Aina Mbalimbali Za Bima

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

1.

BIMA YA AJALI – PERSONAL ACCIDENT

Bima hii hutolewa kwa mtu mmoja mmoja kutegemea na daraja alilo nalo.
Bima hii hulipa mbima pindi akipata ajali wakati wowote awapo Kazini au nje ya mazingira ya
kazi.
Madaraja ya bima hii hutegemea kazi ya mbima na umri wake. Kwa mfano:-

Janga Daraja 1 Daraja 2 Daraja 3 Daraja 4

Kifo na ulemavu 0.2% 0.215% 0.275% 0.3%

Wahusika wa madaraja tajwa:-


1. Maafisa, wauza maduka na wenye kazi zisizo hatarishi
2. Madreva, wafanyakazi viwandani, wajenzi, maafisa wa kazi za ukinzi, wanafunzi kati ya
miaka 10-25, wasafirisha bidhaa(salesmen) nk.
3. Walinzi, Polisi, na wanajeshi wafanyakazi migodini na wote wanaofanya kazi hatarishi
4. Wafanyakazi wa tensheni kubwa ya umeme na kazi hatarishi kama hiyo.

3. BIMA YA NISHIKE MKONO

Bima hii hutolewa kwa vikundi mbali mbali vilivyo na watu kuanzia kumi kwa minajili ya
kusaidia mwana kikundi pindi akipata majanga kutokana na ajali, kuugua ugonjwa sugu au kufa.
Aidha bima hii, hulipa mbima endapo mtegemezi wake akipatwa janga la kifo.
Faida ya bima hii ni pamoja na kuwa uhakika wa pesa endapo janga lililo tajwa hapu awali
likitokea kwake au kwa mtegemezi wake. Ada yake ni shs.48,000/= kwa mwaka kwa kila
mwana kikundi.

2. Bima ya vikundi - Group Credit life Assurance.

Bima hii hutolewa kulinda mtaji wa kikundi pindi mwanakikundi akipatwa janga la
kumsababisha asipate uwezo tena wa kuzalishq kipato kama awali. Kwa mfano ugonjwa sugu
kama kansa, figo. Kupooza, ugonjwa wa akili, ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri
(angani, nchi kavu na majini), ajali za majambazi n.k lakini pia hata kifo.

Bima hii huhakikisha amana ya kikundi inabaki kama ilivyo kwa kulipa masalia ya deni lote la
mwanachama aliyepatwa janga hilo. Hivyo kikundi huwa na uhakika wa pesa zao hata
mwanachama akipatwa lolote la kumsibu. Ada ya bima hutegemea kiasi cha mkopo wa
Mwanakikundi. Hivyo mwanakikundi akiisha lipa tu mara moja halipi tena hadi mwakani.

Ili kukata bima hii lazima upate majibu ya maswali yaliyo kwenye ambatanisho.

Kwa hiari ya kikundi


Kikundi kinaweza kuongezea fao la msiba wa mwanachama. Fao hilo hulipwa pindi
kunapotokea mwanachama akafariki, bima hutoa shillingi isiyozidi 1mill kusaidia shughuli za
msiba. Hivyo wanakikundi hawatembezi daftari.

2. BIMA YA MAISHA NA KITEGAUCHUMI – LIFE ASSSURANCE

Bima hii hulipwa kwa kipindi cha kuanzia miaka saba. Lengo la bima hii ni kumwezesha
mwanachama kujiwekea lengo la kufanya, pindi muda huo ukifika k.m. kununua shamba,
kujenga nyumba, kusomesha mtoto, kuoa n.k,

Bima hii hutenganishwa katika pande mbili za Maisha na akiba (investment). %age ya pande
zote hupangwa na mteja mwenyewe.

Kwa mfano: mteja anaweza kupanga :

Maisha 30% (lengo k.m. nyumba, shamba)

Akiba (savings) - 70%

Wakati mbima anaweka bima hii huenda anataka baada ya miaka saba ajenge nyumba. Bahati
mbaya akafariki baada ya kuchangia miaka miwili tu. Bima itamlipa pesa yake ya AKIBA(70%)
mara moja lakini 30% ambayo ni ya ujenzi haitalipwa, bali kampuni ya bima itaendelea
kuichangia kwa siku zilizo baki zote na kulipwa siku ya kumaliza mkataba ili mrithi ajenge
nyumba iliyo kusudiwa na mbima.

Kiwango cha kuchangia hutegemea umri wa mwanachama na anataka kuweka kiasi gani na kwa
kipindi gani.

4. BIMA YA MOTO (FIRE INSURANCE AND OTHER PERILS)

Bima ya moto hutoa kinga ya fidia kwa chobo kilcho wekewa kinga endapo kitungua kwa moto
halisi au radi. Lakini huenda mbali zaidi kulipa fidia kwa majanga ya mafuriko, upepo mkali,
sunami , matetemeko, moto kutokea jirani n.k

Ada yake hutegemea aina ya jengo linalo wekewa bima. Kwa mfano jengo:-

A) Aina ya jengo:
i) Mjengo ni wa matofali, udongo au mbao
ii) Aina ya patisheni: matofali , mbao au siling bodi
Iii) Jengo limeezewa kwa bati, vigae au makuti n.k

B) Shughuli za Jengo –
I) Makazi, mashule maktaba, nyumba za ibada na ofisi -0.15%
II) Hospitali, nyumba za michezo, klabu zinazotoa chakul (club and mess houses) -
0.175
III) Mghahawa, kiosk na duka lisilouza vitu hatarishi, bakery,
nyumba za udobi n.k – 0.2 %

5. BIMA YA WIZI (Burglary)

Bima ya wizi hukinga janga la kuibiwa kwa njia ya kutumia nguvu wakati wa kuingia au kutoka
wakati wizi unatendeka (yaani lazima mwizi avunje au abomoe ukuta au paa).
Ada yake ni 6% ya thamani ya mali iliyo wekewa kinga.

Madai huanzia Tshs 500,000/=

You might also like