Professional Documents
Culture Documents
Vicoba E-Book
Vicoba E-Book
Nikusihi uisome e-book hii mwanzo hadi mwisho na ukiweza uisome tena
na tena maana utakapokuwa umeimaliza basi utakuwa umeshakuwa
mtaalamu wa mfumo wa vicoba,ambaye hakuna mtu yeyote ambaye
atakudanganya chochote kuhusu mfumo wa vicoba.
karibu
YALIYOMO
5.MIKOPO NA UKOPESHAJI
DHAMIRA YA TAASISI
Kuwa na vikundi bora vya VICOBA ENDELEVU, Vitakavyokuwa na wanachama wenye
maisha bora na ya furaha.
MALENGO YA TAASISI
1. Kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi kwenye shughuli za uzalishaji
mali na shughuli mbalimbali za maendeleo.
2. Kuwawezesha wanavicoba wote kiuchumi ili kuongeza uwezo wao wa kipato kwa
kupitia ujasiriamali na vipaji walivyonavyo.
3. Kuhamasisha na kutoa elimu ya Vicoba endelevu.
4. Kuwawezesha wananchi kupambana na tatizo la changamoto za ajira ili wajiajiri
KAZI ZA TAASISI
1. Kutoa mafunzo ya kujitambua, ujasiriamali na fedha
2. Kuhamasisha, Kuanzisha, kufundisha na kuvisimimamia vikundi vya vicoba
endelevu
3. Kutafuta fursa mbalimbali kutoka kwa wadau binafsi na serikali na kuzipeleka kwa
wanavikundi
4. Kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa wanavicoba katika shughuli za
maendeleo
5. Kuandaa na kuendesha semina na mafunzo mbalimbali kwa wanavikundi ili
kufungua fikra zao za mafanikio
6. Kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea kwenye vikundi
facebook@Yemco Tanzania
Twitter@ YEMCO TANZANIA
Linkedin@ YEMCO TANZANIA
Website: www.yemcotanzania.com
MUONGOZO WA MFUMO WA VICOBA
Watu wengi wamekuwa wanasikia tu kuhusu mfumo wa vicoba lakini hawafahamu kwa undani
juu ya mfumo wa vicoba kupitia ukurasa huu sekunde chache zijazo utakwenda kujifunza kwa
undani juu ya mfumo wa vicoba
VICOBA NI NINI?
VICOBA
Hiki ni kifupi cha maneno Village Community Bank
VICOBA ni benki za kijamii, ambazo zinamilikiwa na wanajamii wenyewe wakiwa kama wabia
na pia wakiwa kama wateja wanaopata huduma kupitia benki hizo. Kwa sera ya huduma ndogo
za fedha ya mwaka 2018 vikundi vya vicoba vimepewa jina la COMMUNITY
MICROFINANCE GROUP
mfumo huu unaundwa na kikundi cha Kuanzia watu 15-50 wenye malengo ya kuwezeshana
kiuchumi, mfumo huu huwawezesha wananchi kujiunga katika kikundi na kuanzisha mfuko wa
kuweka akiba na baadae kuweza kukopeshana kwaajili ya kuanzisha biashara, kuendeleza
biashara au kuanzisha miradi ya kuwaingizia kipato na kutatua matatizo ya dharura
yanayowakabili wananchi husika ya kila siku. mfano magonjwa,vifo,ada za shule,kodi za
pango,shere n.k.
Ndani ya kikundi cha watu 50 watu hawa wanaweza kuwa wanatoka sehemu moja au wanatoka
sehemu mbalimbali lakini wanakuwa na sehem moja ambayo hukutana kila wiki,na wale ambao
ni wafanyakazi au wanafunzi watakuwa wanakutana kila mwezi mara moja kwasababu ya
majukumu yao na kwa watu ambao wanajiunga kwenye kikundi husika lakini wapo mbali na
kikundi kama mkoani au nje za nchi basi wao watakuwa wanahudhuria mara moja kwa mwezi
na wale wan je ya nchi wanahudhuria mara moja kwa mwaka au wanapopata nafasi ya kurudi
nchini kwao,lakini watakuwa wananunua tu hisa zao kwenye kikundi kila wiki.Kwahiyo kama
wewe leo ukijiunga kwenye kikundi cha vicoba utaunganishwa kwenye kikundi ambacho kiko
tayari na utaanza rasmi kufahamiana na wanachama wenzako.Na kama unajiunga na vicoba
lakini uko nje ya nchi au mkoani ukishasajiliwa kama mwanachama utaungwa kwenye grupu la
watsap la wanachama wenzako ili kufahamiana nao na kuanza taratibu za kununua hisa.
Ndani ya kikundi cha watu 15-50 hutengenezwa vikundi vidogovidogo vya watu watano watano
kwaajili ya kudhaminiana wakati wa kuchukuwa mikopo. Vikundi hivi vidogovidogo
huchaguliwa kwa watu wanaofahamiana ambao wanakuwa wameletana kwenye kikundi au
kiongozi wa kikundi ambaye ni mwenyekiti atawapanga tu kwenye makundi yao bila kujali
kufahamiana kwao.Na kama kikundi wanachama wakizidi 50 basi kikundi kimoja cha vicoba
kinaweza kutengeneza vikundi vingine ndani yake na kuvipa majina sawa na kikundi cha
kwanza lakini kwa kuvitenganisha kwa namba au herufi.Kwa mfano MALEZI DAIMA
VICOBA “A”,MALEZI DAIMA VICOBA “B” na kuendelea
Mfumo wa vicoba rasmi umeingia Tanzania mwaka 2002 kutokea India ambako ndio uliasisiwa
na mtu mmoja anaitwa Mohamed Yunus.Baada ya kuona matokeo makubwa ya mfumo wa
vicoba India ndipo ukaingia Tanzania kwaajili ya kuokoa Maisha ya watu masikini sana.
Unapojiunga kwenye kikundi cha YEMCO VICOBA tarajia kupata faida zifuatazo
q Kujengewa uwezo na desturi ya Kujiwekea akiba.Kuweka akiba sio tabia za watu
wengi ndio maana watu wengi wanabakia masikini hivyo unapojiunga na YEMCO
VICOBA tunakujengea tabia ya kuweka akiba kwasababu kuweka akiba kwetu ni jambo
la lazima na usipoweka akiba utatozwa faini hivyo huo ulazima unakuweka wewe
kwenye nafasi ya kujenga tabia ya kuweka akiba tabia ambayo itakupelekea kuwa
Tajiri.Kwahiyo hata ukiwa na malengo yako ni rahisi kuyatimiza lakini pia hata ukipata
dharula au changamoto yeyote ni rahisi sana kuitatua.
q Kupata fursa ya mafunzo,ukijiunga na yemco vicoba utapata mafunzo ya
kujitambua,mafunzo ya ujasiriamali na fedha.Kwahiyo hautakuwa tena na changamoto
ya kukuza biashara yako au kwa wale ambao hawana biashara hautakuwa tena na tatizo
la kukosa biashara
q Kupata mikopo kwa urahisi,ukijiunga na yemco vicoba utapata faida ya kupata mikopo
kwa urahisi Zaidi na isiyokuwa na riba.Yemco vicoba tunatoa mikopo kwa wajasiriamali
na wafanyabiashara ya kuanzisha biashara na kuendeleza biashara lakini pia mikopo ya
dharula.Kwahiyo hautakuwa tena na tatizo la kukuza biashara zako na kufikia malengo
yako.
q Kupata fursa za kukutana na watu mbalimbali katika vicoba,serikalini na wadau
binafsi.yemco itakukutanisha na watu ambao ulikuwa hujawahi kukutan anao kwenye
Maisha yako ambao wengine watakusaidia kutimiza ndoto zako na wengine watakuwa
wateja wako
q Kutimiza malengo yako kwa urahisi, yemco inakusaidia kutimiza malengo yako ambayo
ulikuwa siku nyingi unatamani kuyatimiza.
MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWA MFUMO WA YEMCO
VICOBA
I. KUWAJENGEA UWEZO NA DESTURI YA KUWEKA AKIBA WANANCHI
Mfumo wa YEMCO VICOBA umeanzishwa maalumu kwaajili yakuwajengea watu wapenda
maendeleo desturi na tabia ya kujiwekea akiba.ambapo kila mwanachama ambaye atajiunga
kwenye kikundi cha YEMCO VICOBA atatakiwa kuweka akiba kila wiki.Kwa wafanyakazi
ambao wanataka kuweka akiba kwa mwezi watatakiwa kuweka mwisho wa mwezi lakini
wataweka akiba zao za mwezi mzima.pia hata kwa ambao sio wafanyakazi lakini watataka
kununua akiba zao kwa mwezi wanaruhusiwa lakini utaratibu ni kuwa unanunua hisa za mwezi
ujao na sio mwezi uliopita.Katika mfumo wa YEMCO VICOBA Tunajiwekea akiba katika
maeneo yafuatayo.
(A) MFUKO WA HISA
HISA NI NINI?
Hisa ni akiba ambazo kila mwanachama atakuwa anajiwekea kwenye kikundi kwaajili ya
maendeleo yake binafsi, ambapo hisa hizi mwanachama atakuwa anajiwekea kwaajili ya
kuanzisha biashara, kuendeleza biashara, kujenga au kuboresha makazi au kununua magari
Mwanachama atakuwa anaruhusiwa kununua kuanzia hisa moja mpaka kadri ya uwezo wake
kulingana na malengo yake na ndoto zake mwenyewe kwa kila wiki ambayo mwanachama
anajiwekea akiba. Katika mfumo wa YEMCO VICOBA ununuaji wa hisa utakuwa kwa viwango
tofauti tofauti kulingana na kila mwanachama.Ambapo utaratibu wa kununua hisa Upo kama
ifuatavyo
4.Hisa nyingi ni dhamana kwa mikopo midogo midogo,ukiwa nah isa nyingi
inakusaidia unapokopa mkopo mkubwa zinakuwa kama dhamana ya mkopo wako.Mfano
unahisa za milioni moja unataka mkopo wa laki tis abasi hisa zako ndio dhamana yako.
Jamii ni akiba ambazo mwanachama anaweka kwenye kikundi kwaajili ya kumsaidia kwenye
mambo ya dharula ambayo yanaweza kumkuta mwanachama akiwa hana pesa.Mfano
Kuuguwa,kuuguza,kifo,ada ya shule ya watoto,kodi n.k.Kila mwanachama ataweka jamii kila
wiki Pamoja na hisa kulingana na uwezo wake.Kwenye uwekaji wa hisa kule juu tumeweka
madaraja ya uwekaji wa hisa lakini kwenye jamii hakuna madaraja kwahiyo jamii yenyewe kima
cha chini kwa wiki ni Tsh 2000/= Tu ambapo mwanachama anaweza kununua jamii kwa wingi
ambao anaweza kununua.Kwenye uwekaji wa akiba jamii na hisa mtu anaweza kununua sawa
lakini hawezi kununua jamii nyingi kuliko hisa.Kwahiyo sasa kama wewe ni mwanachama wa
daraja la 10000 kwa wiki la hisa na jamii shilingi 2000 kima cha chini utakuwa unanunua hisa na
jamii tsh 12000/=.Unaweza kununua kwa kiwango kikubwa uwezavyo.
q Mfuko wa jamii pia ni mali ya mwanachama na anastahili kurejeshewa pindi atakapojitoa
kwenye kikundi kwa utaratibu maalum,mfuko wa jamii kama mtu anajitoa kwenye
kikundi basi atachanga kwenye hisa zake na kukatwa 10% kama kawaida kama atakuwa
amejitoa katikati yam waka na zitakazobakia basi atarudishiwa kama kawaida.
q Mwanachama atakaefariki na jamii zake pia atapewa mrithi wake kama alikuwa ahana
deni la mkopo wa jamii.Kama atakuwa na deni basi atakatwa deni lake kwanza kisha
ndio atarejeshewa jamii zake
q Jamii hizi kila inapofika mwisho wa mwaka huwa tunarudishiana kama mtu hadaiwi deni
lolote.zinaonganishwa na faida za mwanachama husika
MIKOPO NA UKOPESHAJI
Kwenye mfumo wa YEMCO VICOBA tuna mikopo ifuatayo
A.MIKOPO YA NDANI YA KIKUNDI
Hii ni mikopo ambayo mwanachama atakuwa anakopa kwa kulingana na akiba zake ambazo
yeye anakuwa ameziweka kwenye kikundi,mikopo hii huanza kutolewa kwa mwanachama baada
yakuwa ametimiza miezi mitatu kwenye kikundi.ambapo katika sehemu hii ya mikopo tuna
mikopo miwili ambayo ni
1. MKOPO WA HISA
2. MKOPO WA JAMII
Kwenye kikundi cha yemco kuna mikopo ya nje ya kikundi,mikopo hii hutolewa kutoka makao makuu ya
taasisi ya YEMCO,mikopo hii ni mikopo ambayo wanachama watakuwa wanakopa bila kuangalia hisa
zao au jamii zao,mikopo hii huanza kukopeshwa kwa kikundi ambacho kinakuwa kimetimiza mwaka
mmoja wa kusimamiwa na taasisi ya YEMCO.Mikopo hii huwa na masharti mbalimbali kulingana na
aina ya mkopo ambapo kikundi kikishatimiza miezi sita sasa kitaanza kuelekezwa aina ya mikopo ya nje
na taratibu zake kama kikundi kinakuwa ndio kimeanza wanachama watatakiwa kusubiri mpaka
watakapoelekezwa kuhusu mikopo ya nje baada ya miezi sita ya kuanzishwa kwa kikundi husika.
MIKOPO YA HISA
v Mikopo ya hisa ni mikopo ambayo hutolewa ndani ya kikundi kutoka kwenye hisa
za mwanachama ambapo mwanachama anaanza kukopa kuanzia mara moja ya
hisa zake mpaka mara tatu ya hisa za mwanachama.lengo la mkopo huu nikuanzisha
biashara,kuendeleza biashara au kufanyia mradi wa maendeleo kwa
wanachama.Mwanachama anapokopa mkopo wa hisa ni lazima atambue kuwa hayo ndio
maeneo ambayo atatakiwa kupeleka mkopo huo na sio maeneo mengine.Mkopo wa hisa
umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni zifuatazo
i. MKOPO WA UWEZESHWAJI.
Mkopo huu ni mkopo ambao mwanachama atakopa kutoka kwenye hisa zake kwa madhumuni
yaleyale ya mkopo wa hisa lakini mwanachama atakopeshwa pesa taslimu kutoka kwenye
kikundi,ambapo kama mwanachama atapewa pesa taslimu basi atarejesha kiasi hicho hicho cha
pesa bila kuongeza kiasi chochote cha fedha.Kiasi alichokopa ndio atakachorejesha,isipokuwa
atalipa Bima tu ya mkopo ya 2% ya mkopo wake ambapo bima zote zinalipwa makao makuu ya
Taasisi ya YEMCO na mwanachama akifa na mkopo basi taasisi italipa deni lililobakia la mkopo
husika kwenye kikundi.Kikomo cha mkopo huu ni Tsh 400,000/= Tu
Mkopo huu ni mkopo ambao mwanachama atakopa kwenye hisa zake kwa utaratibu ule ule wa
mkopo wa hisa lakini mkopo huu mwanachama anakuwa anakopa Zaidi ya 400,000/= ambapo
mwanachama anakuwa anataka mkopo wa kuanzia 500,000/= na kuendelea,mkopo huu sasa
mwanachama hatapewa fedha cash atalipiwa vifaa ambavyo yeye anataka au vitu ambavyo yeye
anataka kukopa,yeye mwanachama atatafuta hivyo vifaa atakubaliana bei na muuzaji halafu
kikundi kitamlipia yeye atakopeshwa vifaa na kikundi.Kwa mfano Mwanachama AMINA
anataka mkopo wa milioni moja,lengo la mkopo ni kwenye kununua madera kwasababu ndio
biashara ambayo anafanya amina.Hivyo amina ataomba mkopo kwenye kikundi wa milioni moja
kisha amina atatafuta duka ambalo anaenda kununua hayo madela kikundi kitamlipa muuzaji na
amina atachukuwa madera,mkopo huu amina akikopeshwa atarejesha na faida ya 10% hiyo ni
faida ya kikundi ambayo kikundi kitagawana mwisho wa mwaka.Endapo mkopaji akiwa
anakopa lakini ananunua bidhaa kutoka kwa wauzaji wengi atajaza fomu ya uwakala ambapo
mwanachama atafanya kazi yakwenda kununua bidhaa hizo kwa niaba ya kikundi.Hapa kikundi
kitampatia fedha AMINA na atakwenda kununua bidhaa,akishanunua atapeleka vithubitisho vya
kununua bidhaa zake kwenye kikundi husika.
TARATIBU ZA MAREJESHO YA MKOPO WA HISA
Mwanachama ambaye anakopa mkopo wa hisa atarejesha kama ifuatavyo
v Mwanachama atapewa mwezi mmoja bila kufanya marejesho na mwezi unaofata
lazima aanze kufanya marejesho.hii huwa inaitwa grace period.Mwanachama akikopa
atakaa mwezi mmoja halafu mwezi wa pili ndio ataanza kurejesha kwa tarehe ile ile
ambayo yeye atakuwa amekopa kwa mfano mwanachama amekopa tar 1/2/2023 ataanza
kurejesha tar 1/4/2023 huo mwezi mmoja anapewa kwaajili ya kukusanya
marejesho,ambapo utaratibu wa kisheria wa marejesho utakuwa kwa mwezi kwa tarehe
ambayo aliombea mkopo,ijapokuwa mwanachama anaweza kurejesha kwa wiki kama
yeye atakuwa anataka kurejesha hivyo.Mwanachama anapokopa marejesho yake
yatagawanywa kulingana na mkopo wake ijapokuwa anapokopa kama anakopa mkopo
wa maendeleo atakatwa kabisa 10% ya faida ya mkopo wake halafu kitakachobakia ndio
atapewa,kwa mfano mwanachama akikopa 1,000,000/= laki moja ya faida itakatwa
kabisa atapatiwa laki tisa halafu marejesho yake yatakuwa ya milioni moja tu.kwahiyo
itachukuliwa hiyo milioni moja na itagawanywa kwa muda wa mkopo wake ambao yeye
anataka kurejesha litaandikwa rejesho lake rasmi.
v Mikopo ya hisa hutolewa kwa miezi mitatu,sita au mwaka,mwanachama ambaye
anakopa laki nne kushuka chini atarejesha kwa miezi mitatu,mwanachama ambaye
atakopa laki sita kushuka chini atarejesha ndani ya miezi sit ana mwanachama ambaye
atakopa mkopo wa kuanzia laki sab ana kuendelea atarejesha ndani yam waka mmoja.
v Mkopo wa hisa unabima ya mkopo ya 2% ambayo na yenyewe hulipwa kabla
mwanachama hajapewa mkopo.Bima hii ya mkopo humsaidia mwanachama atakapokufa
au atakapopata ulemavu wa kudumu.mkopo utalipwa na bima yake na bimah ii hulipwa
moja kwa moja makao makuu ya YEMCO.
v Kila mkopaji atatakiwa kujaza fomu ya mkopo ambayo itasainiwa na wadhamini wake
wanne,ili kama atashindwa kulipa hisa za wadhamini zitakatwa atakapomalizia mkopo
wake.Mwachama ambaye anakopa mkopo wa hisa kuna fomu ya maombi ya mkopo
lazima ajaze ambapo fomu hiyo itakuwa na taarifa zake,taarifa za biashara yake na taarifa
za wadhamini wa mwanacama ambapo wadhamini wanne wanatoka kwenye kikundi na
mdhamini mmoja anatoka nje ya kikundi,ambapo anaweza kuwa mume au mke wa
mwanachama au ndugu wa karibu.
MFANO WA TARATIBU ZA MAREJESHO YA MIKOPO KULINGANA NA MUDA WA
MKOPO
MIKOPO YA JAMII
Kabla hujaomba mkopo lazima uwe umeshafanya mahesabu yako vizuri na ukajua kabisa kiasi
halisi ambacho unahitaji,usiombe mkopo ukiwa hujui kiasi halisi cha mkopo ambao
unahitaji.kwa mfano mtu anakuwa anahitaji laki tano lakini kwasababu anahisa nyingi anaomba
mkopo mkubwa hivyo mwanachama anapaswa kujua kiasi halisi cha mkopo ambacho
anahitaji.Na uhitaji uendane na kitu anachokwenda kufanya.Pamoja na hayo mwanachama
anatakiwa kuangalia hisa zake kwanza zinamruhusu kukopa kiwango hiko ambacho yeye
anakitaka?
2) JUWA NAMNA UTAKAVYO UREJESHA MKOPO WAKO
Kabla hujachukuwa mkopo kaa chini ujue kabisa namna ambavyo utarejesha mkopo wako na
kama umekopa kwaajilii ya kuanzisha biashara lazima ujiulize kuwa kwa mfano hii biashara
ikifa nitatoa wapi marejesho ya mkopo,mwachama ajiridhishe atakavyorejesha kabla ya kukopa
kuepusha usumbufu kwenye marejesho
3) KUPELEKA MKOPO SEHEMU AMBAPO UMEOMBEA MKOPO WAKO
Wapo watu huwa wanadanganya sana kwenye vikundi mtu anakwambia nataka mkopo kwaajili
ya biashara lakini sio kweli kwamba anapeleka kwenye biashara wengine huwa wanapeleka
kwenye mambo yao.Ukiomba mkopokwaajili ya biashara peleka kwenye biashara ili usisumbuke
4) FAHAMU KAMA UNATAKA MKOPO WA KUANZISHA BIASHARA AU WA
KUENDELEZA BIASHARA
Kama unataka kuchukuwa mkopo kwaajili ya kuanzisha biashara ni bora kukopa mkopo kidogo
ili usipate shida kurejesha.
5) CHUNGUZA KAMA NI WAKATI SAHIHI WA WEWE KUCHUKUWA MKOPO
Katika vikundi vya vicoba wapo watu huwa wanachukua mikopo kwasababu wamewaona watu
wengine wanachukuwa mikopo,sasa kila mwanachama anapaswa kufahamu kuwa lazima ajue
kama ni wakati sahihi yeye kukopa kama muda bado bora usikope tu.
6) KUWA NA NIDHAMU YA FEDHA
Hakika hili ni jambo la kuzingatia sana unapokuwa umechukuwa mkopo kwenye kikundi cha
vicoba endelevu kama unamatumizi mabaya ya fedha nakushauri kwanza jifunze kuyapunguza
kisha ndio uanze kufikiria kukopa,kwasababu kama huna nidhamu ya fedha halfu ukachukuwa
mkopo lazima utautumia ndivyo sivyo na mwisho wa siku ni majuto ndio yatafatia.Nidhamu ya
fedha nikutumia pesa inapopaswa kutumia hata kama unauwezo wa kutumia ambapo hakupaswi
kutumika,kwa mfano unaweza kabisa kunywea pombe pesa ya mkopo lakini kwasababu
unanidhamu ya pesa unajizuia,kwahiyo lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu sana kabla ya
kuchukuwa mkopo kwasababu pesa inavishawishi sana.
Mwanachama anapaswa kuhakikisha fomu yake ya mkopo imejazwa kwa ufasaha kabla ya
kuwasilishwa kwenye kikao cha kikundi kwaajili ya kusoma fomu yake,endapo fomu ya mkopo
itakuwa na kipengele ambacho hakijajazwa ipasavyo basi mwanachama hatapatiwa mkopo
mpaka kipengele husika kiwe kimejazwa vzr.
B. KUJIRIDHISHA KWA BIASHARA HUSIKA AMBAYO INAPELEKEWA HUO MKOPO
Mwanachama akiomba mkopo wa kufanya jambo Fulani kikundi kitafanya uchunguzi wa kina
kujirisha juu ya biashara ambayo mwanachama anaombea mkopo na kiwango cha mkopo
ambacho mwanachama anaomba,kama sio biashara basi kitu chochote ambacho mwanachama
anaombea mkopo haswa kwenye mikopo ya hisa lazima kikundi kujiridhisha juu ya pesa na
mahali pesa zinapopelekwa.ikiwa biashara inayofanywa ni kidogo kulingana na mkopo ambao
anoomba mkopo utapunguzwa.kwa mfano mwanachama anaomba mkopo wa milioni moja lakini
biashara inahitaji laki sab abasi mkopo utakaopitishwa ni laki saba tu.
C. KUWA NA WADHAMINI WA MKOPO
Kila mwanachama anapotaka mkopo atapaswa kuhakikisha wadhamini wa mkopo wake wamejaza fomu
vizuri.kwenye kila mkopo kutakuwa na wadhamini wanne wa ndani ya kikundi na mdhamini mmoja wan
je ya kikundi.
Moja ya walengwa wa MFUMO WA vicoba NI watu ambao wanatafuta mafanikio Kwa kupitia
uwezeshwaji wa mikopo isiyokuwa na riba na isiyokuwa na masharti mengi.Hawa ni walengwa wa
MFUMO WA VICOBA kupitia taasisi yetu ya YEMCO.Tukubali tusikubali mikopo ni njia pekee
ambayo inaweza kutusaidia katika kuinuka KIUCHUMI lakini BAADHI ya makampuni yanaturudisha
nyuma sana wajasiriamali lakini VICOBA NDIO MKOMBOZI wetu kwasasa..
4.WAFANYABIASHARA AMBAO WANATAFUTA MASOKO
5.WATU AMBAO WANATAFUTA KUWEKA PESA YAO MAHALI AMBAPO ITAZAA FAIDA
Watu ambao wanatafuta mahali Ambapo wakiweka akiba zao watapata faida ni walengwa wa MFUMO
WA vicoba.Kuna watu WANATAMANI kuweka fedha zao mahali Ambapo mwisho wa mwaka watapata
faida basi hao ni walengwa wa vicoba
NB.Kikundi kinaweza kuwa na mwenyekiti msaidizi na yeye anakuwa na sifa kama hizo
hizo.huyu yeye anakuwa anamsaidia mwenyekiti pia anapokuwa hayupo.
2 WAJIBUWAKATIBU
Katibu wa kikundi anawajibu ufuatao
• Kusimamia utekelezaji wote wa kikundi,kwa lugha nyepesi katibu ndio mtendaji mkuu
wa kikundi hatakiwi kukosa kwenye kikundi maana yeye ndio anaweka kumbukumbu za
kila kinachojadiliwa kwenye kikundi.
• Kutunza kumbukumbu zote za kikundi na kuandika mihutasari ya kikundi.
• Kumsaidia mwenyekiti kuongoza vikao vya kikundi.
• Kumsaidia mweka hazina katika shughuli za fedha .
• Kuwaita wanachama kwa namba wakati wa kuita mahudhurio
Na kuweka hisa na mfuko wa jamii.
• Kutoa na kupokea taarifa mbalimbali za mwakikundi kwa mwenyekiti
SIFA ZA KATIBU
I. PASS BOOK ,hiki ni kitabu cha mwanachama cha kuwekea kumbukumbu zake zote za
ada,kiingilio,hisa,jamii na mikopo,kitabu hiki mwanacha hupatiwa anapojiunga anaweza
kuwa anaenda nacho kwake lakini ili kuepusha kupoteza huwa vitabu vyote hubakia
kwenye begi
II. REJA YA KIKUNDI,hiki ni kitabu kikuu cha kutunzia kumbukumbu za kikundi za
fedha za kikundi kizima na hujazwa na muweka hazina wa kikundi
III. KATIBA
IV. RIPOTI YA MWAKA,kitabu hiki ni kwaajili ya kuandika riporti ya mwaka
V. FOMU YA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA VICOBA,hii ni fomu ambayo inakuwa
na taarifa za mwanakikundi za kutosha na mwanakikundi lazima ajaze yeye mwenyewe
halafu arudishe kwenye kikundi
VI. FOMU YA MAOMBI YA MKOPO WA MWANAKIKUNDI CHA VICOBA
VII. TAARIFA ZA KIKUNDI CHA VICOBA,kitabu hiki hujazwa taarifa za kila siku za
kikundi
VIII. FOMU YA MAREJESHO YA MKOPO
IX. KITABU CHA WAGENI,kama kikundi kinapata mgeni basi atasaini humu
X. REGISTA YA MAHUDHURIO,hiki kitabu kwaajili ya kuandika mahudhurio ya
wanachama ya kila siku
N:B,Pesa zote za kikundi ni lazima ziwekwe benki,hii ni kwa usalama wa kikundi husika
kuepusha upotevu wa pesa lakini wizi wa pesa,lakini pia ni msada wa kikundi kuweza
kukopesheka benki kwa kuangalia miamala yao,maswala ya upotevu wa pesa yamekuwa
makubwa sana kwa vikundi ambavyo vinaweka pesa zao majumbani.Kama hamtaweka benki
basi fedha ziwekwe kwenye m-koba usikubali kujiunga kwenye kikundi ambacho wanaweka
pesa nyumbani kwa mtu.
3. MCHANGO WA KONGAMANO:
Kila mwaka taasisi hufanya kongamano kubwa la kitaifa na kila mwanachama lazima
kuchangia Tsh 10000/= kwaajili ya kongamano,mchango huu huwa haujalishi kama
mwanachama atashiriki au hatashiriki kwenye kongamano hilo lakini kuchangia ni
lazima.Mwanachama anaweza kupoteza sifa za kuwa mwanachama kama akigoma
kuchangia michango hiyo.
Kama tulivyojifunza hapo juu kuwa vikundi vya vicoba endelevu huwa hisa zinaendelea lakini
jamii na faida wanarudishiwa wanachama kwaajili ya kufanya mambo yao,hivyo hapa
tutajifunza kwa pamoja namna ambavyo tutaweza kugawana faida mwisho wa mwaka,katika
safu hii utaweza kujifunza jinsi ya kugawana faida ili uweze kujua ukiwa kwenye kikundi jinsi
ya kukagawana faida.
UNAPOTAKA KUGAWANA FAIDA MWISHO WA MWAKA FATA HATUA ZIFUATAZO
1. Unachukuwa hisa zoote za wanachama halafu unagawanya kwa shilingi 2000 hii ni
thamani ya hisa moja,baada ya kugawanya hapa utapata idadi ya hisa zote kwenye
kikundi.
3. Ukishapata thamani ya hisa moja sasa unakuja kwenye hii hatua ya mwisho ambayo sasa
unaanza kuchukuwa kitabu cha kila mwanachama,unaangalia idadi ya hisa za kila
mwanachama unazidisha na thamani ya hisa moja ambayo uliiipata.Hapa unapata faida
ambayo kila mwanachama anatakiwa kuipata.
MFANO WA KUGAWANA FAIDA ZA KIKUNDI CHA YEMCO VICOBA GROUP
Yemco Vicoba group ni kikundi cha watu 30 wanajumla ya hisa za shilingi million 15 kwa
mwaka.kwahiyo hatua ya kwanza utachukuwa million 15 utagawanya kwa sh 2000 ambapo
utapata idadi ya hisa zitakuwa 7500.Kwa maana kuwa sasa kwa mwaka mzima yemco vicoba
group wameweka hisa 7500.
Hatua ya pili unajumlisha jumla ya faida zote walizopata yemco vicoba group ili ugawanye kwa
idadi ya hisa,sasa kwa mfano kwa mwaka mzima yemco vicoba group wamepata faida ya Tsh
750000/= kwaiyo unachukuwa 750000/= unagawanya na idadi ya hisa ambazo ni 7500 unapata
thamani ya hisa ambayo ni Tsh 100/=,hivyo basi faida ya hisa moja ya yemco vicoba group ni
Tsh 100/=
Hatua ya tatu sasa unaanza kuchukuwa kitabu cha kila mtu mmoja unaangalia idadi ya hisa za
kila mwanachama,sasa kwasababu vitabu vitakuwa vimejazwa pesa taslim unachukuwa ile pesa
taslim unagawanya kwa 2000 unapata idadi ya hisa ya kila mwanachama halafu unazidisha na
faida ambayo ni 100 unapata faida ambayo anatakiwa kupata mwanachama.Mfano Juma pesa
zake zote za hisa ni Tsh 2000000 unachukuwa hiyo pesa unagawanya kwa tsh 2000 unapata
idadi ya hisa 1000 kwaiyo Juma anaidadi ya hisa ya 1000 ukizidisha na faida ya tsh 100 unapata
faida ya juma ambayo ni Tsh 100000/= kwaiyo Juma atapata faida ya Tsh 100000/= kama faida
ya mwaka.
HITIMISHO
Napenda nikupongeze kwa kuweza kujipatia maarifa
haya,ambayo kama utayasoma kwa umakini kabisa kuna
uwezekano mkubwa ukawa umeelewa vizuri kuhusu mfumo
wa vicoba na sasa unaweza kuwa mwalimu mzuri kwa
wengine kuhusu mfumo huu,katika kuhitimisha kitabu hiki
nakusihi ukayafanyie kazi yote ambayo umejifunza katika
kitabu hiki yakawe sehemu ya maisha yako,yakabadilishe
maisha yako lakini pia yakabadilishe maisha ya watu
wengine ambao wanakuzunguuka.
1. Ramani ya Maisha
2. Kanuni 26 za mafanikio
3. Maisha na vyakula jinsi vinavyotuuwa taratibu
4. Umasikini wa waislamu na suluhu zake
5. Siri zilizojificha katika biashara ya mtandao
6. Ujue mfumo wa vicoba vya kiislamu
Vitabu hivi vyote unaweza kuvipata kwa njia ya softy copy kwa kuwasiliana na
mimi kwa simu namba 0715448643
Kuhusu Mwandishi
Amekuwa akiwasaidia watu wengi kutimiza ndoto zao na malengo yao kwa kutumia mfumo wa
YEMCO VICOBA ENDELEVU.
VICOBA ENDELEVU ni msingi utakaokupeleka katika mafanikio makubwa bila kuwa na msongo
wa mawazo.