Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

Posta House cell: +255 766 898 722

Ohio/Ghana (TEHE] Cell: +255 762 042 483


Avenue llala District
Email: tehetrusttz@gmail.com
P.O.
REG.BOX
NO.8525 REG. NO. 000535
Dar es Salaam Ref.No.TEHECORR/105/2023

Date: 06TH AUGUST, 2023

Mr. KIONYWAKI,

MWENYEKITI,

ST. ROSALIA,

ENGLISH MEDIUM SCHOOLS,

DAR ES SALAAM.

YAH: UTOAJI UELEWA WA KINGA YA FIDIA

Kichwa cha barua hapo juu chahusika.

Rejea mazungumzo yetu yaliyofanyika kwa njia ya simu tarehe 06/08/2023; ikihusu somo hilo
hapo juu.

Tanzania Education, Health & Economic Organization (TEHE), ni asasi iliyosajiriwa chini ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na kupewa namba ya usajiri na.
00NGO/R2/000535, tarehe 27/08/2019.

TEHE ikishirikiana na TIRA tumeamua kutoa uelewa wa kinga ya fidia kwa jamii ili iweze
kuondokana na wasiwasi, hofu na hasara pindi inapopatwa na majanga mbalimbali ambayo
hurudisha nyuma maendeleo ya jamii. Aidha ndoto za wanajamii hazitimii kwa sababu ya
kutotumia huduma ya kinga ya fidia kwa sababu tu jamii haina uelewa huo.

St. Rosalia schools, ni mojawapo ya shule zenye mtaala wa Kingereza. Wazazi wa wanafunzi
ni jamii yetu, ambao wengi wao hawana uelewa wa kinga ya fidia, lakini wangetaka kupata
uelewa na huduma hiyo, ili waimarishe uchumi wao, lakini pia watimize ndoto zao kwa watoto
wao.

Kinga ya fidia ya ulemavu wa kudumu utokanayo na maradhi au ajali, na kifo, ndiyo suluhisho
pekee la kuwaondolea msongo wa mawazo (stess) , kwa wazazi, wote wenye ndoto ya watoto
wao wapate elimu bora na maadili mema. Tuna imani kuwa mzazi akiwa na uelewa huu na
kupata huduma hii atakuwa na amani ya moyo na kumsababisha ashughulike na kazi zake bila
wasiwasi wala hofu .

Kwa barua hii tunakuomba kukutana na pia kukutana na kamati yako ya shule ili tuwape
uelewa mpana kuhusu kinga ya fidia hususan ya ” School Fees Guarantee” ili nao waweze
kuijua na kuieleza vizuri kwa wazazi wenzao.

Tumeambatanisha vielelezo vyetu kwa uthibitisho wako.

Wako katika ujenzi wa taifa.

BASIL M. BINTAMANYIRE.
KATIBU MKUU.

You might also like