Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 50

TARATIBU ZA KISHERIA

Kitabu hichi kimeandikwa na Joel Nanauka, kikiwa ni kitabu


cha 2 katika
mfululizo wa Practical Wisdom Series
Haki zote zipo chini ya Joel Arthur Nanauka
Haki zote zimehifadhiwa.

Huruhusiwi kunakili, kudurufu au kutumia sehemu ya kitabu


hiki bila idhini ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa
ni
Ukiukwaji wa haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa kazi
hii.
Mpangilio wa ndani umefanywa na Andrew Rwela.

2020

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 1


UTANGULIZI

Kupitia program maalumu ya mafunzo kwa njia ya mtandao,


watu wengi sana wamebadilisha maisha yao.
Shuhuda nyingi ambazo zimetolewa na watu mbalimbali ni
ushahidi tosha kuwa mafunzo haya yamewabadilisha sana.

Mafunzo haya ambayo hutolewa kwa njia ya mtandao na


Africa Success Online College huwa yanafanyika kwa
lugha ya kiswahili na huwafikia watu walioko
maeneo mbalimbali.

Mwaka 2017 moja ya mafunzo yaliyofanyika ni yale ambayo


yalihusisha kujenga msingi wa mafanikio na unavyoweza
kufanikiwa kifedha, mafunzo haya yalidumu kwa muda wa
miezi 3.

Kupitia mafunzo haya watu wengi sana walifanikiwa kupiga


hatua na kutaka kuyapata mafunzo hayo kwa njia ya kitabu.
Kijitabu hiki ni sehemu ndogo ya mafunzo yaliyotolewa.

Lengo ni kukupa maarifa ili nawe uweze kufanikiwa katika


kuiishi ndoto yako.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 2


SEHEMU YA KWANZA

KUJENGA MTANDAO WA WATU


KIMKAKATI NA KUWA NA
MAHUSIANO BORA
“Hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa kutimiza malengo
aliyonayo kwenye maisha yake kwa kufanya peke yake, kila
mtu anahitaji watu wengine ili aweze kufanikiwa”

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 3


SEHEMU YA KWANZA

Aina Za Marafiki Ambao Unawahitaji Kwenye Maisha Yako


Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kasi.

Katika maisha yako kuna aina ya watu ambao unawahitaji ili


uweze kufanikiwa katika maisha yako na ili uharakishe
kufika kule ambako unataka kufika.

Marafiki hawa huwa hawaji kwa bahati bali unatakiwa


kuweka mkakati na juhudi maalumu za kuweza kuwapata ili
wawe msaada kwako.

Leo ningependa tuangalie aina ya marafiki ambao kila


aliyefanikiwa aliweka juhudi kuwa nao. Swali kubwa hapa
kwako ni je, wewe unao marafiki wa namna hiyo?

1. Rafiki anayeitwa “MUST FRIEND”


Huyu ni rafiki ambaye ni wa muhimu sana katika maisha
yako na ambaye kila linapotokea jambo kubwa linalohusu
maisha yako huwa lazima umtafute ili uongee naye.

Rafiki huyu inawezekana usiwe unaonana naye kila siku au


mara kwa mara lakini ni mtu ambaye unajua kuwa kwa
jambo lolote lile kubwa linalohusu maisha yako ni lazima

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 4


SEHEMU YA KWANZA

utamshirikisha. Mara nyingi rafiki wa namna hii


unamwamini sana na hauna hofu kwamba hata
ukimwambia mambo yako ya ndani basi kesho yake
hautayasikia yakiwa nje yanazungumzwa.
Kila unapokuwa na jambo gumu sana la kuhusu maisha
yako na unapata shida na maamuzi ya kuchukua basi rafiki
huyu ndiye ambaye utamtafuta na kupata ushauri wake.

Mtu wa namna hii ni kwamba shida yako huwa shida yake


na unapokuwa umefanikiwa ama kufurahi naye huwa
anafurahi pamoja nawe kwa dhati kabisa.
Unamuamini kuwa wakati wowote ule utakapohitaji msaada
wake basi atajitahidi afanye kila anachoweza kilicho ndani
ya uwezo wake ili akusaidie.

2. Rafiki anayeitwa “RED CARPET”


Kila mtu huwa kuna wakati anafika na anaanza kuona hofu
juu ya kile kitu ambacho ameamua kukifanya kwenye
maisha yake. Kuna wakati unaweza kufeli kiwango
ambacho haujiamini tena kuwa unaweza kusonga mbele
tena. Hapa ndipo “Red Carpet Friend” anapohitajika.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 5


SEHEMU YA KWANZA

Rafiki huyu ni yule ambaye anaamini sana katika uwezo


wako wakati mwingine zaidi hata ya wewe mwenyewe
unavyoona inawezekana.

Rafiki huyu anaweza kuona madhaifu yako na bado


akayavumilia na kusema zaidi nguvu na uwezo wako kuliko
udhaifu wako.

Kwa maneno mengine huyu ni mtu ambaye kila wakati


atakuwa anatumia muda wake kukutia moyo na
kukuonyesha jinsi ambavyo unaweza kufanikiwa zaidi ya
kiwango ambacho uko kwa wakati huo.

Changamoto kubwa sana ya marafiki hawa huwa ni


wagumu kukukosoa ili uboreshe. Hawa wanaona mazuri
yako tu, na sio kwa unafiki bali ndivyo walivyo.

Hawa ni wa muhimu ili kukusaidia hasa katika kipindi


ambacho unajiona haufai na hauwezi kusogea hatua moja
zaidi. Rafiki huyu pia huwa tunamuita Motivator.

Je, Unaye rafiki wa namna hii?

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 6


SEHEMU YA KWANZA

3.Rafiki anayeitwa “STRICT CORP”


Rafiki huyu huwa haoni shida yoyote ile kukukosoa ama
kukuambia ukweli. Anaweza asiwe mzuri wa kusifia bali
huwa anaona madhaifu na makosa yako kwa haraka zaidi
kuliko wewe mwenyewe ama mtu mwingine. Tofauti kubwa
aliyonayo na wengine wote ni kuwa huwa anafanya kwa
sababu anakupenda.

Ukitaka kumjua ni rahisi sana, hata wewe mwenyewe


ukikosolewa na huyu mara nyingi hukasiriki kwa sababu
unajua anakupenda.

Mara nyingi marafiki wa namna hii huwa wanakuwa ni watu


wanaopenda utani ama kuwakilisha maneno yao kwa kejeli
ama vichekesho ambapo mwisho wa siku unajikuta baada
ya kukasirika na wewe unacheka kwa kuambiwa ukweli
huku anakutania.

Huyu wakati mwingine huitwa the challenger.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 7


SEHEMU YA KWANZA

4. Rafiki anayeitwa “ACCOUNTABILITY PARTER”


Huyu anaitwa rafiki wa kukusaidia kuwajibika.Mara nyingi
sana kama hatuna mfumo wa kutufanya tuwajibike
tumekuwa ni wavivu wa kufikia malengo yetu makubwa
kwenye maisha.

Rafiki huyu ni yule ambaye anajua malengo uliyonayo


maishani na maono makubwa uliyonayo na kazi yake kubwa
ni kukukumbusha na kuona kuwa unaendelea kubakia
kwenye mstari bila kuzembea.

Huyu unashauriwa kuwa unamshirikisha mambo yako na


unapata muda wa kuzungumza naye kila baada ya muda
fulani.Mnaweza kujiwekea mpango maalumu wa namna ya
kukamilisha yale ambayo mmepanga kuyafanya kwa
pamoja na mkawa na nyakati za kufanya tathmini.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 8


SEHEMU YA KWANZA

Mbinu 4 Za Kuwatunza Rafiki Zako Muhimu ili Usiwapoteze

1. Uwepo Wanapokuhitaji.
Hakuna kitu chenye nguvu kama uwepo wako kwa marafiki
zako pale ambapo huwa wanakuhitaji. Inawezekana ikawa
ni wakati wanapopata misiba, siku zao muhimu kama vile
siku ya kuzaliwa, wanapougua n.k kiufupi ni kuwa jitahidi
sana kuwepo katika nyakati zote muhimu za aina 2 za
maisha yao.

a. Wakati ambapo wanakuwa na furaha sana.


Hii inaweza kuwa wakati ambapo wamefanikiwa katika
jambo Fulani. Wamemaliza masomo, wamepewa tuzo n.k

b. Wakati wanapokuwa na huzuni sana.


Kipindi ambapo wamepata msiba, ajali ama tukio baya la
kuhuzunisha kwenye maisha yao.

2. Waambie “Nilikuwa nakufikiria”


Mara nyingi huwa ni ngumu sana hasa kwa wanaume, lakini
kutumia sekunde na kumwambia mtu nakusalimia kwa
sababu nimekukumbuka ni jambo lenye nguvu sana katika
maisha. Wakati mwingine unaweza kuona tukio ama kupita

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 9


SEHEMU YA KWANZA

eneo fulani na likakumbusha mtu fulani basi usisite


kumtafuta kwa kumpigia simu ama kumwandikia kuwa
“Nimekukumbuka leo”. Sio lazima kuwe na kitu cha ajabu
sana cha kumfanyia unapomkumbuka mtu.

Najua hapa unaposoma kuna mtu umeshamkumbuka na


unatamani kumwambia, basi chukua sekunde na
umwambie kuwa umemkumbuka na utaona atakavyofurahi.
Kumbuka hitaji kubwa la mwanadamu sio fedha bali ni
kuonekana kuwa ni mtu wa muhimu.

3. Kubali unapokosea
Moja ya kitu kinachofukuza marafiki sana katika maisha ya
watu wengi ni tabia ya kujiona kuwa wako sawa kila wakati
na hawawezi kukosea hata kidogo. Kuna watu ambao
wamepoteza watu muhimu sana kwenye maisha yao kwa
sababu ya kushindwa kukubali makosa yao.

Hawa ni wale watu ambao huwa wanaitwa Mr. and Mrs.


Right. Huwa wanaamini kila mtu anakosea na wao ndio
wako sawa, Kila wakitoa maoni huwa wanataka yale
wanayosema yakubalike zaidi ya mtu yoyote yule.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 10


SEHEMU YA KWANZA

Kila unapogundua kuwa umekosea na kukubali unaongeza


uimara wa mahusiao uliyonayo na marafiki zako muhimu
kwenye maisha yako.

4. Usidhanie pata uhakika (don’t assume)


Umeshawahi kumkasirikia rafiki yako kwa kitu fulani halafu
alipokuja kutoa maelezo ukajiona ulivyokuwa unawaza ni
tofauti kabisa?

Kati ya kitu kimeharibu mahusiano ya rafiki wengi ni kuweka


dhahania ambayo sio ya ukweli. Kwa kila uhusiano ulionao
jaribu kutafuta ukweli wa mambo kwa uhalisia na sio
kutumia dhahania.

Jifunze kutofanya maamuzi yoyote yale kwenye maisha


yako kwa kutumia dhahania yako bila kutafuta ukweli wa
mambo.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 11


SEHEMU YA KWANZA

ZOEZI
Jaribu kufanya tathimini ya marafiki ulionao na kisha
hakikisha unamtafuta rafiki wa uwajibikaji (Accountability
Friend)

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 12


SEHEMU YA PILI

TAMBUA HATUA ZA
KUKAMILISHA NDOTO YAKO
“Kila ndoto huwa inapitia hatua mbalimbali kabla
haijakamilika. Kwa kila hatua huwa kuna aina ya watu ambao
unawahitaji na pia mambo unayotakiwa kuyafanya"

Lengo: Lengo kubwa la somo hili ni kukusaidia kujua hatua


ambazo kila lengo lazima lipitie na yale unayopaswa
kuyafanya.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 13


SEHEMU YA PILI

UTANGULIZI
Kila lengo ulilonalo huwa ni kama maisha ya mwanadamu
huwa linazaliwa na linakua. Ila pia huwa linaweza kufa kabla
ya wakati wake.

Ili ufanikiwe katika maisha yako ni lazima uhakikishe kuwa


unatambua majira maalumu ambayo wazo lako huwa
linapitia na kujua haswa unatakiwa kufanya nini.

Kila majira fulani inamaanisha kuna mambo maalumu


ambayo unatakiwa kuyafanya ili uweze kufanikiwa kufika
mwisho.

Umeshawahi kuona mtu ameanza vizuri kufanya jambo


fulani lakini mwisho wa siku akaishia njiani na akashindwa
kufikia kilele cha mafanikio ambayo wengi waliyatarajia?

Umeshawahi kuona mtu ana kipaji lakini hafiki mbali


ukilinganisha na mtu ambaye hana kipaji kikubwa ila
anafika mbali sana?

Usipojua mambo yanayotakiwa kufanya kwa kila majira ya


maisha yako basi unaweza kujikuta unakwama kuendelea

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 14


SEHEMU YA PILI

mbele kwenye maisha yako.

UNAIFAHAMU “LAW OF TIMING


(Kanuni ya kuenenda na muda)
Kwenye kitabu cha John Maxwell cha kanuni 21 za Uongozi
amezungumzia kanuni hii muhimu sana kwenye mafanikio
ya mtu yoyote yule.

Ukweli ni kwamba unaweza kuwa na kipaji na uwezo wa


kipekee ila kama haulengi kufanya kitu kuendana na muda
husika unaweza kujikuta unapotea kabisa na unashindwa
kufika ambako unatakiwa kwenda.

Kiini cha kanuni hii inakutaka kutambua kuwa kujua jambo


la KUFANYA bila kujua MUDA wa KUFANYA inaweza kuwa
sababu kubwa kabisa ya kukufanya ufeli katika kila
unachofanya. Kufanya jambo sahihi kwa wakati usio sahihi
kunaweza kupelekea kufeli kwako kwa kiwango cha juu
sana.

USIJILAZIMISHE kufanya kitu kwa haraka kwa sababu kila


mtu anafanya na usichelewe kufanya maamuzi kwa hofu ya
watu watasemaje, ukiona ndani ya moyo wako taa ya kijani

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 15


SEHEMU YA PILI

imekuruhusu kufanya kitu, songa mbele.

Hatua Nne Ambazo Kila Lengo Lazima Lipitie Na Mambo


Unayotakiwa Kufanya.

1. Kupata Wazo (Conception Stage)


Hatua ya kwanza kwenye lengo au ndoto uliyonayo itakuwa
ni kupata wazo kwanza la kufanya jambo fulani.
Mara nyingi hii huwa ni hatua ambayo inakuwa imejaa
furaha na kuona uwezekano usiopingika wa kile ambacho
unataka kukifanya.

Mara nyingi katika hatua hii watu wengi hawawezi kuona


vitu vinavyoweza kukwamisha kile wanachotaka kukifanya
na kila mtu ambaye atajaribu kuwaonyesha mambo ambayo
yanaweza kuhatarisha mafanikio ya kile ambacho wanataka
kufanya huwa wanamchukulia kama adui yao.

Ukiwa katika hatua hii ndio pale unataka kila mtu aone
kama wewe unavyoona na unaanza kujiona ukiwa tayari ni
tajiri hata kabla hujaanza kufanya (hapa ndio hupigwa
mahesabu ya mamilioni kwenye karatasi).
Hapa ndio ule wakati unapiga mahesabu ya faida ya

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 16


SEHEMU YA PILI

mavuno, bidhaa au huduma unayotoa hata kabla haujaanza.

Wakati mwingine unaweza kujikuta unakosa usingizi kwa


furaha ambayo unakuwa nayo wakati wa hatua hii kwani
unaona umeshakuwa bilionea tayari.

Unatakiwa ujifunze katika hatua hii kuwa msikivu haswa


kwa watu ambao unawaamini sana, kwani wanaweza
kukupunguzia madhara yanayotokana na kuchukua hatua
bila kuzingatia mambo ya msingi kwenye kile unachotakiwa
kufanya. Siku zote kumbuka kuna watu ambao wamepewa
uwezo wa kuona kile ambacho wewe hauwezi kukiona.

2. Kulitekeleza wazo (Implementation Stage)


Hatua ya pili ni pale unapoingia katika utekelezaji wa wazo
kwa vitendo. Huu ndio wakati ambao huwa unaona uhalisia
wa mambo wakati mwingine tofauti kabisa na ulivyokuwa
unafikiria hapo mwanzoni.

Katika hatua hii ndio huwa unakutana na vikwazo ambavyo


hukuwa umeviwaza, unagundua wazo lako linahitaji muda
zaidi ya ulivyokuwa unadhania na linahitaji pesa zaidi ya
ulivyodhani pia.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 17


SEHEMU YA PILI

Kiufupi ni kuwa katika utekelezaji ndipo ambapo zile


mbwembwe zote za kufanya jambo fulani huwa zinapotea
kabisa na maswali ya kuanza kujiuliza kama uendelee ama
uishie njiani ndipo huanza kuja.

Watu wengi huishia hatua za mwanzo kabisa wanapoanza


utekelezaji baada ya kugundua kuwa hawawezi tena
kuendelea mbele.

3. Wakati wa Kubaki peke Yako (Isolation stage)


Kama utafanikiwa kuvuka hatua za utekelezaji mbele kidogo
utakutana na wakati wa kubaki peke yako.

Huu ni ule wakati ambao utajikuta kuwa watu wote ambao


ulikuwa unawatarajia wawe msaada kwa biashara ama
kukulipia ada ama kukuunganisha, huwa hawaonekani tena.

Kipindi hiki ndio huwa kinathibitisha kuwa kama lengo


ulilonalo lilitokana na wewe mwenyewe ama lilitokana na
hamasa ya watu nje yako.

Watu wote ambao huwa walianza kitu kwa sababu ya


hamasa ya nje huwa wakifika hatua hii hawawezi kuendelea

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 18


SEHEMU YA PILI

mbele zaidi. Huu ni wakati ambao unaweza kuona kama vile


dunia imekugeuka kabisa.

Unachotakiwa kujua ni kuwa kila ambaye amefanikiwa


aliwahi kupitia hali kama hii katika maisha yake.
Unachotakiwa kujua ni kuwa hii ndio hatua ngumu ila ndio
huwa iko karibu zaidi na kule ambako unaelekea kwenye
mafanikio.

Huu ni wakati wa maumivu makali sana ila unatakiwa


kujitahidi kuvumilia ili ufike upande wa pili. Kwa kawaida
watu huwa hawapendi kujiambatanisha na wewe
utakapokuwa unapitia wakati huu.

4. Wakati wa mafanikio Makubwa (Celebration Stage)


Hatua ya mwisho ambayo unatakiwa kuipitia ni ile ya
mafanikio yanapoanza kuonekana. Jambo la kwanza
unalotakiwa kulijua ni kuwa ukiwa katika hali hii kila mtu
atajifanya ni rafiki yako na wale wote waliopotea utaanza
kuwaona wanarudi taratibu na watakuwa wanataka
waonekane kuwa wamechangia kwenye mafanikio yako.

Ukiwa katika hali hii kila mtu atataka aonyeshe jinsi

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 19


SEHEMU YA PILI

ambavyo anakufahamu na pia kila mtu atataka kuwa karibu


na wewe kwa kila wakati.

Wakati huu unatakiwa uwe makini sana kwani watu wengi


sana huwa wanakosea kwa kuwaacha marafiki wa kweli na
wanajikuta wanaanza kuambatana na marafiki ambao
wanakuwa wamekuja kufuata mafanikio yao tu.

ZOEZI
Kwa lengo kubwa ulilonalo kwa mwaka huu, je uko katika
hatua gani kati ya hizo zilizotajwa?

Umejiandaa kwa hatua zinazofuata kukabiliana na


changamoto zinazoambatana nazo?

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 20


SEHEMU YA TATU

JINSI YA KUANZA UPYA


NA KUJITOFAUTISHA
“Nikiacha kujifunza basi hapo nakuwa nimesitisha safari
ya mafanikio” - JOHN Wooden
(Kocha mkuu wa mpira wa kikapu Marekani ambaye
alishinda vikombe 10 vya ligi ya Taifa)

Jifunze namna bora zaidi ya kuanza kujenga msingi wako


wa mafanikio kupitia mbinu walizotumia watu wengi ili
kufanikiwa.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 21


SEHEMU YA TATU

UTANGULIZI
Wakati fulani ulifanyika utafiti nchini Marekani na
ikagundulika kuwa mtu wa kawaida huwa anaangalia
televisheni kwa muda wa masaa 6.

Hii inamaanisha kama mtu huyu ataishi kwa miaka 60


atakuwa ameitumia sawa na miaka 15 kwa kuangalia Tv tu
ambayo ni sawa na robo ya maisha yake.

Siku moja Mwandishi mashuhuri Jack Canfield alienda


kuomba ushauri kwa tajiri mkubwa wa marekani bilionea
W.Clement Stone juu ya siri ya kufanikiwa kwa haraka. Jibu
alimuuliza huwa anaangalia televisheni kwa masaa
mangapi,

Alipojibu alimwambia “Apunguze lisaa limoja la kuangalia


televisheni, ambapo itakuwa sawa na masaa 365 ya ziada
kwa mwaka, ambayo ni sawa na masaa 40 ya ziada kwa kila
wiki na ni sawa na miezi miwili ya ziada kwenye kila mwaka”

Kisha akamwambia atumie masaa hayo kufanya mambo


yatakayomsaidia kuongeza thamani kwenye maisha yake.
Kwako wewe inaweza kuwa ni masaa mengi unayotumia

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 22


SEHEMU YA TATU

kuperuzi mitandao ya jamii, inaweza kuwa ni ya masaa


mengi kuangalia mpira wa miguu, inaweza kuwa ni masaa
mengi ya kupiga stori n.k
Ili kuanza upya safari yako ya mafanikio ni lazima uamua
kuanza kutumia muda wako tofauti na kawaida ambayo
umeizoea.

MAMBO MUHIMU UNAYOWEZA KUANZA KUYAFANYA LEO


Siku zote usisahau kuwa watu ambao wamefanikiwa kufika
juu sana katika kile wanakifanya wamewekeza sana katika
kujifunza.

Umeshawahi kusikia msemo unaosema “Leaders are


Readers?”

1. Wanaoongoza kwenye field zao huwa ni wasomaji wazuri


Dr.John Demartin aliamua kuweka orodha ya watu wote
ambao waliwahi kupata Nobel Prize, na akajaribu kutafuta
watu ambao wamefanya vizuri na kuongoza katika sekta
mbalimbali za maisha na kisha akaamua kusoma historia
zao.

Hii ilimfanya ajifunze mbinu nyingi sana za mafanikio na

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 23


SEHEMU YA TATU

alipoulizwa kuhusu mafanikio yake akasema ni kwa sababu


amekuwa anasoma sana historia ya waliofanikiwa na
kujifunza.

Hii ndio maana mwanafalsafa wa mafanikio Jim Rohn


aliwahi kusema kama ukitumia muda wa saa moja kila siku
kujifunza au kusoma kitu fulani utakuwa umesoma mambo
ambayo ni takribani sawa na kitabu kimoja kwa wiki

Ambayo baada ya miaka 10 itakuwa ni sawa na kusoma


vitabu 520 na baada ya miaka 20 ni kama sawa na vitabu
1000 ambavyo vitatosha kabisa kukuweka katika 1% ya
watu bora kabisa katika kile unachofanya.

Mbinu za kusoma kitabu kwa ufanisi:


i. Tambua eneo ambalo unataka kuwa bora katika maisha
yako
ii. Chagua eneo maalumu ambalo unataka kujijenga
(Kutunza muda, uwekezaji n.k)
iii. Tafuta watu nguli kwenye eneo hilo
iv. Tafuta maandiko yao(vitabu ama kwa siku hizi unaweza
kutumia kurasa zao za social media)
v. Anza kuwafuatilia kwa kusoma kwa mwendelezo

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 24


SEHEMU YA TATU

Kumbuka kuwa sio kila kitu anachosoma mwingine ni


lazima na wewe ukisome. Soma kulingana na uhitaji ulionao
kwa wakati uliopo na unaokuja.

NB: Kama ungependa kupata vitabu bora kwaajili ya


kujiendeleza, unaweza kuviagiza kutoka Timiza Malengo
Bookshop na utavipata popote ulipo
(Wasiliana kupitia 0743 252 670 / 0756 094 875)

2. Hudhuria semina na mafunzo yanayoendana na kile


unachokitaka.
Ni ukweli usiopingika kwamba katika ulimwengu wa sasa na
hasa hapa Tanzania ni kama vile kuna semina kila mahali
na kila siku. Usipokuwa mwangalifu unaweza kujikuta
unakuwa mtu wa kuhama kutoka semina moja kwenda
semina nyingine bila kupata matokeo muhimu kwenye
maisha yako.

Hivyo ni lazima ujiwekee mkakati wa namna bora


unavyoweza kufaidika na hizi semina. Pamoja na hayo yote
inashauriwa kuwa angalau kila mwezi uwe unahudhuria
semina moja ya kukusaidia kukujengea uwezo zaidi katika
maisha yako. Kwa namna teknolojia ilivyo sasa

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 25


SEHEMU YA TATU

unaweza kuhudhuria semina hizi kupitia mitandao (huwa


tunatoa semina hizi kwa njia ya Whatsapp au YouTube mara
kwa mara).

Hivyo kabla haujaamua kuhudhuria semina yoyote ile


unatakiwa kujiuliza maswali yafuatayo ili usijikute unaingia
katika makumbo wa kuhudhuria kila semina:

i. Semina hii hasa inaenda kufundisha kitu gani?

ii. Hicho kinachofundishwa ndicho ninachokihitaji kwenye


maisha yangu kwa sasa?

iii. Wazungumzaji ni akina nani? na je wana matokeo katika


kile wanachokizungumza?

iv. Je, semina ya mwisho niliyohudhuria nimefanyia kazi


jambo gani? Na ina uhusiano gani na semina hii?

v. Nahudhuria semina hii kwa sababu siku ya semina sina


kitu cha kufanya ama ni kwa sababu ni kitu muhimu kwangu
na hata ningekuwa bize bado ningehudhuria?

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 26


SEHEMU YA TATU

JE WEWE HAUNA MUDA WA KUSOMA VITABU


NA KUHUDHURIA SEMINA?
Mwaka 2015 Mark Zuckeberg, mmiliki wa facebook
aliutangaza kuwa mwaka wa vitabu na alisoma jumla ya
vitabu 52 kwa mwaka.

Zuckerberg ana utajiri wa dola bilioni 62 (2016) na


anaongoza makampuni makubwa duniani, Wewe uko bize
na makampuni mangapi na una utajiri wa kiasi gani hadi
unashindwa kupata muda wa kujisomea?

Richard Branson, Bilionea anayemiliki zaidi ya makapuni


400 na huwa anapata muda wa kujisomea vitabu. Wewe
una kitu gani kinakuweka bize sana hadi unakosa muda wa
kusoma hata kitabu kimoja tu?

Muda mfupi kabla ya kuondoka ikulu Obama aliulizwa siri ya


mafanikio yake katika siasa. Jibu lake lilikuwa fupi sana
“Nilikuwa natumia muda mwingi kusoma vitabu”.

Kiongozi wa taifa lenye nguvu na watu wengi duniani alipata


muda wa kusoma vitabu, wewe ni majukumu gani ambayo
yanakufanya usiwe unasoma vitabu?

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 27


SEHEMU YA TATU

ZOEZI
Andika mkakati wako wa miezi 3 kuanzia sasa wa kutumia
njia hizo mbili hapo juu na uanze kuufanyia kazi.

Anza kwa kuchambua eneo lako mahsusi unalotaka kuwa


bora na fuata hatua zote zilizotajwa katika muongozo hapo
juu.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 28


SEHEMU YA NNE

KUANZA NA WAZO DOGO,


FEDHA KIDOGO ILI KUJENGA
MAFANIKIO MAKUBWA
“Kila pesa inayopita mbele yako ni mbegu ya kukufanya
upate pesa nyingi zaidi.
Ili ufanikiwe sana kifedha ni lazima uamue kuithamini kila
pesa inayopita mikononi mwako”

Lengo: Somo hili linalenga kukusaidia namna unavyoweza


kuanza na wazo dogo na pesa ndogo uliyonayo na kufanya
kitu kikubwa katika maisha.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 29


SEHEMU YA NNE

UTANGULIZI
Somo hili ni muhimu sana kukusaidia kuanza mafanikio
yako ya kifedha. Watu wengi huwa wanadharau mwanzo
mdogo ila wasichojua ni kuwa vitu vidogo vidogo
vikiunganishwa hugeuka kuwa vikubwa sana.

Mwaka 1886 mfamasia John Pemberton ambaye wakati


huo alikuwa anajulikana kwa jina maarufu la Mr. Doc
alikuwa amerudi kutoka vitani, naye alikuwa anawaza
agundue kitu gani ambacho kingeweza kumletea faida ya
kibiashara.

Kabla hajaenda vitani alikuwa amejaribu kufanya vitu vingi


sana lakini havikufanikiwa ikiwemo kujaribu kugundua dawa
kadhaa ambazo hazikufanya vizuri na hazikumletea
mafanikio yoyote yale. Hivyo baada ya kuhamia jiji la Atlanta
ule Marekani aliamua kutafuta namna ya kutengeneza kitu
ambacho kinaweza kutumika kama kinywaji cha
kujiburudisha.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 30


SEHEMU YA NNE

Baada ya kutengeneza “formula” yake ya kikemikali na


kuanza kuiuza ilianza kupendwa sana na watu wengi. Hata
hivyo, hakujua namna nzuri ya kuitangaza na hapa ndipo
Frank Robinson alikuja kumsaidia na wakatengeneza
nembo (logo) na kasha wakatengeneza pia kauli mbiu ya
Coca-Cola ya wakati huo “The Pause That Refreshes,” pia
akaisajili kabisa.

Unachotakiwa kukumbuka ni kuwa biashara hii ya kuuza


soda ya Coca-Cola kwa mwaka wa kwanza ilikuwa mbaya
sana, na walifanikiwa kuuza chupa 25 tu kwa mwaka
mzima.

Baada ya hapo walianza kampeni za matangazo, wakawa


wanatoa kalenda, matangazo madogo madogo ya
kubandika kwenye notebook, magari n.k, pia walianza kutoa
ofa ya soda za bure kila baada ya muda fulani.

Baada ya muda, watu wengi wakaijua Coca-Cola na


wakaanza kuuza kwa kiwango cha juu sana. Kwa sasa
wanauza zaidi ya chupa bilioni 1.8 kwa kila siku kutoka
kuuza chupa 25 kwa mwaka mzima.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 31


SEHEMU YA NNE

Sifa moja kuu unayoihitaji katika maisha yako ili uweze


kufanikiwa katika malengo yako, HASA YA KIFEDHA ni
kukubali kuanza na kile kidogo ulichonacho, ili uweze kufikia
kupata kikubwa sana ambacho unakitafuta katika maisha
yako.

Watu wengi sana wamekwama katika maisha yao kwa


sababu wanasubiri hadi wawe na vitu vikubwa ndipo
waanze kufanya kile wanachodhani wanakitaka.

Kwa Nini Unachelewa Kuanza Kufanya?


Sababu moja kubwa sana ambayo huwafanya watu wengi
kuchelewa kuanza kufanya kitu ambacho wanatakiwa
kufanya katika maisha yao ni ile hali ya kuamini kuwa kile
walichonacho ni kidogo sana.

Inawezekana na wewe ni mmoja wa wale watu ambao siku


zote huwa wanaamini kwamba hawana kitu kikubwa, hivyo
wasubirie hadi watakavyokuwa na kitu kikubwa ndipo
waanze.

Unajua matokeo yake yanakuwa ni nini? Wanajikuta muda


unaenda na umri unaenda na hawajafanya chochote kile.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 32


SEHEMU YA NNE

Wewe ni shahidi, hebu kumbuka ni mara ngapi umesema


kuwa unasubiri uwe na vingi ili uanze na hadi leo bado
haujaanza? Na wakati huo huo kuna watu wengi sana
ambao walikuwa na PESA KIDOGO kuliko hata ambacho
wewe ulikuwa nacho, leo wamefika mbali sana na
unatamani kama na wewe pia ungeanza kidogo kama wao
walivyoanza na leo ungekuwa umefika mbali sana.

Kama mwanzilishi wa Coca-Cola angesema asubiri hadi


awe na mtaji mkubwa sana ili aweze kufanya biashara
kubwa, na sio kuanza na kitu kidogo basi pengine angekufa
akiwa na wazo lake la kuanzisha Coca-Cola, kwani
angekuwa anasubiri awe na vitu vingi zaidi, ujuzi mwingi na
pesa nyingi zaidi.

Tumia Uwezo wako Vizuri ujenge biashara yako na Uongeze


kipato chako. Nakubaliana sana na maneno ambayo Dr.
Myles Munroe aliwahi kusema kuhusu watu ambao
wanashindwa kuanza na kufanya kwani wanaamini bado
walichonacho ni kidogo na matokeo yake huwa hawafanyi
hadi wanajikuta wamezeeka.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 33


SEHEMU YA NNE

Dr. Myles aliwahi kusema hivi: “Sehemu yenye utajiri sana


duniani sio katika visima vya mafuta vilivyoko Uarabuni ama
katika migodi ya almasi au dhahabu iliyoko katika bara la
Amerika Kusini. Sehemu yenye utajiri mkubwa zaidi duniani
ni makaburini.”

Hii ni kwa sababu katika makaburi wamelala watu ambao


walikuwa wawe wafanyabiashara wakubwa sana lakini kwa
sababu ya kutokuwa tayari kuanza na kusubiria hadi wawe
na vingi walikufa wakiwa maskini.

Katika makaburi wamelala watu ambao ilibidi wawe


waimbaji wakubwa ila kwa sababu walisubiri hadi wapate
watu wengi wa kuimba mbele yao, basi wamekufa na vipaji
vyao n.k.

Kuna watu wengi sana kila siku wanafariki wakiwa na


uwezo mkubwa ndani yao kwa sababu ya kudharau kile
kidogo wanachoweza kukifanya. Jiangalie, ili wewe pia
usiwe mmoja wao. Ukidharau kidogo ulicho nacho, hauwezi
kupata fursa ya kumiliki kikubwa ambacho unakitafuta.
Watu wanaotimiza malengo yao sifa mojawapo kubwa
waliyonayo ni kuwa tayari kuanza na kidogo sana

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 34


SEHEMU YA NNE

walichonacho,, huku wakiamini wanaweza kukikuza na


kikawa kikubwa sana.

Biashara kubwa duniani, nyingi zilianza na MTAJI MDOGO


SANA na wakaikuza hadi ikawa biashara kubwa.
Sifa mojawapo unayotakiwa kuwa nayo ni hali ya kujiuliza
kila wakati, “Kuna kitu gani kidogo nilichonacho ambacho
naweza kuanza nacho?”

Hili ndio swali muhimu ambalo watu wanaotimiza malengo


yao huwa wanajiuliza. Watu ambao wanafeli huwa kila
wakati wanaangalia wasichonacho na huwa wanasingizia
kuwa hawawezi kufanikiwa kwa sababu walichonacho ni
kidogo sana na hawawezi kufanyia kitu chochote katika
maisha yao.

Kuanzia leo badilisha mtazamo wako kama kweli unataka


kufikia malengo yako. Namfahamu rafiki yangu mmoja
ambaye kwa sasa anamiliki maabara mbili, ambaye alianza
na kununua vifaa kidogokidogo na kifaa cha kwanza
kununua kilikuwa ni “Microscope” (Kifaa cha kuchunguzia
damu ili kuona kama kuna vijidudu vinavyosababisha
magonjwa).

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 35


SEHEMU YA NNE

Kutokea mwanzo huo mdogo, leo amepiga hatua kubwa


sana. Na wewe acha kusingizia kuwa ulichonacho ni kidogo
sana, hebu jaribu kujiuliza na uamue kuanza na kile
ulichonacho. Kumbuka sikuzote kuwa, Hautaweza kupata
kikubwa usichonacho hadi pale utakapotumia kidogo
ulichonacho.

Je, kuna hatua gani unayotaka kuanza leo? Usichelewe na


usisubiri anza mara moja.

Dola Moja na Dola Milioni Moja Unachagua Ipi?


Katika kuwa tayari na kuanza na kidogo ulichonacho
unatakiwa uwe mtu ambaye unaweza kuvumilia mchakato
wa kukuza kile ulichonacho hadi kiwe kikubwa sana.

Tatizo la watu wengi sana ni kuwa hawako tayari kuvumilia


mchakato wa kukuuza kile walichonacho. Tunaishi katika
dunia ambayo inathamini sana kasi kuliko kitu kingine
chochote. Ndio maana kila mtu akitangaza bidhaa yake uwa
anaielezea jinsi ambayo ina kasi isiyo ya kawaida. Ukienda
kwenye usafiri utakutana na mabasi ya mwendo kasi,

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 36


SEHEMU YA NNE

Fikra hii imetujengea mtazamo wa kwamba kila kitu


kinaweza kupatikana kwa kasi na tunajikuta tunasahau
mchakato muhimu wa kukuza kidogo tulichonacho, na kila
mtu anataka kupata kikubwa kwa haraka.

Leo nikikuuliza swali hivi kama nikikupa dola milioni moja


ama nikuambie nikupe dola 0.01? Bila shaka wengi
watachagua dola milioni moja ukiwemo na wewe pia.

Lakini vipi nikikwambia, uchague dola milioni moja ama


ukichagua dola 0.01 itakuwa inaongezeka thamani kwa siku
thelathini zijazo.

Najua wapo wengi watakaochagua dola milioni moja


wakisema, siku thelathini zitaongeza thamani kiasi gani ya
dola 0.01? na wengine watakuwa na shaka wachague ipi
kwani hawajui matokeo ya kuongezeka thamani mara
mbili yatakuwaje.

Nilikwambia hapo awali kuwa watu waliofanikiwa sifa


mojawapo waliyonayo ni kukubali kuanza na kidogo
walichonacho na hawako tayari kuacha kuanza kwa sababu
wanaona ni kidogo.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 37


SEHEMU YA NNE

Na hii imewasaidia sana kuanza mapema na hivyo kukuza


kile wanachofanya wakati wengine ambao wanaendelea
kusubiri hadi wawe na vingi bado hawajaanza hadi leo.
Kikubwa cha kukijua hapa ni kuwa wale ambao wanatimiza
malengo yao huwa wanaweza kuona KIKUBWA kilicho
MBELENI kwa kutumia KIDOGO WALICHONACHO sasa.

Sasa hebu tuangalie tofauti ya machaguo ya makundi haya


mawili. Aliyechagua dola milioni moja na yule aliyechagua
dola 0.01 ambayo inaongezeka thamani mara mbili kila
baada ya siku moja. Hebu tuangalie yule wa 0.01 atakuwa
amepata kiasi gani baada ya muda wa siku 30:

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 38


SEHEMU YA NNE

Siku ya 1 0.01 Siku ya 11 10.24 Siku ya 21 10,485.76

Siku ya 2 0.02 Siku ya 12 20.48 Siku ya 22 20,971.52

Siku ya 3 0.04 Siku ya 13 40.96 Siku ya 23 41,943.04

Siku ya 4 0.08 Siku ya 14 81.92 Siku ya 24 83,886.08

Siku ya 5 0.16 Siku ya 15 163.84 Siku ya 25 167,772.16

Siku ya 6 0.32 Siku ya 16 327.68 Siku ya 26 335,544.32

Siku ya 7 0.64 Siku ya 17 655.36 Siku ya 27 671,088.64

Siku ya 8 1.28 Siku ya 18 1,310.72 Siku ya 28 1,342,177.28

Siku ya 9 2.56 Siku ya 19 2,621.44 Siku ya 29 2,684,354.56

Siku ya 10 5.12 Siku ya 20 5,242.88 Siku ya 30 5,368,709.12

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 39


SEHEMU YA NNE

Hii tunaita nguvu ya mlimbikizano, “Power of Compound


effect”. Siri mojawapo ya mafanikio ambayo watu wengi
wameitumia ni kuhakikisha kuwa wanatumia kile kidogo
walichonacho kwa uaminifu ili kuzalisha kikubwa
wanachokitafuta.

Hebu fikiria kwa mfano huu ni kuwa yule aliyechukua kidogo


ndani ya mwezi mmoja ameweza kutengeneza mara 5 ya
yule ambaye alionekana amechukua kikubwa. Ila ilihitaji
awe mvumilivu kuzalisha kile kidogo
alichonacho.

Wewe pia unatakiwa ujijengee tabia hii ya kuwa tayari


kuanza na kidogo hadi kizae kiwe kikubwa sana.
Katika kutimiza malengo yako kuanza kufanya mapema ni
muhimu sana ili uweze kupata matokeo yale ambayo
unayatarajia.

Kama unataka kuanza kuwekeza katika soko la hisa,


usisubiri kuwa na pesa nyingi, anza mara moja sasa hivi na
utajikuta baada ya muda fulani umeshafikia kiwango kizuri
na kikubwa tofauti na yule ambaye anasema anasubiri.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 40


SEHEMU YA NNE

Kama unataka kuanza kuweka akiba, basi anza mara moja.


Kumbuka kwamba kuweka akiba, kuwekeza na kuanza
kufanya jambo fulani ni tabia.

Kama hauwezi kuweka akiba ya shilingi elfu kumi kwa laki


moja unayopata leo (asilimia 10 ya kipato chako),
basi ujue pia itakuwa ngumu kwako kuweza kuweka shilingi
laki moja kwa milioni moja utakayoipata kesho (asilimia 10
ya kipato chako kitakapoongezeka).

Ukiona unasema hauwezi kufanya kwa sababu una kiasi


kidogo basi ujue hata ukiwa na kikubwa hautaweza. Njia
rahisi na ya uhakika ya kujihakikishia kuwa unatimiza
malengo yako ya mwaka huu ni kujiwekea tabia ya kuanza
na kidogo ulichonacho bila kusubiri kupata kikubwa.

Je, utaanza kuchukua hatua gani leo ili kuanza na kidogo


ulichonacho?

Je, uko tayari kuungana na wale wanaotimiza malengo yao


ama bado utaendelea kusubiri?

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 41


SEHEMU YA NNE

ZOEZI
Baada ya kusoma sura hii hebu jaribu kutafakari kwa
kutumia kile ulichonacho unaweza kuanza kufanya nini?
Kuna changamoto gani ambazo zinakuzuia.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 42


HITIMISHO

TEMBELEA MITANDANO YA KIJAMII YA JOEL NANAUKA

YouTube: Joel Nanaka


(Utapata VIDEO nyingi za kukufundisha mambo mbalimbali)

Instagram: JoelNanauka_
(Utapata mafunzo kila siku yatakayokusaidia)

Facebook: Joel Nanauka Page


(Utapata mafunzo kila siku na pia shuhuda mbalimbali.)

Kupata vitabu vingine vilivyoandikwa na Joel Nanauka


wasiliana na namba zifuatazo:

0745 252 670

0756 094 875

0683 052 686

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 43


HITIMISHO

Naamini kitabu hiki kitakuwa kimekusaidia sana katika


kujifunza mambo mbalimbali ambayo yataharakisha safari
yako ya mafanikio.Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza
kwa bidii ili upate matokeo makubwa zaidi.

Kumbuka kuwa kuna uwezo mkubwa sana ndani yako na


kama ukiamua kuufanyia kazi basi hakuna kitu ambacho
kitakuzuia.

Nakutakia mafanikio katika ndoto yako na usisite


kuwasiliana nasi kwa uhitaji wowote wa ushauri binafsi,
mafunzo kwa wafanyakazi ama ushauri wa kibiashara.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 44


HITIMISHO

VITABU VINGINE VILIVYOANDIKA NA JOEL NANAUKA

TIMIZA MALENGO YAKO


(Mbinu 60 walizotumia watu maarufu kufanikiwa)

ONGEZA KIPATO CHAKO


(Maarifa juu ya Fedha, Biashara na Uwekezaji)

ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO

NGUVU YA MWANAMKE

ISHI NDOTO YAKO


(Siku 30 za kuishi maisha unayoyatamani)

MONEY FORMULA, Elimu ya Fedha Isiyofundishwa Shuleni

UFANISI KAZINI

JINSI YA KUIFANIKISHA NDOTO YAKO KATIKATI YA


CHANGAMOTO

TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO


MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 45
HITIMISHO

UZALENDO NA UJENZI WA NCHI

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 46


KUHUSU MWANDISHI

Joel Arthur Nanauka,


Ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye
shahada ya Biashara na Uongozi (Bcom-Hons) na
stashahada ya juu katika Diplomasia ya Uchumi (Economic
Diplomasi-5.0 GPA) ambako alitunukiwa kama mwanafunzi
bora katika wahitimu.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 47


KUHUSU MWANDISHI

Aliwahi pia kuwa mwanafunzi bora wa kitaifa mwaka 2002


baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne Kibaha
sekondari.

Joel ametajwa na taasisi ya Avance Media yenye makao


yake makuu nchini Ghana kuwa ndiye kijana mwenye
ushawishi zaidi katika eneo la mafunzo ya kujiendeleza
(Personal Development and Academia) kwa mwaka
2019/2020.

Taasisi ya BMCE bank yenye makao yake makuu


Casablanca nchini Morocco na Taasisi ya Graca Machel
Trust (GMT) iliyoko Africa Kusini inamtambua Joel Nanauka
kama mkufunzi mwelekezi (Mentor) katika program zake.

Mwaka 2012 alitajwa kuwa kiongozi bora kijana duniani


katika kongamano la viongozi vijana lililohusisha nchi
mbalimbali duniani lililofanyika Taiwani, China.

Amewahi kufanya kazi na Shirika la Umoja la Mataifa


UNESCO na ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 15 kwenye
lugha ya Kiswahili,kiingereza na kifaransa.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 48


KUHUSU MWANDISHI

Ni mkufunzi na mshauri katika masuala ya biashara,


uongozi na ufanisi kazini kwenye makampuni mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania.

Joel amemuoa Rachel na wana watoto wawili wa Kike,


Joyous na Joyceline.

MUONGOZO WA MAFANIKIO | Joel Arthur Nanauka | 49

You might also like