Professional Documents
Culture Documents
Kifungo Cha Mila
Kifungo Cha Mila
UTANGULIZI
Mila ni kawaida ya mtu au jamii Fulani. Mila ni taratibu zenye
miiko za watu/jamii Fulani. Mfano: Mila ya kunyoa vipara kwa
ajili ya wafu.
Mila zisizompendeza Mungu ni chanzo cha vifungo vya kiroho
na kimwili kwa watu wengi. Kupitia mila watu
wamejiunganisha na mizimu ya ukoo/familia iliyobeba mila
hizo. Mila zisizofaa hubeba nguvu ya mizimu inayopelekea
vifungo. Mila hugeuka chanzo cha vifungo maana baadhi ya
mila zina Maagano yake ambayo zimebeba SIRI kubwa.
2. Kuabudu Waliokufa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11
Hii ni mila nyingine isiyompendeza Mungu inayofanywa na
watu wengi. Hizi ni ibada ya kutambikia na kutoa kafara kwa
ajili ya jambo Fulani ili mizimu ya marehemu iwasaidie.
Jiulize swali hili, “Tunapaswa kwenda kwa waliokufa kwa ajili
ya walio hai?
ISAYA 8:19
Mila ni ibada isiyompendeza Mungu. Mila huambatana na
sadaka za miungu ile inayosimamia mila hizo.
MUHIMU: Tambua chanzo na dhumuni ya mila hiyo katika
familia yenu. Usikimbilie kufanya mila bila kujua chanzo na
madhumuni utajiunganisha na Maagano ya mila bila kujua, na
madhara yake yatakuwa makubwa.