Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

MPANGO WA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI

Wazo hili la biashara linalenga zaidi mradi wa ufugaji wa kuku wa


mayai (layers) utafanyika katika wilaya ya Sumbawanga Rukwa-
Tanzania. Mtaa wa Utengule, Kata ya Lwiche.

Yaliyomo
1.0 MAELEZO YA MRADI.......................................................................................................................
1.1 Mfano wa Uendeshaji........................................................................................................................
1.1.1 Bidhaa lengwa na soko...................................................................................................................
1.1.2 Pembejeo na ujuzi unaopatikana.....................................................................................................
1.2 Uwezo wa kufanya kazi.........................................................................................................................
1.3 Athari au uvumbuzi wa mfumo wa soko...............................................................................................
1.4 CHANGAMOTO ZA USHINDANI.....................................................................................................
1.5 UENDELEVU WA MRADI.................................................................................................................
2.1 MAKADIRIO YA MAPATO YA MRADI...........................................................................................
3.1 FAIDA YA MRADI…………………………………………………………………………………………………………………………3

4.1 BAJETI YA KUFUGA KUKU.............................................................................................................


5.0 HITIMISHO..........................................................................................................................................

1.0 MAELEZO YA MRADI


1.1 Mfano wa Uendeshaji
1.1.1 Bidhaa lengwa na soko
Mradi huo utahusisha uzalishaji wa mayai kutoka katika ufugaji wa kuku hao
nitakaofuga katika sehemu hiyo kutokana na upungufu wa bidhaa hii na
watumiaji kuongezeka kumekuwa na ufinyu wa upatikanaji wa bidhaa hii ya
mayai ndio maana nikaona fursa katika wazo hili pia Sumbawanga ndio eneo la
uzalishaji na itatupatia masoko ya kawaida na Hoteli ambapo tunaweza kuuza
bidhaa zetu. Soko letu kuu litakuwa watumiaji wa majumbani, migahawa na
hoteli. Pia kwa wauzaji wa jumla na rejareja
Kwa uzoefu nilionao kwa aina hii ya ufugaji nilioanza kufuga kuanzia mwaka
2019 hadi sasa, kutokana na ufinyu wa mtaji nimekuwa nikifuga kienyeji na
kushindwa kupata mapato ya kutosha, kama nitafanikiwa kupata mkopo huu
nitaweza kufuga kisasa zaidi na kupata mapato ya kutosha yatakayowezesha
kurejesha mkopo huu kwa wakati.
1.1.2 Pembejeo na ujuzi unaopatikana
Mbegu bora za kuku wa mayai zinapatikana katika mashamba ya
utotoleshaji wa kuku wa mayai na nyama maarufu kama Mama Patricia
kutoka Mbeya au Silverland kutoka Iringa, pia uagizaji wa cage za
kufugia kuku kutoka Dar es Salaam. Pia Sumbawanga wapo wataalam wa
mifugo juu ya magonjwa makubwa na madogo kulingana na hali ya hewa
pia upatikanaji wa chakula na madawa katika wilaya yetu kutoka kwa
washauri wa mifugo.

1.2 Uwezo wa kufanya kazi.


Mradi huo utafuga kuku 500 ambao nitaweza kuzalisha trei za mayai kati ya 15
hadi 20 kwa siku na kuuza bei rafiki kwa mtumiaji ya Tsh 7,500/= kwa trei
moja na hii ni muendelezo wa kwa miaka miwili mfululizo hii itapelekea kutoa
fursa kwa vijana watakao nisaidia kufikisha bidhaa kwa wateja na pia watakao
nisaidia kulisha na kufanya usafi katika banda la kuku,

1.3 Athari au uvumbuzi wa mfumo wa soko


Mradi utafanya soko la mayai kwa gharama ya chini na bora zaidi. Mayai yana
soko tayari, watumiaji wa majumbani, wauzaji reja reja na wauzaji wa jumla
ambao watakuja wenyewe sehemu yetu ya shamba la ufugaji pia kuwafikishia
wateja walioko mbali kidogo. Mahitaji ya mayai ni mwaka mzima na watumiaji
na wauzaji wengi wataenda kutafuta mayai kupitia simu au kusafiri hadi mahali
pa uzalishaji Sumbawanga Kata ya Lwiche Mtaa wa Utengule. Soko letu
linaloweza kushughulikiwa pia litakuwa moja kwa moja kwa watumiaji wa
nyumbani, wauzaji reja reja na wauzaji wa jumla, migahawa, hoteli, maduka
madogo na makubwa, kwa ujumla.

1.4 CHANGAMOTO ZA USHINDANI


Mayai kutokana na asili yake na hali yake ya asili huzalishwa karibu kote
nchini Tanzania na Watanzania wengi hufanya kibiashara biashara ya mayai. Ni
rahisi kuanzisha bila kujali magonjwa ambayo ni kikwazo kwa kuku wa
mayai. Mahitaji ni makubwa sana, nitatakiwa kutoa ajira kwa kijana mwenye
uzoefu ili kuhudumia idadi kubwa ya wateja ili kuondokana na changamoto
nyingine kwa mazingira ya biashara.,
1.5 UENDELEVU WA MRADI
Mradi huo utatumia teknolojia ya kisasa ya ufugaji ambayo itatumia ufugaji
kwa njia ya cage ambazo na rahisi na salama katika ufugaji na hufanya kuku
wasipate magonjwa ambukizi kwa urahisi. Hii itafanya ufugaji endelevu,
Uzalishaji utakuwa mwaka mzima. bila kujali msimu wa masika au kiangazi.
Uzalishaji utafanywa kwa kiwango kinachohitajika, mayai yanayozalishwa
yatafaa kuuzwa katika maduka makubwa. Ya jumla na rejareja .Tutakuwa
tukishawishi
wauzaji wengine wa jumla ili kuhakikisha kasi ya mauzo ya bidhaa zetu
itakuwa ya juu na endelevu. watu walio karibu na eneo la mradi wanatarajiwa
kutumia ujuzi nitakaokuwa natoa kama darasa bure kwa mifano ili kuendelea
kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja baada kupata ujuzi wa mradi huu na
kupunguza idadi ya vijana walioko mtaani bila kujishughulisha.

2.1 MAKADIRIO YA MAPATO YA MRADI.


Mradi huu utakuwa na mapato ya mauzo ya karibu 4,500,000/= Tshs . Mauzo
yanaanza baada ya miezi 4 na wiki mbili baada ya kupata vifaranga.

3.1 FAIDA ZA MRADI


Mradi huu utatoa faida zifuatazo;
1. Kuzalisha kipato kifedha.
2. Kutoa fursa ya ajira kwa vijana.
3. Kuzalisha samadi bora kwa kilimo.
4. Chakula
4.1 BAJETI YA KUFUGA KUKU
BAJETI YA KUFUGA KUKU 500
MAHITAJI QNT COST TOTAL
CAGE 4 850,000 3,400,000
KUKU 500 2,600 1,300,000
CHAKULA (STASTER) 5 90,000 450,000
CHAKULA (GROWER)) 10 80,000 800,000
JUMLA YA GHARAMA ZA MAHITAJI 5,950,000

MADAWA NA CHANJO
GLUCOSE 1 2,000 2,000
TRIMAZINE 10 8,500 85,000
POWERVIT 2 8,500 17,000
NEWCASTEL VACCINE 2 6,000 12,000
GUMBORO VACCINE 2 7500 15,000
VITANIN (AMIN TOTAL) 2 60000 120,000
JUMLA YA GHARAMA ZA MAHITAJI 251,000

JUMLA YA GHARAMA KUU 6,201,000

5.0 HITIMISHO

Mradi huu utakuwa ni funguo ya fursa ya kuondoa umasikini katika jamii


inayotuzunguka na kuamsha ari ya watu kupambana dhidi ya umasikini.
Utainua kipato changu, jamii na serikali kwa ujumla na kuongeza pato la
serikali.

You might also like