Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Kwa: ken.walibora@gmail.

com
Kutoka kwa: brighton.onyango@koderobara.ac.ke
Kuhusu: Jinsi Matukio Katika Matini Yameathiri Utambulishi Wangu.

Hujambo bwana,
Natumai ujumbe huu wangu utakufikia salama.Ningependa kukuarifu kuwa nilikipenda
kitabu kile cha hadithi fupi ya damu nyeusi uliyeandika.Sifa tele tele zikufikie huko
uliko.Mola aendelee kukupa ujuzi wa kuandika vitabu vinginevyo ili kutuelimisha jinsi
ulimwengu wa kisasa ulivyokumbwa na ubaguzi.Sisi Waafrika tu hapa kukupa moyo ili
uendelee kutuwakilisha katika mashindano hayo mengi ya waandishi bora.

Matukio katika matini hayo yameathiri utambulisho wangu kwani yamenifundisha mambo
mengi.Hapo awali, sikuwa na fununu ya kwamba sisi kama Waafrika tunaweza kufanyiwa
unyama kama ule.Hakika ,hapo mwanzo nilikuwa na hamu ya kuenda nchi za ng’ambo lakini
kutokana na matukio yale ambayo Fikirini alitendewa nimeweza kubadili mienendo
yangu..Kwani sisi Waafrika tunachukuliwa kama binadamu hafifu ambao hawafai kuwa
ulimwenguni.Licha ya sisi kuwa weusi,haimanishi kuwa hatufai ,ni Mola aliyetuumba kwa
upendo wake na ni kwa nehema na rehema zake akaona ilikuwa vyema kuwaumba watu
weusi.Kwani hawa wazungu wanafikiria wao ni nani?

Kumbukumbu za Fikirini bado zipo akilini mwangu, ni machungu sana.Nawaza kwanini


Fikirini alitozwa faini na polisi mzungu ati alivuka barabara huku taa za kuelekezea magari
zikiwa zimewaka rangi nyekundu ilhali wazungu wengine wakifanya hivyo hawaadhibiwi
kwa vyovyote.Hiyo ni ishara kuwa tumechukuliwa kama wanyama na wazungu na mimi
bado nina sisitiza kuwa sitaenda Ulaya liwe liwalo.Mimi ni Mwafrika na nitasalia kuwa
Mwafrika.Hapo niliwaunga mkono wahenga waliponena kuwa mwenda tezi na omo marejeo
ni ngamani.Ingawaje Fikirini alienda Marekani ,alikuwa na nia ya kurudi Afrika nyumbani
mwao.

Pale ambapo Fikirini alikutana na mwanamke mweusi akamchukulia kama dada


yake,wakatabasamu na kuonyesha bashasha.Mwanamke huyo akampeleka kwao japokuwa
Fikirini alichelewa kuenda chuoni.Aliona fujo kwa kuwa hakusalimiwa na mwenye nyumba
na mahali hapo palikuwa chafu.Alipotaka kutoka, mwanamke huyo akadai kuwa Fikirini
alikuwa anataka kumbaka.Je, siku moja nikienda huko nitafanyiwa vivyo hivyo? Maajabu
hayo.Huo ndio mtindo wa kisasa..

Bwana Ken,ningependa kukupa sifa kedekede kwa kuwa umenijuvya kwa mambo ambao
mimi sikuyajua.Ningependa uandike vitabu vingine vingi ili niweze kupata maarifa mengi
kuhusu tabia za wazungu na jinsi wanavyo wanyanyasa Waafrika.Jalali akujalie na akulinde
pia.

Wako mwaminifu,
Brighton.

Kutoka kwa: ken.walibora@gmail.com


Kwa:brighton.onyango@koderobara.ac.ke
Kuhusu:Shukrani.
Hujambo,
Pokea salamu zangu chekwachekwa kama mchanga wa baharini.Unaendelea aje? Na wavyele
wako je,na tumai m salama.Mimi huku ni salama salimini huku ninaendelea kubingirisha
gurudumu la uandishi lililo gumu.Hofu na mashaka tuliwaachia watangulizi wetu enzi hizi ni
kupambana tu.Asante kwa kusoma matini yale kwa kuwa yatakufaidi zaidi.Asante pia kwa
kunipongeza na kunipa moyo.Binadamu kamili ni kama wewe ambaye anawapa moyo
wengine waendelee kufanya kazi.

Usipigwe na butwaa kwa yale ambayo Fikirini alitendewa kwani alienda nchi za ng’ambo
kufanya nini ilhali yeye ni Mwafrika? Mtu akiwa kiherehere mwache ajionee kwa kuwa
mwenye macho haambiwi tazama.Anaenda Marekani kufanya nini? Nina uhakika ya
kwamba hapo kwenu kuna mtu ambaye anataka kuenda nchi za ng’ambo.Mwambie kuenda
nchi za ng’ambo si mbaya ila wajihadhari kabla ya hadhari.

Ikiwa siku moja utaenda huko, tafadhali kuwa na heshima na usisahau kwenu kwa kuwa
hakuna pahali pazuri kama kwenu.Watu wanaoenda nga’mbo aghalabu huwa na matatizo
mengi.Usishangae kuwaona wakiwa nusu uchi.Wengine huenda kwa kiwango cha
kuwatukana wazazi.Juzi nilimwona mmoja akikataa katakata kula ugali ati atapata ugonjwa
wa Waafrika.Nilikuwa ninajiuliza ikiwa kuna ugonjwa wa Waafrika na wa Wazungu.Ama
kweli, dunia rangi rangile ina vituko vyake.Mtu kama huyo enzi zile zetu angenyoroshwa
viboko sawasawa.Huo ni utovu wa nidhamu.

Nikimalizia, ningependa uwahimize wenzako wakinunue kitabu hiki ili wao pia waweze
kupata nafasi ya kukisoma kwa kuwa kina mafunzo mengi.Kitabu hicho cha damu nyeusi ni
cha tukio cha kweli ambacho kilitendeka.Natumai ulikipenda kitabu hicho.Tofauti na damu
nyeusi,kuna vitabu vingine kama siku njema ,kufa kuzikana,ndoto ya alhamasi na vinginevyo
ambavyo pia ni wa kuelimisha, tafadhali pata nafasi na uvisome.

Wako mwaminifu,
Ken.

You might also like