1. ‘‘lakini itakuaje historical injustice nawe Ridhaa hapo
ulipo sicho kitovu chako?’’ Ni maneno ya Ridhaa yalikuwa yakimpiku baada ya kumjibu Tila mawazoni. Hii ni baada ya Ridhaa kukubali maneno ya Tila ya hapo awali. Inadhihiirika kuwa amekubali kuwa yeye ni mgeni si mwenyenji. 2. ‘‘…..Liandikwalo ndilo liwalo since when has man ever changed his destiny.’’ Ni maneno ya Terry akimwanbia Ridhaa mawazoni mwa Ridhaa akiwa nyumbani baada ya familia yake kuangamizwa wakiwa kwa nyumba. 3. ‘’nakumbuka asubuhi ya pili baada ya mtafaruko kuanza.Nilikua sebuleni na wanangu tukitazama runinga.’’ Ni maneno ya Kaizari akikumbuka jinsi machafuko ya baada ya uchaguzi yalivyoadhiri nchi ya wahafidhina. 4. ‘’nitapigana kwa jino na ukucha kuulinda utu wangu.’’ Ni uzungumzi nafsia wa Umu baada ya kutoka mlima wa Simba baada ya kutekwa nyara kwa nduguze, Mwaliko na Dick. 5. ‘’kuukata mkono niliostahili kubusu yalinifika kunifika.’’ Ni maneno ya msimulizi. Kumhusu Dick alipokumbuka jinsi rafiki yake Lemi alikuwa ameuwawa na umati. Anakumbuka haya baada ya kutishwa kuwa angetupwa nje na mwanjiri wake Buda.kisha asingiziwe wizi na kuchomwa moto. 6. ‘‘ Msamehe hakuna mja aliyekamilika.’’ Maneno ya mamake Sauna Akimzungumzia Sauna katika kumbukizi za Sauna baada ya kutendewa unyama na babake mlezi. Sauna anabakwa na kuambulia uja uzito hali inayobainisha mkondo wa maisha ya sauna. 7. ‘‘Kumbe hata mja akafanikiwa vipi kielimu na kitaaluma maisha yake huwa ombwe bila mwana awe wa kuzaa au wa kulea?’’ Msemaji ni Mwangeka Anajisemea kimoyomoyo. Yeye na Neema wakoo katika ofisi ya Annastacia katika kituo cha Watoto wa Benefactor. Wamekwenda kumchukua motto wa kupanga Mwaliko baada ya kukosa kufanikiwa kuwa na wana. 8. ‘‘ una bahati kupata mfadhili mimi mzazi wangu wa pekee ni mama ambaye muuza samaki.’’ Msemaji – Kairu Akimwambia Umu Bweninikatika shule ya Tangamano Ni baada ya Umu kusimulia hadithi yake na jinsi alivyo ufadhili katika makao. 9. ‘‘…Familia yake bado inamiliki mashamba ya michai na miboni pamoja na mashirika mengi..’’ -Maneno ya Chandachema -Akimmwambia Umu , Zohali na Mwanaheri. -wakiwa katika bweni la wasichana katika shule ya Tangamano. -Alikuwa akiwaelezea usuli wa yeye kuwepo katika shule hiyo. 10. ‘‘ kumbe hata wewe shemeji…..?’’ ‘‘ndio tu hapa na wengi’’ Kauli ya (1) Ridhaa Akimwambia Kaizari Kauli ya pili ni jibu la kaizari Katika kambi ya wakimbizi Ridhaa alikuwa amemwona shemeji yake Kaizari alipotoka kutafuta mzizi mwithi kutokana na uhaba wa chakula. 11. ‘‘Maisha yangu yalifaa shubiri tangu utotoni’’ Maneno ya Chandachema Kwa zohali Umu ,Kairu na Mwanaheri Bwwenini shuleni Tangamano. Walikuwa wakihadithia maisha yao ili kumliwaza Umu asione kuwa ni yeye tu amepitia magumu.