Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

UJUMBE MUHIMU KWA SINGLE MOTHER'S WOTE.

MCHUNGAJI KELVIN ZAKARIA MAKOYE.


Hawa ni wale wanawake wote ambao wamezalishwa, wamezaa na badae kutelekezwa au
kujiondoa wenywe Kwa wanaume na wengine wapo kwenye NDOA lakini waume zao
hawafanyi majukumu Yao Kila kitu ni juu ya mama.
UJUMBE HUU KWA WALE WALIOTEREKEZWA na Wale ambao licha ya kwamba wapo
kwenye NDOA wao ndio mama ndio Baba, mwanaume hahusiki na chochote
ZABURI 18:1
1.Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana
>> KAULI hii Daudi alisema pale Mungu alipomtoa vichakani porini alikokuwa anachunga
kondoo na kumfanya kuwa MFALME. Kilichomfanya Daudi kuwa MFALME sio nguvu zake
sio elimu yake Bali ni Mungu Kwa hiyo Daudi ANATAMBUA neema ya Mungu kwenye
maisha yake MKONO WA MUNGU kwenye maisha Yake ulivyomtoa kule porini.
✓. Mungu anakuona mahali AMBAPO Wanadamu hawakuoni, mahali AMBAPO Unafikiri
watu ,hawakuoni mwanaume hakuoni Mungu anakuona.
✓. Mahali AMBAPO jicho la Mwanadamu haliwezi kufika jicho la Mungu linafika.
Kwahyo hata kama watu wamekuacha jangwani ni kama hakuna anayekuona Tena.Nina Habari
njema Juu yako wewe mwanamke.
MITHALI 16:7
7 Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye
>> Adui yako WA kwanza ukimtoa shetani ni huyo mwanaume aliyekuacha, Kwa hiyo kama
huyo ndio adui yako kinachokupasa kufanya sio kumlilia bali njia zako zimpendeze Bwana.
Njia zako zikimpendeza BWANA utakuwa wa thamani( ISAYA 43:4) machoni pa Bwana Hata
huyo mwanaume aliyemtelekeza huyo mtoto atarudi.
>> Kwasasa hupaswi kujipendekeza kwake hupaswi kumuonyesha kwamba umepungukiwa
atakutesa atakuwa anakuja anazini na wewe anakuongezea stress( mawzo) Magonjwa
anakutukana. Bali Amua kufunga vioo kama yeye Alivyoamua kwenda mbali wewe fanya
yafuatayo.
1 _. MPE MUNGU MOYO WAKO_
_ Mithali 23:26
26 Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu
>> Maana yake Moyo wako ukishampendeza Mungu anaanza kukuonyesha wapi ukanyage wapi
upite ni wapi uelekee,nini ufanye nini uguse ili uwe na MATOKEO kwenye maisha
yako,AMUA KURUDI KWA MUNGU.
MATENDO 3:19
19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa
kuwako kwake Bwana
ISAYA 54:1....
1 Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe
usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye
aliyeolewa, asema Bwana.
>> Mungu anaonyesha watu walioachwa Wana thamani Gani mbele zake , Kwahyo Usiogope
_Bali anasema ongeza uwezo WA Kumjua Mungu Ndani yako, na huyo mtoto uliyeachiwa
atamiliki mataifa atakuwa mkuu
✓ Watu wote WAKUU unaowaona Duniani WALITELEKEZWA na baba zao au mama zao,
wengine walitupwa chooni lakini wewe usimtupe mwanao ,haijarishi unapitia kipindi kigumu
kiasi gani fata hiki ninachokwambia.
Andiko la msingi tumwamgalie Mwanamke anayeitwa HAJIRI > Huyu,alikuwa mjakazi Katika
nyumba ya Ibrahimu na Sara, baada ya Sara kuchelewa kuzaa,Ibrahimu alizaa na HAJIRI baadae
Sara akaanza kumpiga vita Hajiri na kumwambia Ibrahimu amfukuze.
MWANZO 21:9-13
9 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu,Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa
mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.
12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo
mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka
uzao wako utaitwa.
13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri
akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-
sheba.
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema,
Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17 *Mungu akasikia sauti ya kijana.* Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni,
akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, *kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa
kubwa.*
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji,
*akamnywesha kijana.*
20 *Mungu akawa pamoja na huyo kijana* , naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga
upinde.
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri
>>> Kwahyo tunaona Pamoja na Kwamba anafukuzwa Kwa Ibrahimu, Hajiri anaondoka na
mtoto wake lakini Mungu anasema atamfanya kuwa taifa kubwa
>> Haijarishi huyo mtoto uliyenaye watu wamemuona sio wakawaida wamemdharau, huyo
mwanaume amemuacha lakini Mungu anataka kuja kumfanya kuwa taifa , *Kwahyo usimchukie
huyo mtoto kwasababu baba yake amemwacha usimtamkie maneno mabaya* mara unafanana
tabia na baba yako, nakuchukia kwasababu baba yako amekuacha, *hapana* _mpende huyo
mtoto kwasababu ni Mtumishi WA Mungu._
*Ukisoma Habari hiyo mpaka mwisho* UTAONA Hajiri anaondoka Kwa Ibrahimu Hana Mali
Wala fedha Bali mkate na maji mwisho maji yanaisha yupo jagwani *hajui anatoa wapi* badae
anakata tamaa anamweka mwanae pembeni ili asimwone akifa *alikata tamaa kabisa* akijua
kinachofata ni kifo badae *Mungu anamtokea* anasema nimesikia kilio Cha mwanao badae
anamuonyesha kisima anapata maji mwanae anakunywa na Biblia inasema *Mungu Akawa
pamoja na yule kijana*
*Kwa Taarifa yako huyu kijana ndio amezaa mataifa 12 ya waarabu yanayomiliki visima vya
mafuta unaona wote hao Dubai wanatembelea Baraka ya huyu Mtoto.*
>>KWAHYO ndani ya huyo mtoto, hao watoto ulioachiwa Kuna HAZINA kubwa
*USIOGOPE* Mlingane Mungu.
*Yeremia 17: 5,7*
5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye
mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana
>> Utakapoendelea kumfikiria huyo mwanaume na kuipuuza NAFASI ya Mungu kwenye
maisha yako maandiko yanasema utakuwa umelaaniwa, usimtegemee huyo mwanaume na si
KWAMBA umdharau hapana na siku akiamua kurudi usimzuie lakini wakati Huu ambao
amekuterekeza wewe wekeza Kwa BWANA
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto;
Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka
wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda
>> Kwanini unalia, kwanini umekata tamaa , kwanini unaona kama haiwezekani?, Leo kupitia
haya maandiko na Huu ushuhuda kupitia Biblia TAKATIFU *nyenyuka upya MWANANGU*
wewe SINGLE MOTHER'S uliyeachiwa watoto au wewe mama uliyeko ndani ya ndoa lakini
baba hatoi chochote kile ni kama vile mzigo wote amekuachia wewe emu haya maandiko yakutie
moyo .

You might also like