Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 13

HULKA ZA WATU

(TEMPERAMENTS)

Joel Wang’uba Okello


KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MBEYA MJINI
HULKA ZA WATU (TEMPERAMENTS)
Utangulizi

Hulka ni tabia ya asili ya mwanadamu isiyoonekana kwa macho bali kwa matendo. Tabia
hii inategemea mtu na mtu, na kwamba kila mmoja ana sehemu/kundi lake. Yakobo 2:17
hutueleza kuwa Imani iendane na matendo hii itatusaidia kujua hulka ya mtu isiyojulikana.

Mungu pekee ndiye ajuaye kila kitu hatuwezi kumficha chochote. Katika utendaji kazi wa
kanisa Mungu alichunguza hulka ya kila mtu na ndio maana wengine ni wachungaji,
wainjilisti, walimu, wafalme,mitume na manabii, Mfano Daudi. Kama tusipojua nafasi ya
hulka katika utendaji kazi wa kanisa/ biashara/ kazi yoyote huduma hiyo inaweza
kudidimia. Kwa nini? (aliyepewa nafasi hana hulka ya uongozi/ hamasisha).

Kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu ni lazima lizingatie huduma za kanisa kulingana


na hulka ya kila mmoja. Roho Mtakatifu anaweka karama sawasawa na apendavyo yeye
kwa kufuata hulka ya kila mmoja ndani yake. Kama wewe ni mpole/ mkimya si dhambi
bali ni nafasi ya kanisa kukutumia unapostahili ili kuujenga mwili wa Kristo. Kama wewe
ni mbunifu na mtu wa ratiba si dhambi bali ni kazi ya kanisa kukuweka katika huduma
ambayo utaleta mapinduzi ya kiroho kwa haraka sana na kubuni mikakati ya Injili.

UMUHIMU WA KUJUA HULKA ZA WATU

Kujua hulka za watu hutusaidia:-

a. Kuwajua watu vizuri

b. Kushughulika na watu kwa urahisi

c. Kuchukuliana na watu kwa uvumilivu

FAIDA ZA MTU KUELEWA HULKA ZA WATU

1. Kutengeneza pale palipo na udhaifu :

Mfano:-

 Kuthibiti hasira na kiburi (Koleriki)

 Kuthibiti hali ya kutojiamini au kukosa ujasiri(Melankoli)

 Kuthibiti tabia ya kuongea kupita kiasi(Sanguine)

 Kuthibiti uvivu na kuwa mchapakazi(Flegmatiki)


MAKUNDI YA HULKA (Temperaments)

Mwanafalsafa aliyeitwa Hippocrates alikuwa wa kwanza kuwaweka watu katika makundi


manne (4).

Makundi hayo ya hulka yalijulikana kama ‘’Temperaments”. Neno Temperaments linatoka


katika lugha ya kilatini na lina maana ya kuchanganya kwa vipimo. Hippocrates
alizungumzia kuchanganya vitu vya majimaji, na majina manne yalimjia mawazoni
ambayo ni;

1. Sanguine

2. Choleric

3. Melancholy

4. Phlegmatic

JINSI YA KUGUNDUA HULKA YAKO

Ili kugundua hulka yako jibu maswali yafuatayo kwa uaminifu.

i. Je huwa ninachukua hatua(react) ya kujibu mapigo muda ule ule ninapotendewa


jambo au huwa sifanyi haraka kuchukua hatua kujibu mapigo kwa jambo
nililotendewa?

ii. Je huwa mimi ni mwepesi wa kutenda mara moja au huwa nabaki mtulivu na kusubiri?

iii. Je huwa natunza kwa muda mrefu hisia kwa jambo lililotendwa kwangu au natunza
kwa muda mfupi tu na kisha kutoweka?

iv. Je ninapokosewa naweza kusamehe?

v. Je huwa ninakuwa na kinyongo na kuchukia ninapotukanwa?

Ikiwa majibu yatakuwa yafuatayo basi mtu huyo ana hulka ya Choleric au Melancholy.

a) Kwa kawaida siwezi kusahahu matusi niliyotukanwa nayakumbuka kwa muda mrefu
na ninapoyakumbuka na kuyafikiria najisikia vibaya.

b) Naweza kuwa na kinyongo dhidi ya aliyenikosea kwa muda mrefu kwa siku nyingi
na kwa majuma mengi

c) Huwa nawakwepa wale walionikosea , sitaki kukutana nao

d) Huwa sitaki kuzungumza na wale walionikosea


Lakini majibu yakiwa yafuatayo basi mtu huyu ana hulka ya sanguine au phlegmatic

a) Situnzi hisia mbaya

b) Siwezi kumkasirikia mtu kwa muda mrefu

c) Huwa ninasahau upesi matusi niliyotukanwa

d) Wakati fulani naelekea kuwa na hasira lakini naidhibiti.

Baada ya kugundua kuwa yeye anaweza kuwa na hulka aina ya choleric au melancholy,
anapaswa kujibu maswali yafuatayo ili ajue hulka yake hasa ni ipi kwamba ni choleric au
melancholy.Maswali hayo ni:-

a) Je, huwa ninaonyesha kwa haraka hali ya kutaka kupambana dhidi ya mabaya
niliyotendewa?.

b) Je, huwa nadhihirisha chuki yangu kwa maneneo au kwa matendo?

c) Je, huwa ni mwepesi kutukana ninapotukanwa?

d) Je, huwa ninapotendewa mabaya nabakia mtulivu kwa nje lakini kwa ndani nikiwa
nahangaika na kuumia?

e) Je, huwa naogopa kupoteza tumaini kiasi kwamba nakosa maneno yafaayo na ujasiri
kwa kujibu na hivyo kuamua kunyamaza kimya?

f) Je, inatokea mara kwa mara ya kwamba sijisikii vibaya muda ule ule ninapotendewa
ubaya lakini baada ya saa chache au kesho yake ndiyo naanza kuwa na hisia kwa
ubaya niliyotendewa?

Kama jibu ni ndiyo kwa swali la (a)-( c) basi mtu huyo ana hulka ya Choleric

Na kama jibu la swali la (d)-(f) ni ndiyo basi mtu huyo ana hulka ya Melancholy

Jibu likiwa ni ndio kwa maswali yafuatayo basi mtu huyo ana hulka ya Sanguine. Maswali
hayo ni:-b

a) Je, huwa natunza hasira ghafla dhidi ya mabaya niliyotendewa?

b) Je, ninakuwa mwepesi kukasirika nakutenda kwa haraka bila kufikiri?

Kama jibu kwa maswali yafuatayo ni ndiyo basi mtu huyo ana hulka ya Phlegmatic.

a) Je, sisumbuliwi na hisia zangu kwa urahisi?

b) Je, huwa nabaki mtulivu, asiyejali ninapotendewa mabaya?


1: SANGUINE- Bwana mtazamia mema
SILIKA YAKE
 Anajipenda/nadhifu
 Anapenda sifa na kutambuliwa kuwa yupo
 Ni muongeaji sana/mtoa hadithi nyingi
 Mchangamfu na anapenda mizaha,/ kuchekesha
 Hana msimamo wala aibu
 Kutokubali kushindwa na kutazamia mzuri(optism)
 Si mwepesi wa hasira

SANGUINE KAMA MZAZI

Familia inakuwa na furaha muda wote: Mama/Baba anachekesha watoto , kuwapa


hadithi za hapa na pale na kucheza nao
Anabadilisha tatizo kuwa kitu cha kawaida:Hubadili ukubwa wa tatizo kuwa wa
kawaida ili kuinusuru familia kukosa furaha
Anasahau majukumu ya watoto: Huingilia majukumu ya watoto na kuwafanya
wasahau ni nini majukumu yao.
Hana Mpangilio: Kazi zake ni za kushitukiza tu_hakuna ratiba
Hasikilizi mpaka mwisho: ni mwepesi kudakia na kusema nimekuelewa kumbe hajui
lolote.
Ana hasira za haraka: Hushindwa kujitawala na kufanya maamuzi bila kufikiria.

SANGUINE KATIKA KAZI

Ni mtu wa kujitolea:Ni wepesi kujitolea kufanya kazi hata kama ni ngumu haiwezi
Ni muhamasishaji mkubwa : Hushawishi wengine kufanya kazi hata kama hawaziwezi
Huanza kazi kwa mbwembwe: Akianza kufanya kazi utadhani itaisha kwa muda mfupi
kwa sababu ya madoido yake
Hakati tamaa mapema na hufanya uamuzi haraka sana
Kwenye kikao anapenda kujua agenda mapema
Anahitaji kusimamiwa: Muda mwingi anautumia kuongea na kutafuta wapi kuna kundi
la watu wamejikusanya.
Mwepesi kusahau majukumu yake:Kazi inaweza isiishe kwa muda uliopangwa na yeye
haoni tatizo.
Hafuati mpangilio: Anaangalia kazi inayombana ndio anahangaika nayo kwanza. Ni
rahisi kutengeneza madeni.
Si mtu wa nidhamu: Ni mtu wa ahadi njoo kesho kila siku kumbe hawezi kufanya, na
ukimkuta kwa bahati mbaya; nilipata dharura, tufanye kesho
SANGUINE KATIKA MARAFIKI

Anatengeneza marafiki kwa haraka sana:Hata kama ni mgeni sehemu yoyote ni


mwepesi kupata marafiki na kuongea nao

Anapenda watu:Anapenda kukaa mahali palipo na watu ili aongee nao

Anaonekana ni mtu wa nidhamu:Hufanya jambo lolote analoambiwa pasipo kupima


uzito, hata hivyo kazi humshinda.

Habebi malalamiko:Ni vigumu kulalamika mbele ya rafiki zake ila hulalamika chini kwa
chini.

Anachukia kuwa peke yake ; Kumkuta akiwa peke yake basi ameshindwa
kabisa.Anapokosekana watu/watoto /marafiki humuulizia

Anapenda kujibu maswali ya wengine:Swali akiulizwa rafiki yake kabla hajajibu yeye
tayari amekwisha msemea/mjibia

Ni mwepesi kuomba msamaha: Aligundua amekosa ni mwepesi kuomba msamaha


hata kwa kupiga magoti-janja yake ili awe salama lakini hajajutia kosa

Hapendi kusikiliza: Anachukia maongezi/maelezo marefu hivyo hukatisha kwa kuingilia


ili naye azungumze.

Anarudia hadithi: Huwa anaongea na kujisahau na kujikuta anarudia aliyoyasema


mwazo

HITIMISHO LA SANGUINE

Inapotokea ukafanya kazi/ ni rafiki wa mtu ambaye ni Sanguine unashauriwa ufanye


yafuatayo:

Muombe Mungu amsaidie kupunguza hasira

Unatakiwa kila wakati uwe na furaha

Unatakiwa uwe mwepesi wa kujua kama amekasirika au anafuraha

Usiache kumsifia katika kila jambo

Uwe mwepesi kuomba msamaha unapogundua umefanya kosa

Unatakiwa usionekana kila wakati umenyong’onyea

Mshirikishe katika kusoma Biblia na maombi


2: CHOLERIC- Bwana chuki
SILIKA YAKE

 Mgomvi na mwepesi wa hasira


 Mchapakazi hodari na mwenye akili nyingi
 Hapendi kukaa bila kazi yeyote
 Si rahisi kukatishwa tamaa
 Amezaliwa ni kiongozi( anapenda ukubwa/vyeo)
 Anajiamini katika kufanya maamuzi

Mfano: Julius Cesar, Hannibal (North Africa), Dikiteta Stalin, Hitler, Mussolini n.k

CHOLERIC KAMA MZAZI

Anatumia sauti ya uongozi: Hutumia uongozi wake hata akiwa nyumbani na


kuudhihirisha kila eneo katika familia yake

Ni mtu wa mipango: Huanzisha mipango na malengo yanayotakiwa kutimizwa na


familia

Anahamasisha familia kutenda: Hapendi kuona familia imekaa bila kazi, kama mtoto
amekaaa bila kazi anajitahidi amtafutie kazi awajibike

Kila wakati anatumia amri: Anaamrisha wakati wote na anatumia sauti ya uongozi hata
kwa mwenza wake, baba/ mama.

Hana uvumilivu kwa utendaji mbovu: Hapendi kuona kazi inafanywa chini ya kiwango
wahusika huwakemea/kuwaonya

Haachi watoto wapumzike: Watoto hawafurahii anapokuwa nyumbani maana muda


wote ni kazi tu na kusumbuana naye.

CHOLERIC KATIKA KAZI

Anatamani malengo yafikiwe: Ni mtu anayependa mipango yake itimie kama


ilivyopangwa

Ni mhamasishaji mzuri: Hapendi kuona watu wamekea bila kazi

Anatazama ukubwa wa kazï: kila kazi inaipa uthamani mkubwa na kujitahidi kuifanya
vizuri

Anatekeleza kwa haraka jambo: sio mtu wa kujivutavuta katika kazi na anasisitiza
uzalishaji
Kosa dogo ni tatizo: Unatakiwa kuwa makini unapofanya kazi na mtu huyu, kosa
kwake ni uzembe unaotakiwa adhabu

Haelezi kazi kwa kina: Anapogawa kazi haielezi kwa kina ambavyo inatakiwa
kufanyika na kwa kiwango gani

Anaweza asiheshimu mawazo ya wengine: Hupuuzia mawazo ya wengi kwa kuamini


ya kuwa akishindwa yeye hakuna mwingine anayeweza

Anachukizwa na vitu vidogovidogo: Huwa na hasira nyingi na hana huruma

Anapenda kuwa kuwa boss na si rahisi kupongeza kwa kitu kizuri

CHOLERIC KATIKA MARAFIKI

Anahitaji marafiki kidogo: si mwepesi kutengeneza marafiki

Anafanya kazi kimakundi:Anapenda kushirikiana na watu katika makundi pale tu


anapoona kuna jambo analohitaji kutoka kwao

Anaongoza na kutekeleza: Yeye ni kiongozi wa wote na huwaelekeza ni nini


kinatakiwa kufanyika.

Kila wakati yuko sahihi:Katika marafiki zake yeye anafikiri anachokifanya ni bora na
sahihi kuliko wengine wanachokifanya

Anafanya vizuri katika dharura.

Anajifanya kutumia watu; Mwanzoni ataonekana anashirikiana na wenzake kumbe


asilimia kubwa anatumia mawazo yake

Anaamua kwa ajili ya wenzake: Anaweza kuamua kwa niaba ya wenzake na uamuzi
huo ni lazima uheshimiwe.

Hawawezi kusema nimekosa: Ni mgumu wa kuomba msamaha

HITIMISHO LA CHOLERIC

Ikitokea ukawa unafanya kazi kwa karibu na choleric unatakiwa kufanya yafuatayo:

Fanya kazi kwa ubora

Usifanye bila kujua anataka ufanyeje yeye

Usijaribu kujionyesha kuwa unajua kuliko yeye

Kila hatua unayoifikia omba akueleze kabla hujaanza hatua nyingine

Usiwe mtu wa kujiamini sana bali tegemea ushauri wake kwanza


Mweleze kuwa unajisikia vizuri kufanya kazi na yeye

Mfanye ajali shida za wenzake

Mshauri awe tayari kusamehe na kuwavumilia wenzake


3. MELANCHOLY- Bwana Mkamilifu
SILIKA ZAKE

 Anapenda nyimbo/muziki na Sanaa


 Ni mkimya , asiye na maneno mengi
 Huuliza maswali kila jambo/Kuhoji
 Hufanya vitu kwa mpango( ratiba, muda)
 Si rahisi kusahau mabaya aliyotendewa
 Ni mtu wa huzuni na mwenye mawazo
 Hapendi kutawaliwa/kuwa chini ya mtu

MELANCHOLY KAMA MZAZI

Anaweka viwango vya juu: Anaamini katika mafanikio ya kiwango cha juu

Anataka kila kitu kifanyike kwa wakati: Mzazi huyu anapenda familia yake ifanye
mambo kulingana na wakati uliopangwa, hapendi mtu kutoa udhuru

Anaweka nyumba katika mpangilio mzuri: Mwanafamilia akitoka ni lazima atoe taarifa
anakwenda wapi? Na akichelewa vivyo hivyo atoe sababu za kuchelewa

Anashawishi kukuza vipaji: anapenda watoto wake wawe wabunifu kwa kuwafundisha
na kuwapa nafasi ya kufikiri kwanza.

Anakatisha tamaa watoto: Hajui kumtia moyo mtoto , ukifanya vibaya unaambiwa
live.

Anaweka malengo yasiyofikiwa: Malengo ni makubwa kuliko uwezo ulio nao familia

Hukasirishwa makubaliano yanaposhindwa kutimizwa:

MELANCHOLY KATIKA KAZI

Ni mtu wa ratiba: ukichelewa hutamkuta, anajali wakati

Anafanya kazi kwa umakini;kazi yake huvutia, hapendi kulipua kazi

Anahitaji ufafanuzi wa kina; kuepusha maswali

Ni mchumi;hatumii pesa ovyo hovyo

Anapenda kumaliza kazi alioianza

Si mtu wa watu-hupenda kukaa peke yake

Huchagua kazi ngumu; lengo apate changamoto


Ni mgumu kuridhika; hadi afanye utafiti wa kujiridhisha

Anafikiria sana kupitisha kazi:kupitisha kazi ifanyike bila kuthibisha hawezi

MELANCHOLY KATIKA MARAFIKI

Anafanya marafiki kwa tahadhari; hapendi marafiki-kukosa imani nao

Ni mwaminifu na wa kujitoa: hufanya jambo bila kulalamika

Husikiliza malalamiko; hupokea na kutatua malamiko

Hufikiria wenzake

Hutatua matatizo ya wengine

Huchukia wanaopinga jambo alilolianzisha

Hana marafiki wa karibu

Haamini mtu mwingine.

HITIMISHO LA MELACHOLY

Ikitokea unafanya kazi na mtu wa jamii ya melacholy unatakiwa ufanye yafuatayo:

Usiwe mchelewaji na mwenye kutoa udhuru

Uwe makini sana na kazi anazokupa kufanya

Hakikisha unamaliza kazi ulizopewa kwa muda na si vinginevyo

Unatakiwa uwe makini na swali analokuuliza

Usiwe na mizaha mbele zake


4. PHLEGMATIC- Bwana Mtulivu
SILIKA YAKE

Mwenda pole kwa kila jambo


Ni mtulivu mwenye subira
Anapenda amani na mwenye upendo
Muoga na mbinafsi(hatoi kitu kwa upendo)
Mvivu(mpenda starehe) na mlalamishi
Ni mvumilivu hakasirishwi kirahisi

PHLEGMATIC KAMA MZAZI

Ni mzazi mzuri:Watoto wanampenda kwa kuwa hawakemei/kuwasumbua

Anachukua muda kwa watoto: Hutumia muda mwingi kukaa na watoto

Hana haraka: hufanya mambo pole pole sana

Hakuna nidhamu: Baba/Mama hana msimamo hivyo maadili ya watoto hupungua

Hakuna mipango yoyote nyumbani; hakuna mpangilio katika kuongoza familia

PHLEGMATIC KATIKA MARAFIKI

Ni rahisi kuambatana na mtu

Ni msikilizaji mzuri

Ana huruma

PHLEGMATIC KATIKA KAZI

Hupenda kutazama wengine wakifanya kazi lakini sio yeye kufanya kazi

Anapenda sana kupumzika

Anapinga mabadiliiko

Anapenda kuhukumu wengine wanapokosea

Hasisimui; kuleta hamasa ya mabadiliko

Hapendi kujishughulisha
HITIMISHO LA PHLEGMATIC

Ikiwa unafanya kazi na mtu wa jamii ya phlegmatic au ndiye mkuu wako wa kazi,
unatakiwa ufanye yafuatayo:

Akikupa kazi usitegemee maelezo ya ziada

Uwe na ujasiri wa kufanya kazi peke yako

Anaweza kukukosoa pasipo maelekezo ya nini ufanye sasa

Omba msaada kwa rafiki mwingine kuliko yeye

Usitegemee akuite , ni lazima ujitume kumaliza kazi yako

Uwe mbunifu la sivyo hutaweza kusonga mbele.

Onyesha ujasiri wa kufanya kazi na kutoa maamuzi

MWISHO

 Je unaridhika na kuishi na tabia hiyo uliyo nayo?

 Yupo mtu mmoja tu anaweza kubadili tabia yako; YESU KRISTO MWANA WA
MUNGU

 Siri ya mabadiliko ya hulka/tabia ni YESU PEKEE

 Chukua hatua umwendee YESU upate kubadilisha tabia yako uwe kiumbe kipya:2
wakoritho 5: 17

You might also like