Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

14 JANUARI 2024

DOMINIKA YA PILI
KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA
MWAKA B

SOMO LA KWANZA 1 Samueli 3:3b-10, 19


Somo katika kitabu cha kwanza cha Samueli.
Siku zile: Samueli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, pale
lilipokuwapo sanduku la Bwana. Bwana akaita: “Samueli, Samueli,” naye
akaitikia, “Mimi hapa!” Naye akamwendea Eli kwa haraka akasema,
“Mimi hapa, kwa kuwa uliniita." Eli akasema, "Sikukuita, nenda ukalale.”
Akaenda kulala. Bwana akaita tena: “Samueli, Samueli!” Naye akam-
wendea tena Eli, na kusema, “Mimi hapa, kwa maana uliniita!” Naye
akajibu, akasema, “Sikukuita mwanangu, nenda ukalale.” Wakati ule
Samueli alikuwa bado hajamfahamu Bwana, na neno la Bwana lilikuwa
bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita tena Samueli mara ya tatu.
Hapo aliamka na kumwendea Eli akasema, “Mimi hapa, kwa maana
uliniita.” Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita kijana.
Akamwambia Samueli, “Nenda ukalale na utakapoitwa, utasema, ‘Nena
Bwana kwa kuwa mtumishi wako anasikia.’” Basi akaenda tena kulala
mahali pake.
Bwana akaja, akasimama, na kuita kama awali: “Samueli, Samueli!” Ndipo
Samueli akaitikia, “Nena Bwana kwa kuwa mtumishi wako anasikia.”
Samueli akakua, na Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuacha neno
lolote lianguke chini.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
ZABURI YA KUITIKIZANA Zaburi 40
(K) Tazama, nimekuja kuyatimiza mapenzi yako, ee Bwana.
Nalimngojea Bwana kwa subira;
akanielekea na kukisikia kilio changu,
akaweka wimbo mpya
kinywani mwangu, sifa za Mungu wetu. (K)

Hukupenda sadaka wala matoleo;


ila masikio wazi kwa kutii;
hukutaka dhabihu za kuteketeza wala sadaka za dhambi;
hapo nilisema, “Tazama, nimekuja.” (K)

Katika gombo la chuo nimeandikiwa amri zako.


Napenda kutimiza mapenzi yako,
ee Mungu wangu, sheria yako imo moyoni mwangu! (K)

Ninatangaza habari za haki yako


katika mkutano mkubwa;
wala sikuzuia midomo yangu,
ee Bwana, wewe wajua. (K)

SOMO LA PILI 1 Wakorintho 6:13c-15a, 17-20


Mwanzo wa barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho.
Ndugu zangu: Mwili si kwa ajili ya anasa, bali ni kwa ajili ya Bwana, na
Bwana ni kwa ajili ya mwili. Na Mungu aliyemfufua Bwana, naye
atatufufua sisi pia kwa uwezo wake. Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni
vyungo vya Kristo? Lakini yeye anayeambatana na Bwana ni roho moja
naye. Ikimbieni zinaa. Makosa yote ayatendayo mwanadamu yapo nje ya
mwili, ila mwenye kuzini huukosea mwili wake wenyewe. Au hamjui ya
kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu? Mwili

2
mmepewa na Mungu! Kwa hiyo si mali yenu. Maana mmenunuliwa kwa
bei kubwa. Basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO LA INJILI
K. Aleluya.
W. Aleluya.
K. Tumemwona Masiya, ndiye Kristo;
neema na kweli zimepatikana kupitia yeye.
W. Aleluya.

INJILI Yohane 1:35-42


Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Yohane.
Wakati ule: Yohane alisimama tena huko pamoja na wawili wa wafuasi
wake, akamwona Yesu akipita njiani, akasema, “Tazameni, Mwanakondoo
wa Mungu.” Wale wafuasi wake wawili waliposikia hayo walimfuata Yesu.
Yesu akageuka, akawaona wanamfuata, akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao
wakajibu, “Rabbi,” inayotafsiriwa mwalimu, “Unakaa wapi?” Akawa-
ambia, “Njoni, mtaona.” Wakafuatana naye, wakaona, wakashinda kwake
siku ile. Ilikuwa saa kumi. Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja
wa wale wawili waliomsikia Yohane na kumfuata Yesu. Huyo alikutana
kwanza na Simoni, nduguye, akamwambia, “Tumemwona Masiya,” (inayo-
tafsiriwa, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema,
“Wewe ni Simoni, mwana wa Yohane; uitwa Kefa,” inayotafsiriwa, Petro.
Injili ya Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

You might also like