Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 44

GODIUS RWEYONGEZA

JINSI YA
KUFIKIA
ndoto
zako TOLEO LA 2

Usipofanyia kazi ndoto zako,


kuna mtu atakuajiri ili ufanyie
kazi Ndoto zake

GODIUS RWEYONGEZA

www.songambele.co.tz Page 1
GODIUS RWEYONGEZA

(Songambele)
www.songambele.co.tz
Vitabu Vingine Vya Mwandishi Huyu

Songambele siyo mgeni kwenye ulimwengu wa


uandishi, vitabu vyake ambavyo vimesaidia watu
wengi ni pamoja na vifuatavyo:

NAKALA NGUMU (HARDCOPIES) ZOTE


ZILIZOPO

1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000).


(hardcocopy)

2. Kutoka sifuri MPAKA KILELENI (20,000)


(hardcocopy)

3. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE (hardcocopy


20,000/-)

4. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA


MAFANIKIO MAKUBWA (hardcocopy)

5. AKILI YA DIAMOND (hardcocopy 10,000/-)

6. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO


(Hardcopy 20,000

www.songambele.co.tz Page 2
GODIUS RWEYONGEZA

7. Kipaji ni dhahabu: Jinsi ya kugundua, kunoa na


kuendeleza kipaji chako

VITABU VILIVYOSOMWA KWA SAUTI


(AUDIOBOOKS)

1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000).


(hardcocopy)

2. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE (hardcocopy


20,000/-)

3. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA


MAFANIKIO MAKUBWA (hardcocopy)

4. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO


(Hardcopy 20,000

VITABU VYA NAKALA LAINI/NAKALA TEPE/


(SOFT COPY/EBOOKS)
1. Maajabu ya kuwkekeza kwenye hisa, hatifungani na
vipande
2. Mambo 55 ya Kuzingatia kabla ya KUANZISHA
BISHARA (Softcopy 5,000)

www.songambele.co.tz Page 3
GODIUS RWEYONGEZA

3. JINSI YA kuibua ubunifu ulio ndani yako ($oftcopy


5,000)

4. MAAJABU ya kusoma vitabu (free ebook &


Audiobook)

5. MAAJABU ya kuweka akiba (($oftcopy 10,000))

6. JINSI ya kuwa mwandishi MBOBEVU ($oftcopy


10,000)

7. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo Ni


rasilimaliwatu tunaowapoteza(volume 1) ($oftcopy
10,000)

8. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA,


HATIFUNGANI NA VIPANDE ($oftcopy 10,000)

9. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kugundua kipaji


chako, kukinoa na kukiendeleza ($oftcopy 10,000)

10. Nguvu ya kuweka malengo (10,000)

11. Zama zimebadilika: Maisha yamebadilika, ajira


hatarini na wewe badilika (10,000)

12. Mwongozo wa wapambanaji (10,000)

13. Ngvu ya ushindi iliyo ndani yako (10,000)

www.songambele.co.tz Page 4
GODIUS RWEYONGEZA

JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

GODIUS RWEYONGEZA
(Songambele)
www.songambele.co.tz

www.songambele.co.tz Page 5
GODIUS RWEYONGEZA

Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako

©GODIUS RWEYOGEZA

Toleo la kwanza Agosti, 2020


DAR ES SALAAM, TANZANIA

Toleo la pii, Aprili,2022


DAR ES SALAAM, TANZANIA

Haki zote zimehifadhiwa


Hakuna sehemu yoyote ile ya kitabu inaruhusiwa
kutolewa upya, kunakiliwa au kuhamishwa kwa
namna yoyote ile. Iwe ni kwa njia zinazofahamika
sasa hivi au zitakazogunduliwa hapo baadaye bila
idhini ya mwandishi.

ISBN: 978-9976-5526-7-6

Mawasiliano: Godius Rweyongeza

Barua pepe: songambele.smb@gmail.com


Tovuti: www.songambe.co.tz
YouTube: Godius Rweyongeza
Facebook: @godiusrweyongeza
Instagram: godius_rweyongeza
Simu: +255 755 848 391

www.songambele.co.tz Page 6
GODIUS RWEYONGEZA

YALIYOMO

Vitabu Vingine Vya Mwandishi Huyu....................................2


TABARUKU...........................................................................6
DIBAJI ....................................................................................7
UTANGULIZI.......................................................................12
Barua Ya Wazi Kwako Ndugu Msomaji...............................12
MGAWANYO KITABU HIKI.............................................20
SEHEMU YA KWANZA .....................................................22
UMUHIMU WA NDOTO NA CHANGAMOTO
ZINAZOWAZUIA WATU KUISHI NDOTO
ZAO................................................................................23
SURA YA KWANZA...........................................................26
Tambua Ndoto Yako .............................................................26
SURA YA PILI .....................................................................40
Wito Kwenye Ndoto Kubwa .................................................40
SURA YA TATU ..................................................................48
Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kabla Ya
Kuachana Na Ndoto Yako..............................................48
SEHEMU YA PILI................................................................54
JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ..................................55
SURA YA NNE ....................................................................57
Mbinu Tisa Unazopaswa Kuzingatia Ili Uweze
Kufikia Ndoto Zako .......................................................57
SURA YA TANO..................................................................69
Je, Unazijua Gharama Unazopaswa Kulipa Ili Kufikia
Ndoto Zako? ...................................................................69
SURA YA SITA....................................................................82

www.songambele.co.tz Page 7
GODIUS RWEYONGEZA

Vigingi Sita Utakavyokutana Navyo Wakati


Unatimiza Ndoto Zako ...................................................82
SURA YA SABA ..................................................................90
Ukweli Kuhusu Ndoto, Na Inaonekana Hujawahi
Kuujua Ukweli Huu .......................................................90
SURA YA NANE..................................................................95
Kitu Kibaya Zaidi Ya Kutokuwa Na Macho Ya Kuona
(Utashangaa Kujua Kitu Hiki Cha Kipekee)..................95
SURA YA TISA....................................................................98
Zingatia Hivi Wakati Unaiendea Ndoto Yako ......................98
SURA YA KUMI ................................................................103
Kauli Ya Kishujaa Ya Kusema Unapokuwa
Umekwama Na Watu Wanaonekana Kwenda
Kinyume Chako............................................................103
SURA YA KUMI NA MOJA .............................................106
Hasara Zitakazojitokeza Endapo Wewe Utaacha
Kutimiza Ndoto Zako...................................................106
SURA YA KUMI NA MBILI.............................................110
Hawa Ndiyo Wezi Rasmi Wa Ndoto Zako .........................110
SURA YA KUMI NA TATU..............................................119
Jitahidi Kwenda Kinyume Na Mazoea (Usijiwekee
Ukomo, Unaweza Kufanya Zaidi Ya Hapo) ................119
SURA YA KUMI NA NNE ................................................127
Kitu Cha Kufanya Ndoto Yako Inapohusisha Watu
Wa Nje..........................................................................127
SEHEMU YA TATU ..........................................................132
HIVI NDIVYO NILIVYOTIMIZA NDOTO ZANGU ......133
SURA YA KUMI NA TANO .............................................135

www.songambele.co.tz Page 8
GODIUS RWEYONGEZA

Arnold Shwarzenegger ........................................................135


SURA YA KUMI NA SITA ...............................................141
Curtis James Jackson III (50 Cent)......................................141
SURA YA KUMI NA SABA..............................................147
Elon Musk ...........................................................................147
SURA YA KUMI NA NANE .............................................152
Strive Masiyiwa...................................................................152
HITIMISHO ........................................................................156
Ndoto Inahitaji Uwe Kichaa................................................157
KUHUSU KITABU: ...........................................................169
KUHUSU MWANDISHI....................................................171

www.songambele.co.tz Page 9
GODIUS RWEYONGEZA

TABARUKU

Kwa wadogo zangu Makrina na Claudia.

Kwangu mwenyewe, kila mara nitakaposoma au


kushika kitabu hiki, nikumbuke juu ya ndoto yangu
kubwa ya kujenga chuo kikuu kikubwa barani Afrika
(Harvard of Africa)

www.songambele.co.tz Page 10
GODIUS RWEYONGEZA

DIBAJI

Nikiwa Mkubwa Nataka Kuwa....

K
umbuka kipindi cha maisha yako, ulipokuwa
mtoto, kati ya miaka mitano mpaka 10, hicho
ni kipindi ambacho kila mtu alikuwa
anakuuliza swali hili; ukiwa mkubwa unataka kuwa
nani?

Uzuri wa kipindi hicho ni kwamba, ulikuwa


mwaminifu, ulikuwa unaeleza kile kilicho ndani yako
na hukuwa na shaka yoyote. Ulipoulizwa ukiwa
mkubwa unataka kuwa nani, huenda ulijibu bila
wasiwasi, nataka kuwa
mwalimu/msanii/fundi/daktari/polisi/rubani na
mengine.

Ulijibu bila ya wasiwasi na bila ya hatia kwa sababu


ulijua unavutiwa na nini na uliona wengine waliofika
huko na hukuwahi kufikiria kwamba unaweza usiwe
kama wao.

Uzuri mwingine wa kipindi hicho cha miaka 5 mpaka


10 ni kwamba hata wale waliokuuliza walikubaliana
na majibu yako, hawakukukatisha tamaa,

www.songambele.co.tz Page 11
GODIUS RWEYONGEZA

hawakukuambia huwezi, walikubaliana na wewe,


walifurahi kuwa una ndoto kubwa na waliamini nguvu
iliyo ndani yako.

Tatizo lilikuja pale ulipoendelea kukua, huku ukiwa


kwenye mfumo wa elimu. Ulipoanza kushindanishwa
na watoto wengine kupitia mitihani ya darasani,
matokeo yako yalianza kutumika kupima ndoto zako.

Kama matokeo yalionesha unashindwa mtihani huku


wenzako wakishinda kwa maksi za juu, watu walianza
kukuambia baadhi ya ndoto zako haziwezekani.
Ulipomaliza darasa la saba na matokeo kutoka, hapo
ndipo hukumu kubwa ya maisha yako ilipotangazwa.
Kama ulifaulu vizuri basi imani kwenye ndoto yako
iliendelea kuwa hai. Ila kama hukufaulu basi watu
walianza kukosa imani kwenye ndoto yako.

Tumeona kipindi cha utoto kikiwa kizuri kwa mtu


kuchagua ndoto yoyote anayovutiwa nayo. Lakini pia
kipindi hicho kina hatari yake, ambayo ni kuamini kile
ambacho watu wazima wanakuambia.

Hivyo, kulingana na matokeo yako ya mtihani wa


mwisho, watu wazima waliokuzunguka walianza
kukuambia ndoto yako haiwezekani tena. Kwa kuwa

www.songambele.co.tz Page 12
GODIUS RWEYONGEZA

ulikuwa mtoto na kwa kuwa uliona watu hao wazima


wanajua mambo mengi kuliko wewe, basi ulikubaliana
nao kwamba ndoto yako haiwezekani tena.

Hali hiyo ya kifo cha ndoto huwatokea watu kwenye


hatua tofauti za makuzi, kuna ambao inawatokea
mapema pale wanaposhindwa mtihani wa darasa la
saba, wengine mtihani wa kidato cha nne, wengine
mtihani wa kidato cha sita.

Aliyekuwa anasema ndoto yake ni kuwa rubani,


alipofaulu darasa la saba aliendelea kuaminiwa na
ndoto yake, lakini aliposhindwa kidato cha nne, imani
ya ndoto yake iliishia hapo. Aliyevuka kidato cha nne
na ndoto yake, ilienda kuishia kidato cha sita au
chuoni.

Sehemu kubwa ya watu kwenye jamii zetu wanafanya


kazi au biashara ambazo siyo ndoto walizokuwa nazo
utotoni. Baada ya kipimo cha mtihani kutumika na
kuambiwa hawawezi tena kufikia ndoto zao,
walikubaliana na hukumu hiyo na kuona kuwa
wanapaswa kufanya kile kinachowezekana ili waishi
maisha yao.

www.songambele.co.tz Page 13
GODIUS RWEYONGEZA

Kwa wale walioendelea kusisitiza ndoto zao hata


baada ya kuambiwa haziwezekani tena, waliambiwa
waache utoto, wapambane na maisha, washukuru kwa
kile walichopata.

Na huenda wewe ni mmoja wa watu hao, umeizika


ndoto yako na kukubaliana na wale waliokuhukumu
miaka mingi iliyopita.

Ni jambo la kushukuru kwamba leo umepata bahati ya


kipekee, ya kujifunza jinsi unavyoweza kuzifikia
ndoto zozote ambazo umewahi kuwa nazo kwenye
maisha yako.

Kwenye kitabu hiki cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO


ZAKO, mwandishi Godius Rweyongeza ametuonesha
kupitia mifano ya watu mbalimbali ambao wamefikia
ndoto zao, kwamba inawezekana kwa kila mtu kufikia
ndoto yoyote aliyowahi kuwa nayo kwenye maisha
yake.

Haijalishi umri, jinsia au rangi, yeyote anayeamua


kweli kwamba anataka kufikia ndoto yake, basi
anaweza kuifikia.

Lakini safari haitakuwa rahisi, hasa ukizingatia jamii


iliyopelekea uizike ndoto yako bado inakuzunguka.
www.songambele.co.tz Page 14
GODIUS RWEYONGEZA

Itakubidi uchague kuwa kichaa, uchague


kutokueleweka na uwe tayari kuweka juhudi kwa
muda mrefu.

Uzuri ni kwamba, juhudi hizo unazoweka


hazitakuchosha, kwa sababu unafanyia kazi kile
ambacho ni ndoto yako, kile ambacho unakipenda. Na
kwa kufanya hivyo, hutanufaika tu wewe mwenyewe,
bali utawanufaisha wengine pia.

Aliyekuwa mwandishi na mwanafalsafa wa nchini


Marekani, Howard Thurman amewahi kunukuliwa
akisema; “Usijiulize ulimwengu unataka nini, bali
jiulize ni kitu gani kinachokufanya wewe uwe hai,
kisha kifanye hicho, kwa sababu ulimwengu
unachotaka ni watu walio hai.”

Kuwa hai ni kuziishi ndoto zako, kuwa hai ni kufanya


kile ambacho kinatoka ndani yako kweli, ambacho ni
kusudi la wewe kuwa hapa duniani. Kama huziishi
ndoto zako, haupo hai, unasukuma tu siku ukisubiri
kuzikwa.

Tumshukuru Godius ambaye anatupa nafasi nyingine


ya kuwa hai, kwa kutupa maarifa sahihi ya kuzifufua

www.songambele.co.tz Page 15
GODIUS RWEYONGEZA

ndoto zetu na kuziishi, bila kuruhusu chochote kuwa


kikwazo kwetu.

Nisikucheleweshe kuyapata maarifa haya adimu sana


kwako, yatakayo kuwezesha kuishi ndoto ya maisha
yako. Nikuambie kitu kimoja tu, soma kitabu hiki na
kisha panga kuchukua hatua mara moja. Usiendelee
tena kusubiri, usiendelee tena kuwa mfu, chagua
kuanza kuishi sasa, kwa kuiishi ndoto kubwa ya
maisha yako.

Kama utasoma kitabu hiki na ukaendelea kubaki hapo


ulipo, hutakuwa na wa kumlaumu tena, utakuwa
umechagua kuishi kama mfu wewe mwenyewe, kitu
ambacho siyo tu kibaya kwako, bali pia ni maumivu
kwa wengine, kwa sababu una ndoto kubwa ambazo
zingeweza kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora.

Nikutakie kila la kheri kwenye maisha mapya ya


ndoto yako unayokwenda kuanza, yatakufanya uwe
hai na ulimwengu unufaike pia.

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio,


Mwandishi Na Mjasiriamali,

www.songambele.co.tz Page 16
GODIUS RWEYONGEZA

www.amkamtanzania.com

www.songambele.co.tz Page 17
GODIUS RWEYONGEZA

UTANGULIZI

Barua Ya Wazi Kwako Ndugu Msomaji

Uwe na ndoto kubwa kama vile utaishi milele na ishi


leo kama vile utakufa kesho.

“S
ehemu yenye utajiri mkubwa hapa duniani
siyo kwenye machimbo ya almasi katika
nchi za Amerika Kusini, au kwenye
machimbo ya dhahabu Afrika Kusini. Aidha, sehemu
tajiri siyo kwenye visima vya mafuta katika nchi za
Uarabuni wala kwenye visima vya gesi huko Urusi.
Sehemu tajiri hapa duniani ni kwenye makaburi.
Kama makaburi yangekuwa yanachimbwa kama watu
wanavyochimba dhahabu, basi wachimbaji wa
makaburi, wangetengeneza utajiri mkubwa sana. Kwa
nini?

Ukweli ni kwamba, makaburini ndiko kuliko na ndoto


ambazo hazikuwahi kufanyiwa kazi. Huko kuna vitabu
ambavyo havikuwahi kuandikwa, kuna mawazo
ambayo hayakuwekwa kwenye vitendo, kuna nyimbo
ambazo hazikuwahi kuimbwa, viwanda ambavyo
havikuwahi kujengwa, michoro ambayo haikuwahi

www.songambele.co.tz Page 18
GODIUS RWEYONGEZA

kuchorwa na ugunduzi ambao haukuwahi kufanyika”


alisema Dr. Myles Munroe.1

Kitabu hiki cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO


kimekuja na mwongozo wa kukusaidia wewe kufanya
mambo makubwa katika maisha yako. Ni wazi
kwamba, kila mtu katika hatua fulani ya maisha, huwa
anakuwa na ndoto ya kufikia kitu fulani. Watoto ndiyo
huongoza kwa kuwa na ndoto kubwa na za kipekee.
Ukiongea na mtoto mdogo atakuambia ndoto yake
kubwa, tena kwa kujiamini kabisa. Ila kadiri mtoto
anavyokua, ndoto yake inapotea taratibu hadi inafikia
hatua ya anapoisahau.

Inashangaza kukuta kwamba mtu aliyekuwa na ndoto


kubwa katika hatua fulani ya maisha, ameshaipoteza
na wala haikumbuki kabisa. Kwa mfano, mtu
aliyekuwa na ndoto ya kuwa mwigizaji, inashangaza
kumkuta akiwa ameshasahau ndoto yake na akiishi
maisha ya kawaida.
1 Maneno haya yamekuwa yakisemwa na Dr. Myles Munroe.
Ameyaandika pia kwenye kitabu chake cha Understanding Your
Potential Hata hivyo, vyanzo vingine mtandaoni vinaonesha
kwamba maneno haya yalisemwa na Les Brown. Steve Jobs naye
aliwahi kunukuliwa akisema; “kuwa mtu tajiri kaburini siyo kitu
ambacho ningependelea. Ila kwenda kulala usiku nikisema kwamba
nimefanya kitu cha maana ndio jambo la maana zaidi.”

www.songambele.co.tz Page 19
GODIUS RWEYONGEZA

Kwa watu wengine siyo tu kwamba wanakuwa na


ndoto kubwa, bali pia vipaji vya kipekee. Lakini kadiri
siku zinavyoenda, hivyo vipaji vyao wanavipoteza
taratibu. Matokeo yake, ndiyo unakuta kwamba, mtu
huyo amekuwa mlalamishi, mtu wa kuomba misaada,
mwenye tabia ya kuwachukia watu waliofanikiwa na
hata kuanza kujiona kwamba hakuwahi kuwa na
bahati maishani mwake. Lakini kumbe, alikuwa na
dhahabu kubwa ya ndoto yake ambayo hakuwahi
kuifanyia kazi. Sasa, anachofanya mtu huyo ni
kusogeza siku ili ifike hatua atakapokufa na hiyo
ndoto yake.
Ukweli huo, ndiyo unaoyafanya makaburi yawe na
utajiri wa vitu vizuri ila ambavyo havikuwahi
kufanyiwa kazi. Ndiyo maana, Benjamin Franklin
(Januari 17, 1706- April 17, 1790) aliwahi kusema
kuwa, kuna watu wanakufa wakiwa na umri wa miaka
25, lakini wanazikwa wakiwa na umri wa miaka 75.
Maana ya kauli hiyo ni kwamba, watu wengine
wanakufa wakiwa bado vijana; kwa kushindwa kuishi
ndoto zao. Hivyo, wanapita tu kwenye maisha bila
mwelekeo huku wakifanya vitu wasivyovipenda
mpaka wanapofariki na kuzikwa makaburini.
Kwa nini watu wanakufa wakiwa na ndoto zao?
Kitabu hiki sasa, kitalijibu swali hilo kiupana zaidi. Je,
inawezekana mtu akaifanyia kazi ndoto yake na
ikatimia? Je, kuna uwezekano wa mtu kuwa na ndoto

www.songambele.co.tz Page 20
GODIUS RWEYONGEZA

zaidi ya moja na zote akazifanyia kazi? Je, ndoto hasa


inapaswa itoke wapi na nitajuaje kwamba hii ni ndoto
ambayo ninapaswa kuifanyia kazi au la? Yote hayo na
zaidi, tutayazungumzia kwa undani kadiri
tutakavyokuwa tunaendelea kufunua kurasa za kitabu
hiki.
Mara nyingi watu huwa wanadhani kwamba ndoto
zipo kwa ajili yao. Yaani, watu wanaacha kutimiza
vitu walivyonavyo ndani yao, kwa kuona kwamba
wao ndiyo wamiliki wa hivyo vitu. Hivyo, wanaweza
kuvitoa au la! Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na
wimbo akawa haoni shida ya kuuimba kwa sababu
wimbo anao ndani yake. Na mwingine anaweza kuwa
na igizo, akawa haoni haja ya kulitoa kwa sababu lipo
ndani yake. Hivyo, kwake suala la kuigiza au
kutoigiza hilo igizo ni sawa tu. Kwa mwingine,
kuchora au kutochora huo mchoro ni sawa tu. Na kwa
mwingine, kutumia uwezo wake wa kiuongozi au
kutoutumia ni sawa tu.
Ninachofahamu mimi ni kwamba, kuna kitu unacho
kwa dhamana ila siyo chako. Ukitaka kunielewa hapa
nitatolea mfano wa mwanamuziki. Mwanamuziki
anaimba wimbo yeye, ila ule wimbo haumburudishi
yeye tu. Unakuburudisha wewe na mimi. Hebu fikiria
wimbo wowote ule ambao wewe unaupenda. Siyo
kwamba wimbo ule uliuimba wewe. Hapana, aliimba
mtu mwingine ila wewe unanufaika na huo wimbo.

www.songambele.co.tz Page 21
GODIUS RWEYONGEZA

Tena hata mwanamuziki mwenyewe anahitaji


mwanamuziki mwingine kumburudisha. Fikiria juu ya
simu au kompyuta. Vifaa hivi hujatengeneza wewe.
Kuna mtu ambaye ametengeneza vifaa hivi, ila yeye
havitumii peke yake. Ametengeneza yeye, ila wewe
ndiye unanufaika. Kwa namna hiyo hiyo, ndivyo
itakavyotokea kwa ndoto yako.
Ndoto unakuwa nayo wewe, ila wanufaikaji ni wewe
mwenye ndoto na watu wengine. Tena unakuta
kwamba, hao wengine wananufaika zaidi ya wewe
unavyonufaika, kupitia hiyo ndoto yako. Asili (nature)
ilivyo ni kwamba, kadiri unavyowasaidia watu zaidi
kupata kile wanachotaka nawe unapata kile
unachotaka, tena unapata zaidi. Hivyo, kadiri
unavyotimiza ndoto yako na ikawasaidia watu wengi
zaidi, ndivyo na wewe unavyonufaika zaidi.
Hapo ulipo, umevaa nguo. Hizo nguo hazikuwa ndoto
yako wewe. Kuna mtu alikuwa na ndoto hiyo na
kuiweka katika uhalisia. Leo hii, wewe unanufaika
zaidi ya yeye aliyetimiza ndoto yake akiwa wa
kwanza. Inawezekana wewe unabadilisha nguo mara
tatu kwa siku, wakati mwenye ndoto ya kutengeneza
nguo hiyo hakuwahi kufanya hivyo.
Kama sasa hivi umeajiriwa, ama ndugu yako
ameajiriwa, unapaswa kujua kwamba umeajiriwa hapo
kwa sababu kuna mtu aliyetekeleza ndoto yake. Kama

www.songambele.co.tz Page 22
GODIUS RWEYONGEZA

hiyo ndoto yake angeificha, basi wewe usingekuwa


umeajiriwa hapo. Inawezekana sasa hivi, mtaani
kwenu kuna vijana ambao hawana ajira, ila mwajiri
wao ni wewe. Wewe una ndoto ambayo ukiifanyia
kazi, utawaajiri hao, ila tu hujafanya hivyo. Na
pengine inawezekana wewe unalalamika sasa hivi
kuwa hakuna ajira. Kwa taarifa yako, hupaswi
kulalamika kwa kukosa ajira, wakati umebeba ajira za
watu wengine.
Sasa ngoja nikuulize swali hili: je, unaenda kuifanyia
kazi ndoto yako au unaenda kuyanufaisha makaburi?
Kama wewe uamuzi wako ni kuzifanyia kazi ndoto
zako na kuifanya dunia iwe sehemu nzuri sana, basi
sura za kitabu hiki zinakuhusu. Katika kitabu hiki,
nimeeleza hatua kwa hatua kuanzia pale unapopata
ndoto mpaka kuifikia. Utakutana na mambo ya msingi
ambayo unapaswa kuyafuata katika kufikia ndoto
zako. Pia, utakutana na gharama ambazo utapaswa
kulipa ili kufikia ndoto zako na mwisho kabisa,
nimekuwekea mifano ya watu ambao wameweza
kufanya mambo makubwa na kutimiza ndoto zao.
Utaweza kujifunza kutoka kwa watu wa aina hii na
kuona ni kwa jinsi gani na wewe unaweza kuanza
kufanikisha ndoto zako leo.
Baada ya kusoma kitabu hiki, ni matarajio yangu
kwamba, utafikia uamuzi na kusema; “sitaki kufa na
ndoto zangu, badala yake nitatumia uwezo wangu

www.songambele.co.tz Page 23
GODIUS RWEYONGEZA

wote kuhakikisha kwamba ninafanya makubwa hapa


duniani.”
Kuna kitu kimoja hapa nitakisema waziwazi, ingawa
chaweza kukushtua. Ukweli ni kwamba, mimi
ninakudai. Ndiyo ninakudai! Ninakudai biashara hiyo
unayoifikiria kuianzisha miaka nenda, miaka rudi ila
unasita kuianzisha. Ninakudai bidhaa hiyo uliyokuwa
unataka kutengeneza ila sasa hata huchukui hatua ili
kuanza kuitengeneza. Ninakudai kitabu hicho,
ninakudai igizo lako hilo.
Inawezekana na mimi ningekuwa shabiki mzuri wa
mpira, ila kwa sababu tu wewe umeamua kukizika
kipaji chako na kuitokomeza ndoto yako ya kuwa
mchezaji wa kimataifa, leo hii mimi ninashindwa
kuwa shabiki wa mpira. Ninakudai. Inawezekana pia,
mfumo wa usafiri ambao tunao sasa hivi, ulipaswa
kuwa umeboreshwa zaidi, ila sasa kwa sababu wewe
umejificha huko hutaki kuweka ndoto yako kwenye
uhalisia, basi ujue kwamba ninakudai. Ninaomba ulipe
deni langu haraka iwezekanavyo kwa kuanza kufanyia
kazi ndoto yako.
Kwa uchunguzi wangu, watu wengi hawajui mambo
mengi kuhusu ndoto. Napenda ufahamu kwamba,
wewe ukishindwa kutimiza ndoto zako, unakuwa
unawazibia mwanya watu wengine kutimiza ndoto
zao. Mfano mzuri tu ni kwenye simu janja

www.songambele.co.tz Page 24
GODIUS RWEYONGEZA

(smartphone). Bila shaka unamfahamu Steve Jobs


(Mwanzilishi wa kampuni ya Apple, (1955-2010)).
Huyu ndiye alitengeneza simu janja ya kwanza. Kwa
kufanya hivyo, amewawezesha watu wengi zaidi
kutimiza ndoto zao kwa viwango vikubwa. Kuna watu
wametengeneza viunzi (apps) na kuviweka kwenye
simu. Mimi na wewe tunavitumia viunzi hivyo. Ndiyo
kusema kwamba Steve Jobs alikuwa amebeba ndoto
za watu wengi sana.
Steve Jobs alizaliwa katika kipindi ambacho kompyuta
zilikuwa zinanunuliwa na kumilikiwa na watu
wachache, taasisi au makampuni makubwa tu. Yeye,
kichwani mwake alikuwa na ndoto ya kwamba ifikie
hatua kompyuta ziweze kumfikia kila mtu kwenye
nyumba au chumba chake. Na kweli alitimiza ndoto
yake. Kwa sababu yeye aliweza kutimiza ndoto yake
vizuri, mimi ninatumia kompyuta ambayo
alitengeneza yeye ili kutimiza ndoto yangu pia.
Ninaamini na wewe utakapomaliza kusoma kitabu
hiki, utasema lazima nitimize ndoto yangu.
Ikumbukwe kwamba, “safari ya maili elfu moja,
huanza na hatua moja.” Kama methali ya Kichina
inavyosema. Nami ninasisitiza kwamba unapaswa
kuanza kutimiza ndoto yako hapohapo ulipo, kwa
kutumia rasilimali zilizopo. Katika hili Strive
Masiyiwa (Januari 29 1961; bilionea wa Zimbabwe na
mwanzilishi wa kampuni ya Econet) anaweka mkazo

www.songambele.co.tz Page 25
GODIUS RWEYONGEZA

mkubwa anaposema, kanuni za kufanikiwa bado ni


zilezile.
1. Unaanza na kile ulichonacho.
2. Unafanya kile unachoweza.
3. Unawekeza unachopata ili uweze kupata
kikubwa zaidi.
Kama hutafanyia kazi ndoto zako, kuna vitu vitatu
ambavyo vitatokea.
Kwanza, utasikia kwenye vyombo vya habari kwamba
vijana machachari sehemu fulani, wameweza kufanya
mambo makubwa. Wakati nawe, ulipaswa kuwa
kijana machahari kama hao wanaotajwa.
Pili, utaanzisha usemi utakaokuwa unautoa kama
hadithi kwa watoto mpaka kwa wajukuu wako.
Utaanza kuwaambia, bwana mnamwona fulani,
nilisoma naye ila sasa hivi hashikiki. Kama si hivyo
huenda ukasema kwamba, nilikuwa ninakaa naye
darasa moja ila sasa hivi amefanikiwa sana. Utasema,
kuna kipindi huyu mtu alikuwa na maisha mabaya ila
sasa hivi maisha yake yamebadilika sana. Au pengine
utasema, mimi ndiye nilikuwa kinara darasani na huyu
jamaa hakuwahi hata kuonekana kwenye zile kumi
bora. Binafsi, nimekuwa ninawavumilia sana wazee
ambao wanasema hivi. Ila wewe, sitakuvumilia hata
kidogo.

www.songambele.co.tz Page 26
GODIUS RWEYONGEZA

Nitakuuliza, wakati hawa wanapambana wewe


ulikuwa wapi? Ni kitu gani kilikuzuia wewe kufanya
makubwa? Je, hawa watu walikufunga kwenye mti
wakaanza kuchapa kazi, sasa ndiyo wamekuja
kukufungua? Kiukweli sitakuvumilia.
Tatu, utawalazimisha wanao wafanye kitu ulichokuwa
unapenda kufanya. Kiukweli zimekuwepo kesi nyingi
za vijana kutaka kusomea kitu fulani ila wazazi wao
wakawa wanaghairisha na kutaka watoto wasomee
kitu kingine. tena wazazi wanatisha kuwa endapo
mtoto hatasomea kitu hicho basi hawatamsomesha
hata kidogo. hii ni dalili kuwa mzazi alikuwa na ndoto
ya kufikia kitu fulani ila hakukifanyia kazi hicho kitu
basi anatumia nguvu yake ya ukubwa na fedha
kumlazimisha mwanae afanye alichotaka yeye
kufanya.
Ninachotaka kukwambia leo ni kuwa fanyia kazi
ndoto zako, na watoto wako watatimiza ndoto zao.
Nakutakia kila la kheri.
Kwa maneno hayo yaliyolenga kukuchokoza kifikra,
ninakukaribisha rasmi ili usome kitabu hiki.
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Wasalaam.

www.songambele.co.tz Page 27
GODIUS RWEYONGEZA

Godius Rweyongeza
24 Juni, 2020

MOROGORO-.

www.songambele.co.tz Page 28
GODIUS RWEYONGEZA

MGAWANYO KITABU HIKI

Kitabu hiki cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako


kimegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya
kwanza, inahusisha sura ya kwanza mpaka ya tatu.
Sura hizi zipo mahususi ili kuhakikisha kwamba
unaitambua ndoto yako.

Sehemu ya pili inahusisha sura ya nne hadi sura ya


kumi na nne. Sura hizi zitakuonesha uhalisia wa safari
ya kufikia ndoto zako na nini unapaswa kufanya ili
uweze kuzifikia.

Sehemu ya tano, inaanzia sura kumi na nne mpaka


kumi na nane. Katika sehemu hiyo, tutakutana moja
kwa moja na hadithi za watu waliokuwa na ndoto,
wakazifanyia kazi mpaka kuzitimiza. Kwenye eneo
hili, utakutana moja kwa moja na safari ya kutimiza
ndoto ya watu kama Elon Musk, 50 Cent, Strive
Masiyiwa na Arnold Schwarzenegger

www.songambele.co.tz Page 29
GODIUS RWEYONGEZA

www.songambele.co.tz Page 30
GODIUS RWEYONGEZA

SEHEMU YA
KWANZA

“Unaweza kuwa na meli bora sana, na


ukawa na nahodha mzuri kuliko wote
duniani, ila kama haujui unaelekea wapi,
ujue utazunguka huku na huko na mwisho
wa siku hautafika sehemu ya maana.”

ARNOLD SHWARZENEGER

www.songambele.co.tz Page 31
GODIUS RWEYONGEZA

UMUHIMU WA NDOTO NA
CHANGAMOTO ZINAZOWAZUIA WATU
KUISHI NDOTO ZAO

Sababu kubwa inayowafanya watu washindwe kufikia


mambo makubwa maishani ni kwa sababu hawajui
haswa ni kitu gani wanahitaji. Ndio, unaweza
kushagaa kila siku unakutana na watu wanafanya kazi
kwa bidii na kujituma ila kumbe watu hawa hata
hawajui ni kitu gani wanahitaji.

Ni sawa na mtu ambaye anaenda kutafuta fedha kila


siku, katika hali ya kawaida mtu wa aina hii
tunategemea kuwa atakuwa na uelewa mkubwa sana
kuhusu masuala ya fedha. Ila uhalisia ni kuwa asilimia
kubwa ya watu wanaenda kazini kufanya kazi ili
kupata fedha, ila hawajui haswa jinsi fedha
inavyofanya kazi.

Kwa hiyo, ni muhimu sana kwako kutambua ni kitu


gani hasa unahitaji maishani mwako. Unapaswa
kufahamu pia jinsi ambavyo unaweza kukifikia hicho
kitu na gharama ambazo unapaswa kulipa ili kuweza
kukifikia huko unapoelekea.

www.songambele.co.tz Page 32
GODIUS RWEYONGEZA

Karibu sana kwenye sehemu hii ya kwanza ambayo


itakufanya utambue ni kitu gani haswa unahitaji
maishani mwako. Na kiufupi sio kwamba unahitaji
vitu vingi unahitaji kitu kimoja tu, yaani ndoto yako.

Binafsi nakubaliana na Joseph Musharika ambaye


anasema kuwa; “kama watu wengi wangejua ni kitu
gani haswa wanapaswa kufanya hapa duniani, basi ni
wazi kuwa idadi ya watu wanaojiua ingekuwa ni sifuri
au hakuna kabisa”, ila kinachotokea ni kuwa asilimia
kubwa ya watu hawajui haswa ni kitu gani ambacho
wanahitaji maishani mwao.

Ndio maana sehemu hii ya kwanza, inalenga


kukusaidia wewe hapo kujua haswa ni kitu gani
ambacho unahitaji. Ndio, sehemu hii ipo ili kukusaidia
kuiweka sawa ndoto yako.

Pengine umekuwa ukiishi maisha ya kawaida, lakini


sasa umefika muda wa wewe kubadili maisha yako.
Maana muda pekee ambao unafanya maamuzi
makubwa kwenye maisha yako na kujitoa kuyatimiza,
ndio muda ambao unakuwa umebadilisha maisha
yako.

www.songambele.co.tz Page 33
GODIUS RWEYONGEZA

Kama utangulizi kuonesha makubwa unayoenda


kupata kwenye sehemu hii, huyu hapa ni Mwalimu
Deogratias Kessy akisema ya kwake kuhusu hiki
kitabu

Kwa mtu yeyote yule ambaye ana ndoto kubwa lakini


hajui wapi kwa kuanzia napendekeza asome kitabu
cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako kwa kupitia kitabu
hiki mtu anapata mwongozo sahihi wa kumwezesha
kufikia ndoto zake.

Kwangu kitabu hiki ni mwongozo wa kufikia ndoto


zangu; kwa mtu ambaye hana menta anaweza kutumia
hiki kitabu na kikamwongoza kufikia mafanikio
makubwa ya ndoto zake.

Kitabu kimesheni mifano mbalimbali ya watu


mashuhuri walioanzia Sifuri Kabisa Mpaka Kufikia
Kileleni.

Kama wao wameweza basi hata wewe utaweza.


Nashauri kwa mtu mwenye ndoto kubwa basi akifanye
kitabu cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako kuwa rafiki
wake wa karibu.

www.songambele.co.tz Page 34
GODIUS RWEYONGEZA

Kila mara watu wenye ndoto kubwa wamekuwa


wananiuliza nisome kitabu gani cha kunisaidia mimi
kufikia ndoto zangu? Bila kusita huwa napendekeza
kitabu hiki cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako kwa
sababu kimeandikwa kwa lugha rahisi na mifano
mbalimbali ya kumpa mtu matumaini na hamasa ya
kuendelea kupambana mpaka kufikia ndoto
alizojiwekea

Haya sasa twende zetu tukasome sura ya kwanza.

www.songambele.co.tz Page 35
GODIUS RWEYONGEZA

Hello, habari.
Kitabu hiki cha jinsi ya kufikia ndoto
zako kinaptikana,
Hardcopy ni 20,000/=
Na audiobook ni 10,000/= tu.

Kupata nakala ya kitabu hiki,


wasiliana na (+255) 0755 848 391
kwa whatsap, SMS au simu ya
kawaida.
BONYEZA HAPA:
https://api.whatsapp.com/message/3P
MZSAFONLHAP1?autoload=1&app
_absent=0

www.songambele.co.tz Page 36
GODIUS RWEYONGEZA

Uhondo zaidi upo ndani ya


kitabu hiki. USIACHE
KUPATA NAKALA YAKO
LEO HII

BONYEZA HAPA sasa


https://api.whatsapp.com/mess
age/3PMZSAFONLHAP1?aut
oload=1&app_absent=0

www.songambele.co.tz Page 37
GODIUS RWEYONGEZA

KUPATA KITABU HIKI


CHOTE, TUWASILIANE
0755848391 au bonyeza hapa
Au bonyeza hapa kukipata
https://api.whatsapp.com/me
ssage/3PMZSAFONLHAP1?aut
oload=1&app_absent=0

www.songambele.co.tz Page 38
GODIUS RWEYONGEZA

KUPATA KITABU HIKI


CHOTE, TUWASILIANE
0755848391 au bonyeza hapa
https://api.whatsapp.com/mess
age/3PMZSAFONLHAP1?aut
oload=1&app_absent=0

www.songambele.co.tz Page 39
GODIUS RWEYONGEZA

VITABU VYANGU
VINGINE HIVI HAPA
NAKALA NGUMU (HARDCOPIES) ZOTE
ZILIZOPO

1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000).


(hardcocopy)

2. Kutoka sifuri MPAKA KILELENI (20,000)


(hardcocopy)

3. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE (hardcocopy


20,000/-)

4. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA


MAFANIKIO MAKUBWA (hardcocopy)

5. AKILI YA DIAMOND (hardcocopy 10,000/-)

6. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO


(Hardcopy 20,000
7. Kipaji ni dhahabu: Jinsi ya kugundua, kunoa na
kuendeleza kipaji chako

VITABU VILIVYOSOMWA KWA SAUTI


(AUDIOBOOKS)

www.songambele.co.tz Page 40
GODIUS RWEYONGEZA

1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000).


(hardcocopy)

2. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE (hardcocopy


20,000/-)

3. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA


MAFANIKIO MAKUBWA (hardcocopy)

4. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO


(Hardcopy 20,000

VITABU VYA NAKALA LAINI/NAKALA TEPE/


(SOFT COPY/EBOOKS)
1. Maajabu ya kuwkekeza kwenye hisa, hatifungani na
vipande
2. Mambo 55 ya Kuzingatia kabla ya KUANZISHA
BISHARA (Softcopy 5,000)

3. JINSI YA kuibua ubunifu ulio ndani yako ($oftcopy


5,000)

4. MAAJABU ya kusoma vitabu (free ebook &


Audiobook)

5. MAAJABU ya kuweka akiba (($oftcopy 10,000))

6. JINSI ya kuwa mwandishi MBOBEVU ($oftcopy


10,000)

www.songambele.co.tz Page 41
GODIUS RWEYONGEZA

7. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo Ni


rasilimaliwatu tunaowapoteza(volume 1) ($oftcopy
10,000)

8. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA,


HATIFUNGANI NA VIPANDE ($oftcopy 10,000)

9. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kugundua kipaji


chako, kukinoa na kukiendeleza ($oftcopy 10,000)

10. Nguvu ya kuweka malengo (10,000)

11. Zama zimebadilika: Maisha yamebadilika, ajira


hatarini na wewe badilika (10,000)

12. Mwongozo wa wapambanaji (10,000)

13. Ngvu ya ushindi iliyo ndani yako (10,000)

www.songambele.co.tz Page 42
GODIUS RWEYONGEZA

Hello, habari.
Kitabu hiki cha jinsi ya kufikia ndoto
zako kinaptikana,
Hardcopy ni 20,000/=
Na audiobook ni 10,000/= tu.

Kupata nakala ya kitabu hiki,


wasiliana na (+255) 0755 848 391
kwa whatsap, SMS au simu ya
kawaida.
BONYEZA HAPA:
https://api.whatsapp.com/message/3P
MZSAFONLHAP1?autoload=1&app
_absent=0

www.songambele.co.tz Page 43
GODIUS RWEYONGEZA

www.songambele.co.tz Page 44

You might also like