Fasihi inayoteg-WPS Office

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

Fasihi inayotegemea mdomo Katika kutolewa na kuenezwa kwake.(M.L.Matteru,1979).

kwa ujumla fasihi


ni tawi la Sanaa inayotumia lugha Katika kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.Fasihi simulizi,Ni
aina ya fasihi inayotumia mazungumzo ya mdomo Katika kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa
Katika fasihi simulizi fanani na hadhira wanaonana ana kwa ana pia hadhira hushirikiana nafanani Katika
kuwasilisha kazi yake hadhira ushirikiana na fanani Katika kupiga makofi,vigelegele pia kuonesha hisia
kama uzuni au furaha.Fasihi andishi ni aina ya fasihi inayotumia maandishi Katika kufikisha ujumbe kwa
hadhira iliyokusudiwa.Katika fasihi andishi fanani na hadhira hawaonani ana kwa ana na mwandishi ndio
mmiliki wa kazi za fasihi pia Katika fasihi andishi hutumia gharama,haiwezi kubadilika papo kwa papo
kama ilivyo kwenye fasihi andishi.

Mkocho,Ni mtaalam Katika matumizi ya mbinu mbalimbali za masimulizi Katika kazi za kifasihi.Mkocho
wa wakocho,ni mbobezi zaidi Katika matumizi ya vipengele mbalimbali vya kimasimulizi Katika kazi za
kifasihi

Si kweli kwamba msimuliaji wa fasihi simulizi pekee ndio mkocho wa wakocho Katika utumiaji wa mbinu
za masimulizi bali hata mwandishi wa kazi za fasihi andishi anaweza kuwa mkocho wa wakocho kupitia
matumizi ya mbinu mbalimbali za masimulizi Katika kazi yake.Diwani ya HEKiMA ZA WAHENGA
iliyoandikwa na H.W.Mapunda na tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI iliyoandikwa na
EMMANUEL MBOGO ni miongoni mwa kazi za fasihi andishi zilizothibisha kuwa hata mwandishi wa kazi
za fasihi ni mkocho wa wakocho kama ifuatavyo

Matumizi ya tamathali za semi;ni matumizi ya maneno yenye maana kinyume na ile ya kawaida na yenye
lengo la kutoa fundisho na kupamba sentensi kwa usanii.Mwandishi wa tamthiya ya NGOMA YA
NG'ANAMALUNDI na diwani ya HEKIMA ZA WAHENGA wametumia tamathali za semi kama ifuatavyo

Takriri;Hii ni mbinu ya kurudiarudia maneno wa lengo la kuonesha msisitizo wa kitu


fulani.katika diwani ya HEKIMA ZA WAHENGA mbinu hii imetumika Katika shairi la "mtani wa
makondeni"Katika ubeti wa 18 (uk43) mwandishi anasema

"hodi hodi kwa watani"

Pia Katika tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI mbinu hii imejitokeza Katika (UK 11) mwandishi
anasema

"Chipupe:hebu simama!simama:"

Tashihisi;hii ni mbinu ambayo vitu visivyo na uhai au visivyo na sifa za ubinadamu hupewa sifa za
kibinadamu Katika tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI (uk9) mbinu hii imetumika kama

"Seche .........huoni hiii sherehe

Imetufyonza damu....."
Tashibiha ;hii ni tamathali ya semi ambayo hutumiwa kufananisha vitu tofauti kwa kutumia
viunganishi.Katika dawani ya "hekima za wahenga"(uk14)shairi la "mkisikia kishindo" ubeti wa 2
mwandishi anasema

" Mwatuwinda kama swala"

Pia Katika tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI Katika (uk72) tashibiha imejitokeza ambapo
mwandishi anasema

"......chidama kajikunyata kama paka"

Matumizi ya majibizano(dayolojia);hii ni mbinu ya mazungumzo ambapo wahusika huongea


kwa kupokezana.katika tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI mwandishi mwandishi ametumia
mbinu hii Katika kufikisha ujumbe mbinu hii imetumika Katika (uk60) mwandishi anasema

Kizuu:Damu!

Wote:Damu!

Kizuu:ua!

Wote:ua!

Hivyo matumizi ya dayolojia au majibizano Katika uandishi wa kazi za fasihi unathibitisha kuwa
mwandishi wa fasihi ni mkocho wa wakocho

Matumizi ya masimulizi (hadithi);hii ni mbinu ambayo mwandishi husimulia tukio au hali


Fulani kwa hadhira yake.katika diwani ya HEKIMA ZA WAHENGA mbinu hii imetumika Katika shairi
la"hekima za wahenga"(uk1)

"Sikia wake uzuri,kama marashi ya Pemba

Wahenga wamehariri,hata kwa kifo na rumba

Nawe ukazikariri,uwe waziimba imba

Ni hekima za wahenga,soma ulishe ubongo"

Pia Katika tamthiya ya NGOMA YA NG'ANAMALUNDI mbinu hii imetumika Katika (uk34) mwandishi
anasema

".......ni usiku kuna sanduku juu ya kitanda.Nguo na vitu

Vya marehemu nyamiti vipo hapo kitandani chibupa

Mwenye huzuni anavipanga ndani ya sanduku

Polepole kimoja baada ya kimoja..."


Ujenzi wa wahusika; wahusika ni watu au viumbe hai au visivyo hai ambavyo mwandishi wa kazi
za fasihi hutumia Katika kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.si kweli kwamba msanii wa fasihi
simulizi ndio yuko vizur Katika ujenzi wa wahusika hata msanii wa fasihi andishi yuko vizur Katika ujenzi
wa wahusika mfano Katika tamthiya ya "ngoma ya ng'wanamalundi"mwandishi amejenga wahusika
wake vizuri na ameweza kufikisha ujumbe kwa jamii kwa mfano Katika (UK 63) mwandishi ametuy
wahusika kama

"Kizuu :(akiitika)ndiyo ua

Chidama!Damu........."

Pia Katika diwani ya "hekima za wahenga"mwandishi ametumia muhusika kama Asha kiduku (uk35)
kufikisha ujumbe wa wadada ambao hawajatulia mwandishi anasema

"Vodonge Asha kameza,mimba ile kuitoa

Lakini havikuweza,ndo kwanza kapalilia

Miezi akatimiza,tayari kujifungua

Itikia,ameni!ameni!

Ilaaaaa!

Acha kuhukumu watu,hiyo kazi ya jalali

Matumizi ya ngomezi;ni mbinu ya kutumia midundo tofauti ya ngoma kwa lengo kufikisha
ujumbe au maana Fulani kama vile kufikisha hali ya hatari, huzuni na furaha.katika diwani ya "hekima za
wahenga"ngomezi inadhihirika Katika (uk27) mwandishi anasema

" Kule uzaramoni,ngoma ni kipaumbele

Kutwa wao mkoleni,cheza nguo tupa kule

Simwambiye yakazini,siye kupiga dole

Neno hili sikubali,laa! Liwe ni utani"

Pia Katika tamthiya ya NGOMA YA NG'WANAMALUNDI ngomezi inadhihirika Katika (uk48)kama


ifuatavyo

Wote(pale ukumbini wanaitikia isipokuwa chipupa)

Sasa wakati umefika wa kucheza ngoma ya

Ng'wanamalundi........"
Hivyo matumizi ya ngomezi Katika fasihi andishi unadhihilisha kuwa mwandishi wa fasihi andishi ni
mkocho wa wakocho.

Matumizi ya taswira ;hii ni mbinu ya kutumia lugha ya picha.katika diwani ya " hekima za
wahenga"mwandishi ametumia taswira mbalimbali mfano Katika (uk35) Katika ubeti wa 5 Katika shairi
la" matango na vibamia"mwandishi anasema

"Kila kitu alikula,matango na vibamia

Utakavyo utalala,cha mende au ngamia

Hata kule palapala,vyovyote tajendea...."

Pia Katika tamthiya ya "ngoma ya ng'wanamalundi"mwandishi ametumia taswira mbalimbali kwa mfano
Katika (uk20) mwandishi anasema

"Vizuu(wanapiga kelele za uoga vilevile)

Aaah.....!wuuu!(eanarudi nyuma

na kujikunyata rundo moja kwenye Kona)

Chidama(anawakemea kwa nguvu) KELELE

(Kimya)melon!

Hivyo kupitia matumizi ya taswira Katika kazi ya fasihi andishi inadhihirisha kuwa hata mwandishi wa
kazi za fasihi ni mkocho wa wakocho.

Hivyo basi sio kweli kuwa msanii wa fasihi simulizi ndio mbobezi wa wabobezi (mkocho wa wakocho)
hata msanii wa fasihi andishi ni mbobezi wa wabobezi kwani wasanii wa fasihi andishi kama vile
ushairi,riwaya, na tamthiya wamekuwa wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali Katika kazi zao pia
wamekuwa wakitumia ubunifu Katika kazi zao lengo la kutumia ubunifu ni kufanya kazi zao ziwe na
uvuto kwa wasomaji pia kujitofautisha na waandishi wengine lengo lingine ni kupunguza kazi za
kikasuku.

MAREJELEO

Mapunda H.W(2021)Hekima za wahenga Toleta international L.T.D Dodoma, Tanzania.

Mbogo E (2008)Ngoma ya Ng'wanamalundi.Dar es salaam:Nyambali nyangwine publisher

You might also like