Faru Script

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 32

FARU

Written by

Shafii Maulidi Satu (Abuthaaqib)

NDOVU FILMS

S.L.P 16833

ARUSHA

0765823120
ii.

Address
Phone Number
1 EXT: PORINI &NDANI YA GARI 1

Ni ndani ya Hifadhi, Linaonekana Gari la Askari wa Hifadhi


Likiwa lipo katika mwendo Huku ikisikika sauti ikiimba Wimbo
wa Kusifu Inchi Ya Tanzania.

(Drone Shot)

SIMBA
"Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa
Moyo wote"

CHUI
"Inchi yangu Tanzania, Jina lako Ni
Tamu Sana"

NYATI
"Nilalapo Nakuota wewe"

TEMBO
"Niamkapo ni heri mama weee"

FARU
"Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa
Moyo Wote"

WOTE
"Tanzania Tanzania, Ninapokwenda
Safarini, kutazama Maajabu Biashara
Nayo makazi, Sitaweza Kusahau mimi,
Mambo Mema ya Kwetu Kabisaa,
Tanzania Tanzania Nakupenda kwa
Moyo Wote".

Ghafla wanaona Gari kwa mbele ikiwemo na watu watatu,Simba


anatoa ishara ya Askari wote Kunyamaza wanasimama ili
kusalimiana nao.

KARAKAL
"The Big 5,Wanyama Watano Ndani ya
Hifadhi yenu Amani Ya Mungu Ipo
Pamoja Nanyi"

walisikika Big 5 wakimwita karakal kwa Bashasha Na


wakionekana kua walimkumbuka sanaa! Walishuka Ndani ya Gari
na Kuanza kusalimiana nae,

SIMBA
"Kitambo kirefu hatukuona karakal"

Tai alimwambia Jaguar


2.

TAI
Hao unaowaona Ndio Askari Ambao ni
Hatari Sana Ndani ya Hifadhi hii,
ni Askari Hodari na wenye Akili,The
Big 5, yule ni
Simba,Chui,Tembo,Faru na Nyati

Wakati Tai anamwambia Jaguar maneno yale kwa mbali yanasikika


maongezi ya kina Big 5 na Karakal

SIMBA
"Karakal kitambo kirefu kaka"

TEMBO
"Leo upo na wageni Gani?"

KARAKAL
"Kaka kaka, Mambo sio Mambo ndo
maana hatuonani, Nipo na Ndugu
wangu Tai na yule Mwingine Ni
Jaguar Ndugu yetu Amekuja
Kututembelea vivutio vya Tanzania"

Tai pamoja na Jaguar wanasogea karibu kusalimiana na Big 5

TAI
"The Big Five,Vipi hali zenu Mpo
sawa?"

Aliwapa tano,kisha Jaguar nae alisogea na kuwapa Tano


Akionekana kama ameudhika

FARU
"Vipi tena Mbona Mmemuudhi Mgeni
wetu, Au hajafurahia Uzuri wa
Hifadhi yetu?"

KARAKAL
"Jini kisirani kamuingia, akimaliza
kununa atacheka tu"

TAI
"Muda sio mrefu vivutio vya Hifadhi
yetu Vitamfurahisha, (Hii ndio
Serengeti bwana")

SIMBA
"Sisi Tuwaache muendelee na
Matembezi, wacha tukaendelee na
Kujenga Taifa".

KARAKAL
"Sawa kaka Tutaonana tena"
3.

TAI
"Kwaheri kaka"

Jaguar alionekana akisoma majina ya askari wale katika vifua


vyao Na kuonekana Mwenye Hasira Baada ya Kuona majina ya
Tembo na Faru

Askari wale waliingia kwenye gari na kuendelea na safari ila


Faru alionekana amewatazama sana wakati wanaondoka alionekana
kama amehisi jambo.

Karakal anasogea na kumfuata Jaguar na kuongea Nae.

KARAKAL
"Sasa Tutawezaje kumaliza Safari
kwa uzuri kama kuna kununiana?"

JAGUAR
"Nina Kisasi Cha Kulipa Ndani ya
Hifadhi Hii"

KARAKAL
"Sio Kazi Ndogo,Tunahitaji Umakini
Mkubwa Na Kazi inahitaji Muda wa
Kutosha"

TAI
"Kazi Hii Haitawezekana Kwa Siku
Ulizopanga wewe Maana Sio kila
Utakalo litatimia Mengine ni Kama
Bahati Nasibu"

KARAKAL
"Faru ni wachache Sana Na pia wengi
wao wapo katika Uangalizi Hivyo
wamefungwa Viashiria Na
wanajulikana wapo wapi Ndo maana
Kabla Hatujaua Lazima Tumkague kama
Kafungwa Kiashiria cha usalama"

JAGUAR
"Mnaongea Upumbavu
Mtupu,Nimewapatia Pesa Nyingi sanaa
Ili mkamilishe Hili,Mtafanya Vile
Nitakavyo"

TAI
"Sio kila jambo Unalipeleka kwa
Hisia Na Kwa Nguvu ya Pesa Mengine
Ni akili Na Uzoefu"
4.

KARAKAL
"Wewe Ni Mgeni Katika Hifadhi
Hii,Tulia Na Lazima Utumie akili
kubwa Maana Moja ya Nguvu Kubwa Ya
serikali ipo Katika Hifadhi Hii"

Jaguar alipiga Gari kwa Hasira Na kuchukua Bangi yake na


Kuanza Kuvuta Huku akionekana mwenye Hasira,Karakal
alimtazama Na Kujisemea.

KARAKAL (CONT'D)
"Ama kweli Nimeamini Bangi sio Mama
yako Useme Itakuonea Huruma"

Karakal alifungua Gari na kuchukua maji matatu na Kumpatia


Tai Na wakati anampatia Jaguar ila jagua aliyapiga Maji yale
Kibao akionyesha ishara kua ameudhika,Karakal alisikitika na
kusogea pembeni.

2 EXT:PORINI 2

Anaonekana Boss Akiwa Ofisini Akipiga simu,Anaonekana Jaguar


anatoa simu Mfukoni akasogea pembeni na kupokea huku Karakal
na Tai wakitizamana

JAGUAR
"Nakusikia Ongea!"

TANZANITE
"Kua na Adabu! Mimi ni Baba
yako,Ujisahaulisha kua Baba yako ni
Kaka Yangu?"

Alishika picha iliyoko mezani na Kuitazama Ambayo alikua yeye


na kaka yake.

JAGUAR
"Sina Muda wa kusikiliza hayo,Toa
Melekezo ya kazi"

TANZANITE
"Mmmh Natumaini Umewaona Hao vinaja
wawili,La muhimu kwa sasa ni kazi
iliyowapeleka,Mteja amepiga simu na
leo ndio atatoa malipo ya awali ya
mzigo wake hivyo fanya hima ,kuhusu
kisasi tutapanga baadae"

JAGUAR
"Nimekuelewa ila kuhusu kisasi
usinipangie muda wa kukilipa"
5.

Alikata simu na kuendelea kuvuta bangi,alisogea na kuwafuata


wenzake, aliokota maji yale aliyoyapiga na kuyafungua akanywa
kisha akasema

Mteja yupo Tayari anasubiri mzigo wake hivyo tufanye hima


kupata Mzigo mapema tuondoke, ikiwezekana naomba upige simu
tujue kinachoendelea

Wanaangaliana Tai na karakal

3 EXT:PORINI 3

Wanaoneoana Askari 5 wa (BIG 5), Askari mmoja alionekana


akitoa chupa tano za maji na kuanza kuwagawia askari wenzie,
Mmoja wao alisikika akisema

CHUI
"Faru, Ungeanza kumpa kaka yako
Tembo,kisha Tukafuata wengine."

TEMBO
"Chui Wewe pia ni kaka Yetu ndio
maana Ameanza na wewe"

CHUI
"Sikia Tembo,Ningeringa sanaa
ningekua Na Undugu na nyinyi, Hivi
kwanini mliamua kujiunga na jeshi
hatari kama hili tena Ndugu wa
Damu?"

FARU
"Baba yetu alikua Askari wa kulinda
wanyama pori, Hivyo tumerithi kazi
ya Baba yetu"

NYATI
"Baba yenu Alikua Hodari kama
Nyinyi?"

SIMBA
"Wanaonekana wanafuata Nyendo za
Baba yao"

TEMBO
"Hatujamfikia Hata theluthi ya
Uhodari wake Afande"

CHUI
"Mnaweza kumfikia na Kumpita kama
Mtamuuliza mama yenu vizuri kuhusu
uhodari wa Baba yenu"
6.

Wote walicheka,Faru alitabasamu kisha akamrushia Chui Maji


Mengine na kumwambia

FARU
"Chukua zawadi ya Kunipa siri ya
Kua Hodari kama Baba yangu"

Ghafla ilisikika Radio ikitoa Maelekezo ya Doria Yao kutoka


Ofisini.

REDIO
"kikosi cha Big 5 Rudia kama
mnanisikia"

SIMBA
"Big 5 Tumekupata Rudia kama
unatusikia"

RADIO
"Natumaini upande huo upo salama
over"

SIMBA
"Tupo salama na kila mahali kupo
shwari over"

RADIO
"Mwelekeo wa leo Kusini mashariki
Over"

SIMBA
"Tumekunakili over"

Wanaonekana kuingia ndani ya gari na kuelekea walipopewa


maelekezo

4 EXT:KIJIJINI 4

Anaonekana mtu mmoja akiwa na baiskeli amebeba mzigo wa kuni


akiwa amezifunika kwa kipande cha mfuko,anasimama na kuweka
kizuizi cha baiskeli yake na kusogea pembeni na kuanza
kukojoa huku akipiga mluzi,mara ghafla simu yake
inaita,anamalizia kukojoa harakaharaka na kuingiza mkono
mfukoni kutoa simu yake

JANGILI
"Haloo,vipi hali yako?"

KARAKAL
"Salama kaka, vipi kila kitu kipo
Tayari au bado"
7.

JANGILI
"Safari hii mnabahati kweli kwa
maana mitego yetu imenasa mapema
sana,mteja wa safari hii ana Baraka
kweli".

KARAKAL
"Acha hadithi nyingi tupe maelekezo
tunaupataje maana Hatuna muda wa
kutosha,hapa tulipo tunatamani
kupaa tukufuate ulipo"

JANGILI
"Ndo nilikua nakaribia kuingia
kijijini, japo njaa inaniuma ila
naona bora niwasubiri maana ingia
toka ingia toka kijijini sio salama
kwa kazi zetu na siku hizi hali sio
shwari saana,tuapambana kiuzoefu"

KARAKAL
"Sawa tukutane upande upi? Usalama
wote upo juu yako".

JANGILI
"Ondoa shaka mimi sina tofauti na
mbwa mwitu,yoyote anayejichanganya
mbele yangu sijawahi kumuacha
salama, tukutane upande wa
mashariki kwenye kituo chetu."

KARAKAL
"Vizuri,Usiogope kuhusu njaa wala
kiu nina chakula na maji."

Karakal alikata simu na kuanza safari na kuelekea eneo husika

5 EXT:NYUMBANI 5

Anaonekana mwanamke mjazito akiwa nyumbani pamoja na mama


mkwe wake, anachukua simu na kupiga, anaonekana anampigia
mume wake lakini simu haipatikani,anaikata na kuiweka
pembeni, kasha anamuita mama.

MKE
"mama mwanao mpaka sasa hapatikani
na mimi leo hali yangu najiona
kabisa sio nzuri,huwenda Mgeni
akaja leo in shaa Allah"
8.

MAMA
"Pole mwanangu,muda mwingine
wapaswa kua jasiri, hata mimi
ujauzito wangu wa kwanza ulikua
unampenda sana baba yenu, hivyo
sikuweza kumkosa machoni mwangu"

MKE
"Kama ni hivyo basi na jina
tumwandalie kabisa huwenda
nikamleta baba"

MAMA
"Inshaa Allah, sote tunategemea
itakua hivyo."

MKE
"In shaa Allah"

6 EXT:PORINI 6

Anaonekana mwakijiji akipishana na mwanakijji mwenzie wote


wakiwa na baiskeli wanasimama nakusalimiana

JANGILI
"Habari ndugu yangu"

SHUSHUSHU
"Salama kaka, vipi mbona unatoka na
kuni kijiji unazirejesha tena
porini?"

JANGILI
"Hahahaha Maisha ya siku hizi bila
simu yaani unaonekana hujaendelea
na chaajabu zaidi, ukiipoteza simu
ndo Matokeo yake haya kuonekana
mwendawazimu, Hata sijafika
nyumbani imebidi nirejee maporini
kuitafuta"

SHUSHUSHU
"Pole sana ndugu yangu,simu
imerahisisha maisha ila simu nayo
inaangamiza maisha,naomba
nikusindikize maana pia wanyama
wakali wapo kila mahala"
9.

JANGILI
"Hapana ndugu yangu,usijisumbue
nitaitafuta mwenyewe,na kuhusu
wanyama, wenyewe wakiniona
wanakimbia kama vichaa,usighairi
safari yako kisa mimi bwanaa."

SHUSHUSHU
"Sawa ila kuna dharura hata za
maradhi kutembea wawili ni bora"

Mara simu ya Jangili inaita mfukoni mwake na kupigwa na


butwaa,shushushu alitabasamu kisha akasema "haya baadae uwe
na safari njema",Jangili alimtazama kwa hasira na kuondoka
zake.

7 EXT:PORINI 7

Wanaonekana askari wakiwa karika Doria ya eneo husika,wote


wapo nje ya gari

FARU
"Jamani ukweli mimi sina imani na
Yule jamaa aliyekua na kina
karatai,sijui kwanini hajanitoka
kwenye akili yangu,wasiwasi
unaniambia sio mtu mwema kabisa."

NYATI
"Una maanisha nini?"

CHUI
"Ina maana hauwaamini pia karatai?"

Simba na tembo walimtazama bila kusema neno lolote kama vile


wanatafakari jambo kwa kina,Faru aliwatazama wote kasha
akasema

FARU
"Naona muda wa swala umeingia ni
bora tuswali kwanza,Huwenda ni
wasiwasi wangu tu,pia ni kawaia ya
ibilisi kutia wasiwasi katika nyoyo
za watu. "

Faru,tembo na simba walionekana kujiandaa na kuanza kuswali


huku Nyati na chui wakiwa katika doria.

8 EXT:OFISINI 8

Tunamuona baba yake Jaguar akiwa ofisini kwake,Mara tunasikia


mlango unagongwa,anageuka na kusema
10.

TANZANITE
"Ingia"

Malango unafunguliwa anaingia kijana mtanashati akiwa


amevalia mavazi meusi mwenye kujiamini

KIJANA WA WILD
"Habari Bwana Tanzanite,nimeagizwa
na bwana Wild nikuletee mzigo wako"

TANZANITE
"Karibu ukae,utahitaji kawaha au
chochote"

Kijana alitoa bahasha kumkabishi Baba yake Jaguar kasha


akamjibu

KIJANA WA WILD
"Hapana Asante Nipo sawa."

Baba yake Jaguar alichukua Bahasa ile na kuhakikisha kilicomo


ndani,alitoa na kukuta hudi ya bank yenye thamani ya million
mia tano,alichua simu na kumpigia bwana Wild.

TANZANITE
"Hello Mr Wild"

WILD
"Hope you receive it Mr Tanzanite"

TANZANITE
"Received"

Alikata simu na kumwambia kijana unaweza kwenda sasa,kijana


aliinuka na kufuangua mlango na kuondoka zake.

9 EXT:NYUMBANI & PORINI 9

Anaonekana Mwanamke mjazito anapiga simu kwa mara nyingine na


anaonekana anampigia mume wake tena.

MKE
"Asante Mungu afadhali inaita sasa"

Huku tunamuona nae karakal simu yake inaita anaitoa mfukoni


na kujisemea

KARAKAL
"Asante Mungu Afadhali amepiga"

Karakal anaipokea na kuanza kuzungumza


11.

KARAKAL (CONT'D)
"Haloo,halooo,netiweki sio nzuri
kabisaaa"

Anapanda juu ya boneti ya gari na kutafuta netiwek huku simu


ikiwa hewani na kuendelea kuita,halooo anajitahidi kuziba
sikio moja.

MKE
"Haloo Mume wangu Kipenzi"

FARU
"Haloo mke wangu Mzuri"

MKE
"Assalaam aleykum mume wangu"

FARU
"Waaleykum salaam mke wangu"

MKE
"Nimekutafuta sana hupatikani mpaka
nikawa na wasiwasi,na leo najionea
tafrani tu,sijui ndo baba yako
anataka kuja."

FARU
"In shaa Allah, Nitafurahi ikiwa
hivyo,msiwe na wasiwasi ni netiweki
tu inasumbua baadhi ya maeneo"

MKE
"Mama mwanao nimepata njoo uongee
nae,Ngoja kwanza umsalimie mama
maana netweki inaweza kututoroka
tusikupate tena."

FARU
"Sawa mke wangu."

Mama alisogea kwa mkwe na kupewa simu aweze kuongea nayo

MAMA
"Haloo Mwanangu,Hamjambo? Poleni na
kazi"

FARU
"Hatujambo mama shikamoo"

MAMA
"Marahaba mwanagu,kaka yako nae
hajambo? Maana nae simu yake
haipatikani"
12.

FARU
"Sote tupo sawa Dua zenu tu."

MAMA
"Mungu awalinde wanangu na Mungu
awafanye muwe mahodari kama baba
yenu"

FARU
"Amiin"

MAMA
"Halooo,halooo"

10 EXT:PORINI 10

Anaonekana karakal akiwa amekaa juu ya gari akihangaika na


simu nae hakiita haloo,scene hii itaunganishwa na mama
alivyojua akiita haloo

KARAKAL
"Haloo,hapo nakusikia,hili ndo
tatizo nalichukia huku kwenu."

JANGILI
"Pole ndo kazi uliyoichagua,jikaze
acha kudeka"

KARAKAL
"Mimi sina tatizo ila kuna kitinda
mimba tupo nae ndo tatizo,najuta
kuja nae kabisaa"

JANGILI
"Njaa inaniuma sana naomba mfanye
haraka"

JAGUAR
"Kuzungushana maporini tuu mwisho
tuliwe na fisi ndo akili zitatukaa
vizuri"

TAI
"Hahahah jikaze wewe, acha kutia
huruma,ulilia jeshi wala ujionee
mwenyewe"

KARAKAL
"Haya safari iendelee".

Wanaingia ndani ya gari na kuendelea na safari yao ya


kuelekea kwa mwenyeji wao
13.

11 EXT:PORINI 11

Anaonekana Baba yake jaguar akiwa ameingia Benk anaonekana


yupo na meneja wa tawi la bank husika wakiwa katika
mazungumzo.

FEDHA
"Karibu Bwana Tanzanite,
hatujaonana kitambo,vipi biashara
zako"

TANZANITE
"Nipo Salama kabisa Bwana
Fedha,kuhusu biashara sio nzuri
sana kwa sasa, ndo kuna mdeni wangu
mmoja ndo amenilipa leo nimeona
nilete mapema maana nina mambo
mengi na yanahitaji pesa"

FEDHA
"Bado upo na just tanzanite au una
biashara ingine,maana watu wakubwa
mnawekeza kwenye mambo mengi"

TANZANITE
"Ni kweli kabisa ,uwekezaji ndio
jambo muhimu sana,kwa sasa bado
nipo na just tanzanite".

Alitoa hundi ile ya fedha kutoka kwa bwana wild na kuisaini


nyuma kisha akumkabidhi meneja,meneja aliipokea na kusema

FEDHA
hakuna tabu tutaifanyia kazi muda
sio mrefu,Kkaribu tena bwana
Tanzaniate.

TANZANITE
"Asante Bwana Fedha,nawe siku moja
upite ofisini kwetu uone biashara
zetu,sio sisi pekee ndo tunakufuata
kila siku"

Wanacheka kwa pamoja

FEDHA
"Nitakuja kukutembelea ondoa shaka"

TANZANITE
"Nitafurahi kukuona"

Wanapeana mikono na Bwana Tanzanite anaondoka zake.


14.

EXT:PORINI
Wanaonekana askari wa hifadhi
wakiwa wanatembea kwa mstari na
huku gari yao ikifuata
polepole,simba anaonekana kushika
simu yake na kupata ujumbe,anatoa
ishara ya kusimama,wanasimama.

SIMBA
"Askari,kuna Taarifa ,kijiji cha
Fisi upande wa mashariki kuna
kiashiria cha ujangili,sote
tunaelekea huko"

WOTE
"Ndio Afande!"

Wote wanaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea


mahala husika walipopewa taarifa za ujangili

12 EXT:PORINI 12

Wanaonekana karatai wakiwa awanaendelea na safari yao


wananonekana kufika mahala na kusita maana wanaonekana
kukosea njia karakal anasuka na kutazama njia vizuri na
kusema.

KARAKAL
"Tumekosea njia tupite ile ya kule
tumebakiza kilometa 2 tu tutakua
tumefika"

JAGUAR
"Mnachekesha sana kumbe hata
hamapajui mnapokwenda?"

TAI
"Ungebaki nyumbani kunyonya
kitindamimba wa watu"

JAGUAR
"Unasemaje?"

KARAKAL
"Haya sasa mnataka kufanya nini?
Kimyaa! Mnajua fika kazi hii ni
hatari lakini bado mnataka kuanza
upuuzi wa kutiliana uchuro."

TAI
"Samahani kaka, alisema kisha
akampiga bega"
15.

13 EXT:PORINI 13

Wanaoanekana askari wanayama pori nao wakiendelea na safari


yao tena kwa mwendo wa kasi.

SIMBA
"Natumaini sote tunajua cha kufanya
na jisi ya kuliendea hili jambo"

WOTE
"ndio afande!"

SIMBA
"Nawakumbusha kua hii ni vita,sote
tuna haki ya kuipigania nchi yetu
na urithi wetu,tunapokwenda kila
mmoja wetu ana ulazima wa kujilinda
na kumlinda mwenzake,tunakwenda
watano na tutarudi
watano,mmenielewa"

WOTE
"Ndio Afande!"

14 EXT:PORINI 14

Anaonekana mwanakijiji aliyekua na mwanakijiji mwenzake pale


awali akiwa amemfuta kwa mara nyingine huku akimwita huku
anamfutuata,hapa tunajua jina halisi la jangili kua anaitwa
mwitu

MWANAKIJIJI
"Mwituu!"

Mwitu anageuka na kushangaa Yule jamaa kafikaje tena


anamtazamaa kwa mshangao

MWANAKIJIJI (CONT'D)
"Samahani kama nimekuudhi mwitu,
nimekuona haupo sawa hivyo
nimekuhofia ndugu yangu usije
ukapatwa na matatizo,na sisi ni
wanaume hata kama una matatizo
niambie takusaidia"

MWITU
"Ama kweli wewe ni nyumbu kama jina
lako,hiyo tabia yako ya
kujisahaulisha mbaya sana, kama mtu
hataki kitu wewe unalazimisha cha
nini? kuna siku itakuponza Haki
nakuambia"
16.

Hapa tayari tumejua jina halisi la mwanakijiji ni


Nyumbu,nyumbu alitabasamu na kumuonyesha anataka amani,ila
Mwitu anaonekana kujawa na hasira kiasi, kasha akamtazama
nyumbu na kucheka kasha akamwambia

MWITU (CONT'D)
"wewe ni mwema sana,jumuika
nami,ukweli wanawake wanaudhi sana
majumbani mwetu,unaweza kuamini
nafika nyumbani badala mtu anipokee
na akushukuru anaanza maneno eti
kuni nyembamba nataka nene mara
sitaki fupi nataka ndefu yaani
ilimradi tu kusiwe na amani ndani
ya nyumba,ndo maana ulishangaa
natoa kuni kijiji na kuzirejesha
mwituni"

NYUMBU
"Pole sana ndugu yangu,mwanamke
anaweza sababisha hata mtu
ukajinyonga buree,eeeeh Mungu
epushia mbali"

MWITU
"Muda mwingine hua nakuja huku
mbali kutazama uzuri wa mandhari
yetu ili kuwa sawa,Hebu anagalia
kunavyopendeza"

Nyumbu alisogea karibu na Mwitu wakiwa wanatazama uzuri wa


mazingira,huku wote wakitabasamu,nyumbu alimgeukia mwitu
kasha akarejesha macho mbele,ghafla mwitu alitoa kisu na
kumchoma kikatili,nyumbu alistuka na huku akisikilizia
uchungu wa kisu kwenye ubavu wake,anashika sehemu ya maumivu
na kurejesha mkono mwilini mwa mwitu ili kujizuia,na
kumchafua kwa damu.

MWITU (CONT'D)
"Wewe ni nyumbu tu,hujawahi kua
makini na maisha yako,hatimaye
mikononi mwa mbwa mwitu,puzika kwa
amani rafiki"

Alimlaza chini kwa upole huku akimuacha akitapatapa,simu ya


nyumbu inadondoka kutoka mfukoni,mwitu anaiokota na kuitazama
anakuta ina namba za siri,anatoa betiri ya simu anaitia
mfukoni anachukua jiwe na kuipasua ile simu na kuchua
baiskeli ya nyumbu akaitia kichakani na kuondoka zake.
17.

15 EXT:PORINI 15

Wanaonekana askari wakizidi kusogea sehemu husika,simba


anachukua simu kasha anapiga,inaonekana simu ya Jaguar inaita
Anaingiza mkono mfukoni na kuitoa anapokea

JAGUAR
"Ongea!"

TANZANITE
"Malipo tushapokea hivyo
wahimize,nakupeni siku mbili mzigo
uwe umekamilika na siku ya tatu
ufike mahala husika"

JAGUAR
"Siku mbili nyingi sana,mzigo upo
tayari ndo tunaenda kuuona kasha
utupatie maelekezo ya kuuchukua"

TANZANITE
"Vizuri,kua makini na usifanye
jambo lolote La kupuuzi,huyo jamaa
unaenda kukutana nae sio mtu wa
mchezo"

JAGUAR
"Nimekuelewa!"

Alikata simu na kuwaambia wenzake

JAGUAR (CONT'D)
"Naombeni tufanye mambo kwa uharaka
maana sitaweza kulala porini,sehemu
hakuna maji wala choo"

KARAKAL
"Kwa safari hii na ulichokifuata
kweli unawaza choo,haya sema
kingine unachoogopa porini?"

TAI
"hahaha alisema anaogopa kuliwa na
fisi"

KARAKAL
"kwa mwendo huu tunaoenda wa kudeka
hivi utaliwa hata na sungura"

JAGUAR
"Wapuuzi"
18.

16 EXT:PORINI 16

Tunarejeshwa ndani ya gari la askari,tunamuona simba


anajaribu kutafuta netiweki

SIMBA
"Sio kawaida ya huyu jamaa
kutokupatikana wala kutotuma ujumbe
wake wowote,nahisi kuna tatizo
maana hajawahi toa taarifa ya uongo
wala hajawahi kuchelewa kutoa
mwendelezo wa taarifa"

NYATI
"Mimi pia nina wasiwasi kama
wako,huwenda kapatwa na jambo baya"

FARU
"Siku ya leo nina wasiwasi
sana,Tuombe Mungu iwe salama"

TEMBO
"Tulia ndugu yangu,kaka yako nipo
hapa hakuna litakalokutokea, na
kama ni kuhusu shemeji basi
atajifungua salama."

FARU
"Amin"

CHUI
"Faru toka Asubuhi aliwahisi wale
jamaa vibaya labda ndio bado
anatembea na hisia zile"

SIMBA
"Simama kwanza hapo mbele tujaribu
kuwasiliana nae tena maana maeneo
yao ndo haya"

Wanasimama na kushuka kwenye gari,simba anapanda juu ya gari


kutafuta netiweki na kupepesa macho huku na kule kuangalia
usalama kabla ya kuendelea na safari,ghafla ilisikika sauti
ya Simba akiita Askari huna nae akishuka wepesi

SIMBA (CONT'D)
"Askari angali kichaka kile kuna
baiskeli imefichwa pekua kila
mahala"

Askari wanajipanga na silaha zao tayari kwa upekuzi,ghafla


faru anakanyaga simu na kutazma chini na kuseme
19.

FARU
"Afande kuna simu imevunjwa huku"

CHUI
"Afande, mbona ni baiskeli ya
Askari wetu"

SIMBA
"Pekuweni kila mahali Tafadhali
zote ni ishara mbaya"

NYATI
"Afande,askari wetu huyu hapa
amejeruhiwa vibaya leta maji
haraka"

SIMBA
"Faru,Nyati,Tembo anaglia hali ya
usalama,chui Huduma ya kwanza
Haraka,tembo ongeza nguvu kwenye
huduma ya kwanza"

Majeruhi akiwa amezuia jeraha kwa shati lake ili kuzuia damu
isimtoke kwa wingi,Wanaonekana wanamfanyia huduma ya kwanza
kukagua mapigo ya moyo na mengineyo

CHUI
"Afande,Bado anahema."

SIMBA
"vizuri hakiksha anakua salama
maana taarifa yote anayo yeye"

CHUI
"Sawa Afande"

Chui anachukua sindano ya kuzuia damu na kumchoma askari Yule


wanamuweka sawa kasha wanampatia maji,wanazuia kidonda chake
kisivuje damu,wanambeba na kumuigiza kwenye
gari,wanamtundikia dripu ya kumpa nguvu,Baada ya dakika 30 za
mapumziko anaonekana kuzinduka na kujikuta mikononi mwa
askari.

SIMBA
"Unamjua aliyekufanyia hivi"

Nyumbu alitikisa kichwa kwa ishara

SIMBA (CONT'D)
"Nani kakufanyia hivi na kaelekea
wapi?"
20.

Nyumbu alisema kwa sauti ya chini akisema na chui akiwa


amesogeza sikio lake karibu na mdomo wa nyumbu nakusikia jina
la Mwitu

SIMBA (CONT'D)
"Amesema nani?"

CHUI
"Amesema Mwitu"

SIMBA
"Ndio Yule tuliyekua tunamfuatilia
kama anajihusisha na ujangili?"

Nyumbu anatikisa kichwa kuashiria ndio.

CHUI
"Afande,Askari wetu hakuumia
sana,pia alijizuia kwa tumia nguo
yake damu isimtoke kwa wingi,jua
lilichangia kumchosha hivyo kwa
sasa anaendelea vizuri"

NYATI
"Afande nashauri,Kama askari wetu
anaendelea vizuri tunaweza
kuendelea na mpango kazi"

Walimtaka Asksri awape muelekeo wa jamaa alipopita

Faru anatafakari kukumbuka jambo

17 EXT:PORINI 17

Scene hii ni kumbukumbu,Asubuhi mapema Askari walipishana na


jamaa akiwa na baiskeli yake wanasimamisha gari.

SIMBA
"Habari,unaelekea wapi mapema yote
na unajua wanyama wakali wapo kila
mahali?"

MWITU
"Salama,ni kweli uyasemayo,ila
naomba mniwie radhi nina mgonjwa
kijiji cha pili naenda kumuona ni
dharura tu,mimi pia najinea
huruma,nimetoka nimechanganyikiwa"

SIMBA
"unaitwa nani?
21.

MWITU
"Naitwa Mwitu Tambarare"

SIMBA
"Pole kwa kuuguza,uwe na safari
njema"

MWITU
"Asante nanyi pia"

kila mmoja akaendelea na safari yake,mwisho wa kumbukumbu.

18 EXT:PORINI 18

Scene hii ni mwendelezo wa scene ya 17 pale faru


alipomkumbuka Mwitu.

FARU
"Afande,kuna jambo
nimekumbuka,huwenda likatuongezea
nyama katika mpango kazi wetu"

SIMBA
"Tuambie faru umekumbuka nini? "

FARU
"Asubuhi tulipishana na mtu na
akatuambia anakwenda kumuona
mgonjwa,na ulipomuuliza jina lake
alisema anaitwa mwitu
tambarare,tumuulize Askari wetu
kama ndiye mtu aliyemdhuru
tunayemtafuta"

NYUMBU
"Ndio yeye Afande Anaitwa Mwitu
Tambarare"

SIMBA
"Vizuri"

TEMBO
"Ndugu yangu nakusifu sana kwa
kumbukumbu nzuri"

NYATI
"nashauri wasiwasi wa Faru uwe ni
wa kuzingatiwa"

Walitabasamu,gari inaonekana inaendelea ana safari.


22.

19 EXT:PORINI 19

Inaokana gari ya kina Karakal ikiwa imesimama na anaonekana


Mwitu anakuja na Baiskeli yake,anasogea karibu yao
anasimamisha baiskeli yake vizuri,karakal anamrushia
maji,Mwitu anayadaka na kuyafungua na kunywa,kasha
anasalimiana nao

MWITU
"Poleni kwa kusubiri,natumaini wote
mnaendelea vizuri"

TAI
"Tupo poa,mbona shati lako na usoni
una damu?"

MWITU
"kuna mzembe alijichanganya
nikamsaidia kumuonyesha njia ya
mbinguni,alale salama tumboni mwa
fisi"

Jaguar anamtazama Yule jamaa kwa sura ya sintofahamu,Karakal


Anachukua maji na kunyunyizia,ananawa na kuitoa damu iliyopo
kwenye shati lake.

KARAKAL
"Hatuna muda,Pakia baiskel
tuondoke"

Wanafungua mzigo wa kuni na hapa tunaona katikati ya kuni


alikua ameficha gobore lake la kuwindia,Wanaifunga baiskeli
kwenye gari na kuondoka kuelekea sehemu husika.

20 EXT:PORINI 20

Wanaonekana askari wakiwa katika gari lao wanasimama na


kushuka wanatazama nyayo vizuri wapi alipoelekea mwana Mwitu

TEMBO
"Afande,alama za tairi za baiskeli
zinaelekea huku"

Wote wanasogea na kutazama mbele kuangalia ala za baiskeli


zilipopita zinapoelekea

FARU
"Afande kuna boma za kimasai zipo
hapo mbele,tujaribu kusogea huwenda
kuna mtu wanahusiana nae anaishi
maeneo hayo,au laa basi ndipo
wanapohifadhi nyara zote"
23.

SIMBA
"Askari,wote ndani ya gari
tafadhali"

Askari wote wanaingia ndani ya gari na kuendelea na safari

21 EXT:PORINI 21

Anaonekna massai mmoja akiwa amesimama anaitazama gari


inakuja,ananyoosha mkono kuwapa ishara gari iweze
kumfuata,gari ya karatai inaenda muelekeo wa massai,wanafika
na kusimama.

MWITU
"Kama nilivyokuambia,safari hii
kila kitu kimekua haraka sana"

MASSAI
"Ndo vizuri maana kukaa na hizi
vitu ndani sio salama,muda mwingine
Askari wanakuja kukagua maboma
zetu,kama metoka huko na meona
hakuna usalama jifanyeni kama
naendelea na safari zenu mtakuja
baadae jua ikizama"

KARATAKAL
"Usiogope Massai,hakuna aliyetuona
wala hatujapishana na mtu"

Masaai alisogea mbele na kuangalia huku na kule kama kuna


hatari yoyote,aliwapa ishara waingize gari bomani,gari
inaingia bomani na kupaki vizuri,wanashuka kwenye gari
karakal na Tai wanachukua silaha na kuziweka kiunoni tayari
kwa biashara na usalama wao

MASSAI
"Karibuni sana,Jisikieni mpo
nyumbani"

KARAKAL
"Asante sana,sasa sisi sio wageni
tena,tupo nyumbani na tunaimani
hali ni shwari"

MASSAI
"ondoeni wasiwasi"

KARAKAL
"Natumaini wengine unatujua,huyu
anaitwa Jaguar ni Ndugu yetu kama
walivyo wengine,ndo kijana wa Bwana
Tanzanite"
24.

MASSAI
"Karibu Jaguar,Baba zako wote
nimefanya nao kazi muda murefu
sana, na walikua wanalala kwenye
hizi maboma, jisikie upo nyumbani

JAGUAR
"Asante sana nimefurahi"

MAASAI
"Unaweza kufanya malipo sasa"

Jaguar aliwatazama na akaona amani imetawala alitoa bunda la


dollar na kumkabidhi massai,Massai alimtazama kisha
akamuuliza

MASSAI
"Hauna pesa za kitanzania?"

JAGUAR
"Tulihofia zitakua nyingi sana na
ingekua mzigo mkubwa"

MASSAI
"Sawa,twendeni mkaone mzigo wenu"

Massai alipokea pesa kisha akawachua na kuwapeleka mzigo


ulipo,wanaingia kwenye Nyumba.

22 EXT:PORINI 22

Wanaonekana Askari wakiwa wamesogea karibu na maeneo ya


maboma ya kimassai

SIMBA
"Askari,kama kawaida tutaacha gari
huku kisha tutakwenda kwa miguu
kufanya upekuzi na mjiandae kwa
vita lolote linaweza kutokea"

WOTE
"Sawa Afande"

Simba alimtazama nyumbu na kumwambia

SIMBA
"Kwa hali yako Utabaki kwenye gari"

NYUMBU
"Sawa Afande"
25.

Askari wanajiweka sawa na kuanza safari ya kuelekea kwenye


boma,wanakwenda kwa mfumo wa ustadi wa kijeshi ili wasiweze
kugundulika wala kuonekana na mtu yoyote,wanasogea mpaka
karibu na maboma,wanaiona gari ya karatai ikiwa imebeba
baiskel.

CHUI
"Si gari ya karatai ile na imebeba
baiskeli?"

FARU
"Hiyo baiskeli huwenda ni ya Mwitu
ambaye ndo mwenyeji wao"

NYATI
"Hakika huwenda Ndivyo"

Simba anatoa ishara ya kuzunguka boma,askari wanazunguka boma


kwa ustadi wa kijeshi kuhakikisha hakuna anayetoka eneo lile.

23 EXT:BOMANI 23

Wanaonekana karatai,Jaguar,massai na Mwitu wakiwa kwenye


mazungumzo wote wameshika vikombe vya chai.

KARAKAL
"Jaguar tupe muongozo kuhusu
usafiri"

JAGUAR
"Kuna canter tumeiandaa itapita
usiku kuchukua mzigo na
utachanganywa na mahindi hivyo
hawatoweza kugundua barabarani"

TAI
"Vizuri"

ghafla wanasikia sauti ya mbwa kwa mbali,Massai anaweka


umakini anasimama na kusogea mbele kutazama,wote
wanashangaa,anawapa ishara ya kutulia,anawapa ishara ya kua
wasimame.

MASSAI
"Askari wamekuja"

KARAKAL
"Hapanaa!"

Anasema kwa hasira akiwa ameuma meno,Mwitu anasogea mbele na


kujiweka sawa,Anashika gobore lake vyema na kusema
26.

MWITU
Msiogope hawa nawahimili
mwenyewe,kaa tayari kwa vita silaha
yako ndio uhai wako

Massai aliingia ndani na kuchukua gobore lake tayari kwa vita


dhidi ya askari wa hifadhi,Mwitu akaanza kushambulia ili
kutia taharuki kwa askari wa hifadhi,risasi zilianza
kumiminika baina ya askari wa hifadhi dhidi ya majangili,vita
iliendelea ya kuwindana mpaka pale Jaguar alipofanikiwa
kumuona faru akiwa kwenye jicho lake la mawindo yake na
kumpiga risasi,faru anaanguka na huku akisikilizia maumivu
makali ya risasi mwilini mwake,Tembo anapata taarifa kua faru
amepigwa risasi nyati amvuruta faru kumuweka sehemu
salama,ghafla alikuja tembo akiwa kwenye taharuki kubwa
akimimina risasi kuwalinda faru na nyati wote wakimwiita jina
lake,simu ya faru inaita pemebeni ikiwa imenguka,tembo
anaichukua simu ile na kutazama ni mama yao,anaitia kufuli na
kuiweka mfukoni,wanaendelea kumtizamia hali yake wanazuia
damu kwa nguo,Chui alisogea haraka kwaajili ya huduma ya
kwanza, nyati anaendelea kupambana, chui anatoa sindano ya
kukata damu na kumchoma haraka,faru hali yake inazidia kuamba
mbaya na kuanza kupotea kwenye uli

mwengu

...KIZA...

Sauti za Askari zanasikika zikimwita Faru zikiambatana na


milio ya risasi, milio ya risasi inasimama na tunasikia jina
la faru likiitwa ,tunasikia mlio wa ishara ya kupotea kwa
fahamu kimyaa kinatawala.

24 INT:HOSPITAL 24

Kiza kinaanza na sauti za gari ya dharura ya wagonjwa


zinasikika,Mlango unafunguliwa na Daktari anatoka na kukutana
na mama akiwa mlangoni anasubiri

MAMA
"Daktari nipe taarifa ya mgonjwa
wangu tafadhali"

DAKTARI
"ondoa wasiwasi,Yupo salama pia
hongera amekuleteeni mtoto wa
kiume"

MAMA
"Alhamdulillah, hakika Mungu
hujawahi kumnyima yoyote akuombae"
27.

Anatoa simu kwa furaha na kumpigia mwanae ili ampe taarifa ya


kujifungua kwa mkewe,anapiga simu

25 EXT:PORINI 25

Scene hii ni mwendelezo wa scene ya 24,tunasikia simu inaita


Tembo anatoa simu mfukoni na anasogea pembeni askari wote
wakiwa wamemzunguka faru na majangili wote wakiwa chini ya
ulinzi, Mara ghafla faru anazinduka kutoka kwenye kuzimia
baada ya kupewa huduma ya kurejea kwa hali yake, Jaguar
anakasirika na kupiga kelele akiwa pale chini kwanini faru
amezinduka wakati kilikua ni kisasi chake.

Jaguar

"Hapanaa!,kufaa Tafadhalii kufaaa"

Watu wote walishangaa kwa maneno yale,Tembo alisogea mbele


zaidi na kupokea simu.

TEMBO
"Haloo mama"

MAMA
"Hongera mwangu mkeo amejifungua
mtoto wa kiume"

TEMBO
"Alhamdulillah, samahani mama ni
mimi tembo,faru ana kazi kidogo na
ameniachia simu yake nitampa
taarifa akitoka"

MAMA
"Sawa mwanangu Mungu awalinde na
awape kila hitajio na moyo wenu"

TEMBO
"Amin asante mama kwa Dua,Mbaki
salama" anakata simu na kusema kwa
sauti "Hongera zake majeruhi
amepata mtoto wa kiume"

Askari wote wanampa Hongera ila Tembo alisogea karibu na


Jaguar kwenda kuchuchumaa na kumuuliza

TEMBO (CONT'D)
"ulisemaje kuhusu kaka yangu"

JAGUAR
"Ningefurahi sana kama angekufa
yeye pamoja na wewe ili kisasi
changu kitimie"
28.

TEMBO
"Kisasi?"

JAGUAR
"Na baba yenu angekua hai ningemuua
kwa mikono yangu Mwenyeweee!"

SIMBA
"Huyo ni mtoto wa marehemu Mzee
FOX,alikamatwa na Baba yako miaka
kumi iliyopita kabla hamjajiunga na
jeshi,Mzee fox alifia magereza
kutokana na maradhi aliyokua nayo"

Tembo alisimama na kumtazama simba kisha akamtazama Jaguar

SIMBA (CONT'D)
"mtoto wa nyoka ni nyoka na vya
kurithi huzidi,pia sikuwahi
kufikiria Karatai mnaweza kua
wahujumu wa hifadhi yetu,ona sasa
mmeishia katika mikono ya sheria"

Karatai waliinamisha vichwa chini kwa hasira.

MWITU
"Mmenikamata kizembe
sana,Hamjanitendea haki kwa
ujangili wangu,nilipaswa kufa kwa
risasi au kuwauwa nyinyi
nyote,ikiwezekana nifungueni
tuchape mkono kiume,Maana risasi
ziliisha na mkanizunguka kizembe
kwa silaha zenu"

SIMBA
"sawa kama utakavypenda bwana
mwitu,Chui una kazi ya kufanya
hapa,Mwitu anataka mapambano ya
kiume"

CHUI
"Ndio Afande"

MWITU
"Sio Chii Tuhata mngeita jeshi zima
msingeniweza"

Chui anasimama na kuja alipoitwa wanamchukua mwitu na askari


wote wanashika silaha na kutengeneza Ulingo,Chui na Mwitu
wanajiweka sawa na kuanza kuzichapa kiume hatimaye Mwitu
anazidiwa na kuomba Msamaha,Nyumbu nae anatokea akiwa
anaugulia maumivu na kumsogelea Mwitu na Kumwambia
29.

NYUMBU
"Ukweli ni kwamba ,Naitwa Duma
niliyekua nimevaa ngozi ya Nyumbu"

Faru aliwapa Askari ishara ya Dole gumba kua kazi nzuri

26 EXT:OFISINI 26

Anaonekana Bwana,Tanzanite,Wild pamoja na Nyika ambaye ni


kijana wa bwana Wild

TANZANITE
"Nimewaita hapa kwa haraka maana
kuna dharura imetokea,vijana wetu
tuliowatuma wamekamatwa na askari
wa hifadhi na ushahidi wote
umekamilika,tupo kwenye hatari
kubwa ya kugundulika kua
tunahusiana nao"

WILD
"What about my money?"

TANZANITE
"Nipe mwezi mmoja kuna vijana
nawasiliana nao tutakupa mzigo
wako"

WILD
"No way"

Bwana Wild anaonekana kuudhika na kutaka kusimama mara ghafla


nyika anatoa bastola na kuwaambia

NYIKA
"Mpo chini ya ulinzi"

Bwana Tanzanite anajaribu kutoa bastola aliwahiwa na bwana


nyika kwa kupigwa risasi ya kifua,Mara ghafla na bwana Wild
anataka kujaribu kutoa Bastola na anawahiwa kwa kupigwa
Risasi na Bwana Nyika,Bwana nyika anatoa simu Mfukoni na
kupiga.

NYIKA (CONT'D)
"Ushahidi wote umekamilika,ila
walitaka kupigana risasi katika
kuwaweka chini ya ulinzi walijaribu
kunishambulia hivyo nikawahi na
wote wamekufa"

NYIKA (CONT'D)
"sawa Afande"
30.

27 EXT:HOSPITALI 27

Wanaonekana mke wa Faru na mama mkwe wake akiwa amemshika


mtoto

MAMA
"Hakika umeniletea mume,sura yake
imelandana sawia na mume wangu,pole
na Hongera sana Binti Yangu"

Mke anatabasamu na kusema "Asante mama"

MWISHO

You might also like