: mitindo/fasheni, msimu, bei n.k.
3. Mapato Yasiyo na Kikomo (residual or passive income).
Ni mapato mtu anayoyapata pasipokuwa na ulazima wa kushughulika/kufanya kazi kwa wakati huo
au kwa maana nyingine ni mapato “Tuli”. Mapato haya mara nyingi yanatokana na kazi au shughuli
uliyokwisha kufanya kitambo na kuendelea kupata mapato haya “Kimya Kimya”. Unayapata kutokana
na vitega uchumi ulivyoweka. Mfano: kama umenunua nyumba na kupangisha na kila mwisho wa
mwezi unapewa kodi ya pango, basi mapato hayo ndiyo yanaitwa yasiyo na kikomo au TULI.
Unashughulika mara moja tu na kisha unaendelea kupata pesa kwa muda mrefu bila hata wewe
mwenyewe kushughulika tena/ zaidi. Pia mapato yatokanayo na Mtandao, nakala za albamu ya
muziki, filamu au vitabu n.k. ni hayana kikomo. Unaendelea kutoa nakala na kuuza miaka na miaka.
Ø Uzuri MapatoYyasiyo na Kikomo (Tuli).
· Unaendelea kupata pesa kwa muda mrefu baada ya kazi/shughuli ya awali
· Unakuwa na MUDA wa ziada kufanya mambo mengine. Unabaki kucheza gofu na kutalii
huku pesa zinaingia
· Hayatozwi kodi kubwa kama mapato ya aina nyingine.
Ø Ubaya MapatoYyasiyo na Kikomo (Tuli)
· Wakati mwingine hugharimu sana kuwekeza katika hatua ya awali.
· Huitaji uvumilivu (patience) kwani yaweza kuchukua muda mrefu kabla ya kuanza kupata
mapato haya. “Lakini Yakianza Kuingia Unatumia Hadi Unasahau”.
Hizi ndizo aina kuu tatu za mapato yatokanayo na shughuli mbalimbali katika maeneo makuu manne
ya mafanikio ya kifedha - Biashara, sanaa, michezo, uvumbuzi wa kisayansi au teknolojia, utunzi wa
vitabu pamoja na kujenga mtandao (Network Marketing Business). Kwahiyo, kama una ndoto ya
kupata mafanikio makubwa kimaisha, unashauriwa kufanya shughuli zinazopelekea kupata mapato
“Tuli”.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba mapato Tuli, ndiyo mapato pekee ambayo ni imara, endelevu na
yanarithika. Sababu nyingine inayotufanya tukushauri kupata mapato haya ni kwamba, watu wengi
waliofanikiwa (matajiri) duniani, wamejipanga na kujikita katika kupata mapato haya. Ili kuendelea

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 54/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
kujielimisha zaidi juu ya undani wa mapato haya - "tuli", kupitia mtandao wako wa maarifashop,
tutaendelea kukuletea mafunzo juu ya aina hii ya mapato, ili hatimaye kila mmoja wetu aweze
kuchukua hatua za maksudi tayari kuelekea kwenye maisha ya ndoto zetu.
~TWENDE KAZI PAMOJA~!

JE? UTAMTABUAJE RAFIKI YAKO MWENYE IMANI SAHIHI JUU YA PESA?

Wakati fulani ndani ya mwezi mwaka huu, nikiwa kwa mtoa huduma ya kubrashi
viatu, nilikutana na jamaa mmoja akiwa akiongelea juu ya mambo ya maisha na
mtoa Huduma huyo. Nilipofika waliendelea na stori zao na mimi mara moja moja
nikawa naruhusiwa kuchangia hoja iliyokuwa mezani. Wakati huo wote walijadili
sana juu ya changamoto za kimaisha, ikwemo tatizo sugu la ukosefu wa pesa na
hivyo kufanya maisha kuwa magumu sana. Mimi pamoja ya kwamba nilichangia
lakini nilikwa nasikiliza zaidi mjadala ulivyokuwa ukienda ili niweze kujifunza kitu.
Baada ya mazungumzo hayo nilipata wazo la kutafakari na kuanza kuandika
makala juu ya “Imani Yako Kuhusu Pesa!” wazo hili lilitokana na ukweli kwamba
watu wawili hawa walihitimisha mjadala kwa kusema kuwa “Fedha ina Siri Kubwa”
wakiamanisha kwamba kanuni au njia ya kupata pesa haijulikani. Ukienda mbele
Zaidi unagundua kwamba, tayari kwenye jamii kumekwisha jengeka imani
kwamba kupata pesa ni kubahatisha, Kiasi kwamba wengi wao wanaotafuta pesa
hawana uhakika kama ipo siku watapata.

Kutokana na hitimisho hilo la kwamba “pesa ina siri kubwa” niwazi kuwa kuna
ombwe la uelewa na ufahamu kuhusu maana halisi ya pesa. Na niseme kuwa
imani iliyopo kwa sasa juu ya pesa yawezekana siyo sahihi (ni potofu). Upotofu
huu wa imani juu ya pesa unajidhihirisha Katika matukio mengi hapa nchini kwetu
Tanzania na nchi za jirani, ambapo kumekuwepo na matukio mengi ya watu
kujaribu kutumia ushirikina ili kupata mafanikio ya haraka na hasa mafanikio ya
kifedha.

Kama ilivyo imani Katika dini kwamba mwanadamu aweza kuwa na imani potofu
juu ya wokovu au akawa na imani iliyo ya kweli kuhusu wokovu na linapokuja

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 55/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

swala la upatikanaji wa pesa ni hivyo hivyo, kwani imani yetu tuliyonayo juu ya
pesa imetokana kiwango cha uelewa tulionao. Lakini niseme kuwa ni bahati
mbaya sana kwamba uelewa wetu juu ya kitu pesa bado ni mdogo sana, licha ya
kuwa “Pesa” ni moja kati ya vitu vichache vinavyopendwa sana duniani. Kama
ilivyo katika dini zetu, kwa waumini wa madhebu yote, ili waweze kuwa na imani
sahihi juu ya muumba wao, wanahitaji kwanza neema ya Mungu, lakini pia
wanahitaji watu ambao wako tayari kujitoa na kufanya kazi ya Mungu ili kusaka
ukweli na kuupeleka ukweli huo kwa watu wote kwa jina la “Habari njema” Hivyo
basi kadili watu wanavyozidi kupata ukweli kuhusu wokovu ndivyo watazidi
kujenga imani ya kweli au sahihi juu ya wokovu au kazi ya Mungu.

Kwahiyo, kutokana na mantiki hii ya wokovu, Ndiyo maana wengine tayari


tumeanza kuchukua hatua ya kusaka ukweli juu ya “Fedha” ili ukweli huu uweze
kusambaa kwa watu wote. Imani yangu ni kwamba, iwapo watu watapata ukweli
huu kupitia makala hii au njia nyinginezo, basi ukweli huu, utawezesha wengi
kubadili na kujenga imani iliyo sahihi. Kadili watu watakavyozidi kujenga imani
sahihi juu ya pesa ndivyo itakavyokuwa rahisi kupata pesa na hivyo kuweza
Kuboresha na kuishi maisha ya ndoto zetu.

Katika kutambua nani mwenye imani sahihi juu ya pesa, unaweza kuangalia
dhana, misemo, methali na nahau juu ya pesa kwa mtu binafsi au kundi la
jamii husika. Hivi vyote, ndivyo vigezo au viashiria tunavyoweza kuvitumia
kupima imani ya mtu aliyonayo juu pesa. Kwa kufahamu imani yake iko wapi ni
rahisi sana kufahamu iwapo huyo mtu ana imani sahihi au imani potofu. Mfano wa
baadhi ya viashiria vya imani ya mtu juu ya pesa ni hivi hapa; ”Pesa ni Sabuni ya
Roho” : Dhana hii ya kuamini kuwa pesa ni sabuni ya roho, inatuonyesha kuwa
ndani ya fikra zetu tunadhani pesa ndilo hitimisho la kazi tuliyokuwa tukifanya bila
kujali tumeifanya na kuumia kwa muda gani. Ukitaka kufahamu nani anaichukulia
pesa kama hitimisho, utamuona tu anavyokuwa amechangamka na kuanza hata
kubadili mfumo wa maisha ikibidi hata vyakula, vinywaji, mavazi, hubadilika
kwasababu mtu huyu anajiona amefika mwisho na roho yake imesafishika. Kama
alikuwa akifuga ng’ombe, sasa ataanza kutokuwajali na baadae mradi utakufa na

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 56/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

mwisho zile pesa ambazo alikuwa ameishaanza kusahau zilikotoka na zenyewe


zitaisha. Iwapo hii ndiyo imani yetu juu ya pesa basi ni wazi kwamba pesa hapa
tunaichukulia na kuitumia kama mapato. Tatizo la kuiona pesa kama mapato
huwezi tena kwenda hatua zinazofuata ili kukamilisha malengo yako ya kimaisha
na badala yake unaishia njiani kabla ya kufika mwisho. Wale waliofanikiwa au
wale matajiri, wakipata pesa bado haichukulii kama mapato badala yake utumia
hiyo pesa kuanzisha mradi mwingine, na pesa yote inayopatikana Ndiyo utumika
tena kuazisha mradi mkubwa zaidi ambao faida yake Ndiyo mtu kuitumia kwenye
vitu vya hanasa (luxuries).

Kwahiyo, hili tuweze kuiishi imani hii ya “Pesa ni Sabuni ya Roho” ni lazima
kufahamu kuwa ukishapata pesa unafurahi sana, lakini ni vizuri furaha hiyo
isitusahaulishe tunako kwenda na tuendelee kuiona kuwa ni makaratasi ambayo
tunahitaji kuyatuma kwa wengine ili tupate pesa nyingi zaidi kwaajiri ya kuwekeza
kwenye kuzalisha vitu na huduma bila kikomo.

“Kupata pesa ni bahati, na kama ukuandikiwa na Mungu kuzipata hata


ungefanyaje! Utapata” Usemi huu unaonyesha kuwa kana kwamba kuna baadhi
ya watu ambao wamezaliwa na bahati ya kupata pesa na inaonekana ni
wachache sana ukilinganisha na wale wasiokuwa na bahati. Kuendelea kuwa na
imani hii vichwani ni janga la kitaifa kwasababu, kila utakapo anza mchakato wa
kutafuta pesa fedha na ukakumbana na vikwazo na changamoto mbalimabli ni
dhahili utakuwa wa kwanza kukata tamaa na kuingia kwenye mtego wa kutafuta
njia za mkato ili kupata pesa.

Hili usiendelee kuamini kuwa kupata pesa ni bahati, ni vizuri ukafahamu kwamba
kila mtu amezaliwa na uwezo wa kupata pesa haitakayo. Kinachohitajika kabla ya
kutafuta pesa ni kuchukua muda wako ukafikiri na kutafakari majibu ya maswali
haya; Je? Pesa ni kitu gani?, Pesa hupatikana wapi?, kwanini wengine kipindi
Fulani pesa na baadae kuishiwa?; Je? Pesa inakujaje kwako na inapoteaje? Je?
Wewe unatafuta shilingi ngapi mwaka huu? Kwako fedha itafuata nini? n.k. Kadili
utakavyoweza kujibu maswali haya wewe mwenyewe itakufanya utafakari kwa

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 57/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa

kina na majibu utakayopata yatakufanya ubadili imani potofu uliyokuwanayo na


baadae kujenga imani mpya kuwa “Kupata pesa ni Kuwa na Kitu au Huduma
ambayo itawafanya watu wengine waitume pesa yao kwako kufuata vitu
ulivyonavyo pamoja na huduma huliyonayo. Na hili uweze kupata vitu na huduma
msingi wake ni kazi na ubunifu, iwapo utavitumia hivi vipaji yaani “Kazi na Ubunifu”
sioni sababu nyingine ya kukufanya ukose pesa.

Ewe mtanzania chunguza imani yako juu ya pesa, ili ujitenge na wale wanaotumia
njia ya mkato na kutafuta utajiri wa haraka. Kama ukikuta imani yako ni potofu,
basi kata shauri leo na kubadili ili uwe na imani sahihi juu ya pesa kabla ya kuanza
kuitafuta.
~KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA~

1 comment:
Unknown said...

TUNATOA MIKOPO YA HARAKA YA € 15,000 Hadi $ 72,000 KIASI CHOCHOTE CHA


UCHAGUZI WAKO NA 2-4
SAA ZA MAFANIKIO YA Ufanisi wa Huduma na Viwango vya Riba 2% KWA
WAFANYABIASHARA
NA BINAFSI
MADHUMUNI SASA TUMIA NA UJUMBE WA BARUA KWA:
philipmorganloanservice00@gmail.com

JAZA NA URUDI

Jina:
Kiasi cha mkopo:
Muda:
Jinsia:
Nchi:
Lengo:
https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 58/59
12/1/23, 6:46 PM MAARIFA SHOP: Ufunguo wa Pesa
Nambari ya simu ya rununu:

JIBU LAKO LINAHITAJIKA MARA MOJA


June 4, 2021 at 4:37 PM
Post a Comment

Home

Subscribe to: Posts (Atom)

Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.

https://maarifashop.blogspot.com/p/blog-page_75.html 59/59

You might also like