Kisw 203-Ushairi Wa Kiswahili

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

GRETSA UNIVERSITY - THIKA

SPECIAL/SUPPLEMENTARY EXAMINATIONS
FOR SEPTEMBER – DECEMBER 2018 SEMESTER

BACHELOR OF EDUCATION (ARTS)

KODI: KISW 203


KOZI: USHAIRI WA KISWAHILI

DATE: 15 APRIL 2019 TIME: 2.00 PM – 5.00 PM

MAAGIZO KWA WATAHINIWA


1. SEHEMU YA KWANZA A: NI YA LAZIMA
2. SEHEMU YA PILI B: JIBU MASWALI YOYOTE MATATU
3. USIANDIKE CHOCHOTE KWENYE KARATASI YA MTIHANI. KWA KUFANYA
HIVYO UTAKUWA UMEVUNJA SHERIA ZA MITIHANI NA UTAADHIBIWA
4. ANDIKA VIDOKEZO VYAKO NYUMA YA KIJITABU CHA MAJIBU KISHA
PIGIA MSTARI BAADAYE

Page 1 of 3
TAHADHARI:- kamera za CCTV zipo kwenye vyumba vyote vya mitihani

SEHEMU YA A: NI YA LAZIMA

Swali La Kwanza

a) Toa kijelezi cha maana kishairi. [Alama 2]


b) Je, maana ya kitamathali ni maana ipi? [Alama 2]
c) Ni vipi urudiaji unaweza kuchangia katika dhamira ya mtunzi wa ushairi? Onesha.
[Alama8]
d) Tathmini umuhimu wa somo hili kwako wewe kama mwalimu mwandaliwa.
[Alama8]
e) Toa kijelezi cha dhana mshata katika ushairi. [Alama1]
f) Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali yafuatayo:
Lauzi, Mwanagu-Mwalaa Mranga Nyanje
Ewe mwanagu Lauzi, Lauzi binti yangu,
Zidarizi beti hizi, hizi wasia wangu,
Ukuapo umaizi, umaizi ulimwengu,
Kwamba hauna mjuzi, mjuzi wa ulimwengu,
Hajawapo pande hizi, hizi toka babu zangu,
Tangu kuwepoWangozi, Wangozi hata Wazungu,
Kila aliye ajizi, ajizi yake ni pingu,
Kisha hulewa ulezi waulimwengu,
Usokuwa nambawazi, mbawazi ila machungu,
Yasikufike mwanangu, mwanangu nakuusia.

Mwanangu nakuusia, nakuusia Lauzi,


Chuo kigumu dunia, dunia hii ni kozi,
Huwezi mia kwa mia, mia kufuzu huwezi,
Utaishia kulia, kulia pasipo chozi,
Muradi ukijitia, ukijitia bazazi,
Kikiki kushikilia, kushikilia ushenzi,
Turudi kuujutia, kuujutia upuzi,
Dunia kikukalia, lia kutoka huwezi,
Ewe mwanangu ridhia, ridhia haya malezi,
Yeye na kila mbawazi, mbawazi na maongozi.

Page 2 of 3
i) Tathmini ufaafu wa kichwa cha shairi hili. [Alama2]

ii) Kichwa hiki kinachangia vipi katika dhamira ya mtunzi wa shairi hili? [Alama2]
iii) Angazia aina ya maana inayojitokeza katika shairi hili na uitoe kwa mujibu wa shairi
hili. [Alama3]
iv) Tathmini muundo wa shairi hili. [Alama5]
v) Eleza maana ya muktadha wa shairi na kisha utoe muktadha halisi wa utunzi huu.
[Alama4]
vi) Jadili suala la mshororo kwa mujibu wa shairi hili huku ukieleza ni aina gani ya shairi.
[Alama3]

SEHEMU YA B: JIBU MASWALI YOYOTE MATATU

Swali La Pili

‘Je, mashairi ya Kiswahili huainishwaje? Egemea katika muundo wake. [Alama20]

Swali La Tatu

a) Je, nafsineni ni nini katika mkabala wa ushairi? [Alama 2]


b) Tathmini nafasi ya nafsineni katika shairi lolote lile. [Alama 3]
c) Ni vipi nafsineni hutambuliwa katika shairi? [Alama 3]
d) Eleza maana ya toni kisha utambue umuhimu wake katika shairi. [Alama 2]
e) Ni vipengele vipi vinavyozingatiwa wakati wa uchambuzi wa shairi? Toa maelezo
mafupi kwa kila kipengele. [Alama10]

Swali La Nne

a) Faragua kikamilifu nafasi ya mtunzi wa ushairi katika jamii yake. [Alama20]

Swali La Tano

a) Onesha uhuru wa mshairi huku ukitolea maelezo na kuyahimili kwa mifano faafu.
[Alama10]
b) Tathmini suala la hisia katika utunzi wa ushairi wa Kiswahili. [Alama10]

Page 3 of 3

You might also like