26/09/2023 Yah: Shauri namba moja . Mgogorowa eneo kati ya ndugu kokino – MTAHIGWA dhidi ya mzee wamtilana kokino wote wakazi wa luchanga A. Wajumbe walio kuweko kusikiliza shauli hili 1. HELENA J. KIBUNGOSHO (KE) 2. JULIUS N. SUMUNI (ME) 3. LAURIAN M. GASPAL (KE) 4. SADIKI SANZU (ME) 5. IRINE P. MANENGERO (KE) 6. MAGRETH FULUGENCI (KE) 7. STEOFN JUSTINE (ME) B. Maelezo ya mdai Bwana kokino Mtahigwa Dini R.c Umri 50. Maelezo ya mdai Mimi kokino mtahigwa ni msimamizi wa mirathi ya marehemu mzee kokino Nduri naambatanisha ruksa ya kusimamia mirathi hiyo kutoka mahakama ya mwanzo kasenyi. Ni kwamba kipindi cha uhai wa mzee kokino nduri alibahatika kuwa na wanawake wawili., wa kwanza alikuwa nyakwantazi lukonza na wa pili alikuwa kahabi msobozi – aliishinao tangu akiwa kwenye mahame. Na ndipo ilipoingia operation vijiji vya mwaka 1974 alihama na kuja kugomwa hapo ambapo pana mgogoro kwa sau, hivyo alihama na familia yake wote yam wake wawili na kuanza maisha mapya mnamo mwaka 1974 marehem kokino nduri alikuwa na familia ya watoto 18 mke mkuu watoto 8 mke mdogo watoto 10 , hapo alienderea kuishi kwa na familia yake vizuri. Mnamo mwaka 1998 alimfukuza kijana wake mkubwa (mtahigwa kokino) Baada ya kushindana kitabia na walio baki walienderea kuishi hapo. Wasichana wao waliolewa wale walio kuwa wakubwa na wale walio kuwa wadogo waliendelea kuishi hapo, 1982 marehemu kokino nduri aliugua na kufariki dunia., Baada ya kufariku dunia eneo lote lililo kuwepo lilibaki chini ya watoto wa marehemu. Pia baada ya kufariki watoto wa marehemu waligawana mashamba ya pembeni, kila watoto walienderea kumiliki mashamba yaliyo kuwa yanamilikiwa na mama zao , na hata wakagawana eneo la mahame kwa kufuata mama zao hivyo waligawana kati kwa kati