Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 6

ECAM, tarehe 11 Januari 2024 imetoa tamko linalosema, hakuna baraka

kwa wapenzi wa jinsia moja kwa Makanisa Barani Afrika.


VATICAN
SECAM: Hakuna Baraka Kwa Wapenzi wa Jinsia Moja Kwa Kanisa Barani
Afrika
SECAM: Hakuna baraka kwa wapenzi wa jinsia moja kwa Makanisa
Barani Afrika. Tamko hili limeridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko
pamoja na Kardinali Victor Fernàndez, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa
la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Hili ni tamko linajadili mafundisho ya
Kanisa kuhusu Ndoa na Tendo la Ndoa; Mwongozo wa Kichungaji kwa
familia ya Mungu Barani Afrika; Msimamo wa Kanisa Barani Afrika
mintarafu mapenzi ya watu wa jinsia moja na hitimisho!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.


Tamko la Mafundisho Tanzu ya Kanisa “Fiducia supplicans” Yaani
“Kuomba Baraka kwa Imani” Maana ya Baraka Kichungaji” lilijadiliwa
katika mkutano wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,
likapelekwa kwa Baba Mtakatifu Francisko na hatimaye, akaridhia
lichapwe kwa kuweka saini yake tarehe 18 Desemba 2023. Tamko hili
linajadili kwa kina na mapana kuhusu: Baraka katika Sakramenti ya
Ndoa, Maana ya baraka katika Maandiko Matakatifu, Uelewa wa baraka
kitaalimungu na kichungaji, na nani anaweza kuomba baraka. Baraka
kwa watu wenye “ndoa tenge” pamoja na wapenzi wa jinsia moja.
Kanisa ni Sakramenti ya upendo wa Mungu. Watu wa Mungu wenye
imani thabiti wanaweza kupokea baraka za Mwenyezi Mungu kwa njia
ya Kristo Yesu na Kanisa na kwamba, Kristo Yesu ni kielelezo cha baraka
kuu kutoka kwa Mungu, baraka ambayo ni chemchemi ya wokovu.
Baraka katika Sakramenti ya Ndoa Takatifu: Kiini cha ndoa ya Kikristo ni
maagano baina ya mume na mke au ukubaliano wao wa hiari
usiotanguka. Muungano huo wa mume na mke na manufaa ya watoto
wao huwataka wawe na uaminifu kamili kati yao. Kwa asili yake ndoa na
mapendo ya wenye ndoa yamewekwa kwa ajili ya kuzaa watoto na
kuwalea; nao ni taji yao. Kwa kweli watoto ni zawadi kuu ya Ndoa na
tunu kubwa ya wazazi wenyewe. Haya ndiyo Mafundisho tanzu ya
Kanisa kuhusu Ndoa na kamwe hayawezi kubadilishwa. Wakati wa kutoa
baraka, Kanisa lina wajibu na dhamana ya kuhakikisha kwamba
halichanganyi madhehebu ya kutoa baraka, ili kusitokee mkanganyiko
na kwamba, Kanisa halina mamlaka ya kutoa baraka kwa wapenzi wa
jinsia moja. Tamko hili likapokelewa kwa hisia tofauti na hivyo kuzua
mjadala mkali wa kiimani, kimaadili, kisheria na utu wema kutoka
sehemu mbalimbali za dunia.
Tamko la SECAM ni sehemu ya mchakato wa Sinodi na Urika wa
Maaskofu
Tamko la SECAM ni sehemu ya mchakato wa Sinodi na Urika wa
Maaskofu

Kardinali Fridolin Ambongo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu


Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM, katika barua yake ya tarehe 20
Desemba 2023 akayaomba Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika
kujadili tamko hili la “Fiducia Supplicans”, ili hatimaye, Kanisa Barani
Afrika liweze kutoa msimamo na mwongozo kwa waamini wa Kanisa
Katoliki Barani Afrika, kwa kutambua dhamana na umuhimu wa
Mabaraza ya Maaskofu katika kuambata mchakato wa Sinodi sanjari na
kukuza urika wa Maaskofu. Tamko la Shirikisho la Mabaraza ya
Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM ni matunda ya
mchakato wa maadhimisho ya Sinodi kwa hiyo ni kwa ajili ya Kanisa
zima la Bara la Afrika. Ni katika muktadha huu, SECAM, tarehe 11
Januari 2024 imetoa tamko linalosema, hakuna baraka kwa wapenzi wa
jinsia moja kwa Makanisa Barani Afrika. Tamko hili limeridhiwa na Baba
Mtakatifu Francisko pamoja na Kardinali Victor Manuel Fernàndez,
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Hili ni
tamko linajadili mafundisho ya Kanisa kuhusu Ndoa na Tendo la Ndoa;
Mwongozo wa Kichungaji kwa familia ya Mungu Barani Afrika;
Msimamo wa Kanisa Barani Afrika mintarafu mapenzi ya watu wa jinsia
moja na hatimaye, SECAM inatoa hitimisho ya tamko lake.
Mapenzi ya jinsia moja na kinyume cha Maandiko Matakatifu
Mapenzi ya jinsia moja na kinyume cha Maandiko Matakatifu

Maaskofu Barani Afrika wanatambua dhamana na nafasi ya Khalifa wa


Mtakatifu Petro katika kukuza umoja wa imani, ushirika na urika kati
yao, daima wakiwa waaminifu kwa tunu msingi za Kiinjili. Wanatambua
mafundisho ya Kanisa kuhusu ndoa na familia ambayo kamwe hayawezi
kubadilika na kwamba, Tamko la “Fiducia supplicans” linatambua
Mapokeo ya Kanisa Katoliki yanayopata chimbuko lake katika Maandiko
Matakatifu na Mamlaka Fundishi ya Kanisa “Magisterium of the Church”
kwamba: Kiini cha ndoa ya Kikristo ni maagano baina ya mume na mke
au ukubaliano wao wa hiari usiotanguka. Kumbe mahusiano ya watu wa
jinsia moja ni jambo lisilokubalika na kwamba, Kanisa Barani Afrika
haliwezi kutoa baraka. Kanisa Barani Afrika linaendelea kujitambulisha
kuwa ni familia ya Mungu inayowajibika na kwamba, litaendelea
kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu Barani Afrika na
kwamba, Mapadre wanahimizwa kutoa huduma kwa watu wenye “ndoa
tenge” na kwamba, mashoga na wasagaji waheshimiwe na utu wao
uthaminiwe lakini wakumbushwe kwamba mahusiano ya kimapenzi ya
watu wa jinsia moja ni kinyume cha mapenzi ya Mungu na kwa mantiki
hii hawawezi kupata baraka ya Kanisa kwani mahusiano haya ni
kinyume cha mapenzi ya Mungu. SECAM inasema Mapokeo yametamka
daima kwamba matendo ya kujamiana ya jinsia moja ni maovu kwa
yenyewe. Ni matendo dhidi ya sheria ya maumbile. Yanatenga paji la
uhai na tendo la kijinsia. Hayatokani na kutimilizana kwa kweli kihisia na
kijinsia. Kwa namna yoyote ile hayawezi kuidhinishwa. Rej. KKK 2357.
Ukoloni wa Kiitikadi na madhara yake
Ukoloni wa Kiitikadi na madhara yake

Mapenzi ya jinsia moja ni kashfa kadiri ya Maandiko Matakatifu. Katika


muktadha wa Kanisa Barani Afrika, mapenzi ya jinsia moja ni kinyume
cha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia na ni vigumu sana watu
wa namna hii kukubalika na hatimaye kupokelewa na jamii kwa sababu
ni matendo yanayokwenda kinyume cha tamaduni na kwamba, huu ni
uovu! SECAM inahitimisha tamko lake kwa kusema, kadiri ya Maandiko
Matakatifu, Mamlaka Fundishi ya Kanisa, tamaduni, kanuni maadili na
utu wema, Kanisa Barani Afrika halitatoa baraka kwa watu wa mapenzi
ya jinsia moja, kwani kufanya hivi ni kuibua kashfa na kwamba, kuna
umuhimu kwa watu wenye shauku ya jinsia moja kutubu na
kumwongokea Mungu ili waonje huruma na upendo wake usiokuwa na
mipaka, tayari kuwa ni chumvi na nuru ya dunia. Rej. Mt 5:13-14.
SECAM inasema, kuna baadhi ya nchi Barani Afrika zimeomba, muda wa
kufanya tafakari na mang’amuzi, ili kutoa maamuzi na kwamba, SECAM
itaendelea kufanya tafakari kuhusu umuhimu wa baraka kwa watu wa
Mungu katika shughuli zake za kila siku. Kanisa Barani Afrika linapaswa
kuendelea kuwa imara na kwamba, Baba Mtakatifu Francisko hataki
kuona ukoloni wa kiitikadi na kitamaduni Barani Afrika! Wakristo Barani
Afrika wawe tayari kusimama kidete kulinda na kutetea tunu msingi za
maisha ya Kikristo!
SECAM: Baraka

Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili
tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba.
Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili
tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba.
12 January 2024, 14:38
https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2024-01/secam-
hakuna-baraka-wapenzi-jinsia-moja-barani-afrika-fiducia.html

You might also like