Professional Documents
Culture Documents
Asili Yako
Asili Yako
Asili Yako
Kila
mwanadamu amezaliwa na mwanamke na wanyama huzaliwa na wanyama
weyewe. MWANZO 1:26-28 Imeandikwa, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu
kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho
juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu
alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia,
Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha;
mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye
uhai kiendacho juu ya nchi.” Mungu aliwabarikia wakaze na kuongezeka
wakaijaze nchi. Maana yake ukazae na kuongeza, na si kuzaa tu bali uzae na
kuongezeka. Chochote unachokishika kizae na kuongeka. Kuongezeka kimasomo,
mtaji, biashara, familia na ustawi.
Hapa Mungu ametupa uhalali wa kuwaganyaga uzao wa nyoka kwa jina la Yesu.
Kazi iliyomezwa, ndoa, masomo leo atatapika kwa jina la Yesu. Hata wewe
umezaliwa na mwanamke bila shaka umefungwa kwenye magereza, kwenye
mashamba leo utatoka kwa jina la Yesu.UFUNUO 12:13-17 imeandikwa, “Na joka
yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule
aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya
tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo
alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama
mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.”
Pamoja na Pennina kumchokoza Hana, Hana hakukata tamaa. Siku moja kuhani
alimkuta Hana midomo yake ikichezacheza akamuuliza kwa nini umelewa asubuhi
hii yote. Hana akamjibu mimi naumimina moyo wangu kwa Bwana. Siku chache
zilizofuata Hana akamzaa shujaa wa Bwana Samweli. Unapochelewa kuzaa usife
moyo Bwana amekuandalia jambo kubwa, endelea kuomba utapokea sawasawa
na haja ya moyo wako. Inawezezkana umepewa taarifa mbaya kutoka kwa
madaktari, hizo ni taarifa za wanadamu lakini leo yupo Yesu atakayerudisha vyote.
Mungu anasema njia zenu sio njia zangu, yeye anatuwazia mema.
Vita ya uzao ni vita ya kufa na kupona, ndo maana shetani ameachilia waume na
wake wa kipepo. Unapokuwa umelala unaingiliwa kwenye ndoto. Inawezekana
una watoto baharini au unanyonyesha ndotoni, katika hali ya kawaida huwezi
kupata ujauzito katika ulimwengu wa mwili. Dalili za mtu aliyefunga ndoa za
kipepo Kiuno, mguu wa kushoto unakufa ganzi, ukiota unatoka bichi (out). Shetani
anafanya hivi kwa sababu anataka uzao wake uchanganyike na uzao wa
mwanadamu ili aweze kutenda kazi kwa urahisi.
ISAYA 14:29b imeandikwa, “Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao
wake ni joka la moto arukaye.” Zaburi 22:10 imeandikwa, “Kwako nalitupwa
tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.” Unakuta
tangu tumboni wengine washaanza kunywa makombe, dua. Unakuta mtu anakula
mkaa, udongo kumbe mama yake alivyokuwa mjamzito alikuwa anakula udongo.
Ukiona mtu anakula udongo ujue tumboni kwake kuna joka. Leo ukatae kula
vyakula vya kipepo kwa jina la Yesu.
LUKA 1:39-43 Imeandikwa, “Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata
nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia nyumbani
kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia
kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti
akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa
wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” Kumbe
mtu anaweza kupokea roho kupitia sauti ya mtu. Mtu anaweza kupata matatizo
au Baraka kupitia salamu. WAEBRANIA 1:7 imeandikwa “Na kwa habari za
malaika asema, Afanyaye malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa
miali ya moto.” ZABURI 104:4 imeandikwa, “Huwafanya malaika zake kuwa
pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali.” Unakuta unapata fursa nzuri
lakini zinapotea, umenyang’anywa kinywa.
Mchungaji Kiongozi Daktari Godson Issa Zacharia akimfungua mtu na uzao wake umekuwa
salama kwa jina la Yesu.
ISAYA 6:8 imeaandikwa, “Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume
nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa,
nitume mimi.” Mungu alikusudia kuokoa uzao kwa kumtoa mwanawe wa pekee.
YOHANA 6:16-17 imeandikwa, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,
bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni
ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” Mungu
aliupenda ulimwengu, kutoa kunaendana na kupenda. Mungu alimtoa mwanawe
ili upate uzima tele. Kazi, ndoa, masomo, biashara yako iwe na uzima tele.
Lazimisha ulimwengu wa roho ukuachilie ili uongezeke. Kila unachokianza maana
yake kizae na kuongezeka.7