Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

SIRI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA MAJARIBIO WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2021

01 KISWAHILI

MAELEKEZO KWA MSIMAMIZI

Zingatia yafuatayo kabla ya kusoma maelekezo kwa watahiniwa:

(i) Hakikisha unasoma hadithi kwa sauti na taratibu kwa mara ya kwanza huku
ukizingatia alama zote za uandishi zilizopo katika hadithi hiyo. Unaposoma kwa
mara ya pili ongeza kidogo kasi ya usomaji.

(ii) Muda utakaotumia kuwasomea watahiniwa hadithi ni dakika tano (05) na muda
utakaotumika kwa watahiniwa kujibu maswali ni dakika tano (05). Sehemu hii
itafanyika kwa dakika kumi (10).

(iii) Wasomee watahiniwa kwa sauti maelekezo (1 hadi 3).

MAELEKEZO KWA WATAHINIWA


1. Nitasoma kwa sauti hadithi mara mbili, hivyo kila mmoja asikilize kwa makini.

2. Nikisoma hadithi kwa mara ya kwanza, sikiliza bila kujibu maswali na nikimaliza
kusoma kwa mara ya pili, jibu swali la 1 hadi 5 kisha endelea kujibu maswali
mengine (6 hadi 45).

3. Ninaanza kusoma hadithi sasa hivyo sikiliza kwa umakini.

HADITHI

Hapo zamani za kale palikuwa na kijiji kiitwacho Faru. Faru ni kijiji kilichokuwa
karibu na msitu mkubwa wenye wanyama wakali. Wanakijiji wa Faru waliishi maisha
ya raha sana. Kiongozi wao aliitwa Adabu, alikuwa kiongozi shupavu na mzalendo.
Ukurasa wa 1 kati ya 2

SIRI
SIRI

Wanakijiji walimpenda kwa sababu alikuwa anajitoa kwa ajili ya kijiji chake,
alipenda haki na alipigania maendeleo ya kijiji chake.

Siku moja Adabu akiwa nyumbani kwake alisikia kelele nje ya nyumba yake.
Alipotoka nje aliona kundi kubwa la wanakijiji wameshikilia silaha mbalimbali kama
vile rungu, sime na magongo, hakujua ni ya kazi gani? Akauliza kwa shauku “kuna
nini?” Mzee Funzi akajibu kwa hofu “tumevamiwa! tumevamiwa! na simba.
“Simba?” Adabu aliuliza huku akikimbia kurudi ndani, akatoka na mshale. Punde si
punde ilisikika ngurumo nyuma ya nyumba yake.

Adabu akawaambia “msiogope” kisha akawagawa katika makundi mawili ili


kumzunguka na kumshambulia simba. Baada ya kukuru kakara za muda mrefu
wanakijiji walifanikiwa kumuua simba. “Ama kweli jifya moja haliinjiki chungu,”
alisikika akisema kijana mmoja. Wanakijiji waliondoka kwa furaha na kila mmoja
alirudi nyumbani. Mpaka sasa wanakijiji wa Faru wanaishi kwa amani na ushirikiano.

Ukurasa wa 2 kati ya 2

SIRI

You might also like