Kitini Cha Mwongozo Wa Ujasiriamali - Kozi Fupi - MWL Shadrack PM

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 29

ELIMU NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

KOZI FUPI

KITINI CHA MWONGOZO WA ELIMU NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI


TOLEO LA TATU

SHADRACK PAULO MWALUBANDA


@2023

1
KUHUSU MWANDISHI:

Bw. SHADRACK P. MWALUBANDA


Bw. Shadrack P. Mwalubanda ni mwalimu na mkufunzi wa masomo ya fani za biashara katika
masomo ya UJASIRIAMALI, UHASIBU NA UTUNZAJI FEDHA Pamoja na masomo
mtambuka. Ni msomi mwenye shahada ya biashara katika Uhasibu kutoka chuo kikuu cha Dar
es salaam, Pamoja na mafunzo ya ujasiriamali. Amekuwa akifanya kazi hii ya kufundisha
Ujasiriamali na masomo mengine ya biashara katika chuo cha Ufundi na Mafunzo VETA,
Pamoja na taasisi nyingine shiriki za kidini n.k.
Bw. Shadrack P. Mwalubanda ni mwandishi wa vitabu vingi vya fani za biashara, ameandika
pia, Kitabu cha mwongozo wa STADI ZA MAISHA (MANUAL FOR LIFE SKILLS,
Mwongozo wa Elimu na Mafunzo ya UJASIRIAMALI (ENTREPRENEURSHIP) Pamoja na
Kitabu cha mwongozo wa misingi ya UHIFADHI WA FEDHA NA UHASIBU (BASIC
BOOKKEEPING AND PRINCIPLES OF ACCOUNTING). Kitini hiki ambacho nit oleo la
TATU kimeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wadogo, vijana kwa watu wazima ili kuelewa
misingi ya Ujumla ya Kijasiriamali na kuishi vyema ili kufikia lengo. KARIBU SANA….!!!

UTANGULIZI:
Kitabu hiki cha mwongozo wa Elimu na Mafunzo ya Ujasiriamali kinatoa elimu, kanuni na
mafunzo yote muhimu ambayo ni lazima sana wajasiriamali kuyajua na kuyafanya kwa
uyakinifu ili kupata faida wanayoitamani. Kinatoa mwongozo wa nadharia za Ujasiriamali,
Elimu ya kujiajiri, namna ya kubuni mawazo ya biashara na kuyageuza fursa nzuri za biashara,
kuanzisha biashara kwa mafanikio na kufanya biashara kupitia mpango kazi wa biashara hiyo.
Hadhira kubwa inayotegemewa kupitia kitabu hiki ni wanafunzi hasa wa vyuo vya kati
ikiwemo wa mafunzo ya kozi fupi kutoka chou cha vet ana vijana shiriki kutoka taasisi
mbalimbali.
Mwongozo huu umejiegemeza sana kutoka misingi ya maelezo ya chuo cha VETA, Mwl Aliko
Mmongele, Mwl Christopher Mbagwa, Mwl Winnie Nguni (CKD) na wengine kibao.
Walimu na wakufunzi wanahimiza sana kupata kitabu hiki kama mwongozo kwa kila
mwanafunzi ili kufanya vyema katika Maisha ya kijasiriamali sasa na baadae.

2
YALIYOMO
1. Dhana ya mjasiriamali na Ujasiriamali…………………………………………..3

I. Maana, sifa binafsi za kijasiriamali


II. Uwezo wa kijasiriamali
III. Dhana ya kujiajiri na kuajiriwa,
IV. Usimamizi wa Muda
V. Uwekaji vipaumbele

2. Uanzishaji wa biashara…………………………………………………………...9

I. Maana ya biashara, Tasnia za biashara


II. Taarifa muhimu za ustawi wa biashara
III. Mawakala wanaowasaidia ukuaji wa biashara
IV. Dhana ya Wazo la biashara na Fursa ya biashara
V. UMAFUTI, Utafiti wa soko na Shughuli za masoko
VI. Kujenga mtandao, na Kutafuta MTAJI.

3. Usimamizi wa rasilimali za biashara ……………………………………………18

I. Umiliki wa biashara, Usimamizi wa Nguvu kazi


II. Usimamizi wa fedha na Mauzo
III. Kumridhisha mteja
IV. Upangaji wa Gharama na upangaji wa bei

4. Kuandaa mpango wa biashara …………………………………………………..27

I. Maana na watumiaji wa Mpango wa biashara.


II. Utaratibu wa kuandaa.

3
1.0: DHANA YA UJASIRIAMALI NA MJASIRIAMALI
UTANGULIZI
 Umuhimu wa kuwa na jamii ya Kijasiriamali.
 Tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini kumekuwa na mwamko mpya wa ujasiriamali
katika jamii. Mwamko huu unaonekana katika: -
 • Kuongezeka kwa idadi ya wajasiriamali
 • Ujasiriamali kupewa kipaumbele katika nchi (tafiti, majarida mbalimbali ya biashara,
mafunzo maalumu ya ujasiriamali, sera za nchi n.k)
 • Kukubalika kwa ujasiriamali katika jamii.
 Mwamko huu wa ujasiriamali unatokana na muonekano chanya wa tabia za
kijasiriamali. Inaaminika kuwa msingi mkuu wa ujasiriamali upo katika ubunifu.
Katika jamii ya sasa, sifa hii si tu inaendana na uendeshaji wa biashara ndogo ndogo
bali pia inamanufaa makubwa katika maisha ya mtu mwenyewe na utendaji kazi wa
jumuia (kampuni kubwa au serikali). Tabia hii mpya imekuwa muhimu katika utendaji
kazi katika dunia hii ya leo.
1.1: MAANA YA UJASIRIAMALI NA MJASIRIAMALI
Maana ya ujasiriamali
 “Ujasiriamali” ni hali au kitendo cha mtu au watu kuthubutu kuanzisha biashara au
kuboresha biashara iliyokuwepo na kusimamiaa kwa lengo la kupata faida.
Maana ya mjasiriamali
 Mjasiriamali ni mtu mwenye uwezo wa kuchunguza mazingira yake, kugundua fursa
zilizopo, kukusanya rasilimali, kuanzisha na kuendesha biashara kwa faida. - Ni mtu
ambaye ana ari, msukumo na nia ya kufanikiwa katika malengo aliyonayo.
Vipengele vya ujasiriamali
 i. Ufahamu wa mazingira uliyomo
 ii. Kunga’amua ufanye nini katika hayo mazingira ili ufaidike nayo (kutafuta fursa)
 iii. Kuainisha na kukusanya rasilimali zinazohitajika katika kufanya hiyo shughuli.
 iv. Kuanza kuifanya hiyo shughuli maandalizi yanapokuwa yamekamilika.
 v. Kuanza kunufaika na hiyo shughuli
Tabia au Sifa zitakazomfanya mjasiriamali afanikiwe
 i. Kutafuta fursa na kuzifanyia kazi ; • Unatakiwa kuzishika na kuzitumia fursa
zisizoonekana na wengine na kuanzisha biashara mpya pale unapoona pana manufaa.
 ii. Kuthubutu; Mjasiriamali anatakiwa kujaribu kufanya kazi bila woga mara tu baada
ya kupima hatari ambayo haitakiwi kuwa chini ya wastani.
 iii. Kupenda ufanisi na ubora;• Anatafuta njia zitakazomwenzesha kufanya shughuli
zake vizuri zaidi, kwa haraka zaidi na kwa urahisi zaidi lakini bila kuhatarisha ubora

4
 iv. Uvumilivu;• Anachukua hatua kukabiliana na vikwazo vinavyojitokeza bila kukata
tamaa
 v. Kutii ahadi na mikataba ya kazi; Jitahidi kuwaridhisha wateja wako na kukirimu
kwa ajili ya mafanikio ya siku zijazo kuliko kujali faida ya muda mfupi
 vi. Kutafuta taarifa ;• Mjasiriamali anatafuta habari kutoka kwa wateja na wasambazaji
wake
 vii. Kuweka malengo;• Weka malengo ya muda mrefu na mfupi ambayo yataleta
matokeo mazuri na pia yanaleta changamoto kwako.
 viii. Kupanga utaratibu na kufuatilia;• Malengo ya muda mrefu yaweke kwenye
vipengele vinavyoweza kutekelezeka na kulingana na muda uliopo
 ix. Kushawishi na kuwa na mtandao;• Tumia mikakati uliyojiwekea kuwashawishi
wengine ili kuwavuta katika bishara yako
 x. Kujitegemea na kujiamini;• Tafuta mamlaka aidha kwa kutumia sheria au kwa
kuwadhibiti wengine ili kulinda hadhi yako ya kibiashara
 NYINGINEZO: Ubunifu, uerevu, kuwa na nia, mwenye kupenda kujifunza n.k
MITAZAMO YA MSINGI KWA WAJASIRIAMALI
 Uhuru wa mawazo/Fikra
 Msukumo wa kubadilika
 kutenda
KUTAMBUA NAFASI/UWEZO WA KIJASIRIAMALI
Uwezo binafsi unaelezewa kama ni uwezo ambao mjasiriamali mmoja anaweza
kufanikiwa Zaidi ya mwingine ikiwa wanafanya kazi katika mazingira yanayofanana
na pia wanafanana hali ya mtaji n.k! Wanazuoni walifanya tathmini na kutambua
makundi matatu tu ya uwezo binafsi ya kijasiriamali.
KUNDI LA MAFANIKIO KUNDI LA MIPANGO KUNDI LA NGUVU YA
KIJASIRIAMALI
1. Kutafuta fursa 1. Kutafuta taarifa 1. Ushawishi
2. Kupima hatari 2. Kuweka 2. Mtandao
3. Uhitaji wa ufanisi na ubora mipango 3. Kujitegemea
4. Uendelevu 3. Uwekaji mzuri 4. Kujiamini
5. Kutii ahadi na mikataba ya wa mipango na
kazi/ kujitoa katika kazi kusimamia

RASILIMALI ANAZOHITAJI MJASIRIAMALI


 Fedha
 Vifaa
 Nguvu kazi
 Ujuzi

5
 Maarifa
 Muda
FAIDA NA HASARA ZA UJASIRIAMALI
FAIDA HASARA (CHANGAMOTO)
 Imeongeza uwekezaji katika teknolojia na ugunduzi  Kuchajiwa ushuru
 Kikuza uchumi kwa wajasiriamali  Ni gharama kuanza
 Hukuza masoko mapya  Ufinyu wa mazingira ya kutenda
 Kukuza umilikaji wa biashara  Ushindani
 Huongeza elimu, mafunzo na maarifa  Kutokuwa na mfumo maalumu
 Hutanua uchumi wa nchi  Huchukua muda mrefu kusimama
 Chanzo cha ajira  Mwanzo mgumu huwatesa wengi
 Husaidia kukidhi mahitaji madogo  Hatari ya kupoteza mtaji wa uwekezaji
 Kuinua hali ya Maisha kwa wajasiriamali  Kutokuwa na mwendelezo
 Tofauti za mapato
 Kukosa mshahara

1.2: DHANA YA KUJIAJIRI


 KUJIAJIRI.
 Ni ile shughuli ambayo kundi la watu (mtu) wanajitengenezea fursa za ajira kwa
kuanzisha biashara yao wenyewe. AU;
 Ni hali ambayo mtu anafanya kazi yake binafsi ili kujiingizia kipato badala ya
kumfanyia mtu mwengine ili kupewa mshahara au malipo. Kujiajiri imekuwa dhana
kubwa sana tangu dunia ilipoanza kuwa na wafanyabiashara wakubwa, kwani matajiri
wengi duniani kwa sasa ni wale ambao wamejiajiri katika makampuni yao binafsi.
SABABU, FAIDA NA HASARA ZA KUJIAJIRI
SABABU FAIDA HASARA
 Kutafuta kilinda kazi.  Kuwa huru  Masaa mengi ya kazi,
 Kutaka kutengeneza faida  Kipato kinatokana na hakuna mpangilio
binafsi. wewe mwenyewe maalumu.
 Kuwa na hadhi katika jamii.  Uongozi binafsi  Majukumu makubwa
 Kurithi biashara au utajiri.  Kujichukulia maamuzi  Kubeba hatari zote
 Changamoto za kimaisha  Kuwa mbunifu Zaidi  Kipato hakisimami
 Kutamani kuwa Tajiri  Kutengeneza kipato  Hakuna muendelezo wa
 Hakuna ajira baada ya masomo binafsi kudumu,mf; ukiumwa,
 Kujiandaa kwa ajili ya  Kupata faida nyingi kifo
kustaafu iwezekanavyo  Hakuna tegemeo la
 Kuepuka kumfanyia mtu  Kutimiza malengo. baadae
mwengine kazi  Kujiinua kiuchumi,  Ndugu na marafiki
 Kujipatia tuzo binafsi kijamii na hali ya Maisha. huchukua faida kwenye
 Kuepuka dhana ya utumwa  Kumudu gharama biashara yako.
 Kutokuwa na furaha kazini ndogondogo za maisha,.
 Kufukuzwa kazi

6
DHANA YA KUAJIRIWA (KAZI/ AJIRA YA MALIPO)
 KUAJIRIWA
Ni ile hali ya kuwa na kazi yenye kupokea malipo kutoka kwa wamiliki wa biashara hiyo.
 Hii husemwa kuwa ajira ya malipo kwani huhusisha mshahara kwa wafanyakazi.
Kampuni na biashara nyingi huajiri watu kufanya kazi kwa manufaa ya wawekezaji ili
kupata faida, kisha hugawa faida kwa ajili ya malipo, uwekezaji na wawekezaji
wenyewe.
TOFAUTI KATI YA KUJIAJIRI NA KUAJIRIWA
KUJIAJIRI KUAJIRIWA
 Wewe mwenyewe ndio mmiliki  Wewe ni mfanyakazi
 Unafanya kazi yako mwenyewe  Unafanya kazi ya mtu au kampuni Fulani
 Mapato ndio faida yako  Mapato ni mshahara wako
 Hakuna kikomo cha faida  Kuna kikomo cha mshahara
 Kazi hubadilika badilika  Kazi haibadiliki badiliki
 Mmiliki anajisimamia mwenyewe  Unasimamiwa na mmiliki
 Ni kalinda Maisha  Sio kalinda Maisha kama utafukuzwa
 Hakuna mafao baada ya kuacha kazi  Kuna mafao baada ya kustaafu kazi.

1.3: KUSIMAMIA MUDA


 Kusimamia muda ni hali ya kujali muda wako binafsi katika kazi na katika Maisha ya
kawaida kwa wafanyabiashara.
 Ili kuweza kutekeleza makubalianao ni muhimu kuelewa jinsi ya kujali na kusimamia
muda. Mara unapokuwa katika biashara, unajikuta kila siku muda hautoshi. Kwa
kuweka malengo utaweza kupanga kazi zako na kuzigawa katika zilizo muhimu sana,
zenye umuhimu wa wastani na zisiyo muhimu. Hatua itakayofuata ni usimamizi wa
muda.
 Usimamizi wa muda unasaidia kuweka kipaumbele kwa mambo yaliyo muhimu sana.
VIDOKEZO MUHIMU VYA USIMAMIZI BORA WA MUDA
 Orodhesha malengo
 Weka vipaumbele
 Tengeneza orodha ya “mambo ya kufanya kila siku”
 Anza na A’s … siyo na C’s
 Yapi ni matumizi bora ya muda wangu wakati huu?
 Shughulikia kila jambo mara moja tu
 Fanya sasa!

Umuhimu wa kuandika mpango wako wa siku


 • Mipango ambayo iko katika mawazo yako haikupi taswira ya mwelekeo wa shughuli
zako na mara nyingi hutibuliwa na mambo mengine
 • Kuandika mipango yako ya kazi za kila siku huwa ni kumbukumbu
 • Mpango ulionadikwa katika karatsi humhamasisha mtunzi kuutekeleza kwa vitendo.
Shghuli zako za kila siku sinakuwa na mfumo mahususi wa utendaji ambao
unakuwezesha kuikabili kazi iliyo mbele yako.

7
1.4: KUWEKA VIPAUMBELE
Maana ya Uwekaji Vipaumbele:
Ni kitendo cha kuchambua shughuli muhimu Zaidi kuwahi kufanyika kuliko shughuli
nyingine,
KUWEKA VIPAUMBELE Vipaumbele husaidia:
 • Kazi hufanyika katika mpangilio unaoeleweka
 • Kazi za haraka hukamilishwa kwa wakati
 • Bughudha hudhibitiwa
 • Uharaka unahakikiwa
 • Fursa mbamblimbali mbadala hubainishwa (kwa kufanya hesabu za kuzidisha)
 • Ratiba za kazi huzingatiwa
 • Mtiririko na matokeo ya kazi yanakuwa ya kuridhisha
 • Wafanyakazi wenzako, viongozi wanaridhishwa na utendaji
JIKUMBUSHE KWA MASWALI HAYA MUHIMU!!!!!
1. Eleza maana ya maneno yafuatayo:
A) Ujasiriamali
B) Kujiajiri
C) Mjasiriamali
D) Vipaumbele
E) Utunzaji Muda
2. Suala la kujua ni zipi shughuli zinazopaswa kufanyika kwanza ni jambo la msingi sana
kwa wafanyabiashara wa sasa. Eleza kwanini.
3. Kazi ya kudhibiti kazi yako kufanyika kwa wakati sahihi na uzalishaji bora ni bure
kama hakuna nidhamu ya kujali muda.
4. A) Taja rasilimali tano muhimu kwa wajasiriamali
B) Fafanua faida 5 za kujiajiri
5. ‘Dhana ya kujiajiri na kuajiriwa ni kama maji na mafuta katika ndoo moja, ni rahisi
sana kutambua baina zao. Tenganisha dhana hizo kwa hoja sita

8
2.0: UANZISHAJI WA BIASHARA
Maana ya neno “Biashara”
Biashara ni neno pana sana hapa ulimwenguni ambalo kila mtu anaweza kudhani na kutafakari
kwa aina yake, wapo wanazuoni mbalimbali waliowahi kujadili na kuhitimisha kwa maana ya
jumla. Inasemekana kuwa Biashara ni shughuli yeyote ile afanyayo mtu ambayo inauwezo wa
kumuingizia kipato,
Hivyo, BIASHARA ni shughuli yeyote ambayo mtu au kundi Fulani hufanya kwa
kubadilishana bidhaa/huduma (mazao) kwa fedha ili kujiingizia kipato. Shughuli hiyo lazima
ihusishe utoaji wa bidhaa au huduma ili kupata fedha. Mfano, Mama mmoja akifungua duka
kila siku ili kuuza bidhaa na nafaka za dukani ili kupata faida baada ya kurejesha gharama zote.
TOFAUTI KATI YA BIDHAA NA HUDUMA
Bidhaa ni vitu ama vifaa vyenye thamani ambavyo hununuliwa ili kutimiza jukumu Fulani.
Mfano, peni, mchele, msanii, n.k
Huduma ni jumla ya shughuli zote ambazo hufanywa ili kutoa bidhaa au kusaidia
ubadilishanaji wa fedha. Mfano, msanii anaweza kutoa huduma ya uimbaji ili kupata fedha.
BIDHAA HUDUMA
 Huonekana  Haionekani
 Hushikika  Haishikiki
 Huweza kuhifadhika  Haihifadhiki
 Haibadiliki badiliki  Hubadilika kutokana na mazingira
 Hufanana  Hazifanani
 Hutenganishwa  hazitenganishwi

2.1: UFAFANUAJI TASNIA NDOGO NA ZA KATI


 TASNIA
Ni kundi la watu wanaojihusisha na shughuli Fulani kijamii, kiuchumi, kisiasa au kiteknolojia
ili kujipatia manufaa yao walioyatamani.
Hivyo basi, tasnia katika biashara ni biashara ya watu waliowekeza wazo lao lenye mipango
linaloweza kufanyika kwa kuleta faida.
Muktadha mdogo: Tasnia ni mradi wa biashara unaofanyika.
AINA YA TASNIA ZA BIASHARA
1) BIASHARA YA KUPATA FAIDA
Hizi ni biashara ambazo hulenga tu kupata faida la uwekezaji.
2) BIASHARA ISIYOLENGA FAIDA
Hizi ni biasha ra ambazo hulenga kutoa huduma kwa jamii na kusaidia makundi ya wahitaji.
Mfano, Watoto yatima, wajane, Watoto wa mitaani aua makundi ya dini.
MGAWANYO WA BIASHARA: Biashara huweza kugawika katika aina za viwango
yaani ukubwa wake au udogo wake na upana.

9
AINA YA BIASHARA WAAJIRIWA MTAJI/MAUZO
Ndogo ndogo 1-4 0-Hadi milioni 5
Ndogo 5-49 5m-200m
Za kati 50-99 200m-800m
Kubwa Zaidi ya 99 Juu/Zaidi ya 800m

VIGEZO KATIKA UGAWAJI;


 Idadi ya waajiriwa au wafanyakazi
 Mtaji/ uwekezaji
 Mauzo/ hisa
BIASHARA NDOGO NDOGO-KATI
 Hizi ni biashara ambazo hufanywa kwa mtaji mdogo wa uwekezaji na eneo lake huwa
si kubwa, aghalabu uwekezaji chini ya milioni 5 katika biashara.
MFANO:
 MACHINGA
 BIASHARA ZA KIOSKI
 MADUKA YA NAFAKA
 WASUSI
 WAPISHI n.k
HATUA ZA KUTENGENEZA TASNIA YA BIASHARA
 Kugundua wazo
 Kupanga shughuli
 Kufanya hiyo shughuli
 Kumaliza shughuli hiyo kwa mafanikio
 Kupokea faida/malipo
FAIDA NA HASARA ZA BIASHARA NDOGO NDOGO – KATI.
FAIDA HASARA (CHANGAMOTO)
 Maendeleo yaliyopangiliwa  Ukosefu wa fedha
 Maendeleo yenye usawa  Ukosefu wa teknolojia sahihi
 Huchochea kukua kwa uchumi  Miundombinu dhaifu
 Kuendelea kwa usafiri na miundombinu  Ukosefu wa watenda kazi sahihi
 Maendeleo ya ugawaji maji  Ukosefu wa uongozi wa biashara
 Kukua kwa huduma za jamii; elimu, afya,  Ukosefu wa ujuzi kwa watenda kazi
mawasiliano n.k wengi
 Kupatikana kwa uduma na bidhaa kwa jamii  Ukosefu wa mwelekeo
 Chanzo cha ajira  Taarifa zisizo sahihi
 Kuondoa kutokuwa na usawa kiuchumi  Ukosefu wa masoko
 Huchochea umiliki binafsi  Hakuna ugunduzi.
 Hupunguza umasikini  Muda haufai kufanya kazi vema.

10
 Huwezesha vijana na makundi maalumu
 Kuchochea kukua kwa masoko

2.2: TAARIFA MUHIMU ZA BIASHARA


Taarifa ni jumbe, mada au Habari inayozushwa na kutokea ili kufikia maamuzi Fulani.
Taarifa hiyo inaweza kumhusu mtu au kundi au jambo Fulani.
Kwanini taarifa ni muhimu?
 Wote tunatambua kuwa taarifa zina thamani. Kama ulishawahi kununua gazeti
utalithibitisha hili. Lakini kwa nini taarifa ni muhimu na kwa nini kipande kimoja cha
taarifa kina thamani kuliko kingine?
Kuna njia tatu ambazo taarifa zinaweza kuwa na thamani kwetu
 1. Zinatuburudisha
 2. Zinatufanya tufanye maamuzi sahihi
 3. Inawasaidia watu wengine kufanya maamuzi sahihi na wanaweza kubadilisha hizi
taarifa na vitu vingine
TAARIFA MUHIMU KATIKA BIASHARA
Baadhi ya taarifa muhimu ambazo wajasiriamali huhitaji zimeorodheshwa hapa;
 A)Taarifa za kiufundi: Aina ya bidhaa/huduma utakayouza, Kuchagua tekinolojia
(upande wa uzalishaji), Mitambo na vifaa utakavyohitaji na Malighafi utazohitaji kwa
uzalishaji
 B)Taarifa za masoko: ▪ Wateja-uwezo wao wa manunuzi, Ushindani wa kibiashara,
Eneo la biashara, Wasambazaji wa bidhaa na Kupanga bei ya vitu na huduma
 C) Taarifa za fedha: ▪ Vyanzo vya mtaji wa biashara, mauzo au gharama.
 D)Taarifa za kisheria; ▪ Namna ya kupata lesseni na usajiili wa biashara yako
VYANZO VYA TAARIFA HIZI:
KIUFUNDI MASOKO FEDHA KISHERIA
 ▪ Vitabu vya  Kuchunguza masoko  ▪ Benki pamoja na  Idara maalumu
VETA (mfano wateja, taasisi zingine za za serikali au
 ▪ Vitabu vya mahali pa biashara) fedha wakala mfamo:
ufundi  ▪ Wasambazaji  ▪ Familia na BRELA
 ▪ Kuchunguza  ▪ Maktaba (vitabu, ndugu (wanaweza  ▪ Chama cha
biashara magazeti na kutoa mtaji) wafanyabiashara
zinazofanana na majarida)  ▪ Biashara zingine  ▪ SIDO na
hiyo  ▪ Chama cha katika eneo hilo, mamlaka
 ▪ Mtandao wa Wafanyabiashara na au jamii nyingine nyingine za
kompyuta Jumuia za kibiashara  ▪ Mtandao wa biashara
 ▪ SIDO  ▪ Mtandao wa kompyuta  ▪ Maktaba
kompyuta  ▪ Mtandao wa
kompyuta

11
2. 3: TAASISI ZA KUSAIDIA BIASHARA
Ni mashirika au makundi ya watu yanayotoa fedha ili kufadhili ama kudhamini biashara
nyingine ili kufikia lengo.
-Taasisi za huduma za kuendeleza Biashara ni taasisi ambazo kwa namna moja ama nyingine
hutoa huduma ambazo husaidia kuanzisha na kuendeleza tasnia/biashara. Kutokana na taasisi
kama hizo wajasiriamali hupata msaada au taarifa mbalimbali ambazo huwaongoza namna ya
kuanziasha biashara zao. Taasisi zimewekwa katika aina tofauti kutokana na aina na upekee
wa huduma maalumu ambayo husaidia biashara.
AINA YA TAASISI ZA KUSAIDIA BIASHARA
 A. Vyama vya kibiashara kama Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), chama cha
Biashara , Viwanda na kilimo Tanzania, (TPSF) , shirikisho la wenye Viwanda Tanzania
(CTI) Jumuiya ya Vibindo.
 B. Wataalam Washauri ambapo hujumuisha washauri wanaojitegemea, kampuni
binafsi na jumuiya za wanataaluma na washauri wa mambo ya biashara.
 C. Taasisi za serikali zinazohusika na utafiti, ubunifu na uendelezaji wa teknolojia ;
taasisi za elimu na mafunzo ambazo hutoa taarifa kwa umma. Mf. SIDO, BRELA,
VETA, TRIDO n.k
 D. Asasi zisizokuwa za serikali (NGOs) ambazo husaidia na kuendeleza jitihada za
sekta binafsi kiuchumi katika programu zao za maendeleo . Mf. SNV ( uholanzi )
 E. Taasis zinazotoa huduma za kifedha; Benki kama CRDB, NMB, NBC, TPB,
VICOBA, PRIDE, FINKA
MAWAKALA WANAOSAIDIA WAFANYABIASHARA

TAARIFA MUHIMU WAKALA

Taratibu za kuanzisha/kusajili biashara BRELA

Taarifa za teknolojia uakinifu SIDO

Kuunganishwa na wajasiriamali wazoefu kwa SIDO


ajili ya ushauri na mwongozo

Taarifa za taratibu za kodi TRA

Namna ya kupata fedha na ushauri kifedha Vyama vya kibiashara

Kusaidia biashara na ushauriW SIDO

12
Mafunzo na elimu VETA, CBE, ILO, AGRA

CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA TAASISI ZA KUSAIDIA BIASHARA


 Ukosefu wa mfumo halali wa mtandao kusaidia biashara
 Ukosefu wa uhusiano kwa taasisi na biashara
 Udhaifu wa taasisi husika
 Matatizo ya kuhalalisha kiserikali
 Ukosefu wa mafunzo ya rasilimali watu
 Kutokuwepo kwa sera kwa serikali na kodi
 Sera za sasa zimelenga uongozi kuliko uhalisi wa biashara

2.4: KUBUNI MAWAZO HALISI YA BIASHARA


 Kubuni wazo la biashara
Mbali na mjasiriamali, mradi mzuri ni muhimu. Unataka kuanzisha shughuli ya aina gani, ni
kwa ajiri ya kupata faida au isiyo na faida? Basi, mwanzo wa hatua za kubuni biashara ni
ukusanyaji wa mawazo ya Biashara.
Hii ni hatua muhimu sana katika uhai wa biashara inayokusudiwa kufanyika.
WAZO???
Ni maoni/dhana/hisi za mtu au kundi Fulani la watu linalokusudia kufanikisha kwa wigo
Fulani.
Wazo pia huweza semwa kama Imani au picha tu ya mtu anayefikiria kufanikiwa jambo Fulani.
WAZO LA BIASHARA
 NI mradi mzuri unaokusudia kuanzisha biashara kwa lengo la kupata faida.
 Wazo la biashara ni lazima lifikirie kwanza namna ya kufanyika kwake kwani ndio
maana ya uhalisia wa wazo hilo.
 Hugusia utoaji wa huduma au bidhaa katika utafutaji fedha na faidaWazo la biashara ni
mradi ambao mjasiriamali hutengeneza ili kutatua changamoto na kuifanya fursa ya
biashara.
 Mfano; wazo la kujenga soko huria, kutengeneza fursa ya kuhudumia watu kwa
kusafirisha bidhaa n.k
VIGEZO (VYANZO) VYA MAWAZO YA BIASHARA
 . Vyombo vya Habari mf; redio, magazeti, tv, n.k ; Kusanya mawazo kutoka vyanzo
mbalimbali kwa mfano kutoka vyombo vya habari kama Radio, magazeti, TV, kupitia
mtandao wa kompyuta,
 Familia, ndugu, jamaa na marafiki. ; Baba, mama, mjomba, Rafiki n.k

13
 Uzoefu katika kazi
 Ujuzi binafsi ulionao
 Biashara inayoshabihiana
 Matakwa binafsi/utashi wa mtu (hobbies)
 Uvumbuzi
 Maonyesho
 Utafiti
 Tafakari na malalamiko.
SIFA ZA MAWAZO MAZURI YA BIASHARA
Ni ukweli usiopingika kwamba kuwa na wazo la biashara ni suala moja na kulibadili wazo
husika kuwa biashara ni suala jingine. Hivyo basi, wazo husika liwe mahususi linajibu maswali
yafuatayo
 • Je kuna soko?-Upatikanaji wa soko
 • Je linarahisisha maisha au kutatua tatizo?-Suluhisho la changamoto
 • Je linatekezeleka ? –Ni rahisi kutekelezeka
 • Je linaweza kuleta faida? –Huleta faida
 • Je upo uwezekano wa kukua?- Kukua kwa masoko na biashara
 Kuwepo kwa ushindani?- Ushindani ni maendeleo kwa biashara
 Kuwepo kwa wateja halisi?-upatikanaji wa wateja muhimu.
2.5: KUBAINISHA FURSA ZA BIASHARA
 Maana ya fursa ya biashara
 Fursa ya biashara inafafanuliwa kama ni kuvutia uwekezaji au mapendekezo yanayotoa
uwezekano wa marejesho mara baada ya mtu kuthubutu kufanya biashara. -FURSA YA
BIASHARA: Ni wazo zuri la biashara linalovutia uwekezaji na lenye uwezo wa
kurejesha faida katika biashara.
SIFA ZA FURSA NZURI YA BIASHARA
 1. Kuwepo kwa mahitaji halisi, yaani kuitikia utashi ambao haujahudumiwa au mahitaji
ya wateja ambao wanauwezo wa kununua na ambao ni chaguo lao
 2. Rejeshao la uwekezaji, kupata faida au rejesho ambalo ni imara, kwa wakati husika
na lililoendelevu kutokana na uthubutiu na juhudi inayohitajika.
 3. Yenye ushindani, yaani nafasi sawa au bora zaidi katika muonekano kwa mteja kuliko
mwengine..
 4. Upatikanaji wa Rasilimali, na umahili, yaani ndani ya uwezo wa mjasiliamali katika
rasilimali, umahili, vigezo vya kisheria,nk.
 Zifikie malengo yaani zifikie malengo na maono au mtu au taasisi inayofanya uthubutu.

14
TOFAUTI KATI YA FURSA NA WAZO LA BIASHARA

WAZO FURSA

Ni mradi na dhana inayoweza tengeneza Ni dhana iliyothibitika kuleta mapato endelevu


fedha

Ni zao la ugunduzi, ujuzi na maarifa Ni zao la uwekezaji

Ni mradi unaoweza kufanyika bila Ni mradi unaofanyika kwa mafanikio


mafanikio

??? ???

2.6: TATHMINI KATIKA BIASHARA


 Ni makadirio ya upimaji wa kiwango cha biashara katika utendaji kazi hadi inapofikia
gawanyo la faida.
 AINA ZA TATHMINI:
 1. Tathmini za kimsingi
 2. Tathmini za hali
 3. Tathmini za kisawa-sawa
 4. Tathmini mchanganyiko

2.6.1: UCHAMBUZI WA UMAFUTI


 UMAFUTI ni kifupi cha maneno ya UWEZO, MAPUNGUFU, FURSA na TISHIO.
 TISHIO huitwa VIKWAZO kwa wakati mwingine, hufanya huo mfumo kuwa
UMAFUVI.
UMAFUTI ni mfumo wa kimkakati unaowekwa na uongozi wa biashara ili kukagua maeneo
yote yanayoweza kuiathiri biashara nje na ndani.
SABABU ZA UCHAMBUZI WA UMAFUTI

SABABU ZA NDANI YA BIASHARA SABABU ZA NJE YA BIASHARA


-Ndani ya udhibiti wa -Nje ya udhibiti wa biashara ya
mjasiriamali/mfanyabiashara mjasiriamali

UWEZO FURSA

15
MAPUNGUFU TISHIO

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHAMBUZI WA UMAFUTI


 Njanja za kifedha
 Rasirimali vitu
 Uongozi na usimamizi
 Soko
 Taarifa za uongozi
 Mazingira
 Upatikanaji wa malighafi.
2.7: UTAFITI WA SOKO
 MAANA YA SOKO; Soko ni watu walio mahali au eneo fulani, wenye mahitaji ambao
wako tayari kununua na wanao uwezo wa kununua bidhaa au huduma wanazohitaji.
Kila biashara inauza bidhaa/huduma kwa wateja. Wateja tunaweza kuwaelezea kama
watu:
 ➢ Wenye kuhitaji bidhaa/huduma

 ➢ Wenye uwezo wa kununua, na

 ➢ Wenye utashi wa kununua bidhaa au huduma.


Katika kutekeleza dhana ya utafiti soko, biashara ndogo lazima:
 a) Iyatambue mahitaji ya wateja (utafiti wa soko)
 b) Itathmini namna ya kushinda ushindani (mkakati wa soko)
 c) Ichague soko maalum la kuhudumia (kulenga soko)
KUTAMBUA WATEJA WAKUBWA (POTENTIAL CUSTOMERS)
Mambo gani mjasiriamali ayafahamu kuhusu wateja?
a) Awafahamu wateja wake. (Who are my customers?)
b) Kufahamu wateja wanachohitaji: (What do they require ?) Kwa kuligawa soko katika
makundi, ni rahisi kuyafahamu mahitaji ya bidhaa/huduma ya kila kundi.
c) Kufahamu wateja wana nunua wapi: (Where do they buy ?) Wajasiriamali wanapaswa
kufahamu ni wapi wateja wanapata mahitaji yao hivi sasa.
d) Kufahamu wakati gani wateja wananunua: (When do they buy ?) Kwa kujua wakati
ambao wateja wana nunua (kila siku, kwa wiki, kwa mwezi, kwa msimu ),
wajasiriamali wataweza kutambua mambo kama;
e) Kufahamu wateja wanavyonunua (taslim/mkopo): ( How do they buy ?) Kwa kufahamu
namna wateja wanavyolipia bidhaa/huduma kwa taslim au mkopo, itamsaidia
mjasiriamali katika kupanga sera za mikopo na bei.

16
2.8: UCHAMBUZI WA MASOKO
Je,Masoko ni nini?
Masoko ni shughuli yoyote afanyayo mjasiriamali kuanzia uzalishaji wa bidhaa hadi mtumiaji
anapotumia bidhaa hiyo zenye lengo la kuongeza mauzo kwenye Biashara yake.
MJUMUISHO WA VIPENGELE VYA MASOKO
Kumbuka kwamba kitu muhimu katika biashara ni kuuza bidhaa/huduma, hivyo mteja ni mtu
muhimu sana katika biashara! Kwa hiyo ikiwa mjasiriamali anapenda wateja kununua
bidhaa/huduma anayotoa ni lazima kutekeleza yafuataya:
 Kuwa na bidhaa/huduma sahihi (BIDHAA)
 Kuuza bei nzuri kwa pande zote (BEI)
 Kuwepo eneo sahihi (BANDA)
 Kutumia njia inayokubalika kutangaza (BANGO)
2.9: KUJENGA MTANDAO
 Mjasiriamali anapofanya biashara anategemea sana mtandao alionao kufanikisha
biashara zake hasa kumwezesha kupata wateja wa bishara zake. Kadili mitandao yao
inavyokuwa mikubwa, ndivyo wanavyokuwa na fursa Kubwa katika kufanikiwa.
 Mjasiriamali anatakiwa kufanya kazi kwa umakini sana kuelekea kujenga (kuimarisha)
mitandao yao binafsi. Tafsiri ya Mtandao (usiyorasmi). Tafiti mbalimbali kuhusu maana
ya neno mtandao zinaonyesha kutofautiana.Kuna tafsiri za aina nyingi.

2.10: UBAINISHAJI VYANZO VYA MTAJI


MAANA YA MTAJI: Ni jumla ya fedha na vitu vyote vya thamani vinavyotumika
katika kuanzishia biashara.
 Kwa mjasiriamali, mtaji ni mali kwani huwa kianzilishi chake cha kipato ambacho ni
thamani ku wa kwake ili kuendeleza na kukuza biashara. Hivyo basi, ni muhimu na si
budi kutunza na kuheshimu mtaji,,,mtaji unatakiwa kukua na sio kupungua kadiri siku
za biashara zinavyozidi kusonga mbele.
 Mtaji huweza kuwa fedha, huweza kuwa mali ambazo ni lazima kwa biashara hiyo, pia
huweza kuwa rasilimali ambzo ni watu, mazingira, wafanyakazi n.k
VYANZO VYA MTAJI
 i. Akiba binafsi (Kujihifadhia) Kutumia fedha zako mwenyewe ni rahisi na ya usalama
zaidi.
 ii. Familia, Ndugu na Marafiki. Hawa wanaweza kukusaidia iwapo unaonyesha dhamira
ya mafanikio, kwani kufanikiwa kwako ni kufanikiwa kwao vile vile.
 iii. Mchezo (upatu) Huu ni mpango wa kikundi cha watu wanaochangiana fedha katika
muda wa kipindi fulani, mtu mmoja mmoja hadi wote watakapopata.
 iv. Kujiunga na vyama vya akiba na mikopo vinavyotambuliwa kisheria ambapo
mwanachama hukopeshwa mara mbili (au zaidi) ya akiba yake chamani. ( Mfano;
SACCOS, VICOBA n.k)

17
 v. Taasisi au mashirika ya fedha yanayofanya biashara ya kukopesha fedha (Mfano PRIDE,
FINCA, FAIDIKA n.k.)
 vi. Wakala wa serikali aliyeteuliwa kuwakopesha wajasiriamali kwa kupewa fedha za
Serikali (Mfano; Mfuko wa raisi – PTF).
 vii. Benki za biashara. Lakini mjasiriamali unatakiwa kuwa makini sana na mikopo ya
benki kwa kuelewa vizuri masharti yake kabla ya kusaini mikataba ya mikopo
MATUMIZI MAKUU YA MTAJI WA BIASHARA
 Fedha taslimu au kianzishio cha biashara
 Kununua vifaa
 Kulipa mishahara
 Kodi
 Soko
 N.k
JIKUMBUSHE KWA MASWALI HAYA MUHIMU!!!!!
1. Ibrahim Bacca amekuwa fundi wa magari kiasi kwamba hajui kabisa maana ya
UMAFUTI, anahitaji kujua vitu vya msingi vinavyounda UMAFUTI, hasara na faida
zake. Unaweza kumsaidia?
2. Mawazo ya biashara, mara chache hutokea yakiwa yamejitenga na mtu kuokota, kwa
kawaida huambatana na vigezo ambavyo ndivyo vyanzo vya mawazo hayo. Jadili.
3. Ni ukweli usiopingika kwamba kuwa na wazo la biashara ni suala moja na kulibadili
wazo husika kuwa biashara ni suala jingine. Hivyo basi, wazo husika liwe mahususi ni
lazima kukidhi vigezo vya fursa. Taja sifa tano za fursa za biashara.
4. ‘’Kumbuka kwamba kitu muhimu katika biashara ni kuuza bidhaa/huduma, hivyo
mteja ni mtu muhimu sana katika biashara!’’Alisema Bw.Matagiri. Kwa hiyo ikiwa
mjasiriamali anapenda wateja kununua bidhaa/huduma anayotoa ni lazima kutekeleza
mambo muhimu katika soko. Fafanua msomo huo kwa hoja NNE.
5. Wote tunatambua kuwa taarifa zina thamani, lakini si taarifa zote zina thamani kwa
wajasiriamali. Fafanua taarifa muhimu kwa biashara.

3.0: USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA


BIASHARA
 Biashara ni shughuli yoyote afanyayo mtu au kundi la watu katika kampuni ili kupata
faida.
 Biashara huweza kuwa na umiliki wa aina tofauti tofauti.
 Hivyo, Biashara huweza kuwa na aina mbalimbali za chimbuko:
 1. Kuanzisha mwenyewe
 2. Kununua biashara iliyokuwepo

18
 3. Ufadhili
3.1: AINA ZA UMILIKI WA BIASHARA
 Umiliki pekee (binafsi) (Mmoja)
 Ushirikiano
 Shirika/ Kampuni
1. UMILIKI PEKEE (MMOJA)
Huu ni umiliki wa biashara ambapo mtu mmoja anawekeza mtaji wake, ujuzi, maarifa na nguvu
kazi binafsi katika kusimamia biashara. Mfano; duka la nyumbani, n.k
2. USHIRIKIANO
Hii ni aina ya umiliki wa biashara ambapo watu au makundi mawili na Zaidi huungana
kutengeneza biashara yao kwa lengo la kupata faida, faida yao hugawanywa kutokana na zao
la uwekezaji.
Mfano: A + B = AB CO.
3. SHIRIKA/KAMPUNI
Hii ni ain aya umiliki wa biashara ambayo huwa na kikomo cha madeni ya uwekezaji. Biashara
huwa na utofauti wa umiliki kwa watenda kazi wake, huweza kuwa ya kutengeneza faida au
kwa ajili ya jamii.
KAMPUNI; Hii ni biashara inayomilikiwa kwa uwekezaji mkubwa wa hisa za watu
mbalimbali, huanzishwa na kuendelezwa kwa sheria za nchi husika.

FAIDA NA HASARA ZA UMILIKI WA BIASHARA


AINA FAIDA HASARA

- Gharama ni ndogo kuanza - Deni halina kikomo


UMILIKI PEKEE - Kodi ndogo - Ukosefu wa mwendelezo
- Udhibiti wa moja kwa moja - Ugumu wa kukuza mtaji
- Mtaji mdogo unahitajika - Kuwajibika kwa maamuzi
yote
- Faida za ushuru
- Mmiliki hupata faida yote

19
USHIRIKIANO - Rahisi kuanzisha - Deni halina kikomo
- Gharama ndogo kuanza - Hakuna mwendelezo
- Mtaji huongezeka - Mamlaka ya pamoja
- Uongozi wa kushirikiana. - Ugumu wa kuongeza mtaji
- Uwezekano wa faida za kodi - Ugumu kupata washirika
wazuri.

SHIRIKA - Kikomo cha deni - Inasimamiwa kwa karibu


- Ugawaji wa uongozi - Ni gharama kuanza
- Kuhama kwa uongozi - vizuizi
- Uwepo endelevu - Utunzaji kumbukumbu ni
mgumu
- Shirika halali
- Kuchajiwa mara mbili kodi
- Kodi zinazowezekana
- Hukuza mtaji kirahisi

Faida yote huwa ya Huwa na ushirikiano Kikomo cha deni


mwanzilishi

UMILIKI PEKEE USHIRIKIANO SHIRIKA


Mtaji mdogo Hakuna kikomo cha Tofauti ya wamiliki na watenda kazi
deni

Mtu mmoja au kundi moja Hugawana faida kwa Huweza kuwa ya kutaka faida
humiliki asilimia za uwekezaji

Haina mwendelezo wa kudumu Ushirika si chini ya Huweza kuwa ya kuhudumia jamii tu


wawili na si juu ya 20

Huchukua eneo dogo Hugawana hasara au Huwa na hisa na wamiliki


hatari kutokana na
asilimia

Hupata hasara yote Hufanya maamuzi kwa Kugawana faida kutokana na uwekezaji
ruhusa ya wote wa hisa

20
Hakuna sheria nyingi Mmoja akifa au Ni kubwa, hulindwa na serikali
kuchizika huvunja
ushirika

 3.2: USIMAMIZI WA WAFANYAKAZI/NGUVUKAZI (MENEJIMENTI YA


WAFANYAKAZI)
Ni kitendo cha kudhibiti na kuhakikisha wafanyakazi wanatumia ujuzi wao kufanya kazi kwa
manufaa ya ofisi kwa wakati sahihi wawapo kazini.
 Huhusisha staili nzuri za uongozi,
 kuhamasisha timu yako,
 kuunda mpango kwa watu,
 njia za kuweka mazingira safi kazini,
 kutunza nidhamu ya watu na afya zao
 MENEJA
Ni watu wanaosimamia biashara ya kampuni kufanya shughuli zote za biashara kusonga mbele.
 Meneja ni mtu anayehusika na usimamizi na udhibiti wa waajiriwa wote kufanya kazi
kwa ufanisi ili kuendeleza kampuni.
 Hufanya shughuli zote za kampuni kwenda kama ilivyopangwa.
 Hufanya: Kutoa mafunzo, Kugawa majukumu, Kuhamasisha, Kutoa mwelekeo, Kutoa
malengo, Kutoa malipo na kushauri wengine na Kuunganisha wengine n.k
KANUNI ZA KUSIMAMIA WAFANYAKAZI
 1; KUSUDI LA HISIA ZA KAWAIDA; Sababu ya wafanyakazi kuwepo kazini ni
majukumu yao ya kawaida ili kutimiza matakwa ya kazi.
 2; MAWAZO MAZURI NA MAADILI; Mfano; uaminifu, upendo, ucheshi, heshima
na utii.
 3; SERA NA SHERIA NZURI; Hujumuisha tabia nzuri zilizokubaliwa katika kazi.
 4; MASHARTI YA WAZI KWA WAFANYAKAZI
 5; TUMAINI
 6; UWAZI
 7; MALENGO YA WAZI YANAYOPANGWA NA KAMPUNI
UMUHIMU WA KUSIMAMIA WAFANYAKAZI
 1. Kupelekea wafanyakazi kujituma na kufanya kazi kwa ufanisi
 2. Hukuza mawasiliano mazuri kwa wafanyakazi
 3. Hutoa tumaini kwa shirika, kampuni n.k
 4. Hutengeneza mazingira ya kuhamasisha wafanyakazi

21
 5. hupelekea ukweli na uhalisi wa wafanyakazi wawapo kazini
 6. husaidia wafanyakazi kufikia malengo yao kazini
 7. huleta matokeo
3.3: UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU KATIKA BIASHARA
MAANA YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU:
Ni kitendo cha kuhifadhi, kujali na kuweka taarifa zote za maandishi katika vitabu muhimu
vya biashara.
AU; Ni kitendo cha kuandikisha taarifa za biashara kwenye vitabu vya kampuni.
AINA ZA UTUNZAJI KUMBUKUMBU:
1. Kumbukumbu za kifedha
2. Kumbukumbu zisizo za kifedha
A) UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZISIZO ZA KIFEDHA.
 Ni utunzaji wa kumbukumbu zisizohusiana na fedha kabisa, yaani zinahusika na
kuendesha biashara lakini si kutokana na fedha. Mfano, bidhaa, majina ya waajiriwa,
rushwa n.k

MIFUMO (MUUNDO) WA KUTUNZA KUMBUKUMBU


 1. KUKUMBUKA KUTOKA KICHWANI
Watu walikuwa wakiweka kumbukumbu kichwani na kuzitumia taarifa ili kuendesha biashara,
hii ilikuwa kabla ya maendeleo ya kisasa.
 2. KUMBUKUMBU ZA MAANDISHI
Kumbukumbu ziliwekwa katika vitabu ili kufanya maboresho ya biashara kirahisi.
UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU
 Husaidia kujua muondoko wa biashara
 Huleta muelekeo wa biashara
 Husaidia kujua miamala yote katika biashara
 Huleta marejeleo ya biashara
 Husaidia kujua bidhaa zipi hutoka kutokana na mahitaji
VIFAA VYA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZISIZO ZA KIFEDHA
 Vifaa tofauti tofauti hutumika kutunz akumbukumbu zisizo za kifedha kutokana na aina
yenyewe ya taarifa hiyo inayotunzwa.
 Mfano; mafaili, vitabu, kadi za kumbukumbu, karatasi za utangulizi n,k
B) UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA KIFEDHA
Kumbukumbu za kifedha ni taarifa zinazohusiana na fedha tu au rasilimali fedha.

22
Kuna aina nyingi zaa vitabu zinatumika kuwekea kumbukumbu, hujulikana kama vitabu vya
ziada. Hutofautiana kati ya biashara moja na nyingine. Hata hivyo kuna baadhi ya vitabu
ambavyo hutumika katika biashara zote.
Kabla ya kuchagua aina ya kitabu unachotaka kutumia, unapaswa kutafuta taarifa unazohitaji
kwa ajili ya kuendesha biashara. Kumbukumbu utakazo andaa lazima ziendane na uendeshaji
wa biashara yako.
USIMAMIZI WA FEDHA
 i) Usichanganye fedha za biashara na za binafsi !
 (ii) Jilipe ujira (mshahara) kutokana na biashara yako. Wewe mwenyewe uwe
mwajiriwa katika biashara yako.
 (iii) Tofautisha fedha zinazotokana na mauzo toka kwenye: fedha za mtaji,akiba na
nguvukazi.
 (iv) Tunza kitabu cha fedha taslimu na andika fedha yote inayoingia na kutoka katika
biashara.
 (v) Tumia fedha iliyotokana na mauzo kwa madhumuni yaliyokusudiwa na kupangwa
VITABU VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBU
 Vitabu vifuatavyo vinaweza kuwa muhimu kwa ajili ya kuandikia taarifa za biashara
yako:
 • Kitabu cha oda
 • Kitabu cha manunuzi
 • Kitabu cha mauzo
 • Kitabu cha fedha taslimu
 • Kitabu cha wadaiwa
 • Kitabu cha wanaokudai
3.4: USIMAMIZI WA MAUZO
Mauzo ni neno linaloakisi muamala baina ya pande mbili yaani muuzaji na mnunuzi ambapo
mnunuzi anapokea bidhaa/huduma wakati muuzaji anapokea fedha (dhamana y mauzo) wakati
wa mabadilishano.
 Pia, hujulikana kama makubaliano ya pande mbili ambapo bidhaa au huduma
hubadilishwa kwa kiasi cha malipo ya kutoa bidhaa/ huduma hiyo.
 Mfano; A; Nahitaji kununua chupa mbili za maji
B; Karibu, chupa moja ni tsh 500
C; Sawa, chukua 1,000, nipe maji.
MBINU/UJUZI UNAOTAKIWA WAKATI WA KUFANYA MAUZO
 Kujiamini
 Kuwa msikivu

23
 Kushawishi
 Kutengeneza mahusiano mazuri
 Hamasa binafsi
 Mtulivu
 Kuwa tayari
HATUA ZA KUZINGATIWA WAKATI WA KUFANYA MAUZO
 1.UTAYARI/UANGALIFU
Ni lazima wauzaji kuwa waangalifu na kuwa tayari wakati wanataka kufanya mauzo,
ni hatua ya kwanza: Mf. Kusalimiana au kushikana mikono
 2. KUTAMANI KUFANYA MAUZO (HAMU)
Muuzaji anatakiwa kutengeneza hamu kwa mteja kutamani bidhaa yake.
 3. KUDHIBITI VIKWAZO
Wakati mwingine mteja huwa na vikwazo kabla ya kununua bidhaa, hivyo, muuzaji
hutakiwa kuwa na macho ya kuona na kudhibiti hilo.
 4. KUTENDA (KUFUNGA MAUZO)
Baada ya kudhibiti kila kitu, muuzaji anabadilishana na mteja wake bidhaa au huduma
kwa fedha kama namna ya mabadilishano.
SIFA MUHIMU KWA WAUZAJI WENYE MAFANIKIO
 Kuwa na mtazamo chanya
 Muonekano chanya (utanashati)
 Kujiamini
 Kuwa msikivu
 Kushawishi
 Kutengeneza mahusiano mazuri
 Hamasa binafsi
 Mtulivu
 Kuwa tayari
3.5: KUMRIDHISHA MTEJA
Mteja ni mtumiaji wa mwisho wa bidhaa/huduma/mazao.
-Kwa maana nyingine, ni mtu au shirika linalonunua bidhaa au huduma kutoka kwa mtu au
shirika jingine.
 Hivyo mteja inabidi aangaliwe kama ndiye uhai wa biashara. Maana ya kumridhisha
mteja Mteja anakuwa ameridhika ikiwa mahitaji, matakwa na matarajio yake
yamekidhiwa.

24
MAKUNDI YA WATEJA
1) Wateja wa ndani: Hawa ni wateja ambao hufanya kazi Pamoja na muuzaji wa
bidhaa/huduma. Ni wafanyakazi wenzi pia!
2) Wateja wa nje: Hawa ni wateja ambao hutokea nje ya sehemu unayofanyia kazi au
kampuni yako.
Umuhimu wa kumridhisha mteja;
 Wateja wanaporidhika inakuwa rahisi hata kulipa bei ya juu zaidi na hivyo kuleta
faida zaidi.
 Wateja wanaporidhika husambaza sifa nzuri za biashara na hivyo kuleta wateja
wapya.
 Wateja wa zamani hurudi tena
 Kuongezeka kwa wateja huongeza mauzo na faida pia
 Wateja wakiongezeka huongeza ari ya mfanyabiashara na wafanyakazi, na hivyo
kuboresha utendaji wao wa kazi.
 Biashara inaweza kuongeza uhai na kushamiri kwa muda mrefu.
3.6: KUPANGA GHARAMA ZA BIDHAA AU HUDUMA
 Kuendesha biashara ndogo kunahitaji kufahamu namna ya kukokotoa gharama na
kupanga bei. Unataka kukokotoa gharama zipi? Utajuaje gharama ya ama kila bidhaa
au huduma? Mbinu zipi zinatumika katika kupanga bei ya kuuzia? Maswali yote hayo
yatashughulikwa katika moduli ya pili.
Maana ya gharama
Gharama ni fedha unayotoa ili kuzalisha/kutengeneza bidhaa/huduma au ni jumla ya fedha
unazotumia katika kuendesha biashara.
Kupanga gharama maana yake ni nini?
 Kupanga gharama ni kukokotoa kiasi ulichotumia katika kutengeneza/kuzalisha bidhaa
au huduma ya kuuza.
Aina ya gharama: Katika biashara kuna aina mbili za gharama:
 Gharama za moja kwa moja
 Gharama zisizo za moja kwa moja.
1. Gharama za moja kwa moja; Gharama za moja kwa moja ni gharama ambazo
zinahusika moja kwa moja katika uzalishaji wa bidhaa au kutoa huduma. Mfano,
gharama za malighafi, na nguvukazi.
2. Gharama zisizo za moja kwa moja; Gharama zisizo za moja kwa moja ni zile
gharama nyinginezo zinazohusu uendeshaji wa biashara na ambazo hazihusiani moja
kwa moja na utengenezaji wa bidhaa au kutoa huduma. Mfano wa gharama zisizo za
moja kwa moja ni: • Gharama ya pango ( nyumba/frame), Kupungua thamani kwa
vifaa, nyumba, mashine, Kukarabati vifaa mashine, Maji na umeme

3.7: KUPANGA BEI ZA BIDHAA AU HUDUMA


KUPANGA BEI; Maana ya Bei ▪ Ni kiasi cha mwisho cha malipo unachotarajia kupata
kutokana na kuuza bidhaa yako baada ya kuongeza faida katika gharama za uzalishaji.
 ▪ Ni Kile ambacho unahitaji wanunuzi walipe kwa ajili ya bidhaa yako unayouza.

25
Maana ya Kupanga bei: ▪ Namna unavyotafuta kiasi gani wateja walipe ili wanunue bidhaa
yako au ▪ Namna unavyoamua kuhusu bei ambayo utawatoza kwa ajili ya bidhaa yako.
Kwanini unapaswa kupanga bei ya bidhaa zako? Yakubidi upange bei ya bidhaa zako ili uweze
kufahamu endapo unatengeneza faida au hasara kwenye biashara yako.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUPANGA BEI
 Gharama ulizotumia
 Faida unayoitaka
 Bei za washindani wako
 Bei ambazo wateja wako tayari.
NJIA ZA UPANGAJI BEI
 1. Njia ya ongezeko la gharama (Cost-plus) Sehemu au asilimia ambayo unaongeza
kwenye gharama za uzalishaji wa bidhaa/ huduma ili kupata bei ya kuuzia huitwa
kiwango cha faida (profit mark up).
Wajasiriamali wengi huchukua 10 – 50% kama kiwango chao cha faida lakini pia hutegemea
hali ya soko. Bei iliyofanyiwa hesabu ni ile ambayo mjasiriamali anataka kuuza bidhaa yake
au huduma. Lakini vile vile inawezekana siyo bei atakayofanikiwa kuuza! Hii inatagemea hali
ya soko.
 2. Njia ya ulinganisho (Comparative method) Njia hii, unalinganisha bidhaa/
huduma yako na soko, kwa kutegemea ubora wake na gharama za uzalishaji, unaweza
kuweka bei rahisi, bei kubwa zaidi au ikalingana na ile ya washindani wako.
 3. Njia ya nini soko linaweza kulipa Njia hii inatagemea dhana ya uwingi na uhitaji
wa bidhaa hiyo kwenye soko.
Kwa mfano, iwapo bidhaa haipatikani kwenye soko, basi bei ya bidhaa hiyo inaweza kuwa ya
juu kuliko ile iliyokadiriwa na nyongeza ya thamani
JIKUMBUSHE KWA MASWALI HAYA MUHIMU!!!!!
1. Toa maana ya maneno haya;
A) Bei
B) Gharama
C) Mteja
D) Mauzo
E) Kumbukumbu za fedha na zisizo za kifedha
2. Eleza faida sita za kutunza kumbukumbu
3. “Ni kweli kwamba, si kila mtu ni muuzaji kwani, Maisha ya muuzaji katika soko ni
Maisha yake binafsi”. Thibitisha msemo huo kwa hoja sita.
4. Kwanini tunapaswa kuwaridhisha wateja wetu?
5. Kwa kinagaubaga eleza, namna yua kuwasimamia wafanyakazi katika biashara.

26
4.0: KUANDAA MPANGO (MCHANGANUO) WA
BIASHARA
Ukiwa na wazo zuri la biashara, hatua inayofuata ni kuandika wazo la biashara.
 Mpango wa biashara ni nini? Mpango wa biashara ni: Ni waraka/maelezo ya kina
uliotayarishwa na mtu/watu wanatarajia kuanziaha biashara au ambaye tayari yupo
kwenye biashara.
Maelezo haya huweka bayana biashara husika na mipango yake kwa kipindi maalum (k.m
mwaka mmoja hadi mitano). Kwa maneno mengine Mpango wa biashara ni kiongozi cha
mjasiriamali katika kuendesha biashara.
NI NINI MATUMIZI YA MPANGO WA BIASHARA?
Mpango wa biashara una matumizi makuu mawili. Inatumika (kwa ajili ya biashara yenyewe)
ndani ya biashara au nje ya biashara. yenyewe.
a) Ndani ya biashara Hapa ni pale ambapo mpango hutumika kama kiongozi katika biashara
ili kumsaidia mwenye biashara kuona namna biashara itakavyoanza au inavyoendelea na pia
kuweza kuona matatizo/vikwazo au fursa. Hapa hutumiwa na menejimenti tu Pamoja na bodi
ya wakurugenzi.
b) Nje ya biashara; Wakati Mpango wa biashara unapotumika kupata mkopo kutoka kwenye
vyombo vya fedha (mpango huo huitwa ni nje ya biashara. Mfano; Benki, Serikali, Wadau,
Mikopo, Watafiti, Wateja, Wasambazaji n.k
NAMNA YA KUTAYARISHA MPANGO WA BIASHARA
Kama utaanzisha biashara mpango wako uahitaji kuonyesha yafuatayo:
1. Maelezo kuhusu asili ya biashara husika.
Maelezo hayo ni pamoja na: - Jina la biashara inayokusudiwa kuanzishwa
 - Aina ya bidhaa/huduma unayotka kuzalisha/kutoa k.m kutengeneza viti na vitanda
 - Tarehe unayokusudia kuanza biashara hiyo k.m tarehe 1 Septemba,2006
 - Jina lako ukiwa ni mmiliki wa biashara hiyo k.m Mohamed na Juma
 - Uzoefu wako katika kuendesha biashara k.m uzoefu wa miaka 2 kama fundi seremala.
2. Mahali/eneo la biashara
Mahali au sehemu utakapofanyia biashara.
3. Bidhaa/huduma
Elezea aina ya bidhaa/huduma biashara yako itahusika na nini.
4. Mpango wa masoko
Inakubidi kufanya utafiti wa soko kwa kujiuliza mwenyewe maswali yafuatayo:
 - Una uhakika wa kuwepo watu watakaohitaji kununua kutoka kwako

27
 - Ni kwanini wanunue kutoka kwako? Je, ni kwa kuwa bidhaa/huduma ni rahisi zaidi
au haipatikani katika eneo husika au ni bora zaidi?
 - Utawafahamishaje watu/wanunuzi kuhusu bidhaa/huduma yako? Utaweka
matangazo/bango sokoni/mahala pa kuuzia au utawatembelea watu majumbani mwao
na kuwaelezea kuhusu/bidhaa/huduma yako? - Utauzaje? Utauza moja kwa moja kwa
walaji au utawauzia wateja wa jumla?
 - Washindani wako watakuwa ni akina nani na bidhaa/huduma zao ni za aina 35ain na
bei zao zikoje n.k?
5. Mpango wa uzalishaji
Hapa unatatakiwa kuonyeha wazi kwamba unafahamu mchakato mzima wa uzalishaji wa
bidhaa/utoaji wa huduma.
6. Uratibu na usimamizi
 Hapa unahitajika kuonyesha ni wasaidizi wangapi watahitajika katika kuendesha
biashara.
 Unaweza kuanza mwenyewe lakini kadiri muda unavyokwenda na biashara kukua
utahitaji watu wa kukusaidia.
 Ni vema pia kuweka makisio ya kiasi cha kujilipa na utakaowaajiri.
7. Ugavi / wasambazaji Hapa unatakiwa kuonyesha :
 - Wapi utapata malighafi / bidhaa
 - Utahitaji kiasi gani.
 - itagharimu kiasi gani.
8. Mashine na vifaa Hapa utatakiwa kuonyesha:
 Vifaa utakavyotumia,
 Mahitaji ya kiwanda (kama jengo, banda n.k)
 Utakakopata vifaa/mashine na gharama yake.
9. Uwekezaji na mpango wa fedha
Hapa utatakiwa kutoa mhutasari wa kiasi cha fedha za kuanzia biashara utakakozipata.
 - Kiasi cha fedha unazohitaji (= uwekezaji) na matumizi yake (k.m kununulia
vifaa/mashine, jengo, malighafi)
 - Kiasi gani cha fedha zako utawekeza katika biashara
10. Mtiririko wa fedha
 Jambo la mwisho ni kutayarisha mtirirko wa fedha/ mapato halisi. Hili utatakiwa
kuonyeha katika kipindi k.m mwaka mmoja: - Kiasi cha fedha unachotarajia kupata
kutokana na mauzo kwa kipindi cha mwezi moja
UMUHIMU WA MPANGO WA BIASHARA:
 Huwa ramani katika Maisha ya biashara
 Hutumika kufanya maamuzi

28
 Huongoza shirika ili kufikia lengo
 Huleta matokeo kirahisi na mrejesho wake
 Hutumika kama kumbukumbu
 Huleta faida kwa wawekezaji
 Hukuza mahusiano baina ya biashara na wadau wake. N.k

JIKUMBUSHE KWA MASWALI HAYA MUHIMU!!!!!


1. Toa maana ya Mpango wa biashara, kisha eleza matumizi yake kwa kina.
2. Elezea wadau wanaoweza kuhusika na mpango wa biashara yako.
3. Jadili faida za kuandaa mpango wa biashara
4. “Kuandaa mpango ama mchangamanuo wa biashara si jambo dogo hata kidogo, na
wala si lelemama, ila linahitaji taratibu Madhubuti ili iwe fanisi”. Onesha taratibu hizo
kwa mpangilio.
5. Toa tofauti kati ya matumizi ya ndani ya biashara dhidi ya nje.

MWISHO WA MWONGOZO WA MADA KATIKA ELIMU NA MAFUNZO YA


UJASIRIAMALI
IMEANDALIWA NA MWL SHADRACK PAULO MWALUBANDA
BCOM ACC-UDSM (HONS), EET (C), HGK (EXC)
0656158658
Shadrackmwalubanda@gmail.com

29

You might also like